Monday 14 April 2014

TAARIFA MUHIMU TOKA CCM TAWI LA UINGEREZA‏

  CCM TAWI LA UINGEREZA - UNITED KINGDOM
Website ccmuk.org,Blog ccmuk.org/blog, Facebook page Chama Cha Mapinduzi Uingereza, twitter CCMUK1
Contacts Phone  +44 74 04 863333, +44 7545 213515
E-mail - itikadi-uenezi@ccmuk.org
MAINA OWINO ANG'ATUKA UENYEKITI WA CCM TAWI LA UINGEREZA - UNITED KINGDOM
PIA HALMASHAURI KUU YA TAWI YAMSIMAMISHA KAZI KATIBU WA TAWI BI. MARIAM  MUNGULA:
Mwenyekiti wa CCM UK, Ndugu Maina Ang'iela Owino jana ametangaza rasmi nia yake ya kujiuzulu Uongozi wa CCM Tawi la UK baada ya kutumikia toka mwaka 2007.
Ndugu Owino alitoa uamuzi huo wa hiari wakati akifungua rasmi kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Tawi la UK kilichokaa jana Jumamosi tarehe 12/04/2014 katika jiji la Reading, Berkshire, Uingereza.
Ndugu Owino aliwakumbusha wajumbe kuwa awali aliomba kukitumikia Chama kwa muhula mmoja wa uongozi na alitaja kumbukumbu ya vikao vya Chama vilivyomuomba aendelee kukisimamia Chama hasa baada ya kuchaguliwa viongozi wakuu wapya wa Tawi mwezi septemba 2012 jijini Manchester.
Ndugu Owino aliwakumbusha mafanikio waliyopata katika muda wa uongozi wake ikijumuisha harakati za kufungua mashina hadi 15 katika miji na Jiji mbalimbali; Kuhamasisha na kujenga mtandao wa kuanzisha Jumuiya ya kwanza ya Watanzania hapa UK na Kuwashirikisha wanaCCM kuanzisha miradi ya kujitegema ikiwepo ari ya kumiliki jengo la CCM UK.
Alikumbusha pia juhudi na msukumo wa kutaka CCM Taifa kuanzisha dawati rasmi la matawi ya nje na kuyapa uwakilishi wa kudumu katika vikao vya juu vya CCM Taifa.
Pia kupigania Sera ya CCM ya Diaspora iboreshwe kwa Kuanzisha Kituo Maalum cha Diaspora nchini Tanzania ili serikali iwashirikishe na kuratibu hoja na haja za wana Diaspora.
Aidha aliwataka wajumbe kutoa ushirikiano wa wazi kwa Idara ya uenezi ambayo kwa sasa inajenga Website ya kisasa na Online TV itakayowapa wanaCCM uhuru wa kutoa maoni na hoja zao bila uwoga lakini kwa nidhamu na kufungua soko la kutangaza bidhaa za Tanzania.
Ndugu Owino alisema wanaCCM hujenga umoja wa kweli na hawaogopi kusingiziwa au kusemwa vibaya na hivyo wasiogope changamoto mbalimbali wakati wanatekeleza Mapinduzi ya umma na kukijenga Chama hapa Uingereza.
Ndugu Owino aliiomba Halmashauri Kuu ya Tawi ishirikiane na Sekretariati ya Halmashauri Kuu ya Tawi kufanya maandalizi na kupanga tarehe ya Mkutano Mkuu wakati wowote kuanzia sasa ili wanaCCM wote wawe huru kumchagua kiongozi atakaye sukuma CCM UK toka hapa tulipofikia.
Wakati huohuo Halmashauri Kuu ya CCM ya Tawi la UK jana iliazimia kwa pamoja kumsimamisha Katibu wake wa Tawi Mariam Mungula baada ya majadiliano ya kina ya kutokuridhishwa kabisa na utendaji na uratibu wake wa kazi.
Kikao hicho kilipeleka shauri lake kwa Kamati ya Maadili na Usalama ili apate haki ya kujitetea ni kwa nini asiachishwe moja kwa moja kazi yake za Ukatibu wa CCM UK. Ndugu Leybab Mdegela anakaimu nafasi yake kuanzia jana 12/04/2014.
Kikao kiliendelea na hoja zake za kuboresha Chama hapa UK na kuweka mikakati yenye mawazo chanya katika kukisaidia chama katika mikakati kuleta maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi wote wa Tanzania.
Imetolewa na Abraham Sangiwa 
Idara ya Itikadi na Uenezi ya Halmashauri Kuu ya CCM UK. 
13/04/2014

Share:

Dk.Bilal,Waziri Magufuli wanusurika ajali ya chopa

Dk.Bilal,Waziri Magufuli wanusurika ajali ya chopa

Baadhi ya watu wakiangalia helikopta iliyokuwa imembeba Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, muda mfupi baada ya ndege hiyo kuanguka eneo la Uwanja wa Ndege Terminal One jijini Dar es Salaam jana.Picha: Mpigapicha Wetu
Makamu wa Rais, Dk. Ghalib Bilal , Waziri wa Ujenzi, Dk.John Magufuli na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick, wamenusurika kifo baada ya Helkopita ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliyokuwa wakisafiria kupata hitilafu angani na kuanguka.

 Wengine walionusurika katika ajali ya helikopta hiyo  iliyokuwa imebeba watu 11 ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova, waandishi wa habari wawili, walinzi wawili na maofisa wengine wa serikali.

Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege, Kamishna Khamis Suleiman,akizungumza na NIPASHE alisema kuwa ajali hiyo ilitokea  jana majira ya saa 3:15 asubuhi katika eneo la uwanja wa ndege wa Air Wing unaotumiwa na jeshi.

 Suleiman alisema viongozi hao baada ya kupata ajali hiyo walikimbizwa hospitali ambayo hakuitaja jina kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Hata hivyo, taarifa ambazo NIPASHE ilizipata zilieleza kuwa viongozi hao baada ya kupata ajali hiyo walipelekwa katika hospitali ya usalama wa Taifa iliyopo Makumbusho jijini Dar es Salaam.

Kamanda Suleiman alisema viongozi hao walipata ajali hiyo wakati wanakwenda kukagua maeneo yaliyoathirika na mafuriko ya mvua zilizonyesha tangu juzi  jijini Dar es Salaam.

Alisema helkopita hiyo muda mfupi baada ya kuruka katika uwanja huo wa Air Wing, ilipata hitilafu ikiwa angani na kuanguka.

Aliongeza kuwa hali za viongozi hao zinaendelea vizuri, na wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo.

Waziri wa Uchukuzi, Dk.Harrison Mwakyembe, alipoulizwa na NIPASHE alisema taarifa za tukio hilo amezipata na kwamba ajali hiyo haijatokea upande wa uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa  Mwl.Julius Nyerere (JNIA)  kama ambavyo baadhi ya watu wanaeleza.

“Kimsingi taarifa za tukio hili unaweza kuzipata zaidi kutoka kwa watu wa jeshi maana ajali imetokea upande wa air wing,”alisema Dk.Mwakyembe.

Wakati huo huo, Kurugenzi ya Habari ya JWTZ, imesema helikopta hiyo ilipata ajali katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl Julius Nyerere (JNIA) kwa upande wa Jeshi wakati ilipokuwa katika hatua ya kuanza kuruka.

 Katika taarifa hiyo iliyotumwa kwa vyombo vya habari na Msemaji wa JWTZ, Kanali Erick Komba imeeleza kuwa mbali na viongozi hao, wengine waliokuwemo ni Dk. Mnzava ambaye ni msaidizi wa Makamu wa Rais, Msaidizi wa Kamanda Kova na waandishi wa habari watatu.  

 Alisema ujumbe wa Makamu wa Rais ulikuwa  katika safari ya kuzungukia maeneo yaliyoathirika na mafuriko  katika jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani kufuatia mvua hizo zilizoanza kunyesha kuanzia Aprili 11, mwaka huu.

Komba alisema Makamu wa Rais pamoja na ujumbe wake hawakupata majeraha katika ajali hiyo. Aidha, rubani na wasaidizi wake pia wametoka salama.
Aliongeza kuwa uchunguzi wa ajali hiyo umeanza mara moja kwa ajili ya kubaini chanzo cha ajali hiyo.
 
Share:

Thursday 10 April 2014

JK: Gas, oil policy in place in October


President Jakaya Kikwete opens 19th Annual Research Workshop organised by Research and Poverty Allevation (REPOA) in Dar es Salaam yesterday. (Photo: Tryphone Mweji)
President Jakaya Kikwete yesterday reassured Tanzanians that the government will finalise the policy and legislation for oil and gas extraction in October, this year.

Speaking at the 19th REPOA Annual Research Workshop held in Dar es Salaam yesterday, President Kikwete said there have been extensive discussions on the role natural resources should play in the country’s economy.

“This is particularly relevant today, considering the recent discoveries of large volumes of natural gas, now approximated at 46 trillion cubic feet, and the vast reserves of forests, minerals, diverse wildlife and land that Tanzania has,” he said.

The President also said that the challenge facing the country is how to link these resources with the aspirations of the 2025 Development Vision and the socio-economic transformation the nation desires.

“The strategies and policies are meant to ensure that our people participate productively in the utilisation of the natural resources we are blessed with.

We are also in the process of putting in place a local content policy that will provide a framework for ensuring adequate participation of Micro, Small and Medium Enterprises and local communities in exploiting and utilising our
natural resources,” he said.

He added: “We hope that the private sector, working closely with the government, will proactively engage in the efforts to build the capacity of Tanzanians in different disciplines that are relevant to the various segments of our natural resources’ value chain”.

He underscored that the oil and gas sector is a priority subsector, given the volume of the resources, the intensity of capital investments, and flow of revenues expected from their commercialisation.

“I hope that this workshop will dwell on these issues too, drawing from the experience of other countries as well, on how the enterprise sector including the MSMEs can be leveraged to participate more meaningfully in the desired socio-economic transformation,” the President said.

The president noted that a sound business environment and regulatory landscape have allowed enterprises, both large and MSMEs to thrive and effectively address the problem of unemployment, especially among the youths.
He added that the quest for inclusive development requires dramatic transformation of mind-sets and attitudes as well.

For his part, REPOA Executive Director Prof Samwel Wangwe said that reviews of trends in growth, employment and poverty in Tanzania have highlighted challenges and risks of achieving high growth which is not accompanied with the requisite transformation of the economy and widespread job creation.

“This signifies the challenge of low productivity and low returns to labour in agriculture and micro and small enterprises is predominantly in the informal economy where majority of Tanzanians derive their livelihoods from,” he said.

He added: “The low returns to labour in agriculture push people out of the sector in search of alternative sources of employment, but most of this migrating labour ends up in the lowest end of the non-farm sectors, mainly trade, other services and a few in manufacturing activities.”

He also said that the resulting kind of urbanisation where the informal economic activities provide low returns to labour carries with it the risk of turning rural poverty into urban poverty.

He insisted that there is a quest for deeper understanding of what it would take to transition from rural and urban poverty to prosperity in both the rural and urban economy.

The main objective of the two-day workshop is to achieve deeper understanding of the dynamics of micro and small scale economic activities and identify options for managing the enterprise transformation process with a view to realising more inclusive growth. 

Share:

Bunge Maalum laanza kusikiliza taarifa za Kamati


Bunge Maalum laanza kusikiliza taarifa za Kamati

Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta amesema mjadala kuhusu  taarifa za Sura ya Kwanza na ya Sita za Rasimu  ya  Katiba  ya Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania unatarajia kuanza wiki ijayo katika Bunge hilo mara baada ya kumaliza kupokea taarifa za Kamati.
 Sitta  alisema hayo  katika ukumbi wa Bunge hilo mjini Dodoma baada  baadhi ya wajumbe kumwomba  kuchangia mjadala wakati ripoti hizo zikiendelea kuwasilishwa.
 Alisema mdajala wa kuchangia sura hizo utaanza mara baada  ya   Kamati 12 za Bunge Maalum la Katiba  kuwasilisha  taarifa zao  za Sura ya Kwanza na ya Sita  kuhusu  Rasimu ya  Katiba  ya Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania katika Bunge hilo.
 Aliongeza kuwa  kwa kujibu wa Kanuni ya namba 33(6) ambayo inasema baada ya  hoja za taarifa za Kamati  Namba Moja  hadi Namba Kumi na Mbili kutolewa katika Bunge Maalum na Mwenyekiti kuelekeza hoja hizo zijadiliwe , mjadala kuhusu taarifa hizo utaanza.
 Mwenyekiti huyo aliwataka baadhi ya wajumbe hao kusubiri mpaka uwasilishaji wa taarifa hizo utakapokamilika ndio watapata nafasi  ya kuchangia kwa muda mrefu  na kuwezesha wajumbe wengi kupata nafasi hiyo.
Share:

Wednesday 9 April 2014

VIDEO:UOZO MTUPU ANGALIA WANAFUNZI HAWA MAMBO WANAYOYAFANYA


Share:

VIDEO:AFUMANIWA NA MME WA MTU CHUMBANI KWAKE AKUTWA NA HIRIZI ZA KUTOSHA


Share:

VIDEO:KANGA MOJA WAKIWA NDANI YA TANGA-LAKI SI PESA MILIONI MATUMIZI


Share:

Tuesday 8 April 2014

VIDEO:JAMAA AFUMANIWA NA MKE WA MTU


Share:

VIDEO:JINSI YA KUSOMA SMS ONLINE BILA YA MWENYE SIMU KUJUA

SOMA KUPITIA HAPA...........BONYEZA

Share:

VIDEO: LOOK HERE THE WONDERS OF GAUCHO


Share:

SOMA HABARI HIZI KUHUSU MASTAA WA BONGO

MASTAA MATAJIRI WACHUNGUZWA



KIMENUKA! Jeshi la Polisi Tanzania kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za serikali zimeanza kuwachunguza watu wenye majina makubwa ‘mastaa’ Bongo ambao wameibuka na utajiri wa ghafla, Uwazi limeambiwa.
Masanja Mkandamizaji.
Kwa mujibu wa chanzo nyeti ambacho kiko ‘jikoni’ kwenye jeshi hilo, mbali na mastaa, wengine ambao tayari orodha yao ipo ni wafanyabiashara, wafanyakazi wa serikali na viongozi wa dini ambao wameibuka kuwa mamilionea kwa muda mfupi huku shughuli zao za…

ANAYEISHI KWENYE HANDAKI BALAA JIPYA!


CHACHA Makenge (38) aliyeripotiwa awali kuishi ndani ya handaki katika eneo la pori la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam sehemu ya Mlimani, amepatwa na balaa jipya baada ya makazi yake kuvamiwa na askari, kukamatwa na mwishowe kupelekwa Muhimbili kitengo cha wagonjwa wa akili kwa ajili ya matibabu.
Chacha Makenge (38) akiota moto nje ya handaki lake katika eneo la pori la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam sehemu ya Mlimani.
Kana kwamba haitoshi, Makenge ambaye aliwahi kuishi…

MAAJABU YA MUNGU!


KATIKA hali ya kushangaza, wagonjwa wa mtindio wa ubongo, Paul Ngido na Asha Yahya wanaolelewa kwenye kituo cha watoto wenye matatizo mbalimbali wakiwemo yatima cha Ngido kilichopo Mazimbu FK mkoani hapa wamejikuta wakizaa watoto wawili, Keisha na Glory ndani ya kituo hicho.
Paul Ngido na Asha Yahya  wanaolelewa kwenye kituo cha watoto wenye matatizo mbalimbali waliowazaa watoto Keisha na Glory.
Mkurugenzi mkuu wa kituo hicho, Linda Cyprian Ngido amethibitisha kutokea…

NJEMBA YAMBAKA MTOTO WA MIAKA MINNE


NI AIBU!Jamaa mmoja anayejulikana kwa jina la Iddi Mgosi anashikiliwa na Polisi wa Kituo cha Wazo jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka minne (jina linahifadhiwa) huko Mivumoni, Madale Machi 18, mwaka huu.
Mtoto wa miaka minne aliyefanyiwa unyama huo.
Mgosi, ambaye umri wake haukuweza kupatikana mara moja, anadaiwa kumrubuni mtoto huyo kutoka nyumbani kwao na kumpeleka kwake, ambako alimuingilia kwa nguvu na baadaye kumtisha…

TATIZO LA MACHINGA LINATAKA BUSARA

NINAWASALIMU kwa jina la Bwana Mungu, mwingi wa rehema na muweza wa kila jambo. Siku zote nimekuwa nikiwasihi kumuweka mbele muumba wa nchi na mbingu, kwani kwake hakuna lisilowezekana.
Wagambo wakiwa kazini katika operesheni bomobomoa maeneo ya Posta mpya.
Hivi sasa kuna kampeni kubwa ya kusafisha jiji kwa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Temeke na Kinondoni kubomoa vibanda vya biashara vilivyojengwa kinyume na taratibu katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Jambo hilo limesababisha usumbufu mkubwa kwa wakazi wa jiji…

UNAKUBALIKA KWENYE JAMII-2

BADO tunaendelea na somo letu ambalo safari hii nagusia upande wa maisha. Ndugu zangu, kukubalika kwenye jamii kuna manufaa makubwa kama nilivyosema wiki iliyopita.

Niliishia pale nilipofafanua hasara za kutokubalika kwenye jamii. Sasa leo tuendelee.
KWA NINI HUKUBALIKI?

Wakati naanza kabisa kuandika mada hii, nimeeleza kwamba kila kinachotokea duniani huwa na sababu zake. Haiwezekani ukawa hukubaliki kwa chuki za watu au watu kukuonea wivu.

Lazima kuna sababu zinazosababisha usikubalike. Najua kila mmoja anaujua ukweli wa maisha yake ndani ya moyo wake.
Hapa nitakuandikia sababu muhimu…

MBWA WALIOMLA MTOTO NUSURA WAMLE BABA MTU

Mtoto Christian Alex aliyeliwa na mbwa enzi za uhai wake.


ZIMEKATIKA wiki mbili tangu kuzikwa kwa mtoto Christian Alex (6)  aliyeuawa kwa kushambuliwa na mbwa watatu waliodaiwa ni wa Ubalozi wa Qatar nchini, mbwa hao wamemkosakosa baba mtu.

Tukio la kuuawa kwa mtoto huyo lilijiri Kunduchi  Jangwani Beach jijini Dar Machi  26, mwaka huu.
Kwa mujibu wa chanzo, mara baada ya kumaliza shughuli ya kumzika marehemu katika Makaburi ya Mburahati jijini Dar, baba mzazi Alex Augustino alikaa kikao na ndugu ili kuangalia uwezekano wa kufika kwenye makazi hayo ya ubalozi na kuzungumza nao kujua hatima ya sakata hilo.
Baada ya makubaliano,…

TUZO YA MWANAMKE BORA, HESHIMA YA KWELI YA MWANAMKE, PINDA NI MSOMI WA UWAZI


Mgeni rasmi, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akihutubia kabla ya kukabidhi tuzo.

Mwanamke wa…

TUUCHOKONOE, TUUPINDUE ILI TUUBORESHE

WAJUMBE wa Bunge Maalum la Katiba wanaendelea na mchakato wa kupitia vifungu vya Rasimu katika ngazi ya kamati, kabla ya keshokutwa kuanza rasmi mjadala wa namna gani Tanzania inaweza kupata katiba mpya, miaka 50 baada ya kuungana kwa nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar.
Katika hatua za awali ngazi ya kamati, tumeshuhudia mambo mengi hasa yanayohusu hatima ya Muungano, ambao umekuwa ndiyo simulizi kuu katika mchakato mzima.
Kwa miaka mingi Watanzania tumeishi tukiaminishwa kuwa Muungano huu uko safi na yeyote aliyeonekana kuuzungumzia kwa namna ya kuukosoa, alichukuliwa kama msaliti, mhaini na mtu asiye na nia njema na nchi yetu.
Mambo mengi yanayohusu uhusiano wa nchi hizi mbili umekuwa siri kubwa, baadhi ya mambo yameharibika au kwenda mrama kwa kuwa kila mmoja alikuwa hataki kuonekana…

Share:

ANGALIA MAJINA HAPA YA WALIOPANGIWA VITUO VYA AFYA (AJIRA) 2013/2014

Share:

SOMA MAGAZETI YA LEO 08/04/2014

1_df6c1.jpg
2_60742.jpg
3_abfda.jpg
4_146e8.jpg
5_46469.jpg
6_6457f.jpg
66854_688389021225559_7905396027206939490_n_b7655.jpg
984038_688393924558402_8227931919131465226_n_48ad2.jpg
1012133_688388851225576_7974244423289239200_n_15ad8.jpg
1511914_688393854558409_4524716445678454352_n_6ca0e.jpg
1618432_688389154558879_4227702238964895763_n_49548.jpg
10150701_688389124558882_2727082128162427829_n_1_968cf.jpg
10151186_688392871225174_6366814600379550084_n_ab357.jpg
10154011_688392311225230_3505961519200983127_n_a0890.jpg
10155426_688398157891312_7651917783195626200_n_35ea1.jpg
10171238_688389074558887_9140776556010772895_n_46b35.jpg
Share:

Monday 7 April 2014

VIDEO:ANGALIA FUMANIZI HILI HATARI SANA MKE WA MTU SUMU


Share:

MATOKEO YA AWALI UCHAGUZI CHALINZE

Share:

VIDEO:ANGALIA LIVE SHOW YA KHANGA MOJA ILIVYOFANA


Share:

Thursday 3 April 2014

VIDEO:MTOTO ALIEZALIWA AKIWA HANA UBONGO


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger