Sunday, 31 August 2025

UZINDUZI WA KAMPENI ZA UCHAGUZI MKUU 2025 GEITA SEPTEMBA 2

 


#MchagueSamia
#MchagueBiteko
#KusemaNaKutenda
#KaziNaUtuTunasongaMbele
#OktobaTunatiki
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI AGOSTI 31,2025

 

magazeti    

  
Share:

Saturday, 30 August 2025

CHUO KIKUU HURIA NA JESHI LA POLISI RUVUMA WATOA MSAADA KITUO CHA WATOTO YATIMA CHIPOLE



Na Regina Ndumbaro, Songea – Ruvuma

Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma kimetoa msaada kwa Kituo cha Kulelea Watoto Yatima cha Chipole kilichopo Kata ya Magagura, Halmashauri ya Songea Vijijini. Msaada huo ulihusisha fedha taslimu shilingi milioni moja na laki mbili (1,200,000) pamoja na mahitaji muhimu kama vyakula, nguo na bidhaa nyingine za matumizi ya kila siku.

Akizungumza wakati wa makabidhiano, Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu Huria, Vincent Mpepo, alisema kuwa waliguswa na hali ya watoto hao baada ya kuona picha na video zilizosambazwa na Inspekta Dominic Msangi, Polisi Kata wa Magagura, ambazo zilionesha mazingira ya kituo hicho na kuhamasisha wadau kujitokeza kusaidia.

Mpepo ameeleza kuwa msaada huo ni mwanzo wa safari ya ushirikiano kati ya chuo hicho na kituo hicho, na kuahidi kuwa wataendelea kujitokeza kadri watakavyoweza ili kusaidia watoto hao kupata maisha bora.

 Pia amesema wana mpango wa kufadhili bima za afya kwa watoto 50, jambo litakalosaidia sana katika kukabiliana na changamoto za matibabu.

Kwa upande wake, Inspekta Msangi alieleza kuwa hatua hiyo ni utekelezaji wa mkakati wa Kamishna wa Polisi Jamii wa kushirikiana na wadau kusaidia jamii, hasa makundi maalum kama watoto yatima, kwa lengo la kuimarisha mshikamano na huruma miongoni mwa Watanzania.

Akizungumza kwa niaba ya kituo, Mtawa Maria Akwinata kutoka Shirika la Watawa wa Chipole alishukuru kwa msaada huo na kueleza kuwa kituo hicho kinalea watoto wa rika mbalimbali kuanzia wanaozaliwa hadi kufikia elimu ya sekondari, hivyo mahitaji yao ni makubwa na yanahitaji msaada wa mara kwa mara kutoka kwa jamii.

Mmoja wa watoto wa kituo hicho, Richard Haule, ameeleza kufarijika kwao kwa kutembelewa na kusaidiwa, akisema kuwa msaada huo umeonyesha kuwa bado wanakumbukwa na jamii.

 Ametoa wito kwa taasisi na watu binafsi kuendelea kujitokeza kusaidia ili kuwajengea watoto hao matumaini na mustakabali mzuri wa maisha.





Share:

WADAU WA UTALII WAZIDI KUITIKIA WITO WA SERIKALI.


-Hoteli ya Kifahari ya Mapito Safari Camp yazinduliwa rasmi Serengeti

Matokeo ya jitihada kubwa za Serikali ya Tanzania kutangaza vivutio pamoja na kuvutia wawekezaji wa kimataifa kuja kuwekeza nchini zinazidi kuzaa matunda kwani alhamisi, Agosti 29, 2025 imezinduliwa hoteli ya Mapito Safari Camp katika kijiji cha Robanda, Serengeti iliyojengwa na kampuni kubwa na maarufu ya hoteli duniani kutoka nchini Marekani ya Marriott.

Dkt. Thereza Mugoba, Mkurugenzi wa Idara ya Utalii Wizara ya Maliasili na Utalii ameshiriki uzinduzi huo akimuwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi, hafla hiyo pia pamoja na wageni wengine imehudhuriwa na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania Bw. Andrew Lentz.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI AGOSTI 30,2025




Magazeti


Share:

Friday, 29 August 2025

NABII RABIEL KUFANYA MAOMBI YA TAIFA

 


Nabii Rabiel Akyoo wa Kanisa la Ukombozi akiongea na waandishi wa habari 


Na Woinde Shizza Arusha Arusha

Nabii Rabiel Akyoo wa Kanisa la Ukombozi anatarajiwa kuongoza maombi ya kitaifa kesho jijini Arusha kwa lengo la kuliombea taifa kudumisha amani na mshikamano wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu.


Akizungumza na waandishi wa habari Nabii Akyoo alisema maombi hayo yatakusanya waumini kutoka maeneo mbalimbali nchini na yatakuwa na ajenda kuu ya kuombea utulivu na mshikikano wa taifa.


“Ni wajibu wa kila Mtanzania kulinda amani Ikitoweka, hakuna kazi, hakuna kipato, na maisha yatakuwa magumu kwa kila mmoja wetu,” alisema.


Sambamba na maombi hayo, kutafanyika harambee ya kuchangia kituo kipya cha habari cha kanisa hicho, kitakachojumuisha televisheni na redio, huku sera yake ikizinduliwa rasmi.


Katika siku hiyo pia kutakuwa na burudani ya nyimbo za injili kutoka kwa waimbaji mbalimbali maarufu akiwemo Upendo Nkone, anayetarajiwa kupamba maombi kwa nyimbo zake za kumsifu Mungu.


Waumini na wananchi wataungana kushiriki ibada ya Meza ya Bwana, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha mshikamano wa kiroho na taifa kwa ujumla.


Nabii Akyoo aliwaasa Watanzania kujitokeza siku ya kupiga kura kwa amani na utulivu, akisisitiza kuwa kura ni sauti ya kila raia, lakini amani ya taifa ni urithi wa kudumu.


“Kura yako ni sauti yako, lakini zaidi ya yote, amani ya taifa letu ndiyo urithi mkubwa tunaopaswa kuudumisha,” alisema Nabii huyo.


Maombi hayo yanatarajiwa kuhudhuriwa na waumini wa madhehebu mbalimbali, viongozi wa dini na wananchi kutoka mikoa tofauti, huku Arusha ikitarajiwa kuwa kitovu cha ibada kubwa ya taifa

Share:

Thursday, 28 August 2025

SHEHENA YA MAGARI INAYOPITA BANDARI YA TANGA INAHUDUMIWA KWA UMAKINI MKUBWA

 


Na Oscar Assenga,TANGA

MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA)  Bandari ya Tanga  imesema kwamba wanatumia umakini mkubwa na ufanisi katika kuhudumia shehena  mbalimbali zinazopita kwenye Bandari hiyo ikiwemo ya magari ambayo imekuwa ikiongezeka kila mara

Hayo yalisemwa na Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga  Bw. Peter Millanzi alipokuwa akitoa ufafanuzi juu ya taarifa zilizosambaa kwa baadhi ya mitandao kuwa  uwepo wa wizi wa baadhi ya vifaa kwenye magari ambayo yanapitia katika Bandari hiyo jambo ambalo limewashangaza kutokana na umakini wao katika kuhudumia shehena hiyo.


Millanzi alisema kwamba , shehena ya mzigo unaopita wanaouchukulia kwa umakini zaidi ambayo watu wengi wana masilahi yao  binafsi  ambapo wametengeneza utaratibu wa kuhakikisha mizigo yote inayoingia na kutoka  bandarini hapo  ipo salama na inafika kwa wateja ikiwa salama.

“Kwa hiyo katika kuhudumia shehena hizo ikiwemo magari kwa tunatengeneza utaratibu ambapo meli inapotia nanga bandarini lazima kuwepo na taasisi mbalimbali ikiwemo Wakala wa Meli (TASAC),Survey, na TPA kwa hiyo magari yanapoteremka yanakaguliwa na  kurekodiwa taarifa zake kwenye fomu maalumu inayoitwa  “VDITT”inaonyesha hali halisi ya gari lilivyopokelewa bandari hapo  na kuna maeneo mbalimbali yanawekwa alama ya vema kuonyesha vifaa ambavyo vilivyoanishwa havijanyofolewa” Aliongeza Millanzi 



“Lakini pia yapo magari tunayapokea yakiwa yamenyofolewa na yenyewe tunaonyeshwa kwenye ile fomu na hao wote waliotajwa wanashuhudia kile kilichojazwa  na yapo makubaliano baada ya kujaza jinsi hali halisi gari lilivyopokelewa kwenye bandari na kutiliana saini ya makubaliano  na hilo gari linapelekwa eneo la kuhifadhi” Alisema Millanzi 

Aidha alisema kwamba katika eneo la kuhifadhi kuna watu wanapokea wa ulinzi na makarani kisha kusaini  ili kuonyesha kwamba magari waliopokea ni sawa na vile walivyojaza na magari yanapokuja kuchukuliwa na mteja anasaini baada ya kulikagua gari lake na wakijiridhisha wanatoa ushuhuda gari lake amelipokea kama lilivyopokelewa  bandarini hapo.


“Baada ya hapo anasaini na kulichukua kwenda zake kiujumla kipindi chote  hatujawahi kupokea tukio lolote la malalamiko kwamba gari limenyofolewa  au kuharibiwa likiwa  mikononi  mwa bandari.”Alisema Kaimu Meneja huyo wa Bandari ya Tanga.

katika hatua nyingine Milanzi alisema kwamba hivi sasa wameongeza ufanisi mkubwa katika kuhudumia shehena hususani Magari kutokana na uwepo wa maboresho makubwa yaliyofanywa na Serikali kwa kutumia kiasi cha Sh.Bilioni 429.1 na hivyo tokea walipoanza kuhudumia magari imepita mwaka mmoja


Millanzi alisema kwamba, kutokana na uwekezaji huo shehena ya Magari imekuwa ikiongezeka mwezi hadi mwezi kutokana kuongezeka kwa ufanisi katika  kuhudumia shehena mbalimbali na hivyo wenye meli na wateja wameamua kupitisha mizigo yao katika Bandari ya Tanga na  magari yalianza kupitia bandari hiyo mwezi Agosti mwaka 2024 .


Alisema kwamba na takwimu zilizopo zinaonyesha kuwa kuanzia mwezi Agosti,  2024 hadi  mwezi Julai , 2025 wameweza kuhudumia meli 45 zilizokuwa zimebeba shehena ya magari na magari yaliyohudumiwa ni magari 9,665 na wamepata bahati ya kupata wateja na mawakala mbalimbali ambao wameamua kupitisha shehena ya magari katika bandari hiyo.


“Shehena hizo za magari yanapita hapa nchini na mengine nje ya nchi kama unavyojua Tanzania imepakana na nchi nyingi ambazo hazipakani na bahari kama vile Rwanda,Burundi,Kongo,Uganda ,Malawi,Zambia na nchi nyengine iliyopo mbali zaidi lakini kutokana na kuwepo huduma bora imeamua kupitisha mizigo yake ni  Zimbambwe  “ Alisema Millanzi


Alieleza pia wamekuwa na vikao mbalimbali na wadau ili kuweza kuona kama kuna changamoto wanakutana nazo ili kuzipatia ufumbuzi kwa kufikia viwango vya juu na meli zinapofika Bandarini kupeleka shehena ya mbalimbali ikiwemo magari zinahudumiwa kwa muda wa saa 72 iwapo mteja amekamilisha taratibu zote za kiforodha mara gari linapopokelewa anayofursa ya kuchukua gari lake.


 -

Share:

ASKARI AVUA SARE KAZI BAADA YA KUPATA HABARI MKEWE ANAISHI NA MCHUNGAJI


Askari mmoja wa kituo cha polisi aliibua mshangao baada ya kuamua kuvua sare hadharani na kutangaza kuacha kazi mara moja. Tendo hilo lililotokea karibu na kituo cha polisi mchana wa saa saba liliwashangaza wengi, huku wakazi wakijitokeza kwa wingi kushuhudia. Wengi walidhani huenda askari huyo alipata mshtuko wa akili, lakini muda si mrefu ukweli wa kusikitisha ulifichuka.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger