RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi ametoa salamu za pole kwa familia, ndugu jamaa wa marafiki kufuatia kifo cha mtangazaji mkongwe wa ZBC televisheni, Bi.Sharifa Maulid.
Katika salamu hizo za pole, Rais Dkt. Mwinyi ameeleza kusikitishwa na kifo cha mtangazaji huyo mkongwe na kuisihi familia ya marehemu kuwa na subira katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo.
“Natoa mkono wa pole kufuatia kifo cha mtangazaji mkongwe wa ZBC televisheni, marehemu bibi Sharifa Maulid, naukumbuka umahiri wake katika utangazaji kwani alikuwa hodari katika kazi yake hiyo na kazi zake nyingine alizozifanya mbali ya utangazaji,”ilieleza sehemu ya salamu za pole alizozitoa Rais Dkt.Mwinyi.
Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amewasihi watangazaji na wafanyakazi wote wa sekta ya habari nchini kufuata nyayo na uzalendo wa marehemu bibi Sharifa Maulid ambaye hadi anafariki dunia alikuwa Afisa Habari katika Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto.
Rais Dkt. Mwinyi amemuomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, Amin.






Mashemasi wakitia saini viapo vyao mbele ya Askofu
Mashemasi wakirudi katika nafasi zao baada ya kusaini viapo vyao
Vicar wa Shirika la Wakapuchini kanda ya Tanzania Pd.Paschal Vincent Dohho (mwenye kanzu ya Ugoro) akiwa katika ibada ya masifu ya jioni Kanisa kuu Ngokolo
Askofu Sangu akiwa katika picha ya pamoja na Mashemasi mara baada ya Ibada ya Masifu ya jioni(Kushoto ni Katibu wa askofu Pd. Deusdedith Kisumo na Kulia ni Paroko wa Parokia ya Mwadui Pd.Michael Msabila)































