Wednesday, 31 July 2019

Waziri Kigwangalla atoa siku Saba kwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Khamis Kigwangalla, ameipa siku saba Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), kuhakikisha wanapeleka mapendekezo ya namna gani watawahakikishia wawekezaji malighafi.

Katika mapendekezo hayo, amewataka kila mwaka walau kwa kipindi kisichopungua miaka mitano waweze kukopesheka kwa urahisi.

Dk. Kigwangalla amesema hayo, alipokuwa akizungumza katika mkutano wake na wadau wa Sekta ya Misitu uliofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, ambapo amesikiliza changamoto zinazowakabili na kuahidi kuzifanyia kazi.

“Kuhusu suala la mikataba ya kuwazia wadau wetu vitalu, TFS ninawapa siku saba mniletee mapendekezo ya kina ni kwa namna gani tunaweza kuwahakikishia wadau wetu ambao ni wawekezaji kwenye viwanda kwa sababu tuna uwezo wa kuwatambua sasa tunawezaje kuweka utaratibu ambao utawahakikishia malighafi kila mwaka walau kwa kipindi kisichopungua miaka mitano ili waweze kukopesheka kwa urahisi ,” amesema.

“Hili ni jambo ambalo halipaswi kushindikana hivyo mjipange mtakavyoweza lakini mtuletee wizarani mapendekezo ni kwa namna gani mtaweka uhakika kwa wadau wetu ambao ni wawekezaji kwenye sekta ya bidhaa ya misitu watapa malighafi kwa uhakika walau katika kipindi cha miaka mitano,” amesema.

Aidha amesema kuwa kwa mwaka Tanzania inaharibu misitu katika eneo la ukubwa wa hekari laki 4.5, ambapo amewapongeza wakazi wa mikoa kusini na baadhi ya mikoa ya Kaskazini na Kaskazini Magharibi kwa jitihada wanazozifanya za kupanda miti kibishara kwa kusema wanasaidia katika ikolojia ya maisha duniani,” amesema Dk. Kigwangalla.


Share:

Tamko la CHADEMA juu ya kukamatwa Mwandishi na kufariki Ofisa wa Wizara ya Fedha

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa waraka kwa waandishi wa habari ambapo wametaka ufafanuzi juu ya matukio mbalimbali yanayotokea nchini ikwemo kukamatwa kwa Mwandishi wa habari za uchunguzi Erick Kabendera na kifo cha Ofisa wa Wizara ya Fedha.


Share:

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMATANO


Manchester United wana nia kusaini mkataba na kiungo wa kati- nyuma wa Barcelona na Ufaransa Samuel Umtiti

Manchester United wana nia kusaini mkataba na kiungo wa kati- nyuma wa Barcelona na Ufaransa Samuel Umtiti, mwenye umri wa miaka 25. (Le10 Sport )

Paris St-Germain wameweka turufu yao ya uhamisho wa mshambuliaji wao Neymar mwenye umri wa miaka 27 kwa Barcelona. (Marca)

Arsenal wanakamilisha mkataba kwa ajili ya mchezaji wa safu ya kushoto-nyumba wa Celtic na Uskochi Kieran Tierney, mwenye umri wa miaka 22. (Mail)Haki miliki ya pichaREUTERSImage captionParis St-Germain wameweka turufu yao ya uhamisho wa mshambuliaji wao Neymar kwa Barcelona

Kiungo wa safu ya mashambulizi wa Inter Milan na Argentina Mauro Icardi, mwenye umri wa miaka 26, anaweza kuwa anaelekea Napoli kwa mkataba wa euro milioni 80 (£73m) . (Corriere dello Sport - in Italian)

Crystal Palace wameweka dau la takriban pauni milioni 14 kwa ajili ya mshambuliaji wa timu za CSKA Moscow na Urusi -Fedor Chalov mwenye umri wa miaka 21 . (Sky Sports)

Mkurugenzi mkuu wa Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge anasema hakuelewa ni kwanini meneja Niko Kovac alisema kuwa klabu hiyo inaamini itasaini mkataba na winga Mjerumani Leroy Sane ambaye anaichezea sasa Manchester City akiwa na umri wa miaka 23. (Bild - in German)Mauro Icardi, mwenye umri wa miaka 26, anaweza kuwa anaelekea Napoli

Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane anasema kuwa hafahamu ikiwa kiungo wa kati wa mashambulizi wa timu ya Colombia -James Rodriguez mwenye umri wa miaka 28 atakuwa kwenye klabu hiyo msimu ujao. (Marca)

West Brom hawajapokea ofa yoyote kutoka kwa Aston Villa kwa ajili ya winga wa uskochi Matt Phillips, mwenye umri wa miaka 28. (Birmingham Mail)

Mlindalango wa Newcastle na England wa kikosi cha walio chini ya umri wa miaka -21 Freddie Woodman,ambaye ana umri wa miaka 22, analengwa na Celtic na Arsenal, pamoja na klabu ambazo hazijatajwa za Championi. (Chronicle)Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane anasema kuwa hafahamu ikiwa James Rodriguez atakuwa kwenye klabu hiyo msimu ujao

Newcastle wamekataliwa dau la pauni milioni 4.5 kwa jili ya kiungo wa kulia nyuma wa Amiens na Sweden Emil Krafth mwenye umri wa miaka 24 . (Sun)

Mchezaji wa klabu ya Partizan ya Serbia anayecheza safu ya kati-nyuma Strahinja Pavlovic, mwenye umri wa miaka 18, "ameshangazwa " na tetesi zinazomuhusisha na kuhamia Celtic. (Daily Record)Freddie Woodman , analengwa na Celtic na Arsenal

Meneja wa zamani wa Chelsea na Manchester United Jose Mourinho atarejea katika utawala wakati fursa itakapojitokeza. (Sky Sports)

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Teddy Sheringham anasema Ole Gunnar Solskjaer anapaswa kumuuza kiungo wa kati Mfaransa Paul Pogba mwenye umri wa miaka 26. (Talksport)Jose Mourinho atarejea katika utawala fursa itakapojitokeza

Kiungo wa kati wa Atletico Madrid Koke anasema kuwa anaamini mshambuliaji wa Ureno Joao Felix mwenye umri wa miaka 19-atakuwa "mmoja wa wachezaji bora zaidi duniani . (ESPN)

Preston North End wamekatalia mbali dau la deni kutoka kwa Wigan Athletic kwa ajili ya kiungo wa kati Daniel Johnson mwenye umri wa miaka 26-mzaliwa wa Jamaica. (Lancashire Evening Post)

CHANZO.BBC SWAHILI
Share:

Tuesday, 30 July 2019

POLISI WATAJA SABABU ZA KUMSHIKILIA MWANDISHI WA HABARI ERICK KABENDERA


Kamanda Lazaro Mambosasa

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa amesema Jeshi la Polisi linamshikilia kwa mahojiano mwandishi wa habari Erick Kabendera aliyekamatwa Julai 29, 2019 nyumbani kwake maeneo ya Mbweni Jijini Dar es Salaam.

Kamanda Mambosasa amesema, mtuhumiwa huyo alikamtwa baada ya kukataa wito wa polisi ambapo awali aliandikiwa barua ya wito kwa ajili ya mahojiano, lakini alikaidi kutii wito huo na kusema kwamba, jeshi la polisi linapomuita mtu kwa hiari na akaacha kutii wito huo, hutumia mbinu ya kumlazimisha atii.

''Baada ya kukamatwa mwandishi huyo, tulisikia taarifa mbalimbali kutoka kwa kada mbalimbali kwenye jamii wakiendelea kusema mwandishi huyo alitekwa niseme kuwa, mwandishi huyo hakutekwa aliitwa, lakini kwa jeuri alikaidi kutii wito huo, sababu pia ya kuitwa ni kuhusiana na utata wa uraia wake, Jeshi linaendelea na upelelezi kwa kushirikiana na maafisa wa uhamiaji'', amesema SACP Mambosasa.

Aidha Kamanda Mambosasa ameongeza kuwa, baada ya upelelezi kukamilika jeshi hilo litahakikisha kosa analotuhumiwa nalo mwandishi huyo, linawekwa mezani ili na yeye aweze kuhakikishia kama ni mtanzania kwa kutoa vielelezo vinavyothibisha uraia wake.
Share:

UTEUZI MWINGINE KUTOKA IKULU MUDA HUU

Share:

Ofisa FEKI Wa jeshi la Polisi Atiwa Mbaroni

Jeshi la Polisi kanda maalum Dar es Salaam linamshikilia Daudi Ramadhani Iddy (23) mkazi wa Tabata Segerea kwa kujifanya ofisa wa Polisi, akiwa amevaa sare za Jeshi la Polisi na cheo cha mkaguzi msaidizi wa Polisi( Assistant Inspector).

July 19, 2019 Jeshi la Polisi lilipata tarifa toka kwa askari wa Jeshi la kujenga taifa (JKT) makao makuu Mlalakuwa, kuwa kuna kijana mmoja amevaa sare za Jeshi la Polisi wana mashaka naye.

Makachero wa Jeshi la Polisi walifika makao makuu ya JKT kumkamata na kufanya naye mahojiano,mtuhumiwa alikiri kujifanya yeye ni afisa wa Polisi na kufanya utapeli.

Pia alikiri kupitia mafunzo Jkt huko Mafinga mwaka 2006 na kujitolea kwa mujibu wa sheria katika kambi hiyo.

Mtuhumiwa alifanyiwa upekuzi na kupatikana na vifaa vifuatavyo; 
1.Sare moja ya Polisi aina ya kaki 
2. Vyeo vya(Cpl, Sgt na cheo cha mkaguzi msaidizi
 3 Pea moja inaya kombati Jungle green. 
4.Pingu moja. 
5.Kofia moja ya askari wa usalama barabarani. 
6.Radio ya upepo moja aina ya motorola
7 Mikanda miwili ya Jkt.
8.Mkanda mmoja wa bendera wa Jeshi la Polisi, buti na viatu vya kawaida.

Kamanda Mambosasa amesema upelelezi wa kina unaendelea na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayomkabili.


Share:

Anayedaiwa kumuua na kumchoma mkewe Apandishwa Kizimbani

Mfanyabiashara Khamis Luwongo (Meshack), anayetuhumiwa kumuua mkewe na kumchoma kwa magunia mawili ya mkaa, amepandishwa kizimbani kwa tuhuma za mauaji ya kukusudia.

Akisoma hati ya mashtaka Wakili wa Serikali Mwandamizi Wankyo Simon amedai leo mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Salum Ally kuwa mshtakiwa anatuhumiwa kwa kosa moja la mauaji  kinyume cha Sheria ya kanuni ya adhabu namba 196 sura 16 kama kilochofanyiwa marejeo mwaka 2002.

Katika kesi hiyo ya mauaji namba 4 ya mwaka 2019, mshtakiwa Luwonga Mkazi wa Kigamboni, Dar es Salaam anadaiwa Mei 15,mwaka huu wa 2019 akiwa Gezaulole eneo la Kigamboni alimuua Naomi Marijani. 

 
Mshtakiwa hakutakiwa kujibu lolote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.

Upelelezi wa kesi hiyo unaendelea ambapo mshtakiwa amepelekwa gerezani hadi Agosti 13, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa.


Share:

MKUU WA MKOA AWASHANGAA MADIWANI MANISPAA YA SHINYANGA KUVUNJA KIKAO CHA BARAZA,AKIRI MADUDU.. AAGIZA WATENGUE KAULI ...WAUFYATA!


Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani wa Manispaa ya Shinyanga leo

Na Marco Maduhu - Malunde1 blog Shinyanga.

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack, ameagiza madiwani wa manispaa ya Shinyanga kutengua maamuzi yao ya kumkataa mkurugenzi wa halmashauri hiyo Geofrey Mwangulumbi, kwamba hawakufuata kanuni na taratibu.


Amesema jambo walilolifanya madiwani hao ni ukiukaji wa kanuni na taratibu, ambapo walipaswa kuitisha kikao maalumu pamoja na kumpeleka malalamiko hayo kwake ili ayafanyie kazi, lakini alishaghaa kusikia tu kikao cha baraza la madiwani kimevunjika madiwani wakimkataa mkurugenzi kutokuwa na imani naye.



Telack amebainisha hayo leo Julai 30, 2019 kwenye kikao cha kawaida cha baraza la madiwani la manispaa ya Shinyanga, ambapo madiwani hao waliamua kuendelea na baraza hilo mara baada ya kutengua maamuzi yao ya jana ya kuvunja kikao cha baraza kwa madai ya kumkataa mkurungezi kutokuwa na imani naye.


Mkuu huyo wa mkoa amesema baraza hilo haliwezi kuendelea kuwepo, endapo kama madiwani hawatatengua maamuzi yao ya kumkataa mkurugenzi, ikiwa kanuni na taratibu zilikosewa kufuatwa.

Kutokana na hali hiyo, madiwani hao walitengua maamuzi yao na kisha kikao cha baraza kuendelea na kujadili ajenda mbalimbali kwa ajili ya maendeleo ya manispaa hiyo.


“Taarifa hizi za kumkataa mkurungenzi nilizipata toka juzi nikaona ngoja niwapime upeo wenu madiwani kama mtafuata kanuni na taratibu... lakini nikashangaa tu mmechukua maamuzi, mkavunja kikao cha baraza bila ya kufuata taratibu, hivyo naagiza maamuzi yenu myatengue kwanza ndipo muendelee na kikao, tofauti na hapo baraza lenu ni batiri,”amesema Telack.


“Ninachotaka kusema madiwani achaneni na malumbano yasiyo na maana kwa kuvunja tu vikao bila ya kufuata taratibu, pale penye mapungufu tuwasiliane ili tuweze kwenda pamoja, nafahamu mapungufu ya manispaa hii, ni kweli yale ambayo mnalalamikia juu ya maazimio yenu kutotekelezwa mko sahihi kabisa,”ameongeza Mkuu wa mkoa.


Aidha amesema tatizo ambalo linasababisha migogoro hiyo kuwepo ni kutoelewana kati ya watumishi wa halmashauri na mkurugenzi wao, sababu kila mtu ni mbabe, na hivyo kusababisha miradi mingi kuwa na usimamizi mbovu na kutotekelezeka, na ndio maana maazimio yenu hayafanyiwi kazi.


Naye Katibu Tawala la mkoa wa Shinyanga Albert Msovela, amewataka watumishi wa manispaa hiyo, madiwani, pamoja na mkurugenzi, kuzungumza lugha moja ili kuondoa makandokando yaliyopo na kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi.


Kwa upande wake Naibu Meya wa manispaa hiyo ya Shinyanga John Kisandu, alisema wametengua maamuzi yao ya kumkataa mkurugenzi huyo, na kukiri kwamba hawakufuata kanuni na taratibu, hivyo wataendelea kufanya naye kazi, na kumtaka maazimio yao awe ana yafanyia kazi.


Aidha jana kikao cha baraza hilo la madiwani la halmashauri ya manispaa ya Shinyanga kilivunjika baada ya madiwani wa halmashauri hiyo kudai kutokuwa na imani na mkurugenzi wa halmashauri Geofley Mwangulumbi, kwamba amekuwa hatekelezi maazimio ambayo huazimia yakiwamo ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.



Baraza hilo limevunjika kwenye kikao cha kawaida cha robo ya nne, ambapo wakati wakusoma na kudhitisha muhtasari, mmoja wa madiwani hao David Nkulila (CCM )kutoka Kata ya Ndembezi, aliibua hoja kuwa kwanini maadhimio yao yamekuwa hayatekelezwi, na kudai kutokuwa na imani na mkurugenzi hoja ambayo iliungwa mkono na madiwani na hatimaye kikao cha baraza kuvunjika.




TAZAMA PICHA HAPA CHINI

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack, akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani la manispaa ya Shinyanga leo Julai 30,2019 na kuwataka watengue maamuzi yao ya kumkataa mkurugenzi wa halmshauri hiyo Geofrey Mwangulumbi, ndipo waendelee na kikao chao tofauti na hapo baraza lao ni batiri, ambapo madiwani hao walitengua maamuzi yao na kukiri hawakufuata taratibu za kumkataa mkurugenzi.Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog.

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack, akikiri pia madai ambayo wanalalamikia madiwani hao ya kutekelezewa mazimio yao ni ya kweli, na kutoa maagizo kwa mkurugenzi akae na watendaji wake na kutekeleza maazimio hayo kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko, akizungumza kwenye kikao cha baraza hilo la madiwani la manispaa ya Shinyanga, na kuonyesha naye kusikitishwa na tukio lililotokea la kuvunjika kwa kikoa cha baraza hilo la madiwani bila ya kufuata utaratibu.

Katibu Tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela, akiwataka Madiwani, watumishi wa manispaa ya Shinyanga pamoja na mkurugenzi kuzungumza lugha moja ili kuondoa makandokando yaliyopo na kuwa kitu kimoja na kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi

Naibu Meya wa manispaa ya Shinyanga John Kisandu, akizungumza kwenye baraza hilo na kutengua maamuzi ya baraza ya kumkataa mkurugenzi wa mansipaa hiyo Geofrey Mwangulumbi kuwa hawana imani naye kutokana na kushindwa kutekeleza mazimio yao.

Madiwani wa manispaa ya Shinyanga wakiendelea na kikao cha baraza, mara baada ya kutengua maamuzi hayo ya kumkataa mkurugenzi wa manispaa hiyo Geofrey Mwangulumbi, kuwa walikosea sababu hawakufuata utaratibu.

Madiwani wakiendelea na kikao cha baraza wakijadili ajenda mbalimbali kwa ajili ya mustakabali wa maendeleo ya manispaa ya Shinyanga.

Diwani wa Kata ya Kolandoto Agnes Machiya akichangia ajenda kwenye kikao cha baraza hilo la madiwani la manispaa ya Shinyanga.

Diwani wa Kata ya Kitangili Khamis Ngunila akichangia ajenda kwenye kikao cha baraza la madiwani la manispaa ya Shinyanga.

Diwani wa viti maalumu manispaa ya Shinyanga Shela Mashandete akichangia ajenda kwenye kikao cha baraza la madiwani la mansipaa ya Shinyanga.

Madiwani wakiendelea na kikao cha baraza.

Watendaji wa manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha baraza la madiwani.

Watendaji wa manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha baraza la madiwani.


Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog.

Share:

MBUNGE WA CHADEMA WILFRED RWAKATARE AKANUSHA KUHAMIA CUF


Na Lydia Lugakila - Malunde1 blog  Bukoba
Mbunge wa jimbo la Bukoba mjini mkoani Kagera,Mhe. Wilfred Muganyizi Rwakatare (CHADEMA) amekanusha uvumi wa kwamba amejiunga na Chama cha Wananchi CUF.

Akitolea ufafanuzi huo leo Julai 30,2019 Rwakatare amesema hivi karibuni kumekuwepo na uvumi ambao umekuwa ukiendelea katika mitandao ya kijamii uliomtaja kujiunga na Chama cha Wananchi (CUF).

Mbunge huyo amesema kuwa siasa kama siasa ina maneno mengi yakiwemo yenye uzushi pale mwanasiasa amekuwa anapoungana na wenzake wa vyama tofauti hasa katika masuala ya kimaendeleo.

Amesema kuwa hivi karibuni alikwenda kwenye ofisi za CUF zilizopo Buguruni jijini Dar es salaam kwa lengo la kuwasalimia baadhi ya viongozi wa chama hicho akiwemo mwenyekiti wa chama hicho Prof. Ibrahimu Haruna Lipumba ndipo uvumi kuwa kajiunga na CUF ulipoanza kusambaa mtandaoni.

Rwakatare ameongeza kuwa aliwahi kuwa kiongozi wa chama cha CUF kama Naibu katibu mkuu wa chama na wakati anaondoka kwenda CHADEMA,na aliondoka pasipo kuwa na chuki na mtu yoyote ndani ya chama na ndiyo maana wakati anakwenda kuwasalimia alipokelewa kwa furaha na shangwe.

Amewataka watu wanaozusha uvumi huo kuacha tabia hiyo mara moja na kuwataka kumfuata mlengwa ili aweze kutolea ufafanuzi wa jambo husika na kuacha tabia za kuvujisha taarifa za kupotosha umma wa Watanzania huku akiongeza kuwa hata siku za nyuma aliwahi kuzushiwa kujiunga na Chama Cha Mapinduzi CCM.

Katika hatua nyingine,Rwakatare amewataka wananchi wa Jimbo la Bukoba Mjini kuunga mkono jitihada za maendeleo katika kipindi hiki ambapo miradi mbalimbali ya maendeleo inaendelea kutekelezwa likiwemo suala la miundombinu za barabara, afya, shule, ukarabati wa meli mpya, michezo , pamoja na ujenzi wa stendi kuu mpya ya mabasi ambayo inajengwa katika kata ya Kyakailabwa mkoani Kagera.
Share:

Kutana na Mohamedi Buruhani Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH .....Anauwezo wakufanya Dua mbalimbali Na Kutafsiri Ndoto

Kutana  na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Mohamedi Buruhani Mtabibu wa Nyota za Binadamu  Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..

JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na  Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Mohamed Buruani Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. 

Anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU. Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie ..Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.

Mohamed Buruhan Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..

Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN, Anatafsiri Ndoto. ,KUSAFISHA NYOTA, Mvuto wa Mwili na BIASHARA, ...MIGUU Kufa GANZI na mengi zaidi (+255  715971688 au (+255  756914036

NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE...


Share:

Nape Nnauye: " Wakubwa Wananichukia, Wacha Wanichukie maana Napigania Haki za Wananchi"

Mbunge wa jimbo la Mtama (CCM), Nape Nnauye amesema hana kinyongo na serikali yake na kwamba anapigania haki ya wananchi wake kama walivyoahidi kuwasimamia.

Nape alisema awali mbaazi ilikuwa inafanya vizuri sokoni baadaye ikashuka kutoka Sh 2000 hadi Sh 100.

“Ndio maana mbunge wenu nikawa mkali bungeni wapo watu wanasema Nape mkali na wakati mwingine wakubwa wanachukia lakini ninasema bora nichukiwe lakini watu wangu waone nimesimamia haki yao

Aliongezea kuwa:” CCM ni chama cha wakulima na wafanyakazi sina jambo baya na mtu sina kinyongo na serikali yangu lakini tuliwaahidi tutasimamia haki yenu wanaosema Nape anaisemea Kusini yote ndio ni kweli Kusini yote ni maskini.

Nape alisema anatambua nia ya Rais John Magufuli alitaka kuwaokoa kutoka katika bei mbaya akapanga mpango bahati mbaya waliomshauri na waliotekeleza wakalikoroga.


Share:

Rwakatale Akanusha Habari Za Kujiunga Na Chama Cha Wananchi CUF

NA AVITUS BENEDICTO KYARUZI, KAGERA.
Mbunge wa jimbo la Bukoba mjini kupitia tiketi ya chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mh wilfredy Muganyizi Rwakatale ametolea ufafanuzi  juu ya uvumi wa kujiunga na chama cha wananchi CUF ambao ulikuwa unasambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii siku za nyuma.
 
Akitolea ufafanuzi huo mbunge Rwakatale amesema kuwa alikwenda kwenye ofisi za CUF zilizopo Buguruni Dar es salaam kwa lengo la kuwasalimia baadhi ya viongozi wa chama icho aKiwemo  mwenyekiti wa chama hicho Prof Ibrahimu Haruna Lipumba.
 
Mh Rwakatale ameongeza kuwa aliwai kuwa kiongozi wa chama icho kama Naibu katibu mkuu wa chama na wakati anaondoka aliondoka pasipo kuwa na chuki na mtu yoyote ndani ya chama na ndiyo maana wakati anakwenda kuwasabai alipokelewa kwa shangwe.
 
Amewataka watu wanaozusha uvumi huo kuacha tabia hiyo mara moja na kuwataka kumfuata mlengwa ili aweze kutolea ufafanuzi wa jambo husika na kuacha tabia za kuvujisha taharifa za kupotosha umma wa watanzania na kuongeza kuwa ata siku za nyuma aliwai kuzushiwa taharifa za kujiunga na chama cha Mapinduzi CCM na kudai kwamba haiwezi kutokea ata siku moja kwa kuwa yeye ni mbunge kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA).
 
Sanjali na hayo mh Rwakatale amewataka wananchi wa Jimbo la Bukoba mjini kuwaunga mkono katika jitihada za maendeleo kwakipindi hiki ambapo miradi mbalimbali za maendeleo zinaendelea kutekelezwa likiwemo suala la miundombinu za barabara, afya, shule, ukarabati wa meli mpya, michezo , pamoja na ujenzi wa stendi kuu mpya ya mabasi ambayo inajengwa katika kata ya Kyakailabwa mkoani Kagera.


Share:

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga Awasili Mkoani Simiyu, Aridhishwa Na Maandalizi Ya Nanenane Kitaifa

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Simiyu
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga tarehe 29 Julai 2019 amewasili Mkoani Simiyu kwa ajili ya kujionea maandalizi ya Maadhimisho 26 ya sikukuu ya wakulima maarufu kama (Nane Nane) yenye lengo la kuwatambua na kuwaenzi Wadau Wakuu wa Sekta ya Kilimo ambao ni Wakulima, Wafugaji, Wavuvi, Wanaushirika, Wasindikaji wa mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi na maliasili kwa mchango wao mkubwa wanaoutoa katika kuendeleza uchumi wa nchi yetu.

Mwaka huu wa 2019, sherehe hizi zinafanyika Kitaifa mjini Bariadi katika Viwanja vya maonesho ya kilimo Nyakabindi katika Mkoa wa Simiyu hivyo Mhe Hasunga amepongeza Uongozi wa mikoa ya Simiyu, Shinyanga na Mara kwa juhudi zao za kufanikisha kuingiza uwanjani huduma za msingi ambazo ni maji na umeme.

Alisema kuwa jukumu hilo kwa Serikali na Wadau wa Sekta Binafsi ni kuendeleza viwanja hivyo vya Nyakabindi kwa kujenga mabanda ya maonesho ya kudumu na kuboresha huduma muhimu za kijamii ili kuwe na maonesho endelevu yenye sura ya Kitaifa na Kimataifa.

Alisema kuwa Serikali kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali, imeendelea kuongeza na kuboresha viwanja vya maonesho katika Kanda mbalimbali hapa nchini, kwa sasa kuna viwanja nane (8) vya maonesho ya kilimo ambavyo ni Themi (Arusha) Kanda ya Kaskazini inayohusisha mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara;  Mwl. J.K.Nyerere (Morogoro) Kanda ya Mashariki ambayo mikoa yake ni Dar es Salaam, Pwani, Morogoro na Tanga;na John Mwakangale (Mbeya) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini inayojumuisha mikoa ya Iringa, Mbeya, Ruvuma, Njombe, Katavi, Songwe na Rukwa;

Vingine ni Nzuguni (Dodoma) katika Kanda ya Kati yenye mikoa ya Dodoma na Singida; Nyakabindi (Bariadi) Kanda ya Ziwa Mashariki yenye mikoa ya Simiyu, Shinyanga na Mara; Nyamuhongolo (Mwanza) Kanda ya Ziwa Magharibi yenye mikoa ya Mwanza, Kagera na Geita; Ngongo (Lindi) Kanda ya Kusini inayojumuisha mikoa ya Mtwara na Lindi na Fatma Mwasa (Tabora) Kanda ya Magharibi yenye mikoa ya Tabora na Kigoma.

Akizungumza na mtandao wa Wazo Huru Blog, Waziri huyo wa kilimo ameeleza kuwa Wakati wa sherehe hizo za Nane Nane, Wakulima, Wafugaji, Wavuvi, Wanaushirika na Wadau wengine katika Sekta za Kilimo; watapata fursa nzuri zaidi ya kuona na kujifunza mbinu na teknolojia sahihi za uzalishaji na usindikaji wa mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi, maliasili na bidhaa nyinginezo kupitia Maonyesho ya Kilimo yanayoandaliwa.

Aidha, kwa Wafanyabiashara itakuwa ni fursa nzuri ya kutangaza bidhaa zao hususani pembejeo na zana mbalimbali za uzalishaji na usindikaji wa mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi na maliasili.

Aliitaja Kaulimbiu ya sherehe za Nane Nane Mwaka huu ni kuwa ni “Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa ukuaji wa Uchumi wa Nchi”.  Kaulimbiu hii imechaguliwa baada ya kutafakari kwa undani suala zima la Uchumi wa Viwanda unavyoweza kuchangia katika kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja, pato la Taifa na wakati huo huo kupambana na Umaskini.

"Ni ukweli ulio dhahili kuwa Kilimo ni Sekta kubwa na muhimu kwa maendeleo kutokana na mchango wake katika uchumi wa Taifa. Mfano katika mwaka 2017, Sekta ya Kilimo ilitoa ajira kwa Watanzania kwa asilimia 65.5, ikichangia asilimia 28.7 ya pato la Taifa. Sambamba na hilo Sekta ya Kilimo inachangia asilimia 65 ya malighafi za viwandani. Takwimu zinaonesha kuwa katika robo ya kwanza ya mwaka 2018 ukuaji wa Sekta ya Kilimo ulifikia asilimia 7.1" Alikaririwa Mhe Hasunga

Ameongeza kuwa Kaulimbiu ya mwaka huu inahamasisha Wakulima, Wafugaji, Wavuvi na Wanaushirika kuleta mapinduzi katika Sekta za Kilimo kwa kuzalisha kwa tija ili kukuza uchumi wa Mkulima, Mfugaji, Mvuvi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Kadhalika, ametoa wito kwa Wananchi na Wadau wote kushiriki kikamilifu na kuhudhuria kwa wingi maonesho hayo kuanzia tarehe 1 hadi 8 Agosti, 2019.


Share:

Mahakama yasema itaifuta kesi ya Halima Mdee dhidi ya Rais

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imesema itaifuta kesi ya kutoa lugha chafu dhidi ya Rais  Magufuli inayomkabili mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee kwa sababu ya shahidi kushindwa kutoa ushahidi wake kwa zaidi ya mara tatu mfululizo.

Hayo yamesemwa leo Jumanne Julai 30,2019 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba baada ya Wakili wa Serikali, Silivia Mitato kudai wakili anayeendesha shauri hilo amepangiwa kazi nyingine hivyo anaiomba mahakama impe muda ili apitie jalada hilo.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Simba amesema kumbukumbu zake zinaonyesha shahidi Abdull Chembea amefika mahakamani hapo zaidi ya mara tatu na hajawahi kutoa ushahidi.

"Hili shauri mimi nitalifuta kwa kuwa shauri hili lipo tangu mwaka 2017 kila nikija namuona huyu shahidi anakuja lakini hakuna kinachoendelea, naona upande wa mashitaka mnakwamisha shauri lisiendelee, nawapa sharti mtakapokuja awamu ijayo nataka shauri hili liendelee," amesema.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 28 na Septemba 4, 2019 kwa ajili ya kusikilizwa.


Share:

Jeshi la Polisi Latoa sababu za kumkamata mwandishi wa habari Erick Kabendera

Polisi kanda maalum ya Dar es salaam imethibitisha kumkamata mwandishi wa kujitegemea, Erick Kabendera kwa kutotii wito alioitwa na jeshi hilo. 

Polisi wamesema kuitwa kwake ni kutaka kutoa utata wa uraia wake na wanaendelea na uchunguzi na kumuhoji kama ni Mtanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Julai 30, 2019, Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amesema walimkamata jana Jumatatu Kabendera baada ya kupelekewa wito wa kufika polisi lakini akakaidi.

"Kuhusu taarifa za Mwanahabari Erick Kabendera ni kwamba July 29 tulimkamata nyumbani kwake baada ya kukataa wito wa Polisi, aliandikiwa barua ya wito kwa ajili ya mahojiano akakaidi, utii wa sheria bila shuruti ni muhimu sana ili kuzuia matokeo ya kukaidi wito halali.

"Sababu ya Erick kuitwa ni kuhusiana na utata wa Uraia wake, Polisi wanaendelea kupeleleza kwa kushirikiana na Uhamiaji ili kuhakikisha lile ambalo anatuhumiwa nalo linawekwa mezani ili athibitishe yeye ni Mtanzania kwa kutoa vielelezo mbalimbali.

"Kama Erick angefika alipoitwa angehojiwa na kuruhusiwa, lakini kwa kuwa ana mashaka ya uraia wake akakataa wito, sasa tuko nae na taratibu za upelelezi zinaendelea, hakutekwa, alikamatwa na wakamataji ni sisi na yuko salama.

"Baada ya kumkamata(Erick), kumezuka taarifa kutoka kwa kada mbalimbali kwenye jamii wengine Wanahabari wakiendelea kusema Mwandishi huyo ametekwa, wala hakutekwa aliitwa lakini kwa ujeuri akawa amekaidi wito huo"- Amesema Mambosasa





Share:

Rais Magufuli afika Nyumbani kwa kina Mbowe kutoa pole ya msiba

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametoa pole kwa familia, kufuatia kifo cha Meja Jenerali Mstaafu Albert Lameck Mbowe aliyefariki dunia juzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.

Rais Magufuli amekwenda nyumbani kwa Marehemu Salasala Jijini Dar es Salaam na kukutana na familia ikiongozwa na Freeman Mbowe ambaye ni Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Pamoja na kutia saini kitabu cha maombolezo, Rais Magufuli ameungana na familia hiyo katika sala ya pamoja ya kumuombea Marehemu Meja Jen. Mstaafu Albert Lameck Mbowe.

Baada ya sala hiyo, Rais Magufuli ameitaka familia hiyo iendelee kuwa na umoja na kumtanguliza Mwenyezi Mungu.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jen. Venance Salvatory Mabeyo amesema pamoja na kustaafu Meja Jen. Mbowe alikuwa mshauri wa karibu wa Jeshi.

Amesema katika utumishi wake wa miaka 36 na siku 27 Jeshini, Meja Jen. Mstaafu Mbowe alitoa mchango mkubwa katika masuala ya fedha.

Meja Jen. Mstaafu Mbowe alizaliwa Januari 1953, alijiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) mwaka 1973 na alistaafu utumishi Jeshini mwaka 2009.


Share:

AUA MTU MMOJA,AJERUHI WAWILI KWA KUWAPIGA MSHALE BAADA YA KUNYIMWA BIA

Kijana mmoja ambaye jina lake halijajulikana ameibua taharuki katika Kijiji cha Kwitete Wilaya ya Serengeti mkoani Mara nchini Tanzania baada ya kutuhumiwa kuua mtu mmoja na kujeruhi wawili akiwemo baba yake wa kambo kwa sababu ya kunyimwa bia.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Mara, Juma Ndaki jana Jumatatu Julai 29, 2019 alithibitisha kuwa tukio hilo limetokea Jumapili Julai 28, 2019 kijijini hapo na mtuhumiwa amekimbia wanaendelea kumsaka.

Amesema aliyefariki ni mgeni hajatambulika jina, lakini kabila lake ni Msukuma ambaye aliongozana na mtu mwingine kwenda kwenye mji huo kwa ajili ya kumsalimia mama mwenye mji ambaye pia ametoroka na kijana wake.

Ndaki amesema walinunua kreti ya bia wakati wanakunywa, mtuhumiwa alipewa chupa mbili alipotaka tena wakamnyima ndipo akaingia ndani na kutoka na upinde na kuanza kuwashambulia na kusababisha mauaji ya mtu mmoja na kujeruhi wawili.

Mmoja wa wahudumu wa Hospitali Teule ya Nyerere ambaye hakutaka kutaja jina lake, amethibitisha kupokea mwili wa mtu anayedaiwa kupigwa mshale ambao umeletwa na polisi wa wilaya ya Serengeti na uchunguzi utafanyika baada ya ndugu kujitokeza.


Na Anthony Mayunga - Mwananchi
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger