Tuesday, 11 November 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE NOVEMBA 11,2025



Magazeti

Share:

Monday, 10 November 2025

ORODHA YA WANAOGOMBEA NAFASI YA SPIKA WA BUNGE LA TANZANIA



Share:

OJADACT : MAANDAMANO OKTOBA 29, UHALIFU HAUKUBALIKI, TUJITAFAKARI

 

Share:

TANZANIA NI KISIWA CHA AMANI NA FURAHA, TUILINDE SIFA HII- MAWANGA




Na Mwandishi wetu,Dar

Wito umetolewa kwa kuilinda na kuitetea sifa ya Tanzania kuwa kisiwa cha amani, raha na furaha, Vijana wakitakiwa kujitenga na makundi na vishawishi vya kujiingiza kwenye vitendo vya kuhatarisha amani na mshikamano uliopo nchini Tanzania.

Akizungumza na Chombo hiki cha habari, Bw. Hussein Thomas Mawanga, amewataka pia Vijana kujifunza kutoka kwa nchi jirani, namna ambavyo ukosefu wa amani umewagharimu wengi, ukidhorotesha ustawi wa wananchi, kufifisha maendeleo ya Mataifa husika pamoja na kuharibu miundombinu mbalimbali na kusababisha maafa mengine ya kijamii, kiuchumi na kiusalama.

Bw. Mawanga amewasihi Vijana na Watanzania kwa ujumla kujifunza na kutambua umuhimu wa amani kwa maendeleo yao na ya Taifa kwa ujumla, akisema mpaka hii leo haamini kile kilichotokea Oktoba 29, 2025 na kusisitiza kila Mtanzania kutambua kuwa anao wajibu wa kulinda na kuitetea amani iliyopo nchini Tanzania.
Share:

MWANZA ILIVYOATHIRIKA NA DHAHAMA YA OKTOBA 29, HUDUMA MUHIMU ZA KIJAMII ZAKOSEKANA



Ghasia, vurugu na uharibifu mkubwa uliofanywa na magenge ya Vijana hapo Oktoba 29, 2025, umewaacha wananchi wa Mkoa wa Mwanza kukosa huduma muhimu za kijamii, huku pia mamia ya wananchi wakikosa ajira na kipato kutokana na matukio ya moto na wizi ulioangamiza maeneo yao ya kazi katika Eneo la Buhongwa Mkoani humo.

Kwa nyakati tofauti, magenge ya Vijana katika siku ya uchaguzi Mkuu wa Jumatano Oktoba 29, 2025, wakati wengine wakipiga kura kuwachagua Viongozi wao watakaowaongoza kwa miaka mitano ijayo, wao walivamia, kuiba na kuchoma moto Chuo cha Ufundi stadi VETA cha Buhongwa Mkoani Mwanza pamoja na kuiba na kuteketeza kwa moto Vituo vya uuzaji mafuta vya Olypic Petrol na Lake Oil Energies pamoja na kituo cha uuzaji wa bidhaa mbalimbali cha Empire store Kilichopo Igoma sambamba na magari yaliyokuwa yamepaki kwenye maeneo hayo.




Share:

WANAHARAKATI WASAMBAZA TAARIFA POTOFU KUCHAFUA HAIBA YA MTU

Kupitia Mitandao ya Kijamii hasa Mtandao wa X (zamani Twitter) baadhi ya Watu wakiwepo wanaojiita Wanaharakati wameonekana wakisambaza picha zenye mfumo wa “screenshot” kumhusisha ndugu Abdul Ameir  Wakimhusisha na vitendo vya uvunjifu wa maadili na kutumia Lugha chafu kuandika jumbe mbalimbali, taarifa ambazo  ni wazi zinalenga kupotosha umma.

Wanaosambaza upotoshaji huo asilimia kubwa ni wale ambao wamekuwa wakiipinga Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo wanafanya hivyo wakiwa na lengo la kuichafua Serikali kutokana na kuhusisha taarifa hizo na mtoto wa Rais Samia Suluhu Hassan.

 

Share:

Sunday, 9 November 2025

UMUHIMU WA MARIDHIANO YA KUJIFUNZA KUTOKA KWA WENZETU



Baada ya taharuki, hatua muhimu ni kuanzisha mchakato wa Maridhiano ya Kitaifa. Lengo ni kuwezesha jamii, kisiasa, na kidini kuketi pamoja, kujadili maumivu, kusamehe, na kuahidi kusonga mbele kwa pamoja.

Mifano ya kimataifa inaonesha faida za maridhiano ni  Afrika Kusini ilitumia Tume ya Ukweli na Maridhiano (TRC) kuponya majeraha ya ubaguzi wa rangi, na Rwanda (baada ya mauaji ya kimbari) imejenga upya Taifa lake kwa misingi ya umoja na maridhiano.

Mmoja wa wanasiasa Mkongwe  anasema: "Maridhiano siyo kuficha matatizo, bali ni kuyajadili kwa uwazi na upendo, na kuamua kwa pamoja kuwa hatutaruhusu kugawanywa tena." Maridhiano yanahitaji utashi wa kisiasa na utulivu wa kimoyo. Wananchi wanataka kuona viongozi wao wakionyesha mfano wa kuweka tofauti za kando na kuungana.

Wananchi wanatoa kauli hizo wakati tayari Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imechukua hatua za  mchakato wa mazungumzo ya maridhiano  ili kuwa na Taifa lenye amani na umoja na kuendelea kuwa mfano wa utulivu katika Afrika na Dunia kwa ujumla.

Halikadhalika, Makamu wa Rais amesema Tanzania ni salama na tulivu na ipo tayari kuendelea kupokea wageni kutoka duniani kote kwa manufaa ya nchi zote. 

Makamu wa Rais amesema hayo wakati akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC), uliyofanyika kwa njia ya mtandao, akiwa mkoani Dodoma.

Amesema dhamira ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha  kuhakikisha Tanzania inapata maendeleo na amani kuendelezwa. 

Share:

TUIJENGE NCHI YETU KWA PAMOJA NA KUOMBEA AMANI IDUMU- KIROBA



Adam Kiroba, Mkazi wa Mkera, Chanika, Wilayani Temeke Mkoani Dar Es Salaam, amewataka watanzania hususani Vijana kote nchini kudumisha amani, mshikamano na upendo kwenye jamii na kujiepusha na vurugu na uvunjifu wa amani kwani mara zote waathirika wakubwa wa vurugu mara zote wamekuwa akinamama, Watoto, Wazee pamoja na wale wasiokuwa na hatia kutoka kundi la wananchi wenye kipato cha chini.

"Mimi ninachowaomba watanzania ni kuwa nchi yetu inasifika kuwa kisiwa cha amani, tuendelee na sifa hiyo kwasababu machafuko ya juzi athari zake tumeziona na wengine mpaka leo biashara na sehemu za kuishi hawana. Niwasihi watanzania wenzangu tudumishe amani iliyopo na tusiwe sehemu ya kuhamasisha hicho kinachoendelea na tuwe wavumilivu na kuangalia namna ya kuijenga nchi yetu." Amesisitiza Bw. Kiroba.

Bw. Kiroba akizungumza na mwandishi wetu wa habari leo Jumapili Novemba 09, 2025 amewataka pia Vijana kutofuata mikumbo kutoka kwa baadhi ya watu, akiwahamasisha pia wale wote wenye kuamini katika Mungu kupitia dini zao na madhehebu mbalimbali kuendelea kuiombea nchi ya Tanzania ili amani, umoja na mshikamano viendelee kudumu kwa maslahi ya kila Mtanzania.

Amesisitiza pia umuhimu wa kutambua faida za amani kwenye jamii, akisema ghasia na vurugu za Oktoba 29, 2025 kumewagharimu pia watu wasiokuwa na hatia, kusababisha ugumu wa upatikanaji wa huduma muhimu za kijamii pamoja na kupanda kwa gharama za maisha na kuyumba kwa uchumi kwa watu wengi wa kipato cha chini.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI NOVEMBA 9,2025


Magazeti
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger