Saturday, 25 October 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA OKTOBA 24,2025


Magazeti
   

 

  

   

 







  
Share:

Friday, 24 October 2025

SADC YAIPONGEZA TANZANIA KWA MAANDALIZI YA UCHAGUZI, YATOA WITO WA AMANI OKTOBA 29



Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) imetoa sifa kubwa kwa Tanzania kufuatia maandalizi yake thabiti kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025. SADC imesisitiza kuwa mafanikio hayo ni kielelezo cha dhamira ya nchi katika kukuza demokrasia na amani.


Wito huo wa pongezi na amani ulitolewa jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Kikosi cha Uangalizi wa Uchaguzi cha SADC (SEOM), uliofanyika Oktoba 21, 2025.


Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa, Ulinzi na Usalama wa SADC, Mhe. Richard Msowoya (akizungumza kwa niaba ya Rais wa Malawi, Profesa Arthur Peter Mutharika), alisisitiza umuhimu wa uchaguzi huru, wa haki na unaozingatia misingi ya amani.


"Tunahimiza wapiga kura wote waliojiandikisha wajitokeze kwa wingi kupiga kura kwa amani. Huo ndiyo msingi wa kuimarisha demokrasia," alisema Mhe. Msowoya, akitoa wito kwa wadau wote – vyama, asasi za kiraia na vyombo vya habari – kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa utulivu.


Ujumbe wa SADC ulishukuru Serikali ya Tanzania kwa ukarimu na kusisitiza kuwa jumuiya hiyo iko tayari kuunga mkono mchakato mzima kwa mujibu wa sheria zake. SADC pia ilieleza kuwa Tanzania ni nchi ya tatu katika ukanda huo kufanya uchaguzi kwa amani na uwazi ndani ya mwezi mmoja.


"Tunawahimiza Watanzania kulinda amani, kuheshimu sheria na kuepuka vurugu. Uchaguzi wa amani ni fahari ya Taifa na urithi kwa vizazi vijavyo," ulisisitiza ujumbe huo.


Kikosi cha SEOM kinaundwa na waangalizi 80 kutoka nchi 10 wanachama wa SADC, ambao watasambazwa katika mikoa yote 27 ya Tanzania Bara na Visiwani kufuatilia hatua zote za uchaguzi
Share:

Thursday, 23 October 2025

DKT. SERERA: MFUMO WA STAKABADHI GHALANI WAONGEZA USHINDANI WA SOKO LA MAZAO



Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Suleiman Serera,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ziara yake ya kutembelea na kujionea maghala yanayotumia mfumo wa stakabadhi ghalani katika Halmashauri ya Karatu, mkoani Arusha.

Na Alex Sonna, Karatu

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Suleiman Serera, ameipongeza Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) kwa kusimamia vyema mfumo wa stakabadhi ghalani unaotekelezwa katika Halmashauri ya Karatu, mkoani Arusha, akisema umeleta tija kubwa kwa wakulima na wafanyabiashara wa mazao.

Akizungumza baada ya kutembelea maghala yaliyopo katika eneo hilo, Dkt. Serera amesema lengo la ziara yake ni kujionea kwa karibu namna mfumo huo unavyofanya kazi pamoja na mwitikio wa wadau.

“Nimejionea na kujiridhisha kwamba mfumo huu unafanya kazi vizuri. Tutaendelea kuelimisha wadau zaidi ili wote watumie mfumo huu wenye faida nyingi kwa taifa,” amesema Dkt. Serera.

Amesema mfumo wa stakabadhi ghalani umeleta ushindani katika soko la bidhaa za kilimo na kuwawezesha wakulima kupata faida kubwa kutokana na bei nzuri za mazao yao.

“Maghala yetu mengi yamewekwa katika hali ya usafi wa hali ya juu. Hakuna mzigo unaoingia ghalani bila kusafishwa na kuandaliwa vizuri. Faida nyingine ni kuwa mfumo huu unahakikisha kila mzigo unapimwa kwa uzito unaostahili,” amesema.

Aidha, amesema Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo imejipanga kuhakikisha bidhaa zote zinazofika kwa mlaji zinakuwa salama na zenye ubora unaozingatia viwango vya usalama wa chakula, ili kupunguza magonjwa yasiyo ya kuambukiza yanayotokana na matumizi ya vyakula visivyo salama.

Dk. Serera ametoa wito kwa wadau wa kilimo na biashara kuendelea kutumia mfumo wa stakabadhi ghalani, huku serikali ikiendelea kushughulikia changamoto ndogo ndogo zinazojitokeza wakati wa utekelezaji wake.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala, Asangye Bangu amesema mfumo huo umepokelewa vizuri na wakulima wa mbaazi wilayani Karatu, na kwamba umechangia kupatikana kwa bei nzuri ya zao hilo sokoni.

“Kwa msimu wa mwaka huu, Karatu imekuwa miongoni mwa maeneo yenye bei kubwa zaidi ya mbaazi nchini. Hii ni ishara ya mafanikio ya mfumo wa stakabadhi ghalani,” amesema.

Ameongeza kuwa Bodi inaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuimarisha sekta ya kilimo na kuweka mazingira rafiki ya biashara kupitia taasisi za wizara husika.

“Tunawahakikishia wanunuzi na watumiaji kwamba bidhaa zinazotolewa kupitia mfumo huu zina ubora unaoendana na thamani ya fedha zao. Mfumo huu unaleta uwazi, usawa na faida kwa pande zote,” amesisitiza.

Awali Mkusanya mali Bi.Gladness Tarimo, amesema mfumo wa stakabadhi ghalani umeleta manufaa makubwa kwa vijana kwani umewapa nafasi ya kuuza bidhaa zao kwa bei shindani na inayojulikana wazi katika soko.

Naye, Evarist Silayo, Mfanyabiashara wa mazao ambaye kampuni yake inamiliki maghala katika maeneo matatu nchini ikiwemo Karatu, amesema mfumo huo umeondoa upunjaji na kuongeza uaminifu kati ya wakulima na wanunuzi.

“Kwa mfano, katika mnada wa kwanza uliofanyika hapa Karatu, bei ya mbaazi kwa kilo ilikuwa zaidi ya Sh.1,000, tofauti na bei ya awali iliyokuwa kati ya Sh.750 hadi Sh.800. Wakulima waliona faida kubwa ya kutumia mfumo huu,” amesema Silayo.,



Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Suleiman Serera,akipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Karatu Mhe. Dkt. Lameck Karanga Ng'ang'a wakati wa ziara yake ya kutembelea na kujionea maghala yanayotumia mfumo wa stakabadhi ghalani katika Halmashauri ya Karatu, mkoani Arusha.



Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Suleiman Serera,akizungumza wakati wa ziara yake ya kutembelea na kujionea maghala yanayotumia mfumo wa stakabadhi ghalani katika Halmashauri ya Karatu, mkoani Arusha.



Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Suleiman Serera,akizungumza wakati wa ziara yake ya kutembelea na kujionea maghala yanayotumia mfumo wa stakabadhi ghalani katika Halmashauri ya Karatu, mkoani Arusha.



Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Suleiman Serera,akizungumza wakati wa ziara yake ya kutembelea na kujionea maghala yanayotumia mfumo wa stakabadhi ghalani katika Halmashauri ya Karatu, mkoani Arusha.



Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Suleiman Serera,akizungumza wakati wa ziara yake ya kutembelea na kujionea maghala yanayotumia mfumo wa stakabadhi ghalani katika Halmashauri ya Karatu, mkoani Arusha.



Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Suleiman Serera,akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala, Asangye Bangu, wakati wa ziara yake ya kutembelea na kujionea maghala yanayotumia mfumo wa stakabadhi ghalani katika Halmashauri ya Karatu, mkoani Arusha.





Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Suleiman Serera,akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala, Asangye Bangu, wakati wa ziara yake ya kutembelea na kujionea maghala yanayotumia mfumo wa stakabadhi ghalani katika Halmashauri ya Karatu, mkoani Arusha.



Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Suleiman Serera,akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala, Asangye Bangu, wakati wa ziara yake ya kutembelea na kujionea maghala yanayotumia mfumo wa stakabadhi ghalani katika Halmashauri ya Karatu, mkoani Arusha.



Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Suleiman Serera,akiendelea kukagua na kujionea maghala yanayotumia mfumo wa stakabadhi ghalani katika Halmashauri ya Karatu, mkoani Arusha.





Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Suleiman Serera,akiendelea kukagua na kujionea maghala yanayotumia mfumo wa stakabadhi ghalani katika Halmashauri ya Karatu, mkoani Arusha.



Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Suleiman Serera,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ziara yake ya kutembelea na kujionea maghala yanayotumia mfumo wa stakabadhi ghalani katika Halmashauri ya Karatu, mkoani Arusha.



Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Suleiman Serera,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ziara yake ya kutembelea na kujionea maghala yanayotumia mfumo wa stakabadhi ghalani katika Halmashauri ya Karatu, mkoani Arusha.



Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala, Asangye Bangu,akimpongeza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Suleiman Serera (hayupo pichani) kwa ziara yake ya kutembelea na kujionea maghala yanayotumia mfumo wa stakabadhi ghalani katika Halmashauri ya Karatu, mkoani Arusha.



Mfanyabiashara wa mazao ambaye kampuni yake inamiliki maghala katika maeneo matatu nchini ikiwemo Karatu Evarist Silayo, akizungumza na waandishi wa habari ambapo ameipongeza Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwajali wakulima nchini.



Mkusanya mali Bi.Gladness Tarimo, akielezea jinsi mfumo huo unavyowasaidia katika kuinua kipatao chao.





Share:

Wednesday, 22 October 2025

WAFANYABIASHARA, WAJASIRIAMALI HANDENI WAFUNGUKA SABABU ZA KUJITOKEZA KUPIGA KURA OKTOBA 29




Na Augusta Njoji, Handeni TC

Makundi mbalimbali ya wananchi katika Halmashauri ya Mji wa Handeni yameeleza namna yalivyojipanga kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025, wakisisitiza umuhimu wa kutumia haki yao ya kikatiba kuchagua viongozi wanaowataka.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wafanyabiashara, wajasiriamali, na wananchi wamesema wamejipanga mapema kuhakikisha wanajitokeza kupiga kura asubuhi ili kuepuka msongamano na kuhakikisha sauti zao zinasikika kupitia sanduku la kura.



Mmoja wa wajasiriamali katika Soko la Kidereko, Hadija Saidi amesema anahamasisha wenzake kupigakura mapema kwa amani na kuendelea na shughuli zao.

Kwa upande wake, Charles Mkomwa, Mfanyabiashara kata ya Kidereko, amesema uchaguzi ni fursa muhimu kwa watanzania kuchagua viongozi watakaosikiliza sauti zao.

Naye, Mwenyekiti wa Kikundi Kinamoto cha utengenezaji samani, Maulid Gumbo, amesema ana kila sababu za kujitokeza kupiga kura Oktoba 29, 2025 ili kuchagua viongozi watakaoendelea kuchochea maendeleo ya wananchi.
Share:

KENYA YATUPA SOMO LA MAUMIVU: TANZANIA INATAKIWA KUSHTUKA,AMANI SI BAHATI NASIBU



Kwa takribani miaka miwili, Kenya, jirani yetu wa karibu, imekuwa uwanja wa majaribio ya vurugu. Maandamano ya mara kwa mara yameacha vifo, majeraha, na uharibifu mkubwa wa mali. Hali hii haikutikisa tu uchumi, bali iliyumbisha kabisa utulivu wa kijamii—na huo ndio msingi wa funzo letu.

Dkt. Daniel Mwaisaka, mchambuzi wa siasa za Afrika Mashariki kutoka Chuo Kikuu cha Bugema, anatoa angalizo la moja kwa moja:

“Kenya ilianza kwa madai ya kisiasa, lakini yakageuka vurugu ya wazi. Uwekezaji uliporomoka ghafla, bei za bidhaa zikapanda kwa kasi, na walioumia zaidi ni wananchi wa kawaida.”

Vurugu hizi ziliiacha Nairobi ikiwa imejeruhiwa. Sekta ya utalii iliporomoka kwa zaidi ya asilimia 40, biashara nyingi zikifungwa, na maelfu ya vijana wakipoteza ajira zao kutokana na hofu ya usalama.

Ushuhuda wa Maumivu: Kura Ni Silaha Bora Kuliko Jiwe

Sauti za walioathirika nazo zinatoa ushahidi usioweza kupingwa. Bi. Amina Yusuf, mfanyabiashara wa soko la Gikomba, anasimulia kwa uchungu wa moyo: "Tulipoteza kila kitu. Maduka yaliibwa, majirani wakagawanyika kisiasa. Tulijifunza kuwa amani ni bora kuliko vurugu.”

Vilevile, Brian Otieno, kijana wa teknolojia kutoka Kenya, anakiri kwa masikitiko: “Nilidhani maandamano yangeleta mabadiliko, lakini sasa naona tulitumiwa kisiasa. Rafiki zangu wawili walipoteza maisha. Sasa naamini kura ni silaha bora kuliko jiwe.”

Kauli hizi za Brian na Amina zinapaswa kuingia akilini mwa kila Mtanzania anayechezea wazo la ghasia.

Wito wa Hekima: Tanzania Si Mahali pa Kujaribu Moto

Wakati maneno ya uchochezi yakizidi kujaa mitandaoni, viongozi wa kiroho na wazee wanarejea kwenye hekima. Askofu Emmanuel wa Kanisa la Wokovu Arusha anatukumbusha: “Watanzania hawapaswi kuruhusu siasa za chuki wala kugawanyika. Maandamano hayajengi taifa, yanabomoa mshikamano.”

Naye Mzee Juma Kihampa kutoka Morogoro anawasihi wazazi: “Tuwafundishe vijana kuwa kura ni silaha salama ya mabadiliko, si mawe wala moto. Tuwalee kwenye misingi ya amani na subira.”

Tanzania imetambulika kimataifa kama "kisiwa cha amani", na urithi huu ni tunu yetu isiyoweza kuwekwa rehani. Wachambuzi wa siasa wanakubaliana: Wanasiasa wana wajibu wa kuhimiza vijana kujenga badala ya kubomoa.

Kila Mtanzania anapaswa kuwa mlinzi wa amani, kukataa kabisa siasa za chuki, na kutumia sanduku la kura kama njia pekee halali ya kutafuta mabadiliko. Tujifunze kutoka kwa Kenya: Vurugu havileti maendeleo—huharibu maisha. Amani ndiyo mama wa maendeleo, tuilinde kwa vizazi vijavyo!
Share:

Tuesday, 21 October 2025

WACHAMBUZI WAONYA KAULI ZA VIONGOZI WA DINI ZISIZOJAA BUSARA KIPINDI CHA MPITO


 Matukio ya hivi karibuni ya kutoweka kwa mapadri, yakiwemo lile la Padre Camillus Nikata wa Jimbo Katoliki la Songea (aliyekutwa salama) na Padre Kibiki wa Mafinga, yameibua mjadala mpana kuhusu umuhimu wa uwajibikaji, uwazi, na busara katika matamko ya viongozi wa dini, hususan Taifa linapoelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29.

Katika nyakati za mpito wa kisiasa, ambapo hisia, matarajio, na changamoto za jamii huongezeka, viongozi wa dini huwa ndio nguzo za matumaini na utulivu. Hata hivyo, namna matukio yenye utata yanavyoshughulikiwa imekuwa somo la pekee.

Somo la Utu na Hekima

Tukio la Padre Nikata, ambaye aliripotiwa kutoweka ghafla lakini baadaye akapatikana salama kijijini kwao, lilikumbusha jukumu la viongozi kuchunga matamko yao.

Kauli iliyotolewa na baadhi ya viongozi wa Kanisa, kama vile Askofu Mkuu Renatus Nkwande wa Jimbo Kuu la Mwanza, ilisisitiza umuhimu wa utu na haki katika kushughulikia tukio hilo. 

Hata hivyo, tukio zima linatoa somo la umuhimu wa kutafakari muda, mazingira, na athari kabla ya kutoa matamko makali kwa umma. Wakati mwingine, "kimya cha hekima ni sauti yenye nguvu kuliko maneno yasiyopimwa."

Ukweli, Uwajibikaji, na Daraja la Amani

Baada ya kubainika kwamba matukio kama yale ya Padre Nikata na Padre Kibiki (ambaye aligundulika alikuwa na msongo wa mawazo kufuatia matatizo ya kifedha) yalihusisha masuala binafsi zaidi ya kiimani, imezua mjadala kuhusu uadilifu na uwazi wa taasisi.

Taasisi yenye ushawishi mkubwa kama Kanisa Katoliki, ambalo limekuwa mwalimu wa maadili, inakabiliwa na wajibu wa kudumisha imani ya waumini kupitia uwazi na uwajibikaji. Maadili hujengwa kwa ukweli, na uwazi ndio unaorejesha imani ya umma, ambapo kufunika kombe kunaweza kuacha doa la mashaka.

Viongozi wa dini wanakumbushwa kwamba wao ni daraja la uelewano kati ya mamlaka, vyombo vya usalama, na wananchi. Lengo lao ni kuwa "wapatanishi" (Mathayo 5:9) na wajenzi wa amani, si wachochezi wa migogoro.

Wito wa Kuhubiri Utulivu Kuelekea Uchaguzi

Maombi, mafundisho, na kauli za viongozi wa dini zina nguvu ya kubadilisha mitazamo na kuimarisha misingi ya utulivu wa Taifa. Wajibu wao ni kuongoza kwa busara, hekima, na upendo, wakidhibiti hisia za waumini na kulinda amani, ambayo ni zawadi na wajibu wa kila kiongozi.

Kama ilivyoandikwa, “Wenye busara watang’aa kama mwanga wa anga, nao waliowaongoza wengi kutenda haki watang’aa milele kama nyota.” (Danieli 12:3) Wakati huu wa mabadiliko, viongozi wa dini wawe taa ya matumaini, wakiliongoza Taifa kuelekea uchaguzi wa amani na maendeleo.

KURA YAKO NI SAUTI YA MAENDELEO: 

Dkt. Samia Alivyobadilisha Taswira ya Miundombinu Tanzania

Dar es Salaam. Kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, wananchi wanahimizwa kutumia haki yao ya kidemokrasia. 

Kauli ya "Kura yako ni sauti ya amani, daraja la maendeleo, na mwanga wa kesho bora" inawahimiza Watanzania "watoke" Oktoba hii, kwenda kupiga kura kama haki yao ya msingi.

Mfanyabiashara wa soko la Chifu Kingalu Morogoro Yusuf Hamad Brush anasema kwamba ni vyema watu wakatoka katika majengo yao na maeneo ya kazi kwenda kupiga kura Oktoba 29 kwa sababu hiyo ndio  maana ya maendeleo.

Anasema usipoenda kupiga kura utakuwa unajimnyima maendeleo yako mwenyewe na hasa uchaguzi wa mtu kukuwezesha kuwa na maendeleo unayoyataka.

Anasema uchaguzi ndio njia pekee ya kupanga maendeleo na Amani ya taifa.

Anasema yeye mwenyewe ataoenda kupiga kura kwa kuwa anaamini kwamba kura hiyo ndio msingi wa mabadiliko anayoyataka nchini.

Katika kuhimiza upigaji kura, rekodi ya mgombea Dkt. Samia Suluhu Hassan inatumiwa kama kielelezo cha maendeleo endelevu ya Taifa. Serikali yake imejikita katika kubadilisha taswira ya miundombinu nchini, jambo linalochukuliwa kama msingi wa kuendeleza uchumi na urahisi wa maisha.

Katika Sekta ya Usafiri na Miundombinu:

Utekelezaji wa miradi mikubwa unatajwa, ikiwemo kukamilisha ujenzi wa barabara ya juu ya Ubungo na kuanzisha mipango ya barabara za juu mikoani. Kazi kubwa inaendelea katika ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza, hatua muhimu itakayobadilisha usafiri nchini.

Dkt. Samia pia anatajwa kusimamia ujenzi wa madaraja makubwa kama Daraja la Kigongo–Busisi na Daraja la JPM, ambayo yanajenga daraja la maendeleo kwa kuunganisha mikoa kwa urahisi zaidi wa kibiashara na kijamii.

Aidha, juhudi zimefanywa kuboresha viwanja vya ndege vya kisasa katika mikoa muhimu kama Dodoma, Mwanza, na Kigoma, huku mfumo wa usafiri wa mwendokasi (DART) jijini Dar es Salaam ukiwa umeboreshwa kwa kuongeza njia mpya na magari ya kisasa.

Mbali na miundombinu ya usafiri, Dkt. Samia pia ametajwa kufanikisha ujenzi wa nyumba bora za watumishi wa umma kote nchini.

Wito unaendelea kutolewa kwa wapiga kura kutumia kura yao "kwa Samia" mnamo Oktoba, wakisisitiza kauli mbiu ya "Kazi na utu tunasonga mbele."

Share:

MAASAI WATIKISA NCHI! TOHARA YAENDA LIKIZO KWA AJILI YA KURA: WATANZANIA WAKATAA NJAMA ZA VURUGU!

NA MWANDISHI WETU

Katika tukio adimu, lenye uzito wa kitaifa na la kihistoria, Jamii ya Kimaasai nchini Tanzania imeonyesha heshima ya hali ya juu kwa Katiba na Demokrasia kwa kuahirisha zoezi lao muhimu la kimila la tohara ili kuhakikisha vijana zaidi ya 1,000 wanashiriki kikamilifu katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Uamuzi huu uliotolewa na Laigwanani Mkuu, Isack Ole Kisongo Meijo, si tu tamko la uzalendo, bali ni pigo zito kwa wale wote wanaopanga njama za vurugu, maandamano, au mbinu za kuvuruga amani na mfumo wa kikatiba wakati au baada ya uchaguzi.

Darasa la Uzalendo kwa Taifa

Kwa kuahirisha tukio hilo kuu la kimila, ambalo kwa kawaida huathiri uwezo wa vijana wengi kushiriki kupiga kura, Maasai wameweka kiwango kipya cha kuheshimu mfumo wa kidemokrasia. 

Laigwanani Ole Kisongo alisisitiza wazi kuwa amani, uwajibikaji wa kiraia, na kura ni kipaumbele kinachozidi hata matukio makuu ya utamaduni wao.

"Jamii ya Kimaasai imeonesha mfano wa kuigwa. Huu ndio uzalendo tunaoutaka. Kura ndiyo sauti ya maendeleo, na amani ndiyo msingi wa taifa letu," alikariri Mkuu wa Mkoa wa Arusha, CPA Amos Makalla, akipongeza hatua hiyo.

Pigo kwa Wapanga Vurugu

Kitendo hiki cha Maasai kimepokelewa kama ishara ya wazi kwamba Watanzania wanajua wanachotaka: Wanaamini katika mabadiliko ya kimaendeleo yanayofuata Katiba na yanayotawaliwa na amani na utulivu.

Uamuzi wa Waasai kuahirisha mila yao kwa ajili ya kupiga kura unatoa ujumbe mkali na wa moja kwa moja kwa wale wanaopanga mbinu za kuingia madarakani au kuleta mabadiliko kupitia njia za vurugu au maandamano yasiyo halali: Watanzania wamechagua sanduku la kura, siyo vurugu.

Kabla ya sherehe kuu za tohara, Maasai wameweka neno la mwisho: Wanaheshimu mfumo wa kidemokrasia na Katiba. 

Ikiwa kabila lenye utamaduni tajiri linaamini kwenye kura, maana yake ni kwamba njia ya amani ndiyo njia pekee ya mabadiliko inayokubalika na Watanzania walio wengi.

Waasai wanawaonyesha Watanzania wote njia: Kura Kwanza, Vurugu Haikubaliki. Hii inathibitisha kuwa utashi wa Taifa ni kuona maendeleo ya nchi yanaendelea katika mazingira ya utulivu na uwajibikaji wa kikatiba.




Share:

Sunday, 19 October 2025

MAANDAMANO YAKOSA WADAU

 

Na Mwandishi Wetu.

Mwanaharakati wa mitandaoni, Mange Kimambi, amejikuta katika hali ya aibu baada ya maandamano aliyoyatisha nchini Marekani tarehe 17 Oktoba 2025 kushindwa kuvutia umati kama alivyotarajia.

Licha ya kufanya kampeni kubwa kupitia mitandao ya kijamii na kutoa ahadi kwamba Watanzania wengi wanaoishi Marekani wangekwenda kumuunga mkono, tukio hilo lilishuhudia mahudhurio duni, hali iliyoashiria ukosefu wa uungwaji mkono wa kweli.

Tukio hilo limebainisha ukweli kwamba sauti kubwa mtandaoni si kigezo cha ushawishi katika uhalisia. Mange, ambaye amejitambulisha kwa  muda mrefu kama msemaji wa wananchi, inaonekana hakusoma kwa  usahihi mtazamo na hisia za Watanzania wanaoishi nje ya Nchi kuhusu ajenda zake za kisiasa na kijamii.

Wengi wa Watanzania wanaoishi Marekani wameonekana kuchoshwa na siasa za majukwaa ya mtandao na badala yake wanaunga mkono mabadiliko ya kweli yanayoendelea kufanywa nchini Tanzania chini ya  uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Kwa ujumla, kushindikana kwa maandamano hayo ni somo muhimu kwa wanaharakati wote kwamba nguvu ya maneno mtandaoni haiwezi kuchukua nafasi ya vitendo halisi.

Ni wazi kwamba watanzania wanatakiwa kutafakari kwa kina kile kilichotokea Marekani na uhalisia wa mambo kwani wao ndiyo hasa wanaoshuhudia maendeleo yanayoendelea kuonekana kuliko hao walioko nje ya Nchi.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger