Thursday, 16 October 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI OKTOBA 16,2025

Magazeti
 
Share this Article
Share:

KUELEKEA OKTOBA 29 MGOGORO WA CHADEMA WAGEUKA ISHARA YA UTULIVU

Na Mwandishi wetu

Wimbi kubwa la viongozi wa CHADEMA kutoka Kanda ya Ziwa (Victoria) kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) limezua simanzi ofisini mwa chama hicho cha upinzani, lakini wachambuzi wa siasa nchini wanatafsiri hatua hiyo kama dalili njema ya kujengeka kwa utulivu wa kisiasa nchini kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Uamuzi wa kuondoka, unaowahusisha viongozi mashuhuri kama Ezekia Wenje, aliyekuwa Mwenyekiti wa Kanda ya Ziwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, unatajwa na wataalamu kuwa ni ishara ya mwelekeo wa utulivu unaotafutwa na Watanzania. Wenje na viongozi wengine zaidi ya 20 wa ngazi za mikoa na wilaya, wamehama wakidai CHADEMA imepoteza dira, imejaa migawanyiko, ubinafsi, na imekuwa chombo cha kufanikisha ajenda binafsi.

"Uamuzi wa kuhama haukuwa rahisi, lakini tumefikia hatua hii kwa sababu CHADEMA imejaa migawanyiko, ubinafsi, na vitendo vya kukandamiza mawazo ya viongozi wake wa chini," alisisitiza Wenje, akihitimisha kuwa chama hicho kinakosa uwezo wa kuongoza.

Mtazamo Mpya: Kutoka Hasira Kwenda Utulivu

Badala ya kuona uhamaji huu mkubwa kama kuporomoka kwa upinzani, baadhi ya wachambuzi wanakazia mtazamo kuwa matukio haya ni dalili za siasa za maridhiano na utulivu zinazokua nchini:

Kutafuta Utulivu wa Kisiasa: Maamuzi ya wanachama na viongozi hawa kujiunga na CCM, hasa wiki mbili kabla ya Uchaguzi Mkuu, yanatafsiriwa kama uthibitisho kwamba wananchi na viongozi wanatenga 'siasa za migogoro' na kujiweka upande wa utulivu, umoja, na maendeleo endelevu. Wananchi wengi sasa wanathamini mustakabali wenye uhakika na amani, kuliko siasa za misuguano.

Kukubalika kwa Dira: Hatua ya viongozi hao kujiunga na Chama Tawala inachukuliwa na CCM kama uthibitisho wa kukubalika kwa sera za maendeleo na uongozi wa uwazi unaotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita. Wanaoondoka wanatafuta uongozi wenye mwelekeo wazi na matokeo yanayoonekana.

Ishara ya Ukomavu wa Kisiasa

CCM imepokea shangwe uhamaji huu, ikisema kuwa ni ishara ya ukomavu wa kisiasa na kukua kwa imani ya wananchi katika chama hicho kuelekea Uchaguzi wa Oktoba 2025.

Kwa hali ilivyo sasa, uhamaji huu mkubwa unatoa ujumbe kuwa mwelekeo wa siasa za Tanzania unaendelea kubadilika. Uongozi wa uwazi, maendeleo yanayoonekana, na siasa za maridhiano zimekuwa kivutio kikubwa kwa Watanzania wanaotaka mustakabali wenye utulivu na matumaini mapya. Maamuzi haya ya wanachama wa Kanda ya Ziwa yanaashiria wananchi wanachagua 'sauti ya utulivu' katika kiongozi wao.

Share:

Wednesday, 15 October 2025

MTAALAMU WA LISHE HANDENI AFICHUA SIRI YA MAKUNDI SITA YA CHAKULA BORA


HANDENI-TC

Afisa Lishe wa Halmashauri ya Mji Handeni, mkoani Tanga, Esther Herman, ametoa wito kwa wananchi kuzingatia ulaji wa chakula bora kinachojumuisha makundi sita muhimu ili kuepuka magonjwa yatokanayo na lishe duni.

Akizungumza katika Maonesho ya Wiki ya Chakula Duniani yanayofanyika kitaifa jijini Tanga, chini ya kaulimbiu “Tuungane pamoja kupata chakula bora kwa maisha bora ya baadaye”, Esther ametaja makundi hayo ni wanga, protini, mboga za majani, matunda, mafuta pamoja na maji.

Amesema kila kundi lina umuhimu wake mwilini, na ulaji usio sahihi unaweza kusababisha udhaifu wa kinga ya mwili, utapiamlo, au uzito uliopitiliza.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa elimu ya lishe kuanzia ngazi ya kaya, akibainisha kuwa jamii nyingi bado hazina uelewa sahihi kuhusu mlo kamili, jambo linalochangia changamoto za afya kwa watoto na watu wazima.
Share:

BARRICK BULYANHULU YAENDELEA KUDUMISHA UHUSIANO MZURI NA JAMII KUPITIA JUKWAA LA MICHEZO

Mchezo kati ya timu ya Mgodi wa Barrick Bulyanhulu na Sixers ukiendelea
Mchezo kati ya timu ya Mgodi wa Barrick Bulyanhulu na Sixers ukiendelea
Wachezaji timu ya Mgodi wa Barrick Bulyanhulu na Sixers wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo

***
Mgodi wa Barrick Bulyanhulu uliopo katika halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga, umeendelea kujenga uhusiano mzuri na jamii za maeneo yanaozunguka mgodi kupitia jukwaa la michezo ambapo Oktoba 14,2025 timu ya mpira wa kikapu inayoundwa na wafanyakazi wa mgodi iliikaribisha timu ya Sixers kutoka Kahama katika mechi ya kirafiki ambapo Bulyanhulu imeibuka na ushindi wa vikapu 33-30.

Migodi ya Barrick ya Bulyanhulu na North Mara inazo programu za kuwawezesha wafanyakazi wake kushiriki katika michezo mbalimbali kwa ajili ya kujenga afya zao.

Pia imekuwa ikiandaa mashindano mbalimbali yanayojumuisha jamii za maeneo yanayozunguka mgodi kwa ajili ya kujenga uhusiano mzuri na kuzipatia fursa kufahamu shughuli za migodi hiyo.
Wachezaji timu ya Sixers wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo
Wachezaji timu ya Sixers wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo
Wachezaji timu ya Mgodi wa Barrick Bulyanhulu wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo
Wachezaji timu ya Mgodi wa Barrick Bulyanhulu na Sixers wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo
Wachezaji timu ya Mgodi wa Barrick Bulyanhulu na Sixers wakipata maelekezo kabla ya mchezo
Wachezaji timu ya Mgodi wa Barrick Bulyanhulu na Sixers wakipata maelekezo kabla ya mchezo
Mchezo kati ya timu ya Mgodi wa Barrick Bulyanhulu na Sixers ukiendelea
Mchezo kati ya timu ya Mgodi wa Barrick Bulyanhulu na Sixers ukiendelea
Mchezo kati ya timu ya Mgodi wa Barrick Bulyanhulu na Sixers ukiendelea
Mchezo kati ya timu ya Mgodi wa Barrick Bulyanhulu na Sixers ukiendelea
Baadhi ya wafanyakazi wa Barrick Bulyanhulu wakifuatilia mchezo
Share:

SIMULIZI YA KUTISHA YA DEREVA WA MALORI: AWAAMBIA WATANZANIA UKWELI MCHUNGU



                 Na Mwandishi wetu 

Dereva wa malori anayejitambulisha kama Sudi Manyangari, amechukua jukwaa la mtandao wa kijamii wa TikTok na kutoa simulizi nzito, yenye kutisha, akilenga kuwaambia Watanzania umuhimu wa kulinda amani yao kwa gharama yoyote. 

Manyangari, ambaye amejitaja kuwa mmoja wa watetezi wa amani nchini, anasema video yake imelenga kuamsha umma kwa vitendo, si kwa maneno matupu.

Katika video hiyo iliyoteka hisia za wengi, Manyangari alisimulia kisa kimoja cha safari zake za usafirishaji wa mizigo nchini Kongo DRC. Alieleza jinsi alivyopita mji iliyobaki mahame akiwa anaelekea eneo la wa Kongo la Beni kwa kupitia mpaka wa Kasindi nchini Uganda.

"Nimeona kutia uzito hili nikupeni kisa kimoja. Mimi nilipita miji kadhaa ya Kongo... la ajabu unakuta miji mikubwa kabisa, miji ambayo kama Kibaha ninapoishi mimi, mji una kila kitu, lakini miji imefungwa, hakuna watu. Nyumba zimefungwa, hakuna mnyama," alisema Manyangari.

Sehemu ya kutisha zaidi ya simulizi hiyo ni anavyoelezea hali aliyoikuta barabarani: "Barabarani unakutana na maiti za wanaume na wanawake zimekatwa vichwa."

Manyangari alieleza jinsi alivyojikuta peke yake bila utingo (turnboy), akijawa na hofu kali  kwa mazingira hayo akitamani kuruka na kukimbia.
Anasema alikwama katika mlima, na kusaidiwa kuondoka katika mlima huo na madereva waliokuwa wanasafirisha shehena kutoka Mombasa.

Dereva huyo alisema kuwa hali hiyo ya machafuko aliyoshuhudia, ambayo anasema ni kama umetembea katika maafa ni mfano mdogo tu wa namna hali inavyokuwa amani inapotoweka.

Ujumbe huu mzito unawahimiza Watanzania kuthamini na kulinda amani yao, wakichukua funzo kutoka kwa hali mbaya ya nchi majirani.



Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger