Monday, 13 October 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU OKTOBA 13,2025


magazeti

Share:

Sunday, 12 October 2025

UJENZI WA MADARAJA LINDI KUIMARISHA MIUNDOMBINU BAADA YA MAFURIKO



Serikali imeanza utekelezaji wa mpango mkubwa wa kujenga na kukarabati miundombinu ya barabara na madaraja yaliyoharibiwa na mafuriko mkoani Lindi, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kudhibiti athari za mvua kubwa na matukio ya hali ya hewa kama El-Nino na Kimbunga Hidaya.

Kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), miradi 13 ya dharura yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 119 inaendelea kutekelezwa katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo ili kurejesha mawasiliano na kuhakikisha wananchi wanaendelea na shughuli zao za kiuchumi bila vikwazo.

Miongoni mwa miradi hiyo ni ujenzi wa madaraja ya Kipwata, Mikereng’ende, Somanga Mtama na Njenga II kwenye Barabara Kuu ya Marendego – Lindi – Mingoyo, pamoja na miradi ya Boksi Kalavati katika maeneo ya Sakura, Songas na Mtandango.

Katika Barabara ya Mkoa ya Nangurukuru – Liwale, ujenzi unaendelea katika madaraja ya Miguruwe, Zinga na Kimambi, huku barabara ya Liwale – Nachingwea ikishuhudia kazi za ujenzi wa madaraja ya Nangano na Mbwemkuru II pamoja na makalavati ya dharura.

Aidha, TANROADS inaendelea na ujenzi wa madaraja ya Nakiu na Kigombo katika barabara ya Kiranjeranje – Namichiga, pamoja na makalavati sita katika barabara ya Tingi – Kipatimo.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa miradi hiyo, Msimamizi wa Kitengo cha Miradi ya Maendeleo TANROADS mkoa wa Lindi, Mhandisi Fred Sanga, alisema zaidi ya shilingi bilioni 58.5 zimeshalipwa kwa wakandarasi na utekelezaji unaendelea kwa kasi, ukitarajiwa kukamilika ifikapo Desemba mwaka huu.

Kwa mujibu wa Mhandisi Sanga, katika mwaka wa fedha 2025/2026 Serikali imepanga kutumia shilingi bilioni 16.2 kwa matengenezo na maendeleo ya barabara mkoani humo, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa kilomita 405.15 za lami na kilomita 901.54 za changarawe pamoja na madaraja matatu katika barabara za Kilwa Masoko – Liwale, Matangini – Chiola – Likunja na Chiola – Ruponda.

Mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa za Oktoba 2023 hadi Mei 2024 yaliharibu kwa kiwango kikubwa miundombinu ya barabara mkoani Lindi, na kusababisha maeneo mengi kukosa mawasiliano. 

Serikali, chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ilitenga shilingi bilioni 19 kwa ajili ya matengenezo ya dharura ili kurejesha miundombinu hiyo kwa haraka.


Share:

SERIKALI KUPITIA TANROADS YATEKELEZA UJENZI WA MIRADI 13 YA DHARURA MKOANI LINDI


Kwa sasa Serikali kupitia Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) inaendelea na utekelezaji wa ujenzi wa miradi 13 ya dharura katika mkoa wa Lindi ambayo itatumia jumla ya shilingi Bilioni 119 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa miradi hiyo ya dharura.

Miradi hiyo ni pamoja na Ujenzi wa Daraja la Kipwata (Mita 40) na Boksi kalavati eneo la Sakura na Songas, Ujenzi wa Daraja la Mikereng’ende (mita 40) na Boksi kalavati katika maeneo ya Mtandango/Stakshari na Masaninga, Ujenzi wa Boksi kalavati la Mbwemkuru I (seli 4, 5m x 4m), na matuta ya kuzuia mmomomnyoko wa udongo ( Spur dykes), Ujenzi wa Daraja la Somanga Mtama (60m) na Ujenzi wa Daraja la Njenga II (60m) ambapo miradi yote hii ipo katika barabara Kuu ya Marendego – Lindi – Mingoyo

Miradi mingine ni Ujenzi wa Daraja la Miguruwe (39m) pamoja na Boksi kalavati nne (4), Ujenzi wa Daraja la Zinga (18m) na Ujenzi wa Daraja la Kimambi (39m) ambayo ipo katika Barabara ya Mkoa ya Nangurukuru – Liwale.

Fedha hizo zinaendelea na utekelezaji wa miradi ya Barabara ya Mkoa ya Liwale – Nachingwea ambayo ni Ujenzi wa Daraja la Nangano (20m) na Makalavati ya Dharura ya mawili ya vipimo 2x2, mawili ya vipimo 5x2.5, Ujenzi wa Daraja la Mbwemkuru II (64m). Katika Barabara ya Mkoa ya Kiranjeranje- Namichiga serikali inaendelea na Ujenzi wa Daraja la Nakiu (70m) na Ujenzi wa Daraja la Kigombo (25m) na kalavati ya vipimo vya 5x4 huku katika Barabara ya Mkoa ya Tingi – Kipatimo Ujenzi wa Makalavati sita (6) ukiwa unaendelea.

Akizungumza mara baada ya kutembelea na kukagua hatua zilizofikiwa za ujenzi wa miradi hiyo Msimamizi wa kitengo cha miradi ya Maendeleo TANROADS Mkoa wa Lindi Mhandisi Fred Sanga amesema kuwa mpaka sasa jumla ya shilingi Bilioni 58.5 zimeshalipwa kwa mkandarasi na kazi inaendelea kwa kasi ambayo itakamilika Disemba mwaka huu.

Aidha, Mhandisi Sanga amesema kuwa katika mwaka wa fedha 2025/2026 serikali imepanga kutumia Bilioni 16.2 kwa ajili ya Miradi ya Matengezo (Maintenance) kwa gharama ya Shilingi bilioni 13.3 huku Miradi ya Maendeleo (Development) ikitarajiwa kutumia shilingi Bilioni 2.9 kwa ajili ya ujenzi wa kilomita 405.15 za barabara za lami sambamba na ujenzi wa kilomita 901.54 za barabara za Changarawe.

Mhandisi Sanga amesema kuwa katika mpango huo kutakuwa na ujenzi wa madaraja 3 katika barabara ya Kilwa Masoko – Liwale, barabara ya Matangini -Chiola - Likunja na barabara ya Chiola – Ruponda

Kuanzia Oktoba, 2023 hadi kufikia Mei, 2024 Tanzania ilikumbwa na kadhia ya mvua kubwa zilizotawala zikichangiwa na tukio la asili la hali ya hewa El-Nino pamoja na Kimbunga Hidaya lililoathiri hali ya hewa nchini na kusababisha athari hasi kwa wananchi kukosa makazi, vifo, magonjwa ya milipuko, uharibifu wa miundombinu ya barabara pamoja na madaraja.

Katika eneo la Miundombinu, Barabara za Mkoa wa Lindi ziliathirika kwa kiasi kikubwa kutokana na madhara ya mvua hizo zilizonyesha mfululizo ambapo hata hivyo Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ikatoa fedha jumla ya Shilingi za kitanzania bilioni 19 kwa ajili ya matengenezo ya dharula na kurejesha mawasiliano kwa haraka.


Share:

MCHENGERWA AWAFUNDA VIONGOZI WAPYA WA UDART, DART


Na John Mapepele

Waziri wa TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa leo amekutana na viongozi wapya wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) na Kampuni ya Mabasi Yaendayo Haraka (UDART) na kuwataka kutatua mara moja changamoto ya usafiri wa jiji la Dar es Salaam na kuifanya historia.

Viongozi hao wapya walioteuliwa hivi Karibuni na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan waliohudhuria kikao hicho kilichoitishwa na Waziri Mchengerwa ni Mwenyekiti wa Bodi ya DART, David Kafulila na UDART, Balozi, Dkt. Ramadhan Dau na Watendaji Wakuu wa taasisi hizo.
Mhe. Waziri Mchengerwa ameambatana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Adorf Ndunguru na Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI, Sospita Mtwale ambapo amesema dhamira ya Serikali ni kuona wananchi wanapata huduma bora.

"Ndugu zangu nendeni mkafanye kazi kwa weledi na kuondoa kabisa changamoto ya usafiri kwa wananchi wetu, hakuna sababu yoyote kwa sasa kuendelea na changamoto hiyo wakati Serikali imeshafanya mapinduzi makubwa kwenye suala la miundombinu na usafiri kwa ujumla katika jiji la Dar es Salaam". Amefafanua Mhe. Mchengerwa 

Amesema baada ya kuboresha huduma hii katika jiji la Dar es Salaam, Serikali itaendelea kupanua katika maeneo mengine nchini.


Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mabasi Yaendayo Haraka (UDART) Balozi Dkt. Ramadhani Kitwana Dau amemhakikishia Mhe. Mchengerwa kuwa viongozi wa UDART na DART wanakwenda kufanya kazi kwa kushirikiana ili kuleta mapinduzi makubwa katika kuondoa kabisa changamoto ya usafiri.

"Mheshimiwa Waziri kwa niaba ya wenzangu naomba nitumie nafasi hii kukuhakikishia kwamba katika kipindi kifupi tunakwenda kutekeleza maelekezo yako ya kuboresha huduma, lakini pia tunaomba utufikishie salamu za shukrani kwa Mhe. Rais kwa imani aliyotupatia ya kututeua katika nafasi hizi. Tunaahidi hatutamwangusha". amesisitiza Balozi Dau.

Aidha, amefafanua kuwa hakuna sababu kwa UDART kupata harasa endapo kutakuwa na usimamizi madhubuti na kusisitiza kwamba uongozi wa sasa utakwenda kusimamia kikamilifu ili kutimiza ndoto za mheshimiwa Rais.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI OKTOBA 12,2025

Magazeti
 
Share this Article
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger