Friday, 4 April 2025

BENKI YA DUNIA YAZITAKA TAASISI ZINAZOTEKELEZA MRADI WA HEET KUONGEZA KASI KATIKA UJENZI WA MIUNDOMBINU


Mwakilishi wa Benki ya Dunia, Bw. Nkahiga Kaboko, akizungumza wakati wa Kikao cha wadau watekelezaji wa Mradi wa HEET waliokutana Dar es Salaam.
........
Benki ya Dunia (WB), imetoa wito kwa Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu Tanzania zinazotekeleza Mradi wa Elimu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET), kuongeza kasi katika eneo la ujenzi wa miundombinu na usimamizi, kutokana na kasi ndogo katika ujenzi wa Miundombinu inayoonekama kwa vyuo vingi kwa sasa.

Hayo yameelezwa leo Alhamisi tarehe 03 Aprili 2025, siku ya pili ya kikao cha pamoja kati ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia; Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu nchini, zinazotekeleza Mradi wa HEET na Benki ya Dunia, kinachoendelea katika Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Akizungumza wakati akichangia kwenye uwasilishaji wa moja ya taarifa za maendeleo ya Mradi; Mwakilishi wa Benki ya Dunia, Bw. Nkahiga Kaboko, amesema ni vizuri vyuo vikaongeza umakini katika kuwasimamia wakandarasi ili kumaliza kwa wakati shuguli za ujenzi kama yalivyo malengo ya mradi, badala ya kutegemea muda wa mradi kuongezwa.

Naye Mkurugenzi wa Elimu ya Juu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Peter Msofe, ametilia msisitizo suala hilo na kutoa msimamo wa Wizara kuendelea kufuatia kwa karibu utekelezaji wa agizo hilo akiwataka wahusika wote wa Mradi kuhakikisha usimamizi wa kutosha unafanyika, ili wakandarasi waweze kutimiza wajibu wao kwa mujibu wa mikataba.

“Jitahidini kuongeza usimamizi na umakini kwa wakandarasi ili wamalize kazi kwa muda uliokubalika, kasi ya ujenzi kwa vyuo vingi bado hairidhishi na muda tuliobaki nao kufika Juni 2026, ni mdogo” alisisitiza

Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji kwa Chuo Kikuu cha Dodoma, Mratibu Msaidizi wa Mradi, Dkt. Happiness Nnko; amesema kwa upande wa Miradi ya Ujenzi, Chuo kinaendelea na Ujenzi wa Madarasa Ndaki ya Sayansi za Ardhi na Uhandisi CoESE, ambao umekamilika kwa asilimia 24.8, ujenzi wa Maabara Ndaki ya Sayansi Asilia na Hisabati (CNMS) asilimia 9%, wakati ujenzi wa Kampasi mpya Njombe bado haujaanza; kutokana na taratibu za manunuzi za kumpata Mkandarasi wa Ujenzi kutokamilika.

Amesema changamoto kubwa katika ujenzi wa miundombinu zinatokana na mlolongo mrefu wa kuwapata wakandarasi wenye sifa huku baadhi ya wakandarasi kukosa vibali na hivyo kuchangia kwa sehemu kubwa ujenzi kuchekewa kuanza.

“Miradi yote hii imepangwa kukamilika mapema mwaka 2026, na Menejimenti ya Chuo Kikuu cha Dodoma, imejipanga kuhakikisha Miradi yote inakamilika kwa wakati uliopangwa pamoja na changamoto zilizopo” Alisisitiza Dkt. Nnko.

Aidha; ameyataja maeneo mengine ambayo UDOM imefanya vizuri kuwa ni pamoja na kuhamasisha wanafunzi kusoma masomo ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hesabu (STEM) ambapo hadi kufikia kipindi cha taarifa hii, Chuo kimefanikiwa kwa asilimia 84.9% ya malengo, ambapo kati ya wanafunzi 44,567 waliokusudiwa kufikiwa nchi nzima, UDOM imewafikia wanafunzi 34,241; kati ya hao wanawake ni asilimia 32.3% na wanafunzi wenye mahitaji maalumu 214.

Kwa Chuo Kikuu cha Dodoma, Mradi wa HEET unatekelezwa kwa tengeo la bajeti la jumla ya Dola za Kimarekani 23,000 na miradi yote inatazamiwa kukamilika mwezi Juni 2026.
Kiongozi kutoka Timu ya Benki ya Dunia, Prof. Roberta Malee, akichangia mada wakati wa majadiliano kuhusu utekelezaji wa Mradi wa HEET wakati wa Mkutano wa Wadau wa Mradi unaoendelea jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Benki ya Dunia, Bw. Nkahiga Kaboko, akizungumza wakati wa Kikao cha wadau watekelezaji wa Mradi wa HEET waliokutana Dar es Salaam.
Mratibu Msaidizi, Mradi wa HEET Chuo Kikuu cha Dodoma, Dkt. Happiness Nnko, akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Mradi kwa Chuo Kikuu cha Dodoma, wakati wa kikao cha Wadau kinachoendelea jijini Dar es Salaam
Wawakilishi wa Vyuo Vikuu mbalimbali nchini wanufaika wa Mradi wa HEET, wakiwa kwenye mjadala wa pamoja baada ya kufanya mawasilisho.
Mkurugenzi wa Elimu ya Juu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Peter Msofe, akizungumza wakati wa kikao cha Wadau wa Mradi wa HEET waliokutana kujadili maendeleo ya Mradi, jijini Dar es Salaam.
Share:

Thursday, 3 April 2025

DKT. NCHIMBI AWAPOKEA WANACHAMA 200 WA ACT WAZALENDO WILAYANI TUNDURU




Na Regina Ndumbaro - Malunde 1 blog

Wanachama 200 wa Chama cha ACT Wazalendo, akiwemo Katibu wa Chama hicho Jimbo la Tunduru Kusini, Saidi Mponda, pamoja na Diwani wa Kata ya Mchoteka, Sefu Hassan Dauda, wamejiunga rasmi na Chama cha Mapinduzi (CCM). 

Uamuzi wao wa kuhama ACT Wazalendo na kujiunga na CCM umetokana na kuridhishwa na utendaji wa Serikali ya Chama cha Mapinduzi chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, hususan katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

viongozi hao waliotoka ACT Wazalendo wamesema wamevutiwa na namna Serikali ya CCM inavyojitahidi kuboresha sekta za miundombinu, afya, elimu na uchumi kwa ujumla. 
Wameeleza kuwa maendeleo yanayoonekana katika wilaya ya Tunduru na maeneo mengine nchini ni kielelezo cha uongozi imara wa CCM, hivyo wakaona ni busara kujiunga na chama hicho ili kushiriki kikamilifu katika maendeleo hayo.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Mlimgoti, wilayani Tunduru, Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Emmanuel Nchimbi, amewapongeza wanachama hao kwa uamuzi wao wa kujiunga na CCM. 

Amesisitiza kuwa CCM ni chama chenye misingi ya maendeleo na akatoa wito kwa wanachama wa vyama vingine kujiunga na chama hicho ili kushirikiana katika kuleta maendeleo kwa Watanzania wote.

Aidha, Dkt. Nchimbi ametumia fursa hiyo kuwaeleza wananchi kuhusu dhamira ya CCM kuendelea kusimamia maendeleo na kuhakikisha kila Mtanzania anafaidika na rasilimali za nchi. 

Amesema kuwa Serikali inayoongozwa na CCM itaendelea kutekeleza miradi ya kimkakati inayolenga kuboresha maisha ya wananchi na kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla.

Dkt. Nchimbi ametoa wito kwa Watanzania wote kuilinda amani ya nchi kwa nguvu zote. 

Amesisitiza kuwa amani ni nguzo muhimu kwa maendeleo na ustawi wa jamii, hivyo ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha taifa linaendelea kuwa na mshikamano na utulivu ili miradi ya maendeleo iweze kuwanufaisha wananchi wote.
Share:

NAIBU WAZIRI NDERIANANGA AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA TATU WA KIMATAIFA WA WATU WENYE ULEMAVU UJERUMANI



NA. MWANDISHI WETU BERLIN – UJERUMANI

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Mheshimiwa Ummy Nderiananga ameongoza ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaoshiriki Mkutano wa Tatu wa Kimataifa wa Watu wenye Ulemavu unaofanyika jijini Berlin, Ujerumani tarehe 2 hadi 3 April,2025.

Mkutano huo umeandaliwa na Shirikisho la Kimataifa wa Watu Wenye Ulemavu (IDA), Serikali ya Ujerumani, na Serikali ya Jordan na kufunguliwa rasmi kwa pamoja na Kansela wa Ujerumani Mhe. Olaf Scholz na Mfalme Abdullah II wa Jordani.

Akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa Mkutano huo Mhe. Scholz amesisitiza juu ya umuhimu wa kushirikiana kimataifa kukuza haki na ujumuishaji wa masuala ya Watu Wenye Ulemavu.

“Ushirikiano wa kimataifa ni nguzo muhimu katika kuhakikisha haki na ujumuishaji wa watu wenye ulemavu unatekelezwa kikamilifu duniani kote kwa kushirikiana, serikali, mashirika ya kimataifa, sekta binafsi, taasisi za elimu, mashirika ya kiraia, na Mashirika ya Watu Wenye Ulemavu tunaweza kuunda sera na mipango madhubuti inayohakikisha usawa wa fursa na ushiriki kamili wa watu wenye ulemavu katika jamii, “ alisisitiza.

Naye Mfalme Abdullah II wa Jordani akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo alisisitiza dhamira ya dhati ya kuendeleza haki na ujumuishaji wa watu wenye ulemavu.

Mfalme Abdullah II alitilia mkazo umuhimu wa ushirikiano wa kimataifa katika kuhakikisha fursa sawa na ushiriki kamili wa watu wenye ulemavu katika nyanja zote za jamii.

Mkutano huo unalenga kuhamasisha juhudi za kimataifa katika kufanikisha ujumuishaji wa watu wenye ulemavu duniani na kuwaleta pamoja wadau wa ngazi za juu kujadili na kushiriki maendeleo katika ujumuishaji wa watu wenye ulemavu, kutoka serikalini, mashirika ya kimataifa, sekta binafsi, taasisi za elimu ya juu, mashirika ya kiraia na mashirika ya watu wenye ulemavu kutoka nchi mbalimbali.

Mkutano wa Kimataifa wa Watu wenye Ulemavu (GDS) ni jukwaa la kipekee la kimataifa linaloangazia uboreshaji wa maisha ya watu wenye ulemavu, hususan kutoka Kusini mwa Dunia.

Mkutano huo ulianzishwa mwaka 2017 kwa lengo la kuwakutanisha wadau wa kimataifa, kikanda, na kitaifa wanaoshiriki malengo na maono ya maendeleo jumuishi kwa watu wenye ulemavu na hatua za kibinadamu.

Mkutano huu unalenga kuziba pengo kati ya nyanja mbili za ujumuishaji watu wenye ulemavu na ushirikiano wa maendeleo.

Mkutano wa Kimataifa wa Watu wenye Ulemavu hufanyika kila baada ya miaka mitatu ni jukwaa linalohusisha utetezi wa mara kwa mara na wadau wa maendeleo ya wenye ulemavu kimataifa pamoja na kuhamasisha vuguvugu la haki za watu wenye ulemavu na washirika wake duniani.

Mkutano huo pia unaangalia namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya nchi wanachama na Mashirika ya Watu Wenye Ulemavu (OPDs) kupitia mipango ya pamoja ya uandaaji wa mkutano.







Share:

Wednesday, 2 April 2025

Video Mpya : SIX MAN - GALUME

 

Share:

JE, HUJUI FEDHA ZAKO ZINAKWENDA WAPI?

Jina langu Paulo kutoka Mbeya, katika maisha yangu hadi sasa nimefikisha umri wa miaka 41, nimefanya kazi sana katika kampuni nyingi, nilikuwa napata fedha za kunitosha mimi na familia yangu.

Kwa moyo wa kujituma na nidhamu, niliendelea kufanya kazi vizuri  kila mwisho wa mwezi nilikuwa naingiziwa kwenye akaunti yangu ya benki, lakini ikawa siku zinavyozidi kwenda sioni fedha zangu wala matumizi yake.

Yaani ilikuwa kila nikipata fedha sijui zinaishaje, sizioni nikizitumia kwa faida hadi nikakata tamaa ila nikawa naendelea kufanya kazi bila kujua fedha zinapotelea wapi, ni jambo ambalo lilikuwa linanipa sana msongo wa mawazo kupita kiasi.

Unajua kila mtu anapofanya kazi anataka kuona na maisha yake yakibadilika na kusonga mbele, hakuna mtu anayetaka kufanya kazi na kuona akiendelea kusalia katika hali ya umaskini au maisha duni yaliyokosa usawa.

Katika kuchunguza na kutafakari kwangu nikaona kabisa kuna kitu hakipo sawa katika maisha yangu hasa upande wa kutunza fedha, ila tatizo ni kwamba sikufahamu naanzia wapi kutatua shida hiyo iliyokuwa inaninyima raha maishani mwangu.

Nakumbuka katika mizunguko yangu, siku moja nilikutana na mama mmoja anatoka kazini, huyu ni rafiki yangu tuliyepotezana miaka mingi, nilimsimamisha na kumuelezea jinsi fedha zangu zinavopotea bila kujua.

Yula mama alinisikiliza na kuniambia kuna mtu atakusaidia matatizo yako, mtu huyo anajulikana kwa jina la Kiwanga Doctors kutokea Migori, Kenya, huyu atakusaidia kila aina ya changamoto unayopitia katika maisha yako. Alisema yule mama.

Alifungua pochi yake na kutoa simu yake ya mkononi kisha kunitajia namba zake, nilipofika nyumbani nikamtafuta nikamuelezea shida yangu.

Nashukuru Kiwanga Doctors alinihudumia (find lost items spell) kwa upendo mkubwa sana hadi nikajihisi vizuri ingawa nilikuwa nimetingwa na matatizo mengi sana. 

Kusema ukweli tangu wakati huo ndio ukawa mwisho wa fedha zangu kupotea, kila nikipata fedha iwe ni mshahara au njia yoyote ile basi isingeisha bila ya mimi kuona maendeleo yake, hakuna fedha inayoenda bila kujua imefanya nini hasa.

Ni watu wengi hadi sasa wamepata uponyaji na furaha kupitia huduma za Kiwanga Doctors ambao unaweza kuwasiliana na kwa namba +254 116 469840 au tembelea tovuti yao kwa maelezo zaidi kuhusu huduma zao ambazo zimewasaidia wengi. 

Share:

Tuesday, 1 April 2025

DUH! MKE AMWAGA HADHARANI SIRI NYETI ZA MUMEWE

Kwanza naomba nikiri kuwa hakuna taasisi ina siri kubwa kama ndoa jamani na hiyo ni kutokana na msingi wake wa kuanzishwa kwake, haifai hata kidogo kutoa siri za ndani ya ndoa kwa marafiki hata kama mnapendana na kuaminiana kwa kiasi gani.

Hata hivyo, nikiri wazi kuna wakati uvumilivu ulinishinda na kujikuta nimetoa siri za ndani ya ndoa yangu, sikuwa na jinsi ilinibidi nifanye hivyo ili kuweza kupata raha kama wanawake wengine au kama ilivyokuwa mwanzo.

Mimi naitwa Mama Jeni kutokea Pwani, nimeishi katika ndoa kwa miaka saba sasa na mume wangu kipenzi na tayari tumejaliwa kupata watoto wawili ambao tayari sasa wamenza shule na wanaendelea vizuri.

Mwanzo wa ndoa yetu mume wangu alikuwa akinitimizia mahitaji yangu ya msingi kama mwanamke na kufurahia sana hadi nikawa najiuliza kwanini nilichelewa kuolewa na kupata raha hizi.

Lakini ghafla mambo yalianza kwenda sivyo, mume wangu alikuwa hawezi kunifikisha katika kilele kama ilivyokuwa mwanzo, hata raundi moja tu nilikuwa sipati wakati mwanzo nilikuwa napata hata raundi nne.

Hali hiyo ilikuwa inaniacha njiapanda kiasi kwamba nilikuwa nalala na kiu, kila mara nilikuwa mtu mwenye hasira, nilijikuta nagombana na watoto hata jambo la kawaida tu ambalo sikupaswa kugombana.

Ndipo ikanibidi nimueleze rafiki yangu kuhusu hali hiyo ninayopitia katika ndoa yangu, alinisikiliza kwa makini na kunitia moyo kuwa hata yeye aliwahi kupitia changamoto hiyo lakini aliweza kuishinda.

Yeye alipata dawa kutoka kwa Kiwanga Doctors ambayo mume wake aliitumia na ndani ya muda mfupi hali ikawa nzuri, alinipatia namba ya Kiwanga Doctors na kunisisitizia niwasiliana naye kwani nitaweza kupata msaada.

Basi nilichukua hatua na kumpigia Kiwanga Doctors na kumueleza shida yote ya mume wangu, basi aliweza kunitumia dawa ambayo imekuja kurejesha furaha katika ndoa yangu ambayo niliitamani sana katika maisha yangu.

Kwa sasa mume wangu anaifanya kazi yake vizuri kiasi kwamba hadi nahisi anataka kuvunja kabisa ili tuende kununua kingine maana shughuli yake sio ya kitoto, napewa raha hadi nalia kama mtoto mdogo vile.

Huwa nafurahia sana hali hiyo maana nilikuwa nimeimisi kwa muda mrefu sana, yaani hadi naandika ujumbe huu namngoja mume wangu arejee kazini aweze kunipa raha hiyo ambayo ndio imenitoa kwa wazazi wangu. 

Ni watu wengi hadi sasa wamepata mafanikio na furaha kupitia huduma za Kiwanga Doctors ambao unaweza kuwasiliana na kwa namba +254 116469840 au tembelea tovuti yao, www.kiwangadoctors.co.tz kwa maelezo zaidi kuhusu huduma zao ambazo zimewasaidia wengi.

Share:

TEAM MARCH WATOA MSAADA KWA WATOTO NJITI NA AKINA MAMA HOSPITALI YA SHINYANGA


Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Kikundi cha watu waliozaliwa mwezi wa tatu, ‘Team March’, kilichopo Manispaa ya Shinyanga, kimetoa msaada wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya watoto wanaozaliwa kabla ya muda (‘pre-mature’) pamoja na vifaa vya mradi wa ushonaji kofia, masweta, na soksi kwa akina mama waliojifungua watoto njiti katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Wanakikundi hao wametoa msaada huo leo Aprili 1, 2025, wakiongozwa na Mwenyekiti wa ‘Team March’, Dkt. Yustina Tizeba, ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Watoto katika hospitali hiyo.

Dkt. Tizeba amesema kuwa vifaa hivyo vitasaidia watoto njiti, lakini pia vifaa vingine vitahusiana na mradi wa ushonaji waliouanzisha katika hospitali hiyo kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kijasiriamali akina mama waliojifungua watoto njiti wakati watoto wao wanaendelea kupatiwa huduma za kiafya hospitalini.

“Team March tumeanzisha mradi wa ushonaji wa kofia, masweta, soksi kwa akina mama waliojifungua watoto njiti. Tunataka kuwawezesha akina mama hawa kwa kuwapa ujuzi wa ushonaji ili waweze kujiinua kiuchumi, huku wakiendelea kutunza watoto wao hospitalini,” amesema Dkt. Tizeba.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dkt. John Luzila, amepokea msaada huo na kuwashukuru wanakikundi kwa kujitolea kuokoa maisha ya watoto njiti.

“Tunaipongeza ‘Team March’ kwa juhudi zao kubwa za kusaidia watoto njiti. Mmeacha alama kubwa katika hospitali hii. Tunawashukuru kwa namna mnavyoguswa na afya za Watanzania na tunawaomba wadau wengine waendelee kutembelea hospitali hii na kusaidia changamoto zinazojitokeza,” amesema Dkt. Luzila.


Mwenyekiti wa ‘Team March’, Dkt. Yustina Tizeba, ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Watoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga akimkabidhi Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dkt. John Luzila vifaa mbalimbali kwa ajili ya watoto wanaozaliwa kabla ya muda (‘pre-mature’) pamoja na vifaa vya mradi wa ushonaji kofia, masweta, na soksi kwa akina mama waliojifungua watoto njiti katika Hospitali hiyo vilivyotolewa na Team March
Mwenyekiti wa ‘Team March’, Dkt. Yustina Tizeba, ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Watoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga akimkabidhi Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dkt. John Luzila vifaa mbalimbali kwa ajili ya watoto wanaozaliwa kabla ya muda (‘pre-mature’) pamoja na vifaa vya mradi wa ushonaji kofia, masweta, na soksi kwa akina mama waliojifungua watoto njiti katika Hospitali hiyo vilivyotolewa na Team March
Team March wakimkabidhi Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dkt. John Luzila vifaa mbalimbali kwa ajili ya watoto wanaozaliwa kabla ya muda (‘pre-mature’) pamoja na vifaa vya mradi wa ushonaji kofia, masweta, na soksi kwa akina mama waliojifungua watoto njiti katika Hospitali hiyo
Team March wakimkabidhi Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dkt. John Luzila vifaa mbalimbali kwa ajili ya watoto wanaozaliwa kabla ya muda (‘pre-mature’) pamoja na vifaa vya mradi wa ushonaji kofia, masweta, na soksi kwa akina mama waliojifungua watoto njiti katika Hospitali hiyo
Team March wakimkabidhi Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dkt. John Luzila vifaa mbalimbali kwa ajili ya watoto wanaozaliwa kabla ya muda (‘pre-mature’) pamoja na vifaa vya mradi wa ushonaji kofia, masweta, na soksi kwa akina mama waliojifungua watoto njiti katika Hospitali hiyo
Sehemu ya vifaa kwa ajili ya watoto wanaozaliwa kabla ya muda (‘pre-mature’) pamoja na vifaa vya mradi wa ushonaji kofia, masweta, na soksi kwa akina mama waliojifungua watoto njiti katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dkt. John Luzila, akizungumza wakati akipokea msaada wa vifaa kwa ajili ya watoto wanaozaliwa kabla ya muda (‘pre-mature’) pamoja na vifaa vya mradi wa ushonaji kofia, masweta, na soksi kwa akina mama waliojifungua watoto njiti na kuwashukuru wanakikundi wa Team March kwa kujitolea kuokoa maisha ya watoto njiti.
Picha ya kumbukumbu
Kikundi cha watu waliozaliwa mwezi wa tatu, ‘Team March’, kilichopo Manispaa ya Shinyanga wakitembelea Chumba maalum cha kuhudumia watoto njiti (Pre - Mature) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga
Kikundi cha watu waliozaliwa mwezi wa tatu, ‘Team March’, kilichopo Manispaa ya Shinyanga wakitembelea Chumba maalum cha kuhudumia watoto njiti (Pre - Mature) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga
Kikundi cha watu waliozaliwa mwezi wa tatu, ‘Team March’, kilichopo Manispaa ya Shinyanga wakitembelea Chumba maalum cha kuhudumia watoto njiti (Pre - Mature) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga
Kikundi cha watu waliozaliwa mwezi wa tatu, ‘Team March’, kilichopo Manispaa ya Shinyanga wakitembelea Chumba maalum cha kuhudumia watoto njiti (Pre - Mature) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga
Kikundi cha watu waliozaliwa mwezi wa tatu, ‘Team March’, kilichopo Manispaa ya Shinyanga wakitembelea Chumba maalum cha kuhudumia watoto njiti (Pre - Mature) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga
Kikundi cha watu waliozaliwa mwezi wa tatu, ‘Team March’, kilichopo Manispaa ya Shinyanga wakitembelea Chumba maalum cha kuhudumia watoto njiti (Pre - Mature) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga
Keki maalumu ya Kikundi cha watu waliozaliwa mwezi wa tatu, ‘Team March’, kilichopo Manispaa ya Shinyanga 
Keki maalumu ya Kikundi cha watu waliozaliwa mwezi wa tatu, ‘Team March’, kilichopo Manispaa ya Shinyanga 
Zoezi la kulishana keki likiendelea
Zoezi la kulishana keki likiendelea
Zoezi la kulishana keki likiendelea
Zoezi la kulishana keki likiendelea
Zoezi la kulishana keki likiendelea
Zoezi la kulishana keki likiendelea
Zoezi la kulishana keki likiendelea
Zoezi la kulishana keki likiendelea
Zoezi la kulishana keki likiendelea
Share:

Video Mpya : JITOLATOLA MWIPWA WA GUDEGUDE - MAISHA

 

Share:

Video Mpya : LIMBU LUCHAGULA Ft. MAYIKU SAYI - JOYCE

 

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger