Monday, 23 September 2024

RC BATILDA AWATAKA WAKAZI WA TANGA KUJIEPUSHA NA VIASHIRIA VYA UVUNJIFU WA AMANI KUELEKEA UCHAGUZI



Na Hadija Bagasha Tanga,

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Dkt. Batilda Burian amewataka wakazi Mkoani Tanga kujiepusha na vitendo vyote vinavyoashiria uvunjifu wa amani katika kipindi hiki ambacho Taifa linaelekea katika Uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi Mkuu baadae mwakani.

Balozi Dkt.  Batilda ametoa wito huo Septemba 22,2024 katika kilele cha tamasha kubwa la Utalii wilayani Lushoto la USAMBARA TOURISM FESTIVAL lililofanyika kwa siku mbili katika viwanja vya Nyerere Square, ambapo amesema ni jukumu la kila mwanatanga kuhakikisha amekuwa sehemu ya amani na utulivu kuanzia kipindi hiki ambacho wananchi wameanza kujiandikisha katika daftari la mpiga kura ili kupata nafasi ya kuchagua viongozi makini watakao waongoza na kuwaletea maendeleo ya kweli.

Katika hatua nyingine Balozi Dkt. Batilda amewataka waratibu na wasimamizi wa uchaguzi kuhakikisha wanaweka juhudi katika kutoa elimu na kuwashirikisha wananchi wa ngazi zote ikiwemo viongozi wa kimila na waandishi wa vyombo vya habari katika kutoa elimu ya uchaguzi.

Awali akizungumzia Utalii Dkt.Batilda amesema Wilaya ya Lushoto imebarikiwa kwa vivutio mbalimbali vya utalii na hivyo kuwa sehemu ya kichocheo cha maendeleo na kupongeza uongozi wa Wilaya ya Lushoto kufanikisha ujenzi wa kituo cha utalii ambacho kitasaidia upatikanaji wa taarifa muhimu za utalii.

Amewaelekeza viongozi wa Wilaya zingine za Mkoa wa Tanga kuwa na vituo vya utalii ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa kwa wageni wanaotembelea maeneo hayo.

Akizungumza kwa niaba ya Benki ya NMB Meneja Mahusiano wa Benki ya NMB na Serikali Peter Massawe amesema Benki hiyo ipo katika mchakato wa kusaidia sekta ya Utalii kwa kukaa na watenda kazi wa Sekta hiyo na kuona wanauhitaji wa mambo gani na kiasi gani ili kushirikiana kwa pamoja kukuza Sekta hii.

Tamasha la Usambara Tourism Festival limefanyika kwa mara ya kwanza Wilayani Lushoto na kuhusisha shughuli mbalimbali ikiwemo kutembelea vivutio vya utalii, maonesho ya biashara, shughuli za taasisi mbalimbali na kufanyika kwa mbio Usambara Marathoni kwa washiriki wa Km 21, Km 10 na KM 5 mbio zilizo ongozwa na mkuu wa Wilaya ya Lushoto Zephania Sumaye

Share:

RC BATILDA AWATAKA WAKAZI WA TANGA KULINDA AMANI KUELEKEA UCHAGUZI

Na Hadija Bagasha Tanga,

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Dkt. Batilda Burian amewataka wakazi Mkoani Tanga kujiepusha na vitendo vyote vinavyoashiria uvunjifu wa amani katika kipindi hiki ambacho Taifa linaelekea katika Uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi Mkuu baadae mwakani.

Balozi Dkt.  Batilda ametoa wito huo Septemba 22,2024 katika kilele cha tamasha kubwa la Utalii wilayani Lushoto la USAMBARA TOURISM FESTIVAL lililofanyika kwa siku mbili katika viwanja vya Nyerere Square, ambapo amesema ni jukumu la kila mwanatanga kuhakikisha amekuwa sehemu ya amani na utulivu kuanzia kipindi hiki ambacho wananchi wameanza kujiandikisha katika daftari la mpiga kura ili kupata nafasi ya kuchagua viongozi makini watakao waongoza na kuwaletea maendeleo ya kweli.

Katika hatua nyingine Balozi Dkt. Batilda amewataka waratibu na wasimamizi wa uchaguzi kuhakikisha wanaweka juhudi katika kutoa elimu na kuwashirikisha wananchi wa ngazi zote ikiwemo viongozi wa kimila na waandishi wa vyombo vya habari katika kutoa elimu ya uchaguzi.

Awali akizungumzia Utalii Dkt.Batilda amesema Wilaya ya Lushoto imebarikiwa kwa vivutio mbalimbali vya utalii na hivyo kuwa sehemu ya kichocheo cha maendeleo na kupongeza uongozi wa Wilaya ya Lushoto kufanikisha ujenzi wa kituo cha utalii ambacho kitasaidia upatikanaji wa taarifa muhimu za utalii.

Amewaelekeza viongozi wa Wilaya zingine za Mkoa wa Tanga kuwa na vituo vya utalii ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa kwa wageni wanaotembelea maeneo hayo.

Akizungumza kwa niaba ya Benki ya NMB Meneja Mahusiano wa Benki ya NMB na Serikali Peter Massawe amesema Benki hiyo ipo katika mchakato wa kusaidia sekta ya Utalii kwa kukaa na watenda kazi wa Sekta hiyo na kuona wanauhitaji wa mambo gani na kiasi gani ili kushirikiana kwa pamoja kukuza Sekta hii.

Tamasha la Usambara Tourism Festival limefanyika kwa mara ya kwanza Wilayani Lushoto na kuhusisha shughuli mbalimbali ikiwemo kutembelea vivutio vya utalii, maonesho ya biashara, shughuli za taasisi mbalimbali na kufanyika kwa mbio Usambara Marathoni kwa washiriki wa Km 21, Km 10 na KM 5 mbio zilizo ongozwa na mkuu wa Wilaya ya Lushoto Zephania Sumaye.


Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU SEPTEMBA 23,2024


Share:

Sunday, 22 September 2024

NAIBU WAZIRI PINDA AONYA MAAFISA ARDHI WANAOKIUKA MAADILI

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda akizungumza katika mkutano wa pamoja wa wananchi na watumishi wa Ardhi ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mkoa wa Kilimanjaro tarehe 19 sept 2024.

********************

Na MwandishI Wetu

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi mhe. Geophrey Pinda amesema kuwa hakuna afisa Ardhi atakayehamishwa eneo la kazi endapo atakiuka maadili ya utendaji wa taaluma yake.

Amesema hayo Septemba 19, 2024 katika mkutano wa pamoja wa wananchi na watumishi wa Ardhi ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mkoa wa Kilimanjaro.

"Nikimwambia Katibu Mkuu huyu utendaji kazi wake unaripotiwa kwamba hafai tutatuma vyombo vitakuja kukutafakari upya".

"Usikubali kwenye dawati lako kiwe chanzo cha mgogoro upelekwe kwa Mkuu wa Wilaya (DC) kwa Mkurugenzi, kwa Mbunge na jamno lile ulilolianzisha wewe linaenda mpaka kwa Rais! Haiwezekani kila mtu akitafakari". Amesema mhe Pinda

Aidha, ametoa maelekezo kwa ofisi za Wasajili wa Hati nchini kuharakakisha mchakato wa utoaji hatimiliki za Ardhi ili wananchi waweze kunufaika nazo ikiwa pamoja na kuaminiwa kupata mikopo katika taasisi za kifedha.

"Maelekezo ninayoyatoa kwenye dawati la usajili usilaze kazi toeni hati ziende kwa wananchi ". Amesema mhe. Pinda

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri wa Ardhi amewaonya Maafisa Ardhi wanaojiuhusisha l na ugawaji kiwanja kimoja mara mbili na kusisitiza kuwa Wizara yake itachukua hatua kali za kinidhamu dhidi ya mtumishi yeyote atakayekiuka maadili ya utumishi wa umma kwa taaluma yake.

"Kama litamhusisha Afisa wa kwetu kwenye jambo la kugawa kiwanja kimoja mara mbili, sasa hivi hatunamswalia Mtume tutachukua hatua kali" amesema Naibu Waziri Pinda.

Naibu Waziri Mhe. Pinda amehitimisha ziara yake mkoani Kilimanjaro jana ambapo mbali mambo mengine alisikiliza na kutatua changamoto za ardhi kwa wananchi wa mkoa huo pamoja na kufanya vikao kazi na watumishi wa Ardhi mkoani humo.
Sehemu ya watumishi wa sekta ya ardhi mkoa wa Kilimanjaro katika kikao chao na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe, Geophrey Pinda uliofanyika ukumbi wa mikutano wa Mkoa wa Kilimanjaro Sept 19, 2024.
Share:

MONGELLA ASISITIZA UMUHIMU KUZINGATIA KATIBA, UTUNZAJI SIRI


Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, ndugu John Mongella, amewasili Kigoma na kufanya kikao - kazi na viongozi waandamizi na watumishi wa CCM mkoani humo, Septemba 21, 2024.

Katika kikao-kazi hicho pamoja na mambo mengine, ndugu Mongella amesisitiza suala la kuendelea kujenga umoja na mshikamano, utunzaji wa siri za vikao, kusimamia Katiba ya CCM, kanuni, miongozo na taratibu mbalimbali za Chama na Jumuiya zake

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI SEPTEMBA 22,2024

Share:

Saturday, 21 September 2024

TANZANIA YA SITA DUNIANI, ONGEZEKO LA WATALII


Ukuaji wa Utalii Tanzania Chini ya Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan: Zama Mpya za Fursa.

Chini ya uongozi wa maono wa Rais Samia Suluhu Hassan, Tanzania inashuhudia ongezeko kubwa la watalii wa kimataifa, jambo ambalo limeongeza kwa kiasi kikubwa uchumi wa taifa. Kulingana na Barometer ya Utalii ya Dunia ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani (UNWTO), Tanzania imeibuka kama moja ya mataifa yanayoongoza kwa utalii, sambamba na nchi kama Qatar na Saudi Arabia. Taarifa hii inaonyesha mafanikio ya sera za Rais Samia za kufufua sekta ya utalii.

Katika muda mfupi tu, Rais Samia ameweka kipaumbele utalii kama injini kuu ya ukuaji wa uchumi. Serikali yake imeanzisha mipango ya kimkakati ya kuongeza mvuto wa kimataifa wa nchi, ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu, kampeni za uhamasishaji, na ushirikiano na mashirika ya kimataifa ya usafiri. Juhudi hizi zimesababisha ongezeko la watalii wanaovutiwa na mandhari nzuri ya Tanzania, wanyamapori wake wa aina mbalimbali, na urithi wake tajiri wa kitamaduni.


Kuongezeka kwa utalii hakuongezi tu mapato, bali pia kunazalisha ajira kwa Watanzania, hususan katika maeneo ya vijijini ambako fursa za kiuchumi mara nyingi ni chache. Hii inaendana na dhamira ya Rais Samia ya kuhakikisha maendeleo ya uchumi jumuishi, ambapo faida za utalii zinawafikia wananchi wote.

Zaidi ya hayo, msisitizo wa Rais Samia kwenye utalii endelevu unaiweka Tanzania mbele kama kivutio kinachowajibika. Kwa kukuza miradi rafiki kwa mazingira, serikali yake inalinda uzuri wa asili wa nchi wakati huo huo ikivutia watalii wanaojali mazingira. Mbinu hii haihifadhi tu mifumo ya kipekee ya mazingira ya Tanzania, bali pia inaimarisha ustahimilivu wa sekta ya utalii dhidi ya changamoto za siku zijazo.

Tanzania inavyozidi kupanda kwenye ramani ya utalii wa kimataifa, kwa msaada wa mashirika ya kimataifa kama UNWTO, uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan unathibitisha kuwa maono wazi na hatua za kimkakati zinaweza kusababisha mabadiliko makubwa ya kiuchumi. Akiwa kwenye usukani, Tanzania sio tu ni kivutio; ni taa ya matumaini na fursa kwa watu wake.

Share:

TANZANIA, SAUDIA ZAINGIA MAKUBALIANO KUDHIBITI UHALIFU


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni akipeana mkono na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Saudi Arabia, Mwanamfalme Abdul Aziz Bin Saudi Al- Saudi(kulia) baada ya kusaini hati ya makubaliano kati ya nchi hizo katika kushirikiana na udhibiti wa matukio ya uhalifu kupitia Jeshi la Polisi na majanga mbalimbali kupitia Jeshi la Zimamoto.Makubaliano hayo yamesainiwa nchini Saudi Arabia.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Ally Senga Gugu akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi wa Serikali ya Saudi Arabia, Mwanamfalme Abdul Aziz Bin Saudi Al- Saudi(kushoto) wakati wa kusaini hati ya makubaliano kati ya nchi hizo katika kushirikiana na udhibiti wa matukio ya uhalifu kupitia Jeshi la Polisi na majanga mbalimbali kupitia Jeshi la Zimamoto.Makubaliano hayo yamesainiwa nchini Saudi Arabia.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni akisaini hati ya makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Saudi Arabia katika kushirikiana na udhibiti wa matukio ya uhalifu kupitia Jeshi la Polisi na majanga mbalimbali kupitia Jeshi la Zimamoto.Makubaliano hayo yamesainiwa nchini Saudi Arabia.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Saudi Arabia, Mwanamfalme Abdul Aziz Bin Saudi Al- Saudi(kulia) alisema wakati wa kusaini hati ya makubaliano kati ya nchi hizo katika kushirikiana na udhibiti wa matukio ya uhalifu kupitia Jeshi la Polisi na majanga mbalimbali kupitia Jeshi la Zimamoto.Makubaliano hayo yamesainiwa nchini Saudi Arabia.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Na Mwandishi Wetu,Riyadh

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesaini hati ya makubaliano na Serikali ya Saudi Arabia makubaliano ambayo yanaenda kugusa sekta mbili muhimu za usalama ikiwemo udhibiti wa makosa mbalimbali ya uhalifu kwa kutumia utaalamu na teknolojia ya hali ya juu kwa Jeshi la Polisi sambamba na udhibiti wa majanga mbalimbali ikiwemo moto,ajali za bararani,maporomoko kupitia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

Hati hiyo ya makubaliano kwa upande wa Tanzania imesainiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni na upande wa Serikali ya Saudi Arabia imesainiwa na Mwanamfalme Abdul Aziz Bin Saudi Al- Saudi huku pande zote mbili zikionyesha nia ya kubadilishana uzoefu na vifaa mbalimbali ikiwemo vifaa vinavyotumia teknolojia katika udhibiti wa matukio ya uhalifu.

‘Nachukua fursa hii kumshukuru Waziri wa Mambo ya Ndani wa Saudi Arabia, Mwanamfalme Abdul Aziz Bin Saudi Al -Saudi kwa kunipa ushirikiano mkubwa katika ziara hii ambayo leo hii imepelekea kukamilisha uwekaji wa saini kwenye hati za makubaliano mbili, moja ikihusisha upande wa Jeshi la Polisi ambapo serikali mbili hizo zinaenda kushirikiana katika kupambana na uhalifu lakini hati ya pili inahusu mashirikiano kwenye Jeshi letu la Zimamoto na Uokoaji na tumezisaini leo hapa na zinakwenda kufungua milango ya kuweza kushirikiana kwa mapana zaidi katika maeneo hayo mawili,hati hii ambayo tumesaini leo itakwenda kufanya sasa nchi yetu kupitia Jeshi la Polisi kuweza kufaidika na fursa mbalimbali za mashirikiano ikiwemo katika kujenga uwezo wa askari wetu katika maeneo mbalimbali na kubadilishana uzoefu na teknolojia na nimefarijika kuona serikali ya Saudi Arabia imeweka msisitizo katika maeneo ambayo hata sisi tumeweka nguvu kuimarisha matumizi ya teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika kutoa huduma bora kwa wananchi..’ alisema Waziri Masauni

Waziri Masauni pia aligusia usalama wa kimtandao ambapo alisisitiza uwepo wa kipengele hicho katika hati ya makubaliano ili kuweza kudhibiti uhalifu wa mitandaoni ambao hivi sasa umeanza kushika kasi nchini.

‘Tumeona wenzetu wameweza kuimarika sana katika matumizi ya teknolojia kudhibiti uhalifu wa kimtandao hivyo ni Imani yangu kwamba kupitia mashirikiano ambayo tumesaini kwenye hati ya makubaliano tunakwenda kufanikisha dhamira njema ya Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kuimarisha jeshi letu la polisi katika eneo hilo nak ama mnakumbuka serikali ya awamu ya sita imewekeza fedha nyingi sana kiasi cha dola za kimarekani milioni mia moja kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya kisasa mbali ya vifaa vingine ambavyo tayari vishaingia mwaka huu ambavyo vinahitaji askari wetu wawe na uwezo na uweledi wa kuvitumia sambamba na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambao tayari walishaanza kupokea magari.’ Aliongeza Masauni

Akizungumza kwa upande wa Serikali ya Saudi Arabia,Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwanamfalme Abdul Aziz Bin Saudi Al- Saudi alisema wapo tayari kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kudhibiti matukio ya uhalifu huku akigusia uhalifu mbalimbali ulivyodhibitiwa nchini Saudi Arabia ambapo kila mwaka maelfu ya waumini wa dini ya kiislam na wageni kutoka mataifa mbalimbali hufika nchini humo.














Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger