Friday, 22 September 2023

OUT CHIMBUKO LA WAHITIMU BORA


Asilimia kubwa ya Wahitimu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), wana uwezo mkubwa wa kuchanganua na kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazokabili jamii yetu.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala, Mhe. George Simbachawene, alipokuwa akizungumza na wahitimu (Alumni) wa chuo hiki wakati wa mkusanyiko wa pili wa jumuiya ya wahitimu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, uliofanyika Septemba 21, 2023, katika kituo cha mkoa wa Dodoma, jijini Dodoma.

“Uzuri wa aliyesoma chuo Kikuu Huria cha Tanzania huwezi kumfananisha na mtu mwingine yeyote sababu huku anafundishwa kujitegemea kwa kutafuta mahitaji yote yampasayo kusoma, mazingira hayo ndio anayokutana nayo kazini. Hivyo wanatengenezwa wahitimu ambao ni viongozi imara.” Amesisitiza Mhe.Simbachawene.

Aidha, ameongeza kuwa, chuo hiki ndiyo chuo pekee ambacho unaweza kujiendeleza huku unaendelea na kazi na shughuli zako. Mhe. Simbachawene alisoma shahada ya sheria ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na kuhitimu kwa miaka Mitatu. Shahada hiyo ilimwezesha kufunzu mtihani wa uwakili na kuwa wakili wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Mhe. Simbachawene ametoa rai na ushauri kwa Watanzania wote kukitumia Chuo Kikuu Huria cha Tanzania katika kujiendeleza kielimu na huku wanaendelea na kazi zao bila kuziacha.

"Chuo Kikuu Huria cha Tanzania ni mkombozi kwa watu ambao wamekosa fursa ya kupata elimu ya juu kwa sababu ya changamoto mbalimbali ikiwemo kubanwa na majukumu ya kazi. Mimi nilikuwa nafanya shughuli zangu huku najiendeleza kielimu kupitia Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na nikahitimu vizuri." Ameongeza Mhe. Simbachawene.

Naye Mbunge wa Singida mjini na Rais mpya wa jumuiya ya Wahitimu wa chuo hiki Mhe. Mussa Sima, ametoa rai kwa wahitimu wenzie kushikamana vyema na chuo chao katika kuchangia maboresho mbalimbali kwani kimekuwa ni msaada mkubwa kwa Watanzania hasa wale waliopo kwenye ajira tayari hususani watumishi wa umma.

“Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kimetusaidia sana. Mtumishi aliyepo kazini badala ya kuacha kazi na kwenda kusoma, sasa ana nafasi ya kupata elimu ya chuo kikuu na bado anaendelea na majukumu ya kazi yake. Hii inamsaidia kuongeza ujuzi na kukua katika ajira kiutumishi.” Amesema Mhe. Sima.

Rais wa Jumiya ya Wahitimu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania anayemaliza muda wake Mhe. Almas Maige ambaye pia ni mbunge wa Tabora Kaskazini, amesema ni wajibu kwa kila muhitimu kushiriki katika chama cha wahitimu ili kushiriki katika kutoa mchango wao wa kimawazo, kiuchumi, kijamii, utafiti na huduma za kitaalam.

“Wahitimu tukishirikiana vyema na chuo tutaweza kuwa sehemu ya majawabu ya baadhi ya changamoto zinazokikabili chuo chetu na wanafunzi wanaohitimu katika vyuo ndiyo chachu na mbegu bora ya maendeleo ya chuo chochote duniani.” Amesema Mhe. Maige.

Kwa upande wake Makamu Mkuu kuu wa Chuo, Prof. Elifas Bisanda, amesema tangu chuo hiki kimeanza kuhitimisha mwaka 1999 hatujawahi kuwatumia wahitimu wetu, lakini ukweli ni kwamba Jumuiya ya wahitimu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania ni wadau muhimu sana kwa maendeleo ya chuo chetu katika Nyanja mbalimbali.

“Tunawahitaji wafanye kazi ya kutangaza huduma zetu kwa jamii, tunawahitaji kwa kupata taarifa za maendeleo ya elimu yao baada ya kuhitimu ili tuweze kuimarisha mitaala yetu lakini pia tunawahitaji wahitimu wetu katika maswala ya harambee ili kufanikisha maendeleo ya miradi mbalimbali ya chuo katika kutoa huduma zake.” Alimaliza kusema Prof. Bisanda.

Naye Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania anayeshughulikia Teknolojia za Kujifunzia na Huduma za Mikoa, Prof. Alex Makulilo, amevutiwa sana na shuhuda mbalimbali kutoka kwa Wahitimu kitu kinachoonesha kwamba chuo kinapiga hatua kubwa sana katika kuzalisha wataalamu wabobezi na wenye ujuzi wa kutosha wa kuwahudumia Watanzania. Akitoa neno la shukurani, amemshukuru mgeni rasmi na wahitimu wote kwa kupokea mwaliko na kuhudhuria kwenye shughuli hii bila kukosa licha ya kuwa na majukumu mengi ya ujenzi wa taifa na kimataifa.

"Tumeona katika kusanyiko hili kuna wahitimu wa chuo chetu kutoka mataifa mbalimbali wamehudhuria jambo linalothibitisha kwamba hiki ni chuo cha kimataifa. Wahitimu ni nguzo muhimu katika kuongeza udahili wa chuo na tunawaomba muendelee kufanya kazi kwa bidii huko mlipo na kutoa huduma bora kwa wananchi ili watu wavutiwe kujiunga na chuo chetu ndani na nje ya nchi." Amesema Prof. Makulilo.

Akifunga kusanyiko hilo, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Fedha, Mipango na utawala, Prof. George Oreku, amemhakikishia mgeni rasmi kuwa Menejimenti na wafanyakazi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania wataendelea kushirikiana na Alumni katika kuongeza ubunifu na kujituma katika kazi ili kuleta matokeo chanya.

Prof. Oreku, amevutiwa na wazo la kufunguwa akaunti maalumu kwa ajili ya wahitimu kuchangia maendeleo ya chuo na uhai wa jumuiya hiyo ya Wahitimu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania. Amesema jambo hili ni zuri sana na Viongozi wetu akiwemo mgeni rasmi, rais mpya wa jumuiya na rais aliyemaliza muda wake waliahidi kila mmoja kuchanga shilingi milioni moja kwa mwaka.

"Wazo la kuanzisha akaunti maalumu ya jumuiya ya Wahitimu wa chuo hiki limekuja wakati muafaka na ni ishara kwamba jumuiya hii ina dhamira ya dhati ya kutaka kushirikiana na Menejimenti ya chuo katika kutimiza malengo ya kuanzishwa kwake ikiwa ni kutoa elimu bora na nafuu kwa watu wote wakiwa mahali popote wakiendelea na kazi zao za ujenzi wa taifa. Tunasema asante sana kwenu wahitimu wote kwa moyo wenu na nia yenu ya dhati ya kushirikiana na chuo chetu." Alihitimisha Prof. Oreku.



Share:

FAHAMU FAIDA ZA KUNYWA MKOJO KIAFYA


Inawezekana ukafikiria kuwa ni jambo la ajabu kunywa mkojo wako kama 'kipimo cha kuishi' katika dharura kama hiyo lakini watu wengi katika maeneo mbali mbali duniani wanaamini kwamba kunywa mkojo wako kuna manufaa kwa maisha 'ya kiafya'.

Lakini Je, kuamka asubuhi na mapema na kunywa mkojo wako mwenyewe kunatibu magonjwa? Je, kupaka mkojo kwenye mwili na uso huifanya ngozi kuwa na laini na yenye afya kama inavyoaminiwa? Madaktari wanasema nini kuhusu hili?

Kelly Oakley, mwalimu wa yoga mwenye umri wa miaka 33 anayeishi Uingereza, hivi majuzi alifichua kwamba kunywa mkojo wake mwenyewe kumemsaidia kukabiliana na matatizo ya muda mrefu. Alisema kuwa dawa hii imempa nafuu ya tezi dume na maumivu ya muda mrefu.

Kelly alilieleza hivi karibuni shirika la habari la Associated Press kwamba amekuwa akikunywa mkojo wake kwa miaka miwili iliyopita.

"Nilisikia kwamba kunywa mkojo kunaboresha mfumo wako wa kinga, husaidia kudumisha afya njema, na ni nzuri kwa ngozi yako," Kelly alisema. Kwa hivyo nilianza kujaribu jaribio langu la kunywa mkojo.


Si kunywa tu mkojo wake kila siku, lakini pia huupaka kwenye ngozi yake. Alisema kuwa dawa hii iliifanya ngozi yake kung'aa zaidi.

Watu wengi huita dawa hii 'tiba ya mkojo'. Dawa hii pia inajulikana kama 'Urophagia'.

Lakufurahisha ni kwamba, Kelly sio mtu pekee anayedai kufaidika kwa kunywa mkojo wake mwenyewe. Hivi karibuni kumekuwa na mifano mingi kama hiyo.

"Kunywa mkojo wangu mwenyewe kumenisaidia kupunguza nusu ya uzito wangu," Sampson, 46, wa Albert, Canada, aliliambia jarida la Sun.

Hapo awali alisema kuwa uzito wake ulipungua hadi kilo 120, jambo ambalo lilikuwa likimsumbua, lakini sasa tangu ameanza kunywa mkojo wake mwenyewe, uzito wake umerudi kawaida.

“Rafiki yangu alinitumia video akielezea tiba ya mkojo. Baada ya kutazama video hiyo, nilikwenda bafuni, nikajaza kikombe na mkojo wangu na kunywa. Ndani ya siku chache, nilianza kuona tofauti ndani yangu.”, alieleza.

Share:

Thursday, 21 September 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA SEPTEMBA 22,2023























Share:

CHANJO YA UKIMWI KUFANYIWA MAJARIBIO AFRIKA KUSINI NA MAREKANI


Afrika Kusini na Marekani zitaanza majaribio ya chanjo mpya ya kuzuia VVU na zimeanza kuwaandikisha washiriki kushiriki katika majaribio ya kimatibabu.

Kulingana na shirika la utafiti la serikali la Marekani la Taasisi za Kitaifa za Afya (NIH), chanjo hiyo, iitwayo VIR-1388, imeundwa kusaidia seli za T za mwili, zinazosaidia mfumo wa kinga kupambana na vijidudu na kukinga dhidi ya magonjwa.

Chanjo hiyo inakusudiwa kuelekeza mfumo wa kinga ya mwili kuzalisha T-seli "zinazoweza kutambua VVU na kuashiria mwitikio wa kinga ili kuzuia virusi kuanzisha maambukizi ya muda mrefu".

Jaribio la chanjo hiyo linafadhiliwa na NIH, Wakfu wa Bill na Melinda Gates na kampuni ya Marekani ya Vir Biotechnology.

Utafiti huo utaandikisha washiriki 95 wasio na VVU katika maeneo manne nchini Afrika Kusini na maeneo sita nchini Marekani.

Matokeo ya awali ya jaribio la chanjo yatatangazwa mwishoni mwa 2024, lakini baadhi ya washiriki wataendelea na majaribio kwa miaka mitatu.

Mnamo mwaka wa 2020, NIH ilisitisha majaribio ya chanjo nyingine ya VVU nchini Afrika Kusini baada ya ukaguzi kugundua kuwa chanjo hiyo haikuwa na ufanisi katika kuzuia maambukizi ya VVU.

CHANZO- BBC SWAHILI
Share:

MWANAMKE ATUPWA JELA BAADA YA KUPOST VIDEO TIKTOK AKILA KITIMOTO

Mahakama ya Indonesia imemfunga jela mwanamke mmoja miaka miwili baada ya kupatikana na hatia ya kukiuka sheria za kukufuru za nchi hiyo katika video ya chakula ya TikTok aliyochapisha mwezi Machi.

Video hiyo ilionyesha Lina Lutfiawati akisoma sala ya Waislamu kabla ya kula ngozi ya nyama ya nguruwe iliyokauka na kukusanya mamilioni ya watu waliotazama .

Nyama ya nguruwe inachukuliwa kuwa 'haram', au hairuhusiwi, chini ya sheria za Kiislamu.

Siku ya Jumanne, mahakama katika mji wa Palembang nchini Indonesia, sehemu ya kusini ya kisiwa cha Sumatra, ilimpata kijana huyo mwenye umri wa miaka 33 kwa hatia ya "Kueneza habari zilizokusudiwa kuchochea chuki au uadui wa mtu binafsi/kikundi kwa misingi ya dini" na kumuamuru kulipa faini ya rupiah milioni 250 ($16,249.59).

Indonesia ni taifa kubwa zaidi duniani lenye Waislamu wengi.

Mahakama ilisema Lutfiawati, ambaye pia anafahamika kwa jina Lina Mukherjee, aliyetambulika kama Muislamu.

Lutfiawati aliomba radhi kwa umma kwa video hiyo na kueleza kushangazwa na hukumu hiyo.

"Ninajua kuwa nina makosa, lakini sikutarajia adhabu hii," Lutfiawati alisema kwenye kituo cha habari cha MetroTV.

Kesi hiyo ni ya hivi punde zaidi kati ya kesi kadhaa za kashfa kote nchini, haswa dhidi ya zile zinazodaiwa kuutusi Uislamu, ambazo wachambuzi wamesema zinadhoofisha sifa ya Indonesia ya kuwa na msimamo wa wastani.

Mnamo Agosti, mkuu wa shule ya bweni ya Kiislamu ambayo iliruhusu wanaume na wanawake kusali pamoja na wanawake kuwa wahubiri alishtakiwa kwa kukufuru na matamshi ya chuki.

CHANZO - BBC SWAHILI
Share:

KIMBUNGA CHAUA WATU 10 CHINA


Watu kumi wamefariki dunia wakati kimbunga kikali kikipiga katika miji miwili katika jimbo la Jiangsu mashariki mwa China.

Hilo ni tukio la hivi karibuni la hali mbaya ya hewa kuikumba nchi hiyo, ambayo katika miezi michache iliyopita imekuwa ikikumbwa na mafuriko makubwa pamoja na mawimbi ya joto kali.

Watu wengine wannewamejeruhiwa vibaya kutokana na kimbunga kikali kilichopiga mji wa Suqian katika jimbo la Jiangsu siku ya Jumanne, kwa mujibu wa kituo cha televisheni cha serikali CCTV. Mkoa huo uko katika pwani ya mashariki ya China.

Zaidi ya watu 400 wamehamishwa na zaidi ya nyumba 130 zimeharibiwa katika mji huo, CCTV iliripoti.

Kwa upande mwingine, kimbunga chenye nguvu zaidi kilisababisha vifo vya watu watano na wanne wakiwa na majeraha madogo Jumanne usiku huko Yancheng - ambayo iko kusini mashariki mwa mji wa Suqian na kaskazini mwa mji mkubwa wa China, Shanghai - CCTV imesema, na kuongeza kuwa watu 129 wamehamishwa.

Tornadoes sio kawaida katikati ya Septemba huko Jiangsu, lakini kimbunga adimu kimetokea kutokana na joto la juu la hivi karibuni ambalo limeleta hali ya hewa kali, vyombo vya habari vya serikali Beijing Youth Daily iliripoti, ikinukuu wataalam wa hali ya hewa.

Share:

RAIS SAMIA AIPONGEZA OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI KUVUTIA WAWEKEZAJI NA KUWEKA MAZINGIRA BORA YA UWEKEZAJI



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameipongeza Ofisi ya Rais - Mipango na Uwekezaji na Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) kuweka mazingira bora ya Uwekezaji pamoja na kuvutia wawekezaji.


Rais Samia ametoa pongezi hizo, Septemba 20, 2023 kwenye hafla ya uzinduzi wa Kiwanda cha Uzalishaji Vioo vya Ujenzi cha Saphire Float Glass kilichopo wilayani Mkuranga, mkoani Pwani.

“Nawapongeza Ofisi ya Rais - Mipango na Uwekezaji, Kituo cha Uwekezaji (TIC) kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji wanaokuja nchini kuwekeza, hali hii ya uwekezaji hapa nchini inachochea ukuaji wa uchumi wetu pia inachagiza ajira nyingi kwa vijana wetu,” amesema Rais Samia.


Aidha, Rais Samia ameeleza kuwa hadi kufika Septemba, 2023 Kituo hicho cha Uwekezaji (TIC) kimesajili jumla ya miradi 417 katika Sekta ya Viwanda kati ya Januari 21 na Septemba 15, 2023. Miradi hiyo ina jumla ya thamani (USD) Bilioni 5 na Milioni 39 sawa na wastani wa Shilingi Trilioni 12 za kitanzania, ikiwa kila mradi umegharimu wastani wa (USD) Milioni 12.


Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo amesema Kiwanda hicho kitaleta mapato mapya ya Kodi takribani Shilingi Bilioni 42.79 kila mwaka sanjari na kuleta ajira nyingi kwa Watanzania wengi kutoka sasa kwenye ujenzi wake ambapo zaidi ya watu 700 wamepata ajira kwenye ujenzi wa mradi huo.


Naye, Waziri wa Viwanda na Biashara nchini, Dkt. Ashantu Kijaji amesema kupitia uongozi mahiri wa Rais wa awamu ya sita, Dkt. Samia, Wawekezaji wa Kiwanda hicho walikubali kuwekeza nchini.


Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni inayojenga mradi huo, Frank Yang ameishuru Serikali ya Tanzania na watu wa Tanzania kwa ukarimu wao wakati wote wa ujenzi wa Kiwanda hicho cha vioo katika eneo hilo la Mkuranga, Pwani.


Mradi huo wa Kiwanda cha Vioo ni mradi mkubwa tangu kusajiliwa kwa miradi hiyo nchini ukiwa umegharimu fedha za Marekani (USD) Milioni 311 sawa na wastani wa Shilingi Bilioni 745 na zaidi ya Milioni 700, Kiwanda hicho ni kikubwa zaidi ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, kikiwa nafasi ya nne Afrika.


Kiwanda hicho cha Vioo kinatarajiwa kuzalisha Tani 700 za Vioo kwa siku katika uzalishaji kamili, awamu ya kwanza. Asilimia 75% ya bidhaa zitauzwa nje ya nchi wakati asilimia 25% za bidhaa hiyo zitauzwa nchini. Pia Kiwanda hicho kinatarajiwa kuzalisha ajira takribani 1650 kwa vijana wa kitanzania.
Share:

POLISI SHINYANGA WANASA NOTI BANDIA, SILAHA, WAGANGA WA KIENYEJI, PIKIPIKI ZILIZOBEBA MIZIGO HATARISHI BARABARANI




Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Jeshi la Polisi linawashikilia watuhumiwa 12 na wengine limewafikisha mahakamani kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo kukamatwa noti bandia 15 zenye thamani ya Tsh, 150,000/=, silaha, wizi na kufanya shughuli za uganga wa kienyeji bila kibali wakiwa na vifaa vya ramli chonganishi.


Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Alhamisi Septemba 21,2023 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi amesema watuhumiwa hao wamekatwa kupitia misako na doria iliyofanywa katika maeneo mbalimbali katika kipindi cha mwezi Agosti mpaka Septemba, 2023 ikiwa ni katika kuendelea kutimiza wajibu wake wa kulinda maisha ya watu na mali zao.


“Katika muendelezo wa misako hiyo tuliweza kukamata noti bandia 15 zenye thamani ya Tsh, 150,000/=, dawa za kulevya aina ya Bangi yenye uzito wa Kg. 40 na kete 18, Heroine kete 01, Pikipiki 16 zilizokuwa zikitumika katika kutendea makosa mbalimbali, mashine 01 ya kufua umeme, mashine 01 ya kuchomelea vyuma, lita 120 za mafuta ya kuendeshea mitambo, pamoja na vipande 880 vya nondo”,ameeleza Kamanda Magomi.
“Lakini pia katika misako hiyo tulifanikiwa kuwakamata waganga 03 wa kienyeji kwa kufanya shughuli za uganga bila kibali na pia wakiwa na vifaa mbalimbali vya ramli chonganishi, Sub-woofer 01, TV 01, viti 20, pamoja na lita 76 za pombe ya moshi”,ameongeza.

Amefafanua kuwa pia wamefanikiwa kukamata Silaha aina ya Shortgun BELGIUM yenye namba 18342 ambayo ilikuwa inamilikiwa isivyo halali, Pia tumekamata silaha nyingine aina ya Shortgun Pump Action yenye namba za usajili TZ CAR 69657A ambayo ilitumika katika tukio la unyang'anyi na kuitelekeza baada ya kugundua kuwa wanafuatiliwa na askari.


“Jumla ya watuhumiwa 12 wanashikiliwa kuhusiana na makosa hayo na wengine wameshafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria huku wengine wakipewa dhamana huku wakisubiri Upelelezi kukamilika”,ameeleza.


Kwa upande wa makosa ya usalama barabarani, amesema Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga kwa kipindi cha mwezi mmoja uliopita lilifanikiwa kukamata jumla ya makosa mbalimbali 3636 ya usalama barabarani ambapo jumla ya magari yaliyokamatwa yalikuwa 2850. magari mabovu ni 1053, kuzidisha abiria ni 429, kutokuwa na Bima ni 163, kuendesha magari kwa njia hatarishi ni 139, kutofunga mikanda ya usalama ni 31, kuendesha magari bila leseni ni 05 na kuendesha magari kwa mwendokasi ni 509, makosa mengineyo 521.
“Pia jumla ya Pikipiki na Bajaji 786 zilikamatwa kwa makosa mbalimbali ambapo Pikipiki mbovu zilikuwa ni 59, kutovaa kofia ngumu ni 182, kuzidisha abiria ni 76, kuendesha Pikipiki bila Bima ni 163, kuendesha pikipiki kwa njia hatarishi ni 33, kulewa na kuendesha pikipiki ni 01, kuendeha pikipiki bila leseni ni 203 na kutokuwa na leseni ya usafirishaji ni 69”,amesema.


Akielezea mafanikio yaliyofikiwa na Jeshi la Polisi katika kipindi cha Mwezi Agosti hadi Septemba 2023, Kamanda Magomi amesema mtuhumiwa 01 wa kesi ya kubaka alihukumiwa kifungo cha maisha jela na watuhumiwa wengine 04 walihukumiwa kifungo cha miaka 30 Jela kila mmoja kwa kosa hilo hilo la kubaka ambapo walitenda makosa hayo katika nyakati tofauti.


“Katika kipindi hicho, kesi za wizi zilikuwa 03 na zilihukumiwa kulipa faini kati ya Tsh. 100,000/= hadi 500,000/=, kesi 01 ya kutelekeza familia mshtakiwa alifungwa miezi 06 jela, kesi 01 ya kutorosha mwanafunzi ilihukumiwa kuchapwa viboko 05, kutupa mtoto kesi 01 ilihukumiwa miaka 02 kutumikia jamii, kupatikana na Bangi kesi 01 ilihukumiwa kutumikia jamii mwa kipindi cha mwezi 01 na pia kupatikana na madawa ya kulevya kesi 02 zilihukumiwa kifungo cha miaka 02 jela”,amesema.

Kamanda huyo wa Polisi amesema Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga linaendelea kuwashukuru raia wema wote wanaotoa taarifa za uhalifu na wahalifu zinazoleta mafanikio haya na linawaasa wananchi wote kuendelea kutii sheria za nchi kuuweka mkoa wa Shinyanga kwenye ushwari.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamis Septemba 21,2023.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamis Septemba 21,2023.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akionesha silaha na vitu mbalimbali vilivyokamatwa na Polisi Shinyanga
Vitu mbalimbali vilivyokamatwa na Polisi Shinyanga
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi vitu mbalimbali vilivyokamatwa
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akionesha bangi iliyokamatwa na Polisi Shinyanga
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akionesha pikipiki zilizokamatwa kwa kubeba mizigo hatarishi barabarani
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akionesha vitu mbalimbali vilivyokamatwa
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akionesha viti vilivyokamatwa
Nondo zilizokamatwa na Polisi Shinyanga
Vitu mbalimbali vilivyokamatwa na Polisi Shinyanga
Pikipiki zilizokamatwa na Polisi Shinyanga

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Share:

Wednesday, 20 September 2023

MERIDIANBET YAWAFIKIA WATU WASIOONA NA KUWAPA MSAADA!!


Maisha ya binadamu yamejaa mambo mengi sana, kuna mengi ya kidunia unaweza kupitia ukajiona hauna thamani tena kwa jamii, lakini uwepo wa Meridianbet umekuwa ni sehemu ya kurejesha matumaini kwa watu wenye mahitaji ikiwemo watu wasioona.

Na kwa kuliona hili safari ya kutoka makao makuu ya Meridianbet wakali wa odds kubwa, michezo ya sloti na kasino ya mtandaoni walitembelea Jumuiya ya watu wasioona Tanzania, maeneo ya Kinondoni kutimiza mahitaji yao kuelekea “Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Fimbo Nyeupe” itakayofanyika Mkoani Njombe Tarehe 15 Oktoba.

Walijikuta na furaha kubwa iliyoambatana na machozi kwa kutokuamini kama ni kweli Meridianbet wameitikia wito wao na kuchangia pesa pamoja na mahitaji yao mengine.

Jamila Mohammed Mweka Hazina wa chama hicho alisema kuwa wana Zaidi ya wananchama 10,000/= mkoa mzima, na mahitaji yao kwa kiasi kikubwa ni fimbo.

“Tunahitaji fimbo kwaajili ya kutembelea, haya ni kama macho yetu sisi, hivyo mkituletea fimbo mtakuwa mmetusaidia kuona, Meridianbet tunawashukuru kwa hiki mlichotupatia sisi ni kikubwa kwetu na wadau wengine waige mfano huu”

Upande wa Meridianbet Amani Maeda alisema kwamba tangu kampuni hiyo imeanza kufanya kazi hapa nchini, imekuwa ikijihusisha na jamii kwa kutoa misaada mbalimbali haswa kwa watu wenye mahitaji maalum.

“Tumetoa kidogo kwa jamii hususani ndugu zetu wasioona kuelekea siku ya kimataifa ya Fimbo nyeupe, lengo ni kuwawezesha kufika Njombe kuhudhuria tukio hilo lenye lengo la kuwaunganisha watu wasioona”-Amani Maeda

NB: Meridianbet wanakupa nafasi ya kuendelea kubashiri na kushinda kila unapojisajili, ili kubeti na kucheza kasino ya mtandaoni unapaswa kujisajili na kisha unapewa bonasi ya ukaribisho. Jisajili hapa.


Share:

WAZIRI NDALICHAKO AZITAKA TAASISI ZA UMMA KUWA NA WATAALAMU WA LUGHA YA ALAMA


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na Waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Septemba 20,2023 jijini Dodoma kuelekea Siku ya maandalizi ya Maadhimisho ya Wiki ya Viziwi yanatarajia kufanyika Septemba 25 hadi 30 mwaka huo jijini Mbeya.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA), Adam Shaibu (kulia) akieleza jambo kwa Waandishi wa Habari kuhusu Maadhimisho ya Wiki ya Viziwi. Katikati ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako na Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Watu wenye Ulemavu, Rasheed Maftah.

Na-Alex Sonna - Dodoma.

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amezitaka Taasisi za Umma kuhakikisha zinakuwa na wataalam wa lugha ya alama ili inapohitajika kutoa huduma kwa wateja wenye Uziwi pasiwe na kikwazo katika kuwasiliana.

Wito huo umetolewa leo Septemba 20, 2023 jijini Dodoma na Waziri Ndalichako wakati akizungumza na waandishi wa Habari kuelekea Siku ya maandalizi ya Maadhimisho ya Wiki ya Viziwi yanatarajia kufanyika Septemba 25 hadi 30 mwaka huo jijini Mbeya.

"Malengo ya Serikali ni kuhakikisha Kila taasisi inakuwa na wataalam wa Lugha ya alama hivyo Miongozo imeandaliwa ni vyema kila taasisi ihakikishe watu wote Wenye Ulemavu wanajumuishwa katika Fursa zote za maendeleo,"amesema Prof.Ndalichako

Aidha Prof.Ndalichako amesema maadhimisho hayo yametokana na mahitaji na changamoto zilizokuwa zinawakabili Viziwi Duniani ndio maana ikatengewa wiki yake ambapo hufanyika Kila Mwaka wiki ya mwisho ya Mwezi Septemba.

"Serikali ya Tanzania inaungana na Viziwi wote Duniani katika maadhimisho ya Wiki hii na tunahimiza matumizi ya Lugha ya alama na ndio maana kauli Mbiu ya wiki hiyo Inasema "Dunia ambayo popote walipo Viziwi wanaweza kutumia Lugha ya alama"amesema Prof.Ndalichako

Hata hivyo amewataka Wananchi kuendelea kuwathamini watu Wenye Ulemavu kwani wameshathibitisha kuwa Ulemavu wao sio kikwazo katika shughuli za maendeleo.

"Nitoe rai kwa wananchi wenzangu wa Tanzania kuwathamini na kuziunga mkono kazi zinazofanywa na Watu Wenye Ulemavu kwani wameshathibitisha kuwa sio kikwazo katika shughuli za maendeleo,"



Aidha amefafanua lengo la kuanzishwa kwa wiki ya Viziwi Duniani ni kutoa fursa Watu wa Jamii ya Viziwi kushiriki kwenye shughuli mbalimbali za Maendeleo kwa kushirikiana na jamii zinazowazunguka bila kuwepo vikwazo vyovyote ikiwemo vikwazo vya mawasiliano yao.

''Serikali inayoongowa na Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuchukua hatua mbalimbali kwa ajili ya ustawi wa Watu wenye Ulemavu nchini ikiwa ni pamoja na Watu wa Jamii ya Viziwi ambapo elimu imeendelea kutolewa kwa umma na wadau mbalimbali kuhusu changamoto zinazo kabili kundi hilo ikiwemo kuhamasisha utamaduni wa kuwasiliana kwa kutumia lugha ya alama.''amesema

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA), Adam Shaibu ameishukuru serikali kwa kutoa ushirikiano na kuwamini Watu wenye Ulemavu ikiwemo kuwapatia fursa za kiuchumi, kijamii, kiuongozi na ajira.

Kauli mbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu 2023 ni “Dunia ambayo Popote Walipo Viziwi Wanaweza Kutumia Lugha ya Alama.”

Kauli mbiu hii inalenga kila taasisi inayotoa huduma kwa jamii inakuwa na mkalimani wa lugha ya alama sambamba na kuwajengea uwezo watumishi wake kuwa na uelewa wa lugha ya Alama.
Share:

GGML YATOA MILIONI 150 KUDHAMINI MAONESHO YA 6 YA TEKNOLOJIA YA MADINI GEITA


Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Terry Strong (kulia) akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa kitengo cha huduma za dharura cha kampuni hiyo pindi waliposhiriki maonesho hayo mwaka jana. Kushoto ni Makamu Rais wa AngloGold Ashanti- GGML anayesimamia miradi endelevu kwa upande wa Ghana na Tanzania, Simon Shayo

Na Mwandishi Wetu 

KATIKA kuendelea kudumisha dhamira ya ubunifu wa kiteknolojia, Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetoa kiasi cha Sh milioni 150 kudhamini Maonyesho ya Sita ya Teknolojia ya Madini yanayofayika mkoani Geita.

Maonyesho hayo ambayo hufanyika kila mwaka, mwaka huu yanatarajiwa kuzinduliwa tarehe 23 na kuhitimishwa tarehe 30 Septemba.

Maonyesho hayo yanafanyika kwa ushirikiano kati ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), katika viwanja vya Bombambili vilivyopo eneo la Mamlaka ya Maeneo ya Usindikaji Nje (EPZA) mkoani humo.

Akizungumzia ushiriki wa GGML katika maonesho hayo mjini Geita jana, Meneja Mwandamizi wa kampuni hiyo anayesimamia mahusiano jamii, Gilbert Mworia alisema maonesho hayo yamekuwa na mvuto wa kipekee tangu yalipoasisiwa kutokana na ufadhili wa GGML kupitia mfuko wa uwajibikaji kwa jamii (CSR) ambao uliwezesha ujenzi wa eneo hilo la EPZA pamoja na eneo la uwanja huo wa maonesho.

"Mbali na maonyesho, tuliwekeza Sh 800 milioni katika ujenzi wa jengo la utawala la EPZA. Tunafurahi kuona mpango wetu wa EPZA mkoani Geita unastawi na kutimiza malengo ya jamii ya wana-Geita kikamilifu," alisema na kuongeza;

"Msaada wetu unavuka usaidizi wa kifedha ambao tumeendelea kuutoa kila mwaka, kwa sababu tulitoa msaada wa maandalizi ya maonesho hayo kama vile mahema, jenereta la dharura na mafuta yanakayotumika kwa wakati wote wa maonesho,” alisema Mworia.

Alisema katika kipindi cha miaka sita ya ushirikiano huo na wadau wa maonesho hayo, GGML imeendelea kuelimisha jamii kuhusu teknolojia inayotumika katika vifaa vya uchimbaji madini hali inayoendelea kukuza uhusiano imara kati yake, kampuni za ndani na wachimbaji madini.

Aidha, alisema ili kutimiza malengo ya muda mrefu ya ukuaji wa uchumi endelevu, GGML inaunga mkono Dira ya 2025 ya serikali. Mpango huu unalenga kuiwezesha sekta ya uchimbaji madini kukua na kufikia kiwango cha asilimia 10 kwenye Pato la Taifa la Tanzania.

Ufunguzi rasmi wa Maonesho hayo ya 6 ya Madini na Teknolojia mkoani Geita utafanywa na Dk. Dotto Biteko, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, tarehe 23 Septemba.

Tarehe 30 Septemba mwaka huu, Rais Samia Suluhu Hassan anayetarajiwa kufunga maonesho hayo yenye kauli mbiu; Matumizi ya teknolojia sahihi katika kuinua wachimbaji wadogo kiuchumi na kuhifadhi mazingira.




Share:

NOVATUS DISMAS AFUATA NYAYO ZA SUNDAY MANARA NA SAMATTA



Walianza watanzania wachache sana kutamba kwenye soka la ushindani tena nje ya ardhi ya Tanzania. Kuna Sunday Manara na Je ni nani asiyefahamu mapambano ya mtoto wa uswahilini mitaa ya Mbagala Mbwana Ali Samatta, hadi kufikia Uingereza na kuifunga Liverpool ya moto chini ya Jurgen Klopp tena kwenye UCL na baadaye kukipiga Ligi Bora duniani EPL.

Harakati hizo zinaendelezwa na Chuga Boy aliyekataa kuwa Jobless mitaa ya Ngarenaro, Unga Limited, Majengo, na Matejoo.

Huyo sio mwingine ni Novatus Dismas Miroshi ambaye anakipiga kwenye ardhi ya Ukraine pale FC Shaktar Donetsk ambaye alimeongeza rekodi yake na baada ya kucheza na FC Porto klabu ya utotoni ya staa wa dunia Cristiano Ronaldo. Pata odds kubwa mechi za UCL zinazoendelea tena leo, ili kufurahia bonasi kibao jisajili na Meridianbet kwa kugusa hapa.

Historia imeandikwa tena kwa kijana mwingine wa kitanzania Novatus Dismas ambaye amefuata nyayo za watangulizi wake kama vile Sunday Manara, Mbwana Samatta kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya FC Porto na mchezo kumalizika kwa timu yake kupoteza mabao 1-3. Bashiri mechi mbalimbali kupitia Meridiabet odds kubwa.

Historia Fupi ya Novatus

Kutoka mitaa Fulani ya uswahilini mtoto wa mtaa huko Arusha Novatus uzao wake ulikuwa huko, akalazimika kuzikataa harakati za mtaa na kuchagua kupambani ugali wake kwenye njia ya soka.

Novatus Miroshi Dismas alisafiri mpaka Dar Es Salaam pale kwenye viunga vya Bakhresa tajiri wa maokoto kama ilivyo kwa Meridianbet matajiri wa odds kubwa na kasino ya mtandaoni, machaguo kibao na michezo mingi ya sloti.

Alicheza kwa muda wa mwaka akatolewa kwa mkopo kwenda Biashara Utd ya mkoani Mara kabla ya kurudi tena Azam FC, hapo ndipo nyota ya kijana huyu wa kitanzania ilianza kung’aa kwa kuonekana na vilabu vingi vya Ulaya kama vile Maccabi Tel Aviv, Beitar Tel Aviv kisha Zulte Waregem, na sasa FC Shaktar Donetsk.

Novatus Dismas ana msaada mkubwa kwenye timu ya taifa ambapo ni mchezaji tegemezi kwa sasa anayeweza kucheza nafasi tofauti ndani ya uwanja, kama vile beki wa pembeni, beki wa tatu, winga, na kiungo wa kati.

NB: Ili kuweza kubashiri mechi hizi zenye odds kubwa na machaguo rahisi kabisa kutiki jamvi lako, unapswa kujisajili Meridianbet kwa kugusa hapa.


Share:

BIL.400/- KUKARABATI BARABARA MTWARA - MINGOYO - MASASI

 

 

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, amesema shilingi bilioni 400 zitatumika katika ukarabati wa Barabara ya Mtwara-Mingoyo-Masasi kupitia majadiliano yaliyofanywa kati ya Serikali na Benki ya Dunia (WB).


Pia, amepongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia kusainiwa kwa mkataba wa ujenzi wa barabara inayounganisha vipande kutoka Masasi- Nachingwea - Liwale (Km 175).

Waziri Bashungwa aliyasema hayo leo katika mkutano wa hadhara wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na wananchi uliofanyika katika Uwanja wa Mitwero mkoani Lindi wakati akitoa salamu na kueleza utekelezaji wa miradi ya kimaendeleo mkoani humo.

Waziri Bashungwa alisema pamoja na Serikali kuendelea kutafuta fedha za ujenzi wa barabara hiyo lakini Rais Dk. Samia Suluhu Hassan tayari ameridhia kusainiwa kwa barabara hiyo.

"Rais Samia Suluhu Hassan umetuelekeza Wizara ya Ujenzi hata kabla fedha wakati tunaendelea kuzitafuta, umeelekeza kwa namna ambavyo unawajali wananchi wa mikoa hii miwili kwamba tusaini huku ukiendelea kupambana kutafuta fedha ya barabara hii ambayo italeta mageuzi makubwa ya kiuchumi kwa Mkoa wa Lindi na Mtwara", alisema Bashungwa.

Ameongeza kuwa Mhe. Rais ameelekeza mkandarasi wa barabara ya Nachingwea - Ruangwa - Nanganga yenye urefu wa kilometa 53.2 ambayo tayari ujenzi wake umefikia asilimia 41 aendelee na ujenzi wa barabara hiyo hadi Nachingwea ambapo itakuwa na jumla ya urefu wa kilometa 106.

Kuhusu Barabara ya Nangurukuru - Liwale (Km230) Waziri Bashungwa alisema tayari Serikali imetenga fedha za kuanza ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 72 kuanzia Liwale hadi Choya.

"Mhe. Rais kama hiyo haitoshi kipo kipande cha Barabara ya Ruangwa- Namichiga kilometa 20 ambacho kwa sasa kipo kwenye mipango ya kuwekwa lami kupitia mradi wa RISE, sasa ukiona mahaba na Watanzania wakijitokeza kwa wingi unakopita ni kwamba wewe ni Rais wa vitendo na wanaona kazi kubwa ya Serikali unayoiongoza", alisema Bashungwa.




Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger