Sunday, 14 May 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI MEI 14,2023

 






Share:

Saturday, 13 May 2023

MWANACHUO AJITEKA BAA AKINYWA BIA KISHA KUTUMA SMS ITUMWE PESA AACHWE


Mwanachuo aliyejiteka

Kennedy Nyangige mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika chuo cha udaktari Bugando anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Mwanza kwa tuhuma za kujiteka na kisha kutuma meseji kwa wazazi, ndugu na viongozi wake wa chuo akidai ametekwa na inatakiwa milioni 3.5 ili aachiwe.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa amesema baada ya kupokea taarifa hizo kutoka kwa daktari wa hospitali ya rufaa ya kanda Bugando aitwaye Matiko Sirari jeshi la polisi lilianza kufanya uchunguzi wa tukio hilo na kubaini kwamba kijana huyo alikuwa anadanganya ametekwa na wakati alijiteka mwenyewe ili pate hiyo hela.

Aidha Kamanda Mutafungwa amesema wakati anatuma ujumbe huo alikuwa kwenye nyumba ya kulala wageni huku anakunywa bia ndipo askari polisi walipomtia mbaroni na kwamba atafikishwa mahakamani pindi upelelezi utakapokamilika

"Sasa baada ya tukio hilo na maelezo hayo huyo mtuhumiwa alikamatwa na kuletwa katika kituo cha polisi kwa mahojiano na tumeweza kuokoa fedha alizokuwa akizitaka kwa njia ya kitapeli kwamba ametekwa kumbe amejiteka mwenyewe, Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza linatoa wito kwa vijana ambao familia zao zimewaamini na kuwapeleka kwenye vyuo vya gharama kubwa kuacha janjajanja kuacha utapeli kwa kujipatia kipati kwa njia isiyo halali," amesema Kamanda Mutafungwa.

CHANZO -EATV
Share:

BIBI AUAWA KWA KUZIBWA PUA TUHUMA ZA KUROGA NA KUGEUZA MSUKULE



Bundala Rajabu mwenye umri wa miaka 32 mkazi wa Kijiji cha Ndami wilayani Kwimba mkoani Mwanza anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani humo kwa tuhuma za kumuua kwa kumziba pua na kumkaba kooni bibi wa miaka 87 anayeitwa Mariam Nyanda kwa imani za kishirikina.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa amesema tukio hilo limetokea tarehe 11 ya mwezi huu ambapo inadaiwa Bundala Rajabu alikuwa anatoka kwenye shughuli zake ndipo akakutana na mtoto wake aliyefariki mwaka jana na kuzikwa katika Kijiji hicho ambapo mtoto huyo alimwambia kuwa anaishi kwa bibi Bundala

Aidha kamanda Mutafungwa amesema wakati anaongozana na mwanae huyo kwnda kwa bibi Bundala ghafla mtoto huyo alipotea katika mazingira ya kutatanisha ndipo baba huyo alipatwa na hasira na Kwenda kwa bibi huyo kumhoji wakati anamhoji ndipo akamkaba kooni na kumziba pua hali liyopelekea bibi huyokupoteza Maisha

‘Huyu mtuhumiwa baada ya kufanya tukio hilo la kikatili kabisa akiwa na Imani kwamba mtoto wake alikuwa amechukuliwa msukule na yule bibi aliondoka na kuripoti kwa jirani yake na kumwambia kuwa yule bibi aliyekuwa anatusumbua hapa kijijini na alimchukua mtoto wangu msukule sasa leo nimefunga kazi yule mwananchi akatoa taarifa kwa viongozi wa sungusungu na wakatoa taarifa polisi huyo mtuhumiwa akakamatwa.

Chanzo - EATV
Share:

CPB YATENGA BILIONI 100 KUNUNUA MAZAO KWA WAKULIMA







Na Mwandishi wetu ,MWANZA.

BODI ya Wakurugenzi k Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) imesema inaenda kufanya mapinduzi makubwa katika sekta ya Mazao na Nafaka kwa ujumla kwa kutenga Sh. Billioni 100 kwa ajili ya ununuzi wa mazao kutoka kwa Wakulima hapa nchini.

Aidha Bodi hiyo imetangaza fursa kwa wakulima wote nchini kulima mazao mengi msimu huu kwani Bodi hiyo inaenda kunu nua mazao hayo kwa wingi na kwa bei ya soko.

Akizungumza jana mara baada ya ziara ya bodi hiyo kutembelea miradi yao  iliyopo Kanda ya Ziwa Mwaza mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi aliyeongea kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi hiyo Kapenjama Ndile alisema wanaenda kufanya mapinduzi makubwa ambayo hayajawahi kutokea katika Shirika hilo.

‘’Tunaenda kufanya mapinduzi makubwa katika sekta ya Mazao na Nafaka kwa ujumla tunaenda kununua mazao ya zaidi ya Sh. Billioni 100 kutoka kwa Wakulima wa hapa nchini’’., alisema Ndile.

Aidha Ndile aliwataka wakulima hapa nchini wazalishe mazao mengi kwani CPB itanunua mazao hayo kwa bei ya soko hivyo inatoa fursa kwa Watanzania kuuza mazao yao katika Bodi hiyo ili waweze kujikwamua Kiuchumi.

‘’CPB ni kimbilio kwa Wakulima tunanunua mazao kutoka kwao, lakini tunaongezea mazao thamani kwa kuchakata mazao kupitia viwanda vyetu vilivyopo katika baadhi ya Mikoa’’, alisema Mkurugenzi huyo wa Bodi hiyo.

Mkurugenzi huyo alisema kipaumbele cha kwanza ni chakula na usalama wa Chakula, ndio maana Serikali iliunda Bodi ya Nfaka na Mazao Mchanganyiko ili kuwe na usalama wa chakula.

Aidha Ndile alisema Bodi hiyo inaendelea kujenga viwanda ikiwemo Kiwanda cha kuchakata Muhogo kitakachojengwa katika Jiji la Mwanza na Kingine kitajengwa Handeni Tanga.

Aidha Mkurugenzi huyo wa Bodi alisema kuwa wataendelea kupanua Viwanda vilivyopo na kuajili wataalamu wa viwandani lengo ni kupanua wigo wa uzalishaji ili waweze kuuza bidhaa ndan I ya nchi na nje ya nchi.

‘’Tuna viwanda Vingine vilivyomo Arusha ambapo kuna Kiwan da cha kuchakata Mahindi, Ngano, kiwanda kingine kipo Iringa kinachakata Mahindi na Dodoma kinachakata Mahindi Alizeti’, alisema Linde.

Naye Mjumbe wa Bodi hiyo Fadhili Ngajilo alisema kuwa kuwa Bodi hiyo imepania kuleta mabadiliko makubwa kwa Watanzania kwa kufungua milango ya biashara kupitia CPB.

Alisema kuwa hivi sasa Bodi hiyo imetengeneza utaratibu wa kuwatambua madalali wa mazao kama wafanyabiashara rasmi kwaajili ya kurahisisha biashara kati ya wakulima na Bodi hiyo.

‘’Bodi  hii imeingia kwenye ushindani wa biashara kwa kufanya biashara na mataifa ya nje  ila tutaboresha kwa viwango vya Kimataifa’’, alisema Ngajilo.

David Shambwe  ambaye pia ni mjumbe wa Bodi hiyo alisema kuwa wakulima walime mazoa mengi Bodi ipo kwajili yao kwani pia kutakuwa na mikata ya wakulima.

‘’Mikataba ya wakulima ina faida kubwa kwa wakulima kwa wanaweza kupata hata mikopo kutoka katika taasisi za fedha kwani watakuwa na vielelezo na mikata inayotambulika’’, alisema Shambwe.

Alisema Kuwa mikataba hiyo ipo kwenye mazao mbalimbali ikiwemo wakulima ya Ngano, Mahindi, Mpunga, Alizeti, ambapo alisistiza Vyama Vya msingi vihamasishe wakulima kulima mazao mengi soko lipo CPB.

CPB ni Shirikala la Kibiashara la serikali lililopo chini ya Wizara ya Kilimo kazi yake kubwa ni kununua mazao kutoka kwa Wakulima na wafanyabiashara wa mazao alafu wanayaongezea thamani kwa kuchakata katika viwanda 

Share:

MBINU UNAYOWEZA KUTUMIA ILI KUONGEZWA MSHAHARA KAZINI

Katika maisha ya kazi hakuna anayependa kubaki sehemu kwa muda mrefu kwani kila mtu hutaka kuwa katika nafasi tofauti (kupanda daraja) kadiri muda unavyoenda, watu wengi husema kuwa kupata cheo fulani katika kazi unayoifanya huwa ni bahati na bidii kwenye kazi ile.

Hiyo ni kweli lakini wakati mwingine waweza kuwa na vyote lakini ikawa ni vigumu kufanikiwa kutokana na aina ya Bosi wako, wapo wenye roho mbaya ambao ni vigumu sana kumpatia mfanyakazi fursa hiyo.

Nilikuwa nimehitimu Chuo Kikuu na kupata Shahada ya teknolojia, nilifanikiwa kupata kazi katika kampuni moja binafsi Jijini Nairobi, licha ya mshahara, hapo nilizidi kupata ujuzi katika mambo ya teknolojia. 

Nilifahamu kwamba siku moja ningepata kazi yenye cheo kikubwa ambayo nilikuwa natamania katika maisha, nilitamani siku moja niwe Meneja katika kampuni fulani ila kampuni ilie ilinipa mshahara mdogo licha ya ueledi wangu katika kazi.

Katika kampuni ile niligundua kuna wafanyikazi wengine hawakuwa na uwezo kabisa wa kitaaluma kuhusu kazi ile, wengi wao walikuwa ni watu waliosaidiwa tu kupata nafasi zile za kazi kwa njia ya mlango wa nyuma kwa kutoa rushwa.

Hali ile ilinikosesha usingizi kwani licha ya wao kutokuwa na Shahada walipokea mshahara mkubwa na mara kwa mara Bosi wangu alipenda kunipa shughuli nyingi pale Ofisini bila ya malipo ya ziada kando na mshahara wangu.

Alinituma safari za mbali bila hata ya posho, nilikumbwa na msongo wa mawazo kwani nilifahamu kuwa iwapo ningeacha kazi ile, ilikuwa ni nadra kupata kazi nyingine. Hali hii ilinipa moyo licha ya kuwa sikuwa nimepata kuongezwa mshahara na kupandishwa cheo.

Jambo lililonishangaza ni kwamba wafanyakazi wageni waliokuja katika Ofisi ile walipandishwa vyeo kila baada ya miezi saba, wakati mimi nilikuwa katika Ofisi ile kwa muda wa miaka mine sikuwahi kupandishwa cheo wala hata kuongezewa mshahara.

Kimani ambaye alikuwa ni rafiki wangu wa kitambo alinishauri kumtembelea African Doctors kwani alikuwa amemsaidia kupata kazi na pia mshahara wake ulikuwa mkubwa.

Alinielekeza hadi zilipo Ofisi za African Doctors, niliweza kufika na kuhudumiwa vizuri na kwa haraka zaidi, siku tatu baada ya kurejea Ofisini kwangu, nilishangaa jinsi mambo yalivyokuwa yakienda. Nilipata barua iliyonifahamisha kuwa mimi ndiye Meneja mpya wa kampuni ile ya Teknolojia na mshahara wangu umepanda mara saba.

Nilifahamu fika kwamba African Doctors alikuwa amenisaidia katika kila hali, ni mtaalam ambaye ana uwezo wa kutibu magonjwa kama vile kisonono, kifafa na mengineyo.

Wasiliana na African Doctors kwa namba; +254 769 404965, tembelea tovuti yao; www.african-doctors.com au watumie email; africandoctorheals@gmail.com.




Mwisho.


Share:

MBUNGE CHIKOTA AITAKA SERIKALI KUJENGA VITUO VYA AFYA MNONGODI NA NYUNDO








Na Mwandishi Wetu

Mbunge wa Nanyamba (CCM), Abdallah Chikota amehoji serikali kuhusu fedha za ujenzi wa vituo vya afya katika Kata za Mnongodi na Nyundo.


Akiuliza swali bunge leo, Chikota amehoji serikali katika bajeti ya TAMISEMI iliyopitishwa ya ujenzi wa vituo vipya vya afya, inatoa tamko gani ujenzi wa vituo vya afya kata za kimkakati jimbo la Nanyamba.

Pia, amehoji kutokana na ujenzi wa kituo cha Kitaya kukamilika lini serikali itapeleka vifaa tiba na wataalamu ili huduma zitolewe.

Akijibu maswali hayo, Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Deogratius Ndejembi, amesema serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya kwenye Kata za Kimkakati nchini ikiwa ni Mnongodi na Nyundo.

Ndejembi amesema katika mwaka wa fedha 2021/22 serikali ilitenga Sh.bilioni 117 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya vya kimkakati kwenye Kata 234 nchini.


“Halmashauri ya Mji wa Nanyamba ilitengewa kiasi cha Sh.milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya Kitaya. Ujenzi wa Kituo hicho upo hatua ya ukamilishaji,”amesema.


Naibu Waziri huyo amesema katika mwaka 2023/24 serikali imetenga Sh.Milioni 400 kwa ajili ya ununuzi vifaa tiba vya zahanati na vituo vya afya kwenye mji huo.

Hata hivyo, amesema serikali itahakikisha inatenga fedha za vituo vya afya vya Nanyamba.

Share:

Friday, 12 May 2023

Picha : JUMUIYA YA WAZAZI SHINYANGA MJINI YAFANYA ZIARA KITANGILI, YARIDHISHWA UJENZI WA DARAJA...."TUWAPE AMANI VIONGOZI WALIOPO MADARAKANI"

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga, Fue Mrindoko na viongozi wa Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini na kamati ya utekelezaji wakitembelea na kukagua ujenzi wa daraja la Kitangili. 

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini imefanya ziara katika kata ya Kitangili na kukagua ujenzi wa mradi wa Daraja, kutoa msaada Chakula kwa watoto wenye ulemavu wa viungo na akili wanaolelewa katika Kituo cha Brothers of Charity na kuzungumza na wanachama na viongozi wa CCM kata ya Kitangili.


Ziara hiyo ya Viongozi wa Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Shinyanga walioambatana na Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya hiyo imefanyika leo Ijumaa Mei 12,2023.


Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga, Fue Mrindoko amesema ziara hiyo pia imelenga kutoa shukrani kwa wanachama wa CCM kufuatia uchaguzi wa ndani ya CCM uliofanyika mwaka jana.

“Tunaendelea na ziara ya kuzitembelea kata zote zilizopo katika wilaya ya Shinyanga Mjini tukihamasisha wanachama na viongozi wa CCM kuipenda CCM na kupinga makundi katika chama ili kuwe na mshikamano kwani mshikamano ndiyo unajenga chama”,amesema Mrindoko.


Mwenyekiti huyo pia amekemea matukio ya ukatili wa kijinsia pamoja na mmonyoko wa maadili unaochangia kuwepo kwa matukio ya ubakaji na ulawiti ambapo amewataka wazazi na walezi kupiga vita vitendo viovu ukiwemo ushoga.


Aidha ametaka hatua kali za kisheria zichukuliwe kwa watu wanaobainika kufanya vitendo viovu katika jamii.
Viongozi wa Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini na kamati ya utekelezaji wakiwasili katika kata ya Kitangili kwa ajili ya kikao na viongozi wa CCM kata ya Kitangili.

Katika hatua nyingine ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuleta fedha nyingi kwa ajili ya maendeleo.


“Katika ziara hii tumeshuhudia miradi ya maendeleo inaendelea kutekelezwa mfano hata hili daraja linalounganisha kata ya Ibinzamata na Kitangiri ujenzi wake unaendelea vizuri na tunatarajia hadi ifikapo Juni 1,2023 daraja hili ambalo limekuwa kero kwa muda mrefu litaanza kutumika”,amesema Mrindoko.


“Ujenzi wa daraja la Kitangili unaridhisha na mwezi Juni wananchi wataanza kupita pale. Mradi huu unaendelea vizuri”,amesema.
Muonekano ujenzi wa daraja la Kitangili Ijumaa Mei 12,2023.

Akizungumza wakati wa kukabidhi chakula kwa watoto wenye ulemavu wa akili wanaolelewa katika Kituo cha Brothers of Charity, Mrindoko amesema ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha anawasaidia watoto hao wenye uhitaji.


“Tunawashukuru walezi wa watoto hawa. Hii kazi mnayofanya kulea na kuwafundisha watoto hawa mambo mbalimbali kwakweli kazi hii mnayofanya ni kazi ya kitume. Tunawashukuru na tunawapongeza sana. Nimeambiwa watoto hawa wenye usonji walikuwa hawajui chochote lakini mmewafundisha jinsi ya kujitambua na sasa wanafanya wao wenyewe. Asanteni sana nasi tunaendelea kukitangaza kituo hiki lakini pia tutaendelea kufika hapa ili tushirikiane kutatua changamoto zinazojitokeza”,amesema.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga, Fue Mrindoko (aliyevaa kofia kushoto) na viongozi mbalimbali wakikabidhi chakula katika kituo cha kulelea watoto cha Brother of Charity kilichopo Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga

Kwa upande Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Bi. Doris Yotham Kibabi amewataka wanaCCM kuacha viongozi waliopo madarakani kuanzia ngazi ya serikali za mitaa, madiwani na mbunge waachwe wafanye kazi na wapewe ushirikiano wa kutosha.

“Viongozi waliopo madarakani waachwe wafanye kazi kwa sababu muda wa kugombea bado haujafika. Tuwape amani viongozi waliopo madarakani na tunaendelea kukemea makundi ndani ya chama yanayotokana na chaguzi zilizopita”,amesema Kibabi.


Kibabi ametumia fursa hiyo kuwakumbusha wanachama wa CCM kuendelea kulipa ada za uanachama, kujisajili kwenye mfumo wa kielektroniki, kuongeza wanachama wapya pamoja na kubuni na kuanzisha miradi ili kujiimarisha kiuchumi.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Bi. Doris Yotham Kibabi akizungumza kwenye kikao na viongozi wa CCM kata ya Kitangili

Naye Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM wilaya ya Shinyanga Mjini kutoka Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Mhandisi James Jumbe Wiswa mbali na kuhamasisha amewataka wazazi na walezi kuepuka mazingira yanayochangia vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa watoto ikiwemo kuwalaza chumba kimoja na wageni.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Kitangili Mariam Nyangaka amesema utekelezaji wa ujenzi wa madaraja unaendelea vizuri na pindi yatakookamilika wananchi wataondokana na kero ya muda mrefu kwani madaraja yamekuwa kero kubwa kwa wananchi.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga, Fue Mrindoko (kulia) akizungumza wakati viongozi wa Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini  na kamati ya utekelezaji wakitembelea na kukagua ujenzi wa daraja la Kitangili leo Ijumaa Mei 12,2023. Picha na Kadama Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga, Fue Mrindoko na viongozi wa Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini na kamati ya utekelezaji wakitembelea na kukagua ujenzi wa daraja la Kitangili leo Ijumaa Mei 12,2023. 
Muonekano ujenzi wa daraja la Kitangili leo Ijumaa Mei 12,2023. 
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Bi. Doris Yotham Kibabi akizungumza katika daraja la Kitangili Mjini Shinyanga
Viongozi wa Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini na kamati ya utekelezaji wakitembelea na kukagua ujenzi wa daraja la Kitangili leo Ijumaa Mei 12,2023. 
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga, Fue Mrindoko (aliyevaa kofia kushoto) na viongozi mbalimbali wakikabidhi chakula katika kituo cha kulelea watoto cha Brother of Charity kilichopo Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga, Fue Mrindoko (aliyevaa kofia kushoto) na viongozi mbalimbali wakikabidhi chakula katika kituo cha kulelea watoto cha Brother of Charity kilichopo Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga, Fue Mrindoko (aliyevaa kofia kushoto) na viongozi mbalimbali wakikabidhi chakula katika kituo cha kulelea watoto cha Brother of Charity kilichopo Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga
Sehemu ya chakula kilichotolewa na Jumuiya ya Wazazi CCM Shinyanga Mjini katika kituo cha kulelea watoto cha Brother of Charity kilichopo Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga, Fue Mrindoko akizungumza kwenye kikao na viongozi wa CCM kata ya Kitangili
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga, Fue Mrindoko akizungumza kwenye kikao na viongozi wa CCM kata ya Kitangili
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga, Fue Mrindoko akizungumza kwenye kikao na viongozi wa CCM kata ya Kitangili
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Bi. Doris Yotham Kibabi akizungumza kwenye kikao na viongozi wa CCM kata ya Kitangili
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Bi. Doris Yotham Kibabi akizungumza kwenye kikao na viongozi wa CCM kata ya Kitangili
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Bi. Doris Yotham Kibabi akizungumza kwenye kikao na viongozi wa CCM kata ya Kitangili
Katibu wa Mbunge Jimbo la Shinyanga Mjini Samwel Jackson akizungumza kwenye kikao na viongozi wa CCM kata ya Kitangili
Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM wilaya ya Shinyanga Mjini kutoka Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Mhandisi James Jumbe Wiswa akizungumza kwenye kikao na viongozi wa CCM kata ya Kitangili
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Kata ya Kitangili Zawia Hassan Mpanda akizungumza kwenye kikao na viongozi wa CCM kata ya Kitangili
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Kata ya Kitangili Gabriel Swila akisoma taarifa ya kazi za jumuiya ya wazazi kata ya Kitangili kwa mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Shinyanga Mjini

Diwani wa kata ya Kitangili Mariam Nyangaka akizungumza kwenye kikao hicho.
Viongozi wa CCM wakipiga picha ya kumbukumbu.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Share:

WAZIRI MCHENGERWA ATEKELEZA AGIZO LA WAZIRI MKUU, AFIKA ENEO LA TUKIO, ATOA POLE NA MAAGIZO MAZITO KWA WATENDAJI.



Na John Mapepele

Agizo la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa alilolitoa jana bungeni la kutaka Waziri wa Maliasili na Utalii na Watendaji wa Wizara hiyo kufika mara moja kijiji cha Mwanavala wilayani Mbarali wakishirikiana na Uongozi wa Mkoa wa Mbeya kutatua migogoro baina ya Hifadhi ya Ruaha na wananchi hao limekamilika leo Mei12,2023 baada ya kufika.

Akiongea kwenye kikao na wananchi hao leo mei 12, 2023 amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kuwachukulia hatua za kinidhamu maafisa wote wa Serikali walioshiriki kwenye migogoro huo.
Hata hivyo amewaomba wananchi kuzingatia sheria ambapo amewataka kutovamia maeneo ya makazi ambapo katika mgogoro huo baadhi ya wananchi walikutwa kilomita kumi ndani ya Hifadhi ndipo walipoanza kutolewa kwa nguvu na wahifadhi.

Mhe. Mchengerwa ametoa mkono wa pole wa shilingi milioni moja kwa wananchi watano kila moja kama kifuta machozi kutokana na ugomvi wa wahifadhi na wananchi hao. Hata hivyo hakuna tukio lolote la kifo.

Amefafanua kuwa tatizo la mipaka katika Hifadhi hiyo linakwenda kumalizika ambapo amesema jumatatu anasaini GN mpya ya mpaka wa eneo hilo.
Hata hivyo imethibitika kuwa madai ya kwamba ng'ombe 250 walishikiliwa siyo ya kweli kwa kuwa wananchi wote katika mkutano wamekubali kuwa hakuna ng'ombe hata moja aliyeshikiliwa na Hifadhi

Aidha amesema mipaka ya Hifadhi hiyo iliwekwa mwaka 1910 wakati Hifadhi hiyo ikijulikana kama Saba Game Reserve na mwaka 1946 ikijulikana kama Hifadhi ya Rungwe na hatimaye mwaka 1964 kama Hifadhi ya Ruaha hadi sasa.

Ameongeza kuwa dhamira ya Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuona kuwa kero zote katika maeneo ya Hifadhi zinatatuliwa kwa amani na upendo.

"Ibara ya 68 ya CCM inasisitiza uhifadhi wa raslimali hivyo sisi sote tunapaswa kushirikiana kwa pamoja tuhifadhi kwa faida ya kizazi cha sasa na baadaye" ameongeza Mhe. Mchengerwa
Katika kikao hicho, bwana Ngalao Laini ameiomba Serikali kuangalia namna bora ya kuwahamisha wananchi na kuwatengea maeneo bora ya makazi pindi inapoamuliwa kuwaondoa katika Hifadhi.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ambaye pia aliambatana katika ziara hiyo na Kamati ya ulinzi na Usalama ya Mkoa, na wilaya ya Mabarali na viongozi wa CCM wa wilaya hiyo aliwaambia wananchi katika mkutano huo kuwa Serikali itahakikisha kuwa wananchi wote wanatendewa haki ikiwa ni pamoja na kufanya tathimini za makazi na kuwalipa fidia stahiki.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger