Saturday, 13 May 2023

MBUNGE CHIKOTA AITAKA SERIKALI KUJENGA VITUO VYA AFYA MNONGODI NA NYUNDO

...







Na Mwandishi Wetu

Mbunge wa Nanyamba (CCM), Abdallah Chikota amehoji serikali kuhusu fedha za ujenzi wa vituo vya afya katika Kata za Mnongodi na Nyundo.


Akiuliza swali bunge leo, Chikota amehoji serikali katika bajeti ya TAMISEMI iliyopitishwa ya ujenzi wa vituo vipya vya afya, inatoa tamko gani ujenzi wa vituo vya afya kata za kimkakati jimbo la Nanyamba.

Pia, amehoji kutokana na ujenzi wa kituo cha Kitaya kukamilika lini serikali itapeleka vifaa tiba na wataalamu ili huduma zitolewe.

Akijibu maswali hayo, Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Deogratius Ndejembi, amesema serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya kwenye Kata za Kimkakati nchini ikiwa ni Mnongodi na Nyundo.

Ndejembi amesema katika mwaka wa fedha 2021/22 serikali ilitenga Sh.bilioni 117 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya vya kimkakati kwenye Kata 234 nchini.


“Halmashauri ya Mji wa Nanyamba ilitengewa kiasi cha Sh.milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya Kitaya. Ujenzi wa Kituo hicho upo hatua ya ukamilishaji,”amesema.


Naibu Waziri huyo amesema katika mwaka 2023/24 serikali imetenga Sh.Milioni 400 kwa ajili ya ununuzi vifaa tiba vya zahanati na vituo vya afya kwenye mji huo.

Hata hivyo, amesema serikali itahakikisha inatenga fedha za vituo vya afya vya Nanyamba.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger