MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga(UVCCM) Ramadhan Omary kulia akiwa na jembe akishiriki kulima na vijana kwa niaba ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Mohammed Kawaida wakati alipotembelea Chuo cha Kilimo (Mati Mlingano )ambacho ni Miongoni mwa Vituo vya Mradi wa jenga kesho yako iliyo bora (BBT).
Na Oscar Assenga, MUHEZA
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga(UVCCM) Ramadhan Omary leo aliongoza ziara ya kamati ya Utekelezaji ya UVCCM Mkoa wa Tanga kwa Niaba ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Mohammed Kawaida kutembelea Chuo cha Kilimo (Mati Mlingano )ambacho ni Miongoni mwa Vituo vya Mradi wa jenga kesho yako iliyo bora (BBT).
Katika ziara hiyo aliwataka vijana kuitumia fursa hiyo ya uwepo wa chuo hicho kwa manufaa yao binafsi na jamii inayowazunguka kwasababu serikali imetumia gharama kubwa kujenga kwaajili ajili ya kuwanufaisha na kuwaajiri Vijana kwenye sekta ya Kilimo,
"Mradi huu wa BBT ni moja kati ya miradi iliyotupa heshma kubwa vijana tuufanyeni kwa kwa ustadi na uaminifu mkubwa"Alisema Omary
Mwenyekiti hiyo alitumia fursa hiyo kushauri uongozi wa chuo kuwa na utaratibu wa kutoa mafunzo kwa wakulima wa maeneo ya hayo na maeneo ya karibu kwa ajili ya kuwanufaisha wakulima wa Maeneo hayo na kuweza kukuza kilimo bora kwa jamii inayokuzunguka,
"Mkoa wetu unafursa nyingi za kilimo kaimu mkuu wa chuo angalieni namna chuo hiki kitaweza kuwanufaisha vijana/ jamii inayo wazunguka ili tuwe na kilimo chenye tija"Alisisitiza Omary
Aidha katika hatua nyengine Omary aliwataka Makada wa CCM na Vijana wa Chuo cha Mati Mlingano kwa niaba ya vijana wote wa Tanga kuwa namna pekee ya Kumlipa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia kuyasema mazuri anayoyafanya na kuyatangaza mema anayoyafanya kwa Watanzania wote kiujumla kwani ameyafanya mengi kwa ajili ya Watanzania.
"Kwa kweli sisi kama vijana katika mkoa wa Tanga tunapongeza kazi kubwa inayofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu hivyo kama vijana lazima tuzitangaze kazi hizo tusiishie kusema mama anaupiga mwingi "Alisema Mwenyekiti huyo
"Lakini pia tumuombe Mungu atujalie viongozi wengi mithili ya Bashe kwa sababu unamuona kabisa anaguswa na changamoto za vijana na jamii ya Kitanzania"Alisema
0 comments:
Post a Comment