Saturday, 20 May 2023

SERIKALI YAJIPANGA KUTOA ELIMU BORA ZAIDI ITAKAYOSAIDIA VIJANA KUSONGA MBELE

...


Na Woinde Shizza ,ARUSHA

Serikali imejipanga kutoa elimu bora zaidi na ambayo itawasaidia vijana kusonga mbele lengo likiwa kuhakikisha kuwa kile kinachofundishwa kwa wanafunzi kinaendana na wazalishaji wa bidhaa pamoja na watoaji wa huduma, ili vijana wanapotoka vyuoni elimu waliyopata iweze kuwasaidia.
Makamu mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ambayo inasimamia wizara ya elimu Mh. Husna Sekiboko akiongea katika uzinduzi rasmi wa maonesho ya Elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi, yaliyoandaliwa na NACTVET

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda wakati wa uzinduzi rasmi wa maonesho ya Elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi, yaliyoandaliwa na NACTVET, ambapo alisema kuwa serikali imejipanga kuwasaidia vijana kupata elimu bora ya Ujuzi ambayo itawasaidia kujiendeleza kiuchumi binafsi na Taifa kwa ujumla.


Aidha alisema kwa kutimiza hilo serikali imejipaga kujenga vyuo vya veta 64 katika wilaya na Chuo kimoja kikubwa cha Veta katika mkoa ,wanaongeza uwezo mkubwa sana wa kufundisha vijana katika vyuo hivyo yote hayo not kuhakikisha vijana wanapotoka shuleni elimu aliyoipata ikamsaidie huko mtaani.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akiongea mara baada ya kuzinduzi rasmi wa maonesho ya Elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi, yaliyoandaliwa na NACTVET,

Kwa upande wa mwenyekiti wa NACTIVET Prof. John Kondoro, alisema kuwa sasa hivi Kama serikali inayovyofanya kupitia mitaala pamoja na sera ya mafunzo ,wao wameanza mapema lakini wanaunga mkono serikali kuhakikisha kwamba wanafunzi wanaopita katika vyuo vyao wanakuwa tayari ni mahiri lakini pia wanaonyesha nini wanafanya kwa kutumia mikono yao ,ni ujuzi gani walio nao ,ni sekta gani wanapokwenda na wanakubaliwaje na soko.


Naye makamu mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ambayo inasimamia wizara ya elimu Mh. Husna Sekiboko alipongeza jitihada za serikali lakini pia alipongeza wizara kwa sababu wameamua kupindua elimu nakuipeleka zaidi katika elimu ya vitendo ili vijana waweze kujiajiri.


"Na mtakumbuka watanzania wote inatokana na wimbi kubwa la vijana wengi kukosa ajira ,sasa profesa mkenda sasa anatamani kijana anapo hitimu awe na ujuzi dhahiri kwa akili ya kwenda kumudu maisha yake", alisema Husna.


Alisema wao kama wabunge kazi yao kubwa ni kuhakikisha Kama kutakuwa na Sheria ,kanuni taratibu zozote ambazo zinatakiwa ama kurekebishwa au kuanzishwa ili kuhakikisha kwamba wizara ama serikali inatekeleza vizuri jukumu hilo wao wapo tayari kufanya hivyo.


Maonesho ya NACTVET yanaendelea katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, maonesho yaliyoanza Tarehe 16 mei na yanatarajiwa kufungwa Rasmi Tarehe 22 mai 2023.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger