Monday, 15 August 2022

BARRICK ILIVYOSHIRIKI UZINDUZI WA KIPINDI CHA THAMANI YA MADINI

Kampuni ya Madini ya Barrick, imeshiriki na kudhamini mbio za Madini Marathon zilizofanyika mjini Shinyanga ambazo zilienda sambamba na uzinduzi wa kipindi kinachohusu sekta ya madini kinachojulikana kama Thamani ya madini kitakachorushwa na kituo cha Runinga cha Channel Ten ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Madini, Dk. Doto Biteko.
Waziri wa Madini, Dk. Doto Biteko akizungumza Agosti 14,2022 wakati wa uzinduzi wa Kipindi cha Thamani Madini kitakachokuwa kinarushwa Channel Ten
Kaimu Meneja Mahusiano na Mazingira wa Barrick Bulyanhulu, Zuwena Senkondo, akiongea kwa niaba ya kampuni katika hafla hiyo.
Kaimu Meneja Mahusiano na Mazingira wa Barrick Bulyanhulu, Zuwena Senkondo, akiongea kwa niaba ya kampuni katika hafla hiyo.
Msimamizi wa ufungaji wa Mgodi wa Barrick Buzwagi, Michael Mhanuka Wilson akiongea wakati wa hafla hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kipindi cha Thamani Madini kitakachokuwa kinarushwa Channel Ten
Wafanyakazi wa Barrick wakifuatilia matukio wakati wa hafla hiyo.
Wadau mbalimbali wakifuatilia matukio wakati wa hafla hiyo.
Wafanyakazi wa Barrick walishiriki kupiga picha ya pamoja na mgeni rasmi,Waziri wa Madini,Dk.Doto Biteko na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Sophia Mjema.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Barrick wakifuatilia matukio ya michezo ya Madini Marathon


Share:

ORODHA YA MASENETA WALIOCHAGULIWA NA KAUNTI ZAO KENYA



001 Mombasa-Mohammed Faki(ODM)

002 Kwale-Isa Juma Boy(ODM)

003 Kilifi-Stewart Madzayo(ODM)

004 Tana River-Danson Mungatana(UDA)

005 Lamu-Joseph Githuk(Jubilee)

006 Taita Taveta-Johnes Mwaruma(ODM)

007 Garissa-Hajji Abdulkadir Haji(Jubilee)

008 Wajir-Abass Sheikh Mohammed (UDM)

009 Mandera-Ali Roba(UDM)

010 Marsabit-Mohamed Said Chute (UDA)

011 Isiolo-Fatuma Dullo(Jubilee)

012 Meru-Kathuri Murungi(UDA)

013 Tharaka Nithi -Julius Mwenda Gataya(UDA)

014 Embu-Alexander Mundigi (DP)

015 Kitui-Enock Wambua(Wiper)

016 Machakos-Agnes Kavindu(Wiper)

017 Makueni- Dan Maanzo(Wiper)

018 Nyandarua-John Methu(UDA)

019 Nyeri-Wahome Wamatinga(UDA)

020 Kirinyaga- James Kamau Murango(UDA)

021 Muranga- Joe Nyutu (UDA)

022 Kiambu-Karungo Thang’wa(UDA)

023 Turkana-James Lomenen (UDA)

024 West Pokot-Julius Murgor(UDA)

025 Samburu-Lelengwe Ltumbesi (UDA)

026 Trans Nzoia-Allan Chesang(UDA)

027 Uasin Gishu – Jackson mandago(UDA)

028 Elgeyo Marakwet-Kipchumba Murkomen(UDA)

029 Nandi-Samson Cherargei (UDA)

030 Baringo-William Cheptumo(UDA)

031 Laikipia-John Kinyua (UDA)

032 Nakuru -Tabitha Karanja(UDA)

033 Narok-Ledema Ole Kina (ODM)

034 Kajiado-Samuel Kanar Seki(UDA)

035 Kericho-Aaron Cheruiyot (UDA)

036 Bomet – Hillary Sigei (UDA)

037 Kakamega-Dr Bonny Khalwale(UDA)

038 Vihiga-Godfrey Osotsi(ODM)

039 Bungoma-Moses Wetangula(Ford K)

040 Busia-Okiya Omutatah(NRA)

041 Siaya – Oburu Odinga(ODM)

042 Kisumu -Tom Ojienda(ODM)

043 Homa Bay -Moses Kajwang(ODM)

044 Migori – Eddy Oketch(ODM)

045 Kisii -Richard Onyonka(ODM)

046 Nyamira -Okong’o Omogeni(ODM)

047 Nairobi -Edwin Sifuna(ODM)
Share:

RAIS WA FEMATA JOHN BINA ATEMBELEA BANDA LA WANAWAKE WACHIMBAJI MADINI 'TAWOMA' ... AKEMEA UTOROSHAJI WA MADINI

Rais wa Chama Cha Wachimbaji wadogo wa Madini Tanzania (FEMATA), John Bina (wa pili kushoto) akiwa katika banda la Chama cha Wachimbaji Wanawake Tanzania (TAWOMA) katika uwanja wa CCM Kambarage Manispaa ya Shinyanga.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Wanawake Tanzania (TAWOMA) , Rachel Njau (katikati) akimwelezea Rais wa Chama Cha Wachimbaji wadogo wa Madini Tanzania (FEMATA), John Bina (wa pili kulia) kuhusu shughuli zinazofanywa na TAWOMA 

Na Mwandishi wetu - Shinyanga
Rais wa Chama Cha Wachimbaji wadogo wa Madini Tanzania (FEMATA), John Bina akizungumza wakati akitembelea mabanda ya washiriki wa madini Marathon Mkoa wa Shinyanga yaliyofanyika katika uwanja wa CCM Kambarage Manispaa ya Shinyanga.


Rais wa Chama Cha Wachimbaji wadogo wa Madini Tanzania (FEMATA), John Bina amelaani vitendo vya Utoroshaji madini na kuwaonya baadhi ya wachimbaji wa madini wanaotorosha madini na baadhi ya watu wanaoshiriki utoroshaji madini.


Rais huyo wa FEMATA ameyasema hayo Agosti 14,2022 wakati akitembelea mabanda mbalimbali ya washiriki wa Madini Marathon Mkoa wa Shinyanga yaliyofanyika Jumapili Agosti 15,2022 katika uwanja wa CCM Kambarage Mkoa wa Shinyanga.


"Kupitia Shinyanga madini Marathon natumia nafasi hii kupongeza
kamati ya maandalizi na kulaani utoroshaji wa madini. Nawaonya
wachimbaji madini na baadhi ya watu wanaoshiriki utoroshaji madini kuacha mara moja tabia hiyo", amesema Bina.


Bina amesema Wachimbaji Wadogo wengi wao hawana mitaji ya kununua Miundo Michundo hivyo kuziomba Taasisi za Kifedha kuangalia njia nzuri ya kuwasaidia Wachimbaji Wadogo wa Madini kwa kuwapatia mikopo kwani hivi sasa bado kuna ugumu katika kuwakopesha wachimbaji hao.


Pia Rais huyo wa FEMATA ametembelea banda la viongozi wa Chama cha Wachimbaji Wanawake Tanzania (TAWOMA) na kuwapongeza kutokana na kazi kubwa wanayoifanya ikiwemo kuwaunganisha wanawake wachimbaji wengine katika chama hicho.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji wadogo mkoa wa Shinyanga SHIREMA Hamza Tandiko amempongeza Rais wa FEMATA kwa kufika mkoani Shinyanga na kushiriki Shinyanga madini Marathon huku katibu wa SHIREMA Gregori Kibusi akiahidi kuendelea kutoa ushirikiano ikiwemo kuhimiza wachimbaji wa madini kulipa kodi na kuepuka kutorosha madini hali itakayo sadia kuchangia ukuaji wa pato la Taifa.
Rais wa Chama Cha Wachimbaji wadogo wa Madini Tanzania (FEMATA), John Bina akiwasalimia washiriki wa madini Marathon Mkoa wa Shinyanga yaliyofanyika katika uwanja wa CCM Kambarage Manispaa ya Shinyanga.



Share:

JIPATIE JOINING INSTRUCTIONS FOR DIPLOMA AND CERTIFICATE HEALTH PROGRAMMES 2014/2015

INNOCENT-THE BLOGGER-BOYJ
                                     

Habazri yenu wadau wa blog hii pendwa ya MAASWAYETU BLOG Leo tena tunaweletea Joining instructions za kozi mbalimbali certificates na diploma kwa mwaka wa masomo 2014/2015.

Tunajua wengi mnazisubiria hizi form kwa hamu sana na mnataka mjue gharama za mafunzo kwa chuo ulichochaguliwa.

Kama kawaida yetu tupo hapa kusaidia watu wote wanaohitaji hizi form za kujiunga na chuo husika.
Ili kujipatia joining instructions ya kozi ulichaguliwa unatakiwa kufanya yafuatayo;
1.Tuma Email address yako
2.Tuma gharama za kutumiwa joining hii Tsh.300 kwa Mpesa
3.Ukishatumiwa kwenye email yako ,nenda staionary yoyote mpe email yako ata kuprintia kwa gharama ndogo zaidi,tofauti na ukienda kama ulivyo kwani gharama yake ni tsh.1500 hadi 2000.
4.Tafadhali tuma email yako kwenda namba 0768260834,then tutakutumia baada ya Mda si mrefu.
5.Maswayetu blog tuna joining za vyuo vipatavyo 42.
NOTE:TUMEFANYA HIVI KUTOKANA NA WATU WENGI KUTOKUWA NA UWEZO WA KUWA NA INTERNET,PIA KAMA UPO SIMIYU-MASWA UNAWEZA UKAPIGA HIYO NAMBA MOJA KWA MOJA KUJIPATIA JOINING YAKO MAPEMA IWEZEKANAVYO.,KWANI NITAKUPATIA KWA GHARAMA YA tsh.700 tu.

Pia faida kubwa ya kutumia huduma zetu,Utaweza kujibiwa Maswali mbalimbali yanyokutatiza.


Joining instruction for diploma and certificate in health Programmes 2014/2015
TANGAZO KWA WANAFUNZI WA AFYA TU
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) pamoja na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii 
inapenda kuwataarifu wanafunzi wote waliochaguliwa kwenye vyuo vya afya vya serikali nchini 
kuwa
Share:

DKT. MPANGO APONGEZA CRDB BANK MARATHON KUKUSANYA SHILINGI BILIONI 1.05 KUSAIDIA JAMII


Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango ametoa pongezi kwa mbio za hisani za kimataifa zinazoandaliwa na Benki ya CRDB “CRDB Bank Marathon” kwa kufikisha lengo la kukusanya shilingi bilioni 1 kwa ajili ya kusaidia jamii.


Dkt. Mpango ametoa pongezi hizo wakati akikabidhi mfano wa hundi kwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya na Hospitali ya CCBRT muda mchache baada ya kukamilika kwa mbio hizo ambazo zilishirikisha zaidi ya wakimbiaji 6,200.


Alipongeza uamuzi wa Benki ya CRDB kuendelea kusaidia upasuaji wa watoto wenye magonjwa ya moyo, pamoja na wazo jipya la kusaidia upatikanaji wa huduma salama za uzazi kwa wakinamama wenye ujauzito hatarishi alibainisha.
“Afya ya mama na mtoto ni moja ya maeneo yanayopewa kipaumbele kikubwa katika Sera ya Afya. Ninafarijika kuona mbio hizi zinasaidia kuimarisha eneo hili kwa kufanikisha upatikanaji wa huduma ya matibabu kwa watoto na wakinamama,” aliongezea.


Dkt. Mpango alisema fedha hizo zilizokusanywa zitasaidia kupunguza makali ya gharama kwa ajili ya upasuaji wa moyo na huduma za uzazi kwa wakinamama wenye ujauzito hatarishi ambazo watu wengi hawawezi kuzimudu pamoja na Serikali kutoa ruzuku ya asilimia 80.
Dkt. Mpango alisema Serikali inaunga mkono na kufurahishwa sana na ubunifu wa taasisi za kizalendo kama Benki ya CRDB kusaidia sekta za kijamii kama vile afya, elimu, mazingira, na uwezeshaji kwa vijana na wanawake.


Viongozi mbalimbali waliongozana na Makamu wa Rais kushiriki mbio hizo ikiwamo Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Mheshimiwa Mussa Azan Zungu, Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa, na Michezo, Mheshimiwa Pauline Gekule, na Waziri wa Michezo Zanzibar, Mheshimiwa Tabia Mwita Maulid.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alibainisha kuwa mbizo za mwaka huu zimevuka lengo la ukusanyaji wa Shilingi bilioni 1, akitoa shukrani kwa makampuni, na taasisi zilizojitokeza kushirikiana na benki hiyo, pamoja na wakimbiaji waliojitokeza kutoka ndani na nje ya nchi.


“Kati ya fedha zote Sh bilioni 1.05 zilizopatikana katika msimu huu wa tatu wa CRDB Bank Marathon, Shilingi Milioni 250 zimeelekezwa JKCI, Sh milioni 220 zimeenda Hospitali ya CCBRT, huku fedha iliyobaki kuelekezwa kusaidia kampeni ya mazingira ya Pendezesha Tanzania, na resi za ngalawa kule Zanzibar kukuza utamaduni,” alisema Nsekela.
Nsekela aliwashukuru Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Prof. Mohammed Janabi na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Brenda Msangi kwa ushirikiano wao huku akiweka mkazo kuwa kauli mbiu ya benki hiyo isemayo “Kasi Isambazayo Tabasamu” imefanikiwa kutokana na mchango wao wa dhati.


Katika mbio hizo washiriki takribani 60 waliofanya vizuri wameweza kujishindia zawadi zenye jumla ya thamani ya shilingi milioni 100. Zawadi hizo zinaifanya CRDB Bank Marathon kuwa mbio zinazolipa zaidi nchini ambapo washindi wa 42km kwa wanawake na wanaume wameondoka na kitita cha Sh milioni 10 kila mmoja.
Akitangaza matokeo ya mbio hizo, Mkurugenzi wa Mawasiliano Benki ya CRDB, Tully Mwambapa alisema kwa upande wa kilometa 42, Joseph Munywoki raia wa Kenya ameibuka kinara akitumi muda wa 02:14:56, wakati Shoron Kosgei raia wa Kenya aliibuka mshindi kwa upande wa wanawake akitumia muda 02:33:56.


Kwa mbio za kilometa 21, mshindi kwa upande wa wanaume alikuwa Samwel Mailu raia wa Tanzania akitumia muda wa 01:02:04, kwa upande wa wanawake mshindi alikuwa Agnes Ngolo raia wa Tanzania baada ya kutumia muda wa 01:09:16.


Katika 10km, mshindi kwa upande wa wanaume alikuwa Gabriel Geay raia wa Zambia alitumia muda wa 00:28:16, kwa wanawake Maysellina Issa raia wa Tanzania ameshika nafasi ya kwanza baada ya kutumia muda wa 00:33:52.


Katika mashindano ya mbio za baiskeli kilometa 65, Richard Laizer raia wa Tanzania aliibuka mshindi kwa upande wa wanaume kwa kutumia muda wa 01:39:24, upande wa wanawake Julia Miringu raia wa Tanzania ameibuka mshindi baada ya kutumia muda wa 01:45:11.


Kati ya washiriki 6,200 walioshiriki katika CRDB Bank Marathon mwaka huu asilimia 79 ya ni Watanzania, wakimbiaji wa kimataifa walioshiriki ni zaidi ya 1,300.
Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango akiwashukuru washiriki waliojitokeza kwenye mbio za hisani za kimataifa za Benki ya CRDB “CRDB Bank Marathon” kwa kufikisha lengo la kukusanya shilingi bilioni 1 kwa ajili ya kusaidia jamii, wakati wa kukabidhi mfano wa hundi kwa Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Brenda Msangi (wa nne kushoto), muda mchache baada ya kukamilika kwa mbio hizo ambazo zilishirikisha zaidi ya wakimbiaji 6,200. Wengine pichani ni Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete (wa pili kushoto), Naibu Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu (kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Dkt. Ally Laay (kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (watatu kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Sanlam Life Assurance, Julius Magabe.
Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango akikabidhi mfano wa hundi kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete, Dkt. Delilah Kimambo (wa nne kushoto), muda mchache baada ya kukamilika kwa mbio hizo ambazo zilishirikisha zaidi ya wakimbiaji 6,200. Wengine pichani ni Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete (wa pili kushoto), Naibu Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu (kushoto), Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul (kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Dkt. Ally Laay (wapili kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (watatu kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Sanlam Life Assurance, Julius Magabe (watatu kulia).
Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete akimkabidhi Mshindi wa kwanza wa Mbio za Kilometa 42 kwa wanaume, Joseph Munywoki raia wa Kenya, hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10 baada ya kuwashinda wenzake katika mbio za hisani za kimataifa za Benki ya CRDB “CRDB Bank Marathon” zilizokuwa na lengo la kukusanya shilingi bilioni 1 kwa ajili ya kusaidia jamii, zilizofanyika leo kwenye viwanja vya farasi Oysterbay, jijini Dar es salaam. Kulia Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Dkt. Ally Laay
Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete akimkabidhi Mshindi wa kwanza wa Mbio za Kilometa 42 kwa wanaume, Joseph Munywoki raia wa Kenya, hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10 baada ya kuwashinda wenzake katika mbio za hisani za kimataifa za Benki ya CRDB “CRDB Bank Marathon” zilizokuwa na lengo la kukusanya shilingi bilioni 1 kwa ajili ya kusaidia jamii, zilizofanyika leo kwenye viwanja vya farasi Oysterbay, jijini Dar es salaam. Kulia Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Dkt. Ally Laay
Naibu Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu akimkabidhi Mshindi wa kwanza wa Mbio za Kilometa 21 kwa wanawake, Agnes Ngolo raia wa Tanzania, hundi yenye thamani ya shilingi milioni tano baada ya kuwashinda wenzake katika mbio za hisani za kimataifa za Benki ya CRDB “CRDB Bank Marathon” zilizokuwa na lengo la kukusanya shilingi bilioni 1 kwa ajili ya kusaidia jamii, zilizofanyika leo kwenye viwanja vya farasi Oysterbay, jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger