Monday, 7 February 2022

MADARASA YAGEUZWA KITUO CHA KUVUTIA BANGI



​​​​​​​WANAFUNZI wanaosoma katika shule mbili za msingi za Kijichi wilayani Temeke mkoani Dar es Salaam, wako hatarini kuathirika kiafya na kimaadili kutokana na madarasa yao kutumika kama sehemu ya kuvuta bangi.

Vitendo hivyo vimefichuliwa juzi na viongozi wa Jumuiya ya Wazazi Kata ya Kijichi waliotembelea shule hizo kwa ajili ya kutoa misaada kwa wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu katika kuadhimiasha miaka 45 ya kuzaliwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumzia suala hilo, Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Kijichi B, Stephano Cherehani, alisema matumizi ya dawa hizo za kulevya tayari yameonekana kuwa na athari katika maendeleo ya elimu kutokana na baadhi ya wanafunzi kupata madhara.

Alisema watu wanaoingia shuleni huko kila siku kwa nia ya kuangalia michezo ya mpira wa miguu, hutumia madarasa kuvuta bangi na kuacha mabaki kila mahali.

Cherehani alisema wakati mwingine watu hao wanavuta nje ya madarasa hayo kipindi cha asubuhi, jambo ambalo linaleta usumbufu kwa wanafunzi wanapotaka kuingia darasani kuanza vipindi vya masomo.

“Jambo hili linatuathiri sisi walimu na wanafunzi pia, uvutaji wa bangi umekuwa kama jambo la kawaida, lakini chanzo kikubwa ni huu uwanja wa mpira ambao unatumika na jamii muda wote,” alisema.

Aliomba serikali kuingilia kati kwa kudhibiti vitendo hivyo ili kuwaweka wanafunzi katika hali ya utulivu na kukidhi matakwa ya mazingira bora ya ujifunzaji na ufundishaji.

“Wanafunzi hawawezi kusoma kwa umakini kama kuna mabaki ya bangi au mtu anavuta nje ya darasa, tunaomba watu hawa wadhibitiwe haraka,” alisema.

Katibu wa Wazazi wa CCM katika kata hiyo, Magdalena Komba, alimhakikishia mwalimu mkuu huyo kuwa watalifanyia kazi haraka kwa kwenda kuripoti katika vyombo husika ili eneo hilo liwe salama kwa utoaji wa elimu kwa watoto.


“Pamoja na kwamba leo (juzi) tumekuja kuwasaidia watoto wetu wanaoishi katika mazingira magumu, lakini suala hili la uvutaji bangi holela limenigusa na nitakwenda kuwasiliana na vyombo husika ili kulikomesha,” aliahidi.

Komba pia alisema jumuiya hiyo ni sawa na kiranja katika malezi ya watoto na ndio maana katika maadhimisho hayo, wameamua kutoa misaada ya sare za shule na madaftari kwa wanafunzi 27 wanaoishi kwenye mazingira magumu.

Mwanafunzi Hamisi Shamte aliyenufaika na msaada huo, aliishukuru jumuiya hiyo kwa kuwatambua na kisha kuwapa msaada huo ambao utawasaidia katika safari yao ya elimu.

Diwani wa Kijichi, Athuman Nyamlani, aliahidi kuliwasilisha suala hilo kwenye vyombo vya dola ili wanaojihusisha na vitendo hivyo wachukuliwe hatua za kisheria.
Share:

BIASHARA YANGU ZILIZOKUWA ZINANISUMBUA SASA ZIMENOGA SANA

Biashara iliyokuwa ikinisumbua kila mwaka sasa hivi imenoga kunoga. Kila jirani yangu ananimezea mate. Mimi Naitwa Frank mzaliwa wa Ilala Tanzania ambako pia nimesomea. Nilitoka kidogo kwenda jijini Dar es salaam baada ya kidato cha nne kisha nikarudi nyumbani manake sikuwa na bahati ya kupata kibarua chochote Mjini. 

Dar kwa hakika nilikaa kwa muda wa mika nne na maisha yangu yalikuwa magumu hata nusra nianze kuiba kwani marafiki wangu wengi walikuwa wezi wa usiku na mchana mitaani. Nilipoona maisha yangu yanaelekea pabaya, niliamua kurudi kwa hiari nyumbani ili nifanye ukulima. 

Nilitoa hela kidogo kutoka kwa ukulima wa sukuma kisha nikaanza kuuza malimali hapo Singida Market lakini hiyo biashara ilinisumbua kwa muda mrefu huku nikiwa sasa nimeoa. 

Maisha yakawa magumu kwa muda mrefu hata karibu nikate tamaa. Kwa bahati nzuri, kuna shangazi yangu anayeishi Uganda alirudi kunitembelea Singida alipopata nikiangaika kila mara. Hata chakula ilikuwa shida. Akaniuliza nini mbaya nikamuambia kazi sina na sina bahati pia ya mjini ndipo alinisimulia alichofanya hadi akawa tajiri kupindukia. 

“Mimi nilitembelea daktari anayeitwa Kiwanga na akanifanyia Spells za biashara yaani Business Spells. Hata haikuchukua siku mbili biashara yangu ya nguo ikanoga na sasa nina magari mawili na ploti Uganda nimelipia nataka kujenga.

 Tafadhali hata wewe jitoe kwenye lindi hili la umaskini,” alinisihi. Kwa kweli nilimuomba nambari za simu za Kiwanga Doctors na kwa bahati akanipatia nikatafuta appointment na Daktari siku iliyofuata aliponifanyia Wealth Spells.

 Leo hii mimi ni tajiri ninauza kila aina ya hardware material. Niko hardware karibu kila mji. Kama una shida kama mimi usisite kumtembelea Daktari Kiwanga. Kiwanga Doctors wanatatua shida nyingi kama Kupata mpenzi, kurudisha mpenzi, kuleta furaha na amani katika familia. Pia wanasaidia kuimarisha nyota yako pamoja na kupata dawa ya mvuto kwa mwanaume au mwanamke. Pia wanatibu magonjwa sugu kama Kisukari, Pressure kwa kutumia miti shamba na mengineyo.

 Wasiliana na Kiwanga Doctors kwa nambari +254 769404965 Kwa WhatsApp ipo pia au tembelea Website yao: www.kiwangadoctors.com. Unaweza kuandika barua pepe yaani Email kwa: kiwangadoctors @gmail.com. Si lazima usafiri hadi ofisi zao. Ongea nao kwa njia ya simu/WhatsApp na utasaidika kwa haraka kama vile watu wengine wanavyopata usaidizi.
Share:

ASKARI WANAOCHAFUA JESHI LA POLISI NCHINI KUCHUKULIWA HATUA


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini,akizungumza na mamia ya wananchi wa Mara, baada ya kupewa nafasi ya kuongea na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano wa Hadhara uliofanyika Hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Kata ya Kwangwa, Musoma Mjini, Mkoani Mara.


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini,akisisitiza jambo kwa wananchi wa Mara, baada ya kupewa nafasi ya kuongea na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano wa Hadhara uliofanyika Hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Kata ya Kwangwa, Musoma Mjini, Mkoani Mara.

...............................................................

Na Mwandishi wetu.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini amesema Wizara itashughulikia askari wanaochafua Jeshi la Polisi kwa kupitia Tume ya Utumishi wa Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uokoaji na Uhamiaji, ili kurejesha imani ya wananchi kwenye Vyombo vinavyosimamia Ulinzi na Usalama wa mali zao.

Amesema kuwa Tume hiyo ni chombo kinachosimamia nidhamu za watumishi wa Vyombo hivyo na kwamba Mwenyekiti wa Tume hiyo ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni na Makamu wake ni yeye, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi hivyo watashugulikia kikamilifu maelekezo aliyoyatoa Rais Samia.

“Kuna maelekezo Mheshimiwa umeyatoa, mimi na Waziri Masauni tutayasimamaia kikamilifu. Ipo Tume ya Utumishi wa Jeshi Polisi, Magereza, Uhamiaji na Zimamoto na Uokoaji, chombo hiki ndio kinasimamia nidhamu za watumishi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama.”

Naibu Waziri Sagini amezungumza hayo leo mbele ya mamia ya wananchi wa Mara, baada ya kupewa nafasi ya kuongea na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano wa Hadhara uliofanyika Hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Kata ya Kwangwa, Musoma Mjini, Mkoani Mara.

Aidha Naibu Waziri Sagini amewataka Watanzania kutii sheria na kujiepusha na vitendo vya uhalifu vitakavyowapelekea kuwa wateja wa Vyombo vya Dola. Amesema kwamba Vyombo hivyo vinasimamia Sheria na utekelezaji wa Sheria na endapo mwananchi atakiuka sheria za Nchi basi lazima sheria itachukuliwa.

“Niwaombe wananchi hivi ni vyombo vya dola, Sisi tusingependa vyombo hivi vipambane na raia. Usipokuwa, raia atakaye kikuka sheria, raia atakayetenda vitendo vya uahalifu, atakaye mnyima mwenzake amani atakuwa tuu mteja wa Polisi, na baadae Mahakama, mwishowe Magereza”
Share:

BUNDI ATUA KANISANI..AIMBA KWAYA KWA MARINGO KAMA BINADAMU, TAZAMA HAPA


Video maridadi inayomuonyesha Ndege aina ya bundi,akiwatumbuiza waumini kanisani katika taifa la Jamhuri ya Dominika imewachangamsha wengi.

Bundi huyo  aliwaacha waumini vinywa wazi pamoja na wanamtandao baada ya kuonekana kanisani wakati wa ibada.

Huku wanakwaya hao wakiwatumbuiza waumini na nyimbo tamu, bundi huyo anaonyeshwa akiwa katika paa la kanisa akisakata densi kama inavyoonyeshwa kwenye video iliyopakiwa na @nowthisnews kwenye Instagram.

"Bundi huyu anaonekana kuwa na wakati mzuri wa kucheza muziki wa injili katika kanisa moja la Jamhuri ya Dominika," video hiyo ilinukuu.

Waumini wa kanisa hilo katika Jamhuri ya Dominika, walisema bundi huyo alicheza nyimbo hizo zote kwa saa moja.


Kwa mshangao wa wengi, bundi huyo alionekana kufurahishwa na wimbo wa wanakwaya waliokuwa wakiwatumbuiza waumini

Huku baadhi ya wanamtandao wakihusisha ndege huyo na uchawi, wengine walisema kuwa wimbo wa kwaya ulikuwa wa kupendeza na kuwaondolea ndege 'bahati mbaya'

@kitschykatz: "Inapendeza sana, siwezi! Mungu ni mzuri sana! Na kiumbe huyu ananitoa machozi!"

@dai_dreaming_ : "Huyo ni mtu ambaye amefariki hivi karibuni na anawatembelea tu!"

@joanflakes "Walifikiri ni mchawi (imani iliyozoeleka katika nchi za Amerika Kusini)."

@myartisindie: "Ndio, ningekuwa nikifanya vivyo hivyo, mara tu baada ya kisanduku cha mpigo kuwashwa."

@callmemisterj: "Bila shaka bundi alikuwa. Mungu, Wadominika na Jamhuri ya Dominika wote ni wa ajabu."

@mrckly: "Nilifikiri walisema ni mchawi na walikuwa wakijaribu kuitisha, lol." abn_ghozt210: Ninaiona kuwa ya kupendeza, lakini katika Amerika ya Kusini na Mexico hii inaweza kuwa roho au ishara mbaya."
Share:

PASTA ALA SUPU NA KUWAPA WAUMINI KIDOLE CHAKE WAKILAMBE KAMA KOMUNYO

Video ya pasta mmoja akiwapa kondoo wake kidole chake walambe kama komunyo imezua ghadhabu kwenye mitandao ya kijamii.

Pasta huyo alikuwa akiwalambisha waumini kidole chake baada ya kula chakula aina ya eba na supu kwenye madhabahu.

 Eba ni chakula kikuu kinacholiwa sana katika ukanda wa Afrika Magharibi, hususan nchini Nigeria na Ghana.

Katika video hiyo, mtumishi huyo wa Mungu anaonyeshwa akichukuwa chakula hicho kutoka kwa mhudumu wa wageni kwenye upande wake kushoto.

 Kisha anaweka kidole kichafu ndani ya mdomo wa muumini mmoja kama komunyo na kukiosha katika beseni iliyokuwa imeshikiliwa na mwanamke mwingine katika upande wa kulia.

Mchungaji huyo mwenye utata alirudia utaratibu huo kwa washarika wote walipokuwa wakienda madhabahuni mmoja baada ya mwingine kupokea 'meza ya Bwana.' 

Si mara ya kwanza pasta huyo kugonga vichwa vya habari na matukio tatanishi anayowafanyia kondoo wake. 

Hivi majuzi alinaswa kwenye video akiwaogesha waumini wa kike kanisani.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU FEBRUARI 7,2022



Rais Samia aagiza mikataba kufutwa kwa wakandarasi walioshindwa kukamilisha ujenzi wa barabara
Share:

RC HAPI CHUPUCHUPU KUFYATULIWA...RAIS SAMIA AGEUKA MBOGO VIONGOZI WOTE WA MARA MTEGONI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipata maelezo kutoka kwa Daktari wa Kitengo cha Magonjwa ya Figo katika Hospitali ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Mkoani Mara Dkt. Ridhiwani Said kuhusu maendeleo ya utoaji wa huduma, wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Hospitali hiyo iliopo katika Kijiji cha Kwangwa Halmashauri ya Manispa ya Musoma Mjini Mkoani Mara leo tarehe 06 Februari, 2022, Mhe. Rais Samia yupo katika ziara ya Kikazi ya siku nne Mkoani Mara kutembelea kukagua Miradi mbalimbali ya maendeleo ya Wananchi.
****


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Mara Ally Hapi, Wakuu wa wilaya na Wakurugenzi wa halmashauri za mkoa wa Mara wajitathmini kama wanafaa kuendelea na nyadhifa zao huku akiagiza watu wote waliohusika na ujenzi wa mradi wa makao makuu ya halmashauri ya wilaya ya Bunda vijijini kukaa pembeni kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazowakabili ikiwemo rushwa hali iliyosababisha kukwama kwa mradi huo.


Rais Samia ametoa maagizo hayo mjini Musoma leo Jumapili Februari 6, 2022 baada kupokea taarifa mbalimbali juu ya kukwama kwa miradi ya maendeleo mkoa wa Mara akisema inasikitisha kuona miradi mingi ya maendeleo inashindwa kukamilika kwa wakati huku kukiwa na uongozi kuanzia ngazi ya mkoa hadi wilaya.


"Mkuu wa mkoa ni kama uliota maana leo nilikuwa nimepanga nikufyatue hapa hapa bahati yako umeeleza matatizo haya ya kukwama kwa maendeleo ina maana unafanya kazi na matatizo haya unayajua na umenoyesha umechukua hatua gani una bahati", amesema Rais Samia.


Amesema matatizo ya kukwama kwa maendeleo ya mkoa wa Mara yanasababishwa na viongozi waliopo ambao amedai kuwa ni wabinafsi na wabadhirifu hivyo kuwataka viongozi hao kujitathmini na kwamba suala la utendaji kazi wa viongozi hao anakwenda kulifanyia kazi na maamuzi atayatoa baada ya watu wake kufanya uchunguzi.

Share:

Sunday, 6 February 2022

KAMPUNI YA BETWAY YAZINDUA PROGRAMU YA MABORESHO YA VIWANJA VYA MICHEZO TANZANIA

Kampuni ya michezo ya kubashiri ya kimataifa, Betway Tanzania imezindua rasmi programu yake ya maboresho ya viwanja vya michezo. Programu hiyo ambayo ni sehemu ya kampuni hiyo kurudisha kwa jamii inalenga kuchangia katika juhudi za maendeleo ya sekta ya michezo nchini. Katika kutekeleza azma yake ya kuendeleza sekta ya michezo nchini Tanzania, kampuni ya Betway imeahidi kufanya mambo kadhaa ikiwemo kuchangia moja kwa moja katika maboresho ya miundombinu ya michezo, kuchangia vifaa na zana muhimu za michezo na kudhamini shughuli mbalimbali za michezo.


Kupitia programu hii ya maboresho ya viwanja vya michezo, Betway imepanga kuanza na viwanja vitano vya jijini Dar es Salaam. Kiwanja cha mchezo wa mpira wa kikapu wa Sea View kilichopo Ocean Road, Ilala, Dar es Salaam ni kiwanja cha kwanza kufanyiwa maboresho. Kiwanja hicho ambacho ni moja ya viwanja vyenye historia kubwa katika mchezo wa mpira wa kikapu jijini Dar es Salaam na nchini Tanzania kwa ujumla kimefanyiwa maboresho makubwa yaliyohitajika kukirudisha katika hadhi ya viwanja vya mpira wa kikapu kitaifa.


Uzinduzi wa programu hiyo umeenda sambamba na bonanza la uzinduzi wa kiwanja cha michezo wa mpira wa kikapu cha Sea View ambacho ni kiwanja cha kwanza kufanyia maboresho. Katika uzinduzi huo wadau mbalimbali wa mchezo wa kikapu wamejumuika kwa kushindana na kuburudika huku wakifurahia mandhari mapya ya uwanja huo.


Akizungumza na wadau walioshiriki hafla ya uzinduzi na makabidhiano ya kiwanja cha Sea View iliyofanyika Februari 5, 2022 jijini Dar es Salaam, Afisa Uendeshaji wa Betway Tanzania, Jimmy Masaoe ametaja maboresho yaliyofanyika katika kiwanja hicho ambacho ni sehemu ya kituo cha michezo cha Gymkhana.


“Kama sehemu ya kuimarisha miundombinu ya michezo na kuwafanya watanzania kuipenda na kufurahia michezo tumefanya maboresho makubwa ya uwanja huu ikiwemo maboresho ya majukwaa, eneo la kuchezea, magoli, na taa kwa ajili ya matumizi ya usiku. Maboresho haya yataongeza hadhi ya uwanja huu wenye historia kubwa katika mchezo wa mpira wa kikapu lakini pia utavutia wachezaji wengi wa mpira wa kikapu kufanya mazoezi na kufanya mashindano.” Alisema Masaoe.


Akifafanua kuhusu muendelezo wa program hiyo, Masaoe aliweka wazi kuwa uzinduzi wa maboresho hayo ni mwanzo wa utekelezaji wa awamu ya kwanza ya maboresho ambayo inatarajiwa kuendelea katika mikoa mingine ya Tanzania.

“Uzinduzi wa leo ni mwanzo wa utekelezaji wa awamu ya kwanza ya maboresho ya viwanja vitano katika jiji la Dar es Salaam. Maboresho hayo yamelenga viwanja ambavyo vina matumizi makubwa katika mchezo husika ili kutoa nafasi kwa wanamichezo na mamlaka kuwa na miundombinu yenye hadhi ya kuendesha shughuli za michezo. Tunawasihi wanamichezo na mamlaka za usimamizi kusimamia vyema miundombinu hii ili iweze kuleta tija inayotarajiwa kwenye michezo kwa muda mrefu.” Alisisitiza Masaoe.

Kwa upande wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Katibu Mkuu wa shirikisho hilo, Mwenze Fiston ametoa shukurani kwa kampuni ya Betway kwa kuja na programu ya maboresho ya uwanja ambayo imeifaidisha tasnia ya mchezo wa mpira wa kikapu. Fiston aliongeza kwamba wataendelea kuhirikiana na Betway na wadau wengine kukuza mchezo wa mpira wa kikapu nchini Tanzania ili kuongeza ajira kwa watanzania wengi zaidi kupitia mchezo huo.

“Ni furaha kubwa kwetu kuona Betway ambayo ni kampuni kubwa ya michezo duniani imeona na kutambua umuhimu wa mchezo wa mpira wa kikapu hapa nchini na kuamua kuelekeza nguvu katika kuboresha miundombinu ya michezo hiyo. Tumepokea kwa furaha sana program hii na tunaamini haitashia hapa bali itaendelea na mikoa mingine. TBF tunawaahidi kushirikiana na mamlaka nyingine kama Shirikisho la Mpira wa Kikapu jijini Dar es Salaam na Serikali katika kutunza miundombinu ambayo imeboreshwa na Betway ili iweze kusaidia michezo kwa muda mrefu zaidi". Alisema Fiston.


Katika bonanza la uzinduzi michezo mitatu ilichezwa ikiwemo mchezo wa maveterani wa wa mpira wa kikapu wa jiji la Dar es Salaam, mchezo kati ya Dream Team na Dar City kwa upande wa wanawake huku Dar es Salaam All Stars wakichuana na Pwani All Stars kwa upande wa wanaume. Wachezaji na mashabiki wa mpira wa kikapu wameonesha furaha yao kufuatia maboresho ya uwanja huo.
Share:

STANSLAUS NYONGO AJITOSA KUWANIA KITI CHA NAIBU SPIKA


Mbunge wa Maswa Mashariki Stanslaus Nyongo akionesha kwa Waandishi wa habari (hawapo pichani) fomu ya kuomba ridhaa kuwania kiti cha Naibu Spika ambapo ameahidi kuwa iwapo atachaguliwa atakuwa kiongozi mwema.

 Na Dotto Kwilasa Malunde 1 blog - DODOMA.

Mbunge wa Maswa Mashariki, Stanslaus Nyongo amefika Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) jijini Dodoma, kwa ajili ya kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea nafasi ya Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akiongea leo Februari 6,2022 na Waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu amesema amefikia uamuzi huo kwa kuwa ana sifa nyingi za ziada zinazomtambulisha kwenye masuala ya uongozi.

"Natambua kuwa naweza kuongoza nafasi hii,mbali na ubunge nina sifa nyingi za ziada zinazonifanya nishawishike kuchukua fomu kutetea nafas hii ,"amesema.

Mbunge huyo wa Maswa Mashariki ametumia nafasi hiyo kuwaomba viongozi wake wa Chama kumuamini na kwamba ana matarajio makubwa katika kuwatumikia wananchi na Serikali.

"Endapo nitaipata nafasi hii,nitaitumia vizuri kuishauri Serikali ili kuleta manufaa kwa wananchi,tunatambua kuwa wananchi wa pembezoni wanahitaji Bunge liishauri vizuri Serikali ili wapate kuboreshewa huduma zote za msingi na kuwa na unafuu wa maisha mazuri,"amefafanua Mbunge huyo.


Mbali na kuwa mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki, Nyongo amewahi kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi ikiwa ni pamoja na Naibu Waziri wa madini kwa Serikali ya awamu ya tano na Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma na maendeleo ya jamii anayoitumikia hadi sasa.
Mbunge wa Maswa mashariki Stanslaus Nyongo akisaini kitabu cha wageni alipowasili Ofisi ya Itikadi na Oganaizesheni ya CCM Jijini Dodoma.

Mbunge wa Maswa Mashariki Stanslaus Nyongo akiongea na Waandishi wa habari Jijini Dodoma mara baada ya kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuwania kiti cha Naibu Spika wa Bunge.
Share:

BENKI YA EXIM, MASTERCARD ZAINGIA MAKUBALIANO KUBORESHA MALIPO YA KIDIJITALI



Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim, Bw Jaffari Matundu (Kulia walioketi) na Rais wa Mastercard Kanda ya Africa, Kusini mwa Jangwa la Sahara Bw. Mark Elliot (Kushoto walioketi) wakitia saini makubaliano ya ushirikiano wa miaka 5 ili kuendeleza ubunifu kupitia njia ya malipo ya kidijitali nchini ikiwa pia ni jitihada za benki hiyo za kutoa ufumbuzi wa hali ya juu wa kibenki kwa wateja wake ili kwenda sambamba na mabadiliko ya haraka ambayo sekta ya huduma za kifedha inashuhudia.

 Hafla ya utiaji saini huo ilifanyika Makao Makuu ya Benki ya Exim jijini Dar es Salaam hivi karibuni ikishuhdiwa na wawakilishi kutoka pande zote mbili.
Share:

TMA YATOA ANGALIZO LA MVUA KUBWA NA UPEPO MKALI




Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo kwa wananchi juu ya hali ya hewa katika siku kadhaa zijazo.

ANGALIZO la mvua kubwa limetolewa kwa maeneo machache ya mikoa ya Morogoro, Iringa, Njombe, Songwe, Mbeya, Ruvuma Lindi na Mtwara.
UWEZEKANO WA KUTOKEA: WASTANI.


KIWANGO CHA ATHARI ZINAZOWEZA KUTOKEA: WASTANI.

JUMATATU 07-02-2022

ANGALIZO la mvua kubwa limetolewa kwa maeneo machache ya mikoa ya Dodoma, Morogoro, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Songwe, Mbeya, Iringa, Njombe, Rukwa, Ruvuma Lindi na Mtwara.

ANGALIZO la upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita 2.0 limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani ya bahari ya Hindi mikoa ya Lindi, Mtwara, Tanga, Dar es Salaam na Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia) pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

UWEZEKANO WA KUTOKEA: WASTANI.
KIWANGO CHA ATHARI ZINAZOWEZA KUTOKEA: WASTANI.

JUMANNE 08-02-2022

ANGALIZO la mvua kubwa limetolewa kwa maeneo machache ya mikoa ya Morogoro, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Songwe, Mbeya, Iringa, Njombe, Rukwa, Ruvuma, Lindi na Mtwara.



ANGALIZO la upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita 2.0 limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani ya bahari ya Hindi mikoa ya Lindi, Mtwara, Tanga, Dar es Salaam na Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia) pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
UWEZEKANO WA KUTOKEA: WASTANI.
KIWANGO CHA ATHARI ZINAZOWEZA KUTOKEA: WASTANI.



JUMATANO 09-02-2022
ANGALIZO la upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita 2.0 limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani ya bahari ya Hindi (mikoa ya Lindi, Mtwara, Tanga, Dar es Salaam na Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia) pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba).
UWEZEKANO WA KUTOKEA: WASTANI.

Utabiri huu umetolewa,
Na, MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
Share:

MHE. RAIS SAMIA ATEMBELEA HOSPITALI YA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE MKOANI MARA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitembelea Hospitali ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Mkoani Mara kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Hospitali hiyo iliopo katika Kijiji cha Kwangwa Halmashauri ya Manispa ya Musoma Mjini leo tarehe 06 Februari, 2022, Mhe. Rais Samia yupo katika ziara ya Kikazi ya siku nne Mkoani Mara kutembelea kukagua Miradi mbalimbali ya maendeleo ya Wananchi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipata maelezo kutoka kwa Daktari wa Kitengo cha Magonjwa ya Figo katika Hospitali ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Mkoani Mara Dkt. Ridhiwani Said kuhusu maendeleo ya utoaji wa huduma, wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Hospitali hiyo iliopo katika Kijiji cha Kwangwa Halmashauri ya Manispa ya Musoma Mjini Mkoani Mara leo tarehe 06 Februari, 2022, Mhe. Rais Samia yupo katika ziara ya Kikazi ya siku nne Mkoani Mara kutembelea kukagua Miradi mbalimbali ya maendeleo ya Wananchi.

Share:

MCHENGERWA-WIZARA IMETEKELEZA AGIZO LA WAZIRI MKUU LA KUTENGA SHULE 56 ZA MICHEZO.


******************************

Na. John Mapepele

Serikali tayari imetenga shule 56 za michezo nchi nzima ili kuibua na kukuza vipaji vya michezo kwa watoto nchi nzima.

Kauli hii imetolewa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa Februari 4, 2022 katika ubalozi wa China jijini Dar es Salaam kwenye siku ya mwaka mpya wa Taifa hilo na siku ya uzinduzi wa mashindano ya mwaka 2022 ya Olympiki ya Beijing ya majira ya baridi.

Utengaji wa shule hizo pia ni utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa wakati akifungua Mashindano ya Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi (UMITASHUMTA) na Sekondari (UMISSETA) kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara Juni 8, 2021 ambapo alielekeza Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na mambo mengine isimamie utengaji wa shule maalum za Michezo nchi nzima.

Aidha, Mhe. Mchengerwa amefafanua kwamba kutenga kwa shule hizo za michezo nchi nzima ni utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi Chama cha Mapinduzi (CCM) unaoitaka Serikali kuibua vipaji vya watoto ili kupata wanamichezo bora na kuimarisha michezo kwa ujumla.

Aidha, amesema hadi sasa Wizara yake kwa kushirikiana na Wizara ya TAMISEMI na Wizara yenye dhamana ya Elimu zimesha ainisha shule hizo kwa ajili ya maboresho mbalimbali ya miundombinu ya michezo.

Ameongeza kuwa Wizara yake itahakikisha inasimamia zoezi hili kikamilifu ili kuleta Mapinduzi makubwa kwenye michezo.

Amemwomba Balozi wa China nchini Chen kuiomba Serikali yake kusaidia uboreshaji wa miundombinu ya michezo ya shule hizo ili Ilani ya CCM ambayo inaendana na ile ya Chama cha CPC cha nchini China iweze kutekelezwa.
Share:

Saturday, 5 February 2022

MAKAMU WA RAIS KUZINDUA SERA YA TAIFA YA MAZINGIRA JIJINI DODOMA



Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Februari 5,2022 kuhusu Uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Mazingira ya Mwaka 2021 unaotarajiwa kufanyika Februari 12, 2022 Jijini Dodoma.


Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Mazingira ya Mwaka 2021 unaotarajiwa kufanyika Februari 12, 2022 Jijini Dodoma. Wengine kulia ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Bw. Edward Nyamanga, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) na Mkurugenzi wa Mazingira Dkt. Andrew Komba.

..................................................................

Na.Alex Sonna,DODOMA

Makamu wa Rais Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Mazingira ya Mwaka 2021 inayotarijiwa kuzinduliwa 12 Februari, 2022 Jijini Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo Februari 5,2022 Jijini Dodoma ,Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga amesema Sera ya Taifa ya Mazingira ya Mwaka 2021 imejumuisha masuala ya mazingira yaliyokuwemo katika Sera ya 1997 na masuala mapya.

Ameyataja masuala mapya katika Sera mpya ya mwaka 2021 ni pamoja na: Udhibiti wa taka za kielektroniki, Usimamizi na matumizi ya kemikali, na Udhibiti wa uchafuzi katika shughuli za utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi.

Bi.Maganga amesema kuwa masuala mengine ni pamoja na Mabadiliko ya tabianchi; Usimamizi wa matumizi salama ya bioteknolojia ya kisasa; na Udhibiti wa viumbe vamizi.

“Sera ya Taifa ya Mazingira ya Mwaka 2021 imeongeza wigo wa masuala na changamoto za mazingira zinazopaswa kufanyiwa kazi katika kipindi husika ili kuleta maendeleo endelevu na imezingatia changamoto mpya za kimazingira zinazoendelea kujitokeza kutokana na mabadiliko ya mifumo ya kiuchumi, kijamii na kimazingira yanayoendelea duniani” ameeleza Bi.Maganga.

Amesema kuwa, Serikali imeamua kuwa na Wiki ya Uzinduzi wa Sera itakayoanza tarehe 07-12/02/2022 ambayo itaambatana na shughuli mbalimbali za hifadhi ya mazingira ikiwa ni sehemu ya masuala ya msingi yanayoelekezwa katika Sera mpya.

Bi. Maganga amezitaja shughuli zitakazofanyika katika wiki hiyo kuwa ni Upandaji miti Jijini Dodoma katika maeneo ya Medeli, Iyumbu, Iseni na maeneo ya barabara inayoanzia Chimwaga, Chuo Kikuu cha Dodoma kuelekea barabara ya Dodoma Dar es Salaam.

Aidha,amesema kuwa watanya usafi pembezoni mwa barabara inayoanzia Shule ya Martin Luther hadi Wajenzi kupitia Nzuguni, Ilazo, Ipagala na Area C; Kutoa elimu kuhusu utenganishaji wa taka, kufanya Usafi katika soko la Changombe pamoja na Utoaji wa Elimu ya Mazingira kwa wananchi na wadau kupita vyombo vya habari.

Dhumuni la kuwepo kwa shughuli hizo ni kurejesha hali ya asili ya mazingira iliyoharibika kutokana na shughuli za kibinadamu kwa kuwa na zoezi la upandaji miti, kuboresha afya ya jamii na elimu ya utenganishaji taka kwa ajili ya udhibiti wa taka ngumu na kuwezesha urejelezaji wa taka kwenye bidhaa na huduma mbalimbali.
Share:

MV KAZI YAENDELEEA KUFANYA KAZI BAADA YA KUPATA HITILAFU

Wananchi wakishuka kutoka katika kivuko cha MV Kazi ambacho kilileta hitilafu hivi karibuni. Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Lazaro Kilahala (katikati) akimsikiliza Mhandisi wa Tehama Magogoni feli Jijini Dar es Salaam Bw.Omary Mayila mara baada ya kutembelea na kuangalia maendeleo ya kivuko cha MV Kazi ambacho kilileta hitilafu hivi karibuni. Wa kwanza kushoto ni Kaimu Mkuu wa Kivuko Magogoni Feli Mhandisi Jamal Waziri.Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Lazaro Kilahala (kulia) akizungumza na fundi wa vivuko magogoni Feli Bw.Benard Kaluse mara baada ya kutembelea na kuangalia maendeleo ya kivuko cha MV Kazi ambacho kilileta hitilafu hivi karibuni.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

*************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Lazaro Kilahala ametembelea na kuangalia maendeleo ya Kivuko cha MV Kazi ambacho kilileta hitilafu kwa siku nzima ya tarehe 04/02/2022.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuona maendeleo ya Kivuko hicho Bw.Kilahala amesema kulitokea hitilafu ya msuguano chini na kuonekana kuingiza maji kwenye kivuko hivyo wakaamua kukisitisha kufanya kazi kwa usalama zaidi na kukifanyia marekebisho.

Aidha Bw.Kilahala amesema tayari kivuko hicho kimeshatengenezwa na kimerudi kuendelea kutoa huduma hivyo amewaomba radhi wananchi kwa usumbufu uliojitokeza kwa siku hiyo.

"TEMESA tumejipanga kuhakikisha wakati wote matengenezo yanafanyika katika vivuko vyote nchini, tuna mafundi wakutosha pia kuna kikosi maalumu cha kuhudumia vivuko hivi". Amesema Bw.Kilahala.

Amesema Serikali imeshatenga fedha za kutosha kuhakikisha vivuko vyote vinafanyiwa matengenezo makubwa na kwa wakati na hivi karibuni kivuko cha MV Kazi kitafanyiwa marekebisho makubwa kuhakikisha hakitaleta usumbufu katika utoaji huduma.

Pamoja na hayo amesema ununuzi wa kivuko cha nne tayari umeshaingia kwenye bajeti ya mwakani kwahiyo kuanzia mwezi Julai wataanza kutengeneza kivuko hicho, hivyo changamoto zitokanazo na vivuko hivyo utaenda kupungua kwa kiasi kikubwa pale watakapoongeza kivuko cha nne.

Kwa upande wa abiria wanaotumia vivuko hivyo wameipongeza Serikali kundelea kuwajari wananchi hasa wanaovuka katika vivuko vilivyopo feli magogoni kwani pindi vivuko vikiwa na hitilafu kidogo mara nyingi hufanya jitihada za haraka kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya vivuko kwa haraka na kwa wakati.

Share:

MGANGA WA JADI AKAMATWA TUHUMA ZA KUUA WATEJA WAKE WAWILI WALIOKUWA WANASAKA UTAJIRI


WATU wawili, Suzana Mtitu (38) na Kassim Kitamkanga (35) wakazi Makambako Mkoani Njombe wamekutwa wamefariki katika msitu wa Tanwat uliopo Njombe huku uchunguzi ukibainisha kuwa wameuawa na mganga wa Jadi baada ya watu hao waliokuwa wateja wake kubaini kwamba dawa za kuwa matajiri walizopewa hazijafanya kazi.

RPC wa Njombe, Hamis Issah amesema Jeshi la Polisi linamshikilia Mganga huyo wa kienyeji, Joseph Mgunda (41) Mkazi wa Sovi Kata ya Mtwango Wilayani Njombe kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo.

“Watu wengi wafanyabiashara huyu Mganga anawaambia ukipeleka hela anaziombea, baadaye zinaongezeka, sintofahamu iliyotokea kwa hawa watu wawili walipewa dawa tayari lakini wakaona matokeo hayaleti mafanikio wakaenda kumuuliza mganga mbona umetupa dawa ambayo haisaidii, Mganga huyo alishikwa na hofu na kushauriwa na ndugu zake kutekeleza mauaji hayo.

“Ndugu zake wakamwambia ukitaka usipate shida waue hawa watu na kweli watu watatu na yeye mwenyewe Mganga akiwa ni wanne wakatekeleza mauaji, mwanaume alikatwa mapanga sehemu za shavuni upande wa kulia na kushoto na kichwani na pia kapigwa rungu na kudondoka na mwanamke alipigwa rungu moja tu na kudondoka chini.

Kamanda Issah amesema watu wengine wanaoshikiliwa kwa tuhuma za mauaji hayo ni Andrew Vahuruka, Gadi Mwanzalila (36) na Kelvin Kilinge (29), Kamanda Issah ametoa wito kwa wananchi kutafuta pesa kwa juhudi za kufanya kazi na sio kutafuta utajiri kwa Waganga kwa kuwa hakuna utajiri unaoletwa na Waganga.
Share:

MKE WANGU ALINITALIKI KWA KUWA NILIKUWA NA UUME MDOGO

 
Ni makadirio ya kila mtu anayeingia katika uhusiano wa kimapenzi kupitia ndoa kuwa mwenzake watakaye ishi naye maishani mwao yote ataweza kumweka sawa na nyakati zao maisha yao yaweze kujawa na furaha yakuwa bibi na bwana.

 Kwangu miye haya yote yamesalia kuwa ndoto kwani ni siku chache zilizopita ambapo mke wangu kwa jina la Halima aliweza kunipa talaka kwa misingi kwamba uume wangu ulikuwa mdogo usioweza kutosheleza mahitaji yake ya kingono, Kabla ya talaka hiyo Halima alikuwa amenifikisha mahakamani na kunishtaki kuwa miye kama mumewe sikuweza kuyatosheleza mahitaji yake ya kimwili kwani ni kinyume na sheria za nchi waja walio kwenye ndoa kutotimiza mahitaji ya kingono ya mwenzie.

Nilipigwa faini baadaye aliweza kuniomba msamaha kwa jambo hilo na nikaweza kumsamehe kwani nilimchukua kama mpenzi wangu wa dhati niliyemthamini kwa kiwango kikubwa saana. 

Uhusiano wangu na Halima ulianza kuchukua mkondo tofauti pale, alipoanza kujitenga nami, japo tuliishi kwenye nyumba moja, hakuwa anaambilika wala kusemezeka, kwa wakati mwingi angependelea kujikalisha peke yake na kukataa kuzungumza nami, alikosa kunipa wakati aliokuwa ananipa hapo nyuma.

 Nikikumbuka Halima alikuwa mwanamke mwenye mapenzi ya dhati na mara kwa mara angeweza kunipigia simu kutaka kujua nilipokua na ikiwa nilikua salama.

Kwa wiki mbili hivi kabla ya kunitalaki hayo yote hayakufanyika, alinyamaza midhili ya maji kwenye mtungi, na kufanya mambo yake kivyake, Siku moja nilimuuliza mbona alisaliti ahadi aliyonipa mbele ya umati wa watu na viongozi wa kanisa siku ile tulifunga ndoa, nikikumbuka vyema Halima aliweza kutoa ahadi mbele ya umati wa watu na kunena kwamba alinipenda kwa udi na uvumba na angeweza kukaa nani maishani mwake wote.

 Pia kabla ya kuona naye kila wakati aliweza kuniarifu kila wakati angependa kuniweka kwenye furaha, na angekosa furaha ikiwa mie pia ningeikosa hiyo furaha. 

Vipi sasa anafanya kinyume na matarajio, nilishidwa mbona aliamua kuyafanya kinyume na mataraji, hayo siyezi yasema bali mwenyewe aliyafahamu. Jibu nilililipata kutoka kwake sijawai lisahau kufikia wa leo kwani alinena kutoka kinywani mwake kuwa mie ni gumegume asiyejua cha kufanya kitandani, na sikuweza kumtimizia mahitaji yake ya kimwili na siku moja angetoka nje ya ndoa na kuweza kumtafuta mume mwingine atakayeweza kuyafanya.

 Jambo hilo lilinikwaza moyoni, nilijaribu kudhibiti nisije nikamfukuza kutoka kwangu kwani nilikuwa ninampenda kama chanda na pete na yeye kukosa maishani mwangu lingekuwa jambo baya sana, nilijua siku moja angeweza kubadilika na kuweza kuniomba msamaha kwa yote aliyoyasema mabaya kwangu.

 Kabla ya ndoa yetu hatukuwai kuweza kujaribu kufanya tendo la ndoa kwani tulilelewa kanisani na kuamini ya kua kuyafanya mapenzi nje ya ndoa ilikua ni laana kubwa kutoka kwa mwenyezi mungu, kulingana na itikadi za ki kristo, Angalau tungalifanya mapenzi mapema kabla ya kuona hatungalifikishana tulipofikishana angaliniondokea, na kwenda kuwataftua waume ambao yeye mwenyewe aliwataka, wanaume wenye mipini kubwa kubwa.

 Jinsi siku zilienda kusonga ndipo tabia zake zilivyozidi kudorora, kwa wakati mwingi Halima alirejea nyumbani akiwa mlevi chakari, asiyeweza kuambilika, nilimkubalia kuingia chumbani bila ya kumuuliza alikotoka masaa hayo.

Aliniacha kwa mafikira chungu nzima nisijue la kufanya, Iwapo jambo mbaya lingemtendekea huko nje, miye ndiye niengelaumiwa kwa kuwa mwanaume anapaswa kumlinda mkewe kila wakati, Nilichoshwa na tabia hizo na nikaamua kumuuliza alikotoka usiku na nani na kwa nini, hapo ndipo aliponieleza alikuwa na mume aliyeelewa cha kufanya, na kuwa amenipa talaka kuenda kwa mume atakaye mtimizia mahitaji yake ya kimwili.

 Nilijaribu kumrai asiondoke kuniacha lakini alidinda, niliachwa na Huzuni mkuu wa kuachwa na kipenzi changu.

 Siku moja moja rafiki yangu alinitembelea na kugundua nilivyokua nisiye na furaha aliuliza kinachoendelea maishani mwangu, hapo ndipo nilifunguka na kumweleza kila kitu, alinionea huruma na kuniliwaza, alinirai nisiwe na Uzuni kwani alikua na suluhu kwa jambo hilo hapo ndipo alinipa nambari ya daktari wa kiasili Daktari kiwanga nikiyempigia simu na kumweleza yote.

 Aliniarifu nisiwe na tashwishi kwani niligonga ndipo alinialika na kunipa dawa aliyoongeza uume wangu ukawa sawa. Pia aliweza kufanya ganga ganga zake na siku chache baadaye mke wangu aliweza kurudi kwangu. Na kuniomba msamaha.

 Namshukuru daktari kiwanga kwa kuweza kulirejesha penzi langu lililokua limepotea. Daktari kiwanga pia Anaponya na kutibu magonjwa kama Kifua kikuu, Viongo vya mwili vilivyovunjika, saratani ya mapafu na mengine mengi , Pia anasuluhisha matatizo yakiwemo ya Kifamilia, Kushinda kesi, Kurejesha mali iliyoibwa na mengine mengi mtembelee leo upate suluhu, Waweza kumpata kupitia wavuti www.kiwangadoctors.com barua pepe kiwangadoctors@gmail.com au piga simu kwa nambari +254769404965.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger