Katibu Mkuu Ujenzi, Balozi Mhandisi Aisha Amour (Kushoto), akipokea zawadi ya maua wakati akiwasili katika ofisi za Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi zilizopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma
Katibu Mkuu Ujenzi, Balozi Mhandisi Aisha Amour akisalimiana na watumishi wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), mara baada ya kuwasili katika ofisi za wizara hiyo zilizopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dododma. Kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu Ujenzi, Ludovick Nduhiye.
Baadhi ya Viongozi wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi wakiwa wamejipanga kwa ajili ya kumpokea Katibu Mkuu Ujenzi, Balozi Mhandisi Aisha Amour (hayupo pichani), katika ofisi za wizara hiyo, zilizopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma. Kutoka kushoto ni Gabriel Migire - Katibu Mkuu Uchukuzi, Ludovick Nduhiye - Naibu Katibu Mkuu Ujenzi pamoja na Richard Mkumbo - Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango (Sekta Ujenzi).
Katibu Mkuu Ujenzi Balozi Mhandisi Aisha Amour akisaini kitabu cha wageni, mara baada ya kuwasili katika ofisi za Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi zilizopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Ujenzi, Ludovick Nduhiye (aliesimama), akizungumza jambo wakati wa kikao cha mapokezi na utambulisho baada ya kuwasili kwa Katibu Mkuu Ujenzi, Balozi Mhandisi Aisha Amour (aliyeketi kushoto kwa Naibu Katibu Mkuu Ujenzi), Katika ofisi za Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi zilizopo mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Baadhi ya Wajumbe wa Menejimenti ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Wakimsikiliza Katibu Mkuu Ujenzi, wakati wa kikao cha Mapokezi na Utambulisho, kilichofanyika leo katika ofisi za Wizara hiyo, zilizopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.


















Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Samuel Gwamaka akipanda mti katika eneo la hifadhi ya Pugu Kazimzumbwi lengo likiwa ni kuhamasisha jamii kupanda miti ili kukabiliana na hewa ukaa.
Kamanda wa Kanda ya Mashariki TFS, Kamishna Msaidizi Caroline Malundo akipanda mti katika eneo la hifadhi ya Pugu Kazimzumbwi lengo likiwa ni kuhamasisha jamii kupanda miti ili kukabiliana na hewa ukaa.
Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Seleman Jafo akizungumza katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya kisarawe kabla ya kutembelea Msitu wa Pugu Kazimzumbwi ulioko wilayani Kisarawe mkoa wa Pwani, kuona namna ambavyo Wakala wa huduma za Misitu Tanzania (TFS) ilivyojidhatiti kuendeleza msitu huo kama sehemu ya kuhifadhi mazingira.
Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Seleman Jafo akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Samuel Gwamaka katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe kabla ya kutembelea Msitu wa Pugu Kazimzumbwi ulioko wilayani Kisarawe mkoa wa Pwani, kuona namna ambavyo Wakala wa huduma za Misitu Tanzania (TFS) ilivyojidhatiti kuendeleza msitu huo kama sehemu ya kuhifadhi mazingira.