Saturday, 18 December 2021

HOTELI YA KISASA 'WITESHI PARADISE HOTEL' YAZINDULIWA MJINI SHINYANGA


Muonekano sehemu ya nje ya Witeshi Paradise Hotel

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Hoteli ya Kisasa ‘Witeshi Paradise Hotel’ imezinduliwa Mjini Shinyanga ikiwa imesheheni huduma mbalimbali ikiwemo malazi ,vyakula, vinywaji, kumbi za sherehe/harusi na mikutano, eneo la michezo kwa watoto, Car Parking n.k

Witeshi Paradise Hotel inapatikana Lubaga nyuma ya Ikulu ndogo Mjini Shinyanga jirani la Shule ya Msingi Lubaga na Agape Church Lubaga pembezoni mwa Barabara ya Old Shinyanga.

Uzinduzi huo umefanyika leo Jumamosi Desemba 18,2021 ukiambatana na Ibada ya kubariki na ufunguzi wa Witeshi Paradise Hotel iliyoongozwa na Paroko wa Parokia ya Moyo Safi wa Maria Shinyanga Mjini, Padre Anatoly Salawa huku wadau mbalimbali waliohudhuria wakipata kifungua kinywa ‘chai/supu’ bure hotelini hapo.

Wakurugenzi wa Witeshi Paradise Hotel, Damian Peter Shirima na Mercy Shirima wametumia fursa hiyo kuwakaribisha wananchi kutoka ndani na nje ya mkoa wa Shinyanga kupata huduma nzuri na bora katika hoteli hiyo kwa gharama nafuu kwani hoteli hiyo kwani lengo ni kumhudumia kila mwananchi.

Mawasiliano zaidi Witeshi Paradise Hotel piga simu namba +255 769 325 583 Email: witeshiparadisehotel@gmail.com
Muonekano sehemu ya nje ya Witeshi Paradise Hotel iliyopo Lubaga nyuma ya Ikulu ndogo Mjini Shinyanga jirani la Shule ya Msingi Lubaga na Agape Church Lubaga pembezoni mwa Barabara ya Old Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Muonekano sehemu ya nje ya Witeshi Paradise Hotel iliyopo Lubaga nyuma ya Ikulu ndogo Mjini Shinyanga.
Muonekano sehemu ya Witeshi Paradise Hotel iliyopo Lubaga nyuma ya Ikulu ndogo Mjini Shinyanga.
Muonekano sehemu ya nje Witeshi Paradise Hotel iliyopo Lubaga nyuma ya Ikulu ndogo Mjini Shinyanga.
Muonekano sehemu ya nje Witeshi Paradise Hotel iliyopo Lubaga nyuma ya Ikulu ndogo Mjini Shinyanga.
Moja ya masanamu ndani ya Witeshi Paradise Hotel iliyopo Lubaga nyuma ya Ikulu ndogo Mjini Shinyanga
Muonekano wa sehemu ya Witeshi Paradise Hotel iliyopo Lubaga Mjini Shinyanga.
Muonekano wa sehemu ya Witeshi Paradise Hotel iliyopo Lubaga Mjini Shinyanga.
Muonekano wa awali sehemu ya michezo ya watoto ndani ya  Witeshi Paradise Hotel iliyopo Lubaga Mjini Shinyanga.
Muonekano wa awali sehemu ya michezo ya watoto ndani ya  Witeshi Paradise Hotel iliyopo Lubaga Mjini Shinyanga.
Muonekano wa awali sehemu ya michezo ya watoto ndani ya  Witeshi Paradise Hotel iliyopo Lubaga Mjini Shinyanga.
Muonekano sehemu ya Witeshi Paradise Hotel iliyopo Lubaga nyuma ya Ikulu ndogo Mjini Shinyanga.
Muonekano sehemu ya Witeshi Paradise Hotel iliyopo Lubaga nyuma ya Ikulu ndogo Mjini Shinyanga.
Muonekano wa awali sehemu ya Bar/Lounge ndani ya Witeshi Paradise Hotel iliyopo Lubaga nyuma ya Ikulu ndogo Mjini Shinyanga.
Paroko wa Parokia ya Moyo Safi wa Maria Shinyanga Mjini, Padre Anatoly Salawa akikata utepe kuzindua Witeshi Paradise Hotel leo Jumamosi Desemba 18,2021.
Paroko wa Parokia ya Moyo Safi wa Maria Shinyanga Mjini, Padre Anatoly Salawa akibariki majengo ya Witeshi Paradise Hotel wakati wa uzinduzi wa hoteli hiyo.
Paroko wa Parokia ya Moyo Safi wa Maria Shinyanga Mjini, Padre Anatoly Salawa akibariki majengo ya Witeshi Paradise Hotel wakati wa uzinduzi wa hoteli hiyo.
Paroko wa Parokia ya Moyo Safi wa Maria Shinyanga Mjini, Padre Anatoly Salawa akibariki majengo ya Witeshi Paradise Hotel wakati wa uzinduzi wa hoteli hiyo.
Paroko wa Parokia ya Moyo Safi wa Maria Shinyanga Mjini, Padre Anatoly Salawa akibariki majengo ya Witeshi Paradise Hotel wakati wa uzinduzi wa hoteli hiyo.
Paroko wa Parokia ya Moyo Safi wa Maria Shinyanga Mjini, Padre Anatoly Salawa akibariki vyumba vya Witeshi Paradise Hotel wakati wa uzinduzi wa hoteli hiyo.
Paroko wa Parokia ya Moyo Safi wa Maria Shinyanga Mjini, Padre Anatoly Salawa akibariki ukumbi wa mikutano Witeshi Paradise Hotel wakati wa uzinduzi wa hoteli hiyo.
Paroko wa Parokia ya Moyo Safi wa Maria Shinyanga Mjini, Padre Anatoly Salawa akibariki vyumba vya Witeshi Paradise Hotel wakati wa uzinduzi wa hoteli hiyo.
Paroko wa Parokia ya Moyo Safi wa Maria Shinyanga Mjini, Padre Anatoly Salawa akibariki vyumba vya Witeshi Paradise Hotel wakati wa uzinduzi wa hoteli hiyo.
Paroko wa Parokia ya Moyo Safi wa Maria Shinyanga Mjini, Padre Anatoly Salawa akisaini kitabu cha wageni Witeshi Paradise Hotel wakati wa uzinduzi wa hoteli hiyo.
Paroko wa Parokia ya Moyo Safi wa Maria Shinyanga Mjini, Padre Anatoly Salawa akiongozana na Mkurugenzi wa Witeshi Paradise Hotel, Damian Peter Shirima (kulia) baada kubariki majengo ya Witeshi Paradise Hotel wakati wa uzinduzi wa hoteli hiyo.
Muonekano wa moja ya vyoo vya Witeshi Paradise Hotel
Muonekano wa moja ya vyumba vya Witeshi Paradise Hotel
Muonekano wa moja ya vyumba vya Witeshi Paradise Hotel
Muonekano wa moja ya vyumba vya Witeshi Paradise Hotel
Keki maalumu wakati wa uzinduzi wa Witeshi Paradise Hotel
Mtoto wa kwanza wa wamiliki wa Witeshi Paradise Hotel akiandaa Keki maalumu wakati Paroko wa Parokia ya Moyo Safi wa Maria Shinyanga Mjini, Padre Anatoly Salawa akijiandaa kuikata wakati wa uzinduzi wa Witeshi Paradise Hotel
Paroko wa Parokia ya Moyo Safi wa Maria Shinyanga Mjini, Padre Anatoly Salawa  (katikati) akijiandaa kukata keki wakati wa uzinduzi wa Witeshi Paradise Hotel
Paroko wa Parokia ya Moyo Safi wa Maria Shinyanga Mjini, Padre Anatoly Salawa  akikata keki wakati wa uzinduzi wa Witeshi Paradise Hotel
Paroko wa Parokia ya Moyo Safi wa Maria Shinyanga Mjini, Padre Anatoly Salawa  akikata keki wakati wa uzinduzi wa Witeshi Paradise Hotel
Mtoto wa mwisho wa wamiliki wa Witeshi Paradise Hotel akimlisha keki Paroko wa Parokia ya Moyo Safi wa Maria Shinyanga Mjini, Padre Anatoly Salawa wakati wa uzinduzi wa Witeshi Paradise Hotel
Paroko wa Parokia ya Moyo Safi wa Maria Shinyanga Mjini, Padre Anatoly Salawa akimlisha keki Mtoto wa mwisho wa wamiliki wa Witeshi Paradise Hotel
Wakurugenzi wa Witeshi Paradise Hotel, Damian Peter Shirima na Mercy Shirima wakilishana keki wakati wa uzinduzi  wa Witeshi Paradise Hotel.
Mtoto wa kwanza wa wamiliki wa Witeshi Paradise Hotel akijiandaa kufungua Shampeni
Wakurugenzi wa Witeshi Paradise Hotel, Damian Peter Shirima na Mercy Shirima wakigonga Cheers na Paroko wa Parokia ya Moyo Safi wa Maria Shinyanga Mjini, Padre Anatoly Salawa (kulia) wakati wa uzinduzi wa Witeshi Paradise Hotel
Furaha ikitawala wakati wa uzinduzi wa Witeshi Paradise Hotel
Paroko wa Parokia ya Moyo Safi wa Maria Shinyanga Mjini, Padre Anatoly Salawa akipata huduma ya supu wakati wa uzinduzi wa Witeshi Paradise Hotel
Wadau waliohudhuria uzinduzi wa Witeshi Paradise Hotel wakipaya huduma ya kifungua kinywa 'chai/supu' bure 
Wadau waliohudhuria uzinduzi wa Witeshi Paradise Hotel wakipaya huduma ya kifungua kinywa 'chai/supu' bure 
Wadau waliohudhuria uzinduzi wa Witeshi Paradise Hotel wakipaya huduma ya kifungua kinywa 'chai/supu' bure 
MC Mama Sabuni akizungumza wakati wa uzinduzi wa Witeshi Paradise Hotel 
Mkurugenzi wa Witeshi Paradise Hotel, Mercy Shirima akiwakaribisha wateja kupata huduma bora katika hoteli hiyo inayopatikana Lubaga nyuma ya Ikulu ndogo Mjini Shinyanga jirani la Shule ya Msingi Lubaga na Agape Church Lubaga pembezoni mwa Barabara ya Old Shinyanga.Mawasiliano zaidi Witeshi Paradise Hotel piga simu namba +255 769 325 583 Email: witeshiparadisehotel@gmail.com

Share:

WAZIRI MBARAWA: FIDIA ZITALIPWA BARABARA YA NYAMUSWA – BULAMBA

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, akifafanua jambo kwa mwananchi wa Wilaya ya Bunda wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Mara.

Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Joshua Nassari, akizungumza jambo mbele ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, wakati Waziri huyo alipowasili wilayani hapo kukagua ujenzi wa barabara ya Nyamuswa – Bulamba (km 56.4), mkoani Mara.
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Mara Mhandisi Vedastus Maribe, akimuonesha Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, hatua za ujenzi wa barabara Makutano – Sanzate (km 51) kwa kiwango cha lami, mkoani humo.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, akisalimiana na wananchi wa Wilaya ya Bunda wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Mara.Muonekano wa sehemu ya barabara ya Nyamuswa – Bulamba (km 56.4) inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Mara.Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, akimsikiliza mwananchi wa Wilaya ya Bunda wakati alipokuwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Mara.

Muonekano wa sehemu ya barabara ya Makutano – Sanzate (km 51), inayoendelea kujengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Mara. Ujenzi wa barabara hiyo umefikia asilimia 91.

PICHA NA WUU

…………………………………………………………..

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amewahakikishia wananchi wa Wilaya ya Bunda waliopisha ujenzi wa barabara ya Nyamuswa – Bulamba (km 56.4) kwa kiwango cha lami, kulipwa fidia zao kiasi cha shilingi zaidi ya bilioni mbili (2).

Prof. Mbarawa amezungumza hayo mara baada ya kuwasili wilayani hapo, mkoani Mara na kukutana na baadhi wa wananchi ambao bado hawajalipwa fidia zao na kusisitiza kuwa Serikali inatambua jambo hilo na itawalipa wale wote wanaostahili kwa mujibu wa sheria.

“Serikali yenu ni sikivu hivyo fedha zitaletwa hapa na wananchi watalipwa fidia zao ili mkandarasi aendelee na kazi zake bila ya kusimama”, amesisitiza Prof. Mbarawa.

Prof. Mbarawa amemtaka wasimamizi wa mradi huo kumsimamia mkandarasi anayejenga barabara hiyo ili kupata barabara yenye viwango na itakayodumu kipindi kirefu.

“Hatutaki barabara hii baada ya miaka miwili mitatu ianze kuharibika, na jibu lake ni moja tu kuwa waadilifu, kuwa wazalendo na kutumia muda mwingi kuisimamia barabara hii kwa weledi”, amefafanua Prof. Mbarawa.

Aidha, Prof. Mbarawa amesikitishwa na tabia za baadhi ya wafanyakazi katika mradi huo kujihusisha na vitendo vya wizi wa mafuta, saluji na vifaa vya ujenzi na kusema kwamba wanarudisha kasi ya maendeleo ya mradi huo na kuelekeza vyombo vya ulinzi kuendelea kuwafuatilia watu hao na kuchukua hatua za kisheria kwa wale watakaobainika.

“Vijana mkipata fursa ya kufanya kazi katika miradi ni heshima hivyo kujihusisha na vitendo vya wizi ni kuhujumu mradi na mfahamu kuwa hamumuibii mkandarasi bali mnaiibia Serikali na wananchi kwasababu vifaa hivyo vimenunuliwa kwa fedha za walipa kodi”, amesema Prof. Mbarawa.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Joshua Nassari, amemueleza Waziri kuwa mpaka sasa watu wanane (8), wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma hizo na wakati wowote watafikishwa mahakani.

Akiwasilisha taarifa ya mradi, Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Mara Mhandisi Vedastus Maribe, amemueleza Waziri huyo kuwa ujenzi wa barabara hiyo unagharimu kiasi cha shilingi bilioni 46.5, gharama za Mhandisi Mshauri ni kiasi cha shilingi Bilioni 2.337 na mradi huo unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Agosti, 2022.

Mradi wa barabara ya Nyamuswa – Bulamba (km 56.4) inayojengwa kwa kiwango lami ni kiungo muhimu kwani inaiunganisha Wilaya ya Bunda, Serengeti na Butiama pia inaunganisha Mikoa ya Kanda ya Ziwa, Mikoa ya Kaskazini pamoja na Kisiwa vya Ukerewe.

Katika hatua nyingine, Waziri Prof. Mbarawa, amekagua ujenzi wa jengo la Ofisi la Halmashauri ya wilaya ya Butiama na kumuagiza Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), kukamilisha ujenzi wa jengo hilo mapema mwanzoni mwa mwaka ujao ili waweze kutumia jengo hilo.

“Jengo hili lilisimama muda mrefu lakini sasa fedha zinakuja kwa wakati na kazi zinaendelea hivyo TBA malizeni haraka ili wafanyakazi na waweze kuhamia hapa kuendelea na majukumu yao kiurahisi”, amesema Prof. Mbarawa.

Waziri Mbarawa yupo mkoani Mara kwa ziara ya siku mbili ya kukagua utekelezaji wa miradi inayoendelea kutekelezwa na Wizara yake.
Share:

Serikali Itaendelea Kuunga Mkono Juhudi Za Mashirika Yasiyokuwa Ya Kiserikali (Ngos)


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo amesema Serikali itaendelea kuunga mkono juhudi za Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali (NGOs) katika shughuli za uhifadhi wa mazingira.

Dkt. Jafo ametoa kauli hiyo  Desemba 17, 2021 wakati akifungua Kongamano la Kukomboa Ardhi iliyochakaa katika Nyanda kame za Tanzania sanjari na Maadhimisho ya miaka 10 ya Shirika la Lead Foundation.

Alisema kuwa kongamano hilo linatoa taswira ya namna gani NGOs zinashiriki kikamilifu katika kusukuma mbele agenda ya mazingira nchini hivyo kuwajengea uelewa kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kulinda na kuhifadhi mazingira.

“Niliwahi kuitisha mkutano na mashirika yanayojihusha na suala zima mazingira na leo najisikia faraja kubwa kuona mashirika haya yanapiga hatua na lengo langu kubwa ni kuona kila mmoja anshiriki katika suala zima la uhifadhi wa mazingira,” alisema.

Aidha Waziri Jafo alisema Serikali itaendelea kusimamia Kampeni Kabambe ya Hifadhi na Usafi wa Mazingira inayowashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo wadau kutoka mashirika hayo.

Alisema anafarijika kutokana na Mpango Mkakati wa miaka 10 uliozinduliwa na Lead Foundation ambao unaonesha namna gani linaunga mkono Serikali katika hatua za kutunza na kuhidhi mazingira hususan katika eneo la mabadiliko ya tabianchi linaloikabili dunia.

Kwa upande mwingine alitumia nafasi hiyo kuwa kutoa rai kwa wanachi kutumia kipindi hiki cha masika kupanda miti kwa wingi na kuitunza ili kukabiliana na ukame ambao huleta athari mbalimbali za kijamii.

Aliwaelekeza wakuu wa mikoa na wilaya kusimamia vizuri zoezi hilo na kuhakikisha misitu haichomwi ovyo ili kuepusha athari za mabadiliko ya tabianchi zinazochangia kukosekana kwa mvua.

Akitoa shukrani, Mwanzilishi wa Shirika la Lead Foundation, Askofu mstaafu Dkt. Simon Chiwanga alisema kazi ya ukumbozi wa mazingira inafanywa kwa namna mbili ambazo ni kuelimisha na kumbadilisha mtu fikra.

Alisema kupitia uwasilisha wa elimu ya mazingira unaofanywa na Waziri Jafo Dkt. Jafo ni wa kipekee na unaweza kubadilisha fikra za wananchi kuona umuhimu wa kushiriki kuhifadhi mazingira.

“Nafurahia sana uwepo wako hapa mheshimiwa waziri na hiyo ‘passion’, hiyo huruma na upendo ulio nao tunamuomba Mungu akubariki sana,” alisema Askofu mstaafu Chiwanga


Share:

Serikali Yakitaka Chuo Cha Mipango Kuongeza Tafiti


Na. Saidina Msangi na Peter Haule, WFM, Mwanza
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amewaagiza watendaji na watalaamu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) kuongeza bidii katika kufanya tafiti zitakazo changia kuondoa umasikini na kukuza uchumi wa nchi.

Hayo yameelezwa na Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA  Leonard Mkude, kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), katika mahafali ya 35 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini na ya tisa kwa upande wa Kanda ya Ziwa yaliyofanyika Mkoani Mwanza.

CPA Mkude alisema kuwa ni jambo la kufurahisha na kutia moyo kuona Chuo kinatekeleza kwa vitendo moja ya majukumu yake ya msingi ya kutoa huduma ya ushauri elekezi kwa jamii, Halmashauri na Taasisi mbalimbali.

‘’ Wizara ya Fedha na Mipango itaendelea kuunga mkono juhudi za ujenzi wa Chuo cha Mipango kwa kuendelea kutoa fedha za Maendeleo na kuweka msukumo ili kiendelee kujenga majengo ya kisasa yanayokidhi mahitaji’’alisema CPA Mkude.

Alifafanua kuwa katika kipindi cha Miaka hii 60 nchi imepiga hatua kubwa ya maendeleo katika nyanja ya elimu, ikiwemo ongezeko kubwa la shule za msingi, sekondari , vyuo vya kati, na vyuo vya elimu ya juu na kuwa Serikali itaendelea kujenga vyuo vya ufundi katika kila Mkoa ili kutoa fursa kwa Vijana wanaomaliza elimu ya Sekondari na Msingi kupata ujuzi.

CPA Mkude aliupongeza uongozi wa Chuo hicho kwa kuwekeza katika ushirikiano na wadau wa maendeleo wakiwemo UNDP, FAO, UNICEF, NUFFIC, EU, AGRA na wengine, katika mapambano dhidi ya ujinga, maradhi na umasikini pamoja na kuwezesha kutoa huduma ya ushauri elekezi kwa jamii.

Aidha, aliwaasa wahitimu kutumia  ujuzi, elimu, na maarifa waliyoyapata chuoni hapo kwa manufaa ya umma kwa kuanzisha vikundi  vya uzalishaji mali kwa kutumia  fursa ya mikopo nafuu inayopatikana katika halmashauri nchini.

Pia alitoa wito kwa waajiri  na wadau wote wa maendeleo nchini kuwatumia vijana hao ambao wameiva na kubobea katika fani ya  mipango ya maendeleo ambayo ni muhimu katika maendeleo ya nchi yoyote duniani.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP), Prof. Hozen Mayaya, aliishukuru Serikali kwa jinsi inavyotenga fedha za Maendeleo ambazo zimesaidia kujenga majengo ya chuo hicho katika eneo la Kitumba “A” Kata ya Kisesa, wilayani Magu, ambapo mahafali ya mwaka huu yamefanyika hapo kwa mara ya kwanza.

Alisema kituo cha mafunzo Kanda ya Ziwa Mwanza kimekuwa na ongezeko la udahili kila mwaka sambamba na ongezeko la Wahitimu ambapo Mahafali ya Kwanza ya Mwaka 2011/12 kulikuwa na jumla ya Wahitimu 269, ilihali mwaka huu kuna jumla ya Wahitimu 2718.

‘‘Ili kuongeza wigo wa fursa za ajira miongoni mwa wahitimu wetu, Chuo kimeanzisha kituo cha ubunifu na ujasiliamali, ambapo wanafunzi wanapata nafasi ya kujifunza masuala ya ubunifu na ujasiriamali, hivyo kuwa tayari kuajiriwa na kujiajiri’’,Alisema Profesa Mayaya.

Alisema kuwa chuo kupitia timu ya wataalamu wake kimefanikiwa kundika maandiko yaliyo pata ufadhili kutoka katika mashirika ya Kimataifa, yakiwemo UNICEF, EU, AGRA na UNDP, na kutekeleza mradi uliofadhiliwa na UNDP, wa namna ya kukabiliana na mabadiliko ya Tabia Nchi na Kupunguza Umasikini katika jamii za Kanda ya Ziwa.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo hicho, Prof. Martha Qorro, alisema kuwa wataendelea kukisimamia chuo kwa weledi ili kiweze kufikia malengo ya kuanzishwa kwake kwa kusimamia utekelezji wa Mpango Mkakati wa Chuo 2021/22 hadi 2025/26 ambao umepitishwa mwaka huu.

‘Tunakuahidi kufanya kazi kwa weledi wa hali ya juu ili Chuo kiendelee kutekeleza majukumu yake ya msingi na ya maendeleo kwa kufuata kanuni, miongozo, sheria na taratibu zilizopo na zitakazotolewa mara kwa mara na mamlaka’ alisema Profesa Qorro.

Mahafali ya mwaka huu ya chuo hicho kwa Kanda ya Ziwa ambayo yamefanyika kwa mara ya kwanza katika majengo mapya ya chuo hicho yamehusisha Wahitimu 2718 wakiwemo wanaume 1,086 na wanawake 1,632 katika fani mbalimbali.



Share:

Friday, 17 December 2021

Administrative Assistant at Catholic Relief Services

Job Title: Administrative Assistant Reports to:  Administrative officer Department:  Operations Location: Mbeya About CRS  Catholic Relief Services is the official international humanitarian agency of the Catholic community in the United States. CRS works to save, protect, and transform lives in need in more than 100 countries, without regard to race, religion or nationality. CRS’ relief and […]

This post Administrative Assistant at Catholic Relief Services has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Project Manager – Water, Sanitation & Hygiene (WASH) at Catholic Relief Services

Job Title: Project Manager – Water, Sanitation & Hygiene (WASH) Reports to: Head of programs Department:  Programs Location: Mbeya About CRS  Catholic Relief Services is the official international humanitarian agency of the Catholic community in the United States. CRS works to save, protect, and transform lives in need in more than 100 countries, without regard to race, […]

This post Project Manager – Water, Sanitation & Hygiene (WASH) at Catholic Relief Services has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

OSHA YAZINDUA MPANGO WA MAFUNZO KWA TAASISI ZA SERIKALI


Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu), Mhe.Ummy Nderiananga akizungumza na watumishi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) wakati akifungua mpango wa mafunzo ya usalama na afya kwa watumishi wa umma ulioanza kutekelezwa na OSHA kwa NIC ambapo utaendelea kutekelezwa kwa Taasisi nyingine za Serikali na Mashirika ya Umma.


Mkurugenzi wa Usalama na Afya wa OSHA, Alexander Ngata akiwasilisha taarifa fupi ya mpango wa mafunzo ya usalama na afya kwa watumishi wa umma unaotekelezwa na OSHA wakati wa ufunguzi wa mpango huo uliozinduliwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Ummy Nderiananga (Katikati). Wakwanza kulia ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Shirika la Bima la Taifa, Lihami Masoli.Mkaguzi wa afya wa OSHA, Dkt. Amin Vasomana akimpima afya mtumishi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) wakati wa ufunguzi wa mpango wa mafunzo ya usalama na afya kwa watumishi wa umma uliombatana na zoezi la upimaji afya kwa washiriki wa mafunzo hayo.

Mkufunzi wa mafunzo ya huduma ya kwanza wa OSHA, Hans Mpera, akionesha namna ya kumpa huduma ya kwanza mtu aliyejeruhiwa kichwani, wakati wa mafunzo ya usalama na afya kwa watumishi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) yanayofanyika Mkoani Morogoro.

******************

Na Mwandishi Wetu

Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) umezindua rasmi mpango wa mafunzo ya Usalama na Afya kwa Taasisi za Serikali na Mashirika ya Umma Tanzania Bara.

Mpango huo ambao umeanza kutekelezwa kwa kutoa mafunzo kwa watumishi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) umezinduliwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu), Ummy Nderiananga ambaye amezitaka Taasisi nyingine za serikali kujiandaa kutekeleza mpango huo.

“Natoa pongezi za dhati kwa menejimenti ya NIC kwakutambua umuhimu wa mafunzo haya na kuamua kushirikiana na Taasisi yetu ya OSHA katika kufanikisha jambo hili muhimu. Hivyo basi, niwasihi nyote mnaoshiriki mafunzo haya kuyazingatia na kwenda kuyatumia ipasavyo katika kuboresha utendaji wenu wa kila siku,” alisema Mhe. Naibu Waziri na kuongeza:

“Aidha, niwaagize OSHA kuhakikisha kwamba wanayafikia Mashirika na Taasisi zote za serikali na kutoa mafunzo ya Usalama na Afya kwa watumishi wote ambapo ni matumaini yetu kwamba endapo yatatolewa na kutekelezwa kikamilifu basi yatasaidia kupunguza ajali, magonjwa na vifo vitokanavyo na mazingira ya kazi yasiyo rafiki. Hii itaisaidia serikali kuepuka gharama za kuwahudumia majeruhi wa ajali na wagonjwa pamoja na kuepuka hasara kubwa ambayo Taifa limekuwa likipata kutokana na kupoteza nguvukazi yake pamoja na uharibifu wa mali na miundombinu mbalimbali za uzalishaji.”

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mpango huo, Mkurugenzi wa Usalama na Afya wa OSHA, Alexander Ngata, ametoa wito kwa Taasisi mbalimbali za serikali kushirikiana na OSHA ili kufanikisha utekelezaji wa mpango huo ambao unahusisha ukaguzi wa usalama kwenye maeneo ya kazi pamoja na uchunguzi wa afya za wafanyakazi.

“Nitoe wito kwa waajiri katika sekta ya umma kutenga bajeti kwa ajili ya kutoa mafunzo ya usalama na afya kwa watumishi wao zoezi ambalo tutaliendesha sambamba na ukaguzi wa mifumo ya usalama na afya kwenye maeneo yao ya kazi pamoja na kuchunguza afya za wafanyakazi kama tulivyofanya kwa Shirika la Bima la Taifa (NIC),” alisema, Bw. Ngata.

Kwa upande wa washiriki wa mafunzo hayo ambao ni viongozi wa NIC wameipongeza OSHA kwa kuja na mpango huo ambao wameuelezea kuwa ni mpango mzuri ambao mbali na kulinda afya na usalama wa wafanyakazi utaleta tija katika biashara na uzalishaji.

“Niwapongeze OSHA kwa kazi nzuri wanayofanya na niwaombe wajitahidi kuwafikia waajiri wengi zaidi kwani wakifanya hivyo hali ya usalama na afya itazidi kuimarika nchini jambo ambalo litatusaidia kuimarisha mifuko ya bima kutokana na kupungua kwa gharama za fidia za majanga mbalimbali,” alieleza Bw. Lihami Masoli, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa NIC ambaye alishiriki mafunzo ya Huduma ya Kwanza yaliyotolewa na OSHA kwa menejimenti ya shirika pamoja na watumishi wengine.

Mshiriki mwingine wa mafunzo hayo, Bi. Florence Samweli, amesema mafunzo hayo ni mazuri na ni muhimu sana hususan kwa wafanyakazi katika maeneo mbalimbali ya kazi.

“Kwakweli mafunzo haya yakitolewa kwa watu wengi yatasaidia sana kuokoa maisha ya watu pindi ajali zinapotokea. Binafsi yamenijenga sana na naweza kusema baada ya kuhitimisha mafunzo haya sipo kama nilivyokuja hapo awali,” amesema Bi. Florence.

Miongoni mwa majukumu ya OSHA ni pamoja na kukuza uelewa wa masuala ya Usalama na Afya miongoni wa Watanzania kupitia kutoa mafunzo mbalimbali ikiwemo mafunzo ya Huduma ya Kwanza mahali pa kazi, Mafunzo kwa wanakamati za Usalama na Afya mahali pa kazi, Uchunguzi wa Ajali mahali pa kazi, Tathmini ya Vihatarisha vya Usalama na Afya mahali pa kazi pamoja na kozi nyinginezo zinazohusu masuala ya usalama na afya mahali pa kazi.
Share:

Matron at The Institute of Construction Technology (ICoT)

POST: MATRON – 1 POST POST CATEGORY(S): HR & ADMINISTRATION SOCIOLOGY, POLITICAL SCIENCE, COMMUNITY AND SOCIAL DEVELOPMENT EMPLOYER: The Institute of Construction Technology(ICoT) APPLICATION TIMELINE: 2021-12-14 2021-12-27 DUTIES AND RESPONSIBILITIES i.To supervise cleaning and domestic staff. ii.To keep students records up to date. iii.To order cleaning, domestic and medical supplies for the students. iv.To carry […]

This post Matron at The Institute of Construction Technology (ICoT) has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Waden at The Institute of Construction Technology (ICoT)

POST: WADEN – 1 POST POST CATEGORY(S): SOCIOLOGY, POLITICAL SCIENCE, COMMUNITY AND SOCIAL DEVELOPMENT EMPLOYER: The Institute of Construction Technology(ICoT) APPLICATION TIMELINE: 2021-12-14 2021-12-27 DUTIES AND RESPONSIBILITIES i.To ensure safe and healthy living and working environment for resident students; ii.To promote a collegiate environment, good order and social harmony in the halls of residence; iii.To enforce discipline […]

This post Waden at The Institute of Construction Technology (ICoT) has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

PAKUA APP MPYA YA MALUNDE 1 BLOG....IMEBORESHWA ZAIDI KUKUPA RAHA YA HABARI NA MATUKIO BURE KWENYE SIMU YAKO


Toleo Jipya Kabisa la App ya Malunde 1 blog, Kama unayo kwenye simu Pakua Upya mtu wangu...  Bofya mara Moja <<Hapa>>
Toleo Jipya Kabisa la App ya Malunde 1 blog, Kama unayo kwenye simu Pakua Upya mtu wangu...  Bofya mara Moja <<Hapa>>
Toleo Jipya Kabisa la App ya Malunde 1 blog, Kama unayo kwenye simu Pakua Upya mtu wangu...  Bofya mara Moja <<Hapa>>

Habari Njema Wasomaji wa Malunde 1 blog !! Ili kuwa wa Kwanza kupata habari na matukio  ya ukweli na uhakika kwa wakati yanayojiri Tanzania na dunia kwa ujumla tunakushauri kupakua/ kudownload Aplikesheni ya Malunde 1 blog

Usikubali kupitwa na habari na Matukio yanayotokea… Pakua leo App ya Malunde 1 blog


Tembea na dunia kiganjani mwako kiulaini kabisa.

Pakua App mpya ya Malunde 1 blog imeboreshwa zaidi ili kukidhi mahitaji ya wasomaji wetu. 


Ni rahisi sana : Ingia Play store kisha Andika Malunde 1 blog halafu bonyeza Install

https://bit.ly/2Qb7qyF

Usikubali kukosa habari kizembe..Pakua app yetu Mpya ya Malunde1 blog Sasa

Toleo Jipya Kabisa la App ya Malunde 1 blog, Kama unayo kwenye simu Pakua Upya mtu wangu...  Bofya mara Moja <<Hapa>>



Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger