Friday, 17 December 2021

Personal Secretaries II 2 Job Opportunities at The Institute of Construction Technology (ICoT)

POST: PERSONAL SECRETARY II – 2 POST POST CATEGORY(S) HR & ADMINISTRATION EMPLOYER The Institute of Construction Technology(ICoT) APPLICATION TIMELINE: 2021-12-14 2021-12-27 DUTIES AND RESPONSIBILITIES i.To type letters, reports and documents; ii.To receive visitors, screen and direct them to relevant officers; iii.To keep in safe custody reports and other records of events; iv.To keep and make appointments […]

This post Personal Secretaries II 2 Job Opportunities at The Institute of Construction Technology (ICoT) has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

Drivers 3 Job Opportunities at The Institute of Construction Technology (ICoT)

POST: DRIVERS – 3 POST POST CATEGORY(S): DRIVER’S ENGINEERING AND CONSTRUCTION EMPLOYER: The Institute of Construction Technology(ICoT) APPLICATION TIMELINE: 2021-12-14 2021-12-27 DUTIES AND RESPONSIBILITIES i.To drive ICoT vehicles skillfully; ii.To maintain and keep up-to-date log-books; iii.To adhere to Maintenance Schedules; iv.To keep motor vehicle in good running conditions and report immediately faults and defects to Transport officer; […]

This post Drivers 3 Job Opportunities at The Institute of Construction Technology (ICoT) has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

Library Assistant at The Institute of Construction Technology (ICoT)

POST: LIBRARY ASSISTANT – 1 POST POST CATEGORY(S): HR & ADMINISTRATION EMPLOYER: The Institute of Construction Technology(ICoT) APPLICATION TIMELINE: 2021-12-14 2021-12-27 DUTIES AND RESPONSIBILITIES i.To display new books and other reading materials; ii.To upkeep back sets of newspapers and journals; iii.To prepare cuttings from newspapers of relevance to the Institute; iv.To handle simple enquiries from readers; and […]

This post Library Assistant at The Institute of Construction Technology (ICoT) has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

Thursday, 16 December 2021

JENERALI ULIMWENGU AWATAKA WAMILIKI WA VYOMBO VYA HABARI KUACHA KUWA SEHEMU YA UKANDAMIZAJI WA UHURU WA HABARI

MWANDISHI Mkongwe na Mchambuzi wa siasa Jenerali Ulimwengu amewataka wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini kushirikiana na waandishi wao katika mapambano dhidi ya Uhuru wa Habari.

Ulimwengu amesema wamiliki wa vyombo vya habari wanatakiwa kujua kwamba licha ya kuwa wamiliki wa vyombo hivyo lakini lengo kuu ni kuhudumia jamii .

Akizungumza jijini Dodoma katika mjadala wa wamiliki wa vyombo vya habari ulioandaliwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (MISA TAN),Ulimwengu amewataka wamiliki hao kutokuwa sehemu ya ukandamizaji wa Uhuru wa habari kwa maslahi yao binafsi.

“Kuna watu wanaanzisha vyombo vya habari lakini lengo ni kulinda itikadi zao za kisiasa maslahi ya biashara zao au marafiki zao wanasahau kwamba vyombo wanavyoanzisha ni mali ya wananchi,kwa sababu vyombo vyote vinaanzishwa ili kuhudumia wananchi.” Alifafanua Ulimwengu.

Jenerali amesema kwa kipindi cha miaka kadhaa nyuma tasnia ya habari imekuwa mfu kutokana na sababu mbalimbali lakini amesema wamiliki wa vyombo vya habari hawawezi kukwepa kudorora huko kwa tasnia muhimu katika jamii.

Ulimwengu amewataka wamiliki ambao kama wanaona hawapo tayari kufanya na kuhudumia jamii ni bora wahamishie mitaji yao katika shuguli nyingine ili kuacha nafasi hiyo kwa watu wenye nia ya dhati ya kusaidia kupaza sauti za wananchi ili kutatua changamoto zinazowakabili.

“Kama una chombo cha habari na hakiwajibiki kwa wananchi ni bora ukafanye kazi nyingine,kazi ya habari inabidi ujikane hadi nafsi yako na kuwa ‘commited’ kwenye kufanya kazi hiyo.” Amesema.

Hata hivyo Ulimwengu amewashauri wamiliki hao kuweka utaratibu mzuri utakaowawezesha waandishi wao kujiendeleza kielimu ili kuongeza maarifa yatakayowasaidia kuchakata kwa weledi maudhui wanayoyapeleka kwa hadhira yao.

Kwa upande wake Mhariri Mwandamizi mstaafu Jesse Kwayu amewataka wamiliki kushirikiana na watendaji wao (waandishi) ili kuweza kurudisha heshima ya vyombo vya habari nchini kama ilivyokuwa miaka iliyopita.

“Vyombo vya Habari kwa sasa haviogopwi kama zamani,Wamiliki ni lazima kushiriki katika harakati za kurudisha vyombo vya habari kurudisha ‘lost glory’ (heshima iliyopotea) katika tasnia ya habari” amesema Kwayu.

Kwa upande wao wamiliki wa vyombo vya habari wameibua changamoto mbalimbali ambazo zikirekebishwa zinaweza kurudisha heshima katika tasnia ya habari.

Mmiliki wa Standard FM (Singida) Daudi James amesema tabia ya waandishi wa habari kuendekeza ‘bahasha ya kaki’ (posho) imekuwa tatizo kubwa katika kutengeneza maudhui yasiyo na faida kwa jamii zaidi ya kumtangaza yule aliyewalipa posho.

“Bahasha(posho) zinatuulia vyombo vya habari,waandishi wengi hawaandiki habari za uchunguzi wanakimbilia kwenye habari zenye posho tu.” Amefafanua mmiliki huyo.

Kwa upande Abdul Diallo akimuwakilisha mmiliki wa kampuni ya Sahara Media Group amesema baadhi ya Wahariri na Waandishi wanashiriki kuminya uhuru wa habari kutokana na kuendekeza itikadi zao za kisiasa.

Dialo amesema katika kipindi cha uchaguzi mkuu uliopita wapo baadhi ya Wahariri na waandishi waandamizi waligombea nafasi mbalimbali katika vyama vya siasa,amesema tukio hilo lilidhhirisha kwa namna gani waandishi wenyewe wana pande ambazo wanazitumikia.

“Kuna wamiliki ni wanasiasa lakini hawaingilii vyombo wanavyovimiliki lakini kuna baadhi ya matukio ya uminywaji wa uhuru wa kujieleza tatizo ni itikadi za wahariri wa habari wamiliki hawatakiwi kulaumiwa”alifafanua Dialo.

Mjadala huo umefanyika wiki hii ukiwa na lengo la kuwajengea uelewa wamiliki wa vyombo vya habari kuhusu kazi ya vyombo vya habari kwenye kuchochea uwazi, haki na demokrasia.

Lengo jingine la mjadala huo kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazoathiri uhuru wa kiuhariri unaosababisha kutokuwepo kwa uhuru wa kiuhariri kwenye vyombo vya habari unapelekea vyombo vya habari kushindwa kutekeleza majukumu yake ya kusaidia jamii.
Share:

IGP SIRRO ARUDI TENA KIBITI NA KUTOA MAAGIZO MAZITO KWA KAMATI ZA ULINZI NA USALAMA

NA  KIBITI, PWANI
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amewataka viongozi wa dini pamoja na viongozi wa Kamati za Ulinzi na usalama za wilaya, tarafa, Vijiji na Vitongoji kuhakikisha wanatimiza wajibu wao katika suala zima la ulinzi na usalama kwenye maeneo yao.

IGP Sirro amesema hayo jana wakati alipofanya ziara ya kikazi Kibiti na Ikwiriri mkoani Pwani na kukutana na Viongozi wa Halmashauri tatu za Mkoa huo ikiwemo Mkuranga, Kibiti na Ikwiriri pamoja na viongozi wengine wa Kamati za Usalama kwa lengo la kuwakumbusha wajibu wao.

Akizungumzia suala la usalama katika maeneo ya Kibiti na Ikwiriri IGP Sirro amesema kuwa, bado zipo changamoto chache kama wizi wa Pikipiki, mifugo na uhalifu mwingine mdogo mdogo ambao unaendelea kudhibitiwa.

Naye Diwani wa Kata ya Ikwiriri Ali Mbwana  amesema kuwa, wananchi wanalipongeza Jeshi la Polisi kwa kuendelea kuchukua hatua mbalimbali kuhakikisha hali ya amani na usalama hasa eneo la Ikwiriri na Kibiti Inazidi kuimarika.

Share:

Marketing Manager at TMT Motors

Position: Marketing Manager Qualifications:   Bachelor in Public Relation and marketing At least two years experience 24 to 34 years old   Qualities:   Social Skills Social Media Skills Story Telling Skills Data Analysis Skills Domain Expertise Collaboration And Exceptional Communication Process Designing Skills   All Job Applications are to be sent on the email: tmtmotor128@gmail.com Deadline: […]

This post Marketing Manager at TMT Motors has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

TASAC na ZMA Zatakiwa Kumaliza Changamoto Zao

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, ameliagiza Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC), na Mamlaka ya Usafiri wa Baharini ya Zanzibar (ZMA), kumaliza changamoto zinazowakabili katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuongeza ufanisi na kuondoa malalamiko kwa wateja.

Prof. Mbarawa amesema hayo jijini Mwanza, wakati akifungua mkutano wa nne wa mashauriano kati ya Watendaji wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) ya Seriali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT), na Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), ambapo amesisitiza kushirikiana na kufanya kazi pamoja katika kusimamia sheria za usalama majini.

Aidha, Prof. Mbarawa ameshauri wataalam hao kupitia upya sheria zilizopo na kuangalia namna ya kuziboresha ili ziwiane na kutoleta mikanganyiko katika utekelezaji.

“Katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, masuala ya usafiri majini yanasimamiwa na Sheria ya Usafiri Majini Sura ya 165, Sheria ya Uwakala wa Meli Tanzania Sura ya 415, Sheria ya Usafiri wa Bahari ya Zanzibar Na. 5 ya mwaka 2006 na Sheria ya Mamlaka ya Usafiri Baharini ya Zanzibar Na. 3 ya mwaka 2009 hivyo uwepo wa sheria nyingi zinazosimamia suala moja unaweza kusababisha changamoto ya sheria hizo kutowiana (harmornised) wakati wa utekelezaji wake“, amefafanua Prof. Mbarawa.

Prof. Mbarawa ameeleza pia umuhimu wa ushiriki wa sekta binafsi katika maendeleo ya nchi kwani Sekta hiyo inasaidia katika uwekezaji, kuipunguzia Serikali mzigo wa uwekezaji na vihatarishi vyake, kuongeza ajira, kuingiza fedha kwenye mzunguko, kuchangia kuleta teknolojia mpya nchini, kukuza uchumi na kuongeza pato la Taifa na fedha za kigeni.

Naye, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi), Bw. Gabriel Migire, amesema kuwa mkutano huo utaibua fursa zilizopo kwa pande zote mbili ikiwemo ya kushirikisha Sekta Binafsi kuwekeza katika masuala ya usafiri majini/baharini ili kuhakikisha kwamba vyombo madhubuti vya usafiri majini vinapatikana katika maeneo yenye uhaba.

Bw. Migire ameongeza kuwa ufumbuzi wa changamoto mbalimbali za kiutendaji zilizokuwa zinajitokeza kutokana na kutokukutana na kukubaliana pamoja, sasa zimepungua kwa kuwa wamekuwa wanakutana mara kwa mara na kutafuta ufumbuzi wa pamoja juu ya changamoto za kiutendaji zinazojitokeza.

Katika hatua nyingine Wajumbe hao wametembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli (Kigongo – Busisi), lenye urefu wa kilometa 3.2 na kuridhishwa na maendeleo yake ikiwemo teknolojia inayotumika katika ujenzi wa daraja hilo.

Mkutano wa nne wa Mashaurino umehusishaWatendaji Wakuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi – SMT) na Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi (SMZ), Wakuu wa Idara na Vitengo kutoka Sekta ya Uchukuzi kwa upande wa SMT na SMZ na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Sekta ya Uchukuzi kwa upande wa SMT na SMZ.

Share:

Data Collector at Compassion International

Data Collector    Compassion International Tanzania is seeking qualified data collectors to administer surveys to children, youth, and adults. The expected data collection window and time commitment for this position is January through March. Duties and Responsibilities   Maintain a personal relationship with Jesus Christ. Is a consistent witness for Jesus Christ, maintains a courteous, […]

This post Data Collector at Compassion International has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

Project Manager at BBC Media Action

Job title: Project Manager, A National Conversation Location: Tanzania Reports to: Senior project manager & editorial lead Duration: 12 months (with possible extension) Special requirements: The right to live and work in Tanzania. Fluent in English and Swahili with ability to write reports in both languages. BBC Media Action:  BBC Media Action is the BBC’s international […]

This post Project Manager at BBC Media Action has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

Wednesday, 15 December 2021

RAIS SAMIA AFUNGUKA KUHUSU KUMSAMEHE FREEMAN MBOWE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
***

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewakumbusha viongozi wa vyama vya siasa kuzingatia na kutii sheria ili kuepuka heshima zao kuondoka.

Rais Samia ameeleza hilo leo wakati akijibu ombi la Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo Ndugu Zitto Kabwe ambaye alimuomba awasaidie kumsamehe Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe.

''Nataka nizungumzie kidogo aliloniomba mwanangu Zitto, kwamba yule mwenzetu msamehe basi aje awe na sisi. Demokrasia ni kuheshimu sheria, heshima ya mtu inakuja kwa kuheshimu sheria za nchi. Naomba tufanye kazi kwa kufuata sheria waswahili wanasema mtaka nyingi na saba... ingawa kusameheana nako kupo,'' ameeleza Rais Samia Suluhu.

Aidha Rais Samia amesisitiza kuwa kuna taifa moja tu ambalo raia wote wanawajibika kulilinda.

''Nitumie fursa hii kuwakumbusha kwamba Duniani kuna nchi moja tu inayoitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ni taifa huru lililojengwa kwa misingi ya amani, upendo, mshikamano na linaloongozwa kwa misingi ya katiba na sheria zilizotungwa na bunge na sio utashi wa mtu au mataifa mengine. Na wenye hili taifa ni sisi,'' amesema Rais Samia Suluhu.

Kiongozi Mkuu wa Chama Cha ACT Wazalendo Ndugu Zitto Kabwe amemuomba Rais Samia kuwasaidia kumtoa Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe ili waungane naye katika kujenga taifa.

Zitto ameyasema hayo alipopata nafasi ya kuongea kwenye Mkutano wa Wadau wa Kujadili Hali ya Demokrasia ya Vyama Vingi Nchini uliofanyika leo Desemba 15, 2021 katika Ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.

”Sisi viongozi wa Vyama tupo hapa lakin na kuna mwenzetu hayupo kwasababu ya changamoto za kisheria na tuna utamaduni sisi wa kumaliza haya mambo na haitakuwa mara ya kwanza, tunakuomba sana kwa mujibu wa sheria na taratibu zote za kisheria tusaidie mwenzetu tuwe naye,” ameeleza Zitto Kabwe.

Katika hatua nyingine Zitto ameeleza wanavyouchukulia Mkutano huo. ”Hatua hii sisi tunachukulia kuwa ni muhimu sana kuelekea katika kuwa na majadiliano ya kisiasa katika nchi yetu na kila jambo lina mwanzo na huu ni mwanzo mwema na Mungu atatuongoza tuweze kuwa na utaratibu huu kama ambavyo tulivyo Tanzania”.

CHANZO - EATV & Global Tv
Share:

Picha : MISA TANZANIA YAKUTANA NA WAMILIKI WA VYOMBO VYA HABARI KUCHOCHEA UWAZI, HAKI NA DEMOKRASIA

Mwandishi wa Habari Mwandamizi nchini Tanzania Jenerali Ulimwengu akizungumza wakati wa Mjadala kwa wamiliki wa vyombo vya habari nchini kuhusu nafasi ya vyombo vya habari na Uhuru wa Kiuhariri.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Taasisi ya vyombo vya Habari Kusini mwa Jangwa la Sahara (Media Institute of Southern Africa - MISA Tanzania) imeendesha Mjadala kwa wamiliki wa vyombo vya habari nchini kuhusu nafasi ya vyombo vya habari na Uhuru wa Kiuhariri.

Mjadala huo umefanyika leo Jumatano Desemba 15,2021 jijini Dodoma ukiwa na lengo la kuwajengea uelewa wamiliki wa vyombo vya habari kuhusu kazi ya vyombo vya habari kwenye kuchochea uwazi, haki na demokrasia.

Lengo jingine la mjadala huo ulioongozwa na Waandishi wa Habari Waandamizi nchini Jesse Kwayu na Jenerali Ulimwengu ni kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazoathiri uhuru wa kiuhariri unaosababisha kutokuwepo kwa uhuru wa kiuhariri kwenye vyombo vya habari unapelekea vyombo vya habari kushindwa kutekeleza majukumu yake ya kusaidia jamii.
Mweka Hazina wa MISA Tanzania, Michael Gwimile akifungua Mjadala kwa wamiliki wa vyombo vya habari nchini kuhusu nafasi ya vyombo vya habari na Uhuru wa Kiuhariri kwa niaba na Mwenyekiti wa MISA Tanzania Salome Kitomari leo Jumatano Desemba 15,2021. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
 Mweka Hazina wa MISA Tanzania, Michael Gwimile akifungua Mjadala kwa wamiliki wa vyombo vya habari nchini kuhusu nafasi ya vyombo vya habari na Uhuru wa Kiuhariri kwa niaba na Mwenyekiti wa MISA Tanzania, Salome Kitomari.
Kaimu Mkurugenzi wa MISA Tanzania, Andrew Marawiti akizungumza wakati wa Mjadala kwa wamiliki wa vyombo vya habari nchini kuhusu nafasi ya vyombo vya habari na Uhuru wa Kiuhariri.
Kaimu Mkurugenzi wa MISA Tanzania, Andrew Marawiti akizungumza wakati wa Mjadala kwa wamiliki wa vyombo vya habari nchini kuhusu nafasi ya vyombo vya habari na Uhuru wa Kiuhariri.
Afisa Habari na Msimamizi wa Miradi MISA Tanzania,  Jacqueline Jones akizungumza wakati wa Mjadala kwa wamiliki wa vyombo vya habari nchini kuhusu nafasi ya vyombo vya habari na Uhuru wa Kiuhariri.
Afisa Habari na Msimamizi wa Miradi MISA Tanzania,  Jacqueline Jones akizungumza wakati wa Mjadala kwa wamiliki wa vyombo vya habari nchini kuhusu nafasi ya vyombo vya habari na Uhuru wa Kiuhariri.
Mwandishi wa Habari Mwandamizi nchini Tanzania Jenerali Ulimwengu akizungumza wakati wa Mjadala kwa wamiliki wa vyombo vya habari nchini kuhusu nafasi ya vyombo vya habari na Uhuru wa Kiuhariri.
Mwandishi wa Habari Mwandamizi nchini Tanzania Jenerali Ulimwengu akizungumza wakati wa Mjadala kwa wamiliki wa vyombo vya habari nchini kuhusu nafasi ya vyombo vya habari na Uhuru wa Kiuhariri.
Mwandishi wa Habari Mwandamizi nchini Tanzania Jenerali Ulimwengu akizungumza wakati wa Mjadala kwa wamiliki wa vyombo vya habari nchini kuhusu nafasi ya vyombo vya habari na Uhuru wa Kiuhariri.
Mwandishi wa Habari Mwandamizi nchini Tanzania Jesse Kwayu akizungumza wakati wa Mjadala kwa wamiliki wa vyombo vya habari nchini kuhusu nafasi ya vyombo vya habari na Uhuru wa Kiuhariri.

Washiriki wa Mjadala kwa wamiliki wa vyombo vya habari nchini kuhusu nafasi ya vyombo vya habari na Uhuru wa Kiuhariri wakiwa ukumbini

Washiriki wa Mjadala kwa wamiliki wa vyombo vya habari nchini kuhusu nafasi ya vyombo vya habari na Uhuru wa Kiuhariri wakiwa ukumbini.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Share:

Video Mpya : MICO TIGER - SIMAMA

Msanii Mico Tiger kutoka Didia - Luhumbo Shinyanga ameachia wimbo mpya unaitwa Simama..tazama video hapa
Share:

BENKI YA CRDB KUWAWEZESHA WATEJA WA ATCL KUFANYA MALIPO YA TIKETI KWA URAHISI

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Denge la Tanzania (ATCL), Mhandisi Ladislaus Matindi wakionyesha ishara ya uzinduzi wa huduma ya malipo ya tiketi za ndege za ATCL kupitia mtandao wa Benki ya CRDB unaojumuisha matawi, CRDB Wakala na SimBanking katika hafla iliyofanyika leo jijini Arusha katika hoteli ya Mount Meru.

Benki ya CRDB imeingia ubia na Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kuwawezesha wateja wanaosafiri na ndege za shirika hilo kulipia tiketi za safari kupitia mtandao wa benki hiyo unaojumuisha Matawi 268 yanayopatikana nchi nzima, CRDB Wakala zaidi ya 20,000, pamoja na huduma ya SimBanking inayowezesha kufanya malipo kidijitali. 

Akizungumza katika hafla ya kusaini mkataba wa makubaliano iliyofanyika katika hoteli ya Mount Meru jijini Arusha, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema ubia huo na ATCL utasaidia kuhakikisha wateja wanafanya malipo kwa urahisi popote pale walipo nchini jambo litakalo saidia kuboresha huduma kwa wateja katika shirika hilo.

“Pamoja na kuwa wateja watakuwa wakilipia tiketi zao kwa urahisi, vilevile uunganishwaji wa mfumo huu wa malipo na mfumo wa ATCL utasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza ufanisi katika upande wa upokeaji wa malipo ya tiketi. Tukiwa Benki ya kizalendo tunajivunia sana ubia huu na Shirika letu hili la ATCL ambalo pia ni la kizalendo,” amesema Nsekela.

Nsekela alibainisha kuwa hapo mwanzoni Benki hiyo ilikuwa ikiwawezesha wateja kulipia tiketi za ndege za ATCL kwa njia ya mtandao kupitia TemboCard, hivyo kuongezeka kwa njia hizo nyengine kunawapa wateja uhuru wa kufanya malipo kwa njia ambayo ni rahisi kwao kwa wakati husika. “Nawakaribisha wateja wote ambao wanasafiri na ndege za Shirika letu la ATCL kutumia njia hizi kufanya malipo kwani ni rahisi na salama, lakini wafanyakazi na CRDB Wakala wetu pia wapo tayari kuwahudumia,” aliongezea.

Naye Mkurungezi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Mhandisi, Ladislaus Matindi ameishukuru Benki ya CRDB kwa ushirikiano wa kibiashara ambapo Benki ya CRDB imekua benki ya kwanza kutoa huduma za benki kwa njia ya mtandao kwa shirika hilo ambalo kwa sasa linashikilia asilimia 75 ya soko la usafiri wa anga hapa nchini. Aidha amesema kuunganishwa kwa mifumo ya malipo ya Benki ya CRDB kunaendana na mikakati ya ukuaji wa shirika hilo ambapo hivi karibuni limeongeza safari za ndege ndani na nje ya nchi.

“Kama mnavyofahamu shirika letu limekuwa na mkakati wa kufika katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi kwa kurahisisha safari za ndege ambapo hivi karibuni shirika hilo linatarajiwa kutanua wigo wa safari za nje ambapo safari za kuelekea Nigeria, Afrika ya Kusini, China na Uingereza zinatarajiwa kuanza hivi karibuni. Mkakati huu wa upanuzi wa biashara unaenda sambamba na kuhakikisha wateja wetu wanaweza kupata huduma bora popote pale walipo. Ni imani ushirikiano huu na Benki ya CRDB utasaidia kufikia azma yetu ya kutoa huduma bora za usafiri kwa njia ya anga,” amesema Matindi.

Akizungumzia namna ya kunua na tiketi na kufanya malipo kupitia mtandao wa Benki ya CRDB, Matindi alisema wateja watafuata hatua ya kawaida ya kuhifadhi wa tiketi kwa kutembelea tovuti ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) www.airtanzania.co.tz au Ofisi ya Mawakala kwaajili ya ambapo atapewa namba  ya uhifadhi wa tiketi (PNR) ambayo utaitumia kulipia tiketi iliyohifadhiwa kupitia mifumo ya Benki ya CRDB.

“Ikiwa mteja atatembelea kwenye tawi la Benki ya CRDB au CRDB Wakala ataonyesha namba yake ya uhifadhi tiketi na kisha kulipa kiasi husika kutokana na safari yake. Kwa upande wa SimBanking mteja baada ya kupata namba ya uhifadhi wa tiketi ataingia kwenye menu na kuchagua malipo kisha atachagua shirika la ndege la ATCL, ataingiza namba ya uhifadhi na kisha kufanya malipo,” amesema Matindi.

Hivi karibuni Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) limeongeza safari zake za ndani na nje ya Tanzania ikiwa ni kipindi kifupi baada ya ujio wa ndege mbili aina ya Airbus, ambazo zimepelekea kuongezeka kwa safari mpya zilizoanza Novemba, 2021. Safari zilizoongezwa ni pamoja na Dodoma-Mwanza, Dar-Mtwara, Dar-Nairobi, Dar-Ndola Dar-Bujumbura ambapo Benki ya CRDB ina kampuni tanzu, pamoja na Dar-Lumbumbashi ambapo Benki hiyo ipo mbioni kufungua kampuni tanzu.</
Share:

WAHITIMU SJUT WATAKIWA KUZINGATIA MAADILI NA KUTENDA HAKI KWA JAMII

Na Dotto Kwilasa, Dodoma

MAKAMU Mkuu wa Chuo kikuu cha St. John's Tanzania (SJUT) Prof. Yohana Msanjila amewataka wanafunzi wanaomaliza muda wao wa masomo chuoni hapo kuzingatia maadili na kutenda haki kwa jamii kupitia taaluma zao.

Amesema hayó mwishoni mwa wiki hii jijini Dodoma katika mahafali ya 12 ya chuo hicho ambapo jumla ya wanafunzi 1248 walitunukiwa vyetu kwa ngazi ya Astashahada,Stashahada ,Shahada na Shahada za uzamili.

Prof. Msanjila amewaambia wanafunzi hao kuwa elimu waliyoipata chuoni hapo ni vema wakaitumia kuleta Maendeleo ya taifa na kwamba kwa kufanya hivyo itakuwa ni sifa nzuri kwa chuo hicho ambacho kinaendana na maadili ya dini.

"Nina furaha kwa kuwa mmemaliza salama,matumaini yangu ni kwamba huko muendako hamuendi kutuaibisha ,hakikisheni mnakumbuka kuitumia elimu nzuri tuliyowatunuku kwa jamii na kukumbuka kwamba ni vema kutoa kuliko kupokea,"amesema Makamu mkuu huyo wa SJUT.

Aidha Prof. Msanjila amesema taswira nzima ya chuo hicho inategemea ubora wa huduma watakayo itoa kwenye jamii katika masuala ya Afya,elimu,Sheria na mengineyo na hivyo kuwataka kupeperusha bendera hiyo kwa kuwa mfano mzuri nchini na duniani kote.

"Mkitenda haki hata jamii itawashukuru na hii ndiyo ahadi mliyoitoa kwenye viapo vyenu kwamba mnaenda kulitumikia taifa kwa moyo wa dhati bila upendeleo wowote na wala kumuonea mtu yoyote,elimu hii ni kichocheo cha ajira na ujasiriamali msiende kujibweteka,"amesisitiza.

Sambamba na hayo amesema kwa zaidi ya miaka 14 chuo hicho kimetengeneza wanafalsafa ,watafiti,wajasiriamali na viongozi mashuhuri na kwamba tunuku hizo ni faida kubwa kwa chuo hicho kwa kuwa inadhihirisha mafanikio .

Naye Mkuu wa Chuo hicho Askofu Mkuu Mstaafu Donald Leo Mtetemela ameeleza kuwa Dodoma ni Jiji linalokua kwa kasi hivyo chuo hicho kinajivunia kuwa sehemu ya ukuaji huo na kuendeleza ushirikiano na vyuo vyote vya elimu ya juu na vya kati.

Katika ujumbe wake alioutoa kwenye hafla ya mahafali hiyo,Askofu huyo amesema"Wahitimu wetu wameenea maeneo mbalimbali,kama Taasisi tunafurahi wakati wote na kuwaombea muwajibike ipasavyo Kwa kuzingatia maadili ya utu wa mtu,"amesema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la chuo hicho (SJUT) Prof. Penina Mlama amesema chuo hicho tangu kimeanzishwa wanafunzi zaidi ya elfu 15 wamehitimu huku akieleza kuwa mchango wa wahitimu wote unaendelea kuboresha hali ya maisha ya watanzania.

Amesema,tangu kuanza kwa chuo hicho, kimefanikisha kuanzisha programu nyingi zikiwemo shahada ya Sanaa na elimu,astashahada ya kilimo,stashahada ya Sheria,shahada ya Benki na fedha,shahada ya uuguzi,shahada ya famasi,shahada ya uzamivu na nyingine nyingi.

"Mwaka huu ni mwaka wa mafanikio kwetu kwa kuwa kati ya wahitimu 1248 ,551 kati yao ni wanawake ambao ni sawa na asilimia 44.2 huku wanaume wakiwa na idadi ya 697 sawa na asilimia 55.8,tunaendeleza zaidi juhudi za kuwawezesha wanawake kupenda kujiendeleza,"amesisitiza.

Ameongeza kuwa mafanikio hayo yamepelekea kupata ithibati ya Tume ya vyuo vikuu (TCU) kwa Miaka na kidhihirisha kuwa elimu inayotolewa hapo inakidhi viwango vya kimataifa.

Aidha amesema katika kuendeleza ari ya kutoa elimu ya viwango vya juu,Chuo hicho kupitia kada ya Sayansi wamenza mchakato wa kuengeneza chanjo ya korona ikiwa ni pamoja na kuboresha maabara za kemia na kuwapa fursa wanafunzi kufanya mazoezi kwa vitendo.

Share:

Boilermaker/Welder at Kilombero Valley Teak Company

The Kilombero Valley Teak Company (KVTC) (www.kvtc-tz.com) in Tanzania is Africa’s largest privately owned teak forest and timber business. It is Tanzania’s biggest exporter of timber products. To enhance this status and improve its performance, KVTC is looking for a suitable candidate for the position of Boilermaker/welder.   This position is for a hands-on skilled […]

This post Boilermaker/Welder at Kilombero Valley Teak Company has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

BENKI YA CRDB YAHITIMISHA MASHINDANO YA “CRDB BANK SUPER CUP” 2021 KWA KISHINDO JIJINI ARUSHA

Mashindano ya CRDB Bank Super Cup 2021 yaliyoshirikisha timu za wafanyakazi wa Idara na Matawi ya Benki ya CRDB nchi nzima, Tanzania Bara na Visiwani, yamehitimishwa leo jijini Arusha ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Abdulmajid Nsekela. CRDB Bank Super Cup mwaka huu ilihusisha michezo ya mpira wa miguu kwa wanaume na mpira wa pete kwa wafanyakazi wanawake.

 Kwa upande wa mpira wa miguu mashindano hayo yalishirikisha timu 16 za mpira wa miguu, kati ya hizo 8 ziliundwa kwa kushirikisha vitengo mbalimbali vilivyopo Makao Makuu ya Benki hiyo, na 8 zingine ziliundwa kutoka katika kanda mbalimbali ambazo zilitokana na Matawi yote ya Benki ya CRDB Tanzania nzima.

Kwa upande wa wanawake timu 8 ziliundwa na kushiriki katika mchezo wa mpira wa pete zikijumuisha timu kutoka Makao Makuu na matawi. Timu zote zilipewa majina yatokanayo na bidha mbali mbali zinazotolewa na Benki hiyoikiwamo, timu za SimBanking, Tanzanite, Hodari, TemboCard, Nia Moja, Ulipo Tupo, nk.

 Akizungumza malengo ya kuanzisha mashindano hayo ya “CRDB Bank Super Cup,” Mkurugenzi Mtendaji wa wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema, dhumuni kubwa la kuanzisha mashindano hayo ikiwa ni pamoja na burudani na kujenga afya ya mwili na akili kwa wafanyakazi, kuimarisha mahusiano baina ya wafanyakazi, pamoja na kuongeza uzalishaji kazini.

 “Tunaamini mashindano haya ni hatua muhimu katika kufikia azma ya kuimarisha afya za wafanyakazi pamoja na kuongeza mshikamano na ushirikiano katika kutekeleza majukumu ya kikazi ili kutoa huduma bora kwa wateja wao. Leo Tunahitimisha mashindano haya kwa mafanikio makubwa ikiwa ni mara ya kwanza mashindano haya kufanyika katika historia ya Benki yetu”. amesema Nsekela. Hitimisho la mashindano hayo liliambatana na utoaji wa zawadi mbalimbali ikiwemo fedha taslimu na makombe kwa washindi mmoja mmoja na timu kwa ujumla. Mshindi wa kwanza alijinyakulia Shilingi Milioni 5 kwa mpira wa miguu na Shilingi Milioni 3 kwa mpira wa pete.

 Benki hiyo pia ilitoa zawadi kwa wachezaji binafsi waliofanya vizuri, ambapo mchezaji bora (Best Player) na mfungaji bora (Top Scorer) walipata Shilingi laki 2, na Shilingi laki 3 ilienda kwa mchezaji bora wa mechi ya fainali.

 Nsekela aliwapongeza wafanyakazi wa Benki hiyo kwa kuitikia wito na kufanikisha mashindano hayo yaliyofana sana na kuleta upinzani baina ya timu shiriki hivyo kuleta chachu ya ubora wa ligi hiyo ya CRDB Bank Super Cup.

 “Huu ni mwanzo, mwaka ujao tutahakikisha tunayaboresha zaidi mashindano haya ikiwa pamoja na kuongeza timu za mpira wa kikapu katika ligi hii na kuongeza zawadi kubwa zaidi za washidi ili kuleta chachu za ushindani,” aliongezea Nsekela.

 Naye Mkurugenzi wa Rasiliamali watu, Siophoro Kishimbo aliwashukuru Wakurugenzi wa Idara, Mameneja wa Kanda na Matawi wa Benki hiyo kwa kutoa ushirikiano wa kutosha na kuwapa wafanyakazi wao ruhusa ya kushiriki katika mashindano hayo. Alisema mashindano hayo yameleta chachu kubwa katika Benki na kuwapa fursa wafanyakazi weke kuonyesha vipaji walivyonavyo.

 Benki ya CRDB imekuwa kwa kipindi kirefu ikiipa michezo umuhimu mkubwa hivyo kufikia kuendesha programu mbalimbali za michezo ikiwamo CRDB Bank Bonanza linalojumuisha timu za wabunge na wizara, CRDB Bank Marathon ambayo mwaka huu imepata usajili wa kimataifa, pamoja na mashindano ya taifa ya mpira wa kikapu “CRDB Bank Taifa Cup” ambayo yalifanyanyika mwezi Novemba mwaka huu yakishirikisha timu za kikapu za mikoa.
Share:

Manager Digital Marketing. at Reliance Insurance Company

Manager Digital Marketing.   The Manager Digital Marketing has the overall responsibility of overseeing all digital strategic communications with external audiences by working closely with the Reliance team to identify and maximize opportunities that will bring the Company mission and achievements to life. This should be achieved through a diverse mix of marketing, advertising, and […]

This post Manager Digital Marketing. at Reliance Insurance Company has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger