Friday, 16 July 2021
RAIS SAMIA AWASILI NCHINI BURUNDI KUANZA ZIARA YA KITAIFA YA SIKU MBILI
MKAKATI WA KOPA MBUZI LIPA MBUZI KUANZA, CHANJO ZA MIFUGO ZATAKIWA VIJIJINI
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akiwa ameshika moja ya aina ya mbuzi wanaozalishwa kwenye Ranchi ya Mkata iliyopo Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogororo mara baada ya kufanya ziara ya kikazi ya siku moja katika ranchi hiyo na kuagiza ranchi hiyo kuendeleza uzalishaji wa mbuzi kwa ajili ya kufuga kibiashara. (Picha na Edward Kondela, Afisa Habari – Wizara ya Mifugo na Uvuvi)
Na. Edward Kondela
Serikali imesema Ranchi ya mifugo ya Mkata iliyopo Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro itakuwa sehemu ya kuzalisha mbuzi kwa wingi kwa ajili ya mkakati wa kopa mbuzi lipa mbuzi ambao unatarajia kuanza hivi karibuni lengo likiwa ni kuwa na mbuzi wa kutosha kwa ajili ya soko la nje ya nchi.
Akizungumza na uongozi wa ranchi na Wilaya ya Kilosa, wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja katika Ranchi ya Mkata, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalllah Ulega amesema ni muhimu kuangalia namna bora ya kufanya ufugaji wa kibiashara katika ranchi hiyo.
Amesema serikali imechagua Ranchi ya Mkata kuwa kituo cha kuzalisha mbuzi kwa wingi ambacho watakuwa wanasambaza katika maeneo mbalimbali nchini.
"Tutakayempa tutataka tujue yupo wapi na ana mbuzi wangapi ili tuwatambue na tuwaingize katika mfumo wetu wa takwimu za kibiashara ili iwapo tunapata mteja wa kilo 50 kwa mwezi kweli tuwe na uhakika wa kupata kilo hizo 50 kwa mwezi.” Amesema Mhe. Ulega
Kutokana na mkakati huo wa kopa mbuzi lipa mbuzi mahitaji ya mbuzi yatakuja kuwa makubwa nchini hivyo ameitaka ranchi hiyo kuzalisha mbuzi kwa wingi ili kuweza kutosheleza soko la ndani na nje ya nchi.
Aidha Mhe. Ulega amesema wafugaji wa mbuzi wafuge kibiashara ili kuweza kutimiza vigezo na masharti ya wateja wa kimataifa kama nchini hizo na kutolea mfano wa nchi za uarabuni ambazo wanataka mbuzi wenye uzito wa kilo kati ya 8 hadi 10 ambao hawajakomaa sana.
Kwa upande wake Meneja wa Ranchi ya Mkata Bw. Oscar Magete amesema ranchi ilianzishwa na serikali kwa madhumuni ya kuendeleza na kueneza ufugaji bora wa mbuzi, kondoo na ng'ombe ambapo ranchi hiyo kwa sasa ina mbuzi 609 kondoo 116 na ng'ombe 47.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri Ulega ametembelea kiwanda cha kuzalisha chanjo cha Nobel Vaccine Bioscience (NOVABI) kilichopo Mkoani Morogoro kinachozalisha chanjo aina ya Tatu Moja kwa ajili ya ya mdondo, ndui ya kuku na mafua ambayo yanaathiri mfumo wa upumuaji na yamekuwa chanzo kikuu cha vifo vya kuku na kuwatia hasara wafugaji.
Akiwa kiwandani hapo Naibu Waziri Ulega ameelekeza chanjo hiyo ya kipekee isambazwe maeneo mbalimbali nchini hususan vijijini ambapo kuna wafugaji wengi wa kuku wa kienyeji ili waweze kuipa mifugo yao chanjo kuondokana na hasara ambayo wamekuwa wakipata ya kuku kufa kutokana na magonjwa hayo.
Ameongeza kuwa ni vyema uongozi wa wizara kuhakikisha chanjo mbalimbali zinazozalishwa ndani na nje ya nchi zinawafikia walengwa hususan waliopo vijijini ili waweze kufuga kibiashara na waweze kunufaika kupitia mifugo yao.
WAZIRI JAFO AUPA 5 MRADI WA UMEME WA JULIUS NYERERE
TGNP YATOA MAFUNZO KWA VITUO VYA TAARIFA NA MAARIFA DAR ES SALAAM, SANGAI ATAKA WATAMBUE RASILIMALI ZA NCHI
Video Mpya : NYANDA MADIRISHA OBHADO 'MALIGANYA' - JIRANI
Video Mpya : NYANDA MADIRISHA OBHADHO 'MALIGANYA' - MITIHANI YA DUNIA
KAY JAY :KUTOKA KUANDIKIA WASANII WENZAKE MPAKA KUWA "ORDINARY GUY"


SERIKALI IWEKE JITIHADA KWENYE KUWEZESHA VIFAA VYA MASOMO YA SAYANSI
Mwalimu wa Taaluma wa Shule ya Sekondari Coastal High School, Isaack Dastan Kifwete akikagua madaftari ya wanafunzi kama inavyoonekana
SERIKALI imeshauri kuweka juhudi kubwa kuwezesha vifaa vya kufundishia ambavyo vitasaidia kuwa na wanasayansi halisi kwa kusoma kwa vitendo ili kuweza kuendana na uchumi wa viwanda.
Iwapo vifaa vya masomo ya sayansi vitakuwepo kwenye shule mbalimbali hapa nchini itawawezesha wanafunzi kuweza kusoma kwa vitendo na hivyo kuongeza ufaulu na hatimaye kuwa na wataalamu wengi
Hayo yalisema na Mwalimu wa Taaluma wa Shule ya Sekondari Coastal High School, Isaack Dastan Kifwete wakati mkutano wao baina yao na waandishi wa habari uliokuwa na lengo la kueleza siri iliyowafanya kung’ara kwenye matokeo ya kidato cha sita 2020/2021..
Shule hiyo imefanya vizuri katika matokeo hayo baada ya Wanafunzi kuwa na ufaulu wa Daraja la Kwanza na Pili tu (Division I na II)yaliyopatikana shuleni hapo na kuifanya kuwa ya kwanza katika wilaya ya Tanga.
Alisema matokeo hayo yamewawezesha kuendelea kuwa shule ya kwanza(Namba 1)katika wilaya ya Tanga mjini huku wakiwa shule ya nne(Namba 4) kwa mkoa wa Tanga.
Aidha alisema mafanikio hayo yamechagiwa na uongozi pamoja na walimu walio bora ikiwemo kujituma bila kuchoka na wanafunzi kuwa na ari katika masomo.
"Kwanza ni ushirikiano kutoka kwa Mkurugenzi wa Shule hii Mathew Marupa kuwa na walimu bora na wanajitoa kwa muda wote hali hii imesaidia kuwezesha kupata matokeo mazuri”Alisema
Alisema pia ni kuwekwa kwa bidii kwenye masomo wanayosimamia pamoja na kuwa na wanafunzi wanaojitambua ambapo pale wanapofika wanapewa malengo ya shule kuwa hautakiwi kufeli unapokua kwenye shule hii"alisema Kifwete.
Aidha alisema kwa miaka minne mfululizo shule hiyo imeendelea kufanya vizuri kwa kuwa wanafunzi wanakuwa katika mazingira bora ya kujifunza na hivyo kupelekea kuelewa kila wanachofundishwa.
Awali akizungumza katika mkutano huo,Mwalimu Msaidizi wa Taaluma Moses Mhina ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Sayansi anafundishi masomo ya Kemia na Biologi alisema matokeo ya kidato cha sita wanakuwa wakifanikiwa kutokana na uwepo wa nidhamu ya hali ya juu ambalo kwao ndio jambo la kwanza kabla ya taaluma.
Alisema wanafunzi wanapofika shuleni jambo la kwanza ni nidhamu,la pili ni ushirikiana kati ya walimu na wafanyakazi wengine,kujitoa ni jambo ambalo ni kubwa sana kwao na wakati mwengine kufanya kazi nje ya muda wa kazi na kuwafundisha wanafunzi kwa waledi ambao unawatengenezea ujasiri.
“Lakini pia ushirikiano walimu na watu wa nje ambao sio walimu hasa wazazi na walezi kwa sababu kunaweza kutokea changamoto ya utoro lakini tunapokutana na wazazi na kuwaeleza utoro unavyokwamisha matokeo mazuri na hivyo wao kutupa ushirikiano “Alisema
Alisema siri nyengine ambayo imewasaidia wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi kufanya vizuri ni kuwatengenezea mtazamo chanja unajua kwenye malezi wanayolelewa mtu tangia akiwa mdogo anasikia habari kwa kaka zake kwamba sayansi ni ngumu lakini wao wanafunzi wanapofika shuleni wanawaelezwaa namna wanavyuoweza kufanya masomo hayo bila woga na hivyo kuwafundisha wanafunzi kwa vitendo .
Mwalimu huyo alieleza kwamba hatua inayoondolea woga kwao na hivyo kuwajengea namna ya kujiamini na kumtengeneza ujasiri wa kujibu maswali na hivyo kuwawezesha kufanya vizuri wanapokuwa kwenye mitihani yao.
“Lakini pia tumekuwa tukifanya ziara ya kutembelea kwenye viwanda na hivyo kuona namna sayansi inayoweza kufanya kazi na hivyo kuwawezesha wanafunzi kupata uelewa mpana “Alisema
Hata hivyo pia siri nyengine ni wao kujitahidi kufundisha kwa waledi na kutoa mazoezi ya kutosha kwa wanafunzi yanayowapa ujasiri wa kutambua mambo mengi na hivyo kuwawezesha kutimiza ndoto zao za kufanya vizuri.


























