Friday, 17 April 2020

Baraza la Maaskofu -TEC lasitisha Uimbaji kwenye Ibada za misa Ili Kukabiliana na Corona

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania ‘TEC’ limetoa tamko kutekeleza agizo alilotoa Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa Aprili 15, juu ya kujilinda na  Corona kwenye masuala ya ibada

TEC imeamua kusitisha mazoezi ya kwaya ili kuepuka mikusanyiko. Pia nyimbo wakati wa ibada zimesitishwa ili Ibada isitumie muda mrefu

Pia mafundisho ya dini kwa watoto na makundi mengine yamesitishwa. Mafundisho yataendelea kwa njia nyingine kama kujisomea katekisimu au njia ya mtandao

Pia kanisa litazingatia umbali wa mtu na mtu wanapokuwa ibadani, matumizi ya vinasa sauti, watanawa mikono kabla ya kuingia kanisani pia watanyunyizia dawa vifaa vya ibada


Share:

Kampuni Ya Barrick Buzwagi Yatoa Vifaa Vya Kujikinga Na Ugonjwacorona Shinyanga Vyenye Thamani Yashilingi Milioni 48

SALVATORY NTANDU
Katika jitihada za kukabiliana na Maambukizi ya  Ugonjwa uanaosababishwa na virusi vya Corona mkoani Shinyanga, Kampuni ya uchimbaji madini ya Dhahabu ya Barrick Buzwagi imekabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya Shilingi  Milioni 48 kwa mkuu wa mkoa huo Bi Zainab Tellack ili kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya virusi hatari vya COVID 19.

Akikabidhi vifaa hivyo Aprili 18 mwaka huu,wilayani Kahama kwa Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Bi Zainab Tellack niaba ya Kampuni ya Barrick Buzwagi Mkuu wa Kitengo cha Usalama na Afya Kazini Mgodi wa Barrick Buzwagi, Dk. Antoinette George amesema kuwa  msaada huo umejumuisha makontena 25 ya kunawia mikono kwa mkoa wa Shinyanga na 30 kwa wilaya ya Kahama, Chroline ndoo tano zenye kilogramu 45 kila moja, gloves pea 50 zitakazotumika kwa watoa huduma, Barakoa (mask) 400, Chemical Suits 40, chemical googles 40 na vipimia joto saba.

Amefafanua kuwa vifaa hivyo  vitatumika katika maeneo yenye mikusanyiko ya watu wengi mkoani humo  hususani katika  Masoko, Minada, Vituo vya Mabasi, Magerezani, pamoja na  Vituo vya Afya ili kuwakinga wananchi dhidi ya janga la kidunia la Ugonjwa  COVID 19.

“Sisi kama Barrick tumetoa   magari manne ya kutoa elimu juu ya ugonjwa huu hatari wa COVID 19 ambayo yatatoa  matangazo  katika maeneo mbalimbali mkoani Shinyanga kwa muda wa miezi miwili sambamba na  kutoa mafunzo kwa maofisa afya 204 kwenye vijiji vyote wilayani Kahama”, alisema Dk George..

Awali  akipokea vifaa hivyo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Bi  Zainab Telack ameishukuru Kampuni ya Barrick Buzwagi kwa msaada huo ambao utasaidia kuongeza nguvu katika mapambano dhindi ya Ugonjwa huu na kuwataka wananchi pindi vifaa hivyo vitakapowekwa kwaajili ya matumizi ni budi wananchi wakazingatia maelekezo ya Serikali ili kujikinga  na COVID 19. 

Mbali na hilo Bi  Tellack ametoa onyo kali kwa wananchi mkoani humo kuacha kutoa taarifa za uongo kuhusiana na ugonjwa huo huku akitolea mfano tukio la kukamatwa kwa mkazi  Mwakitolyo , Mussa Kisinza aliyempigia Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akimdanganya kuwa  anaugonjwa wa COVID 19

"Serikali itaendelea kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wotw watakaobainika kusambaza taarifa uongo kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na ugonjwa huu tutahakikisha tunawashughulikia wote wanaoleta mizaha tunahitaji wananchi wetu wabaki salama na janga hili”,alisema Tellack.

Kwa upande wake  Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Anamringi Macha alisema kuwa  katika wilaya ya kahama kuna  mwingiliano mkubwa wa watu na uwepo wa mabasi mengi ya abiria yanayoanzia safari zake mjini hapo kuelekea mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Bukoba, Arusha na Kilimanjaro na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa COVID 19.

Amefafanua kuwa   wameendelea kuchukua tahadhari katika maeneo yote yenye mikusanyiko na wananchi wameonyesha mwitikio kwa kuunga mkono jitihada hizo za serikali isipokuwa bado changamoto ipo kwa waendesha pikipiki (bodaboda) na wamiliki wa Baa ambao hawataki kufuata maelekezo ya serikali.

Mwisho.


Share:

Serikali Yaboresha Huduma Ya Afya Uyui

Na Frank Mvungi- MAELEZO
Serikali ya Awamu ya Tano imetimiza ndoto ya wananchi wa Wilaya ya Uyui, mkoani Tabora kufikiwa na huduma bora za afya katika maeneo yao.

Akizungumza katika mahojiano maalum wilayani humo, Mkuu wa Wilaya, Gift Msuya amesema kuwa kwa sasa wananchi wa wilaya hiyo wanafikiwa na huduma za afya kupitia vituo vya afya vilivyojengwa na vile vilivyoboreshwa katika kipindi cha miaka mine iliyopita.

“ Tumekamilisha ujenzi wa Hospitali ya Wilaya iliyogharimu Shilingi bilioni 1.5 na iko tayari kuanza kutoa huduma baada ya kuwasili kwa vifaa, hili linaenda sambamba na utoaji wa huduma katika vituo vyetu vya afya ambavyo vinatoa huduma zinazoendana na mahitaji ya wananchi,” alisisitiza Msuya

Aidha, Msuya amesema kuwa Serikali ilitoa milioni 500 zilizowezesha kuboreshwa kwa Kituo cha Afya Upuge na pia shilingi milioni 400 zimetumika katika ujenzi wa Kituo cha Afya Igalula.
 
Kuwepo kwa huduma bora na vifaa vya kisasa kumewezesha Wilaya ya Uyui kutokuwa na vifo vya akinamama wanaopatwa na uchungu pingamizi kwa kuwa sasa huduma ya upasuaji inapatikana karibu na walipo wananchi tofauti na ilivyokuwa awali.

Naye Kaimu Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Upuge, Sr. Dkt. Yustina Raphael amesema kuwa tangu kuanza kwa huduma ya upasuaji kwa akinamama zaidi ya akinamama 100 wamefanyiwa upasuaji kwa ufanisi.

“Jukumu letu ni kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi kupitia kituo hiki cha Upuge kwa kuwa kimeboreshwa na kina vifaa vya kisasa vya kutolea huduma ikiwemo vya maabara na vya kufanyia upasuaji,” alisisitiza Sr. Dkt. Yustina

Awali, kabla ya maboresho ya kituo hiki kilichoanza mwaka 1977 kilikuwa na huduma chache na kwa sasa kimeongeza huduma kama za maabara, upasuaji, mama na mtoto na pia watumishi wameongezwa ili kuendana na mahitaji.

Akizungumzia kuhusu rufaa katika Kituo hicho, Sr. Dkt. Yustina amesema kuwa baada ya maboresho rufaa za wagonjwa zimepungua kwa kiwango kikubwa na hivyo kuwapunguzia wananchi adha ya kutembea umbali mrefu au kusafiri kufuata huduma
za afya.

Kwa upande wake mmoja wa wagonjwa waliofika kupata huduma katika kituo hicho, Bi. Salma Ramadhani aliwapongeza watoa huduma wa kituo cha afya Upuge kwa utendaji bora na wenye tija kwa wananchi wote wanaofika kupata huduma kituoni hapo.

“Tunamshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kuboresha sekta ya afya hasa vituo vyetu vya afya kama hiki cha Upuge kwa sasa tunapata huduma za upasuaji hapa na wahudumu wa hapa wakiwemo madaktari wanatuhudumia vizuri na mazingira yameboreshwa kupitia majengo mapya na vifaa vya kisasa kabisa”, alisisitiza Salma.

Akifafanua amesema kuwa amefanikiwa kujifungua salama kutokana na huduma bora zilizopo katika kituo hicho hali inayowafanya akinamama kuondokana na adha ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma hizo.

Serikali ya Awamu ya Tano imefanikiwa katika kuimarisha huduma za afya ikiwemo ujenzi wa vituo vya afya, hospitali za wilaya, zahanati, ujenzi wa hosptali za rufaa za Mikoa na Kanda na pia upatikanaji wa dawa na vifaa tiba imekuwa chachu ya kuboreshwa kwa huduma katika wilaya na mikoa yote hapa nchini.


Share:

Wagonjwa Wa Corona Kenya Wafika 246....Ni Baada ya Wengine 12 Kuongezeka Leo

Kenya imetangaza kuwa na wagonjwa 246 wa corona baada ya kuthibitisha watu 12 wapya wameambukizwa virusi vya ugonjwa wa Covid 19.

Katika taarifa waziri wa afya wa Kenya Mutahi Kagwe, amesema watano kati ya wale walioambukizwa virusi vya corona ni wahudumu wa hoteli na kuongeza kuwa idadi hiyo ilifikiwa baada ya jumla ya sampuli 450 kufanyiwa uchunguzi.

Jana Rais Uhuru Kenyata alitangaza hatua zifuatazo kukabiliana na Corona nchini humo.

1.Wizara ya Afya na huduma za umma itaanzisha hazina ya kuwasaidia wafanyakazi wa Afya wanaokabiliana na mlipuko wa virusi vya corona


2.Wizara ya elimu itachukua hatua kuwalinda wanafunzi kutokana na athari mbaya za hatua zilizochukuliwa kukabiliana na Covid-19


3.Mamlaka ya usambazaji wa tiba nchini Kenya itaondoa masharti ya ununuzi wa vifaa vya kujilinda dhidi ya Covid-19 kwa takriban miezi mitatu ili kurahisishia kaunti kununua vifaa hivyo.


4.Nyumba za watu wasiojiweza jijini Nairobi zitapewa msaada wa fedha na serikali kusaidia familia zisizojiweza


5.Bunge litapitisha tena mapendekezo na miswada kuhusu vichocheo vya uchumi.


6.Polisi atakayekiuka sheria wakati anatekeleza hatua za kukabiliana na usambaaji wa virusi atakabiliwa na mkono wa sheria.
 


Share:

Picha : MGODI WA BARRICK BUZWAGI WATOA MSAADA WA VIFAA KUKABILIANA NA CORONA SHINYANGA


Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akiishukuru Kampuni ya Barrick kwa kuiunga mkono serikali katika kukabiliana na ugonjwa wa Corona. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Afya na Usalama mgodi wa Barrick Buzwagi, Dkt. Antoinette George.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Dhahabu ya Barrick kupitia Mgodi wa Buzwagi uliopo wilayani Kahama imetoa msaada vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 48 kwa ajili ya kujikinga dhidi ya maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona ‘Covid 19’ katika mkoa wa Shinyanga.

Vifaa hivyo vimekabidhiwa leo Ijumaa Aprili 17,2020 na Mkuu wa Kitengo cha Afya na Usalama mgodi wa Barrick Buzwagi, Dkt. Antoinette George kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack.

Dkt. Antoinette amevitaja vifaa walivyotoa kuwa ni pamoja na Matanki ya kuoshea mikono ‘washing container set’ 88,goggles 40,Impermiable suits 40,Barakoa (face masks) 400, Vipimia joto (contact less thermometer) 6, Hand wash unit,Chlorine powder na chemical gloves jozi 50.

Dkt. Antoinette amesema Kampuni ya Barrick iko bega kwa bega na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona ndiyo maana imechangia vifaa hivyo ili kuwakinga wananchi dhidi ya Corona.

“Kinga ni bora kuliko tiba .Tumekabidhi vifaa vya kujikinga na Corona kwa Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack ili vikatumike kukabiliana na Corona katika maeneo yenye mikusanyiko ya watu ikiwemo masoko,vituo vya mabasi,minada,vituo vya afya na tutaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu ugonjwa wa Corona”,amesema Dkt. Antoinette.

“Leo tumekabidhi vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 48 lakini Kampuni ya Barrick imetoa jumla ya shilingi Bilioni 4 zingine kukabiliana na Corona nchini Tanzania ambapo mkoa wa Shinyanga umetengewa shilingi milioni 600”,ameongeza Dkt. Antoinette.

Akipokea vifaa hivyo,Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack ameishukuru Kampuni ya Barrick kwa kuiunga mkono serikali katika kukabiliana na ugonjwa wa Corona huku akibainisha kuwa ni jukumu la kila mwananchi kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo.

“Tunawashukuru sana Barrick Buzwagi kwa mchango wenu,tutavigawa vifaa hivi katika maeneo mbalimbali mkoani Shinyanga ili kama atapatikana mgonjwa basi tuweze kuokoa maisha ya mgonjwa.Maandalizi haya tunayafanya kama binadamu lakini tuendelee kumuomba Mungu atuepushie ugonjwa huu na tuwaombee waliopata maambukizi wapone ili maambukizi yasiwepo”,amesema Telack.

“Kila mtu achukue tahadhari,kunawa mikono maji safi yanayotiririka na sabuni ndiyo silaha yetu kubwa, ambayo tunajivunia, nawa ukiwa nyumbani, nawa ukiwa katika biashara zako,nawa ukiwa kazini,nawa kila wakati” ,amesema

Hata hivyo Mkuu huyo wa mkoa amewataka wananchi kuendelea kutoa taarifa za wageni wanaofika katika maeneo yao huku akisisitiza kuwa serikali itaendelea kuwachukulia hatua za kisheria watu wanaoleta mzaha kuhusu ugonjwa wa Corona.

Naye Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha amesema sasa wananchi wengi wana muamko wa kutosha kuhusu ugonjwa wa Corona na kwamba changamoto bado ipo kwenye maeneo ya Baa na Klabu ambazo zinaendelea kukusanya watu pamoja na waendesha bodaboda wanaopakiza watu zaidi ya mmoja ‘mishikaki’.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Afya na Usalama mgodi wa Barrick Buzwagi, Dkt. Antoinette George akizungumza wakati akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack (kushoto) msaada vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 48 kwa ajili ya kujikinga dhidi ya maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona ‘Covid 19’ katika mkoa wa Shinyanga leo Ijumaa Aprili 17,2020. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog 
Mkuu wa Kitengo cha Afya na Usalama mgodi wa Barrick Buzwagi, Dkt. Antoinette George akizungumza wakati akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack (kushoto) msaada vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 48 kwa ajili ya kujikinga dhidi ya maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona ‘Covid 19’ katika mkoa wa Shinyanga.
Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Afya na Usalama mgodi wa Barrick Buzwagi, Dkt. Antoinette George akivitaja vifaa vilivyotolewa na Barrick Buzwagi kukabiliana na Ugonjwa Corona mkoani Shinyanga kuwa ni Matanki ya kuoshea mikono ‘washing container set’ 88,goggles 40,Impermiable suits 40,Barakoa (face masks) 400, Vipimia joto (contact less thermometer) 6, Hand wash unit,Chlorine powder na chemical gloves jozi 50. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akinawa mikono katika moja ya Matanki 88 yaliyotolewa na Mgodi wa Barrick Buzwagi yatakayowekwa katika maeneo yenye mikusanyiko ya watu wengi ikiwemo Vituo vya mabasi,minada,sokoni na vituo vya afya. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Afya na Usalama mgodi wa Barrick Buzwagi, Dkt. Antoinette George.
Mkuu wa Kitengo cha Afya na Usalama mgodi wa Barrick Buzwagi, Dkt. Antoinette George  akinawa mikono katika moja ya Matanki 88 yaliyotolewa na Mgodi wa Barrick Buzwagi yatakayowekwa katika maeneo yenye mikusanyiko ya watu wengi ikiwemo Vituo vya mabasi,minada,sokoni na vituo vya afya.
Mkuu wa Kitengo cha Afya na Usalama mgodi wa Barrick Buzwagi, Dkt. Antoinette George akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack (kushoto) vifaa kwa ajili ya kujikinga dhidi ya maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona ‘Covid 19’ katika mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Kitengo cha Afya na Usalama mgodi wa Barrick Buzwagi, Dkt. Antoinette George akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack (kushoto) vifaa kwa ajili ya kujikinga dhidi ya maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona ‘Covid 19’ katika mkoa wa Shinyanga. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha.
Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Afya na Usalama mgodi wa Barrick Buzwagi, Dkt. Antoinette George akizungumza wakati akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack (kushoto) vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 48 kwa ajili ya kujikinga dhidi ya maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona ‘Covid 19’ katika mkoa wa Shinyanga. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akiishukuru Kampuni ya Barrick kwa kuiunga mkono serikali katika kukabiliana na ugonjwa wa Corona. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Afya na Usalama mgodi wa Barrick Buzwagi, Dkt. Antoinette George.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akionya kuhusu watu wanaoleta mzaha kuhusu Ugonjwa wa Corona na kubainisha kuwa serikali haitasita kuwachukulia hatua za kisheria.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akisisitiza umuhimu wa kila mwananchi kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha akielezea hatua zinazoendelea kuchukuliwa na serikali wilayani Kahama katika kukabiliana na maambukizi ya Virusi vya Corona ikiwa ni pamoja na kusititiza wananchi kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni lakini pia kuepuka mikusanyiko ya watu.
Meneja wa Mahusiano na Maendeleo ya Jamii mgodi wa Barrick Buzwagi, Siama Paul akielezea namna mgodi huo unavyoshiriki katika mapambano dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona ambapo amesema wamekuwa wakisambaza vifaa vya kujikinga na ugonjwa wa Corona,kutoa elimu kwa jamii kwa njia ya matangazo ya gari (Public Advertisement PA) na kutoa semina kwa watoa huduma za afya.
Meneja wa Mahusiano na Maendeleo ya Jamii mgodi wa Barrick Buzwagi, Siama Paul akielezea Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack namna mgodi wa Buzwagi unavyoshiriki katika mapambano dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona ambapo amesema wamekuwa wakisambaza vifaa vya kujikinga na ugonjwa wa Corona,kutoa elimu kwa jamii kwa njia ya matangazo ya gari (Public Advertisement PA) na kutoa semina kwa watoa huduma za afya. Wa pili kushoto ni Afisa Mahusiano mgodi wa Barrick Buzwagi Blandina Munghezi.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akimpima kiwango cha joto la mwili Mhe. Anamringi Macha (kulia).
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akimpima kiwango cha joto la mwili Meneja wa Mahusiano na Maendeleo ya Jamii mgodi wa Barrick Buzwagi, Siama Paul (kushoto).
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Share:

Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA) Yatoa Tahadhari Ya Mvua Kubwa

Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA), imetoa tahadhari ya kunyesha kwa Mvua kubwa ndani ya siku nne kuanzia leo Aprili 17, 2020.

Tahadhari hiyo imetolewa jana Alhamisi Aprili 16, 2020 jijini Dar es Salaam na Meneja wa Kituo  Kikuu cha Utabiri wa Mamlaka hiyo, Samwel Mbuya  ambae amesema amesema mvua hiyo ya siku nne inatarajia kunyesha kuanzia ya April 17 hadi 20 mwaka huu.

Aidha ametaja maeneo yanayotarajia kupata vipindi vya mvua kubwa ni pamoja na Mkoa wa Pwani ,Kisiwa cha Mafia ,Tanga, Dar es Salaam pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.


Share:

Watu 4591 Wafariki Kwa Corona Nchini Marekani Ndani Ya Masaa 24 Yaliyopita

Chuo Kikuu cha Johns Hopkins nchini Marekani kimetangaza kuwa karibu watu 4,591 wamefariki dunia katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita kutokana na virusi vya Corona na hivyo kufanya idadi ya waliokufa kwa ugonjwa huo nchini Marekani kufika 34,641.

Aidha taarifa mpya iliyotolewa na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins imesema kuwa katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita karibu watu elfu 30 wengine wameambukizwa virusi vya Corona nchini humo. 


Share:

National Project Coordinator – NOB (DC) at International Labour Organization Tanzania

National Project Coordinator – NOB (DC) at International Labour Organization Tanzania Grade: NOB Vacancy no.: DC/DAR/NO/2020/2 Publication date: 16 April 2020 Application deadline (midnight local time in Dar es Salaam, Tanzania): 14 May 2020 Job ID: 3230 Department: RO-Africa Organization Unit: CO-Dar es Salaam Location: Dar es Salaam Contract type: Fixed Term Contract duration: 1 Year Under article 4.2, paragraph (e) of the Staff Regulations, the… Read More »

The post National Project Coordinator – NOB (DC) at International Labour Organization Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Madson property limited, Inakuletea mkopo nafuu kabisa wa viwanja na mashamba usio kuwa na riba wala dhamana yoyote ile

HII NI OFA KABAMBE KWA WATEJA WETU. WATEJA 50 WA MWANZO WATAPATA PUNGUZO.

SAFARI ZA KWENDA KUONA VIWANJA ZITAANZIA OFISINI KWETU MWENGE TOWER MAPEMA SAA TATU KAMILI MPAKA SAA NNE NA NUSU JUMAMOSI HII YA TAREHE 18/04/2020


Share:

Marufuku Waganga Wa Jadi Kupokea Wagonjwa Wasio Na Ripoti Za Hospitali

Katika jitihada za kupambana na Ugonjwa wa Corona, Chifu wa Mkoa wa Songwe Mbeshena Nzunda ametoa marufuku kwa waganga wa jadi kupokea mgonjwa yeyote ambaye hana ripoti itakayo onyesha tatizo husika limeshindwa kutatuliwa hospitalini.

Chifu Nzunda amebainisha hayo katika kikao cha Kamati ya Amani ya Mkoa ilipokutana kujadiliana hatua zaidi za tahadhari zinazo paswa kuchukuliwa na Mkoa wa Songwe ili kupambana na ugonjwa wa Virusi vya Corona.

Amesema ili mgonjwa apate matibabu kwa mganga wa jadi anapaswa kuonyesha ripoti kuwa baada ya kutibiwa hospitalini hakupona na  wataalamu wa afya wathibitishe hilo pia waganga wa jadi wenye wateja wengi wanapaswa kuwahudumia kwa awamu ili kepusha msongamano.

Chifu Nzunda ameeleza kuwa waganga wa jadi wanatakiwa nao kuchukua tahadhari za Ugonjwa wa Corona kwa kunawa mara kwa mara kwa maji tiririka na sabuni pia kuweka maji hayo kwa ajili ya wateja watakao wahudumia.

Ameogeza kwa kuwataka watumiaji wa pombe za kienyeji kuhakikisha hawachangii vyombo vya kunywea pombe kama ilivyo zoeleka bali kila mmoja awe na chombo chake pia wauzaji  pombe hizo wachukue tahadhari kwa kuweka  maji ya kunawa pia kupunguza misongamano.

Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa wa Songwe Sheikh Hussein Issa amesema kamati hiyo imekubaliana kuchukua baadhi ya hatua ikiwa ni kuongeza tahadhari Zaidi ya Ugonjwa wa Corona huku Uongozi wa Mkoa ukipongezwa kwa jitihada zilizochukuliwa hadi sasa hakuna mgonjwa wa Corona.

Sheikh Issa amesema kuanzia sasa watoto wasiruhusiwe kushiriki katika nyumba zozote za ibada ili kuwaondoa katika hatari ya maambukizi ya Corona pia wazazi wahakikishe watoto wanabaki majumbani.

Ameongeza kuwa nyumba zote za ibada zisiruhusu waumini wengi kujaa bali waingie wachache na wakae mbalimbali bil kusongamana pia maji tiririka ya kunawa na sabuni au vitakasa mikono  viwekwe ndani na nje ya nyumba hizo za Ibada.

Sheikh Issa amesema viongozi wote wa dini mbalimbali wanapaswa kuchukua tahadhari juu ya Ugonjwa wa Corona kwa kufuata maelekezo ya Serikali pia wasiache kumuomba Mungu ili ugonjwa wa Corona usilete maafa katika Nchi ya Tanzania.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela ameipongeza kamati hiyo kwa hatua hizo za tahadhari ya Corona huku akimuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Songwe kuhakikisha anatoa elimu ya tahadhari ya Corona katika nyumba zote za Ibada.


Share:

NFRA Kuanza Kununua Mahindi, Mtama Na Mpunga-milton Lupa

Serikali kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) imeanza kujipanga kuanza kununua mazao ya nafaka kwa wakulima ili punde tu mazao yatakapovunwa shambani yaweze kununuliwa na kuhifadhiwa kwa ajili ya akiba ya chakula.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Ndg Milton Milos Lupa amemuhakikishia katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo ya Kilimo Ndg Jerald Kusaya wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja NFRA Makao makuu Jijini Dodoma kuwa tayari wataalamu wapo mikoani kwa ajili ya kazi hiyo.

Lupa amesema kuwa msimu wa kilimo wa mwaka 2019/2020 NFRA itanunua mazao makuu matatu ambayo ni zao kuu la chakula Mahindi, Mpunga na Mtama.

Amesema kuwa lengo la serikali kuamua kununua mazao hayo matatu ni kujiimarisha vyema katika uhifadhi wa chakula ili inapotokea dharula ya chakula nchini kuwe na hifadhi ya mazao tofauti tofauti.

Akizungumzia lengo la Wakala kuanza kujipanga ili kununua nafaka mapema, amesema kuwa lengo la kufanya hivyo ni kupata mazao bora kwa ajili ya kuhifadhi kadhalika kupata mazao mengi.


Share:

Sekta binafsi Tanzania inavyosaidia kupambana na homa ya kirusi cha Corona

Katika siku za karibuni kumekuwa na habari nyingi kuhusu hatua mbalimbali zinazochukuliwa kupambana na kuenea kwa homa ya kirusi cha corona. 

Wiki hii serikali ya Tanzania imetangaza mpango kujenga hospitali ya kupambana na magonjwa ya mlipuko kama homa hii ya kirusi cha corona. Hospitali hiyo inayokadiriwa kuwa itagharimu shilingi bilioni 7 za Kitanzania inatarajiwa kumalizika ndani ya miezi sita. 

Mbali na hilo, ni faraja kubwa kuona nchi mbalimbali zinakuja pamoja kuhakikisha maisha yanaendelea na adui huyu wa maradhi haya anashindwa. Kwa mfano Jumuiya ya SADC imezisihi nchi washirika zenye bandari kuweka mkakati kuhakikisha bandari hizo zinaendelea kufanya kazi zikisaidia pia nchi zisizo na bandari kuendelea kupokea mizigo yao kama dawa, vyakula na kadhalika.  

Huku serikali na wadau wengine wakiendelea kufanya kila wawezalo, imekuwa pia jambo jema kuona sekta binafsi nchini Tanzania akishiriki katika vita hii dhidi ya kirusi cha corona.  

Mfano kampuni ya Oryx Gas imetoa gesi ya kupikia yenye thamani ya shilingi milioni 25 kwa mahospitali na vituo vya afya. Kampuni ya Puma Energy yenyewe imetoa 50,000 kuwezesha gari za kubeba wagonjwa na zile za kubeba madawa. 

Mitandao ya simu nayo haiko nyuma. Kampuni kama Tigo Tanzania pamoja na mambo mengine inasaidia wenye biashara ndogo na za kati kuwa na mtandao imara wa intaneti kuendelea kufanya biashara na mawasiliano muhimu yanayohitaji data kama mikutano, kuuza bidhaa, kutangaza bidhaa na kufanya malipo. Hii inasaidia wanaotaka kufanya kazi wakiwa nyumbani kufanya hivyo huku wakifurahia intaneti kutoka Tigo na router ya bure nayo toka Tigo.  

Tuko kwenye changamoto kubwa kama taifa na juhudi za sekta binafsi kama hizi na za ziada zinasaidia sana jamii na serikali yetu katika kupambana na kuvuka msimu huu tukiwa imara. Tuendelee kushirikiana katika vita hii. Siku njema na angavu zinakuja.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa April 17





















Share:

Thursday, 16 April 2020

Wagonjwa Wa Corona Nchini Kenya Wafika 234....Ni Baada ya Wengine 9 Kuongezeka Leo

Idadi ya wagonjwa wa virusi vya coronavirus nchini Kenya  sasa imefikia 234 baada ya watu 9 zaidi kuthibitishwa kuambukizwa ugonjwa huo.

Hayo ni kwa mujibu wa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ambaye amelihutubia taifa hilo leo Alhamisi  April 16 akiwa Ikulu ya Nchi hiyo.

Kenyatta amesema kwamba serikali ilipima sampuli zingine 704 kwa muda wa saa 24 zilizopita na ndipo hao  watu  tisa wakathibitishwa kuugua. 

Uhuru pia amesema idadi ya watu 53 wamepona kabisa na kuruhusiwa kwenda nyumbani tangu janga hili lilipotangazwa kuingia nchini humo

Aidha ametangaza kuwa watu 11 wamepoteza maisha yao, wengine 1,000 wakisalia karantini na wengine 156 wakitengwa katika sehemu mbalimbali nchini humo.


Share:

Wakuu wa nchi 20 zenye nguvu kiuchumi wakubaliana kusamehe kwa muda madeni ya nchi masikini duniani ili Ziweze Kukabiliana Na Corona

Wakuu wa nchi 20 zenye nguvu kiuchumi na zinazoinukia kiuchumi duniani, G20 wamekubaliana kusamehe kwa muda madeni ya nchi masikini duniani. 

Mawaziri wa fedha na magavana wa benki kuu wa G20 wamesema wanaunga mkono kusimamisha kwa muda malipo ya madeni kwa nchi hizo ambazo zinahitaji kuvumiliwa. 

Uamuzi huo umefikiwa jana katika mkutano wao uliofanyika kwa njia ya video. 

Muda huo unaanza Mei Mosi hadi mwishoni mwa mwaka 2020 na deni kuu pamoja na malipo yote ya riba yatasimamishwa. 

Mkurugenzi wa Shirika la Fedha Duniani, IMF Kristalina Georgieva ameupongeza uamuzi huo.

 Katika taarifa yao ya pamoja IMF na Benki ya Dunia zimesema zimefurahishwa na hatua hiyo ya G20 ya kuitikia wito wao wa kiziruhusu nchi masikini duniani ambazo ziliomba kuvumiliwa na kusimamishwa kwa muda ulipaji rasmi wa madeni yao kuanzia tarehe moja ya mwezi Mei.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger