Tuesday, 14 April 2020

FULL POWER , ZATI 50 SULUHISHO LA KUDUMU NGUVU ZA KIUME NA UUME MDOGO



Sababu za upungufu wa nguvu za kiume na maumbile madogo ya uume


⇒Ngiri,

⇒Henia

⇒Kisukari

⇒Tumbo kujaa gesi

⇒Kutopata choo vizuri

⇒Utumiaji madawa kwa muda mrefu

⇒Unywaji wa pombe kupita kiasi

⇒Msongo wa mawazo 



⇮⇒Haya yote hupelekea mwili kutokuzalisha homoni ya gesrtogine au kuwa chache na kushindwa kupata mzunguko mzuri wa damu na vichocheo vingine kama madini ya zinki ambayo hukufanya kuwa na msisimko  na kufanya kuwa na muda  mrefu na nguvu za kutosha.


FULL POWER

⇨Ni dawa ya vidonge ya miti shamba inaongeza nguvu za kiume na kutibu kabisa tatizo hilo.

⇨Inaongeza hamu ya tendo la ndoa
⇨Inakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya Dakika 30 na kurudia tendo zaidi ya mara nne na zaidi.

Zati 50

⇨ Inarutubisha maumbile ya uume  na kunenepesha urefu nchi 6,unene sentimita 4

⇨Dawa hii ni ya kutibu kabisa tatizo hilo.

Pia tunatibu Magonjwa mengine Kama

Matatizo ya pumu,Bawasiri, vidonga vya tumbo,Kisukari,Magonjwa sugu ya zinaaa,Kaswende,U.T.I , kiuno,miguu kuwaka moto, Fangasi sehemu za Siri, kupunguza unene wa mwili,tumbo kuunguruma,kujaa gesi, matatizo ya uzazi kwa wanawake, kurutubisha mbegu za uzazi kwa akina baba, matatizo ya meno tunatibu bila kungoa

Kliniki yetu inapatikana Zanzibar, Dar es salaam na Shinyanga.

Wasiliana nasi kwa simu namba 071770 22 27
Share:

BIBI ALAZWA HOSPITALI BAADA YA KUBAKWA NA VIJANA AKITOKA KUTAFUTA TUMBAKU

Na Anthony Mayunga, Mwananchi 
Polisi wilayani Serengeti mkoa wa Mara wamemkamata mtuhumiwa mmoja kati ya wawili wanaodaiwa kumbaka mama mmoja mwenye umri wa miaka 58, mkazi wa Miseke ambaye amelazwa hospitali Teule ya Nyerere kwa ajili ya matibabu.
Tukio hilo linadaiwa kutokea Aprili 6,2020 usiku katika kitongoji cha Senta wakati mama huyo (jina limehifadhiwa), mkazi wa kitongoji cha Majengo akitoka kutafuta tumbaku na mboga na inadaiwa watuhumiwa walimfuatilia kwa nyuma na kumkaba na kumfanyia ukatili huo.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara, Daniel Shillah aliliambia Mwananchi kwa njia ya simu jana kuwa mtuhumiwa Kumari Mongita (23) mkazi wa kijiji cha Miseke amekamatwa na mmoja wanaendelea kumtafuta kwa kuwa alikimbia.

“Watuhumiwa walitajwa na mama huyo aliyefanyiwa ukatili na vijana hao, huyo mmoja kwa ushirikiano na wananchi tunaamini atakamatwa ili wafikishwe mahakamani baada ya taratibu kukamilika,” alisema .

Mganga mkuu wa hospitali ya Nyerere, Tanu Warioba alidai mama huyo ana maumivu kifuani na sehemu nyingine za mwili.
Share:

Manager, Client Coverage at Stanbic Bank Tanzania Dar es Salaam, Tanzania

Job Details Client Coverage – Corporate & Investment Banking Job Purpose Define and execute strategic client plans that will ensure the development of strong business relationships and the delivery of profitable and integrated Standard Bank products and services, with the purpose of ensuring client profitability, increased revenue, risk optimisation and consistent service delivery. Client strategic plan development &… Read More »

The post Manager, Client Coverage at Stanbic Bank Tanzania Dar es Salaam, Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa Apokea Msaada wa Sh. Milioni 500 Kukabili Corona

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea hundi ya mfano ya sh. milioni 500 kutoka kampuni ya Export Trading Group (ETG) zikiwa ni msaada kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa wa homa ya mapafu unaotokana na maambukizi ya virusi vya corona (COVID-19) nchini.

Waziri Mkuu amepokea msaada huo leo (Jumanne, Aprili 14, 2020) ofisini kwake Mlimwa, jijini Dodoma, kutoka kwa Mkurugenzi mkazi wa ETG, Bw. Nilladri Chowdhury aliyefuatana na maafisa uhusiano wa kampuni hiyo, Bw. Frank Mtui na Bi. Fatma Salum Ally.

Akizungumza mara baada ya kupokea kupokea msaada huo, Waziri Mkuu amewashukuru watendaji wa kampuni ya ETG kwa kuunga mkono juhudi za Serikali katika mapambano dhidi ya virusi vya corona, ambapo hadi sasa kesi 49 zimeripotiwa tangu kuanza kwa ugonjwa huo nchini na wagonjwa saba wameshapona.

“Kwa niaba ya Rais wetu, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli tunawashukuru kwa msaada huu ambao utaisadia Serikali kupunguza makali ya kuwahudumia wananchi wetu. Tunahitaji kuungwa mkono na wadau wengine kama ninyi,” amesema.

Waziri Mkuu amewataka wananchi wote wazidishe kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo hasa katika kipindi hiki. “Hatua tuliyofikia hivi sasa, maambukizi yameanza kuongezeka hasa kwa Dar es Salaam na Zanzibar. Tunajua kule kuna watu wengi na shughuli zote za kiuchumi zinaanzia pale, lakini hatuna budi kufuata masharti tuliyopewa ili kuzuia ugonjwa huu usisambae,” amesema.

“Serikali inatoa msisitizo kwa wananchi wazingatie maelekezo yanayotolewa kuhusu kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona ikiwemo kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka pamoja na kujiepusha na mikusanyiko isiyokuwa ya lazima.”

“Muhimu zaidi sote tuendelee kumuomba Mwenyezi Mkungu ili atupunguzie makali ya ugonjwa huu,” amesisitiza.

Mapema, akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kampuni ya ETG, Bw. Mahesh Patel, Mkurugenzi Mkazi wa ETG, Bw. Nilladri Chowdhury alisema wameamua kuchangia ili kuunga mkono juhudi za Serikali katika vita ya kupambana na ugonjwa huo.

“Mwenyekiti wetu amesafiri lakini kama kampuni, tumeamua kuungana na Serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa huu, na ametutuma tutoe mchango wa shilingi milioni 500. Tuna imani na tunaendelea kumuomba Mungu ili atuvushe katika kipindi hiki,” alisema.

Alisema kampuni yao inashughulika na masuala ya kilimo zikiwemo kusambaza pembejeo na kuongeza thamani mazao kupitia kampuni yao ya Kapunga iliyoko Mbeya, viwanda vitatu vya kubangua korosho vilivyoko Mtwara, Newala na Tunduru na viwanda vya kusindika mbegu za mafuta.

Pia wanatoa soko kwa wakulima kwa kununua mazao kama vile korosho, mbaazi, kokoa, mahindi, choroko na ufuta.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU


Share:

Serikali Ya Tanzania Yawataka Madereva Wachukue Tahadhari Dhidi Ya Corona

Na WAMJW- MBEYA.
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeendelea kuwaasa madereva wa vyombo vya usafiri kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na virusi vya Corona.

Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Kitengo cha Maji na Usafi wa Mazingira kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ndg. Anyitike Mwakitalima wakati wa uhamasishaji kwa wananchi wa kuchukua hatua za tahadhari dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa Corona katika Mikoa ya Mbeya na Songwe.

Amesema kuwa, kila dereva na kondakta wake ni lazima wahakikishe gari linakuwa na vitakasa mikono (Sanitizer) kwa ajili ya matumizi yao na abiria. 

Aidha, vituo vyote vya mabasi viwe na sehemu za kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni kwa hii ni hatua muhimu sana ya kujikinga na virusi vya Corona. Aliyasema hayo alipotembelea Stendi Kuu ya mabasi katika Jiji la Mbeya iliyopo eneo la Nane Nane.

“Kondakta hakikisha kila anaepanda gari lako amenawa mikono kwa sabuni na maji safi yanayotiririka au ametakasa mikono yake kwa Sanitizer ndio aruhusiwe kuingia kwenye gari, huu ugonjwa jamani ni hatari na umeua watu wengi” alisema.

Aidha, amewaagiza madereva na makondakta wao kuhakikisha kila siku jioni wanapokuwa wamemaliza kazi zao wahakikishe wanasafisha magari yao kwa dawa maalum aina ya Jiki, ili kuua virusi vinavyoweza kuwepo na kupelekea maambukizi ya ugonjwa wa Corona.

“Madereva na makondakta wote kila siku jioni, hakikisha mnasafisha magari yenu kwa dawa maalum, wote mnaifahamu Jiki hapa, dawa hii inatumika Kutakasa magari, bajaji au pikipiki. Changanya kipimo kimoja cha Jiki na vipimo Sita (6) vya maji ili kupata mchanganyiko unaotakiwa kisha osha chombo chako cha kusafirisha abiria, utajikinga wewe na abiria wako ” alisema.

Nae, Afisa kutoka Makao Makuu Jeshi la Polisi Kamisheni ya Ushirikishaji Jamii Stafu Sajenti Valentino Ngowi, amewataka madereva bodaboda kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi endapo watakutana na mtu alieingia nchini kwa njia za panya, ikiwa ni moja ya jitihada za kupambana na ugonjwa wa Corona, huku akiwataka wasiingie katika vishawishi vya kutaka pesa ya haraka ambayo inaweza kuwagharimu wao na taifa kwa jumla.

“Sasa hivi kuna abiria wengi ambao wanaingia mkoani Mbeya kwa kupita njia za panya, na njia rahisi wanayotumia ni watu wa Bodaboda, hivyo tunawata msiingie kwenye vishawishi vya kutafuta hela ya haraka kwa kuwapitisha watu hao, jambo ambalo ni kinyume na Sheria” alisema

Mbali na hayo, Stafu Sajenti Valentino Ngowi amewataka madereva wote wa vyombo vya moto kuhakikisha wanafuata Sheria bila shurti, ikiwemo kuhakikisha abiria hawasimami kwenye magari (level seat), huku kwa upande wa Bajaj wapande abiria watatu tu.

Kampeni hii ya “Mikono safi, Tanzania salama” inaratibiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana ya Shirika lisilo la kiserikali la Project CLEAR. 

Katika kuchagiza ufikishaji wa elimu ya tahadhari dhidi ya Corona, Wizara inashirikiana na Msanii Mrisho Mpoto (Mjomba) kutoka Mjomba Theatre Gallery, ambae aliwakumbusha wakazi wa Jiji la Mbeya hususani maeneo ya Uyole, Sae, Ilomba, Mwanjelwa, Stendi Kuu, Meta, Nzovwe na Mbalizi kuzingatia unawaji wa mikono kwa maji na sabuni na vile vile kuepuka kushikana mikono na misongamano isiyokuwa na lazima. 

Ziara hii ya utoaji wa elimu ya tahadhari dhidi ya Corona inaendelea katika Mkoa wa Songwe ambao unapakana na nchi ya Zambia.


Share:

Tumia Mwika Kujitibu Busha, Nguvu za Kiume

Mwika ni dawa  ya asili ya nguvu za kiume yenye kutibu matatizo kwa wakati mmoja ;

(1)Nguvu za kiume
(2) Kunenepesha Maumbile
(3)Kuchelewe kufika kileleni

Yajuwe matatizo yanayosababisha upungufu wa nguvu za kiume

(1) Ngiri ya kupanda na kushuka
2.Korondani moja kuvimba
3.Tumbo kuunguruma kujaa gesi
4.Kisukari
5.Presha
6.Kiuno kuuma
7.Kutopata choo vizuri 

Pia tunatibu kisukari siku (14) vidonda vya tumbo siku (30), Miguu kufa ngazi, kuwaka moto .

Pia tunayo dawa ya mvuto wa mpenzi hata yupo mbali amekuacha atarudi na kutimiza ahadi zote mvuto wa biashara.

Wasiliana nasi kwa namba 0747100745 (Whatsap/ Kupiga kawaida)


Share:

Ufaransa Yataka Nchi za Afrika Zisamehewe Madeni Yake Yote Ili Ziweze Kukabiliana Na Virusi Vya Corona

Ufaransa na Ulaya wanatarajia kusaidia Afrika kupambana dhidi ya ugonjwa hatari wa Covid-19 kwa "kuifutia kabisa madeni yake," Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema Jumatatu katika hotuba kwa taifa. Rais Macron ameungana na baadhi ya viongozi duniani kutoa wito huo.

Jumatatu jioni, Emmanuel Macron amesikika akiunga mkono ombi lililotolewa hivi karibuni na viongozi kadhaa wa Afrika, ikiwa ni pamoja  kiongozi wa kanisa Katoliki Papa Francis siku ya Jumapili.

Wito huo unakuja baada ya taasisi kadhaa za fedha za kimataifa kama vile IMF na Benki ya Dunia kutoa wito kwa nchi zilizostawi kiuchumi na kiviwanda kusamehe madani kwa nchi za Afrika katika kuzisaidia kupambana dhidi ya ugonjwa wa Covid-19. 

Ugonjwa huu ambao Umoja wa Mataifa uliutaja kuwa ni janga la kimataifa umeendelea kuwa tishio kubwa ulimwenguni hasa barani Afrika, ambapo nchini nyingi ni masikini, huku raia wao wakiishi katika mazingira magumu.

Suala hilo linatarajiwa kujadiliwa wiki hii na nchi zilizostawi kiuchumi na kiviwanda, G20, kando ya mkutano wa Shirika la Fedha la Kimataifa.


Share:

Wimbo Mpya : MAGENHIRO - NDOA 'BHENGA'


Huu hapa wimbo mpya wa Magenhiro unaitwa Ndoa ' Bhenga' ...usikilize hapa chini

Share:

Fedha Za Rais Magufuli Zaleta Mabadiliko Sekta Ya Mifugo Mkoani Lindi

Na Mwandishi Wetu,MAELEZO
MKOA wa Lindi kihistoria sio wa kiufugaji ma wafugaji wachache waliopo hufuga zaidi mbuzi, kondoo, kuku, bata, kanga, njiwa na ng’ombe ambao kwa uchache sana na mara nyingi hutumiwa kwa kitoweo, shughuli za biashara, kimila na utamaduni.
 
Mara baada ya baada ya Serikali ya Mkoa huo kukubali kupokea mifugo toka Mikoa mingine yenye idadi kubwa ya ng’ombe, sekta ya mifugo imeendelea kukua na kuongeza  mwamko kwa wananchi katika kujiletea maendeleo yao.
 
Mkoa wa Lindi hadi kufikia mwezi Machi, 2018 una jumla ya ng’ombe wa asili 118,760, mbuzi asili 79,183, mbuzi wa kisasa 8,138, na kondoo 9,007, ngamia 10, Nguruwe 5,166, kuku 1,460,491, punda 121, kanga 5,788, bata maji 25,111, bata mzingi 112, Njiwa 1,586 na Sungura 212.
 
Kwa mujibu wa Taarifa ya Mkoa, katika kipindi cha Julai, 2017 hadi Machi 2018 fedha zilizotokana na biashara ya mifugo katika Halmashauri zote mkoani humo zilikuwa ni zaidi ya Tsh. Bilioni 5.1 zilizotokana na ushuru wa machinjio, leseni za wafanyabiashara wa nyama pamoja na usafirishaji wa mifugo.
 
Pamoja na sekta hiyo kuwa chanzo muhimu cha mapato katika Mkoa huo, bado kuna msukumo mdogo wa Serikali katika uendelezaji wa miundo mbinu ya mifugo ikiwemo machinjio, maeneo kwa ajili ya malisho, maeneo ya malambo kwa ajili ya mifugo, majosho pamoja na uchache wa mashamba ya mifugo.
 
Katika kukabiliana na changamoto hiyo, Halmashauri ya Manispaa ya Lindi inatekeleza ujenzi wa mradi wa machinjio ya kisasa katika eneo la Ngongo unaolenga katika kuongeza thamani ya mazao ya mifugo ikiwemo nyama ambayo mahitaji yake yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku mkoani humo.
 
Halmashauri hiyo hadi sasa imetumia kiasi cha Tsh Bilioni 1.4 zilitolewa na Serikali Kuu kwa ajili ya kukamilisha mradi huo, ambao ni moja ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Halmashauri hiyo ili kuiwezesha kujitegemea kimapato katika utoaji wa huduma zake kwa wananchi.
 
Akizungumza katika mahojiano maalum na Maafisa kutoka Idara ya Habari (MAELEZO) waliofanya ziara hivi karibuni Mkoani humo, Mhandisi Godfey Msoma wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, anasema mradi huo ulioanza mwaka 2017 umekamilika kwa asilimia 98, ikiwemo awamu muhimu mbili za mwanzo zinazohusisha jengo la machinjio pamoja na miundombinu yake.
 
Anaongeza kuwa mradi wa machinjio hayo pindi utakapokamilika utaweza kutoa huduma ya kuchinja ng’ombe 100, mbuzi 100 kwa siku na hivyo kufungua milango ya uwekezaji mkubwa na wenye tija kwa kwa wafugaji na wafanyabiashara mkoani huo pamoja na Mikoa jirani katika Ukanda wa Kusini.
 
‘’Kwa Manispaa ya Lindi, hii ni fursa na tutatumia mradi huu kwa ajili ya kuhamasisha wananchi wetu wafuge kisasa kwani kwa kufanya hivyo kutawawezesha kujiongezea fursa ya masoko kwa mifugo yao na kuweza kufanya minada ya mifugo yao na pia kuuza bidhaa za nyama zenye  ubora wa kimataifa’’ alisema Msoma. 
 
Aidha Msoma alisema malengo ya ujenzi wa mradi huo ambao pia ni miongoni mwa miradi mikubwa ya uwekezaji katika Halmashauri hiyo ni kukidhi mahitaji makubwa ya machinjio ya kisasa katika Ukanda wa Kusini kutokana na ukweli kuwa mikoa hiyo kwa sasa  inaendelea kupokea makundi makubwa ya wafugaji wa kutoka mikoa mbalimbali nchini.
 
Kwa mujibu wa Msoma alisema ili kuhakikisha machinjio hayo yanakuwa ya kisasa na endelevu, mradi huo pia utahusisha ujenzi wa nyumba ya Daktari wa wanyama ambaye atakuwa na jukumu la kufanya ukaguzi na uhakiki wa ubora wa nyama inayozalishwa kabla ya kumfikia mlaji ili kuhakikisha kuwa afya za walaji zinalindwa kwa manufaa ya jamii husika.
 
‘’Machinjio haya ni ya kisasa kabisa katika ukanda wa kusini, malengo yetu ni kuhakikisha tunakidhi viwango vya kimataifa katika uzalishaji wa nyama bora ili kuweza kupanua mahitaji ya soko la bidhaa za nyama kimkoa, kitaifa na kimataifa, hivyo tumepanga kuhakikisha kuwa miundombinu yake inakuwa na sifa zinazostahiki’’ alisema Msoma.
 
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi katika Halmashauri hiyo, Dkt. Iddi Nizari ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kutoa kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo, ambao umejengwa katika viwango vya kimataifa kwa kuwa utasaidia kuongeza mapato ya Mkoa wa Lindi na taifa kwa ujumla.
 
Aliongeza kuwa ujenzi wa mradi wa machinjio hayo unatarajia kuongeza chachu ya uwekezaji kwa wafugaji na wafanyabiashara wa nyama mkoani humo kwani utaweza kuhudumia wanyama wengi na hivyo kutoa fursa ya kufanyika kwa minada mikubwa katika Ukanda wa Kusini.
 
‘’Machinjio haya yatazalisha nyama bora zinazouzwa katika maduka mbalimbali na pia kupanua soko letu la nyama katika nchi za nje kwani watumaji wengi wa nyama waliopo nje ya nchi wanaopenda kuona bidhaa iliyozalishwa katika viwango vyenye ubora na hili kwa upande tumejipanga katika kufikia viwango hivyo’’ alisema Dkt. Nizari.
 
Akifafanua zaidi Dkt. Nizari alisema ujenzi wa machinjio hayo utasaidia kutoa hamasa kwa wafugaji mkoani humo kufuga kisasa zaidi hatua itakayowezesha kuongeza tija ya uzalishaji wa bidhaa ya nyama mkoani humo kuweza kufikia mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi.
 
‘’Machinjio tunayoitumia sasa ni ndogo sana lakini pia haina ubora wa kuhudumia mifugo yetu kwa mfano machinjio tunayoitumia kwa sasa katika Halmashauri yetu ina uwezo wa kuchinja ng’ombe 10 na mbuzi 20 kwa siku, hivyo bado hatujaweza kufikia malengo tuliyojiwekea katika Halmashauri’’ alisema Dkt. Nizari.
 
Aidha Wananchi mbalimbali katika Manispaa ya Lindi walitoa pongezi kwa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli kwa ujenzi wa mradi huo, ambao wanaueleza utakuwa mkombozi kwa wananchi wa mikoa ya Kanda ya Kusini kwani utafungua milango ya kiuchumi na kuimarisha sekta ya mifugo katika mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma.
 
Mmoja wa Wananchi wa Kata ya Tulieni, Manispaa ya Lindi Bw. Bakari Mchukuma anasema ujenzi wa machinjio ya kisasa utasaidia kuondokana na ufugaji wa kimazoea kwani hapo awali walikuwa na mifugo mingi katika jamii yao ikiwemo ng’ombe ambao wilitumika katika shughuli mbalimbali za kimila ikiwemo ngoma za asili zinazofanyika kila mwaka mara baada ya kumalizika kwa msimu wa kilimo.
 
‘’Mkoa wetu haukuwa mkoa wa kifugaji, tulikuwa na ng’ombe, Mbuzi, kondoo, kuku na mifugo mingine ambayo mingi ilitumika kwa ajili ya sherehe za kimila ikiwemo ngoma, lakini kwa sasa Serikali ya Rais Dkt. John Maguful imeamua kujenga machinjio kubwa, bora ya kisasa katika manispaa ya Lindi, ambayo itatusaidia kuiuza na kupata pesa kwa ajili ya kuendesha maisha yetu’’ anasema Mchukuma.
 
Aidha Mchukuma aliipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa ujenzi wa mradi huo kwani utasaidia kuongeza idadi ya minada ya mifugo Mkoani humo, ambapo kwa sasa kuna jumla ya minada minne tu ambapo kati ya hiyo, minada miwili inapatikana Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, mnada mmoja uliopo Halmashauri ya Manispaa ya Lindi huku Halmashauri ya Lindi pia ikiwa na  mnada mmoja.
 
Kwa upande wake Bw. Abdul Kasembe Mkazi wa kijiji cha Mitandi Manispaa ya Lindi, ambaye ni mfugaji anayemiliki ng’ombe 30, mbuzi 45 na kondoo 25, aliipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa ujenzi wa mradi wa machinjio hayo kwa kuwa umedhihirisha dhamira ya Rais Dkt. John Magufuli ya kusaidia wananchi wa kipato cha chini katika  kujikwamua kiuchumi.
 
Anaongeza kuwa kwa upande wake machinjio hayo yamempa fursa ya kufuga kisasa, kwani ataweza kuiuza mifugo yake katika minada mikubwa inayotambulika na Serikali na kuwasaidia kulanguliwa na wafanyabiashara wasio waaminifu.
 
Naye Bw. Emmanuel Kwaang, mkazi wa kijiji cha Matopeni Manispaa ya Lindi ambaye pia ni mfugaji wa mbuzi na kondoo anasema uwepo wa machinjio hayo utasaidia kupatikana kwa soko la uhakika wa mifugo mkoani humo, ukilinganisha na hali ilikuwapo hapo awali ambapo walikuwa wakisafiri hadi mikoa ya jirani ikiwemo Mkoa wa Pwani kwa ajili ya kutafuta masoko.
 
Bw. Kwaang aliipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo kwa kuwa utasaidia upatikanaji wa masoko ya uhakika wa mifugo yao sambamba na kupunguza umbali wa kusafirisha mifugo yao, ambayo hupungua thamani pindi wanapoenda kuiuza katika minada iliyopo nje ya Mkoa huo.
 
‘’Nampongeza Rais Dkt. John Magufuli kupitia Serikali ya Awamu ya Tano kwa ujenzi wa machinjio haya kwani imetusaidia sana sisi wafugaji kuweza kupata soko la uhakika la kuuzia mifugo yetu na hivyo kuweza kuchangia pato la Mkoa wetu wa Lindi kutokana na Kodi tutakayoanza kuilipa pindi machinjio haya yatakapoanza kufanya kazi’’ alisema Kwaang.
 
Naye Bw. Hamis Mohamed mfanyabiashara wa bidhaa za nyama na Mkazi wa RahaLeo Manispaa ya Lindi, anasema ujenzi wa machinjio hiyo utawasaidia kuongeza wigo wa biashara yake Mkoani humo na mikoa ya jirani kutokana na ubora wa nyama itakayozalishwa kiwandani hapo kuwa ni yenye ubora na hivyo kufungua milango ya ushirikiano wa biashara baina ya Tanzania na nchi jirani ikiwemo Msumbiji.
 
‘’Pindi machinjio haya yakikamilika na kuanza kazi yatasaidia kupanua mtandao wa biashara baina yetu na mataifa jirani ikiwemo nchi ya  Msumbiji, na kufanya hivi kutasaidia kuongeza kodi ya serikali naipongeza serikali ya Awamu ya Tano kwa kubuni mradi huu ambapo utafungua fursa ya ukuaji wa biashara kwa mikoa ya ukanda wa kusini’’ alisema Mohamed.
 
Serikali kupitia Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) inatekeleza Mkakati Maalum unaolenga kuziwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa ikiwemo Halmashauri kujitegemea kimapato ili kutoa huduma bora zaidi na zenye uhakika kwa wananchi.
 
Kwa kuzingatia sababu hizo, Wizara ya Fedha na Mipango imeanzisha utaratibu kwa Halmashauri mbalimbali nchini kufanya mawasilisho ya miradi yao ya kimkakati katika eneo la kujijenga kimapato kwa madhumuni ya kujitegemea na kuboresha utoaji wa huduma.
 
Kwa msingi huo, ujenzi wa machinjio ya kisasa katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi utasaidia upatikanaji wa mapato ya kutosha na yenye uhakika katika Halmashauri hiyo ikiwa ni  nguzo imara katika kuboresha utoaji huduma nzuri na zenye uhakika kwa wananchi.
 
MWISHO


Share:

Wimbo Mpya : MAGENHIRO - CORONA


Nakualika kusikiliza wimbo mpya wa  Msanii Magenhiro kutoka Shinyanga inaitwa Corona...Hii hapa chini

Share:

Ufaransa Yaongeza Mwezi Mmoja wa Tahadhari Dhidi Ya Corona....Baada ya Muda Huo Shule Huenda Zikafunguliwa

Ufaransa imeongeza muda wa kuendelea kuchukua tahadhari za kudhibiti maamukizi ya virusi vya corona hadi Mei 11. 

Rais Emmanuel Macron amesema ifikapo tarehe hiyo shule zitaanza kufunguliwa. 

Jumatatu Ufaransa imeripoti vifo 574 vinavyotokana na maambukizi ya virusi hivyo, na kuifanya idadi jumla ya vifo kufikia watu15,000. 

Hata hivyo, idadi ya wagonjwa wa COVID-19 wanaohitaji uangalizi maalumu imepungua kwa siku ya tano mfululizo. 

Macron amesema kasi ya janga hilo inaanza kupungua na dalili za kudhihirisha hilo ziko wazi. “Mei 11 itakuwa mwanzo wa awamu mpya. Sheria zinaweza kubadilishwa kulingana na hali itakavyokuwa,” aliongeza Macron.

Serikali mbalimbali kote ulimwenguni ziko chini ya shinikizo la kuokoa uchumi wa dunia usije kuanguka kabisa kwa sababu ya kufungwa kwa biashara na watu kulazimika kubakia majumbani, lakini viongozi pia wanajaribu kuzuia wimbi la pili la ugonjwa huo.


Share:

Hispania: Maelfu ya watu warejea kazini....Hii ni mara ya kwanza tangu kuibuka kwa Virusi vya Corona Vilivyoua Zaidi Ya Watu 17,000 Nchini Humo

Maelfu ya watu nchini Uhispania leo hii wameruhusiwa kurejea kazini, ikiwa ni mara ya kwanza tangu kuibuka kwa mlipuko wa virusi vya corona, ambapo serikali iliweka marufuku ya kufanyika shughuli za kawaida.

Jumatatu ya Pasaka kwa taifa hilo haikuwa siku ya kitaifa ya mapunziko kwa raia badala yake waliruhusiwa kuondoka majumbani mwao, ikiwa hatua ya taratibu ya kuindoa marufuku iliyodumu tangu mwezi uliopita.

Kwa mujibu wa makadirio ya vyombo vya habari, takribani 300,000 walirejea makazini mjini Madrid. Kabla ya hatua hiyo, watu ambao ajira zao zilionekana kuwa na ulazima kufanyika waliruhusiwa kufanya kazi.

Hata hivyo rekodi mpya ya maambukizi zinaonesha watu 3,477 wameambukizwa. Hayo ni katika kipindi cha masaa 24 yaliopita. 

Kwa kuizingatia idadi hiyo, jumla ya maambukizi nchini humo kwa sasa inafikia watu 169,496, ikionesha uelekeo wa kupatikana unafuu kwa taifa hilo lilishambuliwa vikali na virusi. 

Katika kipindi kigumu nchini Uhispania kulirekodiwa hadi maambukizi 8,000 kwa siku. Vifo vipya kwa leo ni 517 na kufanya jumla yake kuwa 17,489.


Share:

BRIGHTERMONDAY TANZANIA YAJA NA MPANGO KUSAIDIA BIASHARA KIPINDI CHA CORONA


Bi. Reshma Bharmal-Shariff, Ofisa Mtendaji Mkuu BrighterMonday Tanzania

KAMPUNI ya ajira ya BrighterMonday Tanzania imezindua mpango unaoitwa 'Umoja Wakati wa Shida ' ambao utatoa nafasi kwa watu binafsi au kampuni kutangaza ajira bure katika kipindi hiki ambacho nchi inapambana na maambukizi ya virusi vya Corona (COVID-19).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kampuni hiyo jijini Dar es Salaam kupitia kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wake, Reshma Bharmal-Shariff ilieleza kuwa kampeni hiyo inalenga kuongeza juhudi za biashara nchini.

“Kampeni inalenga kuendeleza shughuli za biashara na ajira kwa kuwezesha mashirika kupata watu wenye uwezo wa utendaji hasa unaokidhi tija ya nyakati za sasa za changamoto.

“Katika kipindi cha miezi mitatu ijayo, tutawapa waajiri fursa ya kuajiri wataalamu katika tasnia tofauti kwa kuwawezesha waajiri kutangaza kazi kwenye tovuti yetu. Hii itawezesha hospitali, vituo vya huduma ya afya na watoa huduma wengine muhimu katika mapambano dhidi ya corona kuajiri wataalamu waliofuzu viwango, katika kipindi cha muda mfupi kadri itakavyowezekana,” alisema Reshma.

Alisema kupitia mpango huo, waajiri wataweza kufuatilia mchakato mzima wa kuajiri na kupata huduma zingine zilizobuniwa na BrighterMonday ikiwemo zana ya tathmini ya ustadi wa kampuni hiyo ambayo inapima uwezo wa msingi wa waombaji wa ajira na stadi za ziada zinazohitajika katika kazi husika zaidi ya ile iliyowekwa kwenye wasifu (CV) zao wakati wa mchakato wa kuajiri.

“Kwa kuongezea, waajiri wataweza kuona alama za mwombaji mbali na ujuzi mwingine uliozoeleka wa elimu na viwango vya uzoefu ikiwamo matumizi ya mfumo wa Ufuatiliaji wa Maombi wa BrighterMonday (ATS), ambao unarahisisha kufanya tathimini kwa mwombaji wa ajira husika.

“Hivyo kwa njia hii wataweza kulinganisha ustadi, sifa na viwango vya uzoefu wa mwombaji wa nafasi husika, BrighterMonday Tanzania tupo hapa kwa ajili yako jana, leo na hata kesho,” alisema Reshma.
Share:

Jobs at Muhimbili National Hospital (MNH), April 2020

VACANCY ANNOUNCEMENT On behalf of Muhimbili National Hospital (MNH) President’s Office Public Service Recruitment Secretariat invites competent, experienced, highly organized and selfmotivated Tanzanians to fill 3 vacant posts mentioned below;- 1.0 MUHIMBILI NATIONAL HOSPITAL (MNH) Muhimbili National Hospital (MNH) is a tertiary specialised and super specialist hospital in Tanzania organized into nine directorates with bed capacity of 2,178… Read More »

The post Jobs at Muhimbili National Hospital (MNH), April 2020 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

PICHA: Mgonjwa Akiwahishwa Hospitali Nchini Uganda Baada ya Usafiri wa Umma Kupigwa Marufuku Kwa Hofu ya Corona

Mwanaume mmoja akiwa anasukuma usafiri wa asili ili kumuwaisha Hospitali mgonjwa katika Manispaa ya Arua, Uganda...

 Mwanamke  huyo mgonjwa hakuweza kupata Bodaboda au usafiri mwingine  kufuatia usafiri wa umma kupigwa marufuku na Rais Museveni ili kuzuia corona kusambaa.

Credit/ Picha: Daily Monitor 


Share:

Uchaguzi Mkuu Marekani: Sanders hatimaye amuidhinisha Biden kama mgombea urais ili Kumkabili Trump

Seneta wa jimbo la Vermont la Marekani, Bernie Sanders, Jumatatu alimuidhinisha aliyekuwa makamu wa rais Joe Biden kuwa mgombea wa urais kwa chama cha Democratic.

Katika mawasiliano kupitia njia ya video iliyowaunganisha wawili hao, Sanders aliahidi kumsaidia Biden kushinda uchaguzi wa Novemba mwaka huu, akimtaja Trump kuwa mtu hatari zaidi katika historia ya hivi karibuni ya Marekani.

Sanders na Biden walikuabliana kuunda tume maalum zitakazofanya kazi kwa pamoja kuhusu maswala ya sera, jinsi ya kushughulikia maswala muhimu ya mabadiliko ya hali ya hewa, afya na uhamiaji, miongoni mwa mengine.

Sanders aliahidi kuleta Pamoja timu yake ya kampeni na kushirikiana na ya Biden katika kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi Novemba mwaka huu.

“Tunakuhitaji katika White House. Nitafanya kila niwezalo kuhakikisha kwamba hilo linafanikiwa, Joe,” Sanders alimwambia Biden katika video iliyowekwa kwenye wavuti wa Biden na kusambazwa kwa mitandao ya kijamii.

Seneta huyo alimkosoa Rais Trump kwa jinsi amesimamia janga la maambukizi ya virusi vya Corona, pamoja na kumtaja kuwa mbaguzi mkuu wa rangi miongoni mwa mengine, akisisitiza kwamba anastahili kuondolewa madarakani.

Hatua ya Sanders kumuunga mkono Biden ambaye anakuwa mshindani wake mkuu katika kinyang’anyiro cha tiketi ya chama cha democratic, ni muhimu sana wakati chama hicho kinatafuta kuunganisha wafuasi wake dhidi ya Rais Trump katika uchaguzi ujao.

Biden alimshukuru Sanders kwa kumuidhinisha, akisema anamhitaji sana sio kushinda kiti cha urais, lakini hata katika kuongoza Marekani.

"Nadhani hatua yako ya kuniidhinisha ina maana kubwa sana. Ina umuhimu mkubwa sana kwangu. nadhani kuna watu watashangaa kwamba baadhi ya sera zetu hazifanani lakini tunakubaliana katika mambo mengi sana. Nitakuhitaji sana sio tu kushinda uchaguzi bali pia kuongoza taifa,” alisema Biden katika mazungumzo yao.

Biden, akimtaja Sanders kuwa rafiki, alisema ana matarajio makubwa sana kufanya kazi na Sanders akiahidi kufanya kila awezalo kutimiza matarajio yao.

Hii ni mara ya pili kwa Bernie Sanders, kuwania tiketi ya chama cha democratic katika uchaguzi wa urais bila mafanikio. Mwaka 2016, alishindwa na Bi Hillary Clinton.

Credit-VOA


Share:

Mabalozi wa Nchi za Afrika wakutana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje China Kuzungumzia Ubaguzi Wanaofanyiwa Waafrika Huko China

Mabalozi wa Nchi za Afrika wamekutana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje China, Chen Xiaoding kuzungumzia changamoto zinazowakabili baadhi ya raia wa Afrika katika mji wa Guangzhou

Chen amewaeleaza Mabalozi kwamba Serikali ya China haiungi mkono vitendo vya ubaguzi dhidi ya yeyote.

Kuhusu changamoto zilizowasilishwa na Mabalozi wa Nchi za Afrika zinazowakabili Waafrika nchini China, China imesema Mamlaka ya Jimbo la Guangdong itachukua hatua kuzishughulikia ikiwemo Raia wa Afrika ambao wameondolewa kwenye makazi na hoteli kupatiwa makazi mbadala ya muda.

China imewaahidi Mabalozi wa Nchi za Afrika kuwa itahakikisha zoezi la udhibiti wa corona linaendeshwa kwa usawa, kutoa elimu kwa umma ili kuepuka hatua zinazoweza kutafsiriwa kuwa ni ubaguzi na Kuanzisha mtandao wa mawasiliano kati ya Mamlaka za Nchi hiyo na Ofisi za Kibalozi.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger