Monday, 20 January 2020

Kilichoendelea Mahakamani Leo Kesi Ya Tundu Lissu

Mdhamini wa aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, Robert Katula ameiambia mahakama kuwa wakati anamdhamini mshtakiwa huyo hakujua kama atapigwa risasi.

Katula ametoa madai hayo leo Jumatatu Januari 20, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wakati kesi hiyo ilipokuwa ikitajwa.

Amesema Desemba 19 mwaka jana, mahakama iliamuru Lissu afike leo mahakamani lakini amefanya juhudi za kuwasiliana naye akawafahamisha kwamba atawasiliana na wakili wa chama lakini hadi leo kimya.

Mdhamini huyo ameomba apewe muda zaidi wa kuhakikisha anamfikisha mshtakiwa huyo mahakamani.

“Mheshimiwa wakati natoa ahadi kwamba nitahakikisha anafika mahakamani sikujua kama atapigwa risasi, tumemuandikia Mwenyekiti Freeman Mbowe barua atusaidie kumfikisha mshtakiwa nchini,” amedai Katula.

Hakimu Simba ameahirisha kesi hadi Februari 20 mwaka huu na kuamuru kwamba mshtakiwa ni lazima afike mahakamani tarehe hiyo kabla mahakama haijatoa amri nyingine zenye nguvu zaidi dhidi ya wadhamini.

Mdhamini wa mwingine wa Lissu ni Ibrahim Ahmed.

Kesi hiyo ilifunguliwa Juni 14 mwaka 2016 baada ya muda mshtakiwa wa nne, Lissu akapata matatizo yaliyomfanya ashindwe kufika mahakamani.

Mbali na Lissu, washtakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Mhariri wa gazeti la Mawio, Simon Mkina, Jabir Idrisa na Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehboob.

Lissu na wenzake wanakabiliwa na mashtaka matano ikiwamo la kuandika habari za uchochezi kinyume na Sheria ya Magazeti ya Mwaka 2002.


Share:

Serikali Kutumia hekima kuwasaidia ambao wameshindwa kusajili Laini zao za Simu

Serikali  imesema itatumia hekima kuwasaidia wananchi walioshindwa kusajili laini za simu kwa sababu ya kukosa kitambulisho cha Taifa na namba licha ya kuanza mchakato wa kupata kitambulisho hicho.

Imesema wananchi hao ambao taarifa zao zipo katika Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), huenda wamekosa kitambulisho au namba kwa sababu zilizo nje ya uwezo wao.

Hayo yameelezwa Jumapili Januari 19, 2020 na naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye katika mkutano wa ndani wa CCM mkoani Kigoma.

“Serikali itaona jinsi ya kutumia hekima kwa wananchi ambao taarifa zao zipo katika ofisi za Nida kuona namna ya kufanya lakini kwa wengine ambao hawajajaza fomu laini zao zitazimwa,” amesema Nditiye.

Amesema ambao laini zao zitazimwa ni wale waliosajili laini chache na kuacha nyingine licha ya kuwa na kitambulisho hicho.

Amebainisha kuwa usajili wa laini za simu ni endelevu licha ya baadhi ya wananchi kupuuza.


Share:

TFF yatoa Kauli kuhusu Ubaguzi mechi ya Azam dhidi ya Yanga SC




Share:

MASHINDANO YA GOFU YA ZANTEL YAFANA JIJINI DAR ES SALAAM

Mchezaji wa gofu, Amanda Patric Mlula, akipiga mpira wa gofu wakati wa mashindano ya wiki ya gofu yaliyoandaliwa na kampuni ya mawasiliano ya Zantel na kufanyika katika viwanja vya TPDF Lugalo Golf Club, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mchezaji wa gofu, Brigedia Msaafu, Julius Mbilinyi, akipiga mpira wa gofu wakati wa mashindano ya wiki ya gofu yaliyoandaliwa na kampuni ya mawasiliano ya Zantel na kufanyika katika viwanja vya TPDF Lugalo Golf Club, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Mchezaji wa gofu, Nathan Mpangala, akipiga mpira wa gofu wakati wa mashindano ya wiki ya gofu yaliyoandaliwa na kampuni ya mawasiliano ya Zantel na kufanyika katika viwanja vya TPDF Lugalo Golf Club, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Mchezaji wa gofu, Ryan Gosling, akipiga mpira wa gofu wakati wa mashindano ya wiki ya gofu yaliyoandaliwa na kampuni ya mawasiliano ya Zantel na kufanyika katika viwanja vya TPDF Lugalo Golf Club, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.    Meneja wa Ufundi Mauzo ya Jumla wa Zantel Efrem Akwilini (kulia), akikabidhi zawadi ya simu aina ya SMARTA, kwa Isack Daud,mshindi wa jumla wa mashindano ya wiki ya gofu yaliyoandaliwa na kampuni ya mawasiliano ya Zantel na kufanyika katika viwanja vya TPDF Lugalo Golf Club, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, (katikati mwenye fulana nyekundu ) ni Mwenyekiti wa Chama Cha Gofu nchini,Chriss Martin na Brigedia Generali Kondwani Kalino.
Share:

Business and Entrepreneurship Adviser – Remote at VSO Mwanza Tanzania

Business and Entrepreneurship Adviser – Remote at VSO Mwanza Tanzania Role Overview The Ideal person will train the Lake Zone Youth to improve market awareness and help them identify business opportunities. The candidate will work hand in hand with corporate volunteers who will be engaged in the similar position or Life Skills expert to engage marginalized youth on… Read More »

The post Business and Entrepreneurship Adviser – Remote at VSO Mwanza Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Dr. Bashiru: Rais Magufuli Arejesha Matumaini Mapya Kwa Wanyonge

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally ameweka wazi kuwa, jambo moja kubwa lililofanywa na Serikali ya awamu ya Tano chini Mhe. Rais John Pombe Magufuli ni kurejesha matumaini mapya kwa wanyonge na wavuja jasho waliokuwa wamekata tamaa.

Amesema kuwa, wanaCCM wote, watembee kifua mbele kwani, kati ya mambo makubwa ambayo serikali ya CCM ya awamu ya tano imeyafanya ni kurejesha matumaini ya wanyonge, ambapo hilo pekee ni jambo kubwa na limeleta faraja kwa watu wengi, sasa wanaimani kubwa na CCM.

Ameyasema hayo jana tarehe 19 Januari, 2020 Kigoma Mjini akizungumza na viongozi wa Mashina, Matawi, Kata, Wilaya na Mkoa.

“WanaCCM tembeeni kifua mbele, kati ya mambo ambayo awamu ya tano imeyafanya na makubwa hayatasahaulika, ni kurejesha matumaini ya wanyonge, na hilo katika siasa ni jambo kubwa, matumaini mapya kwa watu waliowahi kukata tamaa, matumaini mapya kwa wavuja jasho, matumaini hayo yamerejea chini ya uongozi shupavu, uongozi wenye maono, uongozi wa kizalendo wa Dkt. John Pombe Magufuli.”

Ameongeza kuwa, “wanaCCM mkiulizwa ni jambo gani jipya limefanyika linalopimika , linaloonekana kila mahala na kila mwenye akili na nia njema, waelezeni bila kupepesa macho, jambo kubwa jipya ni kurejesha matumaini mapya kwa wanyonge.”

Amesisitiza zaidi kuwa, kila analolifanya Mhe. Rais Magufuli, kila analolisimamia na kila analoliamua ni kwa maslahi ya kuwapa matumaini mapya watanzania wavuja jasho na katika hili mpaka sasa ameacha alama kubwa, ukiacha ujenzi wa barabara, reli, madaraja na mengine mengi anayoyafanya.

Aidha, Katibu Mkuu ametumia fursa hiyo kuwahakikishia wanaCCM wote kuwa, Chama Kimejipanga vya kutosha kurejesha Jimbo na Halmashauri ya Kigoma Mjini ambapo kwa sasa vyote vinaongozwa na upinzani, hivyo wanachama wote waendelee kuwa na umoja na mshikamano zaidi.

Wakati huo huo, Katibu Katibu amegawa vitambulisho kwa wenyeviti wa mashina ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo kwa wenyeviti hao nchi nzima kupatiwa vitambulisho na watambuliko katika ofisi zote za Umma.

Mkutano huo wa ndani umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma Ndg. Amandus Nzamba na Mkuu wa Mkoa huo Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga.

Leo Katibu Mkuu amehitimisha ziara yake ya kikazi ya siku tatu Mkoani Kigoma iliyolenga kuimarisha na kuhuisha uhai wa Chama, ambapo tayari amewasili Dar es Salaam kuendelea na Majukumu ya kikazi.


Share:

Ijue Sayansi ya Kusimama na Kusinyaa kwa Maumbile ya Kiume ( Sayansi ya Nguvu za Kiume)

Ukosefu  na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume, ni tatizo linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume duniani.

Tatizo  la  ukosefu/upungufu  wa  nguvu  za  kiume ni  nini  ?
Ukosefu  ama  upungufu  wa  nguvu za  kiume  ni  ile  hali  ya  mwanaume  kutokuwa  na  uwezo  wa kufanya  tendo  la  ndoa  kwa  ukamilifu


Hatua  mbili  Muhimu 
Ili  mwanaume   aweze  kufanya  tendo  la  ndoa  na  andelee  kufanya  tendo  la  ndoa, ni  lazima  maumbile yake ya kiume yapitie  hatua  kuu  mbili  kama  ifuatavyo :

Hatua  ya  kwanza, ni  lazima  yaweze  kusimama  barabara  na  kuwa  magumu  kama  msumari.

Na  hatua  ya  pili  ni  lazima, yaendelee  kusimama  kwa  muda  mrefu  wakati  wa  tendo  la  ndoa.  Hatua  zote  mbili  zinapo  kamilika, ndipo  tunapo  pata  kitu  kinaitwa  STRONGER  AND  LONGER  ERECTION

Endelea na Makala hii kwa <<Kubofya Hapa>.


Share:

Waziri Mkuu: Simamieni Elimu Kwa Watoto Wa Kike

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaagiza Wakuu wa Mikoa na Wilaya nchini wasimamie ipasavyo suala la elimu hususani kwa watoto wa kike na kuchukua hatua kwa watakaowakatisha masomo.

Pia, Waziri Mkuu amesema Serikali inawataka  watoto watoe taarifa za watu wanaotaka kuwakatisha masomo yao kwa viongozi  wa shehiya (vijiji) waliopo kwenye maeneo yao.

Alitoa agizo hilo jana jioni (Jumapili, Januari 19, 2020) wakati akizungumza na wananchi baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa chuo cha Mafunzo ya Amali cha Daya kilichopo Mtambwe wilaya ya Wete, Kaskazini Pemba.

Waziri Mkuu alisema Serikali imedhamiria kuwalinda watoto wa kike lengo likiwa ni kuhakikisha wanamaliza masomo yao na hatimaye waweze kujikwamua wao pamoja na familia zao.

Alisema watoto wa kike wanatakiwa waheshimiwe na jamii kwa kuachwa waendelee na masomo yao bila ya usumbufu wowote na atakayebainika kukatisha masomo adhabu yake ni miaka 30 jela.

“Wanafunzi wa kike hakikisha mtu yeyote atakayekugusa, kukufuatilia nenda kamshtaki kwa kiongozi wa Shehiya husika. Vijana jihadharini na watoto wa shule ukikutwa naye jela miaka 30.”

Awali, akisoma taarifa za ujenzi wa chuo hicho, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Bibi Madina Abdallah  alisema mpaka kukamilika kwake mradi huo utagharimu jumla ya Dola za Marekani milioni 25.8 kati yake Dola milioni 23.4 zimetolewa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) huku dola milioni 2.4 zikitolewa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Alisema kwa mujibu wa mkataba wa mradi huo kazi ya ujenzi inajumuisha vituo viwili vya Mafunzo ya Amali ambavyo ni Makunduchi Unguja na Daya Pemba. Pia upanuzi wa Taasisi ya Maendeleo ya Utalii Maruhubi na Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume pamoja na ununuzi wa vifaa vya kufundishia.

(mwisho)
IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU


Share:

Waziri Mkuu Akagua Ujenzi Wa Hoteli Pemba.....Asema Lengo Ni Kuimarisha Shughuli Za Utalii, Kuongeza Ajira

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua mradi wa ukarabati wa Hoteli ya Mkoani ambapo amesema lengo la maboresho hayo ni kuimarisha shughuli za utalii na kupunguza tatizo la ajira.

Amesema ili kuhakikisha lengo la Serikali linafikiwa amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bw. Khamis Mussa Omar ahakikishe mradi huo unakamilika kwa wakati ili kuleta manufaa yaliyokusudiwa.

Ameyasema hayo jana  (Jumapili, Januari 19, 2020) baada ya kukagua mradi huo uliopo katika wilaya ya Mkoani mkoa wa Kusini Pemba. Mradi huo wenye thamani ya sh. bilioni nne unatekeleza na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF)

Waziri Mkuu amesema mradi wa ukarabati wa hoteli ya Mkoani  ni muhimu katika kuimarisha sekta ya utalii na huduma za malazi hususani kwa wageni wanaotembelea kisiwa hicho cha Pemba sambamba na kutengeneza ajira kwa wanawake na vijana.

“Ukarabati huu unatarajia kutoa mchango mkubwa katika kukuza sekta ya ajira, teknolojia, kuongeza mapato ya Serikali na kuimarisha ustawi wa wananchi wetu. Endeleeni kuiamini Serikali yenu.”

Akisoma taarifa ya ukarabati wa mradi huo, Meneja Uwekezaji wa ZSSF, Bw. Abdulaziz Ibrahim Idd amesema ukarabati huo ulianza Julai 2019 na unatarajiwa kukamilika Machi 2020.

Amesema ukarabati wa jengo hilo ambalo awali lilikuwa la ghorofa moja umehusisha pia kuongeza ghorofa mbili na kufikia tatu, hali ambayo italifanya jengo hilo kuwa na vyumba 16 vya kulala kutoka vinane vya awali vikiwemo viwili kwa ajili ya watu mashuhuri.

Meneja huyo amesema kuwa mbali na kuongezeka kwa vyumba pia umejengwa ukumbi wa mikutano wenye uwezo wa kuchukua watu 100, mgahawa wa kisasa pamoja na sehemu ya kufulia nguo kwa ajili ya wageni na watu wote watakaohitaji huduma hiyo.

“Kwa sasa ujenzi huu umefikia asilimia 80  na unatarajia kukamilika mwezi Machi mwaka huu. Mradi huu utakapokamilika utakuwa ni moja ya chanzo cha ajira za kudumu 50, hivyo kuinua uchumi kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.”

Hoteli hiyo inayomilikiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilifunguliwa Septemba 1974 na iliendeshwa na Serikali yenyewe kwa lengo la kutoa huduma kwa wageni na hata wenyeji waliofika Pemba.

Lakini kutokana na uchakavu wake Serikali ikaamua kusitisha huduma zake na kuifunga ili kutafuta mwekezaji ambaye ataiendelea. Hoteli hiyo imekuwa haitumiki kwa kipindi cha takribani miaka 12.

Hata hivyo, Baraza la Mapinduzi chini ya Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein likaamua kuikabidhi ZSSF hoteli hiyo kwa lengo la kuifufua na kuiendeleza.

(mwisho)
IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU


Share:

Wananchi Mkoani Kagera Watakiwa Kufuatilia Na Kuhoji Kuhusu Miradi Ya Kimaendeleo Katika Kata Zao.

Na Avitus Benedicto Kyaruzi, Kagera.
Wananchi katika kata ya Katoma Mkoani Kagera wametakiwa kufuatilia kwa kina na kuhoji viongozi wao kuhusu miradi mbalimbali ya kimaendelao inayotekelezwa katika kata hiyo.
 
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Shirika lisilo la Kiserikali  la Faraja For Hope And Development (FAHODE) bwana Antidius  Augustine wakati akiongea  na wananchi wa kata ya Katoma katika mkutano wa hadhara na kuwataka wananchi hao kuweza kufuatilia kwa kina miradi mbalimbali ya kimaendeleo katika kata hiyo ikiwemo sekta ya maji na kuibua changamoto zinazoikabili sekta hiyo.
 
Shirika hilo lisilo la kiserikali linajiusisha na ufatiliaji wa uwajibikaji wa jamii katika sekta ya majii kwa kata sita za halmashauri ya Bukoba zikiwa ni pamoja na Kemondo, Katoro,Katerelo,Maruku, Katoma na Ibwela.
 
Bwana Antidius amesema kuwa shirika hilo litaendelea kuijengea jamii elimu kuhusu masuara mtambuka  ili kutumia vizuri rasilimali zilizopo na kupanua wigo wa kuendelea kutoa elimu kwa jamii ili kuendelea kutumia maji safi na salama kila siku.
 
Amewataka wananchi kukaa karibu na viongozi wao ili kuhakikisha miradi ya kimaendeleo haikwami kwani kwa kufanya hivo kutawawezesha pia kujua changamoto zinzokwamisha miradi hiyo na kuongeza kuwa FAHODE imekuwa chachu ya miradi mingi kukamilika  kwa wakatina kuwafikia walengwa kutokana na ushirikiano ambao wanazidi kupewa na wananchi hao.
 
Kwa upande wake diwani wa kata ya Katoma mh Deusdelith Rwekaza amesema kuwa wananchi wa kata hiyo pamoja na kata nyingine ambapo shirika hilo linahudumu kutumia vizuri elimu inayotolewa ili iweze kuwanufaisha katika maisha ya kila siku.
 
Aidha mh Rwekaza emewataka wananchi wa kata hiyo kuwa na utamaduni wa mara kwa mara wa kusafisha vyanzo mbalimbali  vya maji vinavyopatikana katika kata hiyo ikiwemo chemichemi  na vyanzo vingine.


Share:

Wakulima Wa Tumbaku Geita waiomba kampuni ya Petrobena kununua zao lao

SALVATORY NTANDU
Wakulima wa zao la Tumbaku katika wilaya za Mbogwe na Bukombe mkoani Geita wameiomba kampuni ya usambazaji wa Pembejeo  za kilimo ya Petrobena kuanza ununuzi wa zao hilo kwenye AMCOS tatu ambazo vizikosa wanunuzi wa zao hilo baada ya kampuni ya Tanzania Leaf Tobacco  Company Limited  (TLTC) kusitsha ununuzi wa zao hilo katika msimu uliopita.

Ombi hilo limetolewa jana na Catherin Agostino mkulima wa Tumbaku kutoka Wilaya ya Bukombe katika Mkutano mkuu wa Chama kikuuu cha Ushirika Mbogwe na Bukombe (MBCU) kilichofanyika jana wilayani Mbogwe na kuhudhuriwa na wajumbe mbalimbali wa AMCOS 35 zilizopo katika Ushirika huo.

“Tangu Kampuni ya TLTC imesitisha ununuzi wa Tumbaku wakulima wengi wamekata tamaa ya kuendelea na kilimo hiki kutokana na kukosa mnunuzi tunaiomba kampuni ya Petrobena kukubali kununua mazao yetu ili tuweze kuendeleza familia zetu”alisema Agostino.

Aliongeza kuwa kama wameweza kusambaza Pembejeo kwa wakulima wote hapa nchini kwa wakati na kuondoa urasimu uliokuwepo hapo awali wa kuchelewa kwa pembejeo na kusababisha wakulima kushindwa kulima kwa tija na kujikuta wameingia katika madeni makubwa ambayo hayawezi kulipika kwa haraka.

“Taarifa tulizonazo sisi wakulima wa Mbogwe na Bukombe ni kuwa kampuni ya PETROBENA msimu wa kilimo wa 2019/20 imefunga mkataba na AMCOS ya ngokolo iliyopo katika chama kikuu cha ushirika kahama (KACU) kwaajili ya kununua tumbaku hivyo tunaimbani ombi letu watalifanyia kazi”alisema Agostino.

Akilitolea Ufafanuzi suala hilo  Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini,  Dk Titus Kamani alisema kuwa serikali ya awamu ya Tano imehakikisha kero za wakulima zinapatiwa ufumbuzi ikiwemo suala la masoko ya mazao kwa kutafuta kampuni mbalimbali za ununuzi ambapo kwa mwaka huu vyama vyote vilivyokuwa vinalima tumbaku zimepata wanunuzi.

“Mbogwe na Bukombe mmepata wanunuzi katika zao la Tumbaku na Pamba changamoto iliyojitokeza  mwaka huu ni kwamba baadhi ya taasisi za kifedha zimegoma kutoa mikopo kwa kampuni ya Grand Tobacco limite ambayo mmefunga nayo mkataba na  AMCOS zetu  sisi kama serikali tutalifanyika kazi na mtapata majibu kwa haraka”alisema Dk Kamani.

Pia Dk Kamani aliwataka pia viongozi wa vyama vikuu na AMCOS kuhakikisha wanatenga fedha kwaaajili ya kununulia pembejeo katika msimu ujao wa kilimo wa 2020/21 ili kuondokana  na mikopo kutoka katika taasisi za kifedha ambayoimekuwa na riba kubwa  isiyokuwa na tija kwa Wakulima.

Dk Kamani aliwataka viongozi wa AMCOS zote zilizaopo katika mkoa wa Geita kuhakikisha wanajiunga na chama kikuu cha ushirika Mbogwe na Bukombe (MBCU) ili wawezekusaidiwa kwa ukaribu na serikali kupita viongozi wao  pindi wanapopata matatizo sambamba na kupata huduma zingine ikiwepo mikopo ya pembejeo za kilimo.

Mwisho.


Share:

Godfrey Simango Nyaisa Ateuliwa Kuwa Afisa Mtendaji Mkuu Wa BRELA




Share:

Waziri Mkuu: Ujenzi Ofisi Na Studio Za Zbc Pemba Ukamilike Kwa Wakati

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua mradi wa ujenzi wa ofisi na studio za Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) na kuwaagiza wahusika wahakikishe mradi huo unakamilika kwa wakati.

Ametoa maagizo hayo jana (Jumapili, Januari 19, 2020) wakati akizungumza na watumishi wa ZBC na wananchi baada ya kukagua mradi huo uliopo katika wilaya ya Chakechake, Mkoa wa Kusini Pemba. Mradi huo wenye thamani ya sh. bilioni 1.4.

Waziri Mkuu amesema kukamilika kwa ujenzi wa ofisi na studio za ZBC kisiwani Pemba kutaboresha sekta ya TEHAMA, hivyo kuwawezesha wananchi kupata taarifa za ndani na nje kwa wakati. “Tunaimarisha ZBC ili kila mtu aweze kupata habari kwa wakati.”

Pia, Waziri Mkuu amewaagiza watumishi wa ZBC waongeze ubunifu katika utayarishaji wa vipindi vyao pamoja na kutenga muda kwa ajili ya kutembelea mashirika mengine ya utangazaji kwa lengo la kujifunza.

Kabla ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuifanyia maboresho studio yake ya kurushia matangazo ya Pemba wananchi wa kisiwa hicho walikuwa wanakaa hadi wiki moja bila ya kusikia habari zinazohusu kisiwa hicho.

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwataka wananchi waendelee kuwa na imani na Serikali kwa sababu imejipanga katika kutoa huduma mbalimbali za kijamii zikiwemo za maji, afya, elimu kwa Watanzania wote bila ya ubaguzi wa aina yoyote.

Pia, Waziri Mkuu amewasisitiza wananchi waendelee kudumisha amani na utulivu na wasikubali kushiriki katika matukio yenye viashiria vya uvunjifu wa amani kwa kuwa hayana tija.

“Amani, utulivu na mshikamo tulionao nchini haujaja kwa bahati mbaya bali umeasisiwa na viongozi wa kwanza wa Taifa letu hayati Mwalimu Julius Nyerere pamoja na Sheikh Abeid Aman Karume hivyo ni muhimu tukawaenzi waasisi wetu kwa kuimarisha amani.”

Awali,Waziri Mkuu alikagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba sita za Askari Polisi zinazojengwa katika eneo la Mfikiwa wilayani Chakechake. Kati ya nyumba hizo sita, tano tayari zimekamilika na zinatumika. Nyumba moja ipo kwenye hatua za kukamilika.

Kadhalika, Waziri Mkuu alishuhudia matofali 52,000 yaliyopo eneo hilo na kuiagiza Wizara ya Mambo ya Ndani itenge fedha za kugharamia ujenzi wa nyumba sita nyingine zinazokadiriwa kugharimu kiasi cha sh. 35,000,000 kwa nyumba moja iwapo zitajengwa kwa mfumo wa force account.


Share:

Ujerumani: Marekani imeshindwa katika makabiliano yake na Iran

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Heiko Maas amekosoa sera za rais Donald Trump wa Marekani za kuongeza shinikizo dhidi ya Iran. 

Maas ameliambia gazeti la Ujerumani la Bild am Sonntag kwamba hawapaswi kudhania kwamba shinikizo kutoka nje dhidi ya Iran litaweza kuimarisha hali ilivyo nchini humo na kuongeza kuwa hatua kama hiyo ilikuwa na matokeo mabaya katika nchi kama Iraq. 

Maas amesema vitisho dhahiri pamoja na hatua za kijeshi na vitisho havijaweza kubadilisha tabia za kiuongozi za Tehran. 

Chama cha Social Democrat, SPD kimesisitiza kwamba mazungumzo ni njia muhimu itakayosaidia kupiga hatua na kuimarisha sera ya Ulaya kuelekea taifa hilo.


Share:

Kiwanda Cha Kuchakata Nyama Cha Tanchoice Kuzalisha Ajira 500

Kiwanda cha kuchakata nyama na machinjio ya mifugo cha Tan Choice kinatarajiwa kuzalisha ajira 500 za kudumu katika fani mbalimbali nchini mara baada ya kuanza kazi rasmi mapema Machi, 2020.

Hayo yamesemwa na Msemaji wa kiwanda hicho Bw. Albert Kilalah wakati akiwasilisha taarifa ya kiwanda kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji nchini Mhe. Angellah Kairuki alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda pamoja na kusikiliza na kutatua changamoto zilizowasilishwa za kiwanda hicho.

Waziri Kairuki alifanya ziara hiyo (Ijumaa tarehe 17 Januari, 2020) ambapo alipata fursa za kukagua maeneo ya kiwanda hicho chenye uwezo wa kuchakata nyama bora (organic meet) na kusema amevutiwa na kupongeza jitihada za uwekezaji huo mkubwa.

“Nimefarijika kuwa hadi sasa mmeweza kutoa ajira zaidi ya 300 na ni matarajio yenu kutoa ajira 500 kiwanda kitakapoanza kazi mapema mwaka huu na tutaendelea kuwaunga mkono ili kuwafikia wananchi kwa utoaji wa bidhaa bora zenye uhakika,”alisema Waziri Kairuki.

Waziri alieleza kuwa huo ni uwekezaji mkubwa wenye tija ambapo hadi sasa umegharimu zaidi ya Tshs bilioni 25, hivyo ni kiwanda cha mfano kwa nchi za Afrika ya Kati na kuahidi kutoa ushirikiano ili kufikia malengo ya kiwanda hicho.

Aidha Msemaji wa Mradi huo alieleza uwepo wa kiwanda hicho ulizingatia mahitaji ya nyama bora na mazingira rafiki ya uwekezaji yaliyopo nchini kwa kuzingatia umuhimu wa wawekezaji na wafanyabiashara.

“Bodi ya Tan Choice ilivutiwa uwekezaji kwenye sekta ya nyama kutokana na uwepo wa mazingira rafiki ya uwekezaji nchini chini ya Serikali ya Awamu ya Tano na uwepo wa mifugo itayowezesha uendeshaji wa miradi huu na kukidhi soko la ndani na nje ya nchi,” alisema Bw. Albert Kilalah

Alieleza kiwanda hicho ni fursa kwa wafugaji na wafanyabiashara wa mifugo nchini ambapo zaidi ya watu 10000 watanufaika kiuchumi kwa kuzingatia uhakika wa soko la nyama na mazao yatokanayo na mifugo.

Alifafanua, Kiwanda hicho kitakuwa cha pili kwa ukumbwa kwa nchi za Africa Mashariki kikifuatiwa na kiwanda cha Ethiopia ambacho kina uwezo wa kuchinja ng’ombe 3,000, kondoo na mbuzi 6,000 kuzalisha zaidi ya tani 300 kwa siku.

“Kiwanda kitakapokamilika kitakuwa kikubwa na bora cha aina yake katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati  na kitakuwa na uwezo wa kuchinja ng’ombe 1,000 na mbuzi na kondoo 4,500 kwa siku nyama na mazao mengine yatakayozaliswa na kiwanda yatazingatia ubora na usalama,”alisema Kilalah.

Alisema kuwa, Tan Choice inatarajia kuuza nyama soko la nchi za Uarabuni Mashariki ya Kati ikiwemo Falme za Kiarabu (UAE) na Saudi Arabia pamoja na masoko yatakayo jitokeza ikiwemo China, Malaysia, Vietnam na Indonesia pamoja kutumia fursa ya soko huru la kibiashara litakaloazishwa barani Afrika na kuuza nyama hiyo.

Akihitimisha taarifa hiyo aliomba Serikali kuendelea kuboresha barabara kutoka eneo la kiwanda hadi Kongowe iboreshwe kwa viwango vya lami ili kurahisisha usafirishaji wa mifugo kiwandani na pamoja na nyama zitakazozalishwa kwenda uwanja wa ndege, bandarini na masoko ya ndani.

Aidha aliomba kuwe na uboreshwaji wa minada ili kuwe na uhakika wa upatikanaji wa wanyama wengi na wenye uhakika.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Mhe. Asupter Mshama alishukuru wawekezaji katika Wilaya yake, na kuwatoa shaka juu ya utatuzi wa changamoto walizonazo na kuendelea kuunga mkono jitihada zao kwa kuhakikisha huduma muhimu ikiwemo, nishati ya umeme, maji, barabara na mawasilino vinazingatiwa ili kuwa na manufaa ya uzalishaji wa kiwanda.

=MWISHO=


Share:

Waasi wa Yemen Wanaoungwa Mkono na Iran Waua Wanajeshi 80

Zaidi ya wanajeshi 80 wa Yemen wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa katika shambulizi la kombora na ndege zisizokuwa na rubani linalodaiwa kufanywa na waasi wa Houthi. 

Shambulizi hilo linafanywa baada ya miezi kadhaa ya utulivu katikati ya vita kati Wahouthi wanaoungwa mkono na Iran na serikali ya Yemen inayotambuliwa na jumuiya ya kimataifa inayoungwa mkono na majeshi yanayoongozwa na Saudi Arabia. 

Vyanzo kutoka hospitali ya Marib ambako wahanga wa shambulizi hilo walipelekwa, vinasema wanajeshi 83 waliuawa na 148 walijeruhiwa. 

Shambulizi hilo linakuja siku moja baada ya muungano unaosaidiwa na majeshi ya serikali kuanzisha operesheni kubwa dhidi ya Wahouthi katika eneo la Nihm, kaskazini mwa mji mkuu Sanaa.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu January 20


















Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger