Monday, 13 January 2020

Breaking News : BASI LA BRIGHT LINE LAPATA AJALI SHINYANGA...KUNA VIFO NA MAJERUHI



Basi la Bright Line lililokuwa linatoka Mwanza kwenda Dodoma limepata ajali katika eneo la Isela barabara ya Shinyanga - Tinde baada ya kugongana na gari dogo na pikipiki. Taarifa za awali zinasema kuna vifo na majeruhi kadhaa. Inaelezwa kuwa mwendesha bodaboda na abiria wake wamepoteza maisha bado wamelaliwa na basi. Tutawaletea taarifa kamili hivi punde





Share:

WALIMU WATATU WAUAWA KWA SHAMBULIZI LA KIGAIDI KENYA



Watu watatu wameuawa baada ya wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa Al Shabab kuvamia mji wa Garisa kaskazini mwa Kenya katika mpaka wa Kenya na Somalia.

Walimu watatu ambao si wa eneo hilo walipigwa risasi hadi kufa huku kituo cha polisi kikichomwa moto na mfumo wa mawasiliano kuharibiwa katika eneo la Kamuthe mapema leo asubihi.

Washambuliaji hao pia wameharibu mawasiliano kabla ya kutoroka.
Maafisa wa polisi wanafuatilia wavamizi hao huku ripoti za kiusalama zikionyesha kwamba wavamizi wameweka vilipuzi chini ya ardhi katika barabara ya eneo hilo.

Kenya imekuwa katika hali ya tahadhari baada ya kupata taarifa za kijasusi kwamba kundi la Al Shabab linapanga kufanya mashambulio zaidi.

Wiki iliyopita, Uingereza imetoa onyo kwa raia wake wanaotaka kusafiri nchini humo dhidi ya kutembelea kaunti ya Garissa na katika eneo la ndani ya kilomita 60 katika mpaka wa Kenya na Somalia.

Hili ni shambulizi la 11 kutekelezwa na kundi la Al Shabab nchini Kenya katika kipindi cha wiki 6. Mashambulizi 4 yakitekelezwa Garissa, 3 Wajir, 2 Mandera na 2 Lamu.
Chanzo - BBC
Share:

Madiwani Waagiza Kuchukuliwa Hatua Kwa Wauguzi Waliosabisha Wakimama Kujifungilia Mapokezi

NA TIGANYA VINCENT
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge wamewaagiza Afisa Utumishi na Mganga Mkuu wa Wilaya (DMO) kuwachukua hatua Wauguzi wote walisababishia baadhi ya wakinamama kujifungulia mapokezi wakiwa wanasubiri huduma.

Azimio hilo limetolewa jana na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo kwenye  mkutano wa Baraza la Madiwani la Sikonge la kujadili na kupitia mapendekezo ya makisio ya mapato na matumizi ya mwaka 2020/21 baada ya baadhi ya Madiwani kulalamikia uzembe wa wauguzi ulisababisha baadhi ya wanawake kujifungua bila msaada wa Muunguzi.

Alisema ni vema wawaonyeshe hatua mbalimbali walizowachukulia Wauguzi wa Zahanati ya Kirumbi, Kisanga na Lembeli na watumishi walevi nyakati za kazi na Baraza la Madiwani lipatiwe taarifa.

Nzalalila alisema kama watashindwa kuwachukulia hatua itabidi Baraza limchukulie hatua Afisa Utumishi na Mganga mkuu wa Wilaya ya kushindwa kuwasimamia watumishi waliochini yao.

Awali Diwani wa kata ya Kipanga Upendo Mgombozi alisema mama mmoja mjamzito alilazimika kujifungulia mapokezi baada ya Muuguzi wa Zamu kudai hawezi kwenda kumsaidia kwa sababu ya hali aliyonayo kiafya.

Alisema mama huyo alijifungua mbele ya mume wake akiwa hana msaada wa Muuguzi yoyote na kuongeza kuwa angaweza hata kupoteza maisha kwa sababu ya kutokuwa na msaada wa mtaalamu.

Diwani huyo aliongeza kuwa hata alipomwita katika Kamati ya Kata kwa ajili ya kumuonya alishikiria msimamo wake kwamba asingeweza kumsaidia mama yule kwa sababu ya hali aliyokuwa nayo siku ile.

Akijibu hoja za Madiwani Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Dkt. Peter Songoro alisema baadhi ya wauguzi waliozembea na kusababisha baadhi ya  wanawake kujifungia wakiwa wanagonja huduma wameshapewa onyo na Muuguzi mwingine tuhuma zake zinaendelea kufanyiwa kazi na itakapokamilika watatoa taaifa ya hatua waliomchukulia.

Aliongeza kuwa Zahanati hazipaswi kufungwa bali zinatakiwa kufanyakazi saa 24 kila siku na kunakuwepo kwa mtumishi wa zamu kulingana na mpango kazi na ratiba ya zamu waliojipangia.

Aidha Dkt. Songoro aliwaomba Madiwani kuwahamasisha wananchi kushiriki katika ulinzi wa Zahanati katika maeneo yao.

Alisema kuwa Zahanati hizo zina miliki vifaa vya gharama kubwa na kunapokuwa hakuna ulinzi inasababisha hatari ya kupotea na wakati mwingine nyakati za usiku inasababisha maisha ya watu ambao wengine wanakaa mbali na Zahanati kuwa hatarini.


Share:

TICTS YAFANYA BONANZA LA MICHEZO KWA WAFANYAKAZI WAKE KUIMARISHA AFYA


Wafanyakazi wa Kampuni ya Kimataifa ya kuhudumia shehena ya kontena bandarini (TICTS), mwishoni mwa wiki walikusanyika kwa pamoja kufanya mazoezi ya kuimarisha afya zao, mazoezi yanayofanyika kila mwanzo wa mwaka kwa Wafanyakazi hao kufanya shughuli mbalimbali za michezo ili kuimarisha afya zao mahala pa kazi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa Bonanza hilo, Mkurugenzi wa Shirika na Maendeleo wa Kampuni hiyo, Donald Talawa amesema wafanyakazi hao wamekusanyika kwa pamoja kufanya shughuli hizo za michezo ili kuimarisha afya zao na kuleta tija wawapo kazini.

“Wafanyakazi wamefanya riadha ya KM 5 na 21, Mpira wa Miguu, kuvuta kamba na michezo mbalimbali, tunaamini hii italeta tija na ufanisi mahala pa kazi kwa kufanya hivi mara kwa mara”, amesema Talawa.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Wafanyakazi hao, Getrude Lamu amesema wamefanyakazi wamefurahi sana kufanya mazoezi katika michezo mbalimbali katika bonanza hilo, amesema wamehamasisha michezo hiyo mahali pa kazi kwa kufanya mazoezi mara kwa mara.

“Wafanyakazi wa TICTS katika bonanza la leo wamefika kwa wingi na wamefurahi sana kufanya bonanza hili, mwezi huu ni mwezi wa mazoezi, tunashughuru utawala wa Kampuni yetu kuleta kitu hiki kwa Wafanyakaziwetu”, amesema Getrude Lamu. 

Endelea kuangalia picha mbalimbali za michezo hiyo hapo chini.

Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu January 13























Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger