Friday, 10 January 2020

JAMBO YATAMBULISHA BIDHAA TATU MPYA “JAWIZA APPLE CRUSH SODA, JAMUKAYA JUISI YA UKWAJU NA UBUYU”

Jawiza Apple Crush  Soda
Jamukaya Ubuyu Juice
Jamukaya Ukwaju Juice

Na Moshi Ndugulile - Shinyanga 
Kampuni ya Jambo Food Products Limited iliyopo Mkoani Shinyanga imezindua bidhaa mpya ya Jawiza Apple Crush Soda,Juisi ya Ukwaju na Ubuyu zenye ujazo wa mili lita 300 ambazo zinapatikana kwa bei ya reja reja shilingi 500/= bei ambayo ni ya kizalendo kwa kila Mtanzania kwenye kipato cha kawaida. 

Bidhaa hizo tatu zenye ubora wa kimataifa zilizotengenezwa kwa ubora wa hali ya juu kwa kutumia teknolojia ya kisasa yenye mitambo kutoka Ujerumani zimetambulishwa rasmi leo Ijumaa Januari 10,2020. 

Akizungumza wakati wa kutambulisha bidhaa hizo, Meneja masoko wa Kampuni ya Jambo Food Products Innocent Mafuru amesema Bidhaa mpya ya Apple Crush Soda ina ladha ya Apple inayotokana na matunda asili yanayopatikana hapa nchini Tanzania. 

“Jambo Food Products Limited tunayo furaha kuwatangazia wateja wetu nchi Nzima ujio rasmi wa wa bidhaa yetu mpya ya Apple Crush Soda. Apple Crush Soda ni kati ya bidhaa tulizonazo na kila mara tumeona ni vizuri kuwapa wateja wetu kitu kipya kulingana na mahitaji yao. 

Bidhaa ya Apple Crush Soda ina ujazo wa mili lita 300 na inapatikana nch nzima kwenye maduka yote ya jumla na reja reja kwa bei ya kizalendo ya shilingi 500/= pesa ya Kitanzania. Tumeweka bei hii ili kumfanya kila Mtanzania awe na uwezo wa kukata kiu na kuonja ladha tofauti kutoka kwetu”,ameeleza Mafuru. 

Mafuru amesema mbali na kuzindua Apple Crush Soda pia wamezindua bidhaa nyingine mbili za Juisi zenye ladha ya Ukwaju na nyingine yenye ladha ya Ubuyu. 

“Bidhaa za Juisi ya Ukwaju na Ubuyu zote zina ujazo wa mili lita 300 na zinapatikana kwa bei ya reja reja shilingi 500/= bei ambayo ni ya Kizalendo kwa kila Mtanzania mwenye kipato cha kawaida”,ameongeza Mafuru. 

"Ubora wa bidhaa hizi ni wa kimataifa ,mchakato wa utengenezaji wake umechukua miezi nane mpaka kupata ubora huu.Bidhaa hizi ni salama na zina faida mbalimbali kiafya,ikiwemo Vitamini C na virutubisho mbalimbali katika kuupa mwili kinga”,amesema Mafuru. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jambo food Products Limited Salum Khamis amesema uwekezaji wa biashara zake umezingatia uzalendo kwa Watanzania na kwamba ni fursa kubwa katika utoaji wa ajira hasa kwa wazawa na kwamba kundi la wanawake linapewa kipaumbele zaidi. 

“Jambo Food Products tumeendelea kuwa wazalishaji wa vinywaji baridi vyenye ubora kwa kutumia teknolojia ya kisasa yenye mitambo kutoka Ujerumani na mwaka huu 2020 tumejipanga kuwafikia wateja wetu nchi nzima kwa kuongeza wasambazaji na mawakala nchi nzima ili kusogeza huduma zetu kwa kila Mtanzania”,ameeleza Khamis. 

“Tumekuwepo sokoni kwa muda wa miaka mitatu lakini kwa muda huo tumeweza kuwafikia wateja wengi hususani Kanda ya Ziwa na tunawashukuru wateja wetu kwa kutufanya kuwa chaguo lao namba moja”,amema Khamis. 

Amewaomba wateja wao kuendelea kufurahia bidhaa zao mpya na wajivunie bidhaa zenye ubora wa kimataifa zilizotengenezwa nchini Tanzania kwa bei ya kizalendo.

Share:

Video Mpya : NYUMBU MJANJA - LETA MBEGE


Hii hapa video mpya ya Nyumbu Mjanja  inaitwa Leta mbege. Itazame hapa chini

Share:

Waziri Mabula Aitaka Bodi Ya NHC Kupitia Upya Gharama Za Nyumba Inazouza

Na Munir Shemweta, WANMM MASASI
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameitaka Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kupitia upya gharama za nyumba zake ilizojenga maeneo ya pembezoni kwa ajili ya kuziuza.

Dkt Mabula alitoa kauli hiyo jana wilayani Masasi mkoa wa Mtwara wakati alipotembelea mradi wa nyumba 54 zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi katika mikoa ya Kusini pamoja na kutembelea miradi inayofanywa na NHC katika maeneo mbalimbali nchini.

Kauli hiyo ya Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi inafuatia kulalamikiwa na wabunge wa Majimbo ya Masasi Dkt Rashid Chuachua na yule wa jimbo la Lulindi  mkoani Mtwara Jerome Bwanausi kuwa pamoja na halmashauri kuhitaji nyumba kwa ajili ya watumishi lakini gharama imekuwa kubwa kiasi cha halmashauri na wananchi kushindwa kuzinunua.

‘’ Ni vizuri bodi ikae iangalia namna ya kupitia upya gharama za nyumba zote zilizopo maeneo ya pembezoni kama hizi za Masasi maana zikiachwe bila kununuliwa itakuwa ni hasara’’ alisema Dkt Mabula.

Naibu Waziri Mabula alisema, hata kama nyumba hizo zilizojengwa kwa ajili ya kuuza hazitanunuliwa basi NHC iangaliae namna ya kuzipangisha na kueleza uhitaji wa nyumba katika eneo la Masasi upo na watumisi wa serikali wanahitaji kuisha maeneo rafiki.

Hata hivyo, amezitaka halmashauri nchini kulitumia Shirika la Nyumba la Taifa kujenga miradi ya nyumba za watumishi kulingana na mahitaji ili kuepuka kujenga nyumba ambazo mwisho wa siku zinaweza zisinunuliwe.

Kwa upande wake Meneja Mawasiliano wa Shirika la Nyumba la Taifa Muungano Saguya alisema shirika lake liko katika hatua za mwisho za kukamilisha mradi huo uliokuwa umesimama kwa muda ambapo takriban milioni 600 zitatumika kuukamilisha na kusisitiza imani yake katika kipindi cha miezi sita ujenzi utakamilika.

Kwa mujibu wa Saguya, bei inayolalamikiwa ya shilingi milioni 54 kwa nyumba moja inatokana na gharama kubwa iliyotumiwa na Shirika la Nyumba la Taifa kuzijenga nyumba hizo na kubainisha kuwa NHC iko mbioni kuzipangisha baadhi ya nyumba ambazo wananchi wameonesha nia ya kupanga.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula alizitembea wilaya za Nanyumbu na Tunduru na kukagua utendaji kazi katika sekta ya ardhi katika halmashauri za wilaya hizo.

Dkt Mabula alibaini utunzaji mbovu wa kumbukumbu za majala ya ardhi pamoja na kiasi kidogo cha makusanyo ya maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi ambapo aliziagiza halmashauri za Nanyumbu na Tunduru kuongeza kasi ya makusanyo ya kodi ya pango la ardhi sambamba na kuzingatia utunzaji majalada ya ardhi kwa kufuata taratibu ikiwemo kuwepo mawasiliano katika majalada hayo kutoka afisa mmoja kwenda kwa mwingine.


Share:

WAZIRI UMMY ATOA MILIONI 2.5 KWA AJILI YA USHONAJI WA SARE 100 ZA WATOTO YATIMA SHULE YA MSINGI JIJINI TANGA


 MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kushoto akimkabidhi fedha Taslimu kiasi cha Milioni 2.5 Mwenyekiti wa Kikundi cha Ushonaji cha Vijana cha Tanga Youth Tailoring Industry (Tayotai) Liliani Michael kwa ajili ya kushona sare 100 za watoto yatima wa shule za Msingi Jijini Tanga ambapo fedha hizo zimetolewa na Mbunge Ummy

 MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kushoto akisisitiza jambo mara baada ya kukabidhi fedha Taslimu kiasi cha Milioni 2.5 Mwenyekiti wa Kikundi cha Ushonaji cha Vijana cha Tanga Youth Tailoring Industry (Tayotai) Liliani Michael kwa ajili ya kushona sare 100 za watoto yatima wa shule za Msingi Jijini Tanga ambapo fedha hizo zimetolewa na Mbunge Ummy

 MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kushoto akisisitiza jambo mara baada ya kukabidhi fedha Taslimu kiasi cha Milioni 2.5 Mwenyekiti wa Kikundi cha Ushonaji cha Vijana cha Tanga Youth Tailoring Industry (Tayotai) Liliani Michael kwa ajili ya kushona sare 100 za watoto yatima wa shule za Msingi Jijini Tanga ambapo fedha hizo zimetolewa na Mbunge Ummy

 MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kushoto akizungumza jambo mara baada ya kukabidhi fedha Taslimu kiasi cha Milioni 2.5 Mwenyekiti wa Kikundi cha Ushonaji cha Vijana cha Tanga Youth Tailoring Industry (Tayotai) Liliani Michael aliyesimama kulia kwa ajili ya kushona sare 100 za watoto yatima wa shule za Msingi Jijini Tanga ambapo fedha hizo zimetolewa na Mbunge Ummy
 MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kushoto akiangalia nguo ambazo zinashonwa na kikundi hicho mara baada ya kukitembelea kulia ni Mwenyekiti wa Kikundi hicho Lilian Michael
 MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katikati akiteta jambo Mwenyekiti wa Kikundi cha Ushonaji cha Vijana cha Tanga Youth Tailoring Industry (Tayotai) Liliani Michael mara baada ya kukabidhi fedha Taslimu kiasi cha Milioni 2.5 Mwenyekiti kwa ajili ya kushona sare 100 za watoto yatima wa shule za Msingi Jijini Tanga kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa na Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji
 MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kulia akitazama nguo ambazo zinashonwa na  Kikundi cha Ushonaji cha Vijana cha Tanga Youth Tailoring Industry (Tayotai)  mara baada ya kukabidhi fedha Taslimu kiasi cha Milioni 2.5 Mwenyekiti  wa Kikundi hicho Lilian Michael kwa ajili ya kushona sare 100 za watoto yatima wa shule za Msingi Jijini Tanga kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa na Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji
 MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kushoto akiangalia nguo zinazoshonwa na kikundi Ushonaji hicho mara baada ya kukitembela kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa na katikati mwenye shati jeuzi na mistari ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji
 MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katikati akiteta jambo na Mwenyekiti wa Kikundi cha Ushonaji cha Vijana cha Tanga Youth Tailoring Industry (Tayotai) Liliani Michael mara baada ya kukabidhi fedha Taslimu kiasi cha Milioni 2.5 Mwenyekiti kwa ajili ya kushona sare 100 za watoto yatima wa shule za Msingi Jijini Tanga kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa na Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji


MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa Afya MAendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto ametoa sh.milioni 2.5 kwenye kikundi cha ushonaji cha Vijana Tanga Youth Tailoring Industry (Tayotai) kwa ajili ya kushona sare 100 za wanafunzi yatima wa shule za Msingi Jijini Tanga.

Fedha hizo zimekabidhiwa na Waziri Ummy kwa Mwenyekiti wa Kikundi hicho Lilian Michael wakati alipotembelea na kujionea namna wanavyofanya shughuli zao ikiwemo changamoto ambazo wanakabiliana nazo huku akihaidi kushirikiana nao.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi fedha hizo, Mbunge Ummy alisema ametoa fedha ili kuweza kuwasaidia wanafunzi hao ambao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali kutokana na kukosa wazazi ambao wanaweza kuwanunulia.

“Niwapongeze kwa kazi nzuri mnayoifanya hapa kwenye kikundi chenu mimi nitawaunga mkono na leo nitawakabidhi milioni 2.5 kwa ajili kuwashonea sare watoto yatima 100 kwenye Jiji la Tanga”Alisema Waziri huyo
.
Aidha pia alimtaka Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji waweke utaratibu wa watoto wanaoanza darasa la kwanza shule za msingi wapate unifomu shuleni kwa kushonewa na kikundi hiki cha vijana cha Tanga Youth Tailoring Industry (Tayotai).

“Kutokana na kwamba kikundi hiki kinafanya kazi nzuri hivyo wapeni tenda ya ajira kwani mtaji umewekwa na vifaa vipo suala lingine ni kutoa maelekezo watoto wanaonza darasa la kwanza kupata sare shuleni “Alisema

Waziri huyo alisema kwamba kikundi hicho walipewa mkopo wa milioni 100 huku akieleza kwamba sera ya maendeleo ya wanawake ambao ni sehemu ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halamshauri ipo chini ya wizara yake.

Alisema kwamba wasije kuwaambia Halmashauri watoe mikopo lakini hatuoni maendeleo kwenye hili huku akiwapongeza Jiji hilo kwa kutekeleza sheria ya kutenge fedha kwa ajili ya wakina mama vijana na watu wenye walemavu.

Waziri huyo alisema kwamba fedha hizo zimetoka kwa kununua vifaa na ela za uendeshaji huku akimtaka Mwenyekiti wa Kikundi hicho kuhakikisha wanafanya kazi kwa ufanisi mkubwa ili matokeo yake yaanze kuonekana.

“Kwa sasa hiyo milioni 100 mliopata kutoka Halmashauri tunachotaka irudi waweze kukopeshwa kikundi kingine sasa tumepeana muda kwa mwenendo walionao nawaombea waongezewe muda ili waweze kurejesha fedha hizo “Alisema Waziri Ummy

Awali akizungumza wakati akitoa taarifa ya mradi wa ushonaji wa Kikundi cha Vijana cha Tanga Youth Tailoring Industry (Tayotai) Mwenyekiti wa Kikundi hicho Liliani Michael alimshukuru Waziri Ummy kwa kuwasaidia kwenye kikundi hicho ambalo alisema kimeanzishwa mwezi Machi 2019 kikiwa na jumla ya wanachama 32 wakiwa ni wasichana.

Alisema kikundi hicho kinajishughulisha na ushonaji wa cherehani ambapo kinashona nguo na mitindo tofauti kwa makundi yote huku akieleza lengo la mradi huo ni kuimarisha maisha ya wanachama kiuchumi na kijamii.

“Lakini pia kutoa suluhisho la tatizo la ajira kwa vijana ikiwemo kusaidia kutatua changamoto za kijamii sambamba na kutekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya serikali ya awamu ya tano inayo ongozwa na Rais Dkt John Magufuli kuelekea uchumi wa viwanda kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025”Alisema

Mwenyekiti huyo alisema kwamba ili kufikia malengo yao waliwa silisha maombi kwa Halamshauri ya Jiji la Tanga ili wapatiwe mkopo kupitia asilimia 10 ya mapato yake ya ndani.

“Hivyo Halmashauri imetupatia mkopo wa milioni 100 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya ushonaji vya kisasa pamoja na mtaji wa kuanzia biashara kupitia mkopo Halmashauri ilikiwezesha kikundi chetu kwa kutununulia vifaa kama vile Cherahani za kisasa za kushonea 35, Overlock 1, Mashine ya kudarizi mashuka na vitambaa 3, kudarizi nguo 2, kufuma masweta 2,kuweka nembo 2,kushona vifungo 1,kugongesha vifungo 3 na kutupatia fedha taslimu kwa ajili ya uendeshaji “Alisema

Share:

Huduma za fedha kwa njia ya simu zinavyosaidia kukuza uchumi nchini

Katika siku za hivi karibuni huduma ya kutuma fedha, kupokea na kulipa kupitia simu za mkononi imekuwa jambo kubwa nchini na kwa kiasi kikubwa kichocheo cha maendeleo yetu. 

Tafiti nyingi zinaonyesha kuwa faida zinazohusiana na huduma za kifedha kwa njia ya simu za mkononi zinachangia sana kwenye kubadilisha nchi yetu kidijitali na kutusaidia kufikia malengo ya maendeleo kuelekea mwaka 2025. 
 
Huduma hii imewezesha watu wengi zaidi katika mfumo rasmi wa kifedha (financial inclusion). Imewapa njia rahisi na ya hakika wananchi wa kawaida na biashara kuweka akiba, kuwekeza, kutuma, kutoa na huduma nyingine lukuki ambazo sote sasa tunazitumia kidijitali. Kwa wafanyabiashara wadogo na wakati imewasaidia kukua zaidi, kukuza mtaji na kuongeza uwekezaji na ajira. 
 
Licha ya maendeleo haya, bado wako ambao huduma hizi rasmi za kifedha na mitaji hazijawafikia. Hatua inayofuata sasa ni kuhakikisha wale wote ambao hawajafikiwa na matunda haya ya maendeleo nao wanayapata na huduma ya fedha kwa njia ya simu ni njia muhimu na kuu zaidi kufikia watu hawa. 

Kukua zaidi kwa huduma hii kunategemea msingi mzuri wa uwekezaji katika sekta ya mawasiliano ya simu na mazingira mazuri ya kufanya biashara.  
 
Tuungane pamoja kuendelea kuipa nguvu sekta ya mawasiliano ya simu ili iendelee kutanuka zaidi ili sote tufaidi matunda yake. Miezi michache iliyopita kampuni mbili za Tigo na Zantel zimeunganisha shughuli zao. 

Hii ni hatua mojawapo ya kuboresha soko na kutoa huduma bora zaidi kwa taifa. Tukianza mwaka huu mpya wa 2020 tuendelee kutumaini kwamba sekta hii itaendelea kuwa bunifu ili kusukuma mbele dira ya maendeleo ya nchi kuelekea mwaka 2025.


Share:

Waziri Lugola Awaondoa Madarakani Maafisa Wa NIDA Mkoa Wa Ruvuma

Na Mwandishi Wetu, MOHA, Songea.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola  amemuondoa madarakani Afisa wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Mkoa wa Ruvuma, Seif Mgonja kwa kosa la kutogawa kwa wananchi Namba za Utambulisho wa Taifa (NIN), 14,493 tangu Disemba 31, 2019, licha ya kuzalishwa na Makao Makuu na kuletewa ofisini kwake Mjini Songea.

Pia Waziri Lugola amemuondoa madarakani Afisa wa NIDA Wilaya ya Namtumbo, Mkoani humo, Thobias Nangalaba kwa uzembe wa kutofika katika kikao chake cha viongozi wa Mkoa na Wilaya, licha ya kupewa taarifa ya kuhudhuria kikao hicho.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Viwanja vya Soko Kuu la Manispaa ya Songea Mkoani humo, leo, Waziri Lugola amesema, amewatengua vyeo
maafisa wawili hao kwa kucheza na kazi za Serikali, kwa kutojali majukumu yao.

“Ndugu wananchi wa Songea, maafisa hawa wamekuwa wakienda kinyume na maagizo ya Serikali la kuwataka waweze kuwakamilishia wananchi usajili wa laini za simu kwa alama za vidole kwa wakati, hivyo hawatufai na wanapaswa watupishe ili wengine waweze kuiongoza NIDA Mkoani hapa, haiwezekani Afisa wa NIDA Mkoa anacheza na wananchi kwa kutopeleka taarifa ili waweze kupata fursa ya kusajili laini zao  ambapo zoezi hilo linatarajia kukamilika Januari 20 mwaka huu,” alisema Lugola.

Alisema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli inawajali wanyonge hivyo yeye Waziri wa Mambo ya Ndani ya Ndani ya Nchi, anapambana na watu wanaokwamisha jitihada za Serikali.

Aidha, Waziri Lugola aliitaka Idara ya Uhamiaji Mkoani humo kufanya kazi usiku na mchana wakishirikiana na Jeshi la Polisi kuwasaka wahamiaji haramu hasa katika eneo la mpaka wa Tanzania na Msumbiji Mkoani humo.

“Ndugu wananchi, toeni taarifa za wahamiaji haramu, itasaidia kuwakamata na pia kuwashughulikia ipasavyo kwakuwa watu hao ni hatari kwa uhalifu,” alisema Lugola.
 
Aliongeza kuwa, Jeshi la Polisi lipo imara na linaendelea kulinda usalama wan chi, matukio ya uhalifu makubwa yamesambaratishwa, na matukio yaliyobaki ni madogo
ambayo hayana nguvu katika amani ya nchi.

“Serikali ya Dkt. John Pombe Magufuli ipo imara, uhalifu sasa haupo, ujambazi tumeusambaratisha kabisa, kama kuna uhalifu basi mdogo mdogo tu, huyu kanitukana hivi na vile lakini matukio ya uhalifu makubwa hayapo nchini, nyie mashahidi na mnaona,” alisema Lugola.

Waziri Lugola anaendelea na ziara yake baada ya kumaliza Mkoa wa Ruvuma, anatarajia kwenda Mtwara na Mkoa wa Lindi.


Share:

Hatutavumilia Washauri Elekezi Wazembe Mradi Wa Sumukuvu

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe amewataka washauri elekezi waliosaini mikataba ya kusanifu miundombinu  kwa ajili ya utekelezaji mradi wa kudhibiti Sumukuvu (TANIPAC) kuifanya kazi hiyo kwa weledi na ubora.
 
Ametoa kauli hiyo jana  Jijini Dodoma wakati wa hafla ya kusaini mikataba mitatu na Makampuni yenye thamani ya Shilingi Milioni 868.7 ,randama mbili za mashirikiano  na taasisi za TBS na VETA kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa kudhibiti Sumukuvu nchini.
 
“Mfanye kazi kwa weledi sana, sasa Wizara ya Kilimo tunazingatia weledi.Hatutamvumilia mshauri elekezi mzembe ,tutawasimamia kwa karibu na kuhakikisha thamani ya fedha inaonekana kwenye miradi hii ya kudhibiti sumukuvu” alisema Mhandisi Mtigumwe.
 
Kampuni zilizo saini mikataba ni M/S Digital Space kusanifu karantine ya maabara ya utafiti wa magonjwa ya kibaiolojia,Sundy Merchant Ltd kufanya tahthmini ya awali ya mradi wa Sumukuvu na A.V Consult kufanya usanifu na ujenzi wa maghala 14 ya hifadhi ya mahindi na karanga.
 
Aidha, Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imesaini randama ya mashirikiano ya kufundisha vijana mafundi mchundo 400 kutengeneza teknolojia ya kuhifadhi mazao wakati Shirika la Viwango (TBS) limeingia makubaliano na Wizara ya Kilimo kusaidia kutoa elimu kwa wajasiliamali na Wafanyabiashara kuzalisha na kuhifadhi mazao kwa kuepuka sumukuvu ili wapate soko la uhakika na salama katika mnyororo wa thamani ya mazao nchini.
 
Akizungumza wakati wa utiaji saini Mkurugenzi Mkuu wa VETA nchini Dkt.Pancras Bujulu alisema ni fursa nzuri wamepata kufundisha mafundi mchundo kutengeneza vihenge rahisi kwa ajili ya kuhifadhi mazao ya wakulima ili kulinda afya za watu kwa kutumia teknolojia bora
 
“Ni wajibu wetu VETA kutoa mafunzo kwa vijana nchini ili wazalishe vifaa bora (vihenge) kwa ajili ya kuhifadhi nafaka na kujipatia ajira” Dkt.Bujulu alisema
 
Aliongeza kusema vijana hawa 400 toka wilaya 18 za Tanzania Bara watakuwa chachu ya kusambaza teknolojia hii rahisi na bora ya uhifadhi nafaka nchini.
 
Mratibu wa mradi wa kudhibiti Sumukuvu (Tanzania Iniatives for Preventing Aflatoxin Contamination-TANIPAC) Clepin Josephat alisema mradi huu wa miaka mitano(2019-2023) unatekelezwa nchini kwa lengo la kuhakikisha usalama wa chakula hususan kwenye mazao ya mahindi na karanga hayachafuliwi na fangasi wanaosababisha sumukuvu.
 
Aliongeza kusema sumukuvu tangu ilipogunduliwa nchini imesababisha madhara kwa wananchi ikiwemo kuongezeka kwa uwezekano wa kansa ya ini,udumavu kwa watoto chini ya miaka 5  na vifo.
 
Katika mwaka 2016 jumla ya watu 19 walikufa na wengine 68 waliugua  na kulazwa kutokana na sumukuvu aina ya Aflatoxin kwenye mikoa ya Dodoma na Manyara ambayo imeathirika zaidi.

Mwisho!
Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Kilimo


Share:

Bunge la Marekani Lajaribu Kumzuia Trump Kuishambulia Iran

Baraza la Wawakilishi la Marekani linalodhibitiwa na chama cha Democratic limepitisha azimio lisilo na nguvu kisheria la kuweka ukomo katika uwezo wa rais Donald Trump kuchukua hatua zaidi za kijeshi dhidi ya Iran.

Azimio hilo linamtaka rais Trump kusitisha mipango yote ya kijeshi dhidi ya Iran hadi pale bunge litakapoidhinisha kuingia vitani na nchi hiyo au kuruhusu matumizi ya nguvu za kijeshi kuzuia mashambulizi dhidi ya Marekani. 

Wiki iliyopita rais Trump alitoa idhini ya kumuuwa kamanda wa ngazi ya juu wa jeshi la Iran Qasem Soleimani kisa kilichozusha hasira kutoka kwa Wademocrat na baadhi ya Warepublican waliohoji sababu na uzito wa kufikia uamuzi huo.

Spika wa Baraza la Wawakilishi Nancy Pelosi amesema licha ya kwamba azimio hilo halina nguvu kisheria lakini ni ujumbe wa wazi kwa rais Trump kwa sababu linaakisi msimamo wa wabunge.
 
 Kiongozi wa Republican ndani ya Congress, Kevin McCarthy ameliita azimio hilo kuwa halina maana huku mnadhimu wa chama hicho akilinanga kuwa ni "taarifa kwa vyombo vya habari".

Trump, kupitia ukurasa wake wa Twitter aliwasihi wawikilishi wote wa Republican "wapige kura ya kulikataa azimio hilo la wazimu la Pelosi."


Share:

Picha : OMBA OMBA MAARUFU MJINI SHINYANGA MZEE ALMASI "MWENZANGU" AFARIKI DUNIA...MSIBA WAKE UTATA MTUPU, SERIKALI YATOA MSIMAMO

Mzee John Shija Tuju (72) maarufu Mzee Almasi ama ‘MWENZANGU’ enzi za uhai wake.
Mzee John Shija Tuju (72) maarufu Mzee Almasi ama ‘MWENZANGU’ enzi za uhai wake.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog 

Kumetokea sintofahamu ya mazishi ya Mzee John Shija Tuju (72) maarufu Mzee Almasi ama ‘MWENZANGU’ kutokana na mtindo wa uombaji pesa aliokuwa anautumia Mjini Shinyanga baada ya serikali ya sasa ya mtaa wa Ngokolo kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga kudai haitambui mzee huyo kama mkazi wa e
neo hilo hivyo kukwamisha shughuli za mazishi.

Wakati serikali ya mtaa iliyopo ikisema haimtambui mzee huyo aliyefariki dunia Januari 8,2020 majira ya saa 11 jioni baada ya kuanguka ,mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo aliyepita John Nangi amesema mzee huyo ni mkazi wa eneo hilo na amekuwa akihudhuria misiba japokuwa huwa hachangii pesa.

Taarifa kutoka mtaa wa Ngokolo zinasema Mzee huyo ambaye alikuwa mlemavu wa viungo ‘mguu mmoja’ aliyekuwa anaishi kwa Kuomba Omba Mjini Shinyanga alikuwa anadaiwa Shilingi 18,000/= na mtaa wake kwa ajili ya kununua vifaa mbalimbali vinavyotumiwa wakati wa misiba.

Inaelezwa kuwa kutokana na deni hilo viongozi wa mtaa huo waliamua kujitenga naye kutokana na kukiuka taratibu za mtaa huku wakidai kuwa Mzee huyo hakuwa amejiorodhesha kwenye daftari la mtaa.

Kwa Mujibu wa mpangaji mwenzake na marehemu, James Lumanyika amesema tangu utokee msiba wa Mzee Almasi Januari 8,2020 hakuna mwananzengo yeyote aliyefika msibani na kila wanapofuatilia kwa viongozi wa mtaa hakuna anayetoa sababu zinazoeleweka zaidi ya kuambiwa marehemu hakuwa mwana mtaa na alikuwa anadaiwa shilingi 18,000/=.

Kwa upande wake mtoto wa marehemu Emmanuel Charles licha ya serikali ya mtaa kusema haimtambui marehemu aliomba asaidiwe kufanikisha mazishi ya baba yake na kuelezwa kuwa familia imekubaliana marehemu akazikwe katika kijiji cha Mwalugoye katika kata ya Chibe.

Akizungumza na Malunde1 blog Mwenyekiti wa Mtaa wa Ngokolo Thomas Joseph Ng’ombe amesema hamtambui Mzee huyo kama mkazi wa Ngokolo kwani alikuwa hajajiorodhesha kwenye daftari la mtaa na alikuwa hahudhurii kwenye misiba.

"Tulipata taarifa za msiba wa Mzee huyu jana Januari 9,2020 na tulikuwa tunaendelea kufuatilia ili kuangalia namna ya kusaidia mazishi yake",alisema Ng'ombe.

Naye Mwenyekiti wa Nzengo ya Ngokolo,Silvester Senga amesisitiza kuwa Mzee Almasi/Charles hakuwa kwenye kitabu cha mtaa na kwamba hakuwahi kumuona kwenye mtaa huo na hajawawahi kujitambulisha kwenye nzengo hivyo anachofanya yeye ni kutekeleza utaratibu uliowekwa na mtaa.

Hata hivyo taarifa za serikali ya mtaa kutomtambua mzee huyo zimepingwa vikali na Aliyekuwa Mwenyekiti wa Mtaa wa Ngokolo John Nangi Masoud ambaye amesema anamtambua mzee huyo kwani amekuwa akiishi na familia yake kwenye mtaa huo kwa kipindi kirefu.

“Mzee Almasi ni mkazi wa mtaa huu.Viongozi wa mtaa wanasema kwamba wananchi wamegomea msiba,hii siyo kweli. Mimi nasema Viongozi wa serikali ya mtaa ndiyo wamegomesha msiba huu. Wanajaribu kukwepa tu. Mzee wetu alikuwa mhudhuriaji mzuri wa misiba tatizo lake ni kwamba yeye huwa hana pesa kwa sababu alikuwa anaishi kwa kuomba omba”,alieleza Nangi.

Kutokana na mkanganyiko huo, Afisa Mtendaji wa Kata ya Ngokolo,Felister Msemelwa ameagiza serikali ya mtaa kumpatia stahiki zote za mazishi marehemu.

“Natoa tamko sasa ni kwamba ndugu yetu apatiwe stahiki za mtaa,ahudumiwe kama vile mmekuwa mkiwahudumia wengine katika mtaa huu. Mtendeeni yale yote anayopaswa kutendewa. Marehemu alikuwa mlemavu na taarifa za makazi ya ndugu yetu zimepishana kati ya serikali iliyopo na iliyopita”,alisema Msemelwa.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Ngokolo Mhe. Emmanuel Ntobi alisema kitendo cha kugomea mazishi ya Mzee Almasi ni kukiuka katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuiomba wananzengo wamsiri mzee huyo.

“Naomba Nzengo izingatie utu tumsitiri kwanza Mzee wetu ndiyo tujadili mengine. Mzee huyu alikuwa Omba omba huyu anaingia kwenye kundi maalumu badala ya kumuingiza kwenye kundi la watu wa kawaida. Mwili utaagwa hapa Ngokolo na utazikwa Chibe baada ya kukosa ushirikiano hapa Ngokolo”,alisema Ntobi.

Nao wakazi wa mtaa wa Ngokolo wameeleza kusikitishwa na kitendo cha viongozi wa serikali ya mtaa kugomea msiba huo wakisema kitendo hicho kinakiuka haki za binadamu huku wengine wakiwataka viongozi kuacha kubagua wananchi wasio na uwezo.

"Viongozi mnafanya hivi kwa sababu Mzee Almasi alikuwa maskini,ombaomba?,angekuwa amefariki dunia tajiri hapa mngekuwa tayari mmeshachukua hatua",alisema Chacha.

Mzee Almasi ambaye ni Omba omba maarufu Mjini Shinyanga atakumbukwa kwa mtindo wa uombaji pesa aliokuwa anautumia ikiwemo "Samahani Mwenzangu nisaidie Ka hela",  "Kijana wangu Hujambo! nisaidie Ka hela", "Kijana wangu naomba hata ka mia tano", "Chenji ninayo"

ANGALIA PICHA HAPA
 Afisa Mtendaji wa Kata ya Ngokolo,Felister Msemelwa akiagiza serikali ya mtaa wa Ngokolo kumpatia stahiki zote za mazishi marehemu John Shija Tuju (72) maarufu Mzee Almasi ama ‘MWENZANGU’ leo Januari 10,2020 . Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa Mtaa wa Ngokolo Thomas Joseph Ng’ombe akiwaeleza waandishi wa habari kuwa hamtambui marehemu John Shija Tuju (72) maarufu Mzee Almasi ama ‘MWENZANGU’ kama mkazi wa Ngokolo kwani alikuwa hajajiorodhesha kwenye daftari la mtaa na alikuwa hahudhurii kwenye misiba.
Mwenyekiti wa Nzengo ya Ngokolo,Silvester Senga akisisitiza kuwa John Shija Tuju (72) maarufu Mzee Almasi ama ‘MWENZANGU’ hakuwa kwenye kitabu cha mtaa na kwamba hakuwahi kumuona kwenye mtaa huo na hajawawahi kujitambulisha kwenye nzengo.
Mtoto wa marehemu Emmanuel Charles akielezea kuhusu msiba wa baba yake John Shija Tuju (72) maarufu Mzee Almasi ama ‘MWENZANGU’
 Mpangaji mwenzake na marehemu, James Lumanyika akielezea kuhusu msiba wa John Shija Tuju (72) maarufu Mzee Almasi ama ‘MWENZANGU’
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Mtaa wa Ngokolo John Nangi Masoud alielezea kuhusu msiba wa Mzee Almasi. Alisema anamtambua mzee huyo kwani amekuwa akiishi na familia yake kwenye mtaa huo kwa kipindi kirefu.
Diwani wa Kata ya Ngokolo Mhe. Emmanuel Ntobi akielezea kuhusu msiba wa Mzee Almasi ' Mwenzangu' ambapo alisema kitendo cha kugomea mazishi ya Mzee Almasi ni kukiuka katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuiomba wananzengo wamsiri mzee huyo.
Mkazi wa Mtaa wa Ngokolo Chacha akiwataka viongozi wa serikali ya mtaa kuacha kubagua wananchi maskini na tajiri.
Sehemu ya wakazi wa Mtaa wa Ngokolo waliofika nyumbani kwa mzee Almasi ' Mwenzangu' leo asubuhi.
Sehemu ya wakazi wa Mtaa wa Ngokolo waliofika nyumbani kwa mzee Almasi ' Mwenzangu' leo asubuhi.
Picha na Kadama Malunde - Malunde - Blog
Share:

Waziri Mkuu Afuta Mnada Wa Nafaka Ulioendeshwa na TRA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefuta mnada wa nafaka ulioendeshwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)  Januari 7, 2020 na kuuagiza uongozi wa mamlaka hiyo kutangaza upya zabuni baada ya kutoridhishwa na taratibu zilifanyika awali.

Mnada huo ambao unahusisha mahindi tani 5,000 na ngano tani 460.12 unafanyika baada ya wahusika kushindwa kutimiza masharti ya kiforodha, hivyo Serikali imeamua kuuza ili kufidia gharama zake. Nafaka hizo ziliingia nchini Machi 2017.

Waziri Mkuu amesitisha mnada huo jana (Alhamisi, Januari  9, 2020) wakati akizungumza na Kamishna wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa wa TRA, Bw. Ben Asubisye, ofisi ndogo ya Waziri Mkuu Magogoni Jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu ameagiza kutangazwa upya kwa mnada mwingine wa kuuza mahindi hayo sambamba na ngano na wahakikishe masuala yote kuhusu mnada huo yanakamilika ndani ya siku tatu kuanzia  tarehe 09 Januari 2020.

“Mahindi yameuzwa kwa bei ya sh. 340 kwa kilo moja ambayo ni chini na bei ya soko kwa sababu bei ya mahindi sokoni kwa sasa ni sh. 800. Zabuni imetangazwa kwa muda mfupi watu wameshindwa kushiriki. Ilifunguliwa saa 8 mchana na imefungwa saa 5 usiku.”

Kadhalika, Waziri Mkuu ameutaka uongozi wa TRA uhakikishe mnada unaofuata unakuwa wa wazi, huru pamoja na kutoa muda wa kutosha kwa wananchi wote kushiriki ili kuondoa malalamiko.

“Kwa kuwa mnada unafanyika kwa njia ya mtandao, hakikisheni matumizi ya mtandao yanakuwa rafiki kwa wananchi wote watakaovutiwa kuwasilisha zabuni zao.”

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesisitiza kuwa TRA ishirikiane na mamlaka nyingine za Serikali kuhakikisha wanunuzi wa nafaka hizo hawaziingizi sokoni kwa ajili ya matumizi ya binadamu. Nafaka hizo zimepimwa na kuthibitika kuwa zinafaa kwa matumizi ya wanyama.

(mwisho)
IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU


Share:

Mangula:Ni marufuku kwa mwanachama anayetarajia kugombea,kutoa misaada wakati uchaguzi unapokaribia

Na Amiri kilagalila-Njombe
Makamu mwenyekiti wa CCM Tanzania bara Mh.Philip Mangula amewakumbusha wanachama wa chama hicho nchini,marufuku iliyopo kwenye katiba kwa mwanachama yeyote anayetarajia kugombea au wakala wake kutoa misaada mbali mbali wakati uchaguzi unapokaribia.

Philip Mangula ametoa marufuku hiyo mkoani Njombe wakati wa kikao cha halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Njombe kilichofanyika katika ukumbi uliopo katika ofisi za chama cha mapinduzi mkoa wa Njombe zilizopo mjini Njombe.

Amesema kwa mujibu wa vifungu na kanuni zilizopo kwenye katiba ya chama zinaeleza wazi utaratibu na marufuku ya utoaji wa zawadi kwa wanaotarajia kugombea au mawakala kutoa misaada mbali mbali wakati uchaguzi unapokaribia kwa kuwa misaada hiyo huwa na lengo la kuvutia kura.

“Kanuni kifungu cha 6 kinasema ni marufuku kwa mwanachama yeyote anayetarajia kugombea au wakala wake kutoa misaada mbali mbali wakati uchaguzi unapokaribia,ambao ni dhahiri lengo lake ni kuvutia kura,isipokuwa kanuni hii haijamhusu Rais,mbunge mwakilishi au diwani ambaye yuko madarakani wakati huo kwa kuwa yeye atakuwa bado anao wajibu wa kuhudumia eneo lake la uongozi”alisema Mangula katiba inaeleza

Awali kabla ya kumkaribisha mwenyekiti wa CCM Tanzania bara,mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Njombe Jasel Mwamwala,amewashukuru viongozi wa chama na serikali kwa kusimamia utekelezaji mzuri wa ilani ya chama cha mapinduzi na kuwaletea maendeleo wananchi,pamoja na kuiomba serikali kabla ya kufika uchaguzi wa Rais kukamilisha ujenzi mkubwa wa barabara za lami zilizoanza kujengwa mkoani humo.

“Tunaomba hizi barabara zikamilike ili tunapofika mwezi wa kumchagua Rais bara bara hizi zote ziwe zimekamilka na zinapitika kwasababu ndio ahadi na wananchi wanapohoji hivi kweli hizi barabara zitakamilika?sisi tunasema zitakamilika”alisema Jasel Mwamwala

Naye katibu wa chama hicho mkoa wa Njombe Ndugu Paza Mwamlima amesema kwa sasa mkoa wa Njombe unaendelea vizuri hususani kuelekea hatua za mwanzo za uchaguzi mkuu kwa kuwa katika zoezi la maboresho na kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura,chama hicho kimeweza kuhamasisha wanachama wake na kupelekea taarifa za awali kuonyesha wilaya ya Njombe kuandikisha wapiga kura 85,508 wilaya ya Wanging’ombe wanachama 24,450 wilaya ya Ludewa 14,936 na wilaya ya Makete 14,623.

Baadhi ya wajumbe wa kikao hicho akiwemo katibu wa siasa na uenezi mkoa wa Njombe Erasto Ngole ametoa wito kwa wanachama wasipite kwenye kata na majimbo ya watu kuonyesha nia ya kugombea kabla chama hakijatoa maelekezo huku.Huku Anaupendo Gombela diwani wa kata ya Mdandu wilayani Wanging’ombe,ametoa wito kwa wanachama kuwaacha madiwani na wabunge wao huru kwa sasa ili watekeleze wajibu wao kabla ya mabalaza au bunge kuvunjwa.


Share:

Profesa Mbarawa Nitazivunja Bodi Za Maji Zitakazoshindwa Kukusanya Mapato Ya Maji

SALVATORY NTANDU,SHINYANGA
Waziri wa Maji, Profesa Makama Mbarawa asema ataifuta bodi mpya ya Maji ya Malmlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Shinyanga (SHUWASA)  endapo itashindwa kukusanya mapato kutoa shilingi milioni 691 za sasa hadi kufikia milioni 700.

Uamuzi huo ameutoa jana mjini Shinyanga katika hafla ya kuipitisha bodi hiyo mpya ambayo imeanza kazi rasmi ya usimamizi na uendeshaji wa shughuli za Maji katika Manispaa ya shinyanga kwa kipindi cha miaka 3.

“Kama hamtafikia makusanyo ya mapato ya shilingi milioni 700 ni lazima niivunje bodi hii, muda wa kubembelezana umekwisha bondi nyingi zimekuwa zikifanya kazi kwa mazoea kwa kupeana posho na safari amabazo hazina tija na kushindwa kuzisimamia mamlaka za maji”alisema Profesa Mbarawa.

Kwa mwaka mamlaka hii inakusanya shilingi zaidi ya shilingi bilioni 5.9  lakini makusanyo ya mamlaka hii yako chini ikilinganishwa na Idadi ya watumiaji wa maji ambao ni wengi jambo ambalo linaonesha kuwa katika Mamlaka hii kuna  uzembe katika usanyaji wa mapato na kuisababishia serikali kukosa mapato.

“Mwezi oktoba mwaka jana mmekusanya shilingi milioni 667, septemba 679,  Agosti 691 fedha hizi hazitoshi ikilinganishwa na maji mnayozalisha  ambayo ni lita milioni  438 lakini maji  lita milioni 365 ambapo maji ambayo yanaonekanakupotea njiani ni lita milioni 75  kwa upotevu  lazima bodi hii mpya ianze kuifanyia kazi suala hili” alisema Profesa Mbarawa.

Waziri mbarawa aliongeza kuwa ni lazima mamlaka zote nchini kuhakikisha zinaongeza makusanyo kwa kuanzisha miradi ya mipya ya maji ikiwa ni pamoja na kuongeza matandao wa maji ili kuhakikisha watanzania wote wanapata huduma za maji karibu na maeneo yao.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA Flaviana Kifizi alisema kuwa watahakikisha wanadhibiti upotevu wa maji kwa kushirikiana na Bodi mpya chini ya Mwenyekiti Mwamvua Jirumbi kwa kutekeleza maagizo yote ambayo yametolewa na serikali ili kuboresha utendaji kazi utakaosaidia kuongezeka kwa mapato.

Amefafanua kuwa SHUWASA inatekeleza miradi ya maji katika wilaya za Kahama kwenda ngogwa hadi kitwana,na Katika wilaya ya Shinyanga ni kutoka Negezi hadi Mwawaza kwa kuwatumia wataalamu wa ndani kupitia Force account ambapo miradi hii imefikia katika  hatua mbalimbali na mafundi wapo katika maeneo ya Miradi.

Nae mwenyekiti aliyemaliza muda wake Deogratius Sulla alisema taasisi za umma zinasuasua kulipa madeni ya Ankara za maji za kila mwezi na kusababisha deni kuendelea kuongezeka hadi kufikia shilingi mlioni 949.

“Mpaka mwezi Disemba mwaka jana JWTZ ilikuwa inadaiwa shilingi milioni 520,244,957,Magereza shilingi milioni 256,520,120,Polisi shilingi 172,346,465”alisema Sulla.

Bodi ambayo imemaliza muda wake ilizinduliwa rasmi Novemba 14 mwaka 2016.

Mwisho.


Share:

Mwekezaji Kutoka India Aonesha Nia Kuwekeza Kilimo Cha Mpunga, Kiwanda Cha Kuchakata Mpunga Simiyu

Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Mwekezaji kutoka nchini India, Bw.Vivek Agarwala ameonesha nia ya kuwekeza kwenye kilimo cha mpunga kupitia umwagiliaji na kujenga kiwanda cha kuchakata mpunga wilayani Busega mkoani Simiyu, ambapo anatarajia kuwekeza katika eneo lenye ukubwa wa ekari zipatazo 2000.

Akizungumza na viongozi na watendaji wa Mkoa wa Simiyu baada ya kutembelea maeneo mbalimbali yenye fursa ya uwekezaji katika kilimo cha mpunga wilayani Busega, Bw. Agarwala amesema mkoa wa Simiyu na Tanzania kwa ujumla ina rasilimali nyingi hivyo ikiwa Makampuni kutoka India yatafanya kazi kwa kushirikiana na Watanzania rasilimali hizo ziatakuwa na manufaa kwa Watanzania.

“Mkoa wa Simiyu na Tanzania kwa ujumla ina rasilimali za kutosha ambazo zipo kwa ajili ya kuwanufaisha Watanzania wenyewe hivyo  kinachohitajika ni teknolojia, uwekezaji, ushirikiano kutoka Serikalini kufanya haya yote yatokee; baada ya ziara hii ninaamini tukiyatekeleza kwa juhudi yale tuliyokubaliana mkoa huu utaendelea kwa kasi,” alisema Agarwala.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amemhakikishia mwekezaji huyo upatikanaji wa eneo la ekari 2000 kwa ajili ya uwekezaji na kubainisha kuwa malengo ya mkoa ni kuhakikisha wilaya ya Busega inakuwa mzalishaji mkuu wa chakula katika mkoa kwa kuwa ndiyo wilaya yenye ziwa Victoria ndani ya Mkoa.

Aidha, pamoja na kutoa ushirikiano kwa mwekezaji kutimiza azma yake Mtaka amesema Serikali ya Mkoa imezungumza na Benki ya CRDB kuona uwezekano wa kuwawezesha wakulima wa mpunga wilayani Busega hususani walio kando ya ziwa Victoria kupitia dirisha la kilimo ili waweze kulima kisasa kupitia umwagiliaji.

Naye Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Ziwa, Bw. Lusingi Sitta amesema Benki iko tayari kumuunga mkono mwekezaji na wakulima wa wilaya ya Busega  kupitia dirisha la kilimo kutokana na wilaya hiyo kuwa na maeneo mazuri na chanzo cha uhakika cha maji (Ziwa Victoria), ambapo alibainisha kuwa tayari benki hiyo ina uzoefu wa kuwezesha miradi mbalimbali ya kilimo cha umwagiliaji.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo amesema wao kama chama wanaunga mkono juhudi za watu wanaoitika huku akiongeza kuwa mkoa huo ni miongoni mwa mikoa inayofanya vizuri kwenye kilimo hususani cha mpunga hivyo ujio wa mwekezaji huyo mkoani hapa utasaidia kuongeza tija kwenye zao hilo.

Katika hatua nyingine  baadhi ya wakulima wamesema kuwa ujio wa mwekezaji  huyo utawasaidia wao kuzalisha kwa tija ikilinganishwa na awali," tukianza kulima kilimo cha umwagiliaji tunaamini tutavuna mavuno mengi maana tutalima zaidi ya mara moja kwa msimu" alisema Monika Msabila

"Kuna kipindi mavuno yanashuka kama mvua zikiwa chache sasa ujio wa mwekezaji huyu tumeupokea maana atatusaidia na sisi kulima kilimo cha umwagiliaji na kuacha kutegemea mvua pekee " alisema Simon Ngelela mkazi wa Kijiji cha Shigala wilayani Busega.

Katika hatua nyingine mwekezajI alipata fursa ya kutembelea kiwanda kinachomilikiwa na Mwekezaji mzawa, Deogratius Kumalija ambacho kinaongeza thamani kwenye mazao ya chakula hususani mpunga na mahindi Busega Mazao Limited  kilichopo wilayani Busega.

MWISHO



Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger