Thursday, 28 November 2019

Picha : AGAPE YAENDESHA KIKAO KUJADILI KUTENGENEZA MUONGOZO WA KUPAMBANA NA UKATILI SOKONI SHINYANGA



Shirika lisilo la kiserikali Agape Aids Control Programme limeendesha kikao cha kujadili namna ya kutengeneza muongozo ambao utatumika kwenye masoko ya Shinyanga Mjini, kwa ajili ya kuzuia na kupambana na ukatili wa kijinsia kwenye Masoko.

Kikao hicho kimefanyika leo Novemba 28, 2019, kwenye ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Liga, ambacho kimeshirikisha viongozi wa masoko sita ya Shinyanga mjini, maofisa ustawi, maendeleo ya jamii, wanasheria, dawati la jinsia, pamoja na wajumbe wa kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto Mtakuwwa.

Akizungumza wakati wa kufungua kikao hicho, Mwansheria kutoka Shirika la Agape Felix Ngaiza, akimwakilisha mkurugenzi wa Shirika hilo John Myola, amesema, utengenezaji wa muongozo huo wa kuzuia na kupambana na ukatili kwenye masoko, utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza matukio ya ukatili wa kijinsia masokoni.

Amesema Shirika hilo limekuwa likitekeleza mradi wa kupambana na matukio ya ukatili wa kijinisa sokoni, uitwao Mpe Riziki Si Matusi, ambapo sasa wameamua watengeneze muongozo ambao utatumika kuzuia na kupambana na matukio hayo ya ukatili wa kijinsia sokoni, ili pawe mahali salama pa kufanyia biashara.

“Muongozo huu ni muhimu sana ambao utasaidia kuzuia na kupambana na matukio ya ukatili wa kijinsia masokoni, na ndio maana leo tumeamua kufanya kikao na viongozi wa masoko, maofisa ustawi jamii, maendeleo, dawati la jinsia, wanasheria, na wajumbe wa Mtakuwwa, ili tupate kuutengeneza na kuanza kutumika,”amesema Ngaiza.

Aidha amesema muongozo huo wa kuzuia na kupambana na ukatili wa kijinsia kwenye Masoko, utakuwa ukitoa faini na adhabu mbalimbali kwa watu ambao watakuwa wakifanya matukio hayo ya ukatili kwenye masoko.

Naye Afisa mradi wa kutokomeza ukatili sokoni wa ‘Mpe Riziki Si Matusi’ Helena Daudi, amesema mradi huo umeanza kutekelezwa tangu mwaka Novemba 2018 ambao unakoma mwaka huu 2019, ambapo mpaka sasa wamefanikiwa kupunguza ukatili huo kwa kiwango kikubwa.

Amesema mradi huo unafadhiliwa na Shirika la UN WOMEN kupitia shirika la Equality for Growth (EFG), ambao umedhamiria kutokomeza ukatili kwenye masoko sita ya manispaa ya Shinyanga dhidi ya wanawake na wasichana, ambayo ni Kambarage, Soko kuu, Nguzonane, Ngokolo, Majengo mapya, na Ibinzamata.

Nao baadhi ya wenyeviti wa masoko akiwemo Alex Stephen kutoka soko kuu la Shinyanga, wamebainisha matukio ya ukatili ambayo yamekuwa yakitendeka ikiwamo kutolewa kwa lugha chafu za matusi ya nguoni, kushikwa maumbile kwa wanawake bila ya ridhaa yao, kutakwa kimapenzi kwa nguvu, kudhulumiwa pamoja na vipigo.


TAZAMA PICHA HAPA CHINI

Mwanasheria wa Shirila la Agape Felix Ngaiza akizungumza wakati wa kufungua kikao cha kujadili namna ya kutengeneza muongozo wa kuzuia na kupambana na ukatili wa kijinsia sokoni. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde 1 blog

Afisa mradi wa kutokomeza ukatili sokoni wa ‘Mpe Riziki Si Matusi’ kutoka Shirika la Agape Helena Daudi, akielezea umuhimu wa masoko kuwa na muongozo huo wa kuzuia na kupambana na ukatili wa kijinsia sokoni, ambapo utasaidia kutokomeza ukatili huo.

Afisa mradi wa kutokomeza ukatili sokoni wa ‘Mpe Riziki Si Matusi’ kutoka Shirika la Agape Helena Daudi, akielezea umuhimu wa masoko kuwa na muongozo huo wa kuzuia na kupambana na ukatili wa kijinsia sokoni, ambapo utasaidia kutokomeza ukatili huo.

Mwanasheria kutoka Shirika la Agape Emmanuel Nyalada akiwasilisha mada kuhusu muongozo wa kuzuia na kupambana na ukatili kijinsia sokoni.

Meneja miradi kutoka Shirika la Agape Peter Amani, akizungumza kwenye kikao hicho.

Mwanasheria wa manispaa ya Shinyanga Mushi Josephat akieleza kuwa muongozo huo wa kuzuia na kupambana na ukatili wa kijinsia sokoni utasaidia kumalizana kesi wao kwa wao zinazohusu ukatili, kuliko kupelekana kwenye vyombo vya Sheria ambapo matukio yote ya ukatili ni Makosa ya Jinai.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha kujadili utengenezaji wa muongozo ambao utasaidia kuzuia na kupambana na matukio ya ukatili wa kijinsia sokoni.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha kujadili utengenezaji wa muongozo ambao utasaidia kuzuia na kupambana na matukio ya ukatili wa kijinsia masokoni.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha kujadiri utengenezaji wa muongozo ambao utasaidia kuzuia na kupambana na matukio ya ukatili wa kijinsia masokoni.

Wajumbe wakiendelea na kikao.

Wajumbe wakiendelea na kikao.

Wajumbe wakiendelea na kikao.

Mwenyekiti wa Soko kuu la Shinyanga Alex Stephen akichangia mada kwenye kikao hicho.

Mhasibu wa Soko la Ibinzamata Juliana Francis akichangia mada kwenye kikao hicho.

Msaidizi wa kisheria kutoka Soko kuu la Shinyanga Zera Semuguruka, akichangia mada kwenye kikao hicho.

Mwakilishi wa Soko la Nguzo Nane Hilda Athanas, akichangia mada kwenye kikao.

Mchungaji wa kanisa la KKKT Makedonia Harold Mkaro, ambaye pia ni mjumbe wa MTAKUWWA, akichangia mada kwenye kikao.

Wajumbe wakiwa kwenye kazi ya makundi.

Wajumbe wakiwa kwenye kazi ya makundi.

Wajumbe wakiwa kwenye kazi ya makundi.

Mwenyekiti wa Soko la Kambarage Seif Mtete akiwasilisha kazi ya kikundi.

Wajumbe wakiendelea kuwasilisha kazi ya kikundi.

Wajumbe wakiwasilisha kazi ya kikundi.

Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

Share:

Video Mpya : PUMARIO - MY LOVER LOVER

Video mpya ya Msanii Pumario inaitwa My Lover Lover

Share:

MSHINDI WA PROMOSHENI YA TIGO CHEMSHA BONGO APATIKANA


Mtaalam wa Huduma za ziada-Tigo, Fabian Felician na Jehud Ngolo- Afisa Mwandamizi Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania. wakimpigia simu Shaban Khamis Ali,mkaazi wa Zanzibar, mshindi wa promosheni ya Tigo Chemsha bongo
Mtaalam wa Huduma za ziada-Tigo, Fabian Felician na Jehud Ngolo- Afisa Mwandamizi Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania. wakimpigia simu Shaban Khamis Ali,mkazi wa Zanzibar, mshindi wa promosheni ya Tigo Chemsha bongo

****
Droo ya mwisho ya promosheni ya ‘Tigo Chemsha Bongo’ imefanyika jijini Dar es Salaam ambapo mkaazi wa Zanzibar, Shabani Khamis Ali (48) amejishindia gari mpya aina ya Renault KWID yenye thamani ya 23m/-. Khamis akiongea baada ya kupigiwa simu na Mtaalam wa Huduma za Ziada kutoka Tigo, Fabian Felician, kumfahamisha kuwa ameibuka mshindi, alisema anayo furaha kufanikiwa kuwa miongoni mwa washindi kupitia promosheni hiyo kwa kujishindia gari mpya. 

“Sikutegemea kabisa kuwa ningeibuka mshindi katika promosheni hii, Habari hizi naziona kama ndoto kwangu, nashukuru Tigo kwa kunifungia mwaka vizuri na kutimiza ndoto yangu ya kumiliki gari, kwani itanisaidia katika mizunguko yangu ya kibiashara “alisema kwa furaha. 

Mtaalam wa Huduma za Ziada kutoka Tigo, Fabian Felician, alimpongeza mshindi huyo na kutumia fursa hiyo kuwashukuru wateja wote wa kampuni ambao walishiriki na baadhi yao kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo zawadi za fedha taslimu ambayo yalitolewa na kampuni hiyo. 

“Tunayo furaha kubwa katika kipindi hiki tunachoelekea katika msimu wa sikukuu kumpata mshindi wetu wa gari ya aina Renault Kwid,yenye thamani ya 23m/-, gari hili ni jipya kabisa, baada ya kumpata mshindi taratibu zengine zitafata ili tuweze kumkabidhi Shaban Khamis Ali gari lake jipya. Tunawashukuru wateja wetu kutoka nchini pote walioshiriki kwenye promosheni hii ya miezi mitatu ambayo imemalizika mwishoni mwa mwezi wa Novemba 2019”. alisema Felician. 

Aliongeza kuwa, promosheni hii ambayo ilianza jijini Mwanza katika msimu wa Tigo Fiesta 2019-Saizi Yako  imepata mafanikio makubwa kutokana na wateja wengi kujitokeza kushiriki na baadhi yao kufanikiwa kujishindia zawadi(fedha taslim) mbalimbali na hivyo Tigo kufanikisha lengo lake ambalo lilikuwa ni kuwashukuru wateja kwa kuiunga mkono kampuni kupitia kununua bidhaa zake mbalimbali. 

Kwa kumalizia Felician aliwashukuru wateja wote wa Tigo kwa kuendelea kuunga mkono kampuni na kuahidi kuwa promosheni mbalimbali za kunufaisha wateja wa kampuni hiyo zinatendelea kubuniwa katika siku za usoni.


Share:

Jumuiya ya Afrika Mashariki yasaini mkataba wa EURO milioni 10 na umoja wa nchi za Ulaya Ili Kusaidia Kuimarisha Usalama

Jumuiya ya Afrika  Mashariki imesaini mkataba wa EURO milioni 10  na umoja wa nchi za Ulaya  kwa ajili ya kuimarisha ulinzi na usalama katika nchi uanachama wa jumuiya hiyo.
 
Mkataba huo umesainiwa  jana katika ofisi za makao makuu ya jumuiya hiyo  na Katibu mkuu wa jumuiya ya Afrika Mashariki ,Liberat Mfumukeko  na Balozi  wa umoja wa nchi za Ulaya Tanzania ,Manfredo Fanti.
 
Akizungumza wakati wa kusaini mkataba huo ,Katibu mkuu wa EAC ,amesema kuwa, fedha hizo zimetolewa na jumuiya ya umoja  huo ili kuziwezesha nchi wanachama kukabiliana na changamoto ya usalama ambayo imekuwa na kikwazo kikubwa Cha maendeleo katika nchi hizo.

Ameshukuru jumuiya hiyo kwa msaada huo ambao umekuja muda muafaka na kuongeza kuwa, jumuiya hiyo itaendelea kushirikiana kwa ukaribu Sana katika nyanja mbalimbali za maendeleo.
 
Hata hivyo ,Mfumukeko amesema kuwa,jumuiya hiyo ya nchi za Ulaya wamekuwa washirikiana kwa muda mrefu na jumuiya hiyo ambapo katika kipindi cha miaka mitano wamekwisha kutoa kiasi Cha EURO milioni  85 .

“Umoja wa Ulaya wamekuwa washirika muhimu katika kusukuma mbele ajenda ya mtangamano wenye lengo la kuwawezesha kiuchumi, ipo miradi mbalimbali ambayo imefadhiliwa na EU tangu mwaka 2007 ambayo imekua na matokeo chanya kwa wananchi wetu.

“Programu hii ambayo tumeizindua itasaidia kupunguza nafasi ya kushamiri kwa uhalifu unaovuka mipaka ya nchi moja kwenda nyingine ambayo unaweza kutishia mchakato wa mtangamano, pia itasaidia kuendeleza sera na utekelezaji wake, uwajibikaji kisiasa na uimarishaji wa taasisi,” amesema Mfumukeko. 

 
Kwa upande wake ,Balozi wa jumuiya ya umoja wa Ulaya nchini Tanzania,Manfredo Fanti amesema kuwa, wataendelea kusaidia jumuiya hiyo katika maswala mbalimbali ya maendeleo .
 
“Tumekuwa tukisaidia jumuiya ya Afrika Mashariki katika miradi mbalimbali tangu mwaka 2007 ambayo imeleta manufaa makubwa kwa wananchi wa nchi hizo na kuondokana na changamoto mbalimbali zinazowakabili.”amesema Balozi huyo.


Share:

CHAMA CHA WAAJIRI ATE: KUJISAJILI WCF NI LAZIMA SIO HIARI

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MKURUGENZI Mtendaji wa Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE), Dkt. Aggrey Mlimuka amewaambia waajiri nchini kuwa kujisajili na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi sio hiari bali ni lazima.
Dkt. Mlimuka ameyasema hayo Alhamisi Novemba 28, 2019 jijini Dar es Salaam wakati akifungua mafunzo ya siku moja yaliyoandaliwa na ATE na kuwaleta pamoja waajiri kutoka sehemu mbalimbali nchini ili kujifunza kuhusu masuala ya Fidia kwa Wafanyakazi.
“Naomba tuelewane toka mapema, siyo hiari kujiunga na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi hilo ni takwa la kisheria Mfuko huu uko pale kisheria na ni vema likaeleweka mapema.”Alisema Dkt. Mlimuka
Alisema Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) kiko kwa maslahi ya waajiri lakini pia kwa maslahi ya waajiriwa (wafanyakazi) kwani wameajiriwa ili kufanya shughuli mbalimbali na wanaweza kuumia au kupatwa na madhara yoyote wakati wakitekeleza majukumu yao na ndio maana upo Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi ambao umeundwa maalum kushughulikia masuala hayo.
“Niwashukuru sana viongozi wa WCF  kwa kuja hapa leo kutupatia mafunzo,  sisi waajiri tutanufaika vya kutosha na mafunzo haya ambayo yataweza kujibu maswali yaliyo mengi kutokana na changamoto mbalimbali.” Alibainisha Dkt. Mlimuka.
Alisema,hapo zamani malipo ya Fidia kwa Mfanyakazi aliyeumia yalikuwa kidogo sana, na ndio maana Serikali ikaanzisha Mfuko huu ambao umesaidia sana katika kutatua changamoto zilizokuwa zikitukabili kutokana na masuala ya Fidia.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF),  Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Dkt. Abdulsalaam Omary alisema, Waajiri wanao wajibu wa kuhakikisha usalama wa wafanyakazi wao unapewa umuhimu wa kwanza na ndio maana WCF inatoa elimu mara kwa mara.
“Ifahamike kuwa sisi WCF wajibu wetu wa msingi ni kulipa fidia stahiki na kwa wakati kwa mfanyakzi aliyeumia, kuugua au kufariki wakati akitekeleza wajibu wake wa kazi… kusajili na kupokea michango kutoka kwa waajiri walio katika sekta ya umma na binafsi Tanzania Bara, lakini pia tunalo jukumu la kisheria la kukuza mbinu za kuzuia ajali na vifo kazini kwa kutoa elimu kwa waajiri lakini pia wafanyakazi wenyewe na hiki ndicho tunachokifanya hapa leo.” Alisema Dkt. Omary wakati akiwasilisha mada yake ya namna ya kudai Fidia.
Washiriki hao walipatiwa mafunzo mbalimbali yakiwemo Sheria iliyoanzisha Mfuko, Kujisajili na jinsi ya kuwasilisha michango WCF na namna ya kuwasilisha madai ya Fidia, lakini pia Mafao yanayotolewa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE), Dkt. Aggrey Mlimuka, akitoa hotuba ya ufunguzi wa mafunzo kuusu masuala ya Fidia kwa Wafanyakazi yaliyotolewa kwa Waajiri kutoka sehemu mbalimbali nchini na kufanyika jijini Dar es Salaam Novemba 28, 2019.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE), Dkt. Aggrey Mlimuka (kushoto), akisalimiana na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omary, mara baada ya kutoa hotuba.
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omary, akizungumza mwanzoni mwa mafunzo ya siku moja kuhusu masuala ya Fidia kwa Wafanyakazi kwa wanachama wa Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) jijini Dar es Salaam Novemba 28, 2019.
 
 Bw, Deo Ngowi kutoka kitengo cha Sheria Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), akiwasilisha mada kuhusu Sheria iliyoanzisha Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi.
 Bw.Pascal Rischard kutoka Kitengo cha Usajili na Uwasilishaji Michango WCF, akiwasilisha mada kuhusu namna ya kujisajili na kuwasilisha michango kupitia Portal ya WCF
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omary,
Meneja Madai Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bi. Rehema Kabongo, akiwasilisha mada kuhusu Mafao yatolewayo na WCF.

 Baadhi ya washiriki w asemina wakifuatilia mafunzo hayo.
 Baadhi ya washiriki w asemina wakifuatilia mafunzo hayo.
 Baadhi ya washiriki w asemina wakifuatilia mafunzo hayo.
 Maafisa wa juu wa WCF, kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, Bi. Laura Kunenge, Bw. Deo Ngowi kutoka Kitengo cha Sheria na Bw. Pascal Richard kutoka Kitengo cha Usajili na Uwasilishaji Michango WCF
Baadhi ya washiriki w asemina wakifuatilia mafunzo hayo.
Share:

Marekani Yawaunga mkono waandamanji Hong Kong, China Yatishia Kulipiza Kisasi

Rais wa Marekani Donald Trump amesaini muswada wa kuunga mkono vuguvugu la maandamano ya kudai demokrasia mjini Hong Kong na kuwa sheria licha ya pingamizi kutoka kwa serikali ya China. 

Sheria hiyo ambayo iliungwa mkono kwa sauti moja bungeni, inahitaji Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani kuthibitisha angalau kila mwaka kwamba uhuru wa Hong Kong haukutatizwa. 

Bunge la Marekani pia limepitisha muswada wa pili - ambao Rais Trump pia ameusaini - unaopiga marufuku usafirishaji na uuzaji wa silaha za kudhibiti maandamano ya umma kwa vikosi vya usalama vya Hong Kong kama vile, mabomu ya kutoa machozi, dawa ya pilipili, risasi za mpira pamoja na bunduki za kutoa mshtuko wa umeme. 

China ilimuonya Trump wiki iliyopita kuwa itachukua hatua za kulipiza kisasi iwapo atasaini miswada hiyo na kuwa sheria.


Share:

Nafasi 62 za Kazi TANESCO | Wanahitajika watu wa Customer Care

Nafasi 62 za Kazi TANESCO | Wanahitajika watu wa Customer  Care 
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬

👉Mwisho wa Kutuma maombi ni; 11/12/2019
👉Elimu ni  Diploma ya Marketing, Public Relations au  Business Administration 
👉Mwenye Elimu Kidogo ya Computer atapewa Kipaumbele
👉Uzoezi ni Mwaka mmoja
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬

==>>Kujua namna ya kutuma maombi <<INGIA HAPA>>


Share:

Tanzania Mwenyeji wa Mkutano wa JPC na Namibia




Share:

MBUNGE BALOZI ADADI AISHUKURU SERIKALI KUWASAIDIA KUWEKA LAMI KWENYE MJI WA MUHEZA

 MBUNGE wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu akizungumza wakati wa halfa ya utiliaji saini  ya kati ya Halmashauri ya Muheza na Mkandarasi wa Kampuni ya ujenzi ya SIMAC Limited kutoka Dar kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara za mita 800 kwenye mji huo kwa kiwango cha lami kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muheza Nassib Mbaga na kushoto ni Meneja wa Tarura wilaya hiyo Mhandisi Joseph Kahoza
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muheza Nassib Mbaga akizungumza wakati wa halfa hiyo kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu kulia ni Katibu  wa CCM wilaya ya Muheza Mohamed Moyo 
 Meneja wa Tarura wilaya hiyo Mhandisi Joseph Kahoza akizungumza wakati wa halfa hiyo kulia ni Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajab
 MBUNGE wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu akimkabidhi nyaraka na michoro mkandarasi wa kampuni ya ujenzi SIMAC LTD kutoka Dar Felix Chawe mara baada ya kusaini nae mkataba kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara za mita 800 katika mji wa Muheza
 
 MBUNGE wa Jimbo la Muheza kushoto Balozi Adadi Rajabu (aliyevaa suti) akisisitiza jambo kwa mkandarasi wa ujenzi huo mara baada ya kutembelea eneo ambalo ujenzi huo utafanyika 
 MBUNGE wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu kushoto akimsikiliza Katibu wa CCM wilaya ya Muheza Mohamed Moyo kulia wakati walipotembelea barabara ya sokoni wilayani humo 


MBUNGE wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu ameishukuru serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli kuwasaidia kuweka lami baadhi ya barabara zilizopo kwenye mji huo.

Huku akiwataka wananchi wilayani humo kumpa ushirikiano mkandarasi ambaye anatekeleza ujenzi huo ili aweze kutekeleza kazi yake kwa wakati kutokana na kwamba amepewa muda wa miezi saba. 


Balozi Adadi aliyasema hayo wakati wa halfa ya utiaji wa saini kati ya kati ya Halmashauri ya Muheza na Mkandarasi wa Kampuni ya ujenzi ya SIMAC Limited kutoka Dar kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara za mita 800 kwenye mji huo. 


Alisema kwamba utiliaji saini huo umeonyesha namna serikali ya awamu ya tano imedhamiria kuhakikisha inaboresha miundombinu kwenye miji mbalimbali hapa nchini.

Mbunge huyo alisema kwamba barabara ni kilomita ya pili ambayo itaanzia Kilimanjaro Bar, Darajani, relini mpaka hospitali ya Teule Muheza na baadae kufika mpaka kwenye kipande ambacho kinatumika na wananchi kwenye maeneo ya karibu na soko la Muheza.

“Serikali ya awamu ya tano imeweza kutusaidia kuweka lami ni jambo kubwa na la faraja kubwa kwetu hivyo kwa sababu lami itawekwa kwenye mji wetu hakikisheni mnapa ushirikiano na niwaombe msimpe vikwazo vya namna yoyote ile “Alisema Balozi Adadi. 


Awali akizungumza wakati wa halfa hiyo Meneja wa Tarura wilaya ya Muheza Mhandisi Joseph Kahoza alisema kwamba mkandarsi aliyekabidhi mkataba huo ni wa barabara za mita 800 kwa ajili ya kuweka lami kwa mji wa muheza.

Alisema mkandarasi huyo ataanza kufanya kazi hiyo kuanzia barabara ya Kilimanjaro darajani, relini mpaka teule ambao utakuwa na thamani ya milioni 386 huku akieleza barabara nyengine ya mita 200 zinazokarabatiwa mjini humo zitatumia zaidi ya milioni 60..

Naye kwa upande wake Mkandarasi wa kampuni ya ujenzi SIMAC LTD kutoka Dar Felix Chawe ambao wamekabidhiwa barabara hiyo alisema kwamba anajisikia furaha kupata nafasi ya ujenzi huo huku akihitaji ushirikiano na kuhaidia kufanya kazi kwa uwezo wake wote na maelekezo yaliyopo kwenye mkataba.

Mwisho.
Share:

Baada ya Rais Magufuli Kupiga Marufuku Halmashauri Kukopa, Waziri Jafo Awapa Wiki Moja Wakurugenzi Kumpa Taarifa Za Mikopo

Na.Alex Sonna/FullShangwe
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo,amezitaka halmashauri zote nchini kutoa taarifa Ofisini kwake  juu ya uchukuaji wa mikopo kutoka mabenki ya kibiashara.

Agizo hilo Mhe.Jafo amelitoa leo ofisini kwake jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Mhe. Jafo amesema kuwa wale wote waliochukua mikopo na hawajaanza kuitumia wairudishe haraka ipasavyo kwani Taasisi zote za Serikali zikiwemo mamlaka za Serikali za Mitaa hazitakiwi kuchukua mikopo kutoka mabenki ya kibiasha.

“Hayo ni maelekezo kutoka katika walaka wa Barua ya Katibu Mkuu Hazina barua ya tarehe 13 /12/2016 barua yenye kumbu kumbu namba CBC.155/233/01 kuwa taasisi zote za serikali na mamlaka za serikali hazipashi kuchukua mkopo kutoka benki za kibiashara” Amesisitiza Mhe.Jafo

Aidha  Mhe.Jafo amesema kuwa halmashauri yoyote itakayo wasilisha taarfa zisizo sahihi itachukuliwa hatua za kisheria.

“Hivyo wito wangu kwa  halmashauri hizo ni kuwasilisha taarfa sahihi kulingana na mikopo waliyo chukua kwani udanganyifu wowote utakao bainika kuwa kuna mikopo ya kimashaka mashaka ambayo haikufuata taratibu sahihi ofisi itachukua hatua mbali mbali za kisheria” amesema Mhe. Jafo

Hata hivyo Mhe.Jafo amemtaka Katibu Mkuu OR-TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamhanga kusimamia  wakurugenzi wake wote kuhakikisha wanafanya kazi kwa kanuni , sheria na taratibu za kazi zinavyowataka kufanya kazi ili kufikia malengo yanayotakiwa katika utendaji wao.

Jafo amesema kuwa baada ya halmashauri zote kuwasilisha taarfa hizo katika ofisi za TAMISEMI itafanya tathimini na kutoa maelekezo baada ya kupima taarfa zilizo wasilishwa.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger