Monday, 25 November 2019

Chadema yatoa majina ya wagombea ngazi ya kanda...Lazaro Nyalandu Naye Yumo

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetangaza wagombea mbalimbali wa uchaguzi ndani ya chama hicho ngazi ya kanda ambao wameteuliwa kwenye kikao cha Kamati Kuu cha Novemba 23, 2019 ambapo mwanasiasa mkongwe, Lazaro Nyalandu, amepitishwa kugombea uenyekiti wa kanda ya kati akichuana na Alphonce Mbassa.

Nafasi hizo za walioteuliwa ni mwenyekiti wa kanda, makamu mwenyekiti na mweka hazina ambapo chama hicho kinatarajiwa kufanya uchaguzi mkuu Desemba 18, mwaka huu.


Share:

Tume Ya Uchaguzi Yatoa Mwaliko Kwa Taasisi Na Asasi Za Kiraia Kutoa Elimu Kwenye Uchaguzi Mkuu Wa 2020

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) nchini Tanzania imetoa nafasi kwa taasisi au asasi zenye nia ya kutoa elimu ya mpiga kura kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2020 kuwasilisha maombi yao kwa tume hiyo.

Taarifa iliyotolewa Novemba 22, 2019 na Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi, Gerald Mwanilwa imesema hatua hiyo inatokana na kifungu cha 4C cha sheria ya taifa ya uchaguzi sura ya 343 kinaeleza Tume ina jukumu la kutoa elimu ya mpiga kura nchi nzima, kuratibu na kusimamia watu wanaotoa elimu hiyo.

Mwanilwa amebainisha vigezo ni; taasisi au asasi itakayowasilisha maombi hayo inatakiwa kuwa na usajili kwa mujibu wa sheria za taifa, iwe imefanya kazi nchini si chini ya miezi sita tangu kusajiliwa kwake.

Vingine ni; asasi au taasisi iwe haina taarifa ya kuvuruga amani au kuchochea fujo ndani ya nchi na nchi nyingine, iwe tayari kujigharamia katika kutoa elimu ya mpiga kura na watendaji wake wakuu watatu, wawili wanapaswa kuwa Watanzania.

Kaimu mkurugenzi huyo amesema maombi hayo yanatakiwa kuambatanishwa na cheti cha usaili, katiba ya taasisi au asasi, majina ya viongozi wakuu wa taasisi au asasi, anuani kamili ya makazi na ratiba kamili ya maeneo wanayotarajia kutoa elimu kwa mpiga kura.


Share:

Majaji Watatu Kutumia Wiki 3 kusikiliza Mashauri 29

Jumla ya mashauri 29 yanatarajiwa kuwasilishwa na kusikilizwa katika Mahakama ya Rufaa ambayo inaanza leo Jumatatu Novemba 25 hadi Desemba 11, 2019 Kisiwani Unguja, Zanzibar.   

Mashauri ya rufaa za madai ni 12, mashauri ya jinai matatu, mashauri ya madai 11 na maombi ya jinai ni matatu.

Hayo yamesemwa leo Jumatatu na Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufaa Amir Khamis Msumi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Msumi amesema kikao hicho cha wiki tatu kitaongozwa na majaji watatu ambapo Mwenyekiti wao atakuwa Jaji Agostona Mahija akisaidiana na Jaji Gerad  Ndika pamoja na Jaji Rehema Kerefu.

Amesema kikao hicho  kimepanga kusikiliza mashauri yote na ikiwezekana kuyatolea uamuzi.


Share:

LIVE: Ziara Ya Rais Magufuli Jijini Dodoma

Tarehe 25 Novemba, 2019 Mhe. Rais Magufuli anaweka jiwe la msingi la ujenzi wa uwanja wa maadhimisho ya kitaifa Ikulu Chamwino, ataweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) katika eneo la Kikombo, ataweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa jengo la Bodi ya Usajili wa Wakandarasi (CRB) na kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji Jijini Dodoma.


Share:

Tangazo La Nafasi Za Kazi Katika zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura -Dodoma

Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Dodoma Mjini anapenda kuwajulisha kuwa, zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika Kata zote za Halmashauri ya Jiji la Dodoma linaanza hivi karibuni. 

Katika zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la  Wapiga kura Vituoni, watatumika Waandishi Wasaidizi na BVR Kit Opeators

Hivyo anakaribisha maombi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi hizo:

Kwa maelezo ya ufafanuzi wa Tangazo, Sifa za Waombaji wa nafasi (Waandishi Wasaidizi na BVR Kit Operators), Majukumu yao na Mambo ya kuzingatia wakati wa kutuma maombi. 



Share:

Mrema Alalamika Kuchezewa Rafu Uchaguzi Serikali za Mitaa

Mwenyekiti wa chama cha TLP, Augustino Mrema, amesema anaenda kulalamika kwa Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, kwa kile alichokidai mgombea wa chama chake kufanyiwa hujuma, ili mgombea wa Chama Cha Mapinduzi ashinde Uenyekiti wa Serikali za Mitaa katika Kijiji alichozaliwa yeye cha Kiraracha.

Mrema amedai katika zoezi hilo walijitokeza baadhi ya watu, yeye mwenyewe hakuwafahamu walimlazimisha wakala wake kunywa bia, wakati zoezi la kupiga kura likiwa linaendelea huku wakala wake akikataa kufanya hivyo.

"Wananchi wangu walimuona Mwenyekiti wao wa zamani aliyekaa miaka 10 anafaa kuendelea kuwaongoza, nilichoshangaa ni kuwa nguvu kubwa ilitumika, kwa sababu kulikuwa na idadi kubwa ya Polisi na wengine walilazimika kuleta bia ili wakala wangu anywe." Amesema Mrema

"Walipoleta bia, wakala wangu alikataa basi wakatumia hiyo nafasi kufanya mgombea wa chama kingine ashinde nafasi hiyo, kilichonishangaza Vijiji vyote havikukubaliwa wagombea wetu ni Kijiji kimoja tu."

Jana Novemba 24, 2019 Watanzania wa maeneo mbalimbali nchini, walishiriki zoezi la kupiga kura kwa kuwachagua viongozi wa Serikali za Mitaa, Vijiji pamoja na Vitongoji.


Share:

MOTO WAUNGUZA NYUMBA NA KUUA WATU WANNE


WAKAZI wa Makueni, Bi Regina Mueni 49, binti yake Faith Mangeli na wajukuu zake Angel Masava na Amelina Masava wamefariki dunia kutokana na ajali ya moto iliyoikumba nyumba yao iliyopo maeneo ya soko la Nyunzu maeneo ya Makueni nchini Kenya.

Katika tukio hilo mama yake Mueni aliyetambulika kwa jina la Monica Matolo, 75, alipata majeraha kadhaa ya moto na kukimbizwa hospitali ya rufaa ya Makueni kwa ajili ya matibabu.


Aidha, katika uokozi huo mali za thamani zilishindwa kuokolewa na zikateketea. Taarifa zinaeleza kuwa nyumba hiyo ilikuwa na harufu kali ya petroli jambo linaloonyesha kuwa kuna mtu alihusika kuunguza nyumba hiyo.



Polisi wanamhisi kaka yake Mueni kuhusika katika tukio hilo kutokana na kuwapo kwa mgogoro wa ardhi wa kifamilia. Aidha, miili minne iliyokutwa katika tukio hilo ilibebwa na kwenda kuhifadhiwa mochwari ya hospitali ya rufaa ya Makueni.
Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu November 25




















Share:

Sunday, 24 November 2019

Radi Yaua Watatu Rukwa

Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi mkoani Rukwa, Justine Matejo, amethibitisha kutokea kwa matukio mawili ya vifo ambavyo vimesabibishwa kwa mvumo wa radi, hali iliyopelekea watu watatu kufariki Dunia.

RPC Rukwa amesema, wamepokea taarifa hizo za matukio mawili tofauti ambalo moja lilitokea Novemba 23 saa 8:30 mchana, na lingine ni Novemba 19.

"Ni kweli kuna taarifa ambazo tumezipata kwamba huko maeneo ya Namanyele kuna kijiji kinaitwa Mwai, kuna watu wawili wamepigwa radi ambao walikuwa wamejihifadhi chini ya mti, hivyo radi ikapiga mti na watu hao wakapoteza maisha, watu hao ni Japhet Gerrald (25) na mtoto Peter Richard (8)" amesema

"Kuna tukio lingine ambao ni la muda lilitokea Novemba 19, maeneo ya kijiji cha Lahela Mume na Mke ambao walikuwa wamelala, kwa bahati mbaya radi ilipiga ila aliyefariki alikuwa ni Mke" ameongeza

Aidha RPC Rukwa ametoa rai kwa wakazi wa mkoani humo kwa kuchukua tahadhari kuwa wasikae katika miti kwa sababu inakuwa ni tatizo.


Share:

Administrative Assistant Job Opportunity at Export-Import Bank of Korea

Position: Administrative Assistant The Export-Import Bank of Korea Job Purpose: General Support to Office Operations Responsibilities: Answer and direct phone calls Organize and schedule meetings and appointments Produce and distribute correspondence memos, letters, faxes and forms Assist in the preparation of regularly scheduled reports Develop and maintain a filing system, maintain computer and manual filing systems Book travel arrangements… Read More »

The post Administrative Assistant Job Opportunity at Export-Import Bank of Korea appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

LIVE: Rais Magufuli Akipokea Gawio Kutoka Taasisi Mbalimbali

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  anapokea gawio, michango na ziada ya Serikali kutoka mashirika, kampuni na taasisi mbalimbali ambazo zinamilikiwa na Serikali.
 
Hafla ya kupokea gawio, michango na ziada hiyo inafanyika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma


Share:

LIVE:HAFLA YA UPOKEAJI WA GAWIO NA MICHANGO KWA SERIKALI-IKULU CHAMWINO

Share:

WASICHANA 91 MSALALA WA JAMII ZA WAFUGAJI WALIONUSURIKA KUOLEWA WANUFAIKA NA ELIMU BURE


Happiness Julias akiweka kemikali katika kifaa cha maabara katika shule ya sekondari Segese.
Kwandu Mahita akichanganya kemikali katika maabara ya shule ya sekondari Segese.
Mtaalamu wa maabara Esta akiwaelekeza wanafunzi namba ya kufanya mazoezi kwa vitendo katika shule ya sekondari Segese.
Wanafunzi wakimsikiliza kwa makini Mwalimu wa sayansi katika maabara ya shule ya sekondari Segese jana hayupo pichani.
Wanafunzi wakimsikiliza kwa makini Mwalimu wa sayansi katika maabara ya shule ya sekondari segese jana hayupo pichani.


Na Salvatory Ntandu - Kahama

Wasichana 91 kati ya wanafunzi 113 wa jamii za Wafugaji waliohitimu darasa la saba mwaka huu katika shule za msingi zilizopo katika kata ya Segese katika halmashauri ya Msalala mkoa wa Shinyanga wameanza kujifunza kwa vitendo masomo ya sayansi ili kuwahamasisha kupenda masomo hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari mratibu darasa maalumu la elimu kwa wanafunzi wakike, Patrick Mahona amesema wamejipanga kikamilifu ili kuhakikisha wasichana hao wanapata haki yao ya msingi ya elimu baada ya kuwanuru wimbi la kuolewa pindi wanapomaliza elimu ya Msingi.

“Wafugaji katika kata ya Segese mwaka huu walipiga marufuku tabia za wazazi kuwaoza watoto wao pindi wanapohitimu darasa la saba kukubaliana kuanzisha darasa maalumu kwa wasichana 90 ili wajifunze masomo ya awali ya kujiandaa na elimu ya sekondari”,alisema Mahona.

Mahona amesema katika jamii hizo ndoa za utotoni zimekuwa zikishamiri pindi watoto wakike wamapohitimu elimu ya msingi kutokana na wengi wao kutowathamini watoto wa kike hali ambayo imekuwa ikisababisha kushindwa kupata elimu kutokana na kuolewa hata kama watakuwa wamefaulu kuendelea na masomo.

Nao baadhi ya Wanafunzi waliopata mafunzo katika darasa hilo Happness Julius na Kwandu Mashita wamewapongeza wadau wa elimu katika kata hiyo kwa kutambua umuhimu wa mtoto wa kike katika masomo hasa kwa kundi la wafugaji.

“Tangu darasa hilo lilipofunguliwa tumejifunza masomo yote ambayo yatatusaidia kujiandaa na masomo ya sekondari hapo mwakani ambapo mpaka sasa tumeweza kuingia katika maabara za sayansi na kujifunza kwa vitendo majaribio mbalimbali",alisema.

Kwa upande Mwalimu Jeconia Mlinda kutoka shule ya sekondari Segese amesema wanafunzi hao wamejifunza masomo yote kwa nadharia na vitendo ambayo yatawasidia kufanya vizuri katika masomo yao hususani ya sayansi.

“Niwaombe wazazi kuwahamsisha watoto wenu kujifunza masomo ya sayansi kwani yatawasidia kukabiliana na wimbi la ajira wataalamu wa sayansi wanahitajika sana katika kada mbalimbali hususani sekta ya afya”,alisema Mlinda.
Share:

Government Job Opportunities at MBEYA District Council | Uboreshaji Daftari la Wapiga Kura

Government Job Opportunities  at MBEYA District Council | Uboreshaji Daftari la Wapiga  Kura



Share:

Clinical Coordinator at Aga Khan Health Services November 2019

Aga Khan Health Services Tanzania (AKHST) – an agency of the Aga Khan Development Network (AKDN) is a non-profit international organization that supports social development programs in Tanzania completed a major expansion to position the institution to become a leading and integrated tertiary and teaching health care system in Tanzania. As part of its health systems strengthening initiatives… Read More »

The post Clinical Coordinator at Aga Khan Health Services November 2019 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

RAIS DKT MAGUFULI NA MKEWE WASHIRIKI MISA YA JUMAPILI KATIKA PAROKIA YA MT.MARIA CHAMWINO JIJINI DODOMA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakishiriki misa ya Jumapili katika Parokia ya Mt. Maria Imaculata Chamwino Ikulu kijijini
Chamwino jijini Dodoma leo Novemba 24, 2019. Hui ni mara ya Kwanza kwa Rais na Familia yake kushioriki katika misa katika parokia hii toka ahamkie rasmi Dodoma

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakishiriki misa ya Jumapili katika Parokia ya Mt. Maria Imaculata Chamwino Ikulu kijijini
Chamwino jijini Dodoma leo Novemba 24, 2019. Hui ni mara ya Kwanza kwa Rais na Familia yake kushioriki katika misa katika parokia hii toka ahamkie rasmi Dodoma
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakitoa sadaka wakati wa misa ya Jumapili katika Parokia ya Mt. Maria Imaculata Chamwino Ikulu kijijini Chamwino
jijini Dodoma leo Novemba 24, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea baada ya  misa ya Jumapili katika Parokia ya Mt. Maria Imaculata Chamwino Ikulu kijijini Chamwino jijini Dodoma leo Novemba
24, 2019

Picha na IKULU
Share:

Digital Marketing Executive Job Opportunity at WORLDPORI Travel And Tours LTD

Position: Digital Marketing Executive Location: Dar es Salaam Job Summary Assist in the planning, execution and optimization of our online marketing efforts. Passion in marketing and technology is key. Responsibilities: Assist in the formulation of strategies to build a lasting digital connection with customers Plan and monitor company presence on social media ( Instagram, Facebook, Tweeter, etc ) Launch… Read More »

The post Digital Marketing Executive Job Opportunity at WORLDPORI Travel And Tours LTD appeared first on Udahiliportal.com.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger