Thursday, 29 August 2019

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMIS AGOSTI 29,2019


















































































Share:

Wednesday, 28 August 2019

Okoa Ndoa Yako Na Afya Yako Sasa Kwa Kutumia Dawa Bora Ya Nguvu Za Kiume Na Kisukari

Ni dawa zilizopimwa na mkemia na kupewa no 341/VOL,XV/36 na TFDA no 0127/F/F/1819/ MTINJETINJE ni dawa ya kisukari .....Hurudisha kongosho katika hali ya kawaidi hata kama limefeli haijalishi unatumia vidonge au sindano za insulin, itaifanya sukari kuwa normal

SUPER MAJINJA ni dawa inayotibu nguvu za kiume yani matatizo yafatayo (1) kushindwa kurudia tendo na mwili kuchoka (2)kuwai kufika kabla ya  mwenzi wako (3)maumbile ya kiume kulegea na kusinyaa (4)maumbile ya kiume  kuingia ndani na kuwa mafupi kwa wale walio jichua (5)miuungurumo ya tumbo,ngiri,kukosa choo,kiuno kuuma

ACHA KUONGOPEWA SASA DAWA HIZI NI TOFAUTI NA ULIZOWAI KUTUMIA

NJOO OFISINI KWANGU MBAGALA KARIBU NA BENK YA KCB NA mwanza yupo wakala piga simu ya DR AGU whatsapp 0783185060. 0620113431


Share:

Job Opportunity at Sanaa WALIPO, Technical Advisor

Sanaa WALIPO (Sanaa WAPOLI LIVING POSITIVE) with its base at Patandi Akheri in Meru DC Arusha Region. Sanaa WALIPO is a community based organisation working to cooperate with various stakeholders in educating, identification linkage to treatment and following up of TB and HIV patient. Sanaa WALIPO seeks to recruit qualified individuals to fill vacancy below Technical Advisor – Fixed… Read More »

The post Job Opportunity at Sanaa WALIPO, Technical Advisor appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Job Opportunity at Room to Read, Manager, Administration

Manager, Administration   Position Overview The incumbent is responsible for administrative operations of the office including day to day logistic arrangement, office management, and all procurement management for both program and non-program items. This position will report to the Director Program Operations, supervise senior Office associate with dotted line support to the field based administration associate/s. Role and Responsibilities:  … Read More »

The post Job Opportunity at Room to Read, Manager, Administration appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

DC NDAGALA AONYA WAFANYABIASHARA WANAONUNUA MIHOGO SHAMBANI..WAKULIMA WATAKA BEI ELEKEZI


Mkulima wa Muhogo akimweleza jambo Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala 

Na Rhoda Ezekiel Malunde1 blog

Mkuu  wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala, amewataka wafanya biashara wa  zao la muhogo kuacha tabia ya kuwaibia wakulima kwa kwenda kununulia shambani mihogo bila kutumia mzani akionya kuwa watakaobainika wananunua zao hilo bila kutumia mzani watachukuliwa hatua kali za kisheria.


Maagizo hayo ameyatoa leo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wakulima wa kata ya Kasanda wilayani Kakonko, ambapo wakulima hao walisema wanalazimika kuuza zao hilo kwa  gunia kwa shilingi 12,000/=.

Ndagala amewaagiza wafanya biashara wote kutumia mizani kupima zao hilo ili kuepuka kuwaibia wakulima, wakulima wengi wilayani Kakonko wanategemea zao la muhogo  kuwapitia kipato na kuinua hali zao za uchumi.

"Kuanzia leo ni marufuku kwa mkulima yeyote kuuza mazao shambani, kwa kuwa itakuwa vigumu kuwabaini wafanyabiashara  wanaowaibia wakulima kwa kutokutumia mizani; hata hivyo niwaombe tutayarishe zao hilo kwa ubora kwa kukausha juu ya turubai au vichanja ili kuwavutia wanunuzi kwa kununua kwa bei nzuri. 

Niwatake wafanyabiashara kuacha tabia ya kuwanyonya wakulima kwa kununua kwa bei ya chini wakati ninyi mnakwenda kuuza na kupata faida zaidi", alisema Mkuu huyo.

Aidha aliwataka wakulima kuunda vikundi na kuweza kupatia mikopo na serikali pamoja na mashirika ilikuanzisha viwanda, waweze kuyaongezea thamani ya mazao hayo na kuuza katika masoko ya nje katika nchi za Burundi, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambako zao hilo linahitajika sana maeneo hayo.

Pia aliwaagiza maafisa biashara wa wilaya na watendaji wa vijiji kufuatilia na kuhakisha kuwa wanunuzi wa zao hilo na mazao mengine wanatumia mizani na iliyohakikiwa na wakala wa vipimo.

Mkazi wa Kasanda, Anthony Mlengera  alisema wao kama wakulima wanalazimika kuuzia shambani kwa kuwa kwa sasa zao hilo halina soko hivyo waliiomba serikali kuwatafutia soko la zao hilo ili waweze kuuza kwa bei nzuri ambapo hapo awali bei ya zao hilo lilikuwa zaidi ya shilingi 500.

Alisema walihamasishwa sana na maafisa kilimo kulima zao hilo kwa kuwa bei yake ilikuwa nzuri na wamelima zaidi. Na kuelezwa kwamba zao la muhogo linahitajika nchini China na sasa hakuna wanaokuja kuchukua zao hilo mbali  ya wafanya biashara kutoka nchi jirani kuja kununua kwa bei ya chini sana hivyo kuwaumiza wakulima.

Naye Kagoma Hamisi mkulima katika Kijiji cha kabingo alisema serikali ikitaka kumaliza tatizo hilo la wakulima kuibiwa na kuuza kwa bei ya chini, kuwepo na bei elekezi ya zao hilo kwa maeneo yote yanayolima muhogo kama ilivyo kwa mazao mengine kama vile pamba ili kuondoa changamoto ya mkulima kuibiwa na kuuza kwa bei ya chini.
Share:

UPDATES: Viongozi wa maandamano ya kushinikiza kuachiwa kwa ndege Ya Tanzania Inayoshikiliwa Afrika Kusini wakamatwa na Jeshi la Polisi

Watu watatu wanaodaiwa kuwa viongozi walioanzisha maandamano ya kushinikiza kuachiwa kwa ndege ya Air Tanzania iliyoshikiliwa nchini Afrika Kusini wamekamatwa  na Jeshi la Polisi.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam  Lazaro Mambosasa, amesema jeshi la polisi  limeyatawanya maandamano hayo kwa kuwa hayana kibali.

Mambosasa amewataka watanzania wawe watulivu kwa kuwa serikali imeshaanza kulishughulikia suala hilo la ndege ya Tanzania  inayoshikiliwa Afrika Kusini



Share:

TaCRI YAHAMASISHA WAKULIMA TARIME KUCHAKATA KAHAWA SAFI

Mkulima Mwita Hechei mkazi wa kijiji cha Mbogi kata ya Mbogi wilayani Tarime aliyeinama chini kuokota Kahawa akijaribu kuona ufanyaji kazi wa mashine aliyonunua sh.Milioni 1,900,000 kwa ajili ya kubangua Kahawa safi


Na Dinna Maningo  -Tarime  

Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania Kituo kidogo cha Sirari Wilayani Tarime (TaCRI) imewataka wakulima wa Kahawa kuchakata kahawa safi kwani kwa kufanya hivyo watajiongezea kipato kikubwa cha fedha.

Akizungumza na wakulima wa zao hilo Meneja wa Kanda wa TaCRI Almas Hamadi alisema Wakulima wa Mara wengi wao huuza Kahawa ya maganda ambayo haiwapatii faida kubwa, hivyo wanapaswa kulima na kuuza kahawa safi iliyochakatwa ili kujipatia kipato kikubwa.

Hamadi alieleza kuwa, baadhi ya wakulima wameonyesha nia ya kuanza kuchakata Kahawa safi ambayo itawapatia faida ikilinganishwa na uuzaji wa Kahawa ya Maganda.

"Wakulima wabadilike waachane na mazoea ya kuuza kahawa yenye maganda sasa wanapaswa kuuza kahawa isiyo na maganda ambayo ni safi itawaingizia fedha nyingi.Nashukuru juhudi za TaCRI zimezaa matunda na mkulima mmoja wa kata ya Mbogi Mwita Hechei amenunua mashine ya kubangua kahawa safi",alisema Hamadi

Mmoja kati ya wakulima waliowezeshwa na TaCRI Joyce Petro alisema kwa kipindi chote walichokuwa wanauza kahawa ya maganda hawajawahi kuuza zaidi ya shilingi 1,400/= kwa kilo moja.

Mkulima wa Kijiji cha Nyarero Petro Bururyo alisema wameamua kuanza kuchakata kahawa safi baada ya kuona wakulima wenzao wa mikoa mingine kama Kilimanjaro wakiuza Kahawa safi kwa bei kubwa mpaka kufikia sh.4,000 kwa kilo.

Mwita Hechei aliyenunua mashine ya kubangua Kahawa kwa bei ya shilingi 1,900,000 alisema mashine hiyo itamsaidia kujipatia kipato lakini pia italeta ushawishi kwa wakulima wengine kuchakata na kuuza Kahawa safi.

Share:

Job Opportunities at Jubilee Insurance, Sales Agents

Position: Sales Agents Job Jubilee Insurance was established in August 1937, as the first locally incorporated Insurance Company based in Mombasa in 1937. Jubilee Insurance has spread its sphere of influence throughout the region to become the largest Composite insurer in East Africa, Handling Life, Pensions, General and Medical Insurance. Today, Jubilee is the number one insurer in East… Read More »

The post Job Opportunities at Jubilee Insurance, Sales Agents appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Job Opportunities at Jubilee Insurance, Bancassurance Relationship Officers

Position: Bancassurance Relationship Officers (BRO) Job Location: DAR ES SALAAM, DODOMA, ARUSHA, MWANZA Jubilee Insurance was established in August 1937, as the first locally incorporated Insurance Company based in Mombasa in 1937. Jubilee Insurance has spread its sphere of influence throughout the region to become the largest Composite insurer in East Africa, handling Life, Pensions, General and Medical Insurance. Today,… Read More »

The post Job Opportunities at Jubilee Insurance, Bancassurance Relationship Officers appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

ob Opportunity at TCCO, Administrative Zone Coordinator

Administrative Zone Coordinator   Job Summary The administrative coordinator will support the technical coordinator in implementing all program activities for the treatment of children in the Coastal zone. He/she will work under the supervision of the National Technical Coordinator and the Country Coordinator, and will collaborate with clubfoot treatment providers, clinic administrators, and vendors. Background: Tanzania Clubfoot Care Organization… Read More »

The post ob Opportunity at TCCO, Administrative Zone Coordinator appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Job Opportunity at ICAP, Finance Assistant Mobile Payments

Finance Assistant Mobile Payments  Job Summary Working under the supervision of the Senior Accountant, the Accountant will assist in the day-today accounting and financial activities and offer support to implementation of the organization’s accounting policies and procedures, posting of data and preparation of timely payments to all regions. Minimum Qualification: Bachelor Experience Level: Entry level Experience Length: 10 years… Read More »

The post Job Opportunity at ICAP, Finance Assistant Mobile Payments appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Job Opportunity at Oxfam, Finance Assistant

Finance Assistant  Location:Tanzania – Kibondo Hours:40 hours per week Salary:As per agreement Region:HECA Job Family:Finance Division:International Job Type:Fixed Term Closing Date:6 September 2019 Finance Assistant Contract Period: Fixed Term – 6 Months Salary: Competitive Package in line with Oxfam Values Location: Kibondo, Tanzania Oxfam is a global movement of people working together to end the injustice of poverty.… Read More »

The post Job Opportunity at Oxfam, Finance Assistant appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Program Field Officer at MiracleFeet Tanzania

Position: Program Field Officer, East Africa Job Summary The Program Field Officer will support the development and implementation of MiracleFeet programs to treat children with clubfoot in East Africa. Minimum Qualification: Bachelor Experience Level: Mid level Experience Length: 3 year Job Description MiracleFeet Overview MiracleFeet is an international nonprofit organization that increases access to proper treatment for children born… Read More »

The post Program Field Officer at MiracleFeet Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Kutana na Mtanzania wa kwanza kuwa Afisa Mkuu wa Fedha,Tigo Tanzania.

Tigo Tanzania ni kampuni inayoongoza katika kubuni, na kuleta huduma na bidhaa bora zinakata kiu ya watanzania, sasa kutana na Innocent Rwetabura mtanzania wa kwanza kuwa Afisa Mkuu wa Fedha

Historia ya bwana Rwetabura inajieleza yenyewe. Alijiunga na kampuni ya Tigo akiwa na uzoefu mkubwa unaotokana na kutumikia katika nyadhifa mbalimbali za juu katika makampuni mengine katika sekta ya mawasiliano.

Kwa mujibu wa maelezo yake, uhasibu upo katika damu yake. Ndio ni ukweli kwamba uhasibu unaambatana na donge nono, lakini hamasa yake haitokani na malipo au mafao yatokanayo na taaluma hiyo, bali hamasa na msukumo wa kuwa mhasibu mahiri unatokana na ukweli kwamba kazi hii inasisimua kitaaluma.

Safari yake katika sekta ya uhasibu na fedha ilianza pale alipochukuliwa kwenda kufanya kazi mara baada ya kuhitimu kutoka katika chuo kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1998.

Kwa mara ya kwanza kabisa aliingia katika sekta ya ajira kama mhasibu msaidizi wa benki, Citibank. Akiwa na miezi michache tu tangu kuajiriwa, Price water house Coopers (PwC) walimpigia simu ya kutaka kufanya naye kazi na akachukua fursa hiyo. 

“Japokuwa mazingira na mafao yalikuwa mazuri sana pale Citibank lakini matarajio aliyokuwa nayo kwa kufanyakazi PwC yalikuwa bora zaidi. Nilihitaji kuwa pale ambapo utendaji upo. PwC ilikuwa ni njia yangu ya kuelekea kuwa mhasibu mahiri katika mazingira ambayo yanatoa kiwango cha juu cha utaalamu wa uhasibu,” alisema bwana Rwetabura.

Ni wazi kabisa kwamba bwana Rwetabura ni mtu mwenye malengo makubwa. Ametumikia makampuni mbalimbali akiwa katika nyadhifa mbalimbali kwa miaka mingi. Amefanya kazi na PwC kwa takribani miaka miwili. Baada ya hapo alihamia katika kampuni ya Celtel (ambayo kwa sasa ni Airtel) kama Meneja wa Fedha akitokea kuwa Mkaguzi wa Mahesabu.

 Alipoanza kazi kama Meneja wa Fedha, kampuni ya Celtel ilikuwa ni ndogo. Kadri ambavyo kampuni hiyo ilivyokuwa inakua, nafasi yake ilipandishwa hadi kufikia kuwa Mdhibiti wa Fedha.

Baada ya mwaka mmoja na nusu, alihamishiwa nchini Sierra Leone akitumikia kampuni hiyo hiyo na katika wadhifa huo huo wa Mdhibiti wa Fedha. Alifanikiwa kupanda vyeo mbalimbali na kufikia ngazi ya Mdhibiti wa Fedha baada ya mwaka mmoja.

Mafanikio yake haya hajayapata pasipokuwa na gharama yoyote. “Sierra Leone ni nchi ambayo ilitokea vita vya wenyewe kwa wenyewe, na kutokana na mtazamo mbaya uliokuwa unasambazwa wakati huo katika vyombo vya habari wakati huo, ilikuwa ni changamoto kwa mke wangu na familia kufwatana na mimi japo kuwa alikuwa akinitembelea mara kwa mara,” Alisema bwana Rwetabura.

Baada ya miaka mitatu, mwaka 2010, bwana Rwetabura aliona kwamba ni wakati mwafaka wa kurudi Tanzania.

Alipowasili, alijiunga na kampuni ya Zantel kama Mkurugenzi wa Fedha. Alishikilia wadhifa huu kwa karibia miaka miwili kabla ya kuhamia katika kampuni ya ulinzi ya G4S. Sababu zilizopelekea kuhama ni kwamba aliahidiwa kuchukua nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji, nafasi ambayo hakupewa.

Baada ya hapo aliachana na kampuni ya ulinzi na kujiunga na kampuni ya Helios Towers japo katika ngazi za chini. Baada ya muda, kampuni hiyo iliamua kuunganisha vitengo vya idara ya fedha na hivyo nafasi yake iliondolewa.

Bwana Rwetabura alipewa muda wa miezi sita kuweka sawa mambo yake. Wakati bado anapangilia hatua inayofwata, kampuni ya mawasiliano ya Tigo Tanzania ilimpigia simu na ilipofika mwaka 2015 safari yake yenye mafanikio na kampuni ya simu ya Tigo Tanzania ilianza rasmi.

Maisha yake katika kampuni ya Tigo
Awali kabisa bwana Rwetabura alishikilia wadhifa wa Mdhibiti wa Fedha katika kampuni ya Tigo. Mwenendo wake binafsi pamoja na taaluma yake ulichangia kwa kiasi kikubwa katika kumteua bwana Rwetabura kushika nafasi ya Afisa Mkuu wa Fedha (CFO). Amekuwa na mafanikio makubwa tangu alipojiunga na kampuni ya Tigo ikiwemo kuongeza ufanisi kwenye matumizi (Operating Expenditure (OPEX) kwa kiwango ambacho kilikuza faida ya kampuni. Timu anayoiongoza ya idara ya Fedha, iliunganisha kwa wakati mifumo ya Tigo na mfumo wa serikali wa ukusanyaji mapato (ERCS), hatua ambayo imesaidia mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kukusanya kodi na ushuru wa bidhaa kielektroniki. 

“Kazi kubwa ya CFO ni kulinda na kusimamia rasilimali za wanahisa na kuhakikisha maslahi yao yanalindwa na kufwatwa. Jukumu hili linajumuisha kiwango kikubwa cha uwekaji wa mikakati, utekelezaji, usimamizi na uendeshaji wa shughuli zote za kifedha za kampuni ikiwepo kuandaa bajeti na kusimamia utekelezaji wake,” alisema bwana Rwetabura

“Wakati mwingine CFO anajiona kama mpinzani wa Mkurugenzi Mtendaji na wakati huo huo, mshirika muhimu. CEO na timu yake ya biashara wanaweza kuja na wazo, Ili wazo hilo litekelezwa CFO anakiwa kukubaliana nalo au kuja na wazo mbadala ambalo ni bora zaidi. Kwa muda mrefu CFO wameokuwa wakionekana kama wapinzani. Lakini kwa sasa CFO wameanza kubadilika na kushirikiana na mfumo mzima kwa lengo la kuleta matokeo chanya kwa manufaa ya kampuni na wanahisa,” Aliongeza.

Ni dhahiri kuwa, mazingira ya usimamizi wa fedha yanabadilika sana na ni muhimu kukidhi viwango vilivyowekwa duniani. Matumizi ya teknolojia za kisasa ni muhimu katika kuongeza ufanisi na kubaini viashiria vya hatari kwa wakati.

“Tunapaswa kuendana na kasi hii ya mabadiliko kama tunataka kusonga mbele. Kwa mfano, taarifa zetu za fedha zinapaswa kukidhi viwango vya utoaji wa taarifa za kifedha vya kimataifa. (International Reporting Standards)Kwa hiyo, kuwa na timu yenye weledi sio tu katika idara ya fedha lakini pia katika kampuni nzima ni jambo la muhimu.” alisema





Share:

ADONDOKA KUTOKA GHOROFA YA TANO AKIFANYA MAZOEZI


Alexa Terrazas alipokuwa akifanya mazoezi
Msichana mwenye umri wa miaka 23, Alexa Terrazas wa nchini Mexico, ameanguka futi 80 kutoka ghorofani pindi alipokuwa akifanya mazoezi ya Yoga.

Alidondoka kutoka ghorofa ya tano na kuangukia katika eneo la kuegesha magari kwenye ghorofa hilo, Jumamosi iliyopita alilokuwa akifanyia mazoezi lakini alipona baada ya kukimbizwa hospitali.

Picha ya msichana huyo kabla hajadondoka kutoka ghorofani ilisambaa katika mitandao ya kijamii, akionekana amejining'iniza kichwa chini miguu juu kwenye uzio wa chuma.

Inaelezwa kuwa alianguka majira ya saa 1:10 Usiku, ambapo alikimbizwa katika hospitali ya karibu na kufanyiwa upasuaji kwa saa 11, kutokana na kukutwa na nyufa katika miguu yake, mikono, kichwani na mapajani.
Share:

Apandishwa kizimbani kwa kumnajisi mtoto

Raia wa Malawi, Paul John (30), amepandishwa kizimbani Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es Salaam kwa tuhuma za kunajisi mtoto wa miaka saba ili ajiridhishe kingono.

Akisomewa hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Esther Mwakalinga, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Hellen alidai Machi 25, mwaka huu eneo la Tegeta Nyuki wilayani Kinondoni, Dar es Salaam mshtakiwa alimuingiza vidole sehemu za siri mtoto wa miaka 7.

Mshtakiwa alikana kutenda shtaka na Hakimu Mwakalinga alisema dhamana ipo wazi kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili Watanzania,  wafanyakazi wa taasisi inayotambulika kisheria, barua kutoka kwa waajiri wao na vitambulisho vya kazi.

Mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti ya dhamana na kurudishwa rumande hadi kesi yake itakapokuja kusomwa tena Septemba 10.


Share:

DKT.GWAJIMA ATAKA WAGONJWA WANAOTUMIA CHF ILIYOBORESHWA WATHAMINIWE


Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia afya Dk. Doroth Gwajima,akizungumza na watumishi wa kituo cha afya cha Chamwino Ikulu alipofanya ziara ya kukagua utoaji huduma za afya kwa wateja wenye kadi za CHF iliyoboreshwa.
Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya Chamwino,Dk.Zipora Mfugale,akizungumzia kuhusu jinsi walivyojipanga kuhakikisha kuwa wanaongeza idadi ya watu wanaotumia mfumo wa CHF iliyoboreshwa na jinsi watakavyotoa ushauri kwa wananchi kujiunga na CHF iliyoboreshwa
Mratibu wa Ugharamiaji wa huduma za Afya-Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Boniphance Richard,akisisitiza jambo kwa watumishi wa kituo cha afya cha Chamwino Ikulu walipotembelea na kukagua utoaji huduma za afya kwa wateja wenye kadi za CHF iliyoboreshwa.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia afya Dk. Doroth Gwajima,akitoa maelezo kwa watumishi wa kituo cha afya cha Chamwino Ikulu (hawapo pichani) alipofanya ziara ya kukagua utoaji huduma za afya kwa wateja wenye kadi za CHF iliyoboreshwa.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Afya Dk.Doroth Gwajima,akiwaonyesha kadi ya CHF iliyoboreshwa wananchi waliofika katika kituo cha Afya cha Chamwino Ikulu alipofanya ziara ya kukagua utoaji huduma za afya kwa wateja wenye kadi za CHF iliyoboreshwa huku akiwahimiza zaidi ili wajiunge na wapate huduma iliyobora.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Afya Dk.Doroth Gwajima,akizungumza na baadhi ya wananchi waliofika katika kituo cha Afya cha Chamwino Ikulu alipofanya ziara ya kukagua utoaji huduma za afya kwa wateja wenye kadi za CHF iliyoboreshwa huku akiwahimiza zaidi ili wajiunge na wapate huduma iliyobora.

*****

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia afya Dk. Doroth Gwajima, amewataka watumishi wa afya kote nchini kuacha kuwabagua au kutowapa kipaumbele wateja wanaotumia kadi za bima ya afya ya jamii CHF iliyoboreshwa kwa kuwahudumia watu wenye fedha mkononi kwanza.

Dk. Gwajima ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa kituo cha afya cha Chamwino Ikulu alipofanya ziara ya kukagua utoaji huduma za afya kwa wateja wenye kadi za CHF iliyoboreshwa wilayani hapo.

Amewataka watumishi wa afya kuwapa kipaumbele wagonjwa wanaotumia kadi hizo ili kuweza kuongeza idadi ya watu wanaotumia mfumo huo nchini.

Dk Gwajima Amewataka watumishi kote nchini kuendelea kuhamasisha matumizi ya kadi hizo ili kuongeza idadi ya watu wanaotumia mfumo huo hapa nchini na watu wengi waweze kujiunga.

Amesema hivi sasa kadi za CHF iliyoboreshwa imefanyiwa marekebisho makubwa na serikali hali ambayo inamwezesha mgonjwa kupata huduma katika hospitali yoyote hadi ngazi ya mkoa.

Pia amewataka watumishi wa afya nchini kutoa huduma zenye ubora ili kuweza kuwavutia wananchi kujiunga na mifumo hiyo ya bima ya afya ya jamii.

"Kama tusipotoa huduma bora hivi vituo vyetu tulivyojenga nchi nzima vitakuwa havina maana lazima sisi kama watumishi wa afya tubadilike ili kuweza kuwavutia wananchi kuja katika vituo vyetu kupata huduma ya afya"

"Sitaki kusikia baada ya siku hizi 14 kuwa kuna kituo kimeshindwa kutuma taarifa zake au mifumo inakataa kwani kila kituo kinatakiwa kutuma taarifa zake za wateja waliohudumiwa ili kuweza kurejeshewa fedha zake ambazo zitatumika katika mahitaji mbalimbali ya eneo hilo"amesema Dkt Gwajima.

Naye mganga mfawidhi wa kituo cha afya Chamwino, Dk. Zipora Mfugale amesema kuwa wamejipa kuhakikisha kuwa wanaongeza idadi ya watu wanaotumia mfumo wa CHF iliyoboreshwa.

Kwa upande wake ,Meneja Mradi wa HPSS Tuimarishe Afya Ally-Kebby Abdallah,amesema kuwa Azma ya Serikali ni kutengeneza mfumo wa bima ambao mwananchi atatambuliwa lakini pesa anayochangia irudi kwenye kituo.
Hivyo ametoa raia kwa watumishi wa kituo cha Afya Chamwino kuwahamasisha wananchi wajiunge na CHF iliyoboreshwa kwa kushirikiana na uongozi wa sehemu husika. 

Mradi wa HPSS Tuimarishe Afya unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo na Ushirikiano la Uswisi kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania wamechangia kwa kiasi kikubwa katika kuunda mfumo wa kutendea kazi wa IMIS na kutoa mafunzo kwa waandikishaji, waratibu na wasimamizi wa CHF Iliyoboreshwa nchini mpaka kufikia hapa.

Mradi wa HPSS utaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania hadi hapo CHF Iliyoboreshwa itakapo wafikia Wananchi wote wasio katika sekta iliyo rasmi.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger