Monday, 26 August 2019

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani Kaamuru Wakandarasi wa Umeme Katavi Vijijini Wakamatwe

 Na Hafsa Omar, Katavi
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ametoa agizo kwa vyombo vya usalama mkoani Katavi kuwakamata wakandarasi waliopewa kazi ya kusambaza umeme vijijini mkoani humo kutoka kampuni ya CRCBEG baada ya kusuasua katika utekelezaji wa kazi.

Alitoa agizo hilo Agosti 25, 2019 wakati akielekea kwenye kijiji cha Ntibiri wilayani Mlele, Mkoa wa Katavi ili kukagua kazi ya usambazaji umeme, mara baada ya kuwasha umeme katika kijiji Kirida wilayani humo.

Waziri wa Nishati pia alitoa agizo la kushikiliwa kwa hati za kusafiria za wakandarasi hao mpaka watakapomaliza kazi zao za usambazaji umeme walizopangiwa na Serikali.

“ Nilitoa mwezi mmoja eneo lote la kilometa 27 muwe mmeshawasha umeme lakini bado, Kijiji cha Majimoto bado hamjawasha, leo nimepita hapa sijaona vibarua wakihangaika, na wala nguzo hazijafika, nimefika Shule ya Sekondari kule nguzo hazijafika na wala hamjasambaza popote.”alisema Dkt. Kalemani.

Waziri Kalemani, pia aliwaagiza Mameneja wa TANESCO kutoondoka katika eneo hilo ili kuhakikisha kazi ya usambazaji umeme inafanyika kwa kasi zaidi, “ninataka umeme ufike Kijiji cha Majimoto, ifikapo tarehe 5 mwezi ujao na mameneja wote mtabaki hapa kusimamia kazi.”

Akizungumza na Wananchi wa kijiji cha Ntibiri, Dkt. Kalemani aliwaeleza wananchi hao kuwa, Serikali imetoa kiasi cha shilingi bilioni 89 kwa ajili ya usambazaji umeme mkoani Katavi na kuwahakikishia kuwa, mkoa mzima utapata umeme.

“Leo nimetoa maelekezo kuwa, eneo la Ntibiri na maeneo ya jirani, wakandarasi watamaliza kazi mwezi wa 12 mwaka huu, hakuna kijiji kitakachobaki, sasa kama eneo lako halijapitiwa na umeme, kuanzia sasa litapitiwa.” Alisema Dkt Kalemani

Akiwa wilayani Mlele, Waziri wa Nishati, pia aliwasha umeme katika Kijiji cha Society katika eneo la wachimbaji wadogo wa dhahabu hali itakayopelekea wachimbaji hao kufanya shughuli zao kwa tija.


Share:

Mahakama Kuu yatupilia mbali Mapingamizi ya Serikali dhidi ya Tundu Lissu

Mahakama Kuu ya Tanzania imetupilia mbali mapingamizi ya  Serikali kupinga kusikilizwa kwa maombi ya kesi namba 18/2019 ya Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu kuhusu ubunge wake kwa sababu hazina mashiko.

Uamuzi huo umetolewa leo Jumatatu Agosti 26,2019 na Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, Jaji Sirillius Matupa wakati akitoa  uamuzi wa pingamizi la awali dhidi ya maombi ya Lissu lililowekwa na Serikali katika maombi yake ya kibali cha kufungua shauri ili kupigania ubunge wake.

Kutokana na hatua hiyo, maombi ya Lissu kutetea ubunge wake wa Singida Mashariki yataendelea kusikilizwa mahakamani hapo mbele ya Jaji Sirilius Matupa.


Share:

Atiwa Mbaroni Kwa Kosa la Kumbaka Mtoto wa Miaka Mitatu

NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
JESHI la polisi mkoani Pwani, linamshikilia Dismas Silyvester (35)  kwa kosa la kumbaka mtoto mdogo mwenye miaka mitatu, huko Mlandizi  A ,kata ya Mlandizi ,Kibaha .

Aidha Mariam Shomari (25) mkazi wa Msongola ,Mlandizi Kibaha ameibiwa mtoto wake mchanga wa miezi mitatu katika mazingira ya kutatanisha ambapo jeshi hilo linaendelea na msako ili kumpata mtoto huyo.

Akithibitisha kutokea kwa tukio la kwanza ,kamanda wa polisi mkoani hapa, Wankyo Nyigesa aliwaambia waandishi wa habari kwamba, Dismas alimuiba mtoto wa miaka mitatu na kwenda nae kichakani na kumfanyia unyama huo.

“Baada ya taarifa kutolewa kwa jeshi la polisi kwa kushirikiana na raia wema lilimkamata mtuhumiwa na mtoto mchanga huyo katika mashamba ya mbogamboga vichakani “alifafanua Wankyo.

Wankyo alieleza ,uchunguzi unaonyesha mtoto huyo ambae jina limehifadhiwa ,ameingiliwa kimwili.

Akielezea tukio jingine Wankyo alisema, agost 25 saa 7 mchana ,Msongola, Mariam Shomari aligundua kuibiwa mtoto wake mchanga Swaumu Sudi mwenye miezi mitatu.

“Mtoto huyo aliibiwa ndani akiwa chumbani alipokuwa amelala baada ya mama yake kutoka kwenda kuomba kibiriti kwa jirani umbali wa mita 200 na mwanamke ambae hajafahamika hadi sasa”

Inadaiwa mwizi huyo wa mtoto alitumia mbinu ya kuvizia mama wa mtoto kutoka na yeye kufika kwenye nyumba hiyo na kumwambia mtoto mdogo Fatima Sudi miaka mitatu aliyekuwa amebaki na mdogo wake kuwa ametumwa na mama yake kuja kumchukua mtoto huyo ili ampelekee na kufanikisha wizi huo.

Jeshi hilo linaendesha msako mkali wa kumtafuta mwizi wa mtoto ambapo ametoa wito kwa viongozi wa serikali za mitaa ,watendaji wa kata ,wenyeviti wa vitongoji na vijiji pamoja na jamii kutoa taarifa iwao watamtilia shaka mtu ambae anaonekana na mtoto asiye wake.


Share:

Vifo ajali ya lori la mafuta Morogoro vyafika 102

Idadi ya watu waliofariki kutokana na ajali ya moto wa lori la mafuta mkoani Morogoro imefikia 102 baada ya majeruhi mmoja aliyekuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kufariki dunia.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano MNH, Aminiel Aligaesha amemtaja aliyefariki ni Grayson Ndabiti (19) hivyo idadi ya majeruhi waliobaki hospitalini hapo ni 13.

Amesema kati ya majeruhi hao saba wako chumba cha uangalizi maalum (ICU) huku wengine sita wakiwa katika wodi ya Sewahaji.


Share:

Tshisekedi atangaza baraza jipya la mawaziri Congo DR

Rais Félix Tshisekedi ametangaza baraza jipya la mawaziri katika Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo.

Serikali ya kwanza ya rais Félix Tshisekedi imetangazwa leo Kinshasa, baada ya kusubiriwa kwa miezi saba.

Katika serkali hiyo mpya, wanawake wamepewa asilimia kumi na saba ya mawiziri na wanaume asilimia 83.

Mnamo Julai mwaka huu Rais wa DR Congo Felix Tshisekedi na mtangulizi wake Joseph Kabila walikubaliana kuunda serikali ya muungano.

Walikubali kuunda serikali itakayo kuwa na mawaziri 66.

Kama walivyo kubaliana, chama cha rais huyo wa zamani sasa kimepata wizara 43, na kile cha rais Félix Tshisekedi kimejinyakulia wizara 23.


Share:

Ambari Nyeupe Ni Suluhu ya Kurekebisha Maumbile ya Kiume YaliyoSinyaa kwa Kujichua

Ipo  idadi  kubwa  ya  wanaume  wanao  kabiliwa na  changamoto  ya  kuwa  na  maumbile  madogo  ya  kiume kutokana na kujichua kwa muda mrefu.

Kama  wewe  ni  mwanaume  ulie  katika  kundi  hili, unaweza  kujitibu  tatizo  lako  kwa  kutumia dawa  asilia  itokanayo  na  AMBARI  NYEUPE.

Ambari  nyeupe  nyeupe  ikichanganywa  na  dawa  nyingine  tatu  za  asili,  hutumika  kama  tiba  ya  kurekebisha  maumbile  ya  kiume  yaliyo  sinyaa.

Kwa  mahitaji  yako  ya  dawa  hii, fika  katika  duka  la  kuuza  dawa  asilia  la  NEEMA  HERBALIST & NUTRITIONAL  FOODS  CLINIC.

Tunapatikana  UBUNGO  jijini Dar  Es  Salaam, jirani  na  SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING  nyuma  ya  jengo la  UBUNGO  PLAZA.

Wasiliana  nasi  kwa  SIMU  NAMBA  0766  53  83  84 au  0693005189

Na kwa  taarifa  Zaidi  kuhusu  huduma  zetu,  tutembelee  katika  blogu  yetu :

www.neemaherbalist.com


Share:

Junior Horticulture Value Chain / Private Sector Development Expert – Deutsche Gesellschaft für Internationale Zusammenarbeit (GIZ) GmbH

Junior Horticulture Value Chain / Private Sector Development Expert (m/f/d) in the Technical Assistance to Support the Implementation of Agriconnect on Sector Enablers and Business Environment for Tea, Coffee and Horticulture in Tanzania Job-ID: P1690V004 Location: Zanzibar City Assignment period: 02/03/2020 – 02/02/2024 Field: Rural Development Type of employment: full-time Application deadline: 09/22/2019 Job description The Deutsche Gesellschaft… Read More »

The post Junior Horticulture Value Chain / Private Sector Development Expert – Deutsche Gesellschaft für Internationale Zusammenarbeit (GIZ) GmbH appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Job Opportunity at VSO, Research, Monitoring and Evaluation Manager

Research, Monitoring and Evaluation Manager Type of role: Advocacy policy and research Location: Dar Es Salaam, Tanzania Salary: Competitive Contract type: Permanent Full Time: 35 hours per week Application Closing Date: 13 Sep 2019 Interview date: to be confirmed Start date: 14th of October 2019 VSO is the world’s leading independent international development organisation that works through volunteers… Read More »

The post Job Opportunity at VSO, Research, Monitoring and Evaluation Manager appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Watendaji wa Kata Nchi Nzima Waitwa Ikulu

Rais John Magufuli wa Tanzania ametoa mwaliko kwa Maofisa Watendaji wa Kata kutoka Halmashauri zote nchini humo kuhudhuria mkutano Septemba 2, 2019 Ikulu jijini Dar es Salaam.

Taarifa iliyotolewa Agosti 23, 2019 na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) na kusainiwa na katibu mkuu wake, Joseph Nyamhanga imeeleza mkutano huo utafanyika katika viwanja vya Ikulu saa 2:00 asubuhi.



Share:

Supply Chain Coordinator (Sourcing) – Dar es Salaam, save the children tanzania

TITLE: Supply Chain Coordinator (Sourcing) TEAM/PROGRAMME: Operations LOCATION: Dar es Salaam with frequent travel to the field GRADE: 3 POAST TYPE: National CHILD SAFEGUARDING: Level 2: either the post holder will have access to personal data about children and/or young people as part of their work; or the post holder will be working in a ‘regulated’ position (accountant,… Read More »

The post Supply Chain Coordinator (Sourcing) – Dar es Salaam, save the children tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Gender, Advocacy & Campaign Coordinator – Dar es Salaam – World Vision Tanzania, ENRICH project

Purpose of the position: To coordinate the development of ENRICH project Gender and Advocacy strategy and oversee the implementation of the strategy. The gender specialist will be responsible for facilitating training on gender equality and Advocacy for staff and partners and for monitoring gender equality and advocacy results. Observe mission and core values of World Vision and demonstrate… Read More »

The post Gender, Advocacy & Campaign Coordinator – Dar es Salaam – World Vision Tanzania, ENRICH project appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Business Development Executive, Personal Banking Sales – Dar es Salaam

Company: Standard Chartered Bank Location: Dar Es Salaam, Tanzania Career Level: Executive Industries: Banking, Insurance, Financial Services Description About Standard Chartered We are a leading international bank focused on helping people and companies prosper across Asia, Africa and the Middle East. To us, good performance is about much more than turning a profit. It’s about showing how you… Read More »

The post Business Development Executive, Personal Banking Sales – Dar es Salaam appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Media (Documentary) Consultant – Restless

MEDIA (DOCUMENTARY) CONSULTANT CLOSING DATE: 30th August (midnight) LOCATION: Tanzania VISA REQUIREMENTS: Must have the right to work in the UK START DATE: As soon as possible ABOUT RESTLESS DEVELOPMENT We know young people have the power to solve the challenges we face in our world, but they are being sidelined. We are the agency that works with… Read More »

The post Media (Documentary) Consultant – Restless appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Jobs at ILO, Finance and Administrative Assistant (G6) – ILO,

Finance and Administrative Assistant – G6(DC) Grade: G6 Publication date: 23 August 2019 Application deadline (midnight local time in Dar es Salaam, Tanzania): 23 September 2019 Vacancy no.: DC/DAR/GS/2019/04 Job ID: 1704 Department: RO-Africa Organization Unit: CO-Dar es Salaam Location: Tabora Contract type: Short Term The recruitment process for General Service positions is subject to local recruitment regulations… Read More »

The post Jobs at ILO, Finance and Administrative Assistant (G6) – ILO, appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

TFF Yawaita Wanaoonesha Mpira Vibandani

Shirikisho la Soka nchini Tanzania TFF, limewaita watu wote wanaoonesha mpira katika vibanda Jijini Dar es Salaam.

TFF imesema kuwa imewaita watu hao kwa ajili ya kufanya kikao cha pamoja cha majadiliano ya ushirikiano, kitakachofanyika katika ofisi za shirikisho hilo, Karume katika manispaa ya Ilala.

Wamiliki hao wa vibanda vya kuonesha mpira wameombwa kufika kesho Jumanne, Agosti 27. Taarifa kamili ya TFF ni kama inavyoonekana hapa chini.


Share:

Naibu Spika Dkt Tulia Akson Awasilisha Kwa Niaba Ya Spika Mambo 15 Yaliyofanywa Na Rais Magufuli

Na Dixon Busagaga,Moshi
Spika wa Bunge, Job Ndugai, ametaja mambo 15 aliyofanya Rais John Magufuli kwa kipindi cha miaka minne alichokaa madarakani na kuwataka watanzania kumuunga Mkono.

Ndugai ameyataja mjini Moshi, wakati wa kongamano la kumpongeza Rais lililoandaliwa na Umoja wa wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT).

Hotuba ya Ndugai ilisomwa kwa niaba yake na Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Akson , katika uwanja wa Majengo na kuhudhuriwa na wanachama wa UWT na wanawake wa mkoa huo.

Ndugai alisema  Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2015-2020, imetekelezwa kwa kiwango kikubwa,na kwamba miongoni mwa mambo ambayo ametekeleza Rais ni kurejesha nidhamu kwa watumishi.

Alisema lingine ni kushughulikia tatizo sugu la Rushwa ndani ya serikali,na ndani ya chama cha mapinduzi hali ambayo itapunguza kwa kiasi kikubwa rushwa ya uchaguzi katika Chaguzi zijazo.

“Serikali pia imepambana na mafisadi na kuanzisha mahakama ya mafisadi na pia amepunguza matumizi yasiyo ya lazima serikalini kwa kusitisha safari za nje zisizokuwa na Tija,” alisema.

Alisema jambo jingine ni kusimamia taratibu za makusanyo serikalini na kuongeza pato la taifa kutoka asilimia 5.1 hadi kufikia asilimia 7.5, kuongeza kasi ya ujenzi wa Miundombinu, kufufua shirika la ndege na kusimamia vyema rasilimali za nchi.

“Serikali imeendelea na mpango wa kutoa elimu bila malipo kwa shule za msingi na sekondari na kuongeza bajeti ya kutoa mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu,kuimarisha miundombinu ya Maji na kuwa mtetezi wa wananchi walioonewa hasa wanawake,” alisema

Alitaja jambo la 11 ni kuteua tume ya uhakiki wa mali za chama , kufanya mageuzi makubwa ili kuhakikisha kilimo kinawanufaisha wakulima, kugawa vitambulisho kwa wafanyabiashara ili kuondoa ushuru wenye kero pamoja na bajeti ya serikali kugusa maisha ya wananchi.

Akizungumza mwenyekiti wa UWT Taifa, Gaudensia Kabaka, alisema kongamano hilo lililenga kumpongeza Rais kwa kazi kubwa aliyoifanya katika kipindi cha miaka minne na kwamba mambo makubwa yamefanyika katika kipindi hicho.


Share:

Aliyedaiwa kumuua mkewe kwa shoka apigwa na kuchomwa moto

Wananchi wenye hasira kali wamemuua kisha kumchoma moto Juma Lugomba mwenye umri wa miaka 61, Mkazi wa Kijiji cha Chiwata Kata ya Chiwata Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara, baada ya Juma kudaiwa kumshambulia Mkewe kwa shoka na kumuua jambo lililosababisha Wananchi hao kupandwa na hasira na kumuadhibu.

Tukio hilo limetokea katika kijijini Chiwata, na limethibitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Selemani Mzee ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya.

Mzee alisema inadaiwa juzi saa 3 usiku, Lugomba alimshambulia mkewe Yolenda Milanzi (59) na kitu chenye ncha kali na kumsababishia majeraha yaliyopelekea kifo baada ya kumjeruhi vibaya kichwani.

Alidai mkazi huyo baada ya kufanya mauaji hayo kwa mkewe, kundi la wananchi wenye hasira kali waliamua kumsaka na walipomkamata walimjeruhi kisha kumchoma moto hadi kusababisha kifo chake na yeye.

“Ni kweli tukio hilo limetokea mume kumshambulia mke wake na kumuua, lakini baada ya yeye kufanya mauaji hayo asubuhi yake wananchi waliamua kumsaka na walipomkamata walimjeruhi kisha kumchoma moto hadi kufa,” alieleza DC huyo.

Alisema bado chanzo cha mume huyo kufanya mauaji kwa mkewe hakijafahamika, lakini Polisi wanaendelea na uchunguzi juu ya tukio hilo.

Mtendaji wa Kijiji cha Chiwata, Thawabu Mturi alisema mume huyo baada ya kufanya mauaji, alikimbilia kijiji cha jirani cha Pemba kujificha ili kukwepa ushahidi.

Alisema wananchi walipogundua kuwa mume huyo amemuua mke wake, walipandwa na hasira ndipo walipoamua kumtafuta wakiwa na wamebeba silaha za kijadi na walipogundua kuwa amejificha katika kijiji jirani walifika huko na walifanikiwa kumkamata hivyo walimjeruhi kisha walimchoma moto hadi kufa.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger