Sunday, 25 August 2019

Picha : ASKOFU MKUU KANISA LA AICT MUSA MAGWESELA AFUNGUA KANISA LA KISASA KAHAMA MJINI

Askofu Mkuu wa Kanisa la AICT nchini,Musa Masanja Magwesela amefungua rasmi nyumba mpya ya kuabudia (kanisa la jipya AICT Kahama Mjini) lililogharimu jumla ya shilingi milioni 900 (902,397,070/=).

Ufunguzi wa kanisa hilo bora na la kisasa lililopo Nyihogo Mjini Kahama umefanyika leo Jumapili Agosti 25,2019 na kuhudhuriwa na viongozi,waumini na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya wilaya ya Kahama.

Akizungumza wakati wa kuweka wakfu na kufungua jengo hilo jipya,Askofu Magwesela alisema ni jengo bora na la kisasa huku akiwasisitiza waumini na kutumia jengo hilo kumwabudu Mungu.

"Kwa heshima ya Mungu nalifungua na kuliweka wakfu jengo hili. Nyumba hii ni kwa ajili ya ibada pekee,naomba mlitumie kwa maksudi yaliyokusudiwa",amesema. 

Akisoma taarifa ya ujenzi,Katibu wa Kanisa la AICT Kahama Mjini,Charles Pambe amesema kanisa la AICT Kahama Mjini limeanzishwa tarehe 15 Novemba,1975 na mpaka sasa limefungua Pastoreti tisa mjini Kahama na Pastoreti mama ya Kahama,Mlima Sayuni,Mhongolo,Mhungula,Nyakato,Lugela,Majengo,Mbulu na Mwendakulima.

Amesema wamejenga jengo jipya kisasa la kuabudia lililotokana na michango ya waumini ambapo lina mahitaji muhimu ikiwa ni pamoja na ofisi sita,vyoo,sehemu ya kubatizia na maombi ya faragha,mabenchi,meza hivyo mpaka jengo linafunguliwa limegharimu jumla ya shilingi 902,397,070/=.

Amebainisha kuwa mbali na kujenga kanisa jipya pia wamejenga nyumba ya kisasa ya Mwinjilisti,madarasa mawili na ofisi zake,bwalo la kulia chakula na kanisa linaendelea na utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa shule ya msingi 'English Medium School',ujenzi wa shule ya sekondari na zahanati na ukamilishaji wa hosteli ya kanisa.
Askofu Mkuu wa Kanisa la AICT nchini,Musa Masanja Magwesela akiendesha ibada ya kufungua na kuweka wakfu jengo jipya la kuabudia katika kanisa la AICT Kahama Mjini leo Jumapili Agosti 25,2019. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Askofu Mkuu wa Kanisa la AICT nchini,Musa Masanja Magwesela akiendesha ibada ya kufungua na kuweka wakfu jengo jipya la kuabudia katika kanisa la AICT Kahama Mjini.
Maaskofu wa kanisa la AICT wakiendelea na ibada ya ufunguzi na uwekaji wakfu jengo jipya la kanisa la AICT Kahama Mjini. Aliyeshikilia kipaza sauti ni Askofu wa Dayosisi ya Shinyanga, Zakayo Bugota.
Muonekano wa jengo jipya la kanisa la AICT Kahama Mjini.

Muonekano wa jengo jipya la kanisa la AICT Kahama Mjini.
Askofu Mkuu wa Kanisa la AICT nchini,Musa Masanja Magwesela akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa  jengo jipya la kuabudia katika kanisa la AICT Kahama Mjini.
Askofu Mkuu wa Kanisa la AICT nchini,Musa Masanja Magwesela akikata utepe wakati wa kufungua jengo jipya la kuabudia katika kanisa la AICT Kahama Mjini.
Askofu Mkuu wa Kanisa la AICT nchini,Musa Masanja Magwesela akifungua jengo jipya la kuabudia katika kanisa la AICT Kahama Mjini.
Askofu Mkuu wa Kanisa la AICT nchini,Musa Masanja Magwesela akifungua mlango kuingia ndani ya jengo jipya la kuabudia/kanisa la AICT Kahama Mjini.
Katibu wa Kanisa la AICT Kahama Mjini,Charles Pambe akisoma taarifa ya ujenzi wa kanisa jipya la AICT Kahama Mjini ambalo limegharimu jumla ya shilingi milioni 900.
Katibu wa Kanisa la AICT Kahama Mjini,Charles Pambe akisoma taarifa ya ujenzi wa kanisa jipya la AICT Kahama Mjini ambalo limegharimu jumla ya shilingi milioni 900.
Askofu Mkuu wa Kanisa la AICT nchini,Musa Masanja Magwesela  akizungumza wakati wa kufungua kanisa jipya la AICT Kahama Mjini na kuwasisitiza waumini kutumia kanisa hilo kumwabudu Mungu pekee.
Askofu Mkuu wa Kanisa la AICT nchini,Musa Masanja Magwesela  akizungumza wakati wa kufungua kanisa jipya la AICT Kahama Mjini.
 Askofu wa Dayosisi ya Shinyanga, Zakayo Bugota akizungumza wakati wa ufunguzi wa kanisa jipya la AICT Kahama Mjini.
Askofu wa Kanisa la AICT Dayosisi ya Tabora, Silasi Kezakubi akiweka wakfu benchi katika kanisa jipya la AICT Kahama Mjini.
Askofu Mkuu wa Kanisa la AICT nchini,Musa Masanja Magwesela  akizungumza baada ya kufungua kanisa jipya la AICT Kahama Mjini.
Viongozi mbalimbali wa Kanisa la AICT wakiwa kanisani wakati wa kufungua kanisa jipya la AICT Kahama Mjini.
Waumini wa kanisa la AICT wakiwa kwenye ibada baada ya ufunguzi wa kanisa jipya la AICT Kahama Mjini.
Waumini wa kanisa la AICT wakiwa kwenye ibada baada ya ufunguzi wa kanisa jipya la AICT Kahama Mjini.
Waumini wa kanisa la AICT wakiwa kwenye ibada baada ya ufunguzi wa kanisa jipya la AICT Kahama Mjini.
Waumini wa kanisa la AICT wakiwa kwenye ibada baada ya ufunguzi wa kanisa jipya la AICT Kahama Mjini.
Waumini wa kanisa la AICT wakiwa kwenye ibada baada ya ufunguzi wa kanisa jipya la AICT Kahama Mjini.
 Askofu wa Kanisa la AICT Dayosisi ya Tabora, Silasi Kezakubi akizungumza kwenye ibada baada ya ufunguzi wa kanisa jipya la AICT Kahama Mjini.
Kwaya ya AICT Chang'ombe wakimsifu Mungu wakati wa ufunguzi wa kanisa jipya la AICT Kahama Mjini.





Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumapili 25 August

















Share:

Saturday, 24 August 2019

VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA WAONYWA KURUBUNI WANANCHI KWENYE UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA


Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera Limbe Benard Limbe

Na Lydia Lugakila - Malunde1 blog 
Katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu, viongozi wa vyama vya siasa mkoani Kagera wameonywa kutowarubuni wananchi kwa jambo lolote kwani ni kosa kisheria na haki hainunuliwi hivyo atakayebainika sheria itachukua mkondo wake.

Onyo hilo limetolewa leo na Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera Limbe Benard Limbe wakati akitoa ufafanuzi juu ya taratibu katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.

Limbe amesema haki ya kuongozwa, haki ya kuchagua na ya kuchaguliwa ni haki ambayo iko huru kwa sababu katiba ya nchi inaruhusu mtu achague ama achaguliwe.

Kutokana na hali hiyo amewaonya wanasiasa kutothubutu kufanya mchezo wa aina yoyote unaolenga kuwarubuni wananchi kwani sheria itachukua mkondo wake kwa yeyote atakayebainika.

Amebainisha kuwa  kama kuna mtu atajitokeza kumrubuni mwananchi ni kosa kisheria kwa sababu kufanya hivyo itakuwa ni kunyima mwananchi haki yake ya msingi ya kuweza kumchagua kiongozi aliye bora kiongozi ambaye ataweza kumletea maendeleo yake mwenyewe katika kutatua shida zake mbalimbali.

Mkurugenzi huyo amesema wananchi wanapaswa kutochagua kiongozi kwa sababu ya kupewa kitu au msukumu flani bali wachague kiongozi atakayewafaa.

Amesema wananchi wajiandae kufanya uchaguzi wa amani ambapo taratibu na miongozi yote itatolewa na serikali na kuwa itakapowafikia wataiwasilisha katika vitongoji, mitaa na kata na kila mhusika atapata taarifa inayostahili ili zoezi hilo liende katika hali inayotakiwa.

Katika hatua nyingine mkurugenzi huyo amesema suala la uchaguzi litahusu Mtanzania halisi yaani Raia awe wa kuzaliwa.

"Atakayehusika katika zoezi hilo ni yule aliyeandikishwa na akapewa Utanzania sio kwamba mtu amekuja kufanya kazi na anataka kupiga kura jambo hilo halitakubaliki", amesema

Limbe amesema wananchi wasiwe na hofu yoyote kwani Matangazo yatapita kila mahali na kuwa hadi muda huu tayari zoezi la kubainisha wale wote watakaoshughulika na zoezi zima la kuandikisha liko tayari.

Ameeleza kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa ni uchaguzi mama kwa kuwa shughuli zote zinafanyika katika serikali za mitaa na wale viongozi ndio viongozi wa ngazi ya mwanzo ambao wananchi wanaishi nao na ambao wananchi ni rahisi kuwafikia.

Aidha ametoa wito kwa wananchi kujiandaa kuchagua kiongozi aliye bora, kiongozi ambaye anaweza kuyaona matatizo ya wananchi kiongozi ambaye yuko tayari kuyatetea, kuyaona matatizo kwa kufuata sheria taratibu na kanuni. 

Aidha amesema miongozo na taratibu ya katiba imewapa muda mwingine tena wa kubainisha kiongozi wanayemtaka na ambaye ni bora ambaye ataweza kutatua mahitaji yao.

Mkurugenzi huyo amempongeza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa kwa jinsi ambavyo amewashirikisha wadau mbalimbali katika uchaguzi wa serikali za mitaa huku akiwataka wananchi kuondoa wasiwasi kwani serikali imejipanga ili kuhakikisha uchaguzi huo unakuwa bora.
Share:

Picha : MASHINE 23 ZA MICHEZO YA KUBAHATISHA ZACHOMWA MOTO SHINYANGA MJINI

Na Annastazia Paul - Malunde1 blog
Jumla ya mashine 23 zinazotumika katika michezo ya kubahatisha zimekamatwa katika maeneo mbalimbali mkoani Shinyanga na kuteketezwa kwa kuchomwa moto kutokana na waendeshaji wa mashine hizo kukiuka kanuni na taratibu za uendeshaji wake.

Akizungumza jana Agosti 23,2019 wakati wa zoezi la kuziteketeza mashine hizo lililofanyika katika dampo la Mwawaza Mjini Shinyanga,Meneja Ukaguzi na Udhibiti kutoka bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania Sadiki Elimsu alisema kuwa amepata taarifa juu ya uwepo wa mashine hizo kinyume na utaratibu kutoka kwa mkuu wa wilaya na kuanza msako ambao umefanikisha ukamataji wa mashine hizo.

"Hivi karibuni tulipata taarifa kutoka kwa mkuu wa Wilaya ya Shinyanga akitufahamisha kwamba kuna waendeshaji wa michezo ya kubahatisha ambao wanaendesha katika maeneo yasiyoruhusiwa kisheria, baada ya kupata taarifa hizo bodi iliagiza maafisa wake ili kuja kujithibitishia na kuchukua hatua zinazostahili",alisema Elimsu.

Amesema katika maeneo waliyotembelea bodi hiyo iligundua ukiukwaji wa uendeshaji wa mashine hizo hivyo kuzikamata kisha kuziteketeza.

"Tulibaini kwamba kuna baadhi ya waendeshaji wanakiuka mashairi ya leseni ambazo wamepewa ambazo zinataka mashine hizi zifungwe maeneo ambayo tayari bodi imeshafanya ukaguzi wake na kujiridhisha kwamba yanakidhi matakwa ya kisheria, hivyo katika maeneo hayo tuliweza kuzikamata mashine hizo na kuzileta hapa katika dampo hili na kuziteketeza",alisema Elimsu.

Alisema kupitia msako huo bodi imebaini baadhi ya waendeshaji ambao walikuwa wanakiuka taratibu za upatikanaji wa leseni.

"Baadhi ya waendeshaji walikuwa wanachukua leseni kutoka katika Mamlaka ambazo hazina sifa za kutoa leseni za kuendeshea michezo hiyo na tulikuwa tukiwaambia leseni hizo zinatolewa na bodi ya michezo ya kubahatisha Tanzania pekee",alieleza Elimsu.

Ameeleza kuwa baadhi ya mashine zilikuwa zimewekwa katika maeneo ambayo hayakukaguliwa na kuidhinishwa na bodi hivyo kuruhusu hata watoto wacheza jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Katika hatua nyingine Meneja huyo wa ukaguzi na udhibiti kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha Tanzania alisema kuna baadhi ya waendeshaji wanaingiza nchini mashine hizo kinyemela na kwambaa mmoja wao ameshakamatwa na yupo jijini Dar-es-salaam akishikiliwa na jeshi la polisi.

"Bado anashikiliwa na jeshi la polisi yeye alipatikana na mashine zinazokadiriwa kuwa ni zaidi ya 1,200 ambazo tayari tumeshazikamata na uchunguzi bado unaendelea kuhusiana na mfanyabiashara huyo",alisema Elimsu.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko aliwaomba wananchi kushiriki kwa kutoa taarifa kwenye vyombo husika ili kuweza kuondosha michezo hiyo katika Wilaya ya Shinyanga.

"Wananchi wote tushirikiane, tushikamane, yeyote mwenye taarifa kwa mashine hizi zipo katika, vijiji, katika kata zetu watoe taarifa mapema na tutakuja kuziondosha ili sasa tudhibiti hao watu ambao wanakwepa kulipa kodi yetu ya serikali, kwasababu wanavyoendesha hizi maana yake wanakwepa kodi za serikali na mapato ya serikali yanapotea bure",alisema Mboneko.

"Tutaendelea kuzikamata na tutaendelea kuhakikisha kwamba hawakai tena katika Wilaya yetu ya Shinyanga",alisema.

Amesema kuwa michezo hiyo inasababisha mmomonyoko wa maadili kwa sababu watoto wanaiba kwa wazazi wao, na hata wananchi wengine pia wanapoteza mali zao kwani wanauza mpaka mashamba na chakula kwaajili ya kwenda kucheza michezo hiyo jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akielezea kuhusiana na kukamatwa kwa mashine hizo.
Mashine zinazotumika katika michezo ya kubahatisha zilizokamatwa katika maeneo mbalimbali mkoani Shinyanga Mashine hizo zikiwa katika kituo cha polisi kabla ya kwenda kuteketezwa kwa moto.
Mashine zikipandishwa kwenye gari kwaajili ya kwenda kuteketezwa.
Meneja Ukaguzi na Udhibiti kutoka bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania Sadiki Elimsu akielezea kuhusu mashine zilizoteketezwa kwa moto.
Mashine hizo zikiwa zinawaka moto

Picha zote na Kareny Masasy - Malunde1 blog
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger