Thursday, 22 August 2019

LAAC Yaiagiza Ofisi ya CAG Kufanya Ukaguzi Nyang’hwale Ndani Ya Miezi 3 Baada Ya Kubainika Ubadhilifu Wa Zaidi Ya Tsh.bilioni 3.

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Kamati ya Bunge ya  kudumu ya Hesabu za serikali za Mitaa [LAAC]imeipa   muda wa  miezi 3 ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali [C.AG] Kwenda kufanya ukaguzi Maalum katika halmashauri ya  wilaya ya Nyang’wale mkoani Geita baada Ya Kubainika Ubadhilifu wa zaidi ya Tsh.Bilioni 3.
Akizungumza  Mbele ya kamati hiyo leo  Agosti 22,2019  Bungeni Jiji Dodoma  ,iliyokutanisha  watumishi wa halmshauri ya  Nyang’hwale,watumishi  wa CAG ,Makamu Mwenyekiti wa LAAC , Abdallah Chikota amesema ofisi ya CAG imetoa hati mbaya kwa halmashauri  hiyo . 

Mhe.Chikota amesema katika halmashauri ya Wilaya Ya Nyang’hwale amesema baada ya ofisi ya CAG Kufanya ukaguzi wa ndani katika halmashauri hiyo kuna upotevu wa Zaidi ya Tsh.Bilioni 3,vitabu 50 vya ukusanyaji mapato havikuwasilishwa Kwa Mkaguzi  wa CAG,Kuna hati za Malipo [Voucher] zenye thamani ya Tsh.Bilioni 1,milioni 49, laki 1,40 elfu na 91  pamoja na uhamisho wa fedha Bilioni 1 na milioni 700 bila kuonesha shughuli zinakokwenda. 

Aidha Makamu Mwenyekiti huyo wa kamati amefafanua kuwa kuna zaidi ya Tsh.Milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya hazipo na kituo cha Afya hakijajengwa  huku kukiwa na Fedha za P4R  kwa Shule za Sekondari  Milioni  576 zikitumiwa nje ya Malengo yaliyokusudiwa ,Mradi wa Maji kulikuwa na salio la Tsh.Milioni 74.1 lakini benki inaonesha milioni 71.1 haipo  na hati za malipo kwenye mradi wa Maji  zenye thamani ya Tsh. Milioni  134.5 hazikuwasilishwa kwa wakaguzi. 

Naibu  Waziri wa TAMISEMI Mwita Waitara amesema jambo la ubadhilifu huo wao kama serikali limewafedhehesha sana huku akitoa wito kwa watendaji wapya kuwa waaminifu katika kuwahudumia Watanzania . 

Naye katibu tawala Mkoa Wa Geita Denis  Bandisa amesema ukaguzi  maalum wa CAG utaenda kuonesha utendaji kazi kwa halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale hata kwa viongozi wa sasa huku akibainisha kuwa wapo tayari kuipokea kamati ya CAG Kufanya ukaguzi huo.


Share:

MWANAMKE ATANGAZA KUOLEWA NA WANAUME WATATU ...."ATAISHI NAO NYUMBA MOJA'


Toyin Lawani

Mwanamitindo na staa wa ubunifu wa mavazi na mfanyabiashara nchini Nigeria Toyin Lawani (37), ametangaza kutaka kuoelewa na Wanaume watatu atakapofikisha miaka 40.

Toyin Lawani ametangaza hivyo kupitia Insta Stori ya mtandao wa kijamii wa Instagram, kuwa yupo tayari kuwajengea nyumba na kuishi nao wote wa watatu kwa pamoja.

Toyin Lawani ameandika kuwa "Kwanini Wanaume wanaruhusiwa kuoa Wanawake watatu na zaidi, mimi nitakapofikisha miaka 40, nitaolewa na wanaume watatu tofauti kwa pesa zangu mwenyewe, nitajenga nyumba kubwa na kuishi nao ila nitakuwa nachagua kila Mwanaume mmoja wa kulala naye kwa kila usiku mmoja".

Pia ameendelea kuandika, ''wanaume wanaaminishwa kuoa wanawake wengi, kwanini wanawake washindwe na sasa hivi dunia imebadilika na wanawake wanatakiwa waheshimiwe''.

Mwisho kabisa ameandika kuwa Wanawake hawawezi kupata ujauzito bila Wanaume, ila wana uwezo wa kununua mbegu za uzazi, mwanamke anabeba mimba kwa miezi 9, miaka miwili ya kumlea mtoto, Mwanaume hawezi kumpa mtoto zawadi wala hajali ila anaweza kukusaliti.







Share:

Serikali Kutumia Wataalam wa Ndani Kutekeleza Miradi ya Maji

Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema Serikali imedhamiria kutumia zaidi wataalam wake wa ndani katika utekelezaji wa ujenzi wa miradi ya maji baada ya mafanikio makubwa yaliyopatikana kwa kazi walizopewa.

Amesema maamuzi hayo yamekuja baada ya wataalam hao kufanya kazi nzuri, zinazochukua muda mfupi kukamilika, zenye viwango na kwa gharama nafuu ukilinganisha na wakandarasi ambao kazi zao zimekuwa na changamoto mbalimbali zinazokwamisha juhudi za Serikali kumaliza tatizo la maji.

Naibu Waziri Aweso amesema kwa muda mrefu Serikali imekuwa na changamoto kubwa katika utekelezaji wa miradi ya maji nchini kutokana na ubabaishaji wa wakandarasi licha ya kutumia fedha nyingi kwa dhumuni la kufikisha huduma ya maji kwa kila mwananchi.

‘‘Tumekuwa na utaratibu wa kuwapa kazi Wataalam Washauri ya usimamizi wa ujenzi wa miradi kwa gharama kubwa, lakini wamekuwa wakishirikiana na wakandarasi kuihujumu Serikali kwa kutotimiza wajibu wao na kuingizia Serikali hasara kubwa’’, Naibu Waziri Aweso amefafanua.

‘‘Baada ya kugundua tatizo hilo tukaamua kutumia wataalam wa ndani waliopo kwenye mamlaka za maji, wahandisi wa mikoa na wilaya kwenye miradi mingi iliyokuwa imekwama au ujenzi wa miradi mipya kwa gharama ndogo na kupata mafanikio makubwa, Aweso ameeleza.

Akieleza kuwa baadhi miradi mingi iliyosimamiwa au kutekelezwa na wataalam wa ndani katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Kigoma, Mbeya na Kanda ya Ziwa imekuwa na mafanikio makubwa, jambo ambalo limeifanya Serikali kudhamiria kutumia zaidi wataalam hao na kuachana na wakandarasi wababaishaji kwa lengo la kupata matokeo mazuri.

Awali, Naibu Waziri Aweso alichukua hatua ya kumkamata Mkandarasi wa Kampuni ya Mbeso Construction Ltd kwa sababu ya kusuasua kwa ujenzi wa miradi ya maji ya Munge na Tella Mande iiliyopo katika Wilaya za Siha na Moshi, mkoani Kilimanjaro bila sababu za msingi.

Hatua hiyo imekuja baada ya Aweso kukagua Mradi wa Maji wa Munge, wilayani Siha na kutoridhiswa na kasi ya mkandarasi na muda wa utekelezaji wake ukiwa umebaki mwezi mmoja na kazi ikiwa ni asilimia 25 hali akiwa hana madai yoyote ya fedha kwa Serikali.


Share:

Ndikilo: Tanzania Ni Salama Kwa Uwekezaji,hususani Mkoani Pwani

NA MWAMVUA MWINYI,MKURANGA
MKUU wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo ,amesisitiza kwamba ,Tanzania hususan mkoani Pwani ni salama kwa uwekezaji na amekemea propaganda na uvumi unaoenezwa na baadhi ya watu wasiolitakia mema Taifa kuwa hakuna uwekezaji unaoendelezwa.

Aidha amewaasa ,wawekezaji na wenye viwanda kuhakikisha wanasajili namba za utambulisho ya mlipa kodi (TIN no) kwa meneja wa mamlaka ya mapato (TRA )mkoani hapo ili hali kuongeza pato la mkoa.

Ndikilo alitoa rai hiyo, wakati alipokwenda kuweka mawe ya msingi katika viwanda vitano vilivyopo wilayani Mkuranga.

“Rais dkt.John Magufuli amekuwa akisisitiza uwekezaji na ujenzi wa viwanda kuelekea uchumi wa kati, sasa akitokea mtu kukwamisha jitihada hizo anakuwa halitakii mema Taifa, Pia mkoa wetu kupitia halmashauri umetenga maeneo hekta 22,937 kwa ajili ya uwekezaji ,nawaomba wawekezaji waje kuwekeza .”alifafanua Ndikilo.

Hata hivyo, mkuu huyo wa mkoa aliwataka wenye viwanda kujali mikataba,haki,maslahi ya wafanyakazi kwa kuzingatia sheria pamoja na kuwapa likizo na kuwawekea vitendea kazi .
Awali mkurugenzi wa kiwanda kinachozalisha matofali yenye ubora (Shaffa Ltd) kitongoji cha Kiguza, Suleiman Amour alibainisha ,ujenzi wa kiwanda umeanza 2018 kinatarajia kitakamilika mwaka 2019.

Amour alisema, lengo la mradi huo ni kuongeza wigo katika sekta ya ujenzi ,na ujenzi utagharimu sh.bilioni 15.3 hadi kukamilika ambapo itatoa ajira 200 mradi ukikamilika.

Kwa upande wake, msimamizi usafirishaji wa kiwanda cha super meals (Cool Blue) kilichopo Vianzi, Charles Malini alisema, ujenzi wa kiwanda umegharimu bilioni 2.7, kuna ajira 50 ,kinalisha maji ya kunywa ya chupa kwa matumizi ya majumbani na ofisini ambapo wanazalisha ujazo mbalimbali kuanzia nusu lita hadi lita 18.

Alitaja changamoto zinazowakabili ni kukosa umeme wa uhakika na miundombinu ya barabara isiyo rafiki .

Ndikilo alizungumzia tatizo la barabara na kuwaeleza ,ataangalia namna ya kuingiza hoja hiyo katika kikao cha barabara kijacho ili kiweze kutetea ipandishwe hadhi ihudumiwe na Tanroads.

Meneja wa shirika la umeme-TANESCO wilayani Mkuranga, Octavian Mmuni alisema tatizo la kukosekana umeme wa uhakika hutokana na maboresho yanayofanyika mara kwa mara.

Mmuni alieleza, kwa sasa shirika hilo limetenga sh.milioni 261 ili kusaidia kubadili nguzo na nyaya chakavu.

Viwanda vingine vilivyowekwa mawe ya msingi  katika wilaya hiyo ,ni kiwanda kinachozalisha zana za uvuvi Taxtrade T2 Ltd ,cha nyaya za umeme -Plug Ltd na kiwanda cha kutengeneza masufulia cha Maxima.


Share:

Taarifa ya TCU Kuhusu Waombaji Vyuo Vikuu 2019/2020 Waliochaguli Zaidi ya Chuo Kimoja




Share:

Job opportunities at Tanzania Civil Aviation Authority (TCAA),

On behalf of Tanzania Civil Aviation Authority (TCAA), President’s Office Public Service Recruitment Secretariat invites competent, experienced, highly organized and self-motivated Tanzanians to fill 8 vacant posts mentioned below;-

The post Job opportunities at Tanzania Civil Aviation Authority (TCAA), appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Picha : BLOGGERS WAJENGEWA UWEZO KUHUSU KANUNI NA MAADILI YA UANDISHI WA HABARI

Waandishi wa habari wanao andika habari kupitia mitandao ya kijamii (Alternative Media) inayohusisha Runinga za Mtandaoni 'Online Tv' na Blogu 'Blogs' wamejengewa uwezo kuhusu Kanuni za Maadili (Ethical Reportage ‘Code Of Ethics’) ili waweze kuandika kwa ufasaha na usahihi zaidi kuhusu habari zinazohusu ukiukwaji wa haki za binadamu,utawala bora na demokrasia.

Mafunzo hayo ya siku mbili yanayofanyika Agosti 22,2019 na Agosti 23,2019 jijini Dodoma ni sehemu ya utekelezaji wa  utekelezaji wa Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA) kupitia vyombo vya habari mbadala (Alternative Media) una Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) kupitia ya Klabu Waandishi wa Habari mkoani Arusha (APC) kwa ufadhili wa Mfuko wa Maendeleo wa Watu wa Marekani kupitia taasisi za Freedom House pamoja na PACT.
Mwezeshaji wa Mafunzo ya Kanuni na maadili ya uandishi wa habari,Allan Lawa akitoa mada kuhusu maadili ya uandishi wa habari na kuwasisitiza waandishi wa habari mtandaoni kuandika habari bila uoga kwa kuzingatia ukweli na uhakika kwa kuzingatia misingi ya uandishi wa habari. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mwezeshaji wa Mafunzo ya Kanuni na maadili ya uandishi wa habari,Allan Lawa akitoa mada kuhusu maadili ya uandishi wa habari


Share:

Yoweri Museveni na Paul Kagame wasaini makubaliano kumaliza mgogoro baina yao

Marais  Yoweri Museveni wa Uganda na Paul Kagame wa Rwanda wamesaini makubaliano ya amani katika mji mkuu wa Angola, Luanda, kumaliza uhasama uliopo kati ya mataifa hayo jirani.

Walifikia makubaliano hayo katika mkutano huo wa pili mbele ya marais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Angola na  Congo Brazzaville waliokuwa wapatanishi katika mgogoro huo.

Joto la kisiasa limekuwepo tangu mwanzoni mwa mwaka huu na limeathiri maisha ya watu kijamii na kiuchumi katika mataifa hayo jirani.

Maofisa nchini Rwanda wameishutumu Uganda kwa kuwafunga na kuwatesa kinyume cha sheria raia wake nchini Uganda, wakati Uganda nayo inaishutumu Rwanda kutekeleza ujasusi katika ardhi yake.



Share:

video: Harmonize Kaandika Barua ya Kuomba Kuvunja Mkataba na Kundi la Diamond la WCB

Meneja wa kundi la Wasafi,  Sallam amesema msanii Harmonize  kwa sasa ndani ya moyo wake hayuko WCB, isipokuwa tu yupo kimakaratasi na tayari ameshaandika barua ya komba  kuvunja mkataba na kundi hilo.

Akizungumza na Wasafi TV, Sallam amesema hata katika tamasha la Wasafi lililofanyika mjini Mwanza, Harmonize alitumia usafiri binafs na  kufanya baadhi ya mambo yaliyotoa tafsiri kuwa ameshajitenga na WCB.

“Hili jambo si sawa kulingana na maudhui ya tamasha hilo. Maudhui ya Wasafi Festival ni umoja. Msanii akiamua kuacha kuambatana na wasanii wenzake ambao wapo pamoja katika tamasha ni kwenda kinyume.

“Sisi katika tamasha letu hatupendi kutengeneza matabaka, tumeamua kuwa kitu kimoja, siyo kwamba Diamond, Rayvany hawakuwa na uwezo wa kutumia usafiri wao binafsi kama alivyofanya Harmonize” amesema Sallam na kuongeza;
 
“Harmonize ameshatuma barua ya maombi Wasafi kuvunja mkataba wake na yupo tayari kufuata sheria zote.

“Sisi tumependezwa na hatua yake kwa sababu labda kuna vitu ameona akivifanya atafika mbali.

==>>Msikilize Hapo Chini


Share:

Waziri Jafo Atoa Maagizo Kwa Wakuu Wa Mikoa Na Makatibu Tawala Mikoa Kote Nchini Kusimamia Vyema Mpango Kazi Wa Taifa wa Uendelezaji Miji Tanzania.

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Waziri wa nchi,Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Seleman Jafo ametoa agizo kwa Wakuu wa Mikoa,na Makatibu tawala wa Mikoa kote nchini kuhakikisha wanasimamia vyema mpango kazi wa Taifa wa uendelezaji wa Miji ili kuepuka ukuaji wa Makazi Holela.
 
Waziri Jafo ametoa Maagizo hayo jijini Dodoma wakati wa Uzinduzi wa Mpango kazi wa wa Taifa wa  Maendeleo ya Miji Tanzania .
 
Waziri Jafo amesema suala la mpango kazi wa Maendeleo ya Miji Tanzania itakuwa ajenda ya Kitalii na itakuwa na faida kubwa ikiwa ni pamoja na urahisi wa huduma za kijamii ikiwa ni pamoja na kupitikika kwa maeneo kwani amesema kuna baadhi ya Mitaa haipitikiki kutokana na Makazi holela  hali ambayo husababisha hata magari ya zimamoto kushindwa kutoa huduma vizuri.
 
“Unakuta nyumba zimekaa kiholela hata gari la zimamoto linashindwa kutoa huduma vizuri na hali ambayo inasababisha kuteketea kwa watu pamoja na mali,maeneo mengine ni ya kusikitisha sana hata kupitisha jeneza ni shida ,Bila shaka kuna Vijana wengine hapa wana Magari Mazuri lakini wanayaengesha nyumba ya ng’ambo kwa jirani  kisa hapapitiki”Alisema 
 
Hivyo Waziri Jafo amesema katika kuhakikisha mpango kazi wa Maendeleo ya Miji Tanzania unafanyika bila vikwazo vyovyote ameagiza Wakuu wa Mikoa na Makatibu tawala wa Mikoa kote nchini kusimamia vyema ili kuleta ufanisi Mzuri katika utekelezaji wake.
 
Naibu Waziri wa Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula amesema  moja ya hatua ambayo Wizara imefanya ni pamoja na kupitia Sera ya Makazi  ya Taifa ya mwaka 2000 na kupanga  sera Mpya ya Nyumba lengo likiwa ni kupunguza Umasikini na Kukuza Uchumi pamoja na Kuboresha huduma za kijamii.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi [ESRF]Dkt.Tausi Kida amesema Mnamo Agosti ,2017 Serikali ya Tanzania iliungana na Taasisi hiyo kuanzisha Maabara ya ukuaji wa Miji Tanzania kwa lengo la kusaidia serikali katika uchambuzi mbalimbali wa ukuaji miji huku Naibu katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw.Adolf Ndunguru akishukuru ushiriki wa Taasisi hizo.


Share:

Korea Kaskazini yapuuza mazungumzo ya nyuklia na Marekani

Korea Kaskazini imesema haioni manufaa ya majadiliano hadi Marekani isitishe kile ilichokiita hatua za uhasama za kijeshi, wakati mjumbe wa Marekani akizuru Korea Kusini kwa jicho la kufufua mazungumzo ya nyuklia na Pyongyang. 

Mazungumzo kati ya Pyongyang na Washington yamekwama, tangu mkutano wa pili wa kilele kati ya rais wa Marekani Donald Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un mjini Hanoi Februari, ulipovunjika bila makubaliano. 

Wawili hao walikutana tena mwezi Juni katika ukanda wa amani kati ya Korea mbili na kukubaliana kuanzisha tena majadliano ya ngazi ya kikazi, lakini mazungumzo hayo bado kuanza. 

Wakati huohuo, Korea Kaskazini imefanya majaribio kadhaa ya makombora ya masafa mafupi katika wiki za karibuni, kupinga mazoezi ya  kijeshi ya kila mwaka kati ya Marekani na Korea Kusini, ambazo inaziona kama mazoezi ya kujiandaa na uvamizi. 

Stephen Biegum, mjumbe maalumu wa Marekani kwa ajili ya Korea Kaskazini, anaeongoza mazunguzo ya kikazi, aliwasili Seoul Jumanne jioni kwa ziara ya siku tatu, na alisema Washington itakuwa tayari kushiriki mazungumzo mara itakaposikia kutoka Pyongyang.


Share:

Kenya yashinda kura ya Afrika kutafuta kuwa mjumbe asiye wa kudumu kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

Kenya imeishinda Djibouti na kupata kura ya Umoja wa Afrika ambayo inatarajiwa kuongeza chachu ya kampeni ya nchi hiyo kuwa mjumbe asiye wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo imesema, Kenya imepata kura 37 dhidi ya 13 za Djibouti wakati wa uchaguzi ulioandaliwa na Kamati ya Kudumu ya Wawakilishi ya Umoja wa Afrika uliofanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Kenya inatarajiwa kuungana na Niger na Tunisia ambazo zilichaguliwa mwezi June kuwa wajumbe wasio wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ameupongeza Umoja wa Afrika kwa kuidhinisha nia ya Kenya ya kuwa na nafasi kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na kuzitaka nchi nyingine wanachama wa Umoja huo kuunga mkono kenya kupata nafasi hiyo.


Share:

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina AIVUNJA Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Maziwa Tanzani

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina, ametangaza kuivunja Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Maziwa Tanzania, kuanzia leo August 22, 2019 kutokana na kutoridhishwa na utendaji wa kazi zao.



Share:

UWT,KAMATI YA SIASA CCM WAFANYA ZIARA KUKAGUA ILANI YA UCHAGUZI WILAYA YA GEITA

KAIMU katibu wa Umoja wa Wanawake(UWT) wilaya ya Geita Angela Simwanza amefanya ziara na kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Geita kukagua utekelezaji wa Ilani ya chama hicho. 

Ujumbe huo umetembelea miradi mbalimbali katika kata ya kata ya Nyarwanzaja ikiwemo ujenzi wa ghorofa katika shule ya sekondari ya Nyarwanzaja.

Akizungumka katika ziara hiyo katibu Angela amemshukuru Rais dkt John Magufuli kwa jitihada anazozifanya za utekelezaji wa ilani.

"Rais wetu anafanya kazi kubwa sana ya kutuletea maendeleo, anatekeleza Ilani ya chama chetu na ametoa miradi ya CSR hivyo tuna kila sababu ya kueleza mafanikio haya ili watu wajue, "alisema katibu Angela. 

Amewashukuru wabunge na madiwani kwa usimamizi mzuri wa miradi inayotekelezwa.

Share:

HAYA HAPA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA VYUO VIKUU TANZANIA

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMIS AGOSTI 22,2019




Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger