Wednesday, 21 August 2019

MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA SHINYANGA ATAKIWA KUSHIRIKIANA NA WANANCHI KUJENGA VYUMBA VYA MADARASA

Mkurugenzi wa halmashauri ya Shinyanga ametakiwa kushirikiana na wananchi ili kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya Msingi Shikizi ya Iyogelo iliyopo katika kata ya Lyamidati halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ili kuwasaidi watoto kusoma katika shule hiyo.

Agizo hilo limetolewa leo Agosti 21, 2019 na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack alipokuwa akizungumza na wananchi waliojitokeza katika ukaguzi wa vyumba vya madarasa ya shule hiyo, na kusema kuwa fedha iliyopatikana kutokana na mauzo ya pamba itumike kumalizia shule hiyo.

"Nimuombe Mkurugenzi kwa sababu yupo, safari hii tumeuza Pamba na tumepata fedha kutokana na ushuru wa pamba, angalia namna bora ya kukamilisha ujenzi huu ukishirikiana na wananchi", amesema Telack.

Pia ametaka eneo hilo la shule liwekewe mipaka ili lisije likavamiwa na watu na kusababisha migogoro.

"Kijiji kimetoa eneo ni vizuri tukahakikisha kwamba tunaweka mipaka ili tusirudi nyuma na kugombana na wananchi waliotoa ardhi hii kwamba sasa wanavamia eneo lao la shule", amesema Telack.

Kwa upande wake Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewapongeza wananchi kwa jitihada zao za kuchangishana na kujenga shule hiyo.

"Kazi waliyoifanya ya kuchangishana na kuweza kusimamisha majengo haya na baadae kusaidiwa na taasisi nyingine kumalizia, ni jambo la kijasiri sana na ni mwamko mzuri wa kujua faida ya elimu kwa watoto wenu",amesema Balozi Iddi.

"Naomba juhudi hizi ziendelee ili watoto wenu hapa waweze kusoma na hasa hasa watoto wadogo",ameongeza Balozi Iddi.

Aidha ameitaka halmashauri hiyo ijitahidi kumalizia sehemu iliyobaki ya shule hiyo ili watoto waweze kusoma hapo.

Pia amewasisitiza wanafunzi wote katika kata ya Lyamidati kusoma kwa bidii ili itoe wasomi watakaolisaidia taifa hapo baadaye.

"Sio kwasababu mnaitwa Shinyanga Vijijini basi muone hamna uwezo wa kutoa wasomi, tunataka Lyamidati itoe mainjinia, mawaziri na hata marubani, kwanini isiwezekane? Kwani hawa walioweza walifanya kitu gani? Na wao walisoma kama mnavyosoma ninyi",amesema Balozi Iddi.

Katika hatua nyingine ametoa shilingi Milioni 1 kwa ajili ya kuchangia ukamilishaji wa ujenzi wa shule hiyo Shikizi ya Iyogelo.

Awali akitoa taarifa fupi ya ujenzi wa shule hiyo Mwalimu Mkuu wa shule hiyo amesema kwamba zinahitajika shilingi Milioni 25 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo.

Shule hiyo Shikizi ya Iyogelo iliyopo kata ya Lyamidati halmashauri ya wilaya ya Shinyanga imejengwa kwa ushirikiano wa michango ya wananchi, serikali ya Tanzania na serikali ya Uingereza kupitia (UKAID) kupitia mradi wa EQUIP Tanzania na ipo chini ya usimamizi wa shule mama ya Ihugi.

Shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 41 wasichana 18 na wavulana 23 na inachukua wanafunzi wa darasa la wali hadi darasa la pili.

Kabla ya kujengwa shule hiyo watoto wa kijiji cha Iyogelo walikuwa wakitembea umbali mrefu wa takribani kilomita tano mpaka kufika shule ya Msingi Ihugi kwa ajili ya masomo, na kukamilika kwa ujenzi wa shule hiyo ya Iyogelo itawasaidia watoto wadogo kupata elimu katika mazingira mazuri na kutotembea umbali mrefu kwenda shuleni.
Na Annastazia Paul - Malunde1 blog
Share:

RAIS WA VENEZUELA ASEMA YUPO KWENYE MAZUNGUMZO NA DONALD TRUMP

Raisi wa Venezuela Nicolás Maduro amesema yupo kwenye mazungumzo na utawala wa raisi Donald Trump kwa miezi kadhaa sasa - licha ya vikwazo vipya vya Marekani kwa taifa hilo.

Mgogoro unaoedelea wa kisiasa na kiuchumi umeianya Venezuela kuwa na marais wawili waliojitangazia uhalali wa kuongoza.

Marekani ni moja ya mataifa 50 ambayo hayamtambui Maduro kama raisi halali wa Venezuela.

Utawala wa Washington ulitangaza vikwazo vipya dhidi ya Venezuela mwanzoni mwa mwezi kama njia ya kumuongezea Maduro shinikizo la kung'atuka.

Hata hivyo jana Jumanne, Maduro amethibitisha kuwa amekuwa kwenye mazungumzo na maafisa waandamizi wa serikali ya Trump kwa miezi kadhaa sasa.

Akizungumza kupitia runinga, Maduro amesema: "Kama nilivyofanya mazungumzo ndani ya Venezuela, pia nimetafuta namna ya kumfanya raisi Trump aisikilize Venezuela."

Raisi Trump pia amethibitisha kuwa utawala wake umekuwa kwenye "mazungumzo na wawakilishi wa Venezuela".

"Sitaki kusema nani, lakini tunazungumza na watu wa ngazi ya juu kabisa," amesema Trump.
Share:

BUNGE LA UGANDA LAPITISHA SHERIA YA KUPINGA ADHABU YA KIFO 'KUNYONGWA'

Bunge la Uganda limepitisha sheria inayopinga hukumu ya adhabu ya kifo kwa baadhi ya uhalifu, na kufanya marekebisho katika sheria nne tofauti ikiwemo sheria ya kupambana na ugaidi.


Kama sheria hiyo itasainiwa na rais Yoweri Museveni , marekebisho hayo yatasitisha hukumu ya kifo kwa uhalifu mkubwa zaidi, kwa maelekezo ya jaji.

Watunga sheria wanasema kuwa hii ni hatua kubwa inayoweza kutokomeza hukumu hiyo, jambo ambalo mahakama iliwahi kupigia kelele.

Kuna wafungwa 133 ambao wamehukumiwa kunyongwa lakini sasa imepita miaka 20 tangu wahukumiwe.

Kumekuwa na kampeni mbalimali za kutokomeza hukumu hilo, kufuatia hukumu ya mwaka 2009 ya mfungwa Susan Kigula ambaye alihoji juu ya hukumu ya kifo kuwa kinyume na katiba.

Mahakama baadae ilitaka hukumu ya kifo isiwe lazima kwa kesi za mauaji, na kuwasisitiza watu kuwa mtu hapaswi kuwekwa jela kwa miaka mitatu wakati amehukumiwa kunyongwa muda huo ukipita mfungwa huyo ni sawa kuwa amepewa hukumu ya kifungo cha maisha.
Via BBC
Share:

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Ampongeza Rais Magufuli Kwa Uwekezaji Mkubwa Alioufanya Katika Sekta ya Afya

Na.Catherine Sungura, WAMJW-Dodoma
KATIBU Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa uwekezaji mkubwa aliouweka katika sekta ya afya nchini.

Dkt. Chaula ameyasema hayo jana wakati wa mahojiano na kituo cha runinga cha Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1) wakati wa taarifa ya habari baada ya Mhe. Rais kutembelea Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali iliyopo jijini Dar es Salaam.

Katika mahojiano hayo Dkt. Chaula alisema kuwa Serikali ya awamu ya tano sio kwamba imewekeza tu kwa mamlaka ya maabara ya mkemia mkuu wa serikali bali katika sekta yote ya afya kwa kuboresha huduma za afya kwa upande wa miundombinu, dawa, vifaa na vifaa tiba katika hospitali pamoja na taasisi zake.

Kwa upande kwa mamlaka ya maabara ya mkemia mkuu wa serikali alisema kuwa serikali kupitia wizara ya afya imefanya jitihada kubwa za kusogeza huduma za mamlaka hiyo katika kanda zote nchini na hivi karibuni inatarajia kuwa na kanda nyingine jijini Dodoma.

“Sisi hapa kwa afrika mashariki, Tanzania tunaongoza kwa kuwa na mitambo ya uchunguzi ya kisasa vya kufanya utambuzi wa miili na tuna imani tutapokea hata vinasaba kutoka nchi za jirani pale panapotokea mkanganyiko hususani kwenye kesi za jinai,ajali,sumu,madawa ya kulevya pamoja na kemikali.

Dkt. Chaula alisema mitambo hiyo ya kisasa inatoa majibu ndani ya siku saba tofauti na zamani ambapo sampuli thelathini na tano zilichukua mwezi kuthibitisha ila kwa sasa wanachukua sampuli hadi mia mbili.

Hata hivyo katibu Mkuu huyo amewashauri watanzania kupenda na kujenga mazoea ya kutumia taasisi za serikali zilizopo nchini hususani mamlaka ya mkemia mkuu wa serikali pale panapotokea mkanganyiko kwa kisheria au utambuzi wa vinasaba mbalimbali.


Share:

Waziri wa Nishati Dr. Medard Kalemani Atoa Ufafanuzi kwa Kamati ya Bunge Kuhusu Uunganishwaji Umeme kwa Wateja wa Vijijini

Na Veronica Simba – Dodoma
WAZIRI wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ameieleza Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuwa idadi ya  wanaounganishiwa umeme vijijini kupitia miradi mbalimbali inayoendelea ni ya awali na itakuwa ikiongezeka kadri wananchi husika watakavyokuwa wakilipia gharama yake ambayo ni shilingi 27,000 tu.

Alieleza hayo jana, Agosti 20, 2019 jijini Dodoma, wakati akijibu hoja iliyoibuliwa na wajumbe kadhaa wa Kamati hiyo walioonesha wasiwasi wao kuwa idadi ya wananchi wanaounganishiwa umeme vijijini ni ndogo.

“Kinachofanyika hivi sasa ni kupeleka miundombinu ya umeme katika maeneo mbalimbali vijijini na kuunganisha wateja wa awali. Wengine wataendelea kuunganishwa kwa wakati wao kadri wanavyolipia,” alifafanua Waziri.

Aidha, kuhusu agizo la serikali kwa wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini, kutumia vifaa vya ndani ya nchi, Waziri ameieleza Kamati husika kuwa msimamo huo unatokana na matumizi ya vifaa vya ndani kuwa na tija zaidi kuliko vinavyoagizwa kutoka nje ya nchi.

Akifafanua, alieleza kuwa kuagiza vifaa nje ya nchi ni gharama kubwa ukilinganisha na kutumia vifaa vya ndani. Pia, alisema, ni rahisi zaidi kwa serikali kusimamia na kudhibiti ubora wa vifaa vya ndani kuliko vinavyotengenezwa nje ya nchi. Vilevile, aliongeza kuwa muda unaotumika kupata vifaa vinavyotengenezwa ndani ya nchi tangu siku vinapoagizwa ni mdogo kulinganisha na ule unaotumika kuagiza na kuletewa vifaa hivyo kutoka nje ya nchi.

Waziri pia alizungumzia katazo lililotolewa na serikali kuhusu wananchi vijijini kulipia nguzo ambapo alisema uamuzi huo ulifikiwa ili kuwapunguzia gharama wananchi hao ambao wengi kipato chao ni kidogo.

“Kwa uhalisia, umeme vijijini unatolewa bure kwa wananchi na gharama zake kuchukuliwa na serikali. Hata hiyo 27,000 wanayolipa ni gharama za ushuru wa thamani tu ambayo ni asilimia 18 ya gharama husika. Sasa ukimlipisha mwananchi huyo nguzo itarudisha tatizo palepale, hivyo nasisitiza tena kwamba wananchi wa vijijini hawatakiwi kulipia nguzo.”

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Amos Maganga, ameieleza Kamati hiyo kuwa, tangu kuanzishwa kwake, REA imetekeleza miradi mbalimbali ikiwemo Miradi ya Awali, Mradi wa Kupeleka Umeme Vijijini Awamu ya Kwanza (REA I), Awamu ya Pili (REA II) na Awamu ya Tatu (REA III).

Amesema kuwa kukamilika kwa miradi hiyo mwaka 2021, kutawezesha vijiji vyote 12,268 vya Tanzania Bara kufikiwa na miundombinu ya umeme.

Katika kikao hicho, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ilikuwa ikipokea taarifa ya maendeleo na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya REA pamoja na changamoto inazokabiliana nazo.

Wengine walioshiriki kikao hicho ni Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara, Haji Janabi pamoja na viongozi mbalimbali wa Wizara na Taasisi zilizo chini yake.


Share:

Naibu Waziri wa Afya: Wananchi Tuungane Pamoja Kupinga Ukatili wa Kijinsia

Na Anthony Ishengoma WAMJW
NAIBU Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amesema kuwa mtoto wa kike uzidi kukua kiuchumi kulingana na muda anaokaa shuleni akiongeza kuwa mwanamke anavyozidi kujiendeleza kielimu upunguza uwezekano wa kuwa na idadi kubwa ya watoto na na kufanyiwa vitendo vya kikatili.

Dkt. Ndugulile amesema hayo leo Jijini Dodoma wakati wa akiitambulisha Kampeni mpya ya Kitaifa ya kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto ijulikanayo kama Twende Pamoja inayolenga kushirikisha wanaume na wanawake kwa lengo la kutoa elimu kwa jamii kupitia mbinu anwai.

Aidha Dkt. Ndugulile amesisitiza kuwa kuwepo kwa elimu bure nchini kwa kiasi kikubwa kumepunguza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake ikiwemo mimba na ndoa za utotoni pamoja na uwepo wa Sheria inayotoa adhabu ya kifungo cha miaka 30 jela kwa anayebainika kufanya vitendo hivyo.

Dkt. Ndugulile ametaja wastani wa watoto kwa mwanamke wa Tanzania kuwa watano hivyo kadri msichana anavyokaa shuleni anapunguza uwezekano wa kuzaa watoto wengi lakini pia akasema uwezi ukalinganisha kipato cha Msichana wa kidato cha nne na yule wa Darasa la Saba.

Akizungumzia kuhusu kauli mbiu ya kampeni hiyo Dkt. Ndugulile ameviambia vyombo vya habari kuwa yeye kama Naibu Waziri anachukizwa na vitendo vya ukatili dhidi ya Wanawake hivyo akachukua fursa hiyo kuhamasisha pia wanaume wengine nchini kuchukia vitendo hivyo akiitaja kauli mbiu ya Kampeni hiyo kuwa ni ''Ukatili wa Kijinsia Tanzania sasa basi’’.

Akizungumzia hali ya ukatili wa kijinsia Nchini Dkt. Ndugulile amesema taarifa ya hali ya Uhalifu nchini ya Mwaka 2017 inaonesha kuwa jumla ya watu 41,416 waliofanyiwa ukatili wa kijinsia walitoa taarifa kwenye vituo vya polisi ikilinganishwa na watu 31,996 waliofanya hivyo mwaka 2016.

Dkt. Ndugulile ameyataja baadhi ya matukio ya ukatili yaliyotolewa taarifa kuwa ni ubakaji, vipigo, matusi, ulawiti, kutupa watoto, ukeketaji na kuwapa mimba wanafunzi na kuongeza kuwa kati ya mataukio hayo 41,416 yaliyotolewa taarifa mwaka 2017 matukio 27,703 sawa na asilimia 67 yalifanywa dhidi ya wanawake na watoto.

Dkt. Ndugulile ameongeza kuwa asilimia 40 ya wanawake wa umri kati ya miaka 15-49 wamefanyiwa ukatili wa kimwili au kingono mara moja au zaidi katika kipindi hicho cha maisha wakati wanawake asilimia 20 wenye umri miaka 15-49 wamefanyiwa ukatili wa kimwili katika kipindi cha miezi 12 iliyopita.

Dkt. Ndugulile amefafanua kuwa Wizara ianshirikiana na wasanii katika kufikisha ujumbe na amemtaja Msanii Nurdin Bilal Maarufu SHETTA kuwa amejitolea kuwa Balozi wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto na atataumia jukwaa la Sanaa kuelimisha jamii kwa kutumia mziki wake na mitandao ya kijamii.

''Ni matarajio yangu kwamba kampeni hii ya Kupinga Ukatilili wa Kijinsia Kitaifa italeta mabadiliko makubwa kupitia jumbe mbalimbali zilizoandaliwa kupitia muziki, machapisho, nyimbo, shuhuda na Semina zitakazokuwa zinaendelea kutolewa kwenye majukwaa mbalimbali kipindi cha kampeni’’. Alihitimisha Dkt. Ndugulile.


Share:

Ufahamu Ugonjwa Wa Ngiri Na Tiba Yake

Tatizo la Ngiri Linavyosababisha Upungufu wa Nguvu za Kiume na Maumbile Kusinyaa, Dalili zake Hizi Hapa..Makala
51 minutes ago

Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Dalili za Ngiri
Tumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume kulegea, kutokuwa na hamu ya kulundia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma.

Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;

Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.


Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.


Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.


Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.


Ugojwa huu wa ngiri unaweza kutibika

Mpate mpenzi wako unayempenda na kumfunga mume,mke mpenzi asitoke kwa mwingine .

Kwa Ushauri na Msaada wa Wasaliana na  0714006521


Share:

Umoja wa Mataifa (UN) Waipongeza Tanzania Kwa Matumizi Mazuri Ya Rasilimali

UMOJA wa Mataifa (UN) umeipongeza Serikali ya Tanzania kwa namna inavyotumia vizuri rasilimali zake za ndani na hivyo kuiwezesha kutekeleza shughuli mbalimbali za kimaendeleo sambamba na kupunguza utegemezi kutoka nje.

Pongezi hizo zimetolewa leo (Jumatano, Agosti 21, 2019) na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa, Bw. Alvaro Rodriguez alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, ofisini kwa Waziri Mkuu Magogoni jijini Dar es Salaam.

Mratibu huyo Mkazi wa Umoja wa Mataifa ambaye alikwenda kumuaga Waziri Mkuu, amesema kuwa Tanzania imeendelea kutumia vizuri mapato yake ya ndani kwa kuimarisha miundombinu na huduma za kijamii kama ujenzi wa hospitali na vituo vya afya.

“Katika kipindi changu cha miaka mitano ambacho nimefanya kazi Tanzania, nimeshuhudia mabadiliko makubwa ya kimaendeleo yanayofanywa na Serikali, ikiwemo kuimarika kwa mahusiano kati ya Serikali na Umoja wa Mataifa na taasisi zake nchini.”

Katika hatua nyingine, Bw. Rodriguez ameisifu Serikali ya Tanzania kwa namna ilivyoweza kuandaa na kuendesha vizuri mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika Agosti 17 na 18 mwaka huu.

Mbali na kuisifu Serikali pia kiongozi huyo amevipongeza vyombo vya habari kwa jinsi vilivyoshirikiana na Serikali kuripoti matukio mbalimbali ya mkutano huo. “Nawapongeza na wananchi kwa ushirikiano walioutoa kwa Serikali wakati wote wa mkutano wa SADC.”

Kwa upande wake, Waziri Mkuu amemshukuru kiongozi kwa pongezi alizozitoa ambazo ni ishara kwamba anatambua jitihada zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli katika kutumia vizuri rasimali zake.

Waziri Mkuu amesema “maelezo yaliyotolewa na Bw. Rodriguez yanaakisi kauli za Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwamba Tanzania si nchi masikini na inayo uwezo wa kutoa misaada kutokana na rasilimali nyingi ilizonazo. Watanzania waendelee kuiunga mkono Serikali yao.”

Pia, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kumpongeza kiongozi huyo kwani alikuwa kiungo kizuri kabaina ya Serikali ya Tanzania na Umoja wa Mataifa. Pia atakumbukwa sana kutokana na mambo mengi aliyoyafanya kipindi cha utumishi wake nchini Tanzania.

Awali, Waziri Mkuu alikutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Afrika Kusini, Mheshimiwa Balozi Thamasanqa Dennis Mseleku ambaye alikwenda kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kufanya kazi nchini Tanzania.

Waziri Mkuu alimpongeza Balozi huyo kwa ushirikiano na mchango alioutoa kwa Serikali ya Tanzania katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo zikiwemo za kiuchumi, elimu, afya, maendeleo ya jamii pamoja na kuimarisha uhusiano baina ya nchini mbili hizo.

Kwa upande wake, Mheshimiwa Balozi Mseleku ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano mkubwa uliompatia katika kipindi chake cha utumishi akiwa nchini na kwamba alitamani aendelee kubaki Tanzania.

(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,        
JUMATANO, AGOSTI 21, 2019.


Share:

Mkurugenzi ATCL Atoa Ufafanuzi Bombardier iliyoharibika

Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), limesema ndege aina Bombardier Q400 iliyokuwa katika matengenezo imeanza kufanya safari zake kama kawaida.

Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Ladslaus Matindi  leo Jumatano Agosti  21, 2019 katika kipindi cha Power Breakfast cha Redio Clouds  

Katika maelezo yake Matindi amesema ndege hiyo ilikuwa na hitilafu na ilitengenezwa kwa siku moja na tayari imerejea katika ratiba zake za safari za kila siku.

“Ndege inaweza kuharibika, kupata hitilafu au kuingiliwa na kitu kutoka nje muda wowote kwakuwa ni mashine hakuna namna ya kuzuia, hilo ni jambo la kawaida kwa mashine hata binadamu,” amesema Matindi.


Share:

Afrika Kusini yaipongeza SADC kwa kutangaza Kiswahili kuwa lugha rasmi ya nne

Bodi ya lugha ya kusini mwa Afrika (PanSALB) jana imepongeza azimio la Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) la kutangaza kuwa itaitumia Kiswahili kama lugha rasmi ya nne ya mawasiliano.

Mwenyekiti wa bodi hiyo Bw. David Maahlamela amesema, mafanikio hayo muhimu ya kutambuliwa na kuongezwa kwa lugha asilia ya Afrika katika kanda hiyo ni juhudi kubwa kwa kuhakikisha maendeleo, matumizi na taaluma ya lugha za urithi katika eneo hilo.

Maahlamela amesema, kwa hatua hiyo,  kwa sasa Kiswahili ndo kitakuwa  Lugha pekee na ya kwanza ya Asili kutumika ndani ya bara la Afrika kati ya taifa moja la jingine ambayo ni wanachama wa SADC.

Amesema, Afrika ndo bara pekee ambalo watoto huanza kufundishwa shuleni kwa lugha  za kigeni huku waafrika walio wengi wakipotoshwa  kuwa Lugha za Kigeni kama Kingereza, Kifarasa, Kireno ndo Muhimu zaidi kwa taifa  la Kiafrika kupiga hatua yoyote ya maendeleo


Share:

Zimbabwe Yapinga Tamko la Nchi za Ulaya....Yasema Kamwe haitaruhusu tishio la mapinduzi linalotolewa na upinzani

Serikali ya Zimbabwe imesema, haitaruhusu tishio lolote linalotolewa na upande wa upinzani la kupindua serikali, huku ikisisitiza kwamba raia wana haki ya kikatiba lakini hawapaswi kukiuka haki za wengine.


Tamko hilo la serikali limekuja baada ya Umoja wa Ulaya na nchi nyingine za magharibi zikiwemo Uingereza na Marekani kutoa taarifa ya pamoja hapo jana, ikiilaumu serikali ya Zimbabwe kwa madai ya kukiuka haki za binadamu wakati wa maandamano yaliyoongozwa na kundi la upinzani huko Harare tarehe 16 mwezi huu.


Share:

Aliyekuwa Makamu wa Rais Zimbambwe akimbilia mafichoni kukwepa kukamatwa

Makamu wa Rais wa zamani wa Zimbabwe ametangazwa na mamlaka nchini humo kama Mhalifu aliyekimbia.

Gazeti linalomilikiwa na serikali la Herald limesema kwamba Phelekezela Mphoko amekimbia kukamatwa na Kamisheni ya kupambana na rushwa nchini humo, ZACC.

Kiongozi huyo aliyekua madarakani mwaka 2014 hadi 2017 amekua akitafutwa ili kufunguliwa mashtaka ya matumizi mabaya ya ofisi pamoja na rushwa. 

Aliwahi pia kua balozi akiwakilisha Zimbabwe nchini Afrika ya Kusini, Botswana pamoja na Urusi

Wakili wa kiongozi huyo, Zibusiso Ncube alisema mteja wake alitoweka baada ya kuhofia kukamatwa na kuwekewa sumu.

Inaelezwa kuwa makamu huyo alikuwa sehemu ya kikundi ambacho kilitaka Neema ambaye ni mke wa Rais Mugabe afanikiwe badala ya Mnangagwa.


Share:

Waandamanaji wachoma jengo la Bunge

Maelfu ya Waandamanaji katika Jimbo la Indonesia  la Papua Magharibi jana wamechoma moto jengo la Bunge wakipinga kile wanachodai ni kukamatwa na kudhalilishwa kwa Wanafunzi.

Waandamanaji hao waliokuwa wakipinga vitendo hivyo vya udhalilishaji wanavyodai vinafanywa na vyombo vya dola dhidi ya Wanafunzi wa Papua, pia waliweka vizuizi barabarani.

Wanafunzi 43 katika maeneo ya Surabaya na Java Mashariki walikamatwa siku ya maadhimisho ya uhuru wa Indonesia baada ya bendera ya nchi hiyo kukutwa nje ya nyumba zao zikiwa zimeharibiwa.

Aidha, msemaji wa Polisi wa Java Mashariki, Frans Barung Mangera amesema kuwa wanafunzi hao waliachiwa huru baada ya kushikiliwa kwa saa kadhaa kutokana na kukosekana vithibitisho kuwa waliharibu bendera hizo.

Hata hivyo, waandamanaji walipatwa na hasira baada ya kusambaa kwa video katika mitandao ya kijamii ikiwaonyesha Polisi wakiwa na Wanajeshi wakiwaita Wanafunzi hao ‘Nyani’ na ‘Mbwa’

Gavana Msaidizi wa eneo hilo, Mohammad Lakotani amesema kuwa wakati mazungumzo yakiwa yanaendelea kati ya waandamanaji na Mamlaka, maandamano hayo yameharibu uchumi wa Papua Magharibi.


Share:

MBATIA ATUMIA JUBILEI YA MIAKA 25 YA KAKA YAKE KUSHAURI JAMBO SADEC

Askofu wa Jimbo la Katoliki la Same,Mhashamu Rogathe Kimario akiongoza ya misa takatifu ya Jubilei ya fedha ya miaka 25 ya Padri Thomas Salekio Kesyy iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Yohani Mtume ,Parokia ya Iwa-Kirua Vunjo mkoani Kilimanjaro.
Mbunge wa Jimbo la Vunjo ,James Mbatia alikuwa miongoni mwa waumini walioshiriki Ibada hiyo ,ambapo Padri Thomas Kessy ni kaka yake mkubwa .
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika Ibada ya Misa ya takatifu ya Jubilei ya fedha ya miaka 25 ya Padri Thomas Kessy .
Padri Thomas Kessy akizungumza wakati wa ibada hiyo.
Baadhi ya ndugu wa Padri Thomas Kessy wakishiriki ibada hiyo.
Mbunge wa jimbo la Vunjo ,James Mbatia akitoa hotuba yake wakati wa ibada ya Misa takatifu ya Jubilei ya fedha ya kaka yake Padri Thomas Kessy .
Askofu wa Jimbo la Katoliki la Same,Mhashamu Rogathe Kimario akimkabidhi Padri Thomas Kessy sululu na vitu vingine vilivyotolewa kanisani hapo kama kumuunga mkono.
Baada ya kumalizika kwa misa hiyo ,shughuli ilihamia nyumbani kwa familia hiyo eneo la Kirua Vunjo wilaya ya Moshi.
Padri Thomas Kessy akiwaongoza ndugu zake kufungua Champegne wakati wa hafala fupi ya pongezi kwa Padri Thomas Kessy kufikisha miaka 25 ya utume.
Mbunge wa jimbo la Vunjo,James Mbatia akiwawekea wageni waalikwa kinywaji cha Champegne wakati wa hafla hiyo
Padri Thams Kessy akikata ndafu katika hafla hiyo.
Padri Thomas Kessy akimlisha kipande cha ndafu  Askofu wa Jimbo la Katoliki la Same,Mhashamu Rogathe Kimario.
Baadhi ya wageni wakiwa katika hafla hiyo.
Wageni wakicheza muziki na Padri Thomas Kessy katika hafla hiyo hiy iliyofanyika nyumbani kwa familia ya Mbatia.

Na Dixon Busagaga .


MWENYEKITI wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) ambaye pia ni Mwenyekiti wa taifa wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, amewapa neno wakuu wa nchi 16 zinazounda Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), katika mkutano ujao kufikiria kuja na ajenda ya pamoja ya sera moja ya elimu inayofanana.

Mbatia amesema kuwa kama itakuwapo dhamira ya pamoja ya kuwa na sera hiyo ya elimu kwa wanachama wa SADC, kunaweza kubadili sura ya Afrika na mageuzi makubwa yakaonekana kwa miaka 20 yakisadifu mfumo wa elimu wa nchi za Ulaya.

Mbatia ametoa kauli hiyo mara  baada ya kumalizika kwa ibada ya misa takatifu ya Jubilee ya fedha ya miaka 25 ya Padri Thomas Salekio Kessy, iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Yohani Mtume, Parokia ya Iwa-Kirua Vunjo, mkoani Kilimanjaro.

Ibada hiyo iliongozwa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Same, Mhashamu Rogathe Kimario, akisaidiwa na Msimamizi wa Jimbo Katoliki la Moshi na Wakili wa Askofu, Deogratius Matiika.


“Kwa mfano, majuzi nilisikia na kusoma baadhi ya maandiko kwamba watu wa Namibia wao wanasema mfano mwanafunzi anayetoka Tanzania na amemaliza kidato cha sita na akienda kwao, kupata Chuo Kikuu kule ni shida, kwa sababu Namibia wao mfumo wao ni mgumu, wao elimu zao wanamalizia kidato cha nne. Unajiuliza hivi silabasi zetu zimeundwa namna gani, nawashauri wakuu wa nchi wanachama ni vizuri tukawa na sera moja ya SADC katika masuala ya elimu,”alisema

Mwaka huu, Tanzania imekuwa mwenyeji wa mkutano wa 39 wa SADC ikiwa imepita miaka 16, tangu mkutano kama huo kufanyika kwa mara ya mwisho mwaka 2003 chini ya utawala wa Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa.

Kuhusu Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika, kuweka mikakati ya kuziwezesha nchi wanachama kufikia malengo ya kuelekea kwenye ukuaji wa uchumi wa kati utakaokuwa maendeleo ya viwanda, Mbatia alisema:

“Mimi nina ushauri kwa SADC, pamoja na mambo ya viwanda na mambo mengine yote ambayo ni muhimu, wakuu wa nchi 16 wajitahidi sana kuhakikisha nguvu kazi ya SADC ambayo ni vijana, wanapata elimu ambayo ni ujuzi na wanaweza kuzalisha kwenye viwanda, wanaweza kuondoa masuala ya umasikini, njaa, watu wakawa na afya njema lakini penda tusipende ni lazima tuangalie je mifumo yetu ya elimu ikoje,”alieleza

Alisema malengo hayo yanatekelezeka, lakini sharti nchi wanachama wawe wamejiandaa vizuri na kwa utafiti alioufanya, bado kuna kazi kubwa mbele ya safari, na akashauri zaidi kuwa malengo hayo yasiwe ya maneno, yaende kwenye vitendo zaidi



Mwisho .


Share:

HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM) 2019/20

Share:

Waziri Jafo Atoa maagizo kwa Katibu Mkuu TAMISEMI

Waziri  wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo, amemwagiza Katibu Mkuu wa ofisi hiyo, Joseph Nyamhanga, kuwarejesha mara moja katika kituo cha kazi cha Ipogoro, Manispaa ya Iringa watumishi saba ambao walihamishwa hivi karibuni.

Jafo alitoa agizo hilo jijini Dodoma jana wakati akifungua mkutano wa mwaka wa waganga wakuu wa mikoa na halmashauri.

Alisema kumekuwa na uonevu wa kuwahamisha vituo vya kazi baadhi ya watumishi jambo ambalo linawafanya wapoteze morali ya kazi.

Aidha, Jafo alimwagiza  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk. Zainabu Chaula, kufuatilia kama mganga mkuu wa wilaya ameondolewa kazini kwa haki, kufanya makosa au kuonewa.

“Huyo mganga mkuu wa wilaya, alikuwa anafanya kazi yake kwa moyo, lakini hivi sasa ameondolewa kazini, sasa nataka ufuatilie je ameondolewa kwa makosa yake au nini kimetokea, fuatilia unipe majibu,”alisema.


Share:

TMDA yatoa ufafanuzi kuhusu Paracetamol aina ya P-500




Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger