Wednesday, 7 August 2019

WANAKIJIJI ZAIDI YA 200 WAUA MIFUGO NA KUICHOMA MOTO KAGERA



Katika hali isiyo ya kawaida na ya kuogofya, takribani wanakijiji zaidi ya 200 wa kijiji cha Kishanda B Wilaya ya Kyerwa Mkoani Kagera, wamevamia shamba la mwananchi mwenzao kisha kuikatakata migomba yote, kuchinja mifugo huku mbuzi wengine wakiwaua kwa kuwachoma na moto.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera Ahmed Msengi, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza vitu vilivyoharibiwa ni pamoja na mashamba ya migomba, kahawa na miti pamoja na kuwaua mbuzi wanne na kuwajeruhi mbuzi wawili, huku chanzo cha mgogoro huo ni umiliki ardhi kubwa, mgogoro ambao tayari ulishafika mahakamani.

Tukio hilo lilifanywa wakati mwenye shamba na mifugo iliyoharibiwa, Tryphone Jeremiah akiwa katika ibada kanisani na kudai kwamba wananchi hao takribani 200, walivamia mashamba na mifugo hiyo saa 6:00 mchana, baada ya kuwepo mgogoro wa ardhi baina ya baba yake na wanakijiji hao tangu mwaka 2007.

"Wananchi wanalalamika kuwa ninamiliki ardhi kubwa, baada ya wanakijiji hao kuvamia mashamba kwa makundi makundi, waliyafyeka kwa muda fupi na kuua mbuzi na kuwachoma moto pamoja na kubomoa nyumba," alidai Jeremiah.

Inaelezwa kuwa wananchi hao walitumia takribani masaa matatu kutekeleza unyama huo na kwa mujibu wa mlalamikaji (Jeremiah), anasema alikuwa na mbuzi 100, hivyo kati ya wale waliochinjwa na waliobaki hai wanaonekana 39 na mbuzi 57 hawaonekani kabisa.
Chanzo - EATV
Share:

BOSI WA JAMII FORUMS ATETEA UHURU WA FARAGHA 'DATA ZA WATEJA MTANDAONI'


Na Fortune Francis - Mwananchi 
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jamii Forums, Maxence Melo amedai sheria za kimataifa zinazoongoza mitandao zinataka wamiliki wa mitandao kuwa na sera ya faragha.

Melo na mwenzake Micke Wlliam wanakabiliwa na kesi namba 456 ya mwaka 2016 ya kuzuia Jeshi la polisi kufanya uchunguzi,

Akiongozwa na Wakili wa utetezi, Peter Kibatala jana Jumanne Agosti 6, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba, Melo alidai kulingana na Katiba ya Tanzania Ibara ya 18 inalinda faragha ya mtu.

Alidai barua ya Februari 2, 2016 iliyosainiwa na Benedict Alex iliandikwa kwa niaba ya Jamii Media Co. LTD ilikuwa na majibu kwa Jeshi la Polisi.

Melo alidai katika majibu ya barua hiyo walieleza wapo tayari kutoa ushirikiano iwapo wataeleza ni kifungu gani cha sheria wametumia kinachowapa mamlaka ya kutaka data za wateja.

"Tuliahidi kutoa ushirikiano mkubwa endapo wangeeleza ni kwa mujibu wa sheria gani," alidai

Akiendelea kujitetea Melo alidai Jamii Forums ni mtandao wa kijamii ulioanzishwa Machi 2006 mwanzoni ukiitwa Jambo Forums ambapo unatoa nafasi ya mtu yeyote kujisajili na kutoa maoni yoyote kwa jina lolote

Aliendelea kudai katika uamuzi wa Mahakama Kuu uliotolewa Machi 8, 2017 na Jaji Korosso na Wenzake (Kitusi na Alfani) ambayo ni hukumu ya Kesi ya Jamii Media dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) ilieleza sheria hiyo wanaitambua na ili mtu kutoa taarifa wanatakiwa kuomba kibali cha Mahakama kabla ya kufungua kesi.

"Tulifungua shauri hili Mahakama Kuu baada ya kupata barua nyingi mfululizo kutoka Polisi na (Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania) TCRA tukiiomba Mahakama isaidie kutafsiri barua hizo kwani tuliona haki ya faragha inaenda kuvunjwa," alieleza Melo

Melo aliiomba Mahakama ipokee hukumu hiyo kama kielelezo.

Hata hivyo, Wakili wa Serikali ya Tanzania, Sylvia Mitanto alipinga kupokelewa kwa kielelezo hicho kwa kuwa ni nakala na kuomba kupatiwa muda wa kutosha kwaajili ya kuipitia hukumu hiyo.

Hakimu Simba alieleza kesi hiyo itakapotajwa tena upande wa pili ulete majibu kuhusu pingamizi lililowekwa.

"Agosti 28 nitatoa uamuzi mdogo juu ya hili pingamizi na kuendelea na utetezi kesi yetu haitakiwi kuvuka Septemba 2019 kabla ya kutolewa hukumu," alieleza Hakimu Simba

Kesi hiyo iliahirishwa hadi Agosti 28 na 29,2019 kwa ajili ya uamuzi mdogo na kuendelea na ushahidi.

Kabla ya utetezi mashahidi wanne wa upande wa mashtaka wameshatoa ushahidi wao dhidi ya washtakiwa.

Katika kesi ya msingi, washtakiwa wanadaiwa kuzuia jeshi la Polisi kufanya uchunguzi, kinyume na Sheria Namba 22 (2) cha Sheria ya Makosa ya Mtandano Namba 14 ya mwaka 2015.

Washtakiwa hao wanadaiwa kutenda kosa hilo, kati ya Aprili Mosi, 2016 na Desemba 13, 2016 katika maeneo ya Mikocheni wilayani Kinondoni.
Share:

Kutana na Sheikh Omary Mwenye Uwezo wakufanya Dua mbalimbali za Matatizo Yako Na Kutafsiri Ndoto kwa kutumia Vitabu vya QUR-AN

Sheikh Omary Ni bigwa wa kutatua matatizo kwa haraka, ni mtu aliye jaliwa kubuli Shufaa pia anatoa Duah  za Ruhia. Ukija na Maradhi yanaondoka hapo hapo bila kungoja kesho,  UKIPEWA MKONO  na Sheikh Omary .
 
Wasiliana na Mtaalam Huyu Kwani yeye hufaulu Pale wote waliko Shindwa na Pia Humaliza kazi zilizo Shindikana ama Zilizo Achwa ndani ya Siku Moja 1.
 
Sheikh Omary ni Mtaalamu wa Nyota za Binadamu  Mwenye Uwezo wa Kubaini Tatizo lako tu Pindi Utakapo Fanya Mawasiliano Kupitia Wasaa Husika.
 
Je una NUKSI  zisizo kwisha.!? JE umekimbiwa na Mume/Mke na Anaishi na Mtu Mwingine..!? Muone Akutatulie,
 
Una kosa bahati ya wanaume au mume wa kukuoa..Unataka nyota ing'ae Au huna hamu na Mkeo/ Mumeo.
 
Jini mahaba. Kama Unakasirika ovyo ukiwa na bwana au mwanamke wako na  kumchukia Mpaka  kushindwa kufanya nae tendo la ndoa.
 
Njoo umuone Sheikh Omary  na ujuwe  yanayo kusibu.Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN

Mawasiliano: Sheikh Omary 0673531992. WhatsApp/Call
Tembelea Page ya @Mtabibu_Omar  @Mtabibu_Omar
Usome Makala Tofauti Tofauti Kama.


Share:

WANNE WAFARIKI DUNIA AJALINI WAKITOKA KUMZIKA MWENZAO


Watu wanne wamepoteza maisha na wawili kujeruhiwa baada ya  gari walilokuwa wakisafiria kuyumba nje ya barabarani kabla ya kugonga miti na kuingia kwenye bonde wakiwa njiani kurejea Nairobi baada ya kuhudhuria mazishi Eneobunge la Kiharu.


Ajali  hiyo imetokea Jumanne, Agosti 6,2019 katika eneo la Ithe Ruui kwenye Barabara ya Kenol-Murang’a nchini Kenya.

Inaelezwa kuwa watu hao  sita walikuwa njiani kurejea Nairobi baada ya kuhudhuria mazishi Eneobunge la Kiharu, wakati dereva alipopoteza mwelekeo wa gari hilo na kuyumba nje ya barabarani kabla ya kugonga miti na kuingia kwenye bonde. 

Kamanda wa Polisi Kaunti ya Murang’a Josphat Kinyua alisema wanne kati ya watu hao walifariki dunia mara baada ya ajali hiyo kutokea.

 Kwa mujibu wa Citizen Digital, wawili walionusurika walipelekwa katika Hospitali ya Maragwa wakiwa na majeraha mabaya. 

Ingawa chanzo cha ajali hiyo hakikujulikana mapema, wakazi katika eneo hilo walisema kwamba, eneo hilo linafahamika sana kwa ajali nyingi kaunti hiyo. 

Miezi miwili iliyopita, naibu chifu wa Nginda aliripotiwa kuaga dunia kufuatia ajali ya barabarani eneo hilo. 

Pia Waziri wa Maji wa Kaunti Water Paul Macharia, alihusika katika ajali ambayo ilimuua dereva wake kwenye barabara hiyo. 
Share:

Serikali Ya Tanzania Na Uganda Zashirikiana Kutekeleza Ujenzi Wa Mradi Wa Umeme Wa Maji Kikagati-murongo

Serikali za Tanzania na Uganda zinatekeleza ujenzi wa Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha kufua umeme wa maji wa Kikagati-Murongo, uliopo kwenye mto Kagera mpakani mwa nchi hizo mbili utakaozalisha megawatts 14.

Inakadiriwa kuwa kila nchi itapata megawatts saba kati ya hizo 14 zitakazozalishwa mara baada ya Mradi huo kukamilika.

Mradi huo wa umeme wa unajengwa na kampuni ya kikandarasi ya PAC ya Italia unasimamiwa na kampuni Binafsi ya Uganda ya Kikagati-Murongo hydropower project ambayo ndio mjenzi wa Mradi huo ulioanza Mwezi Mei 2018 na kutarajia kukamilika Mei 2021 kwa gharama dola Milioni 90.

Ujenzi wa Mradi huo ni makubaliano ya nchi mbili za Tanzania na Uganda ya matumizi bora ya maji ya mto Kagera ambao upo mpakani mwa nchi hizo.

Bw.Geoffrey Mwambe ametembelea eneo la Ujenzi wa Mradi huo ili kukagua Maendeleo ya Ujenzi wake na kutaka maazimio ya Ujenzi wa Mradi huo ya asilimia 50 kila upande wa nchi hizo mbili za Tanzania na Uganda yazingatiwe.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Generali Marco Gaguti alisema kukamilika kwa Mradi huo kutasaidia kupatikana kwa umeme wa uhakika mkoani kwake.

Mhandisi Mshauri wa Mradi huo kutoka Kampuni ya nguvu za Nishati ya Geni Mhandisi Dkt Juliana Pallangyo alisema watasimamia ipasavyo ili kufanikisha Ujenzi wa Mradi huo na kuongeza kuwa kila nchi itanufaika katika kila hatua za Ujenzi na uendelezaji wa Mradi huo.

Mradi huo wa Kikagati-Murongo unajengwa kwenye Wilaya za Kyerwa Mkoani Kagera Tanzania na Wilaya ya Isingilo Nchini Uganda.


Share:

Zoezi La Utayari Kukabiliana Na Ugonjwa Wa Ebola Katika Wilaya Ya Buhigwe Mkoani Kigoma

Kufuatia nchi ya jirani (DRC) kuendelea kukabiliwa na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola tangu Agosti mwaka 2018. Serikali ya Tanzania imeendelea kuchukua tahadhari za ugonjwa huo kwa kupima utayari wa Watoa huduma za Afya kwa mikoa iliyomo hatarini kuathiriwa na ugonjwa huo.

Serikali kupitia uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Menejimenti ya Maafa kwa kushirikiana na Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, pamoja na wadau wa maendeleo; WHO, FAO, USAID, HRH2030, na USAID Global Health Supply Chain Programu, inaendelea na zoezi la utayari wa kukabiliana na ugonjwa huo katika Wilaya za Mkoa wa Kigoma.

Zoezi hilo linalenga kuwaimarisha watumishi hao katika maeneo maalum ikiwemo ya uratibu, utambuzi na ufuatiliaji wa wagonjwa iwapo atagundulika, matibabu ya wagonjwa, uchukuaji na usafirishaji wa sampuli na kuthibitisha maabukizi pamoja kuimarisha mifumo ya utambuzi wa masuala ya Afya kwa kila abiria wanaopita kwenye mipaka ya mkoa wa Kigoma.


Share:

STANDARD CHARTERED YATANUA WIGO WA UWEKAJI WA AMANA KWA WATEJA WAKUBWA

 Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bi. Juanita Mramba akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki kwa Makampuni makubwa, ya kati na taasisi za kifedha wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bw.  James Meitaron wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa huduma mpya ya fedha kwa wateja wake wakubwa ya kuweka fedha katika akaunti zao kwa kutumia mashine maalumu (Cash Deposit Machines services-CDMs) zitakazowekwa kwenye eneo la kazi uliofanyika Hoteli ya Hyatt-The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Bidhaa za makampuni makubwa na ya kati wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bw. Busara Raymond.
 Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki kwa Makampuni makubwa, ya kati na taasisi za kifedha wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bw.  James Meitaron akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu huduma mpya ya fedha kwa wateja wake wakubwa ya kuweka fedha katika akaunti zao kwa kutumia mashine maalumu (Cash Deposit Machines services-CDMs)  zitakazowekwa kwenye eneo la kazi wakati wa hafla fupi ya uzinduzi iliyofanyika Hoteli ya Hyatt-The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Bidhaa wa makampuni makubwa na ya kati wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bw. Busara Raymond na kulia ni Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bi. Juanita Mramba.
 Meneja Bidhaa wa makampuni makubwa na ya kati wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bw. Busara Raymond akizungumza jambo na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa huduma mpya ya fedha kwa wateja wake wakubwa ya kuweka fedha katika akaunti zao kwa kutumia mashine maalumu (Cash Deposit Machines services-CDMs) zitakazowekwa kwenye eneo la kazi  uliofanyika Hoteli ya Hyatt-The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki kwa Makampuni makubwa, ya kati na taasisi za kifedha wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bw.  James Meitaron na kulia ni Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa benki hiyo, Bi. Juanita Mramba.
 Baadhi ya mashine maalumu za kuweka fedha (Cash Deposit Machines services-CDMs) zitakazowekwa kwenye  eneo la kazi kabla ya kuzinduliwa rasmi wakati wa hafla fupi ya uzinduzi iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt-The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.

 Meneja Bidhaa wa makampuni makubwa na ya kati wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bw. Busara Raymond (kulia) akitoa maelezo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) jinsi mashine maalumu ya kuweka fedha (Cash Deposit Machines services-CDMs) kwenye eneo la kazi inavyofanyakazi wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa huduma mpya ya fedha kwa wateja wake wakubwa uliofanyika Hoteli ya Hyatt-The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki kwa Makampuni makubwa, ya kati na taasisi za kifedha wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bw.  James Meitaron.
 Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki kwa Makampuni makubwa, ya kati na taasisi za kifedha wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bw.  James Meitaron akikata utepe ishara ya kuzindua rasmi mashine maalumu ya kuweka fedha (Cash Deposit Machines services-CDMs) kwenye eneo la kazi wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa huduma mpya ya fedha kwa wateja wake wakubwa uliofanyika Hoteli ya Hyatt-The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Meneja Bidhaa wa makampuni makubwa na ya kati wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bw. Busara Raymond pamoja na Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa benki hiyo, Bi. Juanita Mramba.
 Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki kwa Makampuni makubwa, ya kati na taasisi za kifedha wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bw.  James Meitaron (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kuzindua mashine maalumu za kuweka fedha (Cash Deposit Machines services-CDMs) kwenye eneo la kazi wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa huduma mpya ya fedha kwa wateja wake wakubwa uliofanyika Hoteli ya Hyatt-The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa benki hiyo, Bi. Juanita Mramba na kulia ni Meneja Bidhaa wa makampuni makubwa na ya kati wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bw. Busara Raymond.
 Mpiga picha wa gazeti la Mwananchi, Said Nanjundo akiuliza swali kwa uongozi wa Benki ya Standard Chartered wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa huduma mpya ya fedha kwa wateja wake wakubwa ya kuweka fedha katika akaunti zao kwa kutumia mashine maalumu (Cash Deposit Machines services-CDMs) zitakazowekwa kwenye eneo la kazi uliofanyika Hoteli ya Hyatt-The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki kwa Makampuni makubwa, ya kati na taasisi za kifedha wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bw.  James Meitaron katika picha na moja ya mashine maalumu ya kuweka fedha (Cash Deposit Machines services-CDMs) kwenye eneo la kazi wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa huduma mpya ya fedha kwa wateja wake wakubwa uliofanyika Hoteli ya Hyatt-The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.

BENKI ya Standard Chartered jana imezindua huduma mpya ya fedha kwa wateja wake wakubwa, ambao wataweka fedha hizo katika akaunti zao kwa kutumia mashine maalumu (Cash Deposit Machines services-CDMs) zitakazowekwa kwenye eneo la biashara.
Huduma hiyo ni juhudi za benki hiyo kutekeleza matakwa ya wateja wake ya kuwa karibu nao na kurahisisha uwekaji wa fedha na usalama wake.

Huduma hiyo ambayo inawezesha mteja kuwa na mtambo wa kuwekea fedha katika eneo lake la kazi (Cash Deposit Machines services-CDMs) imelenga kwa wafanyabiashara wakubwa kama wenye vituo vya mafuta, maduka makuu, na wauzaji wa vinywaji baridi.
Imeelezwa kuwa CDMs hizo zitafungwa katika maeneo ya biashara hizo na kutoa huduma za kuhifadhi fedha muda wowote ule.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi huo wa huduma za CDMs,  Mkuu wa Kitengo cha huduma za kibenki kwa Mashirika, Biashara na taasisi za kifedha, Bw.  James Meitaron, alisema: “ Benki ya Standard Chartered inazindua Cash Deposit Machines ili kuwezesha wateja wetu wakubwa kuwa na muda zaidi wa kushughulika na kazi na kuacha shaka ya upelekaji wa fedha nyingi kila mara. kwa kuwa na  CDMs wateja wetu sasa wanaweza kuhifadhi fedha katika akaunti zao muda wowote katika mtambo huo. fedha zinazowekwa zitaonesha katika kumbukumbu za kibenki.” 

Aidha alisema kwamba CDMs imeunganishwa na mifumio mingine ya kibenki ya kidigitali ikiwamo Bank’s Corporate Banking Digital platform, S2B, hivyo kumwezesha mteja kuona kinachoendelea katika akaunti yake.

Akizungumzia usalama wa mitambo hiyo, Meitaron alisema kwamba benki inawajibika mara tu fedha hizo zinapowekwa katika mitambo ya CDMs. Pia benki ndiyo itakayosafirisha fedha hizo kutoka katika eneo la mteja hadi benki. 

Mitambo hiyo itawekwa katika maeneo ya mteja yaliyo salama huku hatua zote za kiusalama zikiwa zimetekelezwa.
Pia mitambo hiyo ina uwezo wa kutambua fedha za bandia na kwamba zitakuwa zinaangaliwa na watu ambao watachaguliwa na wateja wenyewe.
“baadhi ya wateja wetu wana huduma hizi na wameomba mitambo zaidi kutokana na haja  kutunza muda na usalama wa fedha. Nashauri wateja wengi  kujaribu huduma hii watafurahi,” alisema Meitaron 

Uzinduzi wa CDMs unafanyika ikiwa ni sehemu ya harakati za benki za kufikia wateja wake pale walipo kwa kutumia njia mbalimbali. Hivi karibuni benki hiyo ilizindua Full Digital Bank on Mobile kwa ajili ya wateja wadogo binafsi na hii ya CDMs ni kwa ajili ya wateja wakubwa.

Share:

RAIS MAGUFULI AFURAHISHWA NA MAENDELEO YA SHIRIKA LA TPDC

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Meneja Mawasiliano na Mahusiano wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Bi. Marie Msellemu mara baada ya kutembelea banda lao katika ufunguzi rasmi wa Maonesho ya Maadhimisho ya Awamu ya Nne ya Wiki ya Viwanda kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wafanyakazi wa TPDC mara baada ya kutembelea banda lao katika ufunguzi rasmi wa Maonesho ya
Maadhimisho ya Awamu ya Nne ya Wiki ya Viwanda kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelezo ya kutoka kwa Meneja Mawasiliano na Mahusiano wa TPDC Bi. Marie Msellemu alipotembelea banda la shirika hilo wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Maadhimisho ya Awamu ya Nne ya Wiki ya Viwanda kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Share:

MWENYEKITI WA KITONGOJI AUAWA KWA MAPANGA KAHAMA ,USHIRIKINA WA RADI ILIYOUA WAWILI YAHUSISHWA

Na Salvatory Ntandu 
Watu wasiojulikana wamemvamia na kumuua papo hapo Mwenyekiti wa kitongoji cha Nyambula kata ya Ngongwa, Halmashauri ya mji wa Kahama Hamisi Kadilanha Salehe(58) kwa kumkata na kitu chenye ncha kali wakati akiwa amelala na mkewe Shija Mkela Maziku(45).

Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa,tukio hilo jana majira ya saa mbili usiku ambapo watu hao walitekeleza mauaji hayo na kisha kumjeruhi Shija Mkela Maziku.

"Chanzo cha tukio hilo kinasadikiwa ni imani za kishirikina 
kutokana na tukio la kupigwa na radi mwezi wa Februari, 2019 ambapo ilisababisha kifo cha mdogo wake na marehemu aitwaye Mhoja  S/O Kadilanha Salehe (45), mkazi wa Nyambula pamoja na mkewe aitwaye Pili Tabu Mabula (36),mkazi wa Nyambula na wakati wengine waliokuwa pamoja nao hawakupata madhara kutokana na radi hiyo",ameeleza.
Amefafanua kuwa, mbinu iliyotumika ni kuvunja mlango na kumvamia akiwa amelala chumbani kwake na mkewe nakuongeza mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Halmashauri Mji wa Kahama.

Kamanda Abwao amesema katika tukio hilo watu hao waliwajeruhi watu wawili ambao ni mke wa marehemu Shija Maziku na Dada yake Pili tabu Mabula ambao wote wanaendelea kupatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Halmashauri ya mji.

Ameongeza kuwa jeshi la polisi kwa kushirikina na wananchi linaendelea kuwatafuta watu hao walifanya mauaji na watakapobainika watachukuliwa hatua za kisheria kama ambavyo wamekuwa wakichukuliwa watu wengine wanaojichulia sheria Mkononi.



Share:

Watu wasiojulikana wafanya mauaji Kahama, huku Imani za kishirikina zikihusiswa na mauaji hayo

NA SALVATORY NTANDU
Watu wasiojulikana wamemvamia na kumuua papo hapo Mwenyekiti wa kitongoji cha Nyambula kata ya Ngongwa, Halmashauri ya mji wa Kahama Hamisi Kadilanha Salehe(58) kwa kumkata na kitu  chenye ncha kali wakati akiwa amelala na mkewe Shija Mkela Maziku(45).

kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa  Shinyanga ACP Richard Abwao, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo nakusema kuwa,tukio hilo jana  majira ya saa mbili usiku ambapo watu hao walitekeleza mauaji hayo na kisha kumjeruhi shija Mkela Maziku.

Amesema chanzo cha tukio hilo kinasadikiwa ni imani za kishirikina kutokana na tukio la kupigwa na radi mwezi wa Februari mwaka huu ambapo ilisababisha kifo cha mdogo wake na marehemu Mhoja Kadilanha Salehe(45) na mkewe Pili Tabu Mabula(36)na wengine waliokuwa nao hawakupata madhara kutokana na radi hiyo.

Amefafanua mbinu iliyotumika ni kuvunja mlango na kumvamia akiwa amelala chumbani kwake na mkewe nakuongeza mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Halmashauri Mji wa Kahama.

Kamanda Abwao amesema  katika tukio hilo watu waliwajeruhi watu wawili ambao ni mke wa marehemu Shija Maziku na Dada yake Pili tabu Mabula ambao wote wanaendelea kupatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Halmashauri ya mji.

Ameongeza kuwa jeshi la polisi kwa kushirikina na wananchi linaendelea kuwatafuta watu hao walifanya mauji na watakapobainika watachukuliwa hatua za kisheria kama ambavyo wamekuwa wakichukuliwa watu wengine wanaojichulia sheria Mkononi.


Share:

Wafanyabiashara Washauriwa Kuwekeza Kwenye Viwanda Vya Mafuta Ya Kula Na Sukari

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Simiyu
Wafanyabiashara nchini Tanzania na nje ya nchi wametakiwa kuwekeza katika viwanda vya uchakataji wa mazao mbalimbali yakiwemo miwa na alizeti.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo Tarehe 6 Agosti 2019 wakati akizungumza kwenye hafla ya ufunguzi wa kongamano la fursa za Kilimo biashara katika viwanja vya Nyakabindi kwenye maonesho ya Sikukuu ya wakulima (Nanenane) katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.

Mhe Hasunga amesema kuwa endapo wakulima watawekeza katika Kilimo cha alizeti ni wazi kuwa wataimarisha upatikanaji wa mafuta ya kula yanayotokana na zao hilo hivyo kuondokana na dhana ya uagizaji wa mafuta kutoka nje ya nchi.

Alisema kuwa Tanzania inauhitaji wa mafuta ya kula kiasi cha Tani 570,000 lakini pamoja na kuwa na ardhi nzuri na yenye rutuba lakini juhudi za uzalishaji bado ni ndogo kwani kama nchi inazalisha Tani 250,000 pekee.

Alisema kuwa kiasi cha Bilioni 678 zilitumika mwaka 2018 kuagiza mafuta ya kula kutoka nje ya nchi ilihali kuna uwezo wa kuzalisha kwa wingi zao hilo na fedha ambazo zinatumika kuagiza  zingeweza kutumika katika kutekeleza miradi mingine.

Kuhusu Sukari, Waziri huyo wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga amesema kuwa Tanzania ina uhitaji wa sukari kiasi cha Tani 675,000 ambapo Tani 175,000 kati ya hizo ni sukari za viwandani ilihali kiasi kilichosalia ni sukari ya kawaida, lakini uwezo wa nchi ni kuzalisha Tani 359,000 pekee.

Alisema kuwa ni jambo la ajabu kuagiza sukari nje ya nchi  kwa kutumia gharama kubwa ilihali kuna maeneo mazuri kwa ajili ya kilimo na kuzalisha miwa.

Aidha, amewasihi wakulima kuzalisha miwa kwa wingi kwani ni miongoni mwa mazao yanayohitajika zaidi katika biashara sambamba na kufanya mabadiliko katika sekta ya Kilimo kupitia mkazo wa Programu ya kuendeleza sekta ya Kilimo awamu ya pili (ASDP II).

Kongamano hilo la fursa za Kilimo biashara katika viwanja vya Nyakabindi kwenye maonesho ya Sikukuu ya wakulima (Nanenane) katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu limefunguliwa na Waziri Mkuu mstaafu wa serikali ya awamu ya nne ambaye ni mjumbe wa kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa Mhe Mizengo Peter Pinda.

MWISHO


Share:

Waziri Jafo Akabidhi Pikipiki 23 Kwa Maafisa Maendeleo Kata Kwa Jiji La Dodoma.

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Seleman Jafo ameshiriki kwa pamoja kikao cha Baraza la madiwani jijini Dodoma na kukabidhi pikipiki   23 kwajili ya maafisa maendeleo ya kata na kulipongeza jiji hilo kwa kazi kubwa linazofanya..

Waziri jafo ameyasema hayo Jijini hapa katika kikao cha Baraza la Madiwani pamoja na kukabidhi pikipiki  kwa maafisa hao, huku akiwataka madiwani hao kuwa na upendo ili kuweza kuipelekea Dodoma mbele.

Aidha, Waziri jafo amewataka kutokubezana,kunyong’onyeshana ,unyanyapaa kwani kuna baadhi ya watu katika maeneo mengine wamekuwa na tabia ya kunyanyapaa wenzao na kwa kufanya hivyo si sawa.
 
Katika hatua nyingine Waziri jafo amempongeza mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma  Godwini Kunambi ,kwa kazi kubwa anayoifanya , kwani katika wakurugenzi  wanaojitahidi, amekuwa akifanya vizuri katika uongozi wake.
 
 Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Bwana Godwin Kunambi amesema kuwa uchangiaji wa miradi ya maendeleo umeongezeka  kutoka shilingi Bilioni 13.590  kwa mwaka wa fedha 2017/2018 hadi kufikia shilingi Bilioni 54.352 kwa mwaka wa fedha 2018/2019  sawa na ongezeko la asimia 74.9%.
 
Mbali na hilo kunambi amesema halmashauri inajukumu jingine la kustawisha makao makuu ya nchi,huku akisema katika mwaka wa fedha 2018/2019 halmashauri ilikisia kukusanya  na kupokea jumla ya shilingi Bilioni 159,Milioni 467,35 elfu 337.
 
Patrobas Katambi ni mkuu wa wilaya ya Dodoma ametumia kikao hicho kumpongeza waziri jafo ,kwa kazi kubwa ambayo anaifanya  pamoja na na kusema kuwa katika utawala bora wamekuwa wakisimamiana vizuri kuweza kuhakikisha kuwa sheria,kanuni ,taratibu,kanuni ,miongozo na maagizo ya viongozi yanafuatwa.
 
 Hatahvyo, Kunambi amesema bajeti ya Halmashauri iliongezeka kutoka  shilini Bilioni 20.798 kwa mwaka wa fedha 2017/2018 hadi shilingi Bilioni 67.149 kwa mwaka wa fedha 2018/2019 sawa na ongezeko la asilimia 69.02% ya makadirio ya mapato ya ndani.



Share:

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Amaliza Mgogoro Wa Ardhi Kati Ya Pori La Akiba La Selous Na Kijiji Uliodumu Kwa Miaka 12 Mkoani Lindi

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu ametatua mgogoro uliodumu kwa miaka 12  baina ya Pori la Akiba la Selous na Wananchi  wa kijiji cha Kikulyungu  kilichopo katika  wilaya ya  Liwale mkoani Lindi

Mgogoro  huo wa ardhi ulianza mwaka 2007 ambapo wananchi  walianza kudai kuwa eneo la Kihulumira ambalo linapakana na  Pori la Akiba la Selous kuwa  ni moja ya maeneo yao  ya Asili.

Kufuatia hali ilipelekea uhasama mara kwa mara kati ya wananchi na askari wanyamapori hasa pale wananchi walipokuwa wakikamatwa kwa madai kuwa wameingia ndani ya Hifadhi bila kibali.

Akizungumza na wananchi wa wa kijiji cha Kikulyungu mara baada ya kutembelea eneo lililokuwa na mgogoro,  Kanyasu alisema eneo hilo lilisajiriwa  mwaka 1975 na kijiji kilisajiriwa mwaka 2005 hivyo eneo hilo si sehemu ya kijiji.


Amesema baada ya kuundwa timu hiyo iliyokuwa ikiongozwa na wataalamu wa Ardhi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazo  ilibainika kuwa eneo hilo si la wananchi na  wala  sio sehemu ya   Pori la Akiba la Selous bali  ni Pori  Tengefu ambalo ni mali ya serikali Kuu na linasimamiwa na Wizara ya Maliasili na Utalii.

Katika hatua nyingine, Kanyasu amewataka wananchi   kuacha  vitendo vya kukata miti ovyo na kuchoma misitu kutoka na uharibifu mkubwa wa misitu aliuona karibu na eneo lililokuwa na mgogoro baina ya pande hizo mbili.

 Kufuatia hali hiyo, Mhe.Kanyasu  amewaagiza viongozi wa vijiji hivyo  kuweka sheria kali ili kudhibiti  hali  ya uharibifu  wa misitu unaoendelea katika maeneo hayo.

Akizungumza  kwa niaba ya wanachi wa wilaya ya Liwale Mbunge Liwale,  Zuberi Kuchauka  ameishukuru serikali kwa hatua iliyofikia kwani mgogoro huo ni wa muda mrefu na ulikuwa haujapatiwa ufumbuzi

Amesema mgogoro huo uliwafanya wananchi wa maeneo hayo kupunguza kasi ya kujiletea maendeleo badala yake wajanja wachache walikuwa wakitumia nafasi ya mgogoro kuendelea kujinufaisha.

" Sitegemei mgogoro mwingine wa ardhi baada ya kumalizika huu, Nawaomba wananchi sasa tuchape kazi" Alisisitiza Kuchauka.

Kutokana na kumalizika kwa mgogoro huo wananchi wa kijiji hicho wameiomba serikali kulitumia eneo hilo kuanzisha Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ili kuinua kipato katika kijiji hicho.



Share:

Upatikanaji Wa Vifaranga Vya Samaki Na Chakula Bora Wawekewa Mikakati.

Na. Edward Kondela
Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeweka mikakati ya upatikanaji wa vifaranga vingi vya samaki pamoja na chakula bora cha samaki sambamba na kuendelea kutoa elimu ya ufugaji ili wananchi waweze kufuga samaki kwa tija.

Akizungumza kwenye maonesho ya wakulima, wafugaji na wavuvi (Nanenane) kitaifa, katika viwanja vya Nyakabindi vilivyopo Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah amesema serikali imelazimika kuweka mikakati hiyo kutokana na wananchi wengi kuwa na mwamko wa kufuga samaki kibiashara licha ya kuwepo kwa changamoto ya upatikanaji wa vifaranga bora na chakula kwa bei nafuu.

“Kwa mfano mwaka jana uhitaji wa mbegu za samaki ulikuwa unafikia takriban samaki Milioni 40 lakini sisi tumeweza kuzalisha kama Milioni 18 kwa hiyo kuna mikakati ipo kuhakikisha vituo vya serikali pamoja na kuhamasisha vile vya watu binafsi kuzalisha vifaranga bora, changamoto nyingine ni chakula ambapo wapo wanaotengeneza hapa nchini lakini vinakuwa havijafikia ubora unaotakiwa na wengine wanaagiza kutoka nje ya nchi ambapo ni bei ghali, hivyo tunaweka mikakati ya uwepo wa chakula bora na bei nafuu pamoja kutoa elimu ya utengenezaji wa chakula hicho.” Amesema Dkt. Tamatamah

Amefafanua kuwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Maonesho ya Nanenane mwaka huu, sekta ya uvuvi imejikita zaidi katika kutoa elimu ya ufugaji bora wa samaki ili kuwavutia wananchi kuwekeza katika ufugaji samaki kibiashara.

Kuhusu ulaji wa samaki nchini Dkt. Tamatamah amesema kulingana na tafiti kutoka Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) kwa sasa kila mtanzania anakula walau Kilogramu 8.2 za samaki kwa mwaka ilhali FAO inapendekeza mtu mmoja kula samaki kilogramu 20.3 kwa mwaka, hivyo serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imekuwa ikiweka pia mikakati ya uwepo wa ongezeko la uzalishaji wa samaki hapa nchini lakini pia kuhakikisha samaki wachache wanaozalishwa wanamfikia mlaji wakiwa katika hali nzuri.

Katibu mkuu huyo anayeshughulika na sekta ya uvuvi amebainisha pia kupitia Maonesho ya 27 ya Nanenane kwa Mwaka 2019 Wizara ya Mifugo na Uvuvi imejikita zaidi katika utoaji wa elimu kwa wadau katika sekta za mifugo na uvuvi ili kutatua changamoto mbali zinazowakabili na kuweza kufuga kwa tija.

Mwisho.


Share:

WAZIRI MKUU MAJALIWA 'AKOSHWA' NA MAONESHO YA VIWANDA YA NCHI ZA SADC

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege nchini (ATCL) Mhandisi Ladislaus Matindi katika Maonyesho ya Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Viwanda kwa Nchi za SADC kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa Tanzania,Mhe. Kassim Majaliwa, akipata maelezo kuhusu ya Reli ya Kisasa kutoka kwa Afisa Habari wa  Shirika la Reli Tanzania (TRC), Jamila Mbarouk alipotembelea banda la Shirika la Reli Tanzania(TRC)  katika maonesho ya Wiki ya Viwanda SADC, yanayoendelea Jijini Dar es Salaam, kulia kwake ni Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea mabanda katika Maonyesho ya Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Viwanda kwa Nchi za SADC kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Agosti 6, 2019. Wapili kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa George Lous Chuwa kuhusu bidhaa mbalimbali wakati alipotembelea banda la Sekretarieti ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) katika Maonyesho ya Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Viwanda kwa Nchi za SADC kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Agosti 6, 2019. Wapili kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na wanahabari mara baada ya kutembelea Maonyesho ya Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Viwanda kwa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Wa pili kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocenti Bashungwa na kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na wanahabari mara baada ya kutembelea Maonyesho ya Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Viwanda kwa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Agosti 6, 2019. Wa pili kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocenti Bashungwa. Wengine kutoka kushoto ni Waziri wa Afya wa Zanzibar, Hamad Rashid, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi, Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega.

Na Mwandishi Wetu.

 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa amewataka watanzania kuchangamkia fursa zitokanazo na maonesho ya Viwanda ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) ili kuwezesha ukuaji wa uchumi wa viwanda ambao Serikali inaujenga.

 Akizungumza mara baada ya kutembelea maonesho hayo yanayoendelea katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere, Viwanja vya Karimjee na Gymkana, Waziri Mkuu amesema kuwa maandalizi ya Mkutano Mkuu wa 39 wa Wakuu wa Nchi za SADC yamekamilika yakihusisha kuwepo kwa maonesho ambayo nchi wanachama wataonesha teknoloji, Ubunifu na bidhaa zao kutoka katika Viwanda vya nchi za SADC.

 Waziri Mkuu alisema kuwa Serikali imetoa fursa kwa wafanyabiashara Wakubwa, wa kati, wadogowadogo na wenye bidhaa zinazozalishwa kwa mikono kuja kuonesha na kuchukua teknolojia kutoka nchi wageni ambao wapo nchini kwa maonesho hayo ya wiki moja.

 “Sisi kama Serikali tumetoa Fursa kwa wale ambao wanafanya kazi na kuzalisha bidhaa zao kwa kutumia mikono kuja kuonesha bidhaa zao ili ziweze kupata masoko kwa nchi wanachama wa SADC kwani nchi zote zinakuja hapa kuleta bidhaa mbalimbali kwa hiyo watanzania wanatakiwa kutumia fursa hii kuwauzia wageni bidhaa zetu”, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Share:

KIGOGO WA SIMBA CREAM TANGA ATUA KWENYE SHEREHE ZA TAWI LA SIMBA DUGA,ATAKA MSHIKAMANO

 KATIBU Msaidizi wa Tawi la Simba Cream la Jijini Tanga Edgar Mdime ambaye pia ni Mweka Hazina kulia akilakiwa na wanachama wa Simba Tawi la Duga mara baada ya kuwasili kwa ajili ya sherehe za Simba Day
 KATIBU Msaidizi wa Tawi la Simba Cream la Jijini Tanga Edgar Mdime ambaye pia ni Mweka Hazina  kulia akisaliana na wanachama wa simba Tawi la Duga
 MMOJA wa viongozi na wanachama wa Simba Tawi la Simba Cream Jijini Tanga wakiwasalimia wenzao wa Tawi la Duga
 KATIBU Msaidizi wa Tawi la Simba Cream la Jijini Tanga Edgar Mdime ambaye pia ni Mweka Hazina kulia akiteta jambo na Katibu wa Tawi la Simba Duga Ramadhani Mlekwa wakati wa sherehe za Simba Day
 KATIBU Msaidizi wa Tawi la Simba Cream la Jijini Tanga Edgar Mdime kulia  ambaye pia ni Mweka Hazina kulia akiwa na viongozi wengine wakipata chakula  kwenye Tawi la Simba Duga wakati wa sherehe za Simba day
 Katibu wa Tawi la Simba Duga Ramadhani Mlekwa wakati wa sherehe za Simba Day akionyesha nembo ya simba 
Sehemu ya wana Simba wakiwa kwenye sherehe hizo
 Sehemu ya wana Simba wakiwa kwenye sherehe hizo
 MMOJA wa wana Simba akizungumza jambo wakati wa sherehe hiyo 
KATIBU Msaidizi wa Tawi la Simba Cream la Jijini Tanga Edgar Mdime ambaye pia ni Mweka Hazina kushoto akiwa na wanachama wa Simba Tawi la Duga  wakati wa sherehe za Simba Day
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger