Friday, 2 August 2019

MAJAMBAZI WAVAMIA MSIBA NA KUPORA FEDHA ZA KUNUNULIA JENEZA LA MAREHEMU

Familia moja katika eneo bunge la Kinangop, Kaunti ya Nyandarua,nchini Kenya iliyokuwa ikiomboleza ilipata majonzi zaidi baada ya kuvamiwa na majambazi walioiba Sh18,000 zilizokuwa zimetengewa ununuzi wa jeneza la kuzika marehemu. 

Kwa mujibu wa Taifa Leo, Rufa Thiga, mkewe na nduguye walivamiwa na majambazi sita mnamo Jumatano usiku, Julai, 27,2019 saa chache tu baada ya wageni waliofika kuomboleza kifo cha dada yao kuondoka.

Mke wa Thiga, Margaret Wambui na nduguye Benson Kigo walijeruhiwa kwenye kisa hicho. Thiga alisimulia jinsi alivyowasikia majambazi hao waking’ang’ana kuvunja lango kuu la kuingia boma lake na jinsi jaribio lake la kutorokea mlango wa nyuma lilivyogonga mwamba. 

“Nilipojaribu kutorokea mlango wa nyuma, watu wawili walinivamia kwa panga huku wengine wakiingia ndani ya nyumba na kumpiga mke wangu kwa silaha butu,” Thika alisema.

Simulizi hiyo inaendelea kwa kusema kuwa, baada ya hapo majambazi hao walimwagiza aingie ndani ya nyumba na awakabidhi pesa alizokuwa amekusanya kugharimia mazishi ya dadake.

 “Walinilazimisha kuingia ndani ya nyumba niwape pesa za matanga. Niliwapa KSh 18,000 ambazo zilikuwa zimetengewa ununuzi wa jeneza la marehemu,” akaongeza kusema. 

Wambui naye kwa masikitiko alisimulia jinsi majambazi hao walivyomfuata hadi kwenye bafu na kumpiga wakidai awape pesa.

“Walitishia kuua familia yote. Nilipata majeraha kwenye mikono, mgongo na kichwani,” akasema. Kigo naye alisema kuwa wezi hao walimlazimisha aingie ndani ya nyumba na akawapa KSh 3,000 ili kuyanusuru maisha yake.

 “Walinieleza kwamba walikuwa maafisa wa polisi kabla ya kunipiga kichwani na kuniamrisha nilale chini,” alisema. 

Haijulikani kufikia sasa ikiwa familia ya Thiga ilifanikiwa kupata pesa zingine na kuuzika mwili wa marehemu.
Via>>Tuko
Share:

TAMASHA LA UIMBAJI KUTIKISA SHINYANGA JUMAPILI HII...HAPA ROSE MUHANDO ,PALE MJESHI BAND..PAPAA JJ,AIC SHINYANGA

Share:

TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA IJUMAA


Manchester City wamekataa daul la pauni milioni 72 kutoka kwa Bayern Munich kwa ajili ya mshambuliaji wa Leroy Sane

Manchester City wamekataa dau la pauni milioni 72 kutoka kwa Bayern Munich kwa ajili ya mshambuliaji wa Leroy Sane raia wa Ujerumani, mwenye umri wa miaka 23. (Metro)

City wanataka walipwe pauni milioni 137 kwa mauzo ya Sane ikiwa hatakuwa na haja ya kusaini mkataba wa kurefusha mkataba wake, unaomalizika Juni 2021. (Telegraph)

Manchester United wanahangaika kufikia makubaliano na mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala, mwenye umri wa miaka 25, na muwakilishi wake, na hivyo kuuweka hatarini mkataba na Juventus wa kubadilishana mchezaji wa safu ya mashambulizi Mbelgiji Romelu Lukaku, mwenye umri wa miaka 26. (Independent)Manchester United wanahangaika kufikia makubaliano na mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala

Manchester City imeingia tena katika mazungumzo na Juventus juu ya kiungo wa safu ya nyuma kulia Mremo Joao Cancelo,mwenye umri wa miaka 25. (Telegraph)

Mlizi wa England Harry Maguire, mwenye umri wa miaka 26, ameachwa nje ya kikosi cha Leicester kitakachocheza mechi ya urafiki baina yao na Atalanta Ijumaa kutokana na hali ya sintohfahamu juu ya hali ya yake ya baadae na Foxes wanaotaka mkataba wa pauni milioni 90 ikiwa Manchester United wanasaini mkataba nae. (Telegraph)

Dau la sasa la Manchester United kwa ajili ya Maguire ni la thamani ya pauni milioni 80 na klabu hiyo inaweza kutumia zaidi ya pauni milioni 150 kwa ujumla kabla ya kipindi cha mwisho cha mchakato wa uhamisho kukamilika (Independent)

Manchester United ilikataa fursa ya kusaini mkataba na mshambuliaji wa Juventus mwenye umri wa miaka 19 Moise Kean, na kumruhusu mtaliano huyo kuwa huru kuhamia Everton. (90min)Dau la sasa la Manchester United kwa ajili ya Maguire ni la thamani ya pauni milioni 80

Liverpool wanapima uwezekano wa kumnunua mchezaji wa safu ya mashambulizi wa Bordeaux na Guinea Francois Kamano na wako tayari kumgaramia kwa pauni milioni 20 kijana huyo mwenye umri wa miaka 23 . (Sun)Manchester City imeingia tena katika mazungumzo na Juventus juu ya kiungo wa safu ya nyuma kulia Mremo Joao Cancelo

Tottenham wanauangalia mkataba kwa ajili ya kiungo wa kati wa Sporting Lisbon na Ureno Bruno Fernandes, mwenye umri wa miaka 24, kama kiungo mbadala wa mchezaji wa Real Beti -Giovani Lo Celso, mwneye umri wa miaka 23. (Evening Standard)

Betis wamekataa ofa kadhaa kutoka kwa Tottenham kwa ajili ya mchezaji wa kimataifa wa Argentina Lo Celso. (SevillaABC - in Spanish)

Kiungo wa kati- nyuma wa Argentina Nicolas Otamendi, mwenye umri wa miaka 31, anataka kuendelea kuwepo Manchester City licha ya kuhusishwa na taarifa za kuihama klabu hiyo.(Sun)Nicolas Otamendi, mwenye umri wa miaka 31, anataka kuendelea kuwepo Manchester City licha ya kuhusishwa na taarifa za kuihama klabu hiyo

Newcastle wanakaribia kusaini mkataba na winga wa Ufaransa Allan Saint-Maximin,mwenye umri wa miaka 22, kutoka Nice katika mkataba wa pauni milioni 16.5 . (Talksport)

Mchezaji wa safu ya nyuma-kushoto wa Brazil Dani Alves anakaribia kuhamia Sao Paulo. Kijana huyo mwenye umri wa miaka 36- yuko huru baada ya kuondoka Paris St-Germain. (Goal)

Crystal Palace wamefany amawasiliano na Cardiff City kumuhusu kiungo wa kati wa Real Betis Muhispania Victor Camarasa mwenye umri wa miaka 25

CHANZO.BBC SWAHILI
Share:

Makombora mapya ya 9M729 ya Urusi yanayoitia tumbo joto Marekani na washirika wake

Marekani inatarajiwa kujitoa rasmi katika mkataba wa nyuklia na Urusi, hatua inayozusha hofu kuhusu ushindani wa silaha mpya.

Mkataba huo unaohusu zana za nyuklia za masafa ya katikati (INF) ulisainiwa na rais wa Marekani Ronald Reagan na kiongozi wa iliyokuwa Sovieti Mikhail Gorbachev mnamo 1987. Ulipiga marufuku makombora ya masafa ya kati ya kilomita 500-5,500.
 
Lakini awali mwaka huu Marekani na Nato ziliishutumu Urusi kwa kukiuka makubaliano hayo kwa kufyetua aina mpya ya kombora, jambo ambalo Moscow inalikana.

Marekani imesema ina ushahidi kuwa Urusi imetuma kombora aina ya 9M729 linalofahamika kwa Nato kama SSC-8. Tuhuma hizi ziliwasilishwa kwa washirika wa Nato wa Marekani ambao wote waliunga mkono madai ya Marekani

Rais Donald Trump mnamo Februari alitangaza kuwa Marekani itajitoa kutoka mkataba huo iwapo Urusi haitotii, na kuweka tarehe ya mwisho kuwa Agosti 2.

Rais wa Urusi Vladimir Putin na yeye  amesitisha majukumu ya taifa lake katika mkataba huo muda mfupi baadaye.

Wachambuzi wanahofia kwamba kutibuka kwa makubaliano hayo ya kihistoria huenda kukachangia ushindani mpya wa silaha kati ya Marekani, Urusi na China.

"Kutokana na kuvunjika kwa mkataba huo sasa, tutashuhudia utengenezaji na utumiaji wa silaha mpya," Pavel Felgenhauer, mchambuzi wa zana za Urusi ameliambia shirika la habari la AFP. "Urusi tayari ipo tayari."

Mwezi uliopita, Katibu mkuu wa Nato Jens Stoltenberg ameiambia BBC kuwa makombora ya Urusi - ambayo alisema kuwa ni "ukiukaji wa wazi wa mkataba huo" - yana uwezo wa nyuklia, ambayo ni magumu kuyatambua na yanaweza kufika katika miji ya Ulaya katika muda wa dakika.

"Hili ni jambo zito," aliongeza. " Mkataba wa INF umekuwa jiwe la msingi katika udhibiti wa silaha kwa miongo kadhaa, na sasa tunashuhudia kuvunjika kwa mkataba huo ."

Ameongeza kwamba hakujakuwepo "ishara zozote" kuwa Urusi itatii makubaliano hayo na kwamba "ni lazima tujitayarishe kwa ulimwengu usiokuwa na mkataba wa INF na ulio na makombora zaidi ya Urusi".

Stoltenberg pia alisema kuwa uamuzi wowote wa Nato kuhusu namna gani ya kujibu utatolewa baada ya kupita muda huo wa mwisho uliotolewa.

Credit:BBC


Share:

Serikali Yapongezwa Mfumo Wa GePG

Na. Peter Haule na Farida Ramadhani, WFM, Simiyu
Mwandishi Mashughuli wa Vitabu nchini kikiwemo cha “Mabala The Farm”, Bw. Richard Mabala, ameipongeza Serikali kwa kubuni mfumo wa kielektroniki wa makusanyo ya maduhuli ya Serikali- GePG kwa kuwa unasaidia kudhibiti ubadhilifu wa fedha za umma na kuweka uwazi wa mapato na matumizi.

Alibainisha hayo alipotembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.

Alisema kuwa Mfumo wa GePG unamanufaa kwa Serikali na wananchi, kutokana na uwazi uliopo lakini pia makusanyo kufika kwa wakati katika maeneo husika kwa ajili ya matumizi ya maendeleo na mengine.

“Mfumo huo utanisaidia malipo ya kodi ya majengo na kodi nyingine kwa kuwa unaondoa urasimu wa kwenda katika ofisi mbalimbali kwa ajili ya malipo na pia unaokoa muda kwa kuwa ni rahisi kuutumia kwa njia ya simu ya mkononi”, alisema Bw. Mabala.

Mwandishi huyo wa Vitabu ametoa wito kwa wadau, ikiwemo Serikali kuhamasisha matumizi ya Simu zenye uwezo wa kutumia mfumo wa GePG, hasa katika maeneo ya vijijini ambako idadi kubwa ya wananchi wakiwemo wakulima wanapatikana.

Tanzania inaidadi kubwa ya vijana ambao wanauwezo wa kutumia mfumo wa kielektroniki katika malipo ya Serikali ukilinganisha na wazee, hivyo umekuja wakati mwafaka na utakua na nafasi kubwa ya kuchochea maendeleleo ya kiuchumi.

Bw. Mabala amesema kuwa, Mfumo huo utasaidia kwa kiasi kikubwa katika Mipango ya Serikali ukilinganisha na awali ambapo mfumo huo haukuwepo hivyo uwepo wa GePG utaongeza ufanisi kiutendaji na kuharakisha maendeleo kulingana na ushindani uliopo katika nyanja mbalimbali duniani hasa katika mifumo ya teknolojia.

Kwa upande wao wanafunzi wa Sekondari ya Biashara iliyopo Bariadi Mkoani Simiyu, wameipongeza Serikali kwa kutumia mfumo wa kisasa wa GePG, hivyo elimu waliyoipata katika maonesho ya Nanenane wataipeleka kwa wazazi wao na jamii inayowazunguka ili waweze kuitumia katika malipo ya Serikali.


Share:

Serikali Kuwachukulia Hatua Waajiri Wanaowanyima Haki Wanawake Likizo Ya Uzazi

 Na Rayson Mwaisemba, WAMJW- DOMOMA
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imetangaza kuanza kuwachukulia hatua Waajiri wote ambao wanavunja Sheria kwa kugandamiza haki ya kupata likizo ya uzazi kwa wanawake pindi anapojifungua.

Hayo yamesemwa jana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika katika ofisi za Wizara ya Afya Jijini Dodoma, yenye kauli mbiu ya “Wawezeshe wazazi kufanikisha unyonyeshaji”.

“Haki ya Mwanamke Kuzaa na kupata likizo ya uzazi ni haki yake ya asili, haitakiwi kuwekewa vikwazo au changamoto yoyote, kwahiyo nitoe wito kwa wanawake ambao wanafanya kazi, ni haki yako kupata likizo, asije mtu anakwambia anaijaza kazi yako kwakuwa umetoka likizo ya kujifungua, tuambie sisi, tutachukua hatua, na huyo Mwajiri tutamtangaza kuwa ni adui wa Wanawake na Watoto wa Tanzania “.Amesema Waziri Ummy.

Waziri Ummy aliendelea kusema kuwa Serikali ipo katika mpango wa kuanzisha dawati la kutoa malalamiko litaloshughulikia kupigania na kutetea haki za wanawake kupata likizo ya uzazi, jambo litalosaidia kudhibiti tabia za baadhi ya Waajiri kukandamiza haki za wanawake baada ya kujifungua.

Kwa upande mwingine, Waziri Ummy amesema kuwa takribani asilimia 97 ya watoto wenye umri chini ya miaka miwili wananyonyeshwa maziwa ya mama, hii inaonesha kuwa hali ya unyonyeshaji wa maziwa ya mama imepungua ikilinganishwa na takwimu ya mwaka 2015/2016 ambayo ilikuwa ni asilimia 98.

Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa idadi ya watoto wanaoanzishiwa kunyonyeshwa maziwa ya mama kwa wakati sahihi (ndani ya saa moja baada ya kuzaliwa) ni asilimia 53 ikilinganishwa na asilimia 51 ya mwaka 2015/2016

Aliendelea kusema kuwa, idadi ya watoto wanaonyonyeshwa maziwa ya mama pekee bila kupewa maji, vinywaji na vyakula vingine katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo baada ya kuzaliwa ni asilimia 58 ikilinganishwa na asilimia 59 ya mwaka 2015/2016.

Hata hivyo, Waziri Ummy amesema kuwa Idadi ya watoto wenye umri wa miezi 6 hadi 23 wanaolishwa chakula kinachokidhi vigezo vya ubora kilishe ni 35%, huku kiwango kikionekana kuongezeka ikilinganishwa na asilimia 10 kwa mwaka 2015/2016.

Mbali na hayo, Waziri Ummy amesema kuwa, takwimu za utafiti wa hali ya lishe nchini za mwaka 2018 zinaonyesha kuwa asilimia 31 ya watoto walio chini ya umri wa miaka mitano wamedumaa ikilinganishwa na asilimia 34 ya mwaka 2015/2016, huku sababu kubwa ya ikiwa ni ulishaji usio sahihi ambao huchangiwa na majukumu mengi yanayomkabili mama na hivyo kukosa muda wa kutosha wa kumtunza mtoto.

Naye Mwakilishi kutoka UNICEF Bw. James Gitau amesema kuwa, unyonyeshaji ni moja ya njia muhimu kuhakikisha Afya Bora kwa maisha ya mtoto, hivyo kutoa wito kwa wanahabari kuhakikisha wanapeleka Elimu kwa wananchi hususan wanawake kuhakikisha wanafahamu umuhimu wa kunyonyesha Watoto mfululizo miezi sita ya mwanzo,

Pia, Bw. James Gitau ametoa wito kwa Serikali kuongeza nguvu katika uhamasishaji juu ya umuhimu na haki ya Watoto kunyonyeshwa, amesema jambo hili litasaidia kuokoa watoto kupata magonjwa yanayotokana na kukosa virutubisho kutoka kwa maziwa ya mama.


Share:

Tanzania Yapiga Hatua Kudhibiti Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele

Na.Catherine Sungura,WAMJW-DSM
Serikali kupitia wizara ya afya imepiga hatua katika kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele nchi.

Hayo yamesemwa na mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mkurugenzi wa Huduma za Dharura na Maafa wa Wizara hiyo, Dk. Elius Kwesi wakati akifungua mkutano wa mwaka wa mapitio ya shuguli wa mpango wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele na mpango kazi wa mwaka.

Dkt.Kwesi alisema mkutano huo ni muhimu kwani watajadiliana na wadau hao kuona namna watakavyoshirikiana na Wizara hiyo kwa upande wa rasilimali fedha.

“Tuna pengo la rasilimali mbalimbali na tumewaita hapa Wadau kujadiliana nao Mpango kazi wetu na kuangalia namna gani watatusaidia kuziba pengo na kutakavyosaidiana kutekeleza,” alisema Dkt.Kwesi

Alisema tangu utekelezaji wa Mpango huo ulipoanza nchini umefanikiwa kupunguza magonjwa hayo kwa kiwango cha asilimia 80.

Awali Mkurugenzi wa huduma za Kinga wizarani hapo Dkt.Leonard Subi alisema magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele yasipodhibitiwa yatapelekea watu wengi kuugua siku zijazo kwani yana athari kubwa na kusababisha upofu na ulemavu kwa jamii.

“mfano ugonjwa wa kichocho kwa watoto huathiri ukuaji na wengine wanaweza kupata saratani katika maisha yao”.Alisema Dkt.Subi

Alisema wizara kushirikiana na wadau wa maendeleo imefanya jitihada kubwa na hivyo kufanikiwa kudhibiti magonjwa hayo kwa kiwango kikubwa

“Wilaya ambazo zilikua zimeathirika sana na matende na mabusha miaka kumi iliyopita zilikua takribani 120 lakini hivi sasa zimebaki wilaya 24 ambazo bado tunaendelea na ugawaji kingatiba na trakoma kulikuwa na wilaya 71 na sasa zimebaki wilaya sita tu”.

Naye Mratibu wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele(NTD) Dkt.Upendo Mwingira amesema kwa upande wa kichocho na minyoo ya tumbo bado inahitajika kuendelea kuwakinga watoto na baadhi ya wilaya wanaendelea kugawa kingatiba za matende na mabusha pamoja na usubi.


Share:

Wizara Ya Kilimo Yaja Na Mkakati Wa Taifa Wa Miaka 10 Wa Usimamizi Wa Mazao Baada Ya Kuvunwa

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Simiyu
Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi inakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo, mabadiliko ya tabianchi ambayo kwa kiasi kikubwa yanachangia kupungua kwa uzalishaji na tija ya mazao, uhaba wa malisho ya mifugo na rasilimali maji, teknolojia duni za kuhifadhi mazao baada ya mavuno, uelewa mdogo wa wadau katika kukabiliana na upotevu wa mazao na uhaba wa miundombinu ya masoko.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga ameyasema hayo wakati akimkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Mama Samia Suluhu Hassan, kwa ajili ya ufunguzi wa Maadhimisho ya Sherehe za Wakulima, Nane Nane, yameanza leo tarehe 1-8 Julai 2019,  katika Viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.

Mhe Hasunga amesema kuwa wakulima na wadau mbalimbali wa kilimo watapata fursa ya kutembelea mabanda mbalimbali ya bidhaa za kilimo  ili kuona hali halisi ya Maadhimisho pamoja na teknolojia za uzalishaji,  uongezaji thamani wa mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi, zilivyoandaliwa. Waoneshaji wengine wako njiani na tunatarajia uwanja huu wa Nyakabindi utafurika kwa maonesho.

Alisema kuwa ili kuweza kukabiliana na baadhi ya changamoto hizo za upotevu wa mazao baada ya kuvuna, Wizara ya Kilimo imetayarisha Mkakati wa Taifa wa miaka 10 wa Usimamizi wa Mazao baada ya Kuvunwa.

Alisema kuwa Mkakati huo umeandaliwa ili kuendana na malengo endelevu ya dunia ya kutokomeza njaa ifikapo 2030, kuhakikisha usalama wa chakula na lishe na kukuza kilimo endelevu kama lengo la pili la Umoja wa Mataifa kati ya Malengo 17.

“Katika utafiti uliofanyika inakadiriwa kuwa ifikapo mwaka 2050 watu watakuwa bilioni tisa (9) na hivyo mahitaji ya chakula yatakuwa asilimia 60 zaidi ya mahitaji ya sasa. Hivyo basi mkazo utakuwa kuzalisha chakula kati ya asilimia 50 – 70 zaidi ya sasa. Hivyo, udhibiti wa upotevu wa mazao ya chakula ni suala muhimu na la kipekee” Alikaririwa Mhe Hasunga na kuongeza kuwa

Mkakati huo utakuwa Mwongozo kwa Sekta za Umma na Binafsi katika kukabiliana na changamoto ya upotevu wa Mazao baada ya mavuno. Aidha, Mkakati huo umezingatia mabadiliko yanayoendelea ya Kitaasisi na Kisera.

Alisema, suala la udhibiti wa upotevu wa mazao ya chakula ni suala muhimu na la kipeee, linalopaswa kupewa kipaumbele na kila Mdau katika mnyororo wa thamani na shabaha yetu ni kupunguza upotevu kwa asilimia 50 ya mazao ya chakula ifikapo 2025.

Waziri Hasunga ametaja Mkakati huo kuwa una malengo makuu tisa ambayo ni Kujenga uelewa  kuhusu usimamizi wa mazao baada ya kuvuna ili kuboresha ufanisi na kupunguza upotevu wa mazao katika mnyororo wa thamani; Kuhamasisha upatikanaji, ufikiaji, unafuu na utumiaji wa teknolojia na mbinu zilizothibitishwa kupunguza upotevu wa mazao baada ya kuvuna; Kuwezesha mifumo ya masoko ya kilimo, ili kuboresha upatikanaji wa soko na kupunguza upotevu wa mazao baada ya kuvuna; na Kuhamasisha tatifi na uvumbuzi wa teknolojia mpya inayoendana na mazingira yetu pamoja na mbinu za kupunguza upotevu wa mazao.

Mikakati mingine ni Kupitia na kuweka sheria mpya ili kuhakikisha kuwa viwango vya ubora vinazingatiwa kwa mujibu wa sheria ili kupunguza upotevu baada ya kuvuna; Kuimarisha uwezo wa taasisi, uratibu, ushirikiano, ubia na ushiriki wa Wadau wa usimamizi wa upotevu baada ya kuvuna katika kuimarisha utekelezaji malengo ya kimkakati; Kutengeneza mifumo ya usimamizi wa mazao  baada ya kuvuna ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi; Kukabiliana na upungufu wa fedha katika kugharamia usimamizi wa mazao baada ya kuvuna; na Kuwa na mbinu za kiwango kinachokubalika za kukusanya taarifa za upotevu wa mazao baada ya kuvuna nchini.

Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na wadau wengine wameandaa mpango wa kutekeleza Mkakati huo. Ili kutekeleza mpango na malengo hayo kwa ufanisi ni vema kushirikikana Wadau wote kwenye mnyororo wa thamani.


Share:

Wawekezaji Nchini Watakiwa Kufuata Sheria Za Kazi

Na; Mwandishi Wetu
Wawekezaji wameshauriwa kufuata taratibu, kanuni na sheria za kazi zilizopo nchini ili kuongeza ufanisi na tija katika sekta ya kazi.

Hayo ameyasema na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alipotembelea Shamba la Katani la China State Farms lililopo wilayani Kilosa ikiwa ni ziara yake ya kutembelea maeneo ya kazi.

Akizungumza mara baada ya kuwasili katika  shamba hilo alieleza kuwa wawekezaji wakiwa kama waajiri lazima wahakikishe wanafuata sheria za kazi katika maeneo yao ya uzalishaji kwa kuzingatia masuala ya msingi ya wafanyakazi ili waweze kuzalisha kwa tija na kuwahamasisha kufanya kazi zao kwa juhudi.

 “Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli imeendelea kuboresha mazingira ya biashara ambayo yamekua yakivutia zaidi wawekezaji, hivyo sera nzuri zilizopo nchini zimekuwa chachu kwa wawekezaji kuwekeza katika nchi yetu,” alisema Mhagama

Alieleza pia, endapo wawekezaji watafuata miongozo ya kisheria katika masuala ya kazi na ajira yatawarahisishia utendaji wao wa kazi.

Akitolea mfano kuhusu masuala ya kuongeza ujuzi kwa wafanyakazi, likizo ya uzazi kwa wanawake, uwazi wa mikataba ya ajira, uhuru wa mfanyakazi kujiunga na chama cha wafanyakazi, haki ya kupatiwa vitendea kazi na maslahi ya wafanyakazi ni baadhi ya vitu vya msingi ambavyo mwekezaji inabidi atoe kwa mfanyakazi wake kwa kuzingatia taratibu na sheria.

Hata hivyo aliongezea kuwa ushirikiano na vyama vya wafanyakazi ni jambo la muhimu kwa kuwa vimekuwa vikitetea masuala ya wafanyakazi ambayo yamekuwa yakijitokeza katika maeneo yao ya kazi, pamoja na kuwa na mkataba wa hali bora za wafanyakazi baina ya mwajiri na mwajiriwa.

Sambamba na hilo Mheshimiwa Mhagama alitoa maagizo kwa timu ya wataalamu ambao aliambatana nayo kutoka Idara ya Kazi, Wakala wa Usalama na Afya mahala pa Kazi (OSHA), Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya jamii (NSSF), Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Tume ya Usuluhisi na Uamuzi pamoja na Viongozi wa vyama vya Wafanyakazi kuendelea kutoa elimu kwa umma hususan wafanyakazi ili watambue sheria za kazi na namna taasisi hizo zinaweza kuwasaidia katika kupata ufumbuzi wa masuala yao ya kazi.

 Aidha, Waziri Mhagama alitoa pongezi vilevile kwa wawekezaji wa Shamba la Katani la China State Farms kwa kuwajali wafanyakazi wao ikiwa na kuwajengea nyumba bora za kuishi wafanyakazi wao.

“Nimpongeze mwekezaji kwa kuona umuhimu wa kuwajengea makazi wafanyakazi ambayo yatamaliza kabisa tatizo la upatikanaji wa nyumba na umbali ambao wafanyakazi wamekua wakitumia kwenda kazini,” alisema Mhagama

Pia, alitumi muda huo kuwahamasisha wafanyakazi kutumia muda wao wa ziada katika mashamba yao binafsi na kujiunga kwenye mashamba ya ushirika yatakayo wawezesha kupata soko la uhakika kutoka kwa mwekezaji huyo ili waweze kuimarika kiuchumi.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe. Adam Mgoyi alisema kuwa Sheria za kazi zimekuwa zikitoa mwongozo mzuri kwa wawekezaji katika kuimarisha shughuli zao za uzalishaji, kutoa ajira pamoja na kuchangia kwenye mapato ya nchi.

Kwa upande wake, Meneja wa Kiwanda hicho Bw. Majuto Chitema alitoa pongezi zake kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kusifu juhudi alizonazo katika kuboresha na kuwajengea mazingira wezeshi wawekezaji, kwani serikali yake imeweza mstari wa mbele kuweka sera, miongozo, kanuni na sheria ambazo zimekuwa haziwabani wawekezaji.

Miongoni mwa Wafanyakazi wa China Estate Farms Bw. Azory Andrea alisema kuwa Serikali iendelee kuangalia namna ya kuwa kuwasimamia wawekezaji waliopo nchini ili waweze kutekeleza wajibu wao kwa wafanyakazi kwa mujibu wa sheria za kazi.

Kabla ya ziara hiyo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama aliwasili katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kupata taarifa ya maeneo aliyoandaliwa kutembelea katika ziara yake mkoani hapo.


Share:

Waasi wa Yemen Wanaoungwa Mkono na Iran Wshambulia Kwa Makombora Gwaride la Kijeshi La Saudi Arabia na Imarat na Kuua Wanajeshi 60

Makombora yaliyorushwa na waasi wa Kihouthi wanaoungwa mkono na Iran katika mji wa Aden ulio kusini mwa Yemen pamoja na mashambulizi kadhaa ya kujitoa muhanga yameuwa zaidi ya wanajeshi 60  na kuwajeruhi wengine kadhaa.

Shahidi mmoja aliliambia shirika la habari la Reuters kwamba aliona miili tisa baada ya mripuko kutokea kwenye kambi ya kijeshi inayomilikiwa na kikosi maalum cha Yemen kinachoungwa mkono na Umoja wa Falme za Kiarabu, ambayo imo kwenye muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia kupambana na Wahouthi.

Kwa mujibu wa chanzo kimoja cha hospitali, miongoni mwa watu 51 waliouawa, yumo kamanda wa kijeshi. Chanzo chengine kilicho karibu na jeshi la serikali kimemtambua kamanda huyo kuwa Brigedia Jenerali Muneer al-Yafee, mmoja wa viongozi wakubwa wa kijeshi kusini mwa Yemen.

Yafee alikuwa ndio kwanza ameshuka jukwaani kumuamkia mgeni rasmi wakati bomu liliporipuka. Kwenye gwaride hilo, bendera za zamani za iliyokuwa Yemen Kusini na zile za makundi yanayounga mkono ushirika wa kijeshi dhidi ya Wahouthi zilikuwa zimetanda, huku bendi ya kijeshi ikitumbuiza.

Mashahidi wanasema wanajeshi walisikika wakipiga makelele na kuwakimbilia waliojeruhiwa kuwawahisha hospitalini. Sare, viatu, na vifaa vyengine vya kijeshi vilikuwa vimechawanyika aridhini na huku vikiwa vimetapakaa damu.

Shirika la Madaktari Wasiokuwa na Mipaka (MSF) lilituma taarifa kupitia mtandao wa Twitter kwamba makumi ya watu waliojeruhiwa wanapatiwa matibabu mjini Aden baada ya mripuko huo, lakini baadaye shirika hilo lilisema kwamba mashambulizi mengine tafauti yalifanyika kwenye kituo kimoja cha polisi kusini mwa mji huo wa bandari. Taarifa hiyo ilisema watu kumi waliuawa na wengine 16 kujeruhiwa.

Kituo rasmi cha televisheni kinachoendeshwa na Wahouthi, Al Masirah, kilisema kundi hilo lilifanya mashambulizi kwa kutumia makombora ya masafa ya kati na ndege isiyo rubani dhidi ya gwaride hilo la kijeshi, ambalo kimesema lilikuwa ni matayarisho ya uvamizi dhidi ya majimbo yanayoshikiliwa na kundi hilo.

Chanzo chengine kimeliambia shirika la habari la AP kuwa bomu liliripuka nyuma ya jukwaa ambalo sherehe zilikuwa zikifanyika kwenye kambi ya kijeshi ya Al Jalaa wilaya ya Buraiqa.

Muungano unaoungwa mkono na mataifa ya Magharibi ukiongozwa na Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu uliingia kijeshi nchini Yemen mwaka 2015 kwa madai ya kuirejesha madarakani serikali inayotambuliwa kimataifa iliyokuwa imepinduliwa mwaka 2014 mjini Sanaa na Wahouthi.

Hata hivyo, wengi wanasema lengo la uvamizi huo wa kijeshi lilikuwa ni kuizuwia Iran kujipenyeza kwenye taifa hilo masikini la Kiarabu kupitia utawala wa Kihouthi, ambao nao ni sehemu ya madhehebu ya Shia.


Share:

Korea Kaskazini Yafyatua Kombora Jingine la Tatu

Korea kaskazini imefyatua kombora la masafa mafupi ambalo halijabainika mara mbili , kwa mujibu wa maafisa wa Korea Kusini , katika jaribio la tatu la silaha hizo katika kipindi cha wiki moja pekee.

Ufyatuaji wa makombora hayo ulifanyika katika eneo la mwambao wa mashariki mwa taifa hilo mapema Ijumaa.

Hatua hiyo inaonekana kama hatua ya taifa hilo inayolenga kujibu mazoezi ya kijeshi ya baina ya Korea Kusini na Marekani yanayotarajiwa kuanza mwezi huu.

Wakati huo huo Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zimeitaka Korea kaskazini kushiriki mazungumzo ya "maana " na Marekani.

Baada ya mkutano wa faragha katika baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa , mataifa yalisema kuwa vikwazo vya kimataifa vinapaswa kuimarishwa hadi utawala wa Pyongyang utakapoangamiza mipango yake ya nyuklia ya makombora ya masafa.

Ufyatuaji wa makombora hayo ulifanyika katika eneo la Yonghung katika jimbo la South Hamgyong katika bahari ya Japan, inayofahamika pia kama Bahari ya Masharik , kwamujibu wa Mkuu wa kikosi cha pamoja cha Korea kaskazini na Korea Kusini (JCS).

Eneo hilo linaonekana kama kituo cha kufyatulia makombora ambacho hakijawahi kutumiwa awali , amesema Ankit Panda, afisa katika shirikisho la wanasayansi wa Marekani - Federation of American Scientists.

"Hiki ni kielelezo kingine cha enzi ya Kim Jong-un zaidi ya ufyatuaji wa makombora ya usiku : kufyatua kutoka vituo ambavyo havikuwahi kutumiwa awali au ambavyo havitumiwi"
 
Akizungumza katika ikulu ya White House, rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa hana hofu na ufyatuaji wa hivi karibuni wa  makombora kwasababu ni ya masafa mafupi na "ni ya kiwango cha kawaida ".



Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Ijumaa 02 August

























Share:

Thursday, 1 August 2019

Africa Initiative for Governance (AIG) Scholarships 2020/2021 for Study in the University of Oxford UK (Fully Funded)

Africa Initiative for Governance (AIG) Scholarships 2020/2021 for Study in the University of Oxford, UK (Fully Funded). Application Deadline: September 23, 2019 Every year, Africa Initiative for Governance (AIG) will fund five scholarships for outstanding individuals from West Africa to pursue the Master of Public Policy degree at the Blavatnik School of Government, University of Oxford. AIG Scholars… Read More »

The post Africa Initiative for Governance (AIG) Scholarships 2020/2021 for Study in the University of Oxford UK (Fully Funded) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Call for Proposals: Women’s Peace and Humanitarian Fund& Spotlight Initiative

Call for Proposals: Women’s Peace and Humanitarian Fund& Spotlight Initiative. Application Deadline: August 23, 2019. The Women’s Peace & Humanitarian Fund is excited to announce its first call for proposal in Nigeria. Apply for new funding opportunities that support your local women’s civil-society organization. WPHF seeks to fund qualifying projects in Nigeria that are high impact, innovative, and… Read More »

The post Call for Proposals: Women’s Peace and Humanitarian Fund& Spotlight Initiative appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Thomson Reuters Foundation 2019/2020 Reporting on Illicit Finance in Africa workshop for African Journalists (Fully Funded to Cape Town, South Africa )

Thomson Reuters Foundation 2019/2020 Reporting on Illicit Finance in Africa workshop for African Journalists (Fully Funded to Cape Town, South Africa ) Application Deadline: 13th August 2019 Thomson Reuters Foundation, in partnership with the Institute for the Advancement of Journalism, is looking for journalists based anywhere in Africa who are motivated to understand how their country could be… Read More »

The post Thomson Reuters Foundation 2019/2020 Reporting on Illicit Finance in Africa workshop for African Journalists (Fully Funded to Cape Town, South Africa ) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Standard Bank Industry 4.0 Challenge 2019 for high technology Entrepreneurs (Fully Funded to ITU Telecom World 2019 in Budapest, Hungary)

Standard Bank Industry 4.0 Challenge 2019 for high technology Entrepreneurs (Fully Funded to ITU Telecom World 2019 in Budapest, Hungary) Application Deadline: August 5th 2019 In Partnership with Department of Telecommunications and Postal Services Standard Bank is assisting with identifying and supporting 5 high technology entrepreneurs. 5 Selected companies will receive development support and and an opportunity to… Read More »

The post Standard Bank Industry 4.0 Challenge 2019 for high technology Entrepreneurs (Fully Funded to ITU Telecom World 2019 in Budapest, Hungary) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Vital Voices (VV) GROW Fellowship 2020 Global Accelerator Program for Female Entrepreneurs

Vital Voices (VV) GROW Fellowship 2020 Global Accelerator Program for Female Entrepreneurs VV GROW FELLOWSHIP Research indicates that the real drivers of the global economy are women. As business leaders, employees, consumers and entrepreneurs, women are accelerating economic growth and improving conditions in their communities. Despite the proven benefits of women’s economic engagement, women business owners face disproportionate barriers in growing… Read More »

The post Vital Voices (VV) GROW Fellowship 2020 Global Accelerator Program for Female Entrepreneurs appeared first on Udahiliportal.com.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger