Tuesday, 28 May 2019

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne May 28




Share:

Monday, 27 May 2019

Picha : MASHINDANO YA MICHEZO YA UMISSETA 2019 YAFUNGULIWA SHINYANGA...RC TELACK ATAKA WANAFUNZI KUONESHA VIPAJI VYAO


Mashindano ya Umoja wa Michezo na Sanaa kwa shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA) yamefunguliwa rasmi mkoani Shinyanga, ambapo wanafunzi wataonyesha vipaji vyao kwa kushiriki katika michezo mbalimbali.

Mashindano hayo ya (UMISSETA) yamefunguliwa leo Mei 27,2019 na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainabu Telack kwenye viwanja vya michezo vya CCM Kambarage Shinyanga Mjini na kuhudhuriwa na wanafunzi wa shule za sekondari kutoka halmashauri sita za mkoa huo sambamba na kusindikizwa na wadogo zao wa shule za msingi.

Michezo ambayo itashindaniwa ni mpira wa miguu, Mpira wa pete, kikapu, Wavu, Mikono, Riadha, Mpira wa Meza, kucheza ngoma, pamoja na kuimba kwaya, ambayo itadumu kwa muda wa siku tatu, ambapo washindi watakwenda kushindana kitaifa.

Akifungua mashindano hayo,Telack aliwataka wanafunzi hao kudumisha nidhamu kwenye mashindano hayo hata wale ambao watachaguliwa kwenda Mtwara kushiriki kitaifa wakaonyeshe nidhamu ya hali ya juu.

Alisema michezo ni afya, humjenga mtoto kiakili,kinidhamu, kuibua vipaji na hivyo kusikitishwa na shule binafsi ambazo zimezuia wanafunzi wao kushiriki kwenye michezo hiyo na kuwataka waiche tabia hiyo mara moja, ikiwa huko ni kumnyima mtoto kuonyesha kipaji chake na kuweza kupata ajira hapo baadae.



“Kuna taarifa tunazo eti baadhi ya shule binafsi zimezuia wanafunzi wao kutoshiriki michezo hii ya UMISSETA, ni jambo la ajabu sana, mfano baba yake na Mbwana Samatta angekuwa wakimzuai mtoto wake kushiriki kwenye michezo leo asingekuwa mchezaji wa kimataifa, hebu waruhusuni watoto wenu  waonyeshe vipaji vyao kwani michezo ni ajira pia,”aLIsema Telack.

“Na niye wanafunzi ambao mnashiriki michezo hii ya UMMISSETA naombeni muonyeshe vipaji vyenu ambavyo mmepewa na Mungu, pamoja na kudumisha nidhamu ya hali ya juu hata huko mtakapokwenda Mtwara na siyo kwenda kuendekeza mapenzi, nataka muje na makombe hapa ya ushindi likiwEmo la nidhamu,”aliongeza.

Pia aliziagiza halmshauri zote za mkoani humo kutenga bajeti ya kila mwaka wa fedha shilingi Milioni 2 kwa ajili ya kufanikisha michezo hiyo ya UMISSETA licha ya kupata fedha zingine kutoka wahisani ili kuwa rahisishia maisha wanafunzi wakaokuwa kambini.

Kwa upande wake Ofisa Elimu mkoa wa Shinyanga Mohamed Kahundi akisoma risala ya ufunguzi wa michezo hiyo ya UMMISSETA, alisema changamo ambayo wanakabiliana nayo kuendesha mashindano hayo hadi ngazi ya taifa ni ukata wa fedha na hivyo kuomba wahisani waendelee kujitokeza kufadhili michezo hiyo.

Alisema kwa mwaka jana (2018) mkoa ulifanikiwa kupeleka timu kwenye mashindano ya kitaifa, lakini haukufanya vizuri kwani ulishika nafasi ya 20 kati ya 28 sababu ya maandalizi kuwa mabaya kutokana na upungufu wa rasilimali fedha ambapo hata baadhi ya timu zilishindwa kuzipeleka kushiriki kwenye mashindano hayo.


Kauli mbiu ya  (UMISSETA) mwaka huu inasema "michezo na sanaa kwa elimu bora na ajira".


TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack akizungumza kwenye ufunguzi wa michezo ya UMISSETA kwa shule za Sekondari mkoani Shinyangana kuwataka wanafunzi waitumie michezo hiyo kuonyesha vipaji vyao, ikiwa michezo ni afya pamoja na ajira na kukemea shule binafsi ambazo zimezuia wanafunzi wao wasishiriki michezo hiyo.Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack akiwataka wanafunzi ambao wanashiriki michezo hiyo ya UMISSETA wadumishe nidhamu kwenye michezo hiyo pamoja na kupata ushindi wa makombe mengi pale watakapo kwenda kuishiriki ngazi ya kitaifa.

Afisa Elimu mkoa wa Shinyanga Mohamed Kahundi akisoma risala kwenye ufunguzi wa michezo hiyo ya UMISSETA na kumuomba mgeni rasmi mkuu wa mkoa kuwatafutia wafadhili ambao watakuwa wakifadhili michezo hiyo kila mwaka pamoja na halmashauri kutenga fedha za mapato ya ndani, ili kuondoa changamoto ya ukata wa Fedha na kusababisha kufanya vibaya kwenye mashindo ya kitaifa kama ilivyotokea mwaka jana.

Awali mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akimkaribisha mkuu wa mkoa huo wa Shinyanga Zainab Telack kufungua michezo hiyo ya UMISSETA kwa shule za sekondari ambayo itadumu kwa muda wa siku tatu.

Wanafunzi wakiwa kwenye ufunguzi wa mashindano ya michezo ya UMISSETA Mwaka (2019) mkoani Shinyanga yaliyofanyika kwenye uwanja wa michezo wa CCM Kambarage.

Wanafunzi wakiwa kwenye ufunguzi wa michezo ya (UMISSETA) Mkoani Shinyanga.

Wanafunzi wakiwa kwenye ufunguzi wa michezo ya (UMISSETA) Mkoani Shinyanga.

Wanafunzi wakiwa kwenye ufunguzi wa michezo ya (UMISSETA) Mkoani Shinyanga.

Wanafunzi wakiwa kwenye ufunguzi wa michezo ya (UMISSETA) Mkoani Shinyanga.

Viongozi mbalimbali wa Serikali na wa kidini wakishuhudia ufunguzi wa michezo hiyo ya shule za Sekondari (UMISSETA) Mkoani Shinyanga.

Viongozi mbalimbali wa Serikali wakishuhudia ufunguzi wa Mashindano ya UMISSETA  Mkoani Shinyanga.

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akitoa cheti cha Shukrani kwa meneja wa Benki ya CRDB Mkoani Shinyanga Said Pamui kwa kufadhili kutoa Makombe 24 ambayo watakabidhiwa washindi katika michezo hiyo ya (UMISSETA) Mkoani Shinyanga.

Meneja wa Benki ya CRDB Mkoani Shinyanga Said Pamui akipanga makombe kabla ya kumkabidhi mkuu wa mkoa huo wa Shinyanga Zainab Telack ambayo watapewa washindi kwenye michezo hiyo ya Shule za Sekondar UMISSETA.

Meneja wa Benki ya CRDB Mkoani Shinyanga Said Pamui akimkabidhi Kombe mkuu wa mkoa huo Zainab Telack kwa ajili ya kukabidhiwa washindi kwenye michezo ya UMISSETA mkoani Shinyanga.

Wafadhili kutoka Taasisi ya kifedha NMB nayo ikikabidhii Tracksuit kwa ajili ya wachezaji wa michezo hiyo ya (UMISSETA) mkoani Shinyanga.

Shule binafsi ya Savannah Plains Highschool ya mkoani Shinyanga nayo ikifadhili Tshirt 100 kwa ajili ya washiriki wa michezo hiyo ya UMISSETA .

Awali wanafunzi wakiingia kwa maandamano kwenye ufunguzi wa michezo hiyo ya Shule za Sekondari (UMISSETA) Mkoani Shinyanga.

Wanafunzi wakiingia kwa maandamano kwenye ufunguzi huo wa michezo ya UMMISETA.

Wanafunzi wakionyesha jumbe za mabango kwenye ufunguzi wa michezo ya (UMISSETA) Mkoani Shinyanga.

Awali mgeni Rasmi mkuu wa mkoa wa Shinyanga akiwasili kwenye uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga Mjini kwa ajili ya kufungua michezo hiyo ya shule za sekondari UMISSETA.

Mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack katikati akiwasili kwenye uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga Mjini kwa ajili ya kufungua michezo hiyo ya UMISSETA.

Wanafunzi wakiimba nyimbo ya taifa kwa ajili ya kuwa tayari kufungua michezo hiyo ya shule za Sekondari (UMISSETA) Mkoani Shinyanga.

Mpira wa miguu ukichezwa kwenye ufunguzi wa michezo hiyo ya UMISSETA Mkoani Shinyanga kati ya watumishi wa Benki ya CRDB na watumishi kutoka serikalini ambapo walitoka bila bila.

Na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog
Share:

Breaking : LAZARO NYALANDU AKAMATWA


Aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu amekamatwa na watu wanaodhaniwa kuwa ni Polisi akiwa anasimamia uchaguzi wa kata wa Chadema mkoani Singida.

 Mkurugenzi wa Itikadi na Uenezi John Mrema
Share:

JAMAA AUA MAMA MJAMZITO,JIRANI NA MAMA MKWE AKIDAI WANAJUA SIRI YA MCHEPUKO

Mtu mmoja ajulikanaye kwa jina la Michael John Mwandu mwenye umri wa miaka 54 mkazi wa Dumila wilaya ya Kilosa amejiua mwenyewe kwa kunywa sumu baada ya kufanya mauaji ya kumuua mke wake Leonola Ernest mwenye miaka 37 akiwa na ujauzito wa miezi kati ya 7 hadi 8.

Tukio hilo limetokea tarehe 24/5/2019 usiku huko Dumila mkoani Morogoro.

Akizungumza na waandishi wa habari Leo Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro ASCP Wilbrod Mutafungwa amewataja marehemu wengine kuwa ni mama mkwe wa muuaji Magreth Yohana mwenye umri wa miaka 59,Salma Iddi jirani yao mwenye umri wa miaka 52 na pamoja yeye mwenyewe marehemu Michael John ambaye amejiua baada ya kufanya mauaji hayo.

 Chanzo cha vifo hivyo ni wivu wa kimapenzi alioubaini akimtuhumu mke wake kuwa na mahusiano na mwanaume mwingine huku akidai hao wengine walikuwa wakifahamu jambo hilo.

Marehemu ametumia panga kumuua mama yake mkwe huku yeye na marehemu wengine wakinywa sumu aina ya Carbon Furan ambayo ni dawa ya kuua wadudu kwenye mimea
Baadhi ya waandishiwa habari wakimsikiliza Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro ASCP Wilbrod Mutafungwa wakati akizungumzia mauaji hayo.
Baadhi ya ushahidi ulioonyeshwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro ACP Wilbrod Mutafungwa.
Share:

Shule za Sekondari 1241 Zajengewa Mabweni

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa ,na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Seleman Jafo, amesema hadi sasa shule za sekondari 1,241 zimejengewa mabweni kati ya shule za sekondari 3,634 zilizopo kwa kutumia ruzuku kuu.

Jafo amesema hayo leo Jumatatu Mei 27, bungeni jijni Dodoma, wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Azza Hilaly Hamad (CCM).

Katika swali lake, Azza alihoji serikali ina mkakati gani wa kujenga mabweni katika shule za sekondari zilizoanzishwa kitarafa ili kuwasaidia watoto wa kike kupata elimu bora.


Share:

Almasi Yenye Thamani ya Bilioni 3.2 Yaipaisha Sekta ya Madini Tanzania

Na Mwandishi Wetu-MAELEZO
Tanzania imetajwa kuweka historia katika tasnia ya madini baada ya Almasi yenye Karati 512.15 kupatikana hivi karibuni katika eneo la Maganzo Mkoani Shinyanga  na kuuzwa kwa jumla ya shilingi Bilioni 3.2.
 
Akizungumza katika mahojiano maalum kuhusiana na madini hayo,Naibu  Waziri wa Madini Mhe. Stanslaus  Nyongo amesema kuwa  kutokana na kupatikana kwa almasi hiyo Serikali itapata mapato ya takribani shilingi  milioni 235,000/- kama kodi na tozo mbalimbali ikiwemo mrabaha ambayo yamelipwa Serikalini baada ya mauzo hayo.
 
Kuuzwa kwa jiwe hilo moja la almasi katika soko la madini mkoani Shinyanga ni muendelezo wa tija inayopatikana kupitia masoko hayo toka kuanzishwa kwake nchini,jumla ya shilingi bilioni 34.3 zimepatikana kwenye biashara ya dhahabu iliyofanyika katika kipindi cha mwezi mmoja tu kati ya Machi 17 mpaka Aprili 17 mwaka huu katika masoko ya madini kote nchini, kwa mujibu waziri wa Madini,Doto Biteko, aliyetoa taarifa hiyo hivi karibuni.
 
“Natoa wito kwa wachimbaji wote,madalali na mawakala,kuyatumia ipasavyo masoko hayo kwakuwa kila mmoja atapata stahiki yake tofauti na awali kabla ya kufunguliwa kwa masoko hayo ambapo wachimbaji hawakuwa kwenye mikono salama kufutia kutokuwa na mfumo rasmi wa uuzaji madini yao”.Alisisitiza mhe. Nyongo
 
Akifafanua amesema kuwa kila mchimbaji anapaswa kuzingatia sheria na Kanuni za sekta ya madini ili kuepuka mkono wa sheria na hatua nyingine ikiwa ni pamoja na kutaifishwa kwa madini yao pale watakapobainika kutaka kutorosha madini ama kujihusisha na magendo.
 
Aliongeza kuwa baada ya kupatikana kwa almasi hiyo wataalamu wa Wizara hiyo walifanya tathmini ili kuona ubora wake na kiwango kilichopatikana ili kuhakikisha kuwa Serikali inapata mapato yake.
 
“ Serikali ya Awamu ya Tano imeweka makazo katika kuimarisha sekta ya madini nchini ili itoe mchango unaostahili katika uchumi wetu ndio maana tunaona kuwa kupitia masoko ya madini tuliyoanzisha hata mchimbaji huyu aliyepata hii almasi pale Maganzo aliiuza kupitia soko letu la madini baada ya kufuata taratibu zote” alisisitiza Mhe. Nyongo

Tanzani ni moja ya nchi zenye utajiri mkubwa wa madini ya aina mbalimbali ikiwemo Almasi, Tanzanite, Dhahabu na mengine mengi.
 
Serikali ya Awamu ya Tano imeweka mkazo katika kuimarisha sekta ya madini ikiwemo kuimarisha taratibu za uuzaji wa madini yote yanayozalishwa hapa nchini, kuimarisha usimamizi, kuwawezsha wachimbaji wadogo ili waweze kuchimba kwa tija.


Share:

Serikali kujenga viwanda vya kusindika mazao ya uvuvi nchini

Serikali inatarajia kujenga viwanda vya kusindika mazao ya uvuvi nchini kupitia Shirika la Uvuvi Tanzania (Tafico).

Hayo yameelezwa leo Jumatatu Mei 27 na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega wakati akijibu swali la Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema).

Katika swali lake Kubenea, lililoulizwa kwa niaba yake na Mbunge wa Viti Maalumu, Tunza Malapo (Chadema), alihoji ni lini na ni wapi Kiwanda cha Samaki cha Pwani kitajengwa hapo.


Share:

Mifuko Ya Fidia Kwa Wafanyakazi Ya Zambia Na Tanzania Yasaini Mkataba Wa Ushirikiano

NA Mwandishi wetu, Dodoma
TANZANIA na Zambia kupitia Mifuko ya Fidia kwa Wafanyakazi, wamesaini mkataba wa ushirikiano utakaosaidia kubadilishana uzoefu kati ya mifuko hiyo.

Akizungumza mara baada ya kutiliana saini mkataba huo, kwenye ofisi za WCF jijini Dodoma Jumatatu Mei 27, 2019, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Masha Mshomba alisema, Zambia inauzoefu wa zaidi ya miaka 40 katika sekta ya hifadhi ya jamii katika kulipa mafao ya Fidia kwa Wfanyakazi kwa hivyo makubaliano hayo yana manufaa makubwa.

Alisema makubaliano hayo ni ya kawaida kati ya mifuko na kwamba WCF na WCFCB watabadilishana uzoefu katika masuala ya namna ya ulipaji mafao, namna ya kuzuia ajali na magonjwa kazini kwa sababu mambo hayo ni muhimu sana katika mifuko ya fidia.

“Nguvu kazi ya taifa inapolindwa tija huongezeka makazini na jambo hili hudhihirika pale pato la taifa linaongezeka hususan kwetu sisi ambao tunajenga uchumi wa viwanda jambo hilo ni muhimu sana.”Alisema Bw. Mshomba.

Alisema kwa uzoefu ambao Zambia watakuwa wameupata kutoka kwao wataweza kuboresha huduma zao, na tayari Dkt. Nkumbula amethibitisha kuwa serikali ya Zambia inautegemea Mfuko huo katika kusaidia nguvu kazi ya taifa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Zambia (WCFCB), Dkt. Elizabeth Lungu Nkumbula alisema, imekuwa ni siku njema kwao kwa kujenga ushirikiano wa pamoja katika eneo la hifadhi ya jamii.

“Zambai na Tanzania chini ya uongozi wa Dkt. Keneth Kaunda na Mwalimu Nyerere, waliweza kujenga reli ya TAZARA na bomba la mafuta TAZAMA kwa hivyo ushirikiano huu wa leo ni kumbukumbu ya ushirikiano uliojengwa kwa muda mrefu na viongozi hao wa mataifa hayo mawili.” Alifafanua.

AlIsema ushirikiano huu utasaidia pande mbili kubadilishana uzoefu katika kutoa huduma za ulipaji fidia na mbinu za kuzuia majanga yatokanayo na kazi na hivyo kusaidia mataifa hayo kukuza uchumi.


Share:

Mradi Wa Reli Ya Kisasa (SGR), Mwamba Wa Changamoto Za Usafirishaji Nchini

 Na Paschal Dotto-MAELEZO
Ni Takribani Miaka 120 ambapo historia iliandikwa, mwaka 1912, Serikali ya Kikoloni nchini iliamua kuimarisha sekta ya usafirishaji Kwa kujenga Reli, ambapo njia zake ziliunganisha Miji hasa maeneo ya kilimo, uzalishaji na kibiashara, reli kuu kutoka Dar es Salaam mpaka Mwanza, hatimaye Kigoma na Tanga.

Ni dhahiri sasa tunaona Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akifanya mageuzi makubwa Kwa kujenga reli ya kisasa, maarufu SGR (Standard Gauge Railway) ambapo kwa vyovyote tutasogeza nyuma zaidi kuhusu historia ya reli nchini, kwani Rais anatakeleza Ujenzi wa Reli ya Kisasa, Standard Gauge Railway (SGR) kwa maslahi makubwa kiuchumi.

Katika hafla ya uwekaji wa Jiwe la msingi la ujenzi wa Reli ya SGR awamu ya pili, Morogoro-Makutupola, iliyofanyika 14, Machi, 2018, Rais Magufuli aliwakumbusha Watanzania kuwa Tanzania imekuwa nchi ya pekee Barani Afrika katika kutekeleza mradi huo mkubwa kwa pesa za walipa kodi wake.

“Kwa bahati nzuri, hivi karibuni tulitembelewa na Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, na alishuhudia kwamba Tanzania tumetayarisha fedha zetu wenyewe, kwa nguvu zetu wenyewe, na walipa kodi ni watanzania wenyewe, Tsh Trilioni 2.8 na kutangaza tenda zilizokuwa wazi, makampuni zaidi ya 40 yalijitokeza kuwania tenda, na bahati nzuri kampuni kutoka Uturuki ikashinda tenda hii,” alisema Rais Magufuli na kuongeza kuwa Uturuki itatupa mkopo wa masharti nafuu kwa awamu zingine za ujenzi, Rais akaongeza, “ kwa hiyo Tanzania tunaweza”,

Rais Magufuli aliwataka watanzania kutambua fursa za upitapo mradi wa SGR na kuwataka wafanyabiashara wakubwa, wadogowadogo, mama ntilie, kunufaika wakati wa ujenzi na mara baada ya ujenzi, na kwamba itakuwa nguzo kubwa kwa usafarishaji kwenye maeneo hayo na nchi nzima.
 
“Katika uchumi wa nchi yoyote duniani, Sekta ya Usafirishaji ni muhimu sana, kwa hiyo Serikali kuchukua hatua madhubuti ya kuimarisha sekta ya usafirishaji kwa kujenga reli ya kisasa, SGR, ni moja ya Mwarobaini wa kutatua changamoto ya usafirishaji mizigo na kulinda usalama wa barabara”. Alisikika mmoja wa wahandisi akiwaeleza waliowatembelea.

Mageuzi ya Rais Magufuli yanalenga kuwaimarisha wananchi, si tu wafanyabiashara bali hata wasafiri kwa utekelezaji wa ujenzi wa Reli ya kisasa, SGR yenye kasi ya 160km/saa utakuwa na faida kuwabwa kwani masaa 2.5 Dar es Salaam-Morogoro na masaa tisa kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza, ni dhahiri kutakuwa na Furaha kubwa kwa watu kuwahi kufika Mwanza mapema badala ya saa saba usiku au kulala Shinyanga.

“Ujenzi wa Reli hii (SGR), kwa Tanzania siyo chaguo bali ni lazima, kwani hatua hii ilitakiwa ifikiwe zamani, lakini sasa Rais Magufuli ameamua kutufikisha kwenye teknolojia mpya katika sekta ya usafirishaji, kwani matatizo mengi ya barabara yanatokea kwababu ya mizigo mizito, hakuna reli imara ya kubeba mizigo hiyo, kwa hiyo ujenzi wa Reli hii ni maamuzi sahihi kwa Serikali yetu.”, Anaeleza Mkurugenzi TRC, Masanja Kadogosa.

Kadogosa anasema, Reli hiyo ambayo inatumia nishati ya umeme imekuja wakati mwafaka ikiwa Serikali inatekeleza mradi mkubwa wa kuzalisha umeme wa Mto Rufiji (Rufiji Hydroelectric Power), wenye kutoa Megawati 2,115, kwa hiyo treni hiyo itapata umeme wa kutosha.
 
“SGR, Ni mradi mkubwa ambao unatekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Magufulu kwa kutumia fedha za walipa kodi wake kwahiyo ni vyema watu wakafahamu kuwa kodi yao inaenda wapi Trilioni 7 siyo mchezo”, alisema Kadogosa.

Ili kutekeleza adhima ya kuutangaza mradi huo kwa wananchi, Mei 17, 2019, Jopo la Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri pamoja na Makatibu Tawala takribani 400 wakiongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Seleman Jafo walitembelea kuona mradi huo ili kupeleka ujumbe kwa wananchi.

Kabla ya Safari hiyo Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa aliwapitisha kidogo wageni wake katika shule ndogo kuhusu mradi ili kutambua umuhimu wa Mradi huo kwenye sekta ya usafirishaji na kwa wananchi.

Masanja alieleza kuwa Reli hiyo inayojengwa inaenda kufuta zana mbalimbaliikiwemo ile historia ya kikoloni, kuwa reli iliyopo ilijengwa na wakoloni, lakini pia ujenzi wa Reli hiyo sasa unaenda kuimarisha sekta ya usafirishaji. Serikali inatekeleza ujenzi huo Kwa Kipande cha Dar es Salaam-Morogoro, Morogoro-Makutupola na badae kutekeleza ujenzi huo hadi Mwanza, kilometa 1,219.

Kadogosa alisema kuwa Reli hiyo, SGR inauwezo wa kubeba tani milioni, 10,000, kwa mkupuo sawa na malori 500 yenye tani 20, Treni tano zenye tani 10,000 na kuwa na kasi kubwa ya 160km/saa, tofauti na ya sasa ambayo inakasi ya 30km/saa, kwa Afrika itakuwa ni Reli pekee yenye uwezo mkubwa kama huo, tani Miliomi 10-17 zitasafirishwa kwa mwaka, kwa hiyo SGR ni mwamba sekta ya usafirishaji nchini.

Aidha, Kadogosa alieleza kuwa ujenzi wa Reli (SGR), Dar es Salaam-Morogoro unatekelezwa na Kampuni kutoka Uturuki, Yapi Merkezi takribani Trilioni 2.7, lakini kwa sehemu nyingine ni Yapi Merkezi na Portuguese Construction Group Motel-Engil.

kukamilika kwa mradi huo kutakuwa na ufanisi mkubwa kwenye sekta ya usafirishaji nchini kwa kubeba mizigo tani nyingi lakini pia kasi yake katika kusafirisha abiria, kutoka Dar es Salaam- Dodoma treni itakuwa inafanya safari mara nane kwa siku, kwa hiyo ni hatua kubwa kwa sekta ya usafirishaji.

Kadogosa alizitaja baadhi ya Faida za Mradi huo Kwa sasa kwa wananchi na uchumi wa nchi kwa ujumla kwani kwa sasa watanzania walioko sehemu za ujenzi wanafaidika na kupeleka malighafi za ujenzi, mama ntilie kupika chakula na biashara zingine.

“Takribani mifuko ya simenti milioni, 9,200,000 ambayo ni sawa na tani 600, nondo kilo milioni 115 sawa na tani 1500 na mataluma 1,400,000, kutoka kwa wasambazaji wa malighafi hizo takribani 500, wafanyakazi 10, 000, huku asilimia 94 ya wafanyakzi hao ni watanzania, pia asilimia 48 ya wataalam ni watanzania, kwa hiyo pamoja na mradi huu  kuwa nguzo imara ya usafirishaji nchini, SGR imekuja kutoa Fursa za ajira kwa watanzania”, Alisema Kadogosa.
Kadogosa alisema kuwa mradi huo ni mkubwa na uwezo wake ni wa juu, na sasa matatizo ya usafarishaji nchini yatapata suluhu kubwa, kuimarisha na kulinda barabara nchini.

Katika sekta ya usafirishaji wa mizigo hasa ile mikubwa inayotoka bandarini kwenda sehemu zingine za nchi na mengine nje ya nchi, kwani kuwepo kwa Reli imara itasababisha utendaji kazi wa bandari kuwa na ufanisi mkubwa, “Bandari inategemea kuwepo kwa miundombinu imara kwa upande wa nchi kavu, hakuna ufanisi wa Bandari bila kuwa na Reli imara, Serikali imeliona hilo ndiyo maana ikaamua kutekeleza haraka ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) na Reli yetu hii inabeba mizigo mingi Takribani Tani Milioni 17 kwa mwaka, hakuna Reli kama hii Barani Afrika” Kadogosa.


Share:

Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani Asema Hakuna Upungufu wa Nyaya wa Nguzo za Umeme

Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani amesema Tanzania haina upungufu wa nguzo za umeme, nyaya wala transfoma hivyo akaomba wakandarasi wa umeme kuacha visingizio.

Dk Kalemani ametoa kauli hiyo bungeni leo Jumatatu Mei 27, 2019 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Nyang’ hwale (CCM), Hussein Amar.

Mbunge huyo ametaka kujua ni kwa nini mkandarasi wa umeme katika jimbo lake ametandaza nguzo lakini hafungi umeme kwa kisingizio cha upungufu wa nyaya.

Waziri amesema kauli kuwa hakuna nyaya za umeme haina ukweli kwani katika kipindi hiki hakuna upungufu wowote kuhusu vifaa hivyo na akaonya kwa wakandarasi wanaotoa sababu hizo waache mara moja na badala yake wakafunge umeme kwa wakati waliopangiwa.


Share:

Rais Magufuli Apokelewa Na Mwenyeji Wake, Rais Hage Geingob Wa Namibia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akipokewa na Mwenyeji wake Rais Hage Geingob wa Namibia alipowasili katika Ikulu ya nchi hiyo, Jijini Windhoek leo Mei 27, 2019. Rais Dkt. Magufuli amewasili nchini Namibia kwa Ziara Rasmi ya Kikazi ya Siku
mbili.



Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger