Jeshi la Polisi Makao Makuu Kitengo Maalum cha Kupambana na uhalifu kikiongozwa na Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Naibu Kamishna Liberatus Sabas, kimeshirikina na Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe kuendesha Operesheni Maalum ya kukabiliana na matukio ya mauaji ya watoto wadogo ambayo yamejitokeza mkoani humo, mpaka sasa watuhumiwa 30 wamekamatwa waliojihusisha na matukio hayo, Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Naibu Kamishna Liberatus Sabas, amesema watuhumiwa hao ifikapo Jumatatu watakuwa wamefikishwa Mahakamani kukabiliana na tuhuma za mauaji ya watoto, Aidha Naibu Kamishna Sabas, amewataka…
Saturday, 9 February 2019
BINTI ALIYETAKA KUWA MKE WA PILI AUAWA KWA KUCHOMWA SEHEMU ZA SIRI

Binti aliyejulikana kwa jina la Joyce Jackson (18) mkazi wa kijiji cha Rusega kata Karenge wilayani Biharamulo, mkoani Kagera ameuawa kwa kuchomwa na vitu vyenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwemo sehemu za siri.
Inaelezwa kwa tukio hilo limetokea Februari 8,2019 majira ya saa moja asubuhi ambapo agundulika kuwa ameuawa ndani ya nyumba alimokuwa akiishi.
Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Revocatus Malimi Joyce alivamiwa na watu wasiojulikana na kumchoma na vitu vyenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwemo sehemu za siri.
Inadaiwa kuwa binti huyo alikuwa katika mipango ya kuolewa na Balushamina Mtondo kama mke wa pili.
Tayari jeshi la polisi wanamshikilia mke wa kwanza wa baba huyo Jenesia Jacobo (29 ) kwa mahojiano zaidi kuhusiana na mauaji hayo.
Na Mwandishi wa Malunde1 blog
HATMA YA CAG,HALIMA MDEE KUJULIKANA BUNGE LIJALO..NDUGAI ASEMA 'TUSIDHARAULIANE'

Bunge limemaliza vikao vyake jijini Dodoma leo Jumamosi Februari 9, 2019 huku Spika, Job Ndugai akisogeza mbele kueleza taarifa za kuhojiwa kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad na mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee.
Januari 21, 2019 Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ilimhoji Profesa Assad aliyeitwa mbele ya kamati hiyo kueleza kauli yake kuhusu “udhaifu wa Bunge.”
Profesa Assad aliitwa mbele ya kamati hiyo kujieleza kuhusu kauli aliyoitoa wakati alipokuwa akihojiwa na Kituo cha Televisheni cha Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa (UN) akiwa New York, Marekani alikokuwa akihudhuria mkutano.
Alitumia neno “udhaifu” wa Bunge alipokuwa akieleza sababu za kutofanyiwa kazi kwa ripoti zake ambazo zimekuwa zikibainisha ufisadi.
Mbali na Assad, Januari 22 kamati hiyo ilimhoji Mdee ambaye aliunga mkono kauli ya CAG kuhusu Bunge.
Akizungumza bungeni leo, Ndugai amesema taarifa za kamati hiyo ziko tayari lakini muda haukutosha kuzisoma hivyo zitasomwa Bunge lijalo.
"Waheshimiwa wabunge taarifa za kamati ya maadili ziko tayari lakini tunakosa muda kama mnavyoona wenyewe, tutazileta katika mkutano ujao," amesema Ndugai
Amesema hana pingamizi na Bunge kukosolewa lakini si kwa kushambulia kama wanavyofanya wengine.
"Tushauriane, tusaidiane lakini tusidharauliane, haiwezekani mtu mmoja kutoka nje na kushambulia Bunge, sisi sote hapa ni watu wazima na tumechaguliwa na Watanzania," amesema.
Na Habel Chidawali, Mwananchi
BUNGE LAAHIRISHWA DODOMA,WAZIRI MKUU ASEMA MAUAJI NJOMBE YANAFANYWA NA WAHUNI WACHACHE
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kasimu Majaliwa leo Jumamosi Februari 9,2019 ametoa hoja ya kuahirisha mkutano wa 14 wa Bunge la 11 jijini Dodoma huku akitoa maagizo kwa watendaji.
Kabla ya kutoa hoja hiyo, Majaliwa amewataka viongozi wa mikoa, wilaya na vijiji kukutana na viongozi wa dini kujadiliana masuala ya maendeleo.
Amesema mkutano uliofanyika kati ya viongozi wa dini na Rais John Magufuli ulikuwa na tija hivyo ni muhimu viongozi wakaiga mfano huo.
Amebainisha kuwa mkutano wa Rais Magufuli na viongozi wa dini ulionyesha viongozi hao wana mchango mkubwa ambao hautakiwi kubezwa.
Kiongozi huyo amegusia mauaji ya watoto mkoani Njombe akisema yanafanywa na wahuni wachache.
Majaliwa amesema kauli ya Serikali iliyosomwa bungeni na Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola ilionyesha hadi sasa watoto saba wameripotiwa kuuawa na mmoja kujeruhiwa.
“Lakini tayari watuhumiwa zaidi ya 29 wamekamatwa kwa uchunguzi," amesema Majaliwa
Waziri Mkuu amesema Serikali inalaani vitendo vyote vibaya vinavyofanywa dhidi ya watoto.
Na Habel Chidawali, Mwananchi
MO DEWJI AWATAJA MASHABIKI WA KWELI SIMBA

Mohammed Dewji
Kuelekea mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba SC dhidi ya Al Ahly Jumanne ijayo, mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi Simba Mohammed Dewji, amesema mashabiki wa kweli ni wale wenye kuishangilia timu katika nyakati zote.
Ujumbe huo wa Mo Dewji anayemiliki asilimia 49 ya hisa za Simba, umekuja siku moja baada ya kuweka wazi mipango ya timu hiyo katika kuhakikisha wanafanya vizuri katika michuano hiyo.
''Nirahisi kujitokeza nakuchukua sifa iwapo Simba itashinda, lakini mashabiki wa kweli ni wale ambao wanajirudi na kushangilia Simba pindi inapopita katika kipindi kigumu. Mashabiki wa kweli wanakuwepo wakati mzuri na wakati mbaya'', ameandika Mo Dewji.
Simba ina kibarua cha kushinda mchezo huo ili iweze kufufua matumaini ya kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo, jambo ambalo Mo Dewji jana aliweka wazi kuwa linawezekana.
Mchezo huo utapigwa kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam Jumanne Februari 12, 2019 kuanzia saa 10:00 jioni. Tayari viingilio vimeshatangazwa ambavyo ni 15,000, 10,000 na 2,000.
TOZO YA USHURU YA MCHUZI WA ZABIBU YAPUNGUZWA TOKA Tsh 3,315 MPAKA Tsh 450,MBUNGE DITOPILE AUNGURUMA
Hatimaye Serikali ya CCM chini ya uongozi wa Mh Rais Dr John Pombe Joseph Magufuli imesikia kilio cha wakulima wa Zabibu mkoani Dodoma cha ukosefu wa soko la zabibu kutokana na tozo kubwa ya ushuru wa bidhaa iliyokuwa ikitozwa Tsh 3,315 kwa lita kwa kinywaji kikali kitokanacho na mchuzi wa zabibu. Akichangia leo Bungeni katika Muswada wa Marekebisho ya Sheria Na.2/2019 Mbunge wa Viti Maalum Mh Mariam Ditopile ameishukuru serikali kwa kuleta mabadiliko hayo ya ushuru wa bidhaa na kupunguza tozo hiyo ambayo itawasaidia wakulima kupata soko la uhakika wa…
Picha : SHEREHE YA WATAWA YAFANYIKA KANISA KATOLIKI KAHAMA

Kanisa katoliki Jimbo la Kahama leo Jumamosi Februari 9,2019 limefanya Sherehe ya Watawa wa jimbo Katoliki la Kahama ambapo imefanyika kuadhimisha misa takatifu iliyokwenda sambamba na watawa sita na padri mmoja kumshukuru Mungu kwa Jubilee ya miaka 25 ya Utawa.
Siku ya Watawa hufanyika duniani Februari 2 kila mwaka lakini Jimbo Katoliki Kahama lilisogeza mbele sherehe hizo imefanyika kufanya leo Februari 9,2019. Picha zote na Patrick Mabula - Kahama

Misa takatifu ya sherehe ya Watawa ya jimbo katoliki la Kahama katika kanisa kuu la Mtakatifu Karoli Lwanga parokia ya Kahama Mjini ikiendelea.

Watawa wa kanisa Katoliki jimbo la Kahama wanaoadhimisha sherehe miaka 25 ya Utawa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Karoli Lwanga ,Parokia ya Kahama Mjini


Sherehe ya Watawa ,jimbo Katoliki la Kahama mapadri na Masista wakiandamana kwenda kanisani kuadhimisha misa takatifu


Sherehe ya Watawa ,jimbo Katoliki la Kahama mapadri na Masista wakiandamana kwenda kanisani kuadhimisha misa takatifu pia kuna watawa 6 wamemshukuru Mungu kwa Jubilee ya miaka 25 ya Utawa.



Kwaya shirikisho kanisa kuu la Mtakatifu Karoli Lwanga parokia ya Kahama mjini wakiimba wakati wa sherehe ya Watawa pamoja na kuwapongeza Masista 6 kwa jubilee ya miaka 25 ya Utawa.

Wageni wa jimbo katoliki la Kahama wakiwa pamoja na waumini katika sherehe ya Watawa .

KULALA GUEST NJOMBE SASA LAZIMA UWE NA KITAMBULISHO
Mkuu wa wilaya ya Njombe, Ruth Msafiri amesema watu wote wanaoingia kwenye nyumba za kulala wageni ni lazima waonyeshe kitambulisho kinachotambulika na Serikali.
Msafiri ametoa kauli hiyo leo Jumamosi wakati akizungumza na maofisa ustawi wa jamii ngazi ya wilaya na kata katika semina ya Kamati ya Ulinzi wa Mwanamke na Watoto iliyokuwa ikitolewa na maofisa kutoka wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto.
Semina hiyo pia ilitoa mafunzo ya namna ya kukabiliana na matukio ya utekaji na mauaji ya watoto yanayoendelea wilayani Njombe.
“Katika kipindi hiki tuhakikishe tunajisimamia maeneo yetu tunayoishi. Mgeni yeyote iwe ni kijijini au mjini tutoe taarifa kwa viongozi wetu na kwenye nyumba za kulala wageni tumeshatoa maelekezo.”
“Kila anayeingia nyumba ya kulala Njombe hii awe na kitambulisho ninaamini hakuna mtu atasema hana kitambulisho cha mpiga kura au cha taifa kama huna basi wewe si raia wa Tanzania,” amesema Msafiri.
Amesema mtu ambaye hatakuwa na kitambulisho chochote kile awe na barua ya utambulisho alikotoka vinginevyo hatakubaliwa kupokelewa popote ndani ya wilaya yake.
“Tunafanya hivyo si kutaka kuwanyanyasa hapana bali ni kuona suala la ulinzi na usalama linazingatiwa na tunakuwa salama zaidi,” ameongeza.
Na Godfrey Kahango, Mwananchi
BABU WA MIAKA 70 ASHAMBULIWA KISHA KUKATWA NYETI ZAKE NA WASIOJULIKANA

Mzee mmoja mwenye umri wa miaka 70 aitwae Peter Mutisya Mutongoi anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Machakos Level Five baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana na kumkata sehemu zake za siri 'nyeti'.
Inaelezwa kuwa alishambuliwa akiwa katika soko la Bishop Ndingi kata ndogo ya Mwala Kaunti ya Machakos nchini Kenya mwendo wa saa tatu usiku Ijumaa, Februari 8,2019.
Afisa mkuu wa polisi eneo la Mwala Henry Kimathi alithibitisha kisa hicho na kusema mzee huyo aliokolewa na watu waliomkuta akivuja damu kwa wingi na akiwa katika hali mbaya.
"Wafanyabiashara watatu katika soko ya bishop Ndingi walimkuta mzee huyo akivunja damu nyingi nusra ya kufa, walimchukua na kumkimbiza katika hospitali ya Machakos Level Five Hospitali," Kimathi alisema.
Mwanawe Mutisya alisema visa vya watu kukatwa sehemu nyeti katika kijiji hicho vimekithiri sana na wanaamini wanaofanya vitendo hivyo wanatumia sehemu hizo katika kufanya ushirikina.
Maafisa wa polisi wameanzisha uchunguzi dhidi ya waliotekeleza unyama huo na wameahidi kuwachukulia hatua kali ya kisheria.
FISI AUA MWANAFUNZI AKIJIANDAA KWENDA SHULE

Wakazi wa kijiji cha Leleshwa kaunti ya Laikipia nchini Kenya wameachwa vinywa wazi huku wakitizama fisi akimshambulia na kumuua mvulana mwenye umri wa miaka 17 nyumbani kwao.
Mvulana huyo aliripotiwa kushambuliwa nyumbani kwao na mnyama huyo majira ya saa kumi na moja alfajiri alipokuwa akijiandaa kwenda shuleni.
Babake mwathiriwa alikuwa chumbani mwake akiwa amelala huku mamake akiwa jikoni akiandaa kifungua kinywa ambaye pia alivamiwa na fisi huyo na kuachwa na majeraha mabaya sana.
Wazazi wake walijaribu kumuokoa mtoto wao lakini pia wao walishambuliwa na kuachwa na majeraha mabaya.
Majirani walifika nyumbani kwa mwathiriwa ila hawakuweza kumuokoa mvulana huyo wao pia walifukuzwa na fisi huyo kila walipojaribu kumnusuru mvulana huyo.
Maafisa wa shirika la huduma kwa wanyama pori KWS waliofika nyumbani kwa waathiriwa walisema fisi huyo ni mmoja wa wanyama pori waliotoroka msituni kufuatia moto uliozuka.
Afisa anayesimamia mbuga ya wanyama ya Laikipia West Mohammed Madela alisema, wanyamapori kadhaa wameripotiwa kuvamia makazi ya binadamu na wanashughulikia suala hilo.
Wazazi wa mvulana huyo walikimbizwa katika hospitali ya rufaa ya Nyahururu ambapo wanaendelea kupokea matibabu.
Chanzo - Tuko blog
RPC ATAJA MAJINA YA WATU WALIOFARIKI KWENYE AJALI YA HIACE, LORI NA PIKIPIKI NA BUKOBA
Kamanda wa polisi mkoani Kagera Revocatus Malimi amewataja watu waliopoteza maisha katika ajali ya gari la mizigo aina ya Canter yenye namba za usajili T223 ATK gari la abiria aina ya Hiace lenye namba T 869 CHT na pikipiki iliyotokea jana usiku katika katika mlima Nyangoye eneo la Hamugembe Manispaa ya Bukoba.
Amesema waliofariki katika ajali hiyo kuwa dereva wa lori Dickson Bakuza (25) na Niace Gervaz ambaye ni dereva wa Hiace inayomilikiwa na Huberth Ifunya.
Kamanda Malimi amewataja marehemu wengine kuwa ni Peter Ifunya (31) ambaye ni kondakta wa Hiace na mwendesha pikipiki Prudence Themistokres (30).
Amesema watu wanne waliofariki ni wakazi wa Rwamishenye katika Manispaa ya Bukoba.
Aidha amewataja majeruhi wawili waliolazwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Kagera kuwa ni Amir Mohamed 30) na Athanas Josephat (34) ambao hali zao zinaendelea vizuri.
Amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa Hiace na mwendesha pikipiki ambao walikuwa wakifuatana kutoka Mjini Bukoba kuelekea nje ya Mji na walipofika katika mlima Nyangoye eneo la Hamugembe, walijaribu kulipita Gari aina ya Noah bila uangalifu na kugongana uso kwa uso na Canter.
Amesema baada ya kugongana Hiace iliwaka moto na kusababisha Canter nayo kushika na kusababisha vifo hivyo na majeruhi.
Na Mwandishi wa Malunde1 blog Bukoba
PAKUA APP YA MALUNDE1 BLOG HAPA MARA MOJA
PAKUA APP YA MALUNDE1 BLOG HAPA MARA MOJA
MA DC NA RC MSINIPONZE,WAZIRI MKUCHIKA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), George Mkuchika, amewataka baadhi ya wakuu wa Wilaya na mikoa nchini kuacha kuwaweka ndani watu kwa saa 48 wakati hakuna sheria inayowapa mamlaka hayo. Mkuchika amewataka wakuu hao wa Wilaya kuacha kutumia mabavu kwenye utendaji wao wa kazi wa kila siku kwa kuwa wakiendelea na tabia hiyo watakuwa wanahatarisha kazi yake ya uwaziri. Ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma wakati akichangia na kueleza kuwa wakuu wa wilaya na mikoa wanapaswa kutumia busara katika kuwaweka ndani raia, ambapo Waziri Mkuchika amesisitiza Wakuu…
TRUMP NA KIM KUKUTANA TENA HANOI
Rais wa Marekani, Donald Trump amesema mkutano wake na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un utafanyika baadae mwezi huu, kwenye mji mkuu wa Vietnam, Hanoi.
Trump ameandika leo katika ukurasa wake wa Twitter kwamba wawakilishi wake wameondoka Korea Kaskazini baada ya kufanya mazungumzo yaliyofanikiwa na wamekubaliana kuhusu muda na siku ya kufanyika kwa mkutano huo wa kilele kati yake na Kim.
Amesema mkutano huo wa pili kati ya viongozi hao utafanyika Februari 27 na 28, Trump na Kim walikutana kwa mara ya kwanza mwaka uliopita huko Singapore.
Trump amebainisha kuwa Korea Kaskazini chini ya uongozi wa Kim, itakuwa nchi yenye uchumi mkubwa zaidi. Kiongozi huyo wa Marekani amesema amejiandaa kukutana na Kim ili kuendeleza mchakato wa amani.
Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema kuwa mjumbe maalum wa Marekani nchini Korea Kaskazini, Stephen Biegun atakutana tena na maafisa wa Korea Kaskazini kabla ya mkutano wa Trump na Kim.
Biegun amewasili Seoul, Korea Kusini akitokea Pyongyang baada ya kufanya ziara ya siku tatu ambako alijadiliana na maafisa wa Korea Kaskazini kuhusu mkutano wa viongozi hao.
TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA 09.02.2019 HAZARD KUTIMKIA MADRID

Meneja wa Chelsea Maurizio Sarri, amesema hatakuwa kizingiti kwa Eden Hazard ikiwa nyota huyo wa miaka 28 ataamua kujiunga na miamba wa ujispania Real Madrid msimu ujao. (Star)
Lakini Cesc Fabregas anaamini Hazard huenda akasaini mkataba mwingine na Chelsea katika hatua ambayo itakomesha tetesi kuhusu uhamisho wako. (Independent)
Tottenham wanajiandaa kuweka dau la pauni milioni 35 kumnunua kiungo wa kati wa West Ham Declan Rice, 20, licha ya kukabiliwa na ushindani kutoka kwa mahasimu wao katika ligi ya Uingereza, Liverpool. (Daily Express)
Manchester Unitedwanatarajiwa kuminyana na mahacimu wao Manchester City kumsaini kiungo wa kati wa Lyon Tanguy Ndombele, 22 msimu ujao. (Mirror)
Tanguy Ndombele (kushoto) aliisaidia Lyon kushinda Manchester City katika ligi ya mabingwa mwezi uliyopita
Vilabu vya Chelsea, Manchester United na Liverpool vinapania kumnunua nyota wa Benfica Joao Felix, 19. (Talksport)
Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amepuuzilia mbali tetesi kuwa klabu hiyo itatumia fedha nyingi msimu ujao kuwasajili wachezaji wapya. (Teamtalk)
Kipa David de Gea, 28, anakaribia kutia saini kandarasi ya miaka mitano na klabu ya Manchester United. (Metro)
Chanzo:Bbc
MKUCHIKA APIGILIA MSUMALI MWINGINE KWA WAKUU WA WILAYA
.jpg?itok=8aV321lz×tamp=1549701071)
Waziri George Mkuchika.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), George Mkuchika, amewaumbua baadhi ya wakuu wa Wilaya nchini wanaowaweka ndani watu kwa saa 48 wakati hakuna sheria inayowapa mamlaka hayo.
Mkuchika amewataka wakuu hao wa Wilaya kuacha kutumia mabavu kwenye utendaji wao wa kila siku kwa kuwa wakiendelea na tabia hiyo watakuwa wanahatarisha kazi yake ya uwaziri.
Akiwa bungeni wakati akichangia na kueleza kuwa wakuu wa wilaya na mikoa wanapaswa kutumia busara katika kuwaweka ndani raia, ambapo Waziri Mkuchika amesisitiza Wakuu wa Wilaya wasimponze.
“Msiniponze. Mimi nataka Rais Magufuli asinibadili hapa, mimi nataka Rais Magufuli aseme mzee endelea, tuache masuala ya umwamba, nawaomba huko mliko msiniharibie kazi yangu. Mimi ndiye mwenye cheo cha utawala bora, mimi ndiye Waziri mwenye dhamana ya utawala bora, ukiendesha mambo kinyume cha utawala bora unaniharibia kazi,” alisema Mkuchika.
Akielezea madaraka ya wakuu wa wilaya kuwaweka ndani watu saa 24, lugha iliyotumika ni kwa usalama wake, maana yake mtu ameua mtu, na jamaa zake wamekasirika wanataka kumpiga yule aliyeua na hapo ndipo dhana ya kumweka huyo mtuhumiwa ndani saa 24 inatumika kwa usalama wake.
Alisema mkuu wa wilaya akishamweka mtu huyo ndani ya saa 24 na muda huo ukamalizika, ikifika asubuhi ni lazima apelekwa mahakamani.
“Nataka niseme mahali popote mkuu wa wilaya kumweka ndani mtu saa 48 ni makosa kwa sababu sheria inampa saa 24 na mkuu wa mkoa amepewa saa 48, na pia siyo lazima umuweke.” alisema Mkuchika.
Januari 29, mwaka huu Rais Magufuli akiwa kwenye hafla ya kuwaapisha majaji, wakuu wa wilaya na wakurugenzi wapya Ikulu jijini Dar es Salaam, aliwataka wakuu wa wilaya aliowateua kwenda kusimamia sheria, kutoitumia vibaya sheria ya kuwaweka watu polisi.
Chanzo:Eatv
Chanzo:Eatv


