Saturday, 9 February 2019

KONDOMU ZAADIMIKA MJI WA MAKAMBAKO,MADIWANI WAMPA SIKU SABA MKURUGENZI KUSHUGHURIKIA

Na.Amiri kilagalila Baraza la madiwani la Halmashauri ya Mji wa Makambako Mkoani Njombe limetaarifu kuadimika kwa Kondomu kote madukani halmashauri ya mji wa Makambako mkoani Njombe hivyo kuwaagiza wataalamu wake kutafuta mwarobaini kwani ni kikwazo katika jitihada za kukabiliana na maradhi ya Ukimwi. Wajumbe wa Baraza hilo wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo hanana mfikwa walisema licha ya kuadimika hata zile zinazopatikana zimekuwa zikiuzwa hadi Tsh 800 moja kiwango ambacho wanakitaja kutokuwa rafiki kwao. Madiwani wa kata mbalimbali katika Halmashauri ya Mji wa makambako wamekutana katika kikao cha baraza la…

Source

Share:

MKURUGENZI ANAYEDAIWA KUUA KANISANI AFUNGUKA "NIMEPAKAZIWA TU"


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itigi, Pius Luhende anayedaiwa kuhusika na mauaji ya Isaka Petro (28) amezungumza na Mwananchi akisema “nimepakaziwa tu.”

Luhende alitoa kauli hiyo baada ya mwandishi wetu kumtembelea katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida alikolazwa tangu Jumanne wiki hii baada ya kupewa rufaa kutoka Hospitali ya Wilaya ya Manyoni.

Kwa mujibu wa mganga mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk Ng’hungu Kuzenza, Luhende anasumbuliwa na pumu (asthma) na mapigo ya moyo.

Mkurugenzi huyo ni miongoni mwa watu saba wanaoshikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo yaliyotokea Jumamosi iliyopita katika Kanisa la Wasabato Kijiji cha Kazikazi mkoani humo.

Inaelezwa kuwa mauaji hayo yalitokea baada ya Luhende kuwafuata watuhumiwa wa kosa la kuharibu mali ya mlalamikaji Rose Andrew aliyedai kuharibiwa mali yake iliyopo ndani ya shamba la Tanganyika Packers linalomilikiwa na halmashauri hiyo.

Taarifa ya Polisi inasema kuwa Luhende alipoingia ndani ya kanisa hilo ilitokea vurugu na akaamua kutoka nje kabla ya askari wanyamapori waliokuwa na silaha kufyatua risasi kadhaa na moja ikampiga Isaka na kufariki dunia papo hapo.

Hata hivyo, waumini waliokuwepo katika kanisa hilo wakati mauaji hayo yakitokea walizungumza na Mwananchi na kupingana na polisi wakisema kuwa mkurugenzi huyo ndiye alimfyatulia risasi Isaka.

Luhende ambaye alikuwa akilindwa na askari kanzu wanne wodini alisema bado kifua kinambana mara kwa mara hasa nyakati za usiku.

“Hata hivyo, namshukuru Mungu kwa kunipigania naendelea vizuri kuliko nilipokuwa hospitali ya Manyoni,” alisema Luhende ambaye alikuwa amejilaza kitandani huku mikononi akiwa hajafungwa pingu.

Na Gasper Andrew, Mwananchi
Share:

WEZI WATUMIA MABOMBA YA KINYESI KUIBA PESA BENKI


Wezi nchini Ubelgiji wamewashangaza wananchi wa taifa hilo na ulimwengu baada ya kutumia mitaro na mabomba ya maji taka na kinyesi kusafiri hadi kwenye Tawi la Benki ya BNP Paribas Fortis, ambapo waliiba pesa ambazo hazikujulikana kiwango chake.

Wezi hao wanasemekana kutumia mabomba hayo ya upana wa sentimita 40 kupitia chini ya ardhi hadi eneo ambapo pesa zinahifadhiwa katika benki iliyo karibu na wilaya ya Antwerp.

Polisi walifahamishwa kuhusu tukio hilo na walipofika eneo panapohifadhiwa pesa ndani ya benki hiyo, japo mlango ulikuwa umefungwa, masanduku 30 ya pesa yalikuwa yameibwa.

Hata hivyo, bado polisi hawajatangaza kiwango cha pesa ambacho wezi hao waliondoka nacho. Maofisa wanaosimamia maji na usafi wa mazingira mji huo, hata hivyo, walisema kuwa wezi hao walihatarisha maisha yao kwa kutumia mbinu hiyo.

“Kwanza kabisa, kuchimba shimo ili kutokezea katika mabomba ya kusafirisha uchafu ilikuwa hatari kwani kulikuwa na uwezekano wa ardhi kuporomoka. Ndani ya mabomba hayo ya uchafu, kuna hatari nyingi kama hewa chafu inayotoka ndani ya uchafu huo,” amesema Els Liekens ofisa wa kampuni ya maji.

Wizi wa aina hiyo umewahi kutokea nchini Ufaransa mnamo mwaka 1976 uliwafanya wezi kuishi kwa miezi wakichimba ndani ya mabomba ya kusafirisha uchafu, kisha baadaye wakaiba mamilioni ya pesa pamoja na mali iliyokuwa ndani ya masanduku 200.
Share:

HABARI KUBWA KWENYE MAGAZETI YA TANZANIA LEO FEBRUARI 9,2019.

Fahamu yote yaliyojiri katika Magazeti ya Tanzania leo Februari 9, 2019. Hapa unapata habari zote zilizopewa uzito katika kurasa za mbele na kurasa za nyuma za habari za michezo na burudani.

Source

Share:

Friday, 8 February 2019

BREAKING NEWS:MAGARI MAWILI YAGONGANA BUKOBA,YASABABISHA VIFO

Ajali mbaya imetokea usiku huu katika manispaa ya Bukoba kata ya Hamugembe Mkoani kagera ikihusisha magari mawili Toyota hiace T-869 CHT na fuso T-223 ATK yamegongana na kusababisha moto kulipuka ambao umepelekea abiria waliokuwemo kwenye magari Hayo kuungua vibaya. Kamanda wa polisi mkoani Kagera Revocatus Malimi amesema tayari wameokoa maiti nne kutoka kwenye ajali hiyo. Matukio katika picha

Source

Share:

Breaking News : HIACE YAGONGANA NA LORI KISHA KUWAKA MOTO MLIMA NYANGOYE BUKOBA, KUNA TAARIFA YA VIFO


Watu kadhaa wanahofiwa kupoteza maisha katika ajali  iliyohusisha magari aina ya Canter lenye namba za usajili T223ATK na Hiace yenye namba za usajili T869 GHT kugongana  katika Mlima Nyangoye  eneo la Hamugembe Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.

Ajali hiyo imetokea usiku huu Februari 8,2019

Taarifa za awali kutoka eneo la tukio zinasema kuna taarifa ya vifo vya abiria,idadi haijulikani na bado mamlaka husika hazijazungumzia tukio hilo.

Malunde1 blog inaelezwa kuwa Hiace /daladala yenye Jina la Kitunze Kidumu inayofanya safari zake Bukoba - Mtukula ilikuwa inaelekea kupaki.

Taarifa Kamili tutawaletea hapa Malunde1 blog

Share:

WATUMISHI 50 WILAYA YA MAKETE KUSIMAMISHWA KAZI KWA UDANGANYIFU

Na.Amiri kilagalila Baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Makete mkoani Njombe limepitisha na kuridhia kuwasimamisha kazi watumishi wapatao 50 waliojipatia ajira kwa njia ya udanganyifu na mtumishi mmoja aliyethibitika kuwa ni mtoro kazini . Akitangaza mapendekezo ya kamati mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya makete mh Egnatio mtawa amesema hayo ni mawazo ya baraza la madiwani lilojigeuza kuwa kamati ili kuweza kujadili juu ya jambo hilo. “kamati imefikisha mapendekezo kwenye baraza kwamba wtumishi wapatao 60 watendaji wa vijiji,afisa mifugo mmoja,fundi sanifu mmoja na madreva wanne wathibitishwe kwenye ajira zao…

Source

Share:

NABII MAARUFU ATABIRI ATAUAWA KISHA KUFUFUKA BAADA YA SIKU TATU KAMA YESU


Nabii maarufu David Owuor
Nabii maarufu David Owuor ametabiri jinsi atakavyoondoka humu duniani baada ya kukamilisha kazi aliyotumwa kufanya na Mungu. 


Owuor alisema muda wake umekaribia kufika ukingoni hapa duniani na Mungu amefurahishwa na kazi yake na kwamba kifo chake kitalinganisha na kile cha Yesu .

 Owuor ambaye hujitaja kuwa nabii mwenye nguvu zaidi ulimwenguni alisema ataondoka humu duniani jinsi Yesu alivyoondoka. 

Akitoa unabii kwa wafuasi wake katika kanisa la Repentance and Holiness Ministry, Owuor alisema alikutana na Mungu mawinguni na akamuelezea  habari ya kifo chake

Akitoa unabii kwa wafuasi wake, Owuor, alisema atauawa katika Mji wa Yerusalemu na mwili wake hautazikwa ila baada ya siku 3 atafufuka na kuenda mbinguni kukutana na Mungu. 

"Baba yangu na Mungu wangu amezungumza nami, alianza kuzungumza nami akiwa mwenye furaha kuu, aliniambia kwamba nitauawa pindi nitakapokamilisha kazi yake," Owuori alisema. 

 "Nitakufa kwa siku 3 na baada ya hapo nitafufuka na Mungu atanichukua kuenda mbinguni kulingana na kitabu cha Ufunuo 11:7.1," Owuor alisema.

 " Nitauawa baada ya kumaliza kufanya kazi ya Mungu, sitazikwa na kwa siku ya 3 Mungu atanichukua kuenda mbinguni, nitauawa Yerusalemu na hii sio mara ya kwanza mimi kuzungumza na Mungu, " Owuor aliongezea.

Picha za Owuor kwenye matukio mbalimbali

Share:

ZANTEL YAZINDUA PROMOSHENI YA WATUMAJI WA HUDUMA YA EZYPESA


Mkuu wa Masoko na Huduma ya Fedha za simu za mkononi wa Zantel, Sakyi Opoku, akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa promosheni kwa watumiaji wa huduma yake ya kifedha ijulikanayo kama EzyPesa ili kuwezesha wateja wake kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo fedha taslimu .Wengine pichani ni Maofisa Waandamizi wa Zantel
Mkuu wa Huduma na Bidhaa wa Zantel, Aneth Muga, akifafanua jambo kwa waandishi wakati wa uzinduzi huo.
Meneja Bidhaa Kitengo cha EZYPESA wa Zantel, Leonard Kameta, akiongea wakati wa uzinduzi huo
Mkuu wa Masoko na Huduma ya Fedha za simu za mkononi wa Zantel, Sakyi Opoku (kushoto) akimkabidhi simu mwandishi wa gazeti la The Guardian, Beatrice Philemoni, baada ya kujishindia simu kupitia droo ndogo ya waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi huo.
Wafanyakazi wa Zantel wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi huo
Wafanyakazi wa Zantel wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi huo

Kampuni ya mawasliano Zantel, imezindua promosheni kwa watumiaji wa huduma yake ya kifedha ijulikanayo kama EzyPesa ili kuwezesha wateja wake kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo fedha taslimu.

Promosheni hii itakayodumu kwa kipindi cha miezi mitatu, ni rasmi kwa ajili ya wateja wote wanaotumia Ezypesa pamoja na wateja wapya wanaoendelea kujiunga na huduma hio. Kila mara mteja atakapotuma ama kupokea fedha kupitia EzyPesa, atajiweka kwenye nafasi ya kujishindia zawadi nono kama simu za mkononi zinazotumia interneti (Smartphones) na fedha taslimu kuanzia shilingi 200,000/- hadi shilingi 1,000,000/-

Akiongea wakati wa uzinduzi uliofanyika jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Masoko na Huduma za kifedha kupitia simu za mkononi wa Zantel, Sakyi Opoku, alisema promosheni hii itawezesha watumiaji wa huduma ya EzyPesa kujipatia motisha kama vile kurudishiwa fedha kwenye akaunti zao na kujishindia zawadi mbalimbali.

Watumiaji wa huduma ya EzyPesa watakaongeza salio la muda wa maongezi kuanzia shilingi 500/- watarudishiwa fedha zao. Wateja watakaotuma au kupokea kiasi cha shilingi 10,000/-wataingia kwenye droo ya wiki inayowezesha kujishindia simu ya kisasa (Smartphone). Kila wiki droo itakuwa na washindi 10 wa fedha taslimu na washindi 15 wa simu. Droo ya mwezi italenga kuwapata wateja 10 waliotuma na 10 waliopokea fedha kwa wingi.

EzyPesa ndio huduma pekee ya mtandao hapa Tanzania inayowezesha wateja wake kufanya miamala ya malipo ya kodi kwa ZBR na kununua umeme wa LUKU na TUKUZA. Huduma ya EzyPesa inaondoa adha ya wateja kupoteza muda mwingi wakipanga foleni ili kupata huduma za kibenki na kulipa ankra zao mbalimbali. Vile vile, EzyPesa sasa inapatikana katika program mpya ya simu za mkononi (Mobile Application) inayowezesha wateja kufanya malipo mbalimbali kwa njia rahisi zaidi.

Kwa sasa wastani wa miamala inayofanyika kwa mwezi kupitia huduma hii inafika million 5.6 na Zantel ina malengo ya kufikisha huduma hio kwa wateja 100,000 wapya kila mwezi. Zantel pia inaendelea kufanya majadiliano na taasisi mbalimbali za kifedha ikiwemo benki za CRDB na NBC kuhusu ushirikiano katika kutoa huduma za kifedha kupitia mtandao wake.
Share:

DAWASA YAJIBU KERO YA MAJI KWA WAKAZI WA MBEZI KWA MSUGULI NA VITONGOJI VYAKE


Meneja wa DAWASA- Kimara jijini Dar es Salaam Paschal Fumbuka (kulia) na Msimamizi wa Bomba kubwa la MajiSafi na MajiTaka la DAWASA Mhandishi Gibson Baragula (kushoto) wakimwonyesha mwanahabari bomba lililotobolewa ili kuweza kusambazia maji wakazi wa Mbezi kwa Msuguli jijini Dar es Salaam na vitongoji vyake. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Meneja wa DAWASA- Kimara jijini Dar es Salaam Paschal Fumbuka (kulia) wakimwonyesha mwanahabari jinsi maji yanavyotoka katika maungio ya bomba lililotobolewa ili kumaliza mgao kwa wakazi wa Mbezi wa Msuguli jijini Dar es Salaam na vitongoji vyake.

Wafanyakazi wa DAWASA wakiendelea na zoezi la uunganishaji wa mabomba.

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Wakazi wa Mbezi Kwa Msuguli na vitongoji vyake jijini Dar es Salaam wanatarajia kuanza kupata maji bila ya mgao mara baada ya kukamilika uunganishwaji wa bomba jipya.

Bomba hilo jipya la Mamlaka ya MajiSafi na MajiSafi (DAWASA) litajibu kero ya mgao waliyokuwa wakipata wakazi wa Bwaloni, Msaki, Saranga, Majengo mapya mpaka Malamba Mawili, Msingwa, Kanisa la Udongo, Kisiwani na vitingoji vyake.

Akizungumza mara baada ya kumaliza zoezi la utomboaji wa Bomba, Msimamizi wa bomba kubwa la MajiSafi wa DAWASA Mhandisi Gibson Baragula amesema kwa kazi hiyo ilikuwa ni kutoa toleo la nchi 8 katika bomba kubwa la nchi 40 ambapo kazi imefanyika usiku wa kuamkia leo na zoezi hili linaenda kukamilika haraka.

"Niwaombe wakazi wa Mbezi wa Msuguli na Vitongoji vyake wavumilie tumalize ili waweze kupata ya uhakika kwa vile yatakuwa na presha ya kutosha na wataweza kupata wote kwa wakati mmoja," amesema Mhandisi Baragula.

Nae Meneja wa DAWASA- Kimara jijini Dar es Salaam Paschal Fumbuka amesema kazi kubwa imefanyika na inatarajiwa kumalizika mara baada ya masaa 48 na kuzaa matunda ili kuweza kuwapatia maji wakazi wa maeneo ya Mbezi kwa Msuguli na vitingoji vyake maji.

"Kazi kubwa ilinakaribia kukamilika na wakazi wa Mbezi kwa Msuguli wakae mkao wa kunywa maji safi na salama," amesema.

Ametoa wito kwa wakazi wote wa maeneo hayo kuendelea kuwa mabalozi wema kwa kuendelea kulipia bili zao za maji kwa wakati ili wawepe huduma bora.

"Sisi wajibu wetu tunaenda kuukamilisha hivyo basi niwaombe wale wote wanaodaiwa kulipa madeni yao na pia tutapita nyumba kwa nyumba kufanya msako wa uhakiki wa wateja, Amesema.

Maeneo ya Mbezi kwa Msuguli yamekuwa wakikosa huduma ya maji safi na salama kwa kipindi kirefu kutokana na miundombinu na jografia ya maeneo hayo.
Share:

MWANAMKE AUAWA KWA KUTAFUNWA NA NGURUWE

Mwanamke mmoja nchini Urusi ameuawa na nguruwe aliokuwa anawafuga baada ya kuanguka kwenye banda la wanyama hao.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Urusi, mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 56 alikuwa akiwalisha nguruwe ndipo ghafla akaanguka na nguruwe hao wakamtafuna.

Inasadikiwa kuwa chanzo cha kuanguka kwake ilikuwa ni kuzirai ama kupatwa na kifafa.

Tukio hilo limeripotiwa kwenye wilaya Malopurginsky jimboni Udmurtia, lililopo katikati ya Urusi.

Vyombo vya habari vya Urusi vinaarifu kuwa mume wa marehemu alikuwa amelala wakati mkewe alipokuwa akiwahudumia nguruwe hao. Bwana huyo inasemekana alikuwa mgonjwa.

Baada ya kuamka alianza kumtafuta mkewe na kukuta mwili wake ndani ya banda la nguruwe.

Inataarifiwa kuwa alifariki baada ya kupoteza damu nyingi. Tayari upelelezi wa polisi juu ya tukio hilo umeshafunguliwa. 

Oktoba mwaka 2012 tukio kama hilo liliripoptiwa nchini Marekani katika jimbo la Oregon. Bwana Terry Vance Garner, aliyekuwa na miaka 69 wakati huo alienda kuwalisha nguruwe wake lakini hakurejea.

Baadae, familia yake ilikuta mabaki ya mwili wake kwenye banda la nguruwe huku sehemu kubwa ya mwili huo ikiwa imeshaliwa na wanyama hao.

Mamlaka za eneo hilo ziliripoti kuwa mmoja wa nguruwe hao hapo awali alishawahi kumng'ata marehemu lakini aliweza kujinasua.

Kaka wa bwana huyo, Michael, alidai kuwa nguruwe hao walishawahi kujaribu kumtafuna na yeye na bwana Garner aliahidi kuliua dume kubwa ambalo ndio lilikuwa tishio zaidi.

Hata hivyo, baadae alibadili mawazo na kuendelea kuwafuga mpaka pale walipomuua.
Chanzo- BBC
Share:

BWANA HARUSI NA MPAMBE WAKE WAFARIKI KWA KULIPUKIWA NA BOMU

Bwana harusi na mpambe wake wamefariki dunia nchini Ethiopia kwenye mlipuko wa bomu la kutupa kwa mkono.

Mamlaka nchini humo zinaarifu kuwa bomu hilo lilikuwa linamilikiwa na bwana harusi.

Mlipuko huo ulitokea kwenye karamu iliyoandaliwa na mpambe baada ya kumalizika katika sherehe za fungate ya siku 10.

Bibi harusi hakuwepo eneo la tukio wakati bomu hilo likilipuka na hivyo amepona.

Tukio hilo limetokea kwenye Kijiji cha mbali katika mkoa wa Amhara, kaskazini ya mji mkuu Addis Ababa.

Bomu hilo lilikuwa likimilikiwa kinyume cha sharia na bwana harusi huyo, polisi wameileza BBC.

Bwana harusi huyo amefahamika kama Mohammed Hassan Mohammed mwenye umri wa miaka 25. Na mpambe wake amefahamika kama Bogale Sebsibe Abera, 24.

Mamlaka nchini Ethiopia zimekuwa zikishutumiwa vikali kwa kushindwa kudhibiti wa umiliki wa silaha kinyume cha sheria. Wengi wa wamiliki hao wasio halali hufyatua risasi angani katika matukio makubwa kama misiba na harusi. Bwana harusi na mpambe wake walipuliwa na bomu.
Chanzo- BBC
Share:

LEMA : TUMEMUONDOA ZITTO KABWE ALIKUWA ANAFUATILIWA USIKU


Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe.

Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amesema juzi Jumatano Februari 6, 2019 walilazimika kumuondoa mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe baada ya kufuatiliwa na watu ambao hakuwataja.

Akizungumza wakati akichangia taarifa ya kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria leo Ijumaa Februari 8, 2019, Lema amesema kama CCM wakitawala kwa haki, kwa kufuata sheria na Katiba hana tatizo hata wakitawala milele.

“Leo mwenyekiti (Mussa Azzan Zungu), Zitto hayuko bungeni tumemuondoa juzi alikuwa anafuatiliwa usiku kwa kazi za kibunge sio za kuuza madawa ya kulevya si za kubaka watoto ni kazi za kibunge.”

Lema ameongeza kuwa, “Lengo letu ni kuwaona mnatutawala kwa haki na ndio maana ya upinzani lakini leo hii chuki inajengwa leo kiongozi mmoja M-NEC anasema Lissu akitua ashambuliwe".
Share:

HATIMAYE DEREVA AFUNGUKA TUKIO LA TUNDU LISSU KUPIGWA RISASI


 Adam Bakari, dereva wa mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, amesema shambulizi walilofanyiwa akiwa pamoja na mbunge huyo lilikuwa likijulikana na kutaka watu kutomhusisha na jambo hilo.

Amedai ndio maana siku ya tukio hilo Septemba 7, 2017 katika makazi ya mbunge huyo hakukuwa na ulinzi wa aina yoyote.

Bakari ametoa kauli hiyo katika mahojiano na Idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Ujerumani DW Deutsche Welle.

Mbunge huyo alishambuliwa kwa zaidi ya risasi 30 akiwa ndani ya gari, nje ya nyumba yake, Area D mjini Dodoma lakini dereva wake huyo ambaye walikuwa wote hakupatwa na risasi na Lissu mara kadhaa amekuwa akieleza jinsi alivyomsaidia.

Dereva huyo amesema katika eneo ambalo shambulizi lilifanyika hulindwa na askari wenye silaha kila siku ila siku ya tukio hawakuwepo.

“Lakini mbona mimi sikujificha baada ya tukio na tuliwaambia kama wanataka kunihoji waje Nairobi mbona hawakufanya hivyo licha ya muda wote niliokuwepo pale,” amesema Bakari.

Akisimulia tukio hilo amesema siku hiyo walikuwa wakitokea bungeni kurudi katika eneo wanaloishi ndipo aligundua kwa nyuma kuna magari mawili yanawafuatilia.

“Nilipoona yapo nyuma yetu kwa muda nikaona bora niyapishe lakini hayakupita hivyo nikakunja kona ya kwanza nikaona gari bado zipo, nikakunja kona ya pili zipo nikaona hizi gari sio salama kwetu na nikaamua kuongeza mwendo,” amesema Bakari.

“Wakati huo sikumwambia chochote bosi (Lissu). Tukafika karibu na nyumbani kuna ‘club’ inaitwa ‘84’ gari iliyokuwa inanifuatia mimi ni V8 (Toyota) ikapaki pembeni ile Nissan iliyokuwa nyuma yake ilikuja kwa speed (kasi) kunifuata mimi nilipoingia getini na yenyewe iliingia.”

Ameongeza, “Tukapaki gari na wenyewe wakapaki wakiwa wamevaa kofia na miwani wakawa wanazungumza pale bila sisi kusikia. Walipomaliza gari ilirudi nyuma speed na ilipofika usawa wa gari yetu ilisikika tu milio ya risasi.”

Amesema aliposikia kelele za milio ya risasi na kelele za Lissu aliyekuwa ameketi upande wa kushoto, alifungua mlango wa gari upande wa kulia na kumvuta mbunge huyo nje.

Amesema wakati akifanya jambo hilo risasi zilikuwa zikiendelea kumiminwa katika gari hilo, “mimi nilichanwa na vioo katika baadhi ya maeneo.”

Na Aurea simtowe, Mwananchi 
Share:

SUMAYE AUGUA GHAFLA KWENYE ZIARA YA CHADEMA TANGA


 Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye ameugua ghafla akiwa mkoani Tanga.

Sumaye ambaye ni mjumbe wa kamati kuu ya Chadema amepatwa na tatizo la afya akiwa katika majukumu ya kichama.

Taarifa iliyotolewa leo mchana Ijumaa Februari 8, 2019 na Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Habari wa Chadema, Tumaini Makene imesema, “Sumaye alikuwa mkoani Tanga, akiendelea na ratiba ya ziara ya shughuli za chama kabla ya kupatwa na shida ya afya ghafla leo asubuhi.”

“Baada ya kutibiwa hali yake inaendelea vizuri na sasa amepumzika wakati mipango ya kumsafirisha kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo hii kwa ajili ya uchunguzi zaidi ikifanyika.”

Share:

WANANCHI NA VIONGOZI CCM NGARA WASHIRIKI UJENZI WA DARASA

Ngara: Na Mwandishi wetu. Wakazi wa kata ya Rulenge kwa kushirikiana na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Ngara mkoani Kagera wameshirikiana kujenga madarasa ya shule ya msingi Murugalagala ili kupunguza adha ya wanafunzi kusongamana katika chumba kimoja. Akiongoza ujenzi huo Katibu wa Ccm wilaya ya Ngara John Melele alisema viongozi na wanajamii wameungana kuonesha mshikamano na kuguswa na changamoto za shule hiyo katika utoaji wa taaluma. Melele alisema wameshiriki kusomba mawe, matofali na kujenga chumba kimoja kati ya viwili vinavyojengwa ambapo ametoa mifuko mitatu ya saruji na kuchangia…

Source

Share:

EBITOKE AKIRI KUBEBA MUME WA MTU


Msanii wa kike wa vichekesho nchini, Annastazia Xavery maarufu kama Ebitoke, hatimaye amefunguka juu ya tuhuma za siku nyingi za kuwa na mahusiano ya kimapenzi na bosi wake, director Timoth.

Akizungumza na Big Chawa kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Ebitoke amefunguka kwamba yeye hakumfuata Timoth ili kuwa naye kwenye mahusiano, licha ya kuwa Bosi wake huyo ni mume wa muigizaji mwenzake, Mama Ashura.

Baada ya kuulizwa tetesi za kugombana na Mama Ashura kwa kumchukulia mume, Ebitoke alikiri haya. “sasa ananimind mimi ndio nilimfuata Timoth nikamwambia njoo kwangu, Haya mambo yalishapitwa na wakati”.

Tetesi za etioke kuwa na mahusiano na Timoth Conrad zilikuwapo kwa muda mrefu lakini wawili hao wamekuwa wakikanusha, na pia kutajwa kuwa ndio chanzo cha Ebitoke kuapa kutorudi Timamu hata apigwe na maisha kwa kiasi gani.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger