Thursday, 7 February 2019

BALOZI WA TANZANIA MAREKANI AMJIBU TUNDU LISSU,AKANUSHA TUHUMA DHIDI YA SERIKALI

Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Wilson Masilingi jana usiku walihojiwa katika kipindi cha Straight Talk Africa kinachorushwa na kituo cha televisheni cha Sauti ya Marekani (VOA), huku kila mmoja akipangua hoja za mwenzake.

Masilingi amekuwa balozi wa pili kumjibu Lissu baada ya siku tano zilizopita Balozi  wa Tanzania nchini Ujerumani, Dk Abdallah Possi kumjibu Lissu baada ya mbunge huyo kueleza madai mbalimbali kuhusu Serikali na jinsi alivyoshambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 Septemba 7, 2017 wakati akihojiwa na kituo cha televisheni cha Deutsche Welle cha nchini humo.

Katika kipindi cha jana kilichoongozwa na mtangazaji maarufu, Shaka Ssali kilichokuwa na mada ya ‘Haki ya Uhuru wa kujieleza’, kilikuwa na wanajopo wengine ambao ni Jon Temin kutoka taasisi ya Freedom House na mwanasiasa wa upinzani wa Uganda, Robert Chagulani maarufu kama Bobi Wine.

Akijibu maswali ya mtangazaji huyo kuhusu uhuru wa kujieleza na sababu ya Lissu kushambuliwa kwa risasi, Balozi Masilingi amesema licha ya eneo aliloshambuliwa kuwa ni la nyumba za Serikali lakini halina uhusiano na kubanwa kwa uhuru wa kujieleza.


Kwa upande wake Tundu Lissu alipinga hoja inayotolewa na serikali kuwa yeye anazuia uchunguzi kufanyika baada ya shambulizi la risasi lililofanywa na watu wasiojulikana dhidi yake na dereva wake nchini Tanzania.

“Kama ningelikufa na dereva wangu angelikufa kusingekuwa na uchunguzi?” alihoji Lissu.

Akijibu shutuma zilizotolewa na Lissu, Balozi wa Tanzania, Marekani kwanza alikosoa lugha anayotumia Lissu na kusema kuwa anasikitishwa na kitendo chake cha kutotambua kwake kazi nzuri ya serikali.

“Kutotambua kazi nzuri ya serikali ukazunguka dunia nzima unamtukana rais wako, vyombo vya dola, na kuwaambia watanzania kwamba hamna haki nchini kwenu sio sawa,” alisema Balozi huyo na kungeza;

“Kitendo cha Lissu kuzunguka dunia nzima hakisaidii. BBC, Radio Ujerumani -DW, Sauti ya Amerika -VOA, sio mahakama. Unachofanya ni kutuchafua na kutuvunjia heshima na kujichafua yeye mwenyewe.”

Lissu alipoulizwa dhana hasi juu ya kutembea kwake nchi za nje akieleza hali ya taifa la Tanzania na vitendo vya mashambulizi alivyofanyiwa kuwa ni kitendo cha kulichafuwa taifa au yeye kuwa ni adui wa Tanzania, alieleza:

“Lazima tutofautishe kati ya serikali na taifa. Serikali sio taifa. Serikali inatakiwa kuongozwa na katiba, na katiba yetu imeweka wazi mipaka ya mamlaka. Sisi raia ambao ndio taifa tunahaki ya kuwakosoa viongozi wetu” alieleza Tundu Lissu

“Kwa hivyo tunapoeleza juu ya matendo mabaya iwe tuko ndani ya Tanzania, au nje ya Tanzania au mahali popote tunatimiza wajibu wetu kama raia,” alisisitiza Lissu.

Akijibu hoja hiyo ya Lissu, Balozi alisahihisha kwa kusema kuwa nafasi ya rais na amiri jeshi mkuu wa nchi, ni nembo ya taifa na hivyo (raia) hutakiwi kumtukana rais.

“Unazungumza vitu ambavyo havipo na unapaswa uniheshimu kwa sababu mimi ni kaka yako,” Alisema Balozi  na kuongeza;

“Mimi kama Balozi nimekuja hapa kutetea heshima ya Tanzania, kwa kuwa wewe umekuwa ukitukana nchi yako,”

Balozi alimkumbusha Tundu Lissu kuwa kama kuna sababu zozote za kiushahidi, Tanzania ina Katiba ,inasheria, inamahakama huru na inabunge.

Katika majibu yake Lissu alisema, “Nilishambuliwa kwenye nyumba za Serikali, nilipigwa mara 16 na nimefanyiwa operesheni 22. Swali la kujiuliza, nani aliyetoa agizo la kuondoa ulinzi katika nyumba za Serikali?”

“Pili, hilo eneo linalindwa na CCTV (kamera) ziliondolewa siku moja kabla ya tukio. Hakuna anayejua zilikopelekwa kwa sababu polisi hawasemi zilipelekwa wapi. Ninazungumza na watu, hakuna mtu aliyehojiwa.”

Hata hivyo Balozi alimjibu Tundu  Lissu akisema: "Wewe ulikuwa hospitalini mwaka na nusu unaletewa taarifa za kukuchonganisha na serikali na unazikubali kama zilivyo. Wewe kama mwanasheria huwezi ukachukua ushahidi wa kuambiwa.

"Kama mnadhamira ya dhati ya kutaka uchunguzi ufanyike, kwa nini hutaki kurudi nyumbani ukatoe ushahidi wewe na dereva wako na badala yake unazunguka kutukana na kuichafua nchi"
Share:

NDUGAI ASEMA KUNA HAJA YA KUSIMAMISHA MSHAHARA WA TUNDU LISSU

Spika wa Bunge, Job Ndugai (Mb) amesema kuna haja ya kusimamisha mshahara wa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kwa sababu hayupo bungeni, jimboni kwake wala hospitalini, na hajapewa taarifa zozote na daktari.

Spika Ndugai ametoa taarifa hiyo Bungeni wakati akijibu Muongozo wa Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Msukuma ambapo amesema Mbunge huyo hayupo Hosipitali,Hayupo Bungeni na hayupo Tanzania wala hajulikani anafanya kitu gani huko aliko hivyo hana sababu ya kuendelea kulipwa.

Tundu Lissu ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, yupo katika ziara ya siku 10 nchini Marekani baada ya kufanya hivyo kwenye nchi za Ujerumani na Uingereza.
Share:

KIUMBE CHA AJABU CHAZUA TAHARUKI SHULENI..CHURA SI CHURA,BINADAMU SI BINADAMU...


Jeshi la Polisi mkoani Rukwa limethibitisha uwepo wa tukio la uwepo wa kiumbe cha ajabu katika maeneo ya shule ya Msingi Kalalasi iliyopo Wilaya ya Kalambo, mkoani Rukwa, hali iliyozua taharuki kwa wanafunzi na walimu.

Kimwonekano, kiumbe hicho kinafananishwa na binadamu ila tu tofauti ni kuwa ni kidogo na kina urefu kati ya sentimita 12-15 tu.

Akizungumza na Daily News Digital leo asubuhi, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Rukwa, George Kyando amekiri kutokea kwa tukio hilo Jumanne wiki hii (Februari 5, 2019).

Kamanda ameeleza kuwa hadi sasa haijajulikana asili ya kiumbe hicho japo wakazi wa maeneo ya jirani na shule hiyo wameanza kulihusisha tukio hilo na ushirikina.

“Wengi wanahusisha na imani za kishirikina lakini sisi kama Jeshi la Polisi bado tunachunguza tujue kama ni binadamu au ni kitu gani maana kimofolojia ni kama mtu kina umbo la binadamu lakini sio binadamu wa kawaida.

“Kwa hiyo tumekikabidhi kwa wataalamu wa afya ili waweze kukifanyia kiumbe hiki utafiti kama huyu ni binadamu au ni kitu gani,” amesema Kamanda Kyando.


Kwa Upande wake shuhuda wa tukio hilo aliyefahamika kwa jina la Nicodemus Kapele amesema kuwa kiumbe huyo alionekana maeneo ya shule hiyo nyakati za asubuhi na kuzua taharuki miongoni mwa wanafunzi na walimu shuleni hapo hali iliyopelekea wanafunzi kuanza kukishambulia kiumbe hicho kwa mawe na kufanikiwa kukiua.

Mwalimu aliyekuwa zamu siku hiyo, Thomas Stephano ambaye alikuwa zamu siku hiyo alieleza kuwa siku ya tukio (Jumanne) alishangaa kuona kuwa muda wa mapumziko umekiwisha (saa 4:30 asubuhi) ila cha kushangaza wanafunzi bado walikuwa nje kwenye kikundi.

“Ilibidi niwafuate kuona nini kilikuwa kinafanyika kufika tu nikakuta wakikiua kiumbe hicho. Tulikimwagia maji tukione vizuri maana niliwaambia usikute ni chura…wao wakasema ni binadamu. Kweli, baada ya kumwagiwa maji, kiumbe huyo ana umbile la binadamu,” ameeleza mwalimu huyo ambaye amefundisha shule ya Msingi Kalabasi kwa miaka minne sasa. 


Naye Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Billy Philipo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ila hakuwa tayari kutoa maelezo zaidi kwa kile alichodai kuwa hawezi kuzungumzia suala hilo kwa kina kwa kuwa uchunguzi unaendelea.


Na Ombeni Utembele - Habarileo
Share:

POLISI 'WAMCHOMOA' MKURUGENZI WA HALMASHAURI MAUAJI KANISANI...WAUMINI WASISITIZA NDIYE ALIYEFYATUA RISASI


Unaweza kusema Jeshi la Polisi mkoani Singida ‘limemchomoa’ mkurugenzi wa Halmashauri ya Itigi, Pius Luhende katika tuhuma za kuhusika na mauaji ya Isaka Petro (28).

Taarifa ya polisi mkoani humo inaeleza kuwa watu saba wanashikiliwa akiwemo mkurugenzi huyo .

Taarifa hiyo ya Polisi inasema kuwa Luhende alipoingia ndani ya kanisa hilo ilitokea vurugu na akaamua kutoka nje kabla ya askari wanyamapori waliokuwa na silaha kufyatua risasi kadhaa na moja ikampiga Isaka na kufariki papo hapo.

Hata hivyo waumini waliokuwepo katika kanisa la Wasabato kijiji cha Kazikazi mkoani humo wakati mauaji hayo yakitokea Jumamosi iliyopita walipingana na polisi na kusema kuwa mkurugenzi huyo ndiye alimfyatulia risasi Isaka.

Alipoulizwa kuhusu taarifa hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Sweebert Njewike alishindwa kuikataa wala kuikubali taarifa hiyo, “kuhusu tukio hilo nimeshatoa taarifa tangu jana (juzi), hilo jambo nimeshalizungumza na kwa sasa nipo mpirani (Singida vs Yanga) nipigie baadaye.”

Mwananchi lilipotaka kufahamu zaidi kuhusu taarifa hiyo, hasa inavyoeleza kuwa mkurugenzi hakuwepo ndani ya kanisa alisema, “taarifa hiyo nimeshatoa.”

Taarifa hiyo imewataja watu wengine sita wanaoshikiliwa akiwemo mkurugenzi huyo kuwa ni Silvanus Lungwisha (ofisa kilimo na mifugo wa Itigi), Elik Paul (ofisa sheria Itigi), Eliutha Augustino (ofisa tarafa), Yusuph John (ofisa mtendaji wa kijiji cha Kazikazi), Rodey Elias na Makoye Steveni (wote maofisa wanyamapori).

Inaeleza kuwa mauaji hayo yalitokea baada ya Luhende kuwafuata watuhumiwa wa kosa la kuharibu mali na mlalamikaji Rose Andrew aliyedai kuharibiwa mali yake iliyopo ndani ya shamba la Tanganyika Packers linalomilikiwa na halmashauri hiyo.

“Maofisa walipata taarifa kuwa baadhi ya watuhumiwa wa kosa la kuharibu mali wapo katika Kanisa la Wasabato lililopo kijijini hapo ndipo walipokwenda kwa lengo la kuwakamata,” inaeleza taarifa hiyo.

Baba asimulia kifo cha mwanaye

Baba mzazi wa Isaka, Petro Chambalo alisema alikuwa na ugomvi na Luhende na kuna kesi mbili mahakamani alizodai kubambikiwa na mkurugenzi huyo.

Alisema tangu 2017 amekuwa akitofautiana naye na mara kadhaa ameagiza akamatwe na hakuna aliloelezwa zaidi ya kushinda siku nzima polisi na wakati mwingine kufikishwa mahakamani bila kusomewa shtaka lolote.

“Luhende ndiye alikuja na wenzake sita, alianza kuingia yeye na kufuatiwa na mtendaji wa kijiji kuanza kutupiga ngwala, lakini yeye ndiye alinyoosha bunduki kumpiga mwanangu,” alisema Petro.

Alisema mkurugenzi huyo aliingia kanisani akitaka John amuonyeshe aliokuwa anawataka huku nje risasi zikiwa zinapigwa.

“Waumini wengine walikuwa kimya na Isaka alisimama kuhoji mbona wamevamia kanisani kuna nini. Hakujibiwa zaidi ya mwenzetu James Jackson kuburuzwa nje akiwa amekabwa na watu wawili na mmoja nilimtambua ni ofisa kilimo anaitwa Lungwisha,” alisema.

“Nilisimama na kwenda kumsaidia nikitaka watuambie nini kimetokea, lakini mkurugenzi aliponishika nilimsukuma na hapo ndipo aliondoka kwenda kwenye gari yake kisha akachukua silaha na kurudi tena.”

Alisema wakati mkurugenzi akirejea tena kanisani, marehemu alikuwa akiimba nyimbo za sifa, “alizunguka upande wa dirishani watu wakimuona kisha akamlenga na kumpiga kichwani.”

Elias ambaye ni kaka wa marehemu alisema, “Alitoka (Isaka) mbele ya kanisa na kumsihi baba asigombane nao ndani ya kanisa. Alimsikiliza na kuacha lakini milango ikafungwa wakati risasi zikilia nje.”

“Mlango tulisaidia wote kuusukuma ukafunguka kisha tukajibanza kwenye kona wote wawili, lakini (huku akilia) niliona mtu anadondoka kugeuka nikakanyaga ubongo wake kwani kichwa kilifumuliwa.”

Alisema mkurugenzi huyo alikuwa na bunduki na walidhani kuwa atapiga risasi hewani lakini alimuelekezea mdogo wake na kufyatua risasi iliyopiga hadi ukutani.

Mke wa marehemu, Leah Pius alisema,”Mume wangu alikuwa anakaribia kupata daraja la uchungaji, ameniachia watoto watatu mkubwa akiwa na miaka sita tu.”

Kwa upande wake shuhuda mwingine wa tukio hilo, James alisimulia alivyobebwa juu kutolewa nje ya kanisa hilo, jinsi waumini wenzake walivyochukizwa na kitendo hicho na kuanza kuhoji kulikoni.

Neema Festo, mke wa mwinjilisti wa kanisa hilo, alisema wakiwa ndani ya kanisa aliingia mkurugenzi huyo na kutamka “Tumsifu Yesu Kristu”, akiwa ameongozana na mtendaji wa kijiji.

“Huyu Mtendaji wa Kijiji ndiyo namfahamu kabisa maana nyumba aliyopanga na nyumba ninayoishi zinatazamana hivyo namfahamu, aliingia na wengine pia wakawa wakali wakionyesha kama wanamtafuta mtu mwingine,” alisema.

“Lakini ujue pale paligeuka uwanja wa vita, hakuna mtu aliyetuambia tulale bali risasi zilikuwa zinapigwa nje mfululizo hadi nikahisi kama vile tuko vitani, mimi nilikuwa na wanangu hawa wawili nikaamua kujikunyata nao lakini nikiendelea kuimba mara nikasikia wameua ndo nikaona Shemasi amelala kichwa kimefumuliwa na ubongo kumwagika.”

Chanzo cha mgogoro

Mgogo wa ushuru wa mashamba katika mbuga ya kitongoji cha Boma la kati unatajwa kuwa ndiyo chanzo cha tukio kwani halmashauri inasema mashamba hayo ambayo awali yalikuwa yakimilikiwa na Tanganyika Packers ni sehemu yao.

Maswali 10

1. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itigi alifuata nini kanisani?

2. Je, ni kweli mkurugenzi huyo ana ugomvi na baba wa marehemu?

3. Je, mkurugenzi ndiye aliyetoa bunduki na kumfyatulia Isaka Isaka na kumuua?

4. Polisi wanasema tukio la mauaji lilitokea wakati mkurugenzi akiwa amekimbia je, ni nani aliyefanya mauaji hayo?

4. Polisi wanasema mkurugenzi huyo alikimbia na kufunga mlango, kwa nini alifunga mlango wa kanisa?

5. Baba wa marehemu anasema alishuhudia mkurugenzi akifyatua risasi, nani anazungumza ukweli, baba au polisi?

6. Je, ni kweli kuna kesi mbili mahakamani kati ya mkurugenzi na baba wa marehemu?

7. Kulikuwa na ulazima wowote wa mkurugenzi na msafara wake kwenda kudai ushuru wa mashamba kanisani?

8. Je, ni kawaida kwa mkurugenzi kupita mtaani kudai ushuru kwa wananchi?

9. Ni kwa nini Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo ameshiriki mazishi ya Isaka Isaka na kutoa ubani wa Sh1 milioni?

10. Je, ni kwa nini polisi, uongozi wa Singida haukutoa ushirikiano kwa waandishi wa habari kuzungumzia sakata hilo lilipotokea siku hiyo?
Na Habel Chidawali, Mwananchi
Share:

WAZIRI WA UTALII AZINDUA SHINDANO LA KUTAFUTA WANAWAKE WENYE MAKALIO MAKUBWA


Wanawake wenye makalio makubwa (picha kutoka mtandaoni)
Waziri waziri wa Utalii Godfrey Kiwanda akizindua shindano la kusaka mwanamke mwenye makalio makubwa
Waziri wa Utalii Godfrey Kiwanda akiwa na warembo wa Uganda

Wizara ya Utalii nchini Uganda imewaainisha wanawake wenye umbile namba 8, makalio makubwa na miguu minene kuwa kivutio cha utalii nchini humo.

Akizindua shindano la "Miss Curvy" ambalo litaonyesha shepu halisi ya wanawake wa Kiafrika ambalo litawawezesha wanaweke kuonyesha makalio yao makubwa, Februari 5,2019, Waziri wa Utalii Godfrey Kiwanda alisema Uganda ina wanawake warembo wenye shepu za kuvutia na hivyo serikali itawatumikia wanawake hao kukuza sekta ya utalii.

 Gazeti la Daily Monitor, lilisema kuwa wanawake wote wenye figa nzuri watashiriki katika shindano la kubaini nani ndiye aliye na umbile bora zaidi na atachaguliwa kuwakilisha nchi hiyo. 

"Tuko na wanawake warembo sana humu nchini, wenye shepu ya kudondosha mate kwa kila mwanaume, mbona tusiwatumie hawa watu kukuza sekta ya utalii humu nchini?" Waziri Kiwanda alisema.

Ann Mungoma ambaye ni mwandalinzi wa shindano hilo alisema, sekta ya utalii itaboreshwa punde tu mwanamke mwenye figa na makalio ya kuvutia atakapochaguliwa.

 Mungoma alisema Waafrika wanapaswa kuelewa kuwa watu wanene pia wanaweza kuwa warembo wala sio wembamba pekee. 

 "Miss Curvy in tamasha ambalo litaonyesha shepu halisi ya wanawake wa Kiafrika, tamasha hilo ni la kipekee ambalo litawawezesha wanaweke kuonyesha makalio yao makubwa, umbile namba 8 na kila kitu walichojaliwa nacho mwilini mwao," Mungoma alisema. 

Share:

LEMUTUZ AWAJIA JUU WANAOICHAFUA EQUITY BANK

LIVE STRAIGHT TALK: The Art of FACTS mimi ni mteja wa Equity Bank I was shocked last week kuona habari za kuichafua my Bank ambayo kabla ya kufungua my account tayari nilishafanya utafiti wa kutosha na kuijua vizuri bank hii ambayo wala sio siri kwa maoni yangu ndiyo THE BEST BANK nchini so far ambayo ilianzishwa Mwaka 2012 na kwa sasa ina Branches 15 Tanzania nzima pamoja na Zanzibar na tayari wanazo ATM’s 21 wakiwa na nia ya kubadilisha maisha ya Wananchi wa kawaida kiuchumi kwa kuwapatia huduma bora na fursa.

Equity Bank Limited Tanzania ni part of Equity Group Holdings Plc iliyoanzishwa Mwaka 1984 kutokea Kenya na Mkurugenzi wake wa kwanza akiwa Dr. James Mwangi na leo Equity ipo Africa nzima na inaongoza masoko ya nchi za Kenya, Uganda na Rwanda, Congo-DRC, South Sudan.
Bank hii ina wateja Millioni 21.8 na mtaji wa jumla ya Dola za Kimarekani USD 5.7 Billioni, kwa ujumla wake ni Bank ambayo inashika nafasi ya 11 Duniani kwa Matokeo na Mali ilizonazo.
Mwaka uliopita ilishinda zawadi ya “African Bank of the Year” na Mkurugenzi wake Mkuu Dr. James Mwangi ameshinda pia zawadi ya “African Banker of the Year 2018”.
Sasa kwahayo machache naomba kuwakumbusha wale wote wanaohangaika kuichafua Bank hii kwamba mmepotea sana ushindani wa bank ufanyike kwa kazi na sio kuchafuana mitandaoni cause binafsi siwezi kunyamaza kuona Bank yangu inachafuliwa kwa sababu za kiushindani wa kibiashara …I salute you Equity Bank endeleeni kusaidia Wajasiriamali wanyonge nchini kwa mikopo yenye riba nafuu na pia endeleeni kutusaidia hata sisi wajasiriamali wadogo wadogo kwa mikopo nafuu ..haya makelele ya Social Media niachieni mimi hahahahaha U know …MUNGU AIBARIKI TANZANIA! AMEN! – @ lemutuz_superbrand
Share:

BUNGE KUSIMAMISHA MSHAHARA WA TUNDU LISU

Spika wa Bunge Job Ndugai amesema atasimamisha Mshahara na Malipo yote ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lisu kutokana ana Ofisi yake kutokuwa na Taarifa sahihi ya mahali alipo kwasasa na anachokifanya huko. Spika Ndugai ametoa taarifa hiyo Bungeni wakati akijibu Muongozo wa Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Msukuma ambapo amesema Mbunge huyo hayupo Hosipitali,Hayupo Bungeni na hayupo Tanzania wala hajulikani anafanya kitu gani huko aliko hivyo hana sababu ya kuendelea kulipwa.  Tundu Lissu ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, yupo katika ziara ya siku 10 nchini Marekani baada…

Source

Share:

MAJAMBAZI WATATU WAUAWA USIKU WA MANANE MWANZA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, limeua watu watatu kwa tuhuma za ujambazi. Inadaiwa watu hao walikuwa na silaha ya moto ambayo haijafahamika ni ya aina gani katika maeneo ya Nyakabungo Kata ya Isamilo wilayani Nyamagana. Kaimu Kamanda wa jeshi hilo mkoani Mwanza Advera Bulimba, alithibitisha kuuawa kwa watuhumiwa hao, huku akifafanua kuwa wengine watatu wanasadikika kutokomea kusikojulika. Tukio hilo lilitokea  juzi majira ya saa nane usiku, baada ya askari kupokea taarifa toka kwa raia wema kuwa katika maeneo hayo kunasikika milio ya risasi ambayo ilikuwa inaashiria kuwapo kwa uvunjifu…

Source

Share:

Video Mpya : RAYVANNY FT DIAMOND PLATNUMZ - TETEMA

Itazame hapa video ya Rayvanny Ft Diamond Platnumz - Tetema

Share:

Wednesday, 6 February 2019

Pata Habari 24 Hours : Pakua Upya App ya Malunde 1 blog ...Imeboreshwa Kukupa Raha zaidi

Kuwa wa Kwanza kupata habari na matukio yanayojiri Tanzania na dunia kwa ujumla kwa kupakua/ kudownload App ya Malunde 1 blog tukuhabarishe masaa 24.

Tembea na dunia kiganjani mwako sasa.

Pakua App mpya ya Malunde 1 blog imeboreshwa zaidi ili kukidhi mahitaji ya wasomaji wetu. Hii ndiyo mpya kabisa,ina alama hii ↡↡
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Ni rahisi sana : Ingia Play store kisha Andika Malunde 1 blog halafu bonyeza Install

https://bit.ly/2Qb7qyF

NB: App uliyokuwa unatumia mwanzo tumeifuta na kuleta mpya ya kisasa zaidi..Tafadhali fuata maelekezo hapo juu... Usikubali kukosa habari kizembe..Pakua app yetu Mpya ya Malunde1 blog Sasa
Share:

DC KABEHO AZITAKA MAHAKAMA TARIME KUWATENDEA HAKI WANYONGE

Na Dinna Maningo,Tarime  Mkuu wa wilaya ya Tarime Charles Kabeho amewataka Mahakimu,Waendesha Mashtaka na Wanasheria  kutenda haki katika kesi zinazofikishwa Mahakamani zikiwemo kesi za wananchi wanyonge ambao matumaini yao ni kuona Mahakama inawatendea haki. Kabeho ameyasema hayo wakati  wa maadhimisho ya siku ya Sheria yaliyofanyika kiwilaya katika Mahakama ya wilaya ya Tarime yaliyohudhuriwa na wadau mbalimbali baadhi yao wakiwemo watumishi wa Mahakama za Tarime, Mawakili wa Serikali,Mawakiki wa kujitegemea,Waendesha mashtaka wa Polisi,Askari,Magereza,Takukuru,Asasi za Kiraia,Ofisi ya Ustawi wa Jamii Tarime na Wananchi. Kabeho alisema kuwa haki ikitendeka inaleta imani kubwa kwa…

Source

Share:

KESI YA MAUAJI YA MWANAFUNZI SPELIUS ERADIUS YASIKILIZWA KAGERA

Na: Mwandishi wetu Kagera. Mkoa wa Kagera katika kuadhimisha kilele cha wiki ya Sheria Februari 6, 2019 Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Bukoba chini ya Jaji Mfawidhi Lameck Mlacha imeweza kusikiliza kwa mara ya kwanza kesi Namba 56 ya mwaka 2018 ya Mwalimu Respikius Patrick Mtazangira na Mwalimu Erieth Gerald dhidi ya mauaji ya Mwanafunzi marehemu Spelius Eradius wa Kibeta Shule ya Msingi Manispaa ya Bukoba aliyepigwa hadi kupelekea umauti wake tarehe 27.08.2018 Katika shauri hilo upande wa Jamhuri uliwakilishwa na Wakili Msomi Chema Maswi Kaimu Mwendesha Mashitaka Ofisi ya…

Source

Share:

ACSEE Exam 2019 Time Table | Ratiba ya Mtihani Kidato cha sita 2019

ACSEE Exam 2019 Time Table | Ratiba ya Mtihani Kidato cha sita 2019

NOTICE TO CANDIDATES
1. You are required to appear for the examination(s) at the centre(s) under which you are registered unless
otherwise advised by the Council in writing.
2. You are required to observe all instructions given to you by the Supervisor, Invigilators or Officers of
the Council responsible for the conduct of the examinations.
3. If you arrive more than half an hour late for an examination, you will not be admitted.
4. You are required to attend punctually at the time shown on your timetable. If you arrive more than half
an hour late for an examination, you will not be admitted.
5. After the first half-hour, you may leave as soon as you have finished your paper and handed in the
script to the Supervisor/Invigilator. You may leave the room temporarily at any time after the first halfhour but only with the permission of the invigilator.
6. You may bring into the examination room only instruments which are specifically permitted. If you are
suspected of cheating or attempting to cheat, or assisting someone else to cheat, the facts will be
reported to the Council. You may in consequence be disqualified from the examination and excluded
from all future examinations of the Council. Any notes or other unauthorised material found in the
examination room may be retained by the Council at its discretion.
7. Communication, verbal or otherwise, between candidates is not allowed during the examination. If any
candidate wishes to communicate with the invigilator he should raise his hand to attract attention.
8. You must write your examination number correctly on every answer sheet of the answer booklet/answer
sheet used. Using anybody else’s examination number is considered a case of dishonesty that may
lead to cancellation of examination results. Names, initials or any other mark that would identify a
candidate should never be written on answer books or sheets of paper.
9. If you are found guilty of dishonesty in connection with the examination you may be disqualified in the
entire examination.
10.You should not write any notes on your question paper. Use the last pages of your answer booklet to
do rough work but ensure that you cross to indicate that it is not something to be marked.
11.You should not take anything from the examination room, unless instructed otherwise. You should not
destroy any paper or material supplied in the examination room.
12.Write in blue or black ink or ball pen. Draw in pencil.
13.Smoking is not permitted in the examination room.
14.Private candidates should produce a letter from the Council allowing them to sit for the particular
examination at the prescribed centre, otherwise they will not be allowed to sit for examination.
However, they are strictly not allowed to write anything in new letter.
15.The examination will continue as scheduled even if it falls on a public holiday.

The post ACSEE Exam 2019 Time Table | Ratiba ya Mtihani Kidato cha sita 2019 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

PAPA FRANCIS AKIRI HADHARANI MAASKOFU NA MAPADRE KUWANYANYASA KINGONO WATAWA



Mtawa
Papa Francis 
Papa Francis amekiri kuwa makasisi wa kanisa katoliki wanawatumikisha kingono watawa wa kanisa hilo na kwamba tatizo hilo limekuwa likiendelea.

Papa Francis alikitaja kisa hicho wakati akilijibu swali kuhusu unyanyasaji wa kingono unaofanywa na mapadre dhidi ya watawa wakati wa kikao cha waandishi wa habari hapo jana aliporejea nyumbani kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu. 

Ilikuwa ni mara ya kwanza ya kwa Papa Francis kukiri hadharani kuhusu tatizo la mapadre na maaskofu kuwanyanyasa kingono watawa.

 Alisisitiza kuwa kanisa katoliki limekuwa likilishughulikia saala hilo kwa muda sasa na akaapa kuchukua hatua zaidi.

Alisema kuwa mtangulizi wake Papa Benedict, alilazimika kufunga shirika la zima la watawa ambao walikuwa wakidhulumiwa kingono na makasisi.

Inaaminiwa kuwa hii ni mara ya kwanza Papa Francis amekiri hadharani kuhusu dhuluma za kingono dhidi ya watawa wa kanisa hilo kubwa zaidi duniani.

Amesema kuwa kanisa limejaribu kukabiliana na tatizo hilo na kwamba juhudi hizo bado ''zinaendelea''.

Alikiri kuwa makasisi na maaskofu wamekuwa wakiwanyanyasa watawa, na kwamba kanisa "linashughulikia suala hilo".

"Ni mpango ambao tumekuwa tukiendeleza,"alisema.

Hata hivyo Kanisa Katoliki leo limeyafafanua matamashi ya Kiongozi wa kanisa hilo Papa Francis kuhusu kisa cha kile alichokiita kuwa ni "utumwa wa ngono" katika shirika moja la watawa la kifaransa, likisema kuwa alimaanisha matumizi mabaya ya madaraka ambayo yalionekana katika matukio ya unyanyasaji wa kingono.

Mwezi Novemba mwaka jana kongamano la kimataifa la watawa wa kanisa katoliki duniani lililaani "utamaduni wa ukimya na usiri" ambao unawazuia kuzungumzia changamoto wanazopitia.

Siku chache zilizopita jarida la wanawake wa Vatican linalofahamika kama Women Church World lililaani vikali unyanyasaji huo ikiongeza kuwa katika visa vingine watawa wanalazimishwa kuavya mimba ya makasisi hao kwasababu kuwa na watoto-ni kitu kinachoenda tofauti na maadili ya ukatoliki.

Jarida hilo limesema vugu vugu la #MeToo limewasaidia wanawake wengi kujitokeza na kusimulia visa vyao.

Chanzo -DW Swahili & BBC Swahili
Share:

MTOTO AUAWA KISHA KUTUPWA KWENYE DAMPO

Mtoto anayekadiriwa kuwa umri wa miezi saba amekutwa ameuawa kikatili na mwili wake kutelekezwa katika kontena la taka lililopo soko la Kihesa manispaa ya Iringa.

Akizungumza na mtandao huu Mwenyekiti wa Mtaa wa Sokoni Agustino Kimulike amesema kuwa dampo hilo linatumika na mitaa mitatu hivyo kama serikali wanaendelea kushirikiana na wananchi ili kumbaini mwanamke aliyefanya kitendo hicho.

Kwa upande wake Mtendaji wa Kata ya Kihesa, Swebe Datus amesema kuwa wananchi wanapaswa kukomesha matukio kama hayo kwani yanaleta sifa mbaya katika jamii.

Nao baadhi ya wananchi wa Mtaa huo Kata ya Kihesa wamelaani wanawake na mabinti wanaofanya vitendo hivyo kuongeza kuwa kama hawana uwezo wa kulea ni vyema wakatumia uzazi wa mpango ili kuepuka kubeba mimba zisizotarajiwa.

Mwili wa mtoto huyo umechukuliwa na jeshi la polisi kwajili ya taratibu za mazishi na kutoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi kwa lengo la kubaini mtu aliyefanya tukio hilo.


Via Nipashe
Share:

MAHAKAMA YAANZA KUSIKILIZA KESI YA MWALIMU ALIYEUA MWANAFUNZI

 
Picha hii haihusiani na habari

Mahakama kuu kanda ya Bukoba, leo imeanza kusikiliza kesi ya mauaji ya kukusudia inayomkabili Herieth Jerald ambaye ni mwalimu wa shule ya msingi Kibeta iliyoko Manispaa ya Bukoba.

Mwalimu huyo pamoja na mwenzake, Respicius Patrick wanadaiwa kutekeleza mauaji ya mwanafunzi wa darasa la tano katika shule hiyo aliyejulikana kwa Sperius Eradius aliyekuwa na umri wa miaka 14, akimtuhumu kuiba pochi yake.

Mwanafunzi huyo Sperius Eradius katika kesi hiyo anadaiwa kuuawa na walimu hao kwa kupigwa Agosti 27 mwaka jana, akidaiwa kuiba pochi ya mwalimu Heriet Jerald baada ya kumpokea mizigo wakati akiingia kazini.

Mahakama imeelezwa na mwendesha mashtaka kiongozi wa serikali, Chema Maswi kuwa washtakiwa hao walimuua kwa kukusudia mwanafunzi huyo katika eneo la shule ya msingi Kibeta, ambapo washtakiwa walikana mashtaka hayo.

Mshtakiwa mmoja kati ya sita waliokuwa wameletwa mahakamani hapo Benidius Benezeth ambaye ni mwendesha pikipiki aliyemsafirisha mwalimu Herieth Jerald alitoa ushahidi dhidi ya mwalimu huyo na kudai kuwa wakati akimsafirisha hakuona kama katika kikapu alichokuwa amebeba kuna pochi maana hakukikagua.

Baada ya kesi hiyo kuhairishwa hadi Februari 08 mwaka huu ushahidi utakapoendelea kutolewa, mwendesha mashtaka kiongozi wa serikali Chema Maswi ameeleza mwenendo wa kesi hiyo kwa upande wa serikali.
Chanzo- EATV
Share:

WATATU WAUAWA KWA KUPIGWA RISASI MWANZA



Moja ya mwili aliyepigwa risasi

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limefanikiwa kuwaua majambazi watatu waliokuwa na silaha za moto na silaha za kijadi ambao walifika katika maeneo ya Nyakabungo, Kata ya Isamilo wilayani Nyamagana kwaajili ya kufanya uhalifu wa kuvunja maduka ya wafanyabiashara.

Majambazi hao walifika katika mtaa huo kwa lengo la kuvunja maduka ya wafanyabiashara ndipo raia wema walipotoa taarifa kwa Jeshi la Polisi.

Askari Polisi waliokuwa doria baada ya kupata taarifa hizo walifika katika eneo la tukio na majambazi walipogundua uwepo wa askari katika eneo hilo walianza majibizano ya risasi ili kujihami.

Advera Bulimba ni Kaimu Kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza amethibitisha kuuawa kwa majambazi hao pamoja na kutoa wito kwa wananchi wanaofanya uhalifu mkoani humo kutojihusisha na matukio ya kihalifu.

Miili ya majambazi hao watatu imehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa ya Mwanza Sekoutoure kwa ajili ya utambuzi.
Via>EATV
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger