Sunday, 27 January 2019

ASKOFU KAKOBE AGOMA KUTEULIWA NA RAIS MAGUFULI..AIKANA CHADEMA NA CCM


Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zacharia Kakobe

Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zacharia Kakobe amesema hajawahi kumiliki kadi ya chama chochote cha siasa nchini, bali amekuwa akishiriki shughuli za vyama hivyo kutokana kupewa mialiko kufika kama mtumishi wa kiroho.

Kakobe ametoa kauli hiyo Jijini Dar es salaam wakati wa muendelezo wa ibada yake ya kila Jumapili kanisani kwake ambapo hana mahusiano na viongozi wowote wa kisiasa hasa wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.

Kakobe amesema, "sijawahi kuwa mwanachama wa chama cha Chadema wala CCM, na sina kadi ya vyama hivyo, na wala sijawahi kuwasiliana na kiongozi yoyote wa CHADEMA wala kuonana nao ana kwa ana, wala hawajawahi kuja ofisini kwangu, halijawahi kutokea"

Aidha ameongeza kuwa, "niliwahi kuitikia mwaliko wa chama cha CHADEMA mara moja tu miaka michache iliyopita kwenye mkutano uliofanyika eneo la Mlimani City na nilienda kama baba anayeweza kualikwa na watoto".

Kiongozi huyo amesema hayuko tayari kupokea nafasi yeyote kama akiteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kile alichokidai kuwa tayari anayo kazi ya kufanya ambayo ni kumtumikia Mungu.

"Hata Rais Magufuli akiniteua Leo siwezi kukubali, nitamueleza nina kazi maalum ya kumtumikia Mungu, siwezi kuwa mbunge alafu nikakaa bungeni miezi mitatu niache kumtumia Mungu".

Chanzo - EATV
Share:

POLISI WAKANUSHA TAARIFA YA MAJAMBAZI KUVAMIA GESTI NA KUBAKA WAHUDUMU MBEYA


Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linapinga vikali taarifa iliyotolewa na gazeti la Nipashe katika toleo Na.0579824 la Januari 26, 2019 yenye kichwa cha habari “Unyama wa kutisha” Majambazi wavamia gesti, wabaka wahudumu na kupora fedha….baada ya kuwapa vinywaji na biskuti zenye….

Ni kwamba Januari 24, 2019 saa 06.00 asubuhi iliripotiwa taarifa kuwa huko katika Bar na nyumba ya kulala wageni ijulikanayo kwa jina la Malema iliyopo maeneo ya Makunguru, Kata ya Manga, Tarafa ya Sisimba, Jiji na Mkoa wa Mbeya watu watatu waliofahamika kwa majina ya LUCY MWAPASI [36] Mhudumu na mkazi wa Mwanjelwa, CHRISTINA KIPESI [37] Mkazi wa Ituha na DICKSON ALLY [22] Mlinzi na Mkazi wa Makunguru waligundua kuibiwa simu zao za mkononi tano [05] na fedha taslimu za mauzo ya Bar na nyumba ya kulala wageni kiasi cha shilingi 701,000/= na watu wawili wanaowafahamu kwa sura.

Inadaiwa kuwa watu hao walifika katika nyumba hiyo ya kulala wageni na mmoja wapo alichukua chumba namba 11 ambapo aliishi hapo kwa siku tatu [03] hivyo kujenga mazoea ya karibu na wahudumu hao.

Januari 23, 2019 saa 23:30 usiku muda wa kufunga Bar ulipofika, walibaki wahudumu wawili huku mmoja akiwa wa Bar na mwingine wa nyumba ya kulala wageni na mlinzi ndipo watu hao walitoka chumbani kwao na kuwaambia wale wahudumu kuwa wanataka kuwapa offer ndipo walikubali na kuwanunulia juice ya azam na biskuti wahudumu hao, vitu ambavyo vinadaiwa kuwa na madawa yadhaniwayo ya kulevya na baada ya kula wote walianza kulegea na kulala na kupoteza fahamu na kisha watu hao kutekeleza adhima yao ya wizi.

Wahanga walipata msaada toka kwa wasamaria wema majira ya saa 09:00 asubuhi ambapo walipelekwa Hospitali ya Rufaa Mbeya kwa matibabu. Kwa mujibu wa mganga wa zamu aliyewafanyia uchunguzi na kugundua kuwa wahanga hao watakuwa wamekula/kunywa chakula chenye sumu au kinywaji chenye sumu hivyo aliwapatia matibabu kuondoa sumu mwilini na baada ya siku moja waliruhusiwa kutoka Hospitalini baada ya kupata nafuu.

Baada ya tukio hilo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanya upelelezi wa shauri hili na kubaini kuwa wahudumu hao hawakubakwa kama ilivyoripotiwa katika gazeti tajwa hapo juu. Aidha uchunguzi wa kitabibu uliofanywa na daktari wa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya unaonyesha kuwa wahanga wa tukio hili hawakubakwa.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linapinga vikali taarifa hiyo iliyotolewa na gazeti la Nipashe na kulitaka gazeti hilo kuomba radhi na kukanusha kupitia gazeti hilo taarifa waliyochapisha kwenye toleo Na. 0579824 la Januari 26, 2019 kwani ni kinyume na kifungu cha sheria ya “Media Service Act 36 (12) ya mwaka 2016 na kifungu cha sheria ya Media Service Act 50 (12) (1) (a) – (f) na (2) (a) – (c) ya mwaka 2016.
Share:

Pata Habari 24 Hours : Pakua Upya App ya Malunde 1 blog ...Imeboreshwa Kukupa Raha zaidi

Kuwa wa Kwanza kupata habari na matukio yanayojiri Tanzania na dunia kwa ujumla kwa kupakua/ kudownload App ya Malunde 1 blog tukuhabarishe masaa 24.

Tembea na dunia kiganjani mwako sasa.

Pakua App mpya ya Malunde 1 blog imeboreshwa zaidi ili kukidhi mahitaji ya wasomaji wetu. Hii ndiyo mpya kabisa,ina alama hii ↡↡
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Ni rahisi sana : Ingia Play store kisha Andika Malunde 1 blog halafu bonyeza Install

https://bit.ly/2Qb7qyF

NB: App uliyokuwa unatumia mwanzo tumeifuta na kuleta mpya ya kisasa zaidi..Tafadhali fuata maelekezo hapo juu... Usikubali kukosa habari kizembe..Pakua app yetu Mpya ya Malunde1 blog Sasa

Share:

SIMBA YATAJA MASHARTI YA MKATABA WA KOCHA AUSSEMS


Kocha Patrick Aussems

Kufuatia gumzo kubwa mitandaoni baada ya Simba kutolewa katika mashindano ya SportPesa, uongozi wa klabu hiyo umeweka wazi juu ya makubaliano ya mkataba wa kocha mkuu, Patrick Aussems.

Hatua hiyo imefikia baada ya mashabiki wengi wa Simba kukasirishwa na kitendo cha klabu hiyo kushindwa kusonga mbele katika mashindano hayo, ikitolewa na Bandari FC ya Kenya.

Akizungumzia juu ya matokeo yasiyoridhisha na hatma ya kocha Aussems, Ofisa Habari wa Simba , Haji Manara amesema katika mkataba wa Simba na kocha huyo hakuna makubaliano juu ya makombe mengine zaidi ya kombe moja na sharti ambalo tayari amelitimiza.

"Kwenye mkataba wa Aussems tumemwambia kwamba tunahitaji atufikishe hatua ya makundi ya Klabu Bngwa Afrika jambo ambalo amefanikiwa kulifanya na lipo kwenye mkataba pamoja na kutupatia ubingwa wa Ligi Kuu Bara ambao upo mikononi mwetu", amesema Manara.

"Hayo makombe mengine hatujaweka kwenye makubaliano tunashiriki kulinda heshima na tukifanikiwa kupata ni jambo jema hivyo kushindwa kuyapata kwetu haina maana kwamba kocha hafai hapana tuna mipango yetu na tunafanya kazi kwa utaratibu", ameongeza.

Katika siku za hivi karibuni, Simba imeshuhudia ikipoteza nafasi moja ya kushiriki michuano ya kimataifa baada ya kuondolewa na Mashujaa FC katika mzunguko wa nne wa kombe la shirikisho, ambapo hivi sasa inategemea nafasi ya kushinda ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara au ishinde ubingwa wa Klabu Bingwa Afrika ili ipate tiketi ya kucheza michuano ya kimataifa msimu ujao.
Share:

MATANGAZO YA MICHEZO YA KUBAHATISHA YAZUIWA TANZANIA

Michezo ya kubatisha nchini Tanzania imekuwa maarufu huku washiriki zaidi wakiwa vijana lakini sasa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha imezuia kwa muda urushaji wa matangazo ya michezo hiyo kupitia redio na televisheni.

Bodi hiyo imedai kuwa matangazo hayo yamekuwa mengi kiasi cha kuharibu taswira ya mchezo huo.

Taarifa ya bodi hiyo ya Januari 23, 2019 iliyosainiwa na kaimu mkurugenzi mkuu, James Mbalwe inaeleza kuwa hatua ya kusitisha matangazo hayo ni kutokana na malalamiko miongoni mwa wananchi juu ya kukithiri kwa matangazo kwenye vyombo hivyo vya habari.

“Kumekuwa na ongezeko la malalamiko kutoka kwa umma juu ya kukithiri kwa matangazo ya michezo ya kubahatisha hapa nchini,” inaeleza taarifa hiyo.

“Bodi imesitisha kwa muda urushaji wa matangazo ya michezo ya kubahatisha kupitia redio na televisheni. Matangazo yanayotolewa kupitia vyombo vingine hayaathiriwi na zuio hili.”

Share:

DAWASA YAAHIDI KUWAPA MAJI WAKAZI WA GOBA NA VITONGOJI VYAKE


Waziri wa Maji na Umwangiliaji Profesa Makame Mbarawa (mwenye kofia nyeusi) akiwa ameongozana na msimamizi wa miradi alipofanya ziara katika Kata ya Goba, Manispaa ya Ubungo manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na kuwahakikishia wakazi hao kupatiwa maji ifikapo Februari Mosi mwaka huu. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Waziri wa Maji na Umwangiliaji Profesa Makame Mbarawa (mwenye kofia nyeusi) akipata maelezo toka kwa msimamizi wa miradi mara alipofanya ziara katika Kata ya Goba, Manispaa ya Ubungo manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Moja ya mita za maji ambazo zimeshasafungwa kwa wakazi wa Goba Kinzudi jijini Dar es Salam.

Waziri wa Maji na Umwangiliaji Profesa Makame Mbarawa (kulia) akijibu hoja za mkazi wa Goba Kinzudi jijini Dar es Salaam Waziri wakati alipofanya ziara katika Kata ya Goba, Manispaa ya Ubungo manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na kuwahakikishia wakazi hao kupatiwa maji ifikapo Februari Mosi mwaka huu.
Mkazi wa Goba Kizudi jijini Dar es Salaam Waziri akitoa shukrani zake za pekee mbele ya wanahabari kwa Serikali jinsi ambavyo imepanga kuwapatia maji.
Waziri wa Maji na Umwangiliaji Profesa Makame Mbarawa (kulia) akijibu hoja za mkazi wa Goba Kinzudi jijini Dar es Salaam Waziri wakati alipofanya ziara katika Kata ya Goba, Manispaa ya Ubungo manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na kuwahakikishia wakazi hao kupatiwa maji ifikapo Februari Mosi mwaka huu.
Mkazi wa Goba Kinzudi akimshukuru waziri kufika eneo lao na kusikiliza changamoto zao.

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Serikali imewathibitishia wakazi wa kata ya Goba, Manispaa ya Ubungo manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam uhakika wa kupata maji safi na salama kuanzia Februari mosi Mwaka huu.

Akizungungumza baada ya kufanya ziara katika maeneo hayo, Waziri wa Maji na Umwangiliaji Profesa Makame Mbarawa amesema Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA ) imepeleka vijana wapatao 50 kukamilisha mradi wa usambazaji maji katika maeneo hayo.

Amesema vifaa vyote vimefikishwa katika eneo hilo na vijana wameanza kazi rasmi.

"Kuanzia Ijumaa Februari mosi maji katika maeneo haya yataanza kutoka na kila mwananchi atapata maji safi na salama hivyo naomba muendelee kuwa wavumilivu wakati shughuli ya uunganishwaji mabomba inaendelea," amesema Profesa Mbarawa.

Amesema katika mitaa ya Kinzudi na kwa Ubarikio zilizopo katika kata hizo wanatarajia kuunganisha wateja wapya mia saba (700) ambao wanatarajia kuongeza mapato ya DAWASA.

"Tunakiri kukosea kwa kuwa hakukuwa na haja ya mradi huo kuchelewa kutokana na kutekeleza miradi mingi kwa wakati mmoja na sasa tumekubaliana kuwekeza nguvu  katika mradi mmoja na utakapokamilika tunahamia mwingine kwa wingi," amesema.

Kwa upande wao wakazi wa Mtaa hiyo wameishukuru serikali kwa kuwaahidi kupata maji kwani wamekuwa wakiteseka kwa kutumia muda mrefu kutafuta maji.

Mmoja wa wakazi hayo Juma Saidi amesema wamechimba mitaro  ili wapatiwe huduma hiyo ambapo kwa sasa wanaishukuru DAWASA kuwatua mzigo huo.

"Huku kwetu maji yamekuwa ni lulu maana yanauzwa shilingi 500 kwa ndoo jambo linalotufanya kuhangaike hata kuyapata," amesema.
Share:

HABARI KUBWA KWENYE MAGAZETI YA TANZANIA LEO JANUARI 27,2019

Fahamu yote yaliyojiri katika Magazeti ya Tanzania leo Januari 27, 2019. Hapa unapata habari zote zilizopewa uzito katika kurasa za mbele na kurasa za nyuma za habari za michezo na burudani.

Source

Share:

Saturday, 26 January 2019

TUNDU LISSU KUANZA ZIARA BARANI ULAYA KUANZIA JUMATATU


Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi katika nchi mbili barani Ulaya kuanzia Jumatatu Januari 28, 2019.
****

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA

ZIARA YA MWANASHERIA MKUU TUNDU LISSU (MB) ULAYA NA MAREKANI

Mwanasheria Mkuu wa Chama Mhe. Tundu Lissu anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi katika nchi mbili za Ulaya na Marekani kuanzia Jumatatu, Januari 28, mwaka huu, ambako mbali ya kufanya vikao kadhaa na viongozi wa kiserikali na jumuiya mbalimbali, pia atapata fursa ya kutoa mihadhara ya kitaaluma na kufanya mahojiano na vyombo vya habari.

Siku hiyo ya kwanza ya ziara yake, Mhe. Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki na Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, atakuwa nchini Ujerumani kwa siku mbili, ambako atakutana na baadhi ya maofisa wa Serikali pamoja na wabunge wa Bunge la Ujerumani.

Baadae Mhe. Lissu atazuru Makao Makuu ya Jumuiya ya Ulaya (EU) mjini Brussels, Ubelgiji ambako atakutana na baadhi ya watendaji wa jumuiya hiyo, wabunge wa EU pamoja na wanadiplomasia wa mataifa mbalimbali wanaowakilisha nchi zao EU.

Baada ya Ubelgiji, Mhe. Lissu ataelekea Washington DC, Marekani kwa siku 10 ambapo mbali ya kukutana na Watanzania wanaoishi nchini humo, hususan katika maeneo ya Washington, Houston, Texas, Birmingham na Alabama, atakutana pia na Maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani pamoja na  Watendaji wa Shirika la Kimataifa la Misaada la Marekani (USAID). Halikadhalika atakutana na Kamati za mabunge yote mawili ya Marekani zinazohusika na Uhusiano wa Nje (Afrika).

Katika ziara hiyo, Mhe. Lissu atapata fursa ya kuwasilisha mada juu ya masuala mbalimbali katika taasisi kadhaa muhimu, ikiwa ni pamoja na Center for Strategic and International Studies (CSIS) na The Atlantic Council and the World Resources Institute (WRI). Mhe. Lissu ana historia na taasisi ya WRI kwani aliwahi kuwa mmoja wa watafiti wake miaka ishirini iliyopita. 

Akiwa mjini Washington DC, Mhe. Lissu atakutana na kufanya mahojiano na baadhi ya vyombo vya habari vya kitaifa na kimataifa vilivyoko Mji Mkuu wa Marekani.

Mhe. Lissu atahitimisha ziara hiyo kwa kufanya mhadhara mkubwa wa umma katika Chuo Kikuu cha George Washington (GWU). Chuo hicho ni moja ya taasisi kongwe na kubwa za elimu ya juu nchini humo na duniani kwa ujumla.

Kutokana na umuhimu wa ziara hiyo kwa Chama, siasa za Tanzania na mapambano ya kutafuta mabadiliko ya kweli nchini kwa ujumla, siku ya Jumapili, Januari 27, mwaka huu, Mhe. Lissu atazungumzia baadhi ya masuala kuhusu ziara hiyo pamoja na maendeleo ya matibabu na hali ya afya yake.

Imetolewa leo Jumamosi, Januari 26, 2019 na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA
Share:

MWANAFUNZI MBARONI KWA KUMUUA MWALIMU WAKE KISA SIMU YA MKONONI

Wanafunzi wakilia kuomboleza kifo cha mwalimu wao

Mwanafunzi anatuhumiwa kumuua mwalimu wake katika shule sekondari nchini Kenya. Mwanafunzi huyo wa kidato cha nne ni mmoja wa washukiwa watatu wanaotuhumiwa kumuua mwalimu huyo, ambaye alimpokonya simu mmoja wao.

Taarifa kutoka shuleni hapo zimeeleza kuwa marehemu Peter Omari aliyekuwa mwalimu wa somo la Fizikia juzi Alhamis alimpokonya mwanafunzi wa kidato cha nne simu ya mkononi aliyokuwa amepewa na watu wawili kupitia ua wa shule.

 Maafisa wa polisi wanaamini kuwa, watu hao wawili walipanga njama na mwanafunzi huyo kumuua mwalimu Omar kwa nia ya kulipiza kisasi, kwani inasemekana mwaka 2017 watu hao hao walikamatwa wakimpa mwanafunzi mwingine simu ya mkononi.

Chifu anayesimamia eneo la Barut David Kering anaeleza kuwa mwili wa mwalimu huyo ulipatikana usiku wa juzi nyuma ya nyumba yake, dakika chache baada ya kutoka shuleni alikokuwa akisimamia masomo ya ziada.

"Mimi pamoja na maafisa wetu wa polisi tulifahamishwa jana usiku kuwa kuna mwalimu ameuawa katika shuel ya upili ya Hopewell. Tulifika hapa na kweli tukapata mwili wa mwalimu ukiwa chini, ikiwa dhahiri kwamba amepasuliwa kichwa kwa kupigwa kitu kizito,'' amesema chifu Kering na kuongeza kuwa maafisa wamemkamata mwanafunzi mmoja kutoka shule hiyo na mwingine kutoka shule jirani ambao wanasaidia kwa uchunguzi. 

''Kama serikali tutafanya uchunguzi na tuone kwamba waliohusika wametiwa nguvuni na kushtakiwa.” Ameahidi chifu afisa huyo.

Wahalifu waigeuza shule uchochoro wao

Eneo palipo shule hiyo pamehusishwa na uhalifu mwingi ambapo dawa za kulevya, vileo na simu za mkononi kati ya vitu vingine vimesemekana kuingizwa shuleni humo kwa njia isiyo halali. 

Vitalis Kahenda, mkurugenzi wa shule hiyo ya upili ya Hopewell anaieleza hii kama changamoto kubwa inayowakabili. "Tuna wanafunzi zaidi ya 400, wavulana kwa wasichana ingawa huduma za bweni ni za wasichana pekee. Swala la uhalifu katika eneo hili ni kero kubwa na limeathiri shule yetu pakubwa.'' Amelalamika Kahenda.

Mkuu huyo wa shule amesema pia kwamba wamelalamika mara kadhaa kwa maafisa wa usalama hasa kuwahusu hao watu wawili ambao walionekana shuleni hapo. ''Sio vileo pekee, hata dawa za kulevya huuziwa wanafunzi wetu, lakini hakuna lolote lililofanywa na maafisa hao. Hatuna udhibiti wa mambo lakini maafisa wa usalama wana kazi kubwa ya kufanya.” amemalizia.

Wanafunzi wamlilia mwalimu wao

Tukio hili limeibua hali ya majonzi na wasiwasi katika shule hiyo, wanafunzi wakionekana kumuomboleza mwalimu waliyemtaja kama mwalimu mwenye bidii. Faiza Otunga, mmoja wa wanafunzi anakumbuka matukio ya jana usiku, "mwalimu wetu alikuwa akitembelea kila darasa kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne. aliwazungumzia wanafunzi kwa upole. Huwa anatupa ushauri mzuri sana.”
Lango la kuingia katika shule ya sekondari ya Hopewell

Mwingine, Alvin Ochieng amesema ameshtushwa sana na kifo cha mwalimu wake, "ni kwa huzuni kubwa tunamuomboleza mwalimu Peter Omari, aliyekuwa mwalimu wetu wa somo la Fizikia na Kompyuta. Tulimpenda sana hata siwezi kuelezea.”

Mke wa mwalimu huyo ni mlezi katika shule hiyo na alikuwa amewachwa nyuma kuhakikisha kuwa wanafunzi wote walio kwenye mabweni wamelala bila kufahamu kuwa wahalifu hao walikuwa wanamsubiri mme wake kando ya nyumba yao ilioko karibu na shule hiyo.

Mamake marehemu, Florence Kerubo amesema amempoteza mtoto wa kwanza wa kiume aliyekuwa mwaminifu na mwenye upenzo mwingi. "Nimetumia pesa nyingi kumsomesha Peter na nilikuwa na matumani makubwa kwake. Wakati alipata kazi hapa akaendelea kuifanya alijiunga na chuo kikuu cha Mt. Kenya, sahii alikuwa mkufunzi alikuwa amalizie mwezi wanne, sssa ndoto yake imeishia hapo.'' amesema kwa majonzi mama huyo, na kuiomba serikali kufanya uchunguzi wa kina ijulikane sababu ya mtoto wake kuuawa.

Mwili wa Peter umehifadhiwa katika chumba cha maiti cha hospitali kuu ya kaunti ya Nakuru huku washukiwa watatu akiwemo mwanafunzi wakizuiliwa katika kituo cha polisi mjini Nakuru.

Mwandishi: Wakio Mbogho/DW Nakuru

Mhariri: Daniel Gakuba
CHANZO- DW
Share:

CHUO KIKUBWA CHA UFUNDI STADI VETA KUANZA KUJENGWA KAGERA.

Na,Mwandishi Wetu-Kagera Serikali imekamilisha miundombinu yote muhimu ikiwemo Maji, umeme na barabara kwa ajili ya kuanza kwa ujenzi wa Chuo Cha Ufundi stadi VETA mkoani Kagera. Kauli hiyo ya serikali imetolewa na Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako baada ya kuzindua chanzo Cha Maji ambacho kitatumika kwa ajili ya kujenga VETA hiyo katika kijiji Cha Burugo, Kwenye halmashauri ya Bukoba. “Dhamira ya Serikali ya awamu ya Tano ni kuwa nchi ya uchumi wa kati hadi ifikapo mwaka 2025 ili kutimiza malengo hayo ndiyo serikali imewekeza zaidi katika kujenga…

Source

Share:

Picha : BWAWA LAVUNJA KINGO NA KUUA WATU



Watu 200 hawajulikani waliko baada ya bwawa la maji kuvunja kingo zake katika mgodi wa kampuni ya chuma kusini mashariki mwa Brazil.

Maji yaliyochanganyika na matope yaliwafunika mamia ya wafanyakazi wa shirika hilo.

Shughuli ya kuwatafuta manusura inaendelea karibu na mji wa Brumadinho, katika jimbo la Minas Gerais.

Gavana wa jimbo hilo Romeu Zema amesema kuna hofu huenda watu wengi wamefariki katika mkasa huo.

Kufikia sasa watu tisa wamethibitishwa kufariki.Barabara zilizoharibiwa zinatatiza oparesheni ya kuwatafuta manusura

Baadhi ya watu waliyokwama kwenye matope, waliokolewa kwa kutumia helikopta baada ya barabara kuharibiwa.

Watu wengine wamehamishiwa kutoka makaazi yao kutokana na sababu za kiusalama.

Kwa mujibu wa afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya uchimbaji madini ya Vale, Fabio Schvartsman thuluthi moja ya wafanyikazi karibu 300 hawajulikani waliko.

"Nina hofu nataka kujua hali ni mbaya kiasi gani'' alisema Helton Pereira mmoja wa jamaa za watu waliyoathiriwa na mkasa huo aliyezungumza na BBC nje ya hospitali ya Belo Horizonte.

Anasema mke wake na dada yake wote hawajulikani waliko kwa sababu walikuwa wanaendesha biashara ya chakula karibu na eneo la tukio.

Shughuli ya kuwatafuta manusura inafanywa na maafisa 100 wa kukabiliana na hali ya dharura huku wengine zaidi wakitarajiwa kupelekwa katika eneo hilo.

"kuanzia sasa matumaini ya kuwapata waliyohai havuna pengine tutoe miili iliyokwama kwenye matope," alisema gavana Romeu Zema wa jimbo la Minas Gerais.Bwawa hilo linamilikiwa na kampuni kubwa ya uchimbaji madini ya Vale, Brazil
Rais wa Brazil Jair Bolsonaro ametaja mkasa huo kama ''janga la kitaifa''.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter aliandika "Tunajaribu kila tuwezalo kuwaokoa manusura zaidi wa mkasa huu,".

Maafisa wengine wakuu serikalini wamezuru eneo hilo.Watu wengi wanahofiwa kufariki baada ya bwawa la maji kuvunja kingo zake kusini mashariki mwa Brazil.Maji yaliyochanganyikana na matope yalisomba mkahawa wa chakula uliyokuwa na mamia ya wafanyakaziRais Jair Bolsonaro pamoja na maafisa wengine wakuu serikalini wanatarajiwa kuzuru eneo la mkasa
Share:

TCU: Scholarship Opportunities tenable in Republic of Turkey Institutions for the academic year 2019/2020

MINISTRY OF EDUCATION, SCIENCE AND TECHNOLOGY SCHOLARSHIPS TENABLE IN REPUBLIC OF TURKEY
INSTITUTIONS FOR THE ACADEMIC YEAR 2019/2020

1.0 Call for Application
Applications are invited from qualified Tanzanians for Bachelor’s, Master’s and Doctorate scholarships tenable in Republic of Turkey for the academic year 2019-2020

NB: IMPORTANT NOTES FOR THIS SCHOLARSHIP (MUST READ)

What the Scholarship Covers

How To Apply

Application Criteria

Scholarship Programs

2.0 MODE OF APPLICATION

i. The online application system : https://www.turkiyeburslari.gov.tr/
ii. Application Requirements click here: https://www.turkiyeburslari.gov.tr/en/page/prospectivestudents/application-criteria
iii. List of eligible study programs that the student can select from is available
here:https://www.turkiyeburslari.gov.tr/en/page/prospectivestudents/scholarship-programs
iv. Assessment and selection description is available
here: https://www.turkiyeburslari.gov.tr/en/page/prospectivestudents/evaluation-and-selection

NB:

i. Applications sent by mail or on hand will not be accepted.ii. Application are free of charge.
iii. Application is open to all academic levels (Bachelor’s, Master’s and Doctorate)

Applicant Must submit all required documents/forms online not later than Wednesday, 20 February 2019

 

NB: IMPORTANT NOTES FOR THIS SCHOLARSHIP (MUST READ)

What the Scholarship Covers

How To Apply

Application Criteria

Scholarship Programs

The post TCU: Scholarship Opportunities tenable in Republic of Turkey Institutions for the academic year 2019/2020 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

MATUSI YA WATANI, MASHABIKI KICHAPO CHA BANDARI KWA SIMBA YAMPA TABU MANARA

Uongozi wa Simba umeshangazwa na tabia za mashabiki kuwalaumu viongozi baada ya kupoteza mchezo wa jana wa SportPesa Cup hatua ya nusu fainali kwa kufungwa bao 2-1 na Bandari ya Kenya.

Simba jana ilitolewa kwenye hatua ya nusu fainali ya michuano ya SportPesa na kuyeyusha mipango ya kucheza na Everton ya England pamoja na kupishana na fuko la fedha za mshindi wa kwanza zaisi ya milioni 60.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema mashabiki wa Simba na watani zao wamekuwa wakiwasema kwa maneno mazito ambayo si ya kiungwana hali ambayo kishabiki haina maana.

"Wengi wananivaa mimi na kunipa lawama ambazo sistahili kisa tumefungwa, mashabiki wanapaswa watambue kuwa mimi si mchezaji, siwezi kufunga kazi yangu kubwa ni kuhamasisha mashabiki pamoja na wachezaji kucheza kwa morali.

"Wanalalamika mara Niyonzima amekosa nafasi ya wazi mnataka mimi nifunge? Okwi ameshindwa kufunga mimi nifanye nini, najua tumefungwa michuano ya SportPesa Cup tunashindwa kucheza na Everton ila lawama na matusi tunashushiwa viongozi, mashabiki tubadilike ," alisema Manara.

Chanzo- Saleh Jembe blog
Share:

WAKUU WA MIKOA WAITWA DAR JUMATATU VITAMBULISHO VYA JPM


 Wakuu wa mikoa wote nchini Tanzania wameitwa jijini Dar es Salaam kupeana mbinu mbalimbali kuhusu ugawaji vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo.

Imeelezwa kuwa vitambulisho hivyo vilivyotolewa na Rais John Magufuli ugawaji wake katika mikoa mbalimbali nchini ni wa kusuasua.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumamosi Januari 26, 2019 mjini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Seleman Jafo katika ufunguzi wa mkutano wa siku moja kwa ajili ya mikakati ya uanzishwaji wa masoko ya madini.

Washiriki wa mkutano huo walikuwa maofisa na wafanyakazi wa wizara ya madini, wakuu wa mikoa na makatibu tawala mikoa.

Akizungumza mbele ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Jafo amesema kuna mikoa inasuasua zaidi katika zoezi hilo licha ya kuwa baadhi ya mikoa imeshafikia hadi asilimia 94.

Bila kuitaja mikoa iliyofanya vizuri na ambayo inasuasua, amesema kitendo hicho hakifurahishi kwani kinarudisha nyuma juhudi za Rais Magufuli.

"Niwatangazie kuwa Jumatatu tunatakiwa Dar es Salaam na Rais kwa ajili ya maelekezo zaidi na mbinu za kufanya katika kazi hii," amesema Jafo.

Share:

WAZIRI MKUU ASHANGAZWA VIONGOZI KUCHAPANA MAKONDE OFISINI


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema tabia zinazoendelea kwa baadhi ya viongozi wa mkoani Kilimanjaro zinalitia aibu Taifa na kuwashushia hadhi wahusika.


Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Januari 26, 2019 mkoani Dodoma wakati akifungua mkutano wa siku moja kwa wakuu wa mikoa unaolenga kujadili namna bora ya upatikanaji wa masoko ya madini nchini.

Amesema taarifa alizozipata kutoka Kilimanjaro kwamba viongozi walipigana ofisini na kubainisha kuwa hilo si jambo zuri huku akishangazwa na watu hao kushindwa kufuata maelekezo ya mkuu wa mkoa.

“Hivi kuna nini Kilimanjaro, eti mkuu wa mkoa tueleze, inakuwaje hivi karibuni tunaleta mawaziri wakazungumza kwa mapana na tukadhani kumetulia lakini ghafla tena watu wanapigana ngumi, hii ni aibu, "amesema Majaliwa.

“Hatupendi kufika huko lakini msitulazimishe na mamlaka husika ziamue kuchukua hatua, si jambo jema, lazima mambo kama haya yasipewe nafasi kabisa.”

Amesema lengo la uteuzi kwa viongozi ni kutakiwa kufanya mambo ambayo kiongozi wao anayafanya ikiwemo kushirikiana na viongozi na taasisi nyingine na kukaa pamoja na kujadiliana kuhusu rasilimali za nchi.

Na  Habel Chidawali, Mwananchi 


Share:

MCHEZAJI WA SIMBA AREJEA KUELEKEA MECHI YA AL AHLY


Kuelekeza mchezo wa 3 Kundi D ligi ya Mabingwa Afrika, klabu ya Simba kupitia kwa kocha wake Patrick Aussems, amethibitisha kuwa mshambuliaji wa timu hiyo John Bocco ameshapona na anatarajiwa kuanza kucheza muda wowote.

Akitoa ufafanuzi juu ya kutolewa kwenye michuano ya SportPesa, Aussems pia aligusia suala la Bocco na kuweka wazi kuwa maendeleo yake ni mazuri.

“Kuhusu mshambuliaji John Bocco yupo vizuri, anamalizi mazoezi mepesi ya mwisho na anaweza kucheza kabisa mechi yetu ijayo dhidi ya Al Ahly'', alisema Aussems.

Bocco aliumia kwenye mechi ya kwanza ya Kundi D dhidi ya JS Sauora iliyopigwa kwenye uwanja wa taifa Dar es salaam Januari 12.

Wachezaji wa Simba ambao bado wapo majeruhi ni Erastoi Nyoni aliyeumia kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi pamoja na Shomari Kapombe aliyeumia kwenye kambi ya timu ya taifa mwaka jana.
Share:

LAKI SITA ZATAKA KUMKATISHA UHAI MWEKA HAZINA WA KIKUNDI CHA KUKOPESHANA NJOMBE

Na.Amiri kilagalila Mkazi mmoja wa mtaa wa Kihesa mjini Njombe aliyefahamika kwa jina la Maria mgeni (26) amenusurika kifo mara baada ya kujaribu kujiua kwa kunywa sumu kutokana na kushindwa kuwasilisha baadhi ya michango ya wanachama inayokaribia kiasi cha shiringi laki sita Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Rashid Ngonyani,alisema kuwa binti huyo mfanyabiashara ndogo ndogo wa mboga mboga alijaribu kujiua kwa kunywa sumu ambayo bado haijajulikana pamoja na kujichana maeneo ya kitovuni na kitu chenye ncha kali. “Mnamo tarehe 25 mwezi…

Source

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger