Thursday, 17 January 2019

CCM YAGOMA KURUDI KWENYE CHAMA KIMOJA TANZANIA


Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema wanaodhani kuwa chama hicho kinataka mabadiliko ya sheria ya vyama vya siasa ili nchi irudi kwenye mfumo wa chama kimoja wanakosea.

Akizungumza na wanachama wa CCM mkoani Dodoma leo katika mkutano wa kukusanya maoni kuhusu Muswada wa sheria ya Vyama vya siasa, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt..Bashiru Ali amesema mfumo wa vyama vingi umeiimarisha CCM.

"Sheria hii si ya kwanza kutungwa na haitakuwa sheria ya mwisho...Ukiendesha siasa kwa urasimu hutatenda haki", amesema.

Amebainisha kuwa wanatetea muswada huo kwasababu umeongeza uhakika wa utawala na kulinda misingi ya utaifa.

Aidha Dkt. Bashiru ameongeza kwamba, "Mimi natamani sana kwenye sheria hii hata koma(alama ya nukta) isiondolewe lakini mnaweza kutoa maoni yenu ya kuboresha ambayo hayaondoi maudhui", ameongeza Dkt. Bashiru.

Pakua App mpya ya Malunde 1 blog imeboreshwa zaidi ili kukidhi mahitaji ya wasomaji wetu. 

Ni rahisi sana : Ingia Play store kisha Andika Malunde 1 blog halafu bonyeza Install

Share:

MWANDISHI WA HABARI AUAWA KWA KUPIGWA RISASI

Mwandishi wa habari za upelelezi nchini Ghana amepigwa risasi hadi kufa wakati akiendesha gari kwenda nyumbani, baada ya mwanasiasa kuitisha adhabu dhidi yake.


Vyombo vya habari vya ndani vinaripoti kuwa watu wasiojulikana wakiwa katika pikipiki walimpiga risasi Ahmed Hussein-Suale mara tatu katika mji mkuu wa Accra.

Alikuwa ni miongoni mwa wahusika wa shirika binafsi la upelelezi Tiger Eye na alipepeleza rushwa katika ligi ya mpira wa miguu Ghana.


Taarifa hiyo ya uchunguzi kuhusu rushwa ilisababisha kufungiwa maisha kwa aliyekuwa kiongozi wa shirikisho la kandanda nchini Ghana.

BBC Afrikan Eye ilifanya makala kuhusu skendo hiyo mwaka 2018 baada ya kupata uchunguzi huo kwa ruhusa ya mwandishi machachari Anas Aremayaw Anas, ambaye anaiongoza Tiger Eye.

Baada ya BBC kurusha makala hiyo, mbunge wa Ghana Kennedy Agyapong alisambaza picha za mwandishi huyo Hussein-Suale na kutaka adhabu dhidi yake.

Chanzo:Bbc
Share:

HAWA JAMAA WALISHAPOTELEA WAPI

Kupitia ukurasa wake wa Facebook,Mwandishi wa habari Costantine Mathias amepost ujumbe huu

NIMEWAZA TU........
Miaka ya 2000 kurudi nyuma walikuwepo watu maarufu sana katika maeneo mengi ya usukumani, Waleta Mvua wa Asili (BAGHEMI BHA MBULA), mvua zikigoma kama sasa walikuwa wakitafutwa kwa gharama yoyote ile.

Basi kijiji kinajadili kupitia mkutano wake (Dagashida), ulioongozwa na Ntemi, Mganga anafuatwa anafanya matambiko yake, kuna wakati mvua ilinyesha kwa kuamini wamefanikiwa maombi yao, kuna wakati iligoma na kuona mganga kashindwa kazi..

Yalikuwepo pia maeneo maalumu yaliyotengwa kwa ajili ya kaudhimisha tambiko hilo la kimila ambayo yalikuwa ni visima, milima na maeneo mengine muhimu kwa kazi hiyo.

Walikuwepo wazee maalumu kwa kazi hiyo (Wanaume kwa wanawake) ambao walikuwa na mavazi yao rasmi yenye rangi ya nyeusi na nyekundu.

Siku ya matambiko walichinja ng'ombe mweusi, huko milimani/visimani, wanampika kwenye chungu bila kumwekea chumvi na kutafunwa bila ugali au wali, tena wanapakulia kwenye majani.

Mtaalamu huyo alikuwa akilipwa ujira wa Ng'ombe mmoja, pia wakati akitekeleza shuguli hizo alikuwa akitunzwa sana kwa sababu alionekana kuleta neema katika eneo hilo.

Lakini pia ilikuwepo siku maalum ya kuadhimisha siku hiyo ya matambiko kwenda kuabudu (KUHUMBA), pia kama watabaini kuna mtu (ke/me) anazuia hayo maombi yao yasifanikiwe walikuwa wakilowekwa kwenye dimbwi la maji na kuchapwa fimbo, pia kufukuzwa kijijini.

........HAWA JAMAA WALISHAPOTELEA WAPI.........
Share:

WAZIRI MAY KUWASHIRIKISHA WAPINZANI

Großbritannien Ansprache Theresa May nach Misstrauensvotum (Reuters/C. Kilcoyne)
Baada ya mpango wake wa Uingereza kujiondoa katika Umoja wa Ulaya kukataliwa bungeni na yeye pia kuponea kura ya kutokuwa na imani naye, Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May sasa anajaribu kuwashirikisha wapinzani.

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May leo anakabiliwa na mkwamo mwingine kuhusu mpango mpya wa mchakato wa Uingereza kujiondoa katika Umoja wa Ulaya - Brexit. 
Hii ni baada ya May kupata ushindi mdogo kwenye kura ya kutokuwa na imani naye, kufuatia kushindwa kwa mpango wa awali wa Brexit.

 May na waliounga mkono mpango wake, walipata kura 202 pekee huku walioupinga wakipata kura 432 bungeni.
Bibi May amewatolea wito viongozi wa upinzani kukutana naye kwa mazungumzo ya pamoja ya vyama vyote vya kisiasa, kabla ya kuwasilisha pendekezo mbadala kwa bunge la nchi hiyo siku ya Jumatatu wiki ijayo. 
Lakini wapinzani wake wamewasilisha orodha ya matakwa yao ili kuwezesha ushirikiano na May, ikiwemo kufuta uwezekano kwamba Uingereza itaweza kujiondoa katika Umoja wa Ulaya mwezi Machi bila ya makubaliano kabisa.
 
Hata hivyo bibi May amesema milango bado iko wazi kwa yeyote kushiriki.
Hayo yakijiri nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya pia zinajadiliana kuhusu namna ya kusonga mbele baada ya bunge la Uingereza kuyakataa makubaliano ya May kuhusu Brexit.
Uingereza inatarajiwa kujiondoa katika Umoja wa Ulaya ifikapo Machi 29.
Chanzo:Bbc
Share:

MATUKIO YA MAUAJI NJOMBE YANAHUSIANA NA USHIRIKINA:KAMANDA NGONYANI

Na Amiri kilagalila Jeshi la polisi mkoa wa Njombe limezungumza na waandishi wa habari Kufuatia matukio ya utekaji, kujeruhi na mauaji yaliyoibuka hivi karibuni mkoani Njombe ambapo pamoja na kuthibitisha uwepo wa matukio hayo jeshi hilo limesema yanatokana na imani za kishirikina kwa asilimia kubwa. Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo katika Ofisi za polisi makao makuu ya polisi mkoani Njombe kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Rashid Ngonyani amesema kuwa matukio hayo kwasasa yametawala zaidi katika Eneo la Njombe mjini ambapo wahanga wakubwa wa Matukio hayo…

Source

Share:

Usikubali Kupitwa na Habari : Pakua Upya App ya Malunde 1 blog ...Imeboreshwa Kukupa Raha zaidi

Kuwa wa Kwanza kupata habari na matukio yanayojiri Tanzania na dunia kwa ujumla kwa kupakua/ kudownload App ya Malunde 1 blog tukuhabarishe masaa 24.

Tembea na dunia kiganjani mwako sasa.

Pakua App mpya ya Malunde 1 blog imeboreshwa zaidi ili kukidhi mahitaji ya wasomaji wetu. Hii ndiyo mpya kabisa,ina alama hii ↡↡
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Ni rahisi sana : Ingia Play store kisha Andika Malunde 1 blog halafu bonyeza Install

https://bit.ly/2Qb7qyF

NB: App uliyokuwa unatumia mwanzo tumeifuta na kuleta mpya ya kisasa zaidi..Tafadhali fuata maelekezo hapo juu... Usikubali kukosa habari kizembe..Pakua app yetu Mpya ya Malunde1 blog Sasa

Share:

GITEGA KUWA MJI MKUU WA BURUNDI

Bunge nchini Burundi limeidhinisha mswada wa sheria ya kuhamisha mji mkuu ya serikali kutoka Bujumbura hadi Gitega.

Bujumbura itasalia kuwa mji wa kibishara wa taifa hilo dogo katika kanda ya Afrika Masharika.

Akielezea kwa kina mpango huo waziri wa mambo ya ndani Pascal Barandagie alisema lengo la hatua hii kwanza ni kuwasongezea utawala wananchi wa mikoa mbalimbali, na kutenganisha makao makuu ya kisiasa na kiuchumi kwa kuacha mji wa Bujumbura kuwa mji wa kibiashara.


Mpango huo pia unalenga, kupunguza dhana ya watu wa mikoani kwamba Bujumbura ndio sehemu tu ya kufaulu maishani na hivyo kutoa fursa kwa mji huo kupumua kutokana na msongamano wa watu.

Serikali imetilia maanani suala la usalama ikisema kwamba Gitega ni mahali salama zaidi ikizingatiwa kuwa iko katikati ya Burundi tofauti na Bujumbura ambayo iko pembezoni na karibu nampaka na nchi jirani.

Tayari serikali ya Burundi imetangaza kuwa vikao vya baraza la mawaziri vitafanyika mjini Gitega kuanzia mwezi hu wa Januari.

Wizara tano za serikali pia zinatarajiwa kuhamia mji mkuu huo mpya wa Burundi.

Baraza la seneti linaelekea kukamilisha maandalizi yake ya kuhamia mji huo uliyo na wakaazi laki tatu.

Chanzo:Bbc
Share:

KAMATI YA MAENDELEO YA KATA YATOFAUTIANA NA MAAMUZI YA DC NJOMBE

Na Amiri kilagalila Kamati ya maendeleo ya kata ya Ramadhani halmashauri ya mji wa Njombe mkoani Njombe imesema haitaweza kusitisha zoezi la wazazi kuchangia fedha kiasi cha shiringi elfu thelathini kwa ajili ya madawati kwa kuwa hakuna mzazi yeyote katika kata hiyo anayependa mtoto wake kukaa chini. Siku chache zilizopita Mkuu wa Wilaya ya Njombe Ruth Msafiri alilazimika kusitisha zoezi la kuchangia kiasi hicho cha fedha na kuagiza kushushwa vyeo afisa elimu wa kata ya Ramadhani Estar Mjululu, na Huruma Mgeyekwa pamoja na Mkuu wa Shule ya Sekondari Maheve, Valeno…

Source

Share:

KAULI YA UPANGAJI WA MATOKEO YAMTOKEA PUANI MANARA

Haji Manara.

Hivi sasa mambo yamegeuka na huenda Haji Manara anatamani maneno haya, kama ambavyo Yanga na Azam FC wanapanga matokeo, yafutike lakini teknolojia imetunza na yanatumika kama kumbukumbu ikimkumbusha kuwa mambo yamegeukia kwake wakati huu ambao Simba ina viporo 7 vya ligi kuu soka Tanzania bara.

Akiwa kwenye moja ya mikutano ya klabu na wanahabari miaka iliyopita Manara alisema, ''Kwa kawaida timu inatakiwa kucheza mechi moja na kupumzika ndani ya saa 72 lakini bodi ya ligi inatoa maelezo mengi kitu ambacho si sawa.

Aidha Manara aliweka wazi kuwa Yanga ambayo ilikuwa na viporo 9 ilikuwa inapanga matokeo kwa kutumia mfumo wa 'Indirect' kwani kuna baadhi ya timu ambazo zilikuwa zinakaribia kushuka daraja huenda zisingekuwa na ushindani wakati ambao zitacheza na Yanga.

Hata hivyo kwa upande wa pili ambao ni Yanga na Azam FC msimu huu wao wapo kimya na hawajalalamika licha ya Simba kupumzika kwa zaidi ya saa 72 lakini imekuwa haichezi mechi zake za ligi na kuendelea na maandalizi ya michuano ya kimataifa.

Chanzo:Eatv
Share:

CAG AMJIBU SPIKA NDUGAI...ASEMA ANA NIA YA KUHOJIWA

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad amesema ana nia ya kuitikia wito wa Spika Job Ndugai kwa sababu ofisi yake haiwezi kufikia ufanisi unaohitajika katika utendaji wake kama ripoti zake hazifanyiwi kazi ya kuridhisha na Bunge.

Profesa Assad ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Januari 17, 2019 katika mkutano wake na waandishi wa habari huku akibainisha kuwa neno udhaifu ni la kawaida kwa wakaguzi katika kutoa maoni ya utendaji wa mifumo ya taasisi mbalimbali.

Mkaguzi mkuu huyo wa hesabu za Serikali ametoa kauli hiyo baada ya kuibuka mzozo kati yake na Ndugai kutokana na Profesa Assad wakati akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa kusema kushindwa kutekelezwa kwa ripoti anazowasilisha bungeni huenda kunatokana na udhaifu wa chombo hicho kauli ambayo Ndugai alisema ni ya kudhalilisha Bunge na kumtaka kufika mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge Januari 21, 2019 kuhojiwa.

Amesema majibu yake yaliyozua mjadala hayakuwa na nia ya kuidhalilisha Bunge kama dhaifu bali ni lugha ya kawaida kwa wakaguzi katika kutoa maoni ya utendaji wa mfumo wa taasisi mbalimbali.

" Ni wazi kuwa watu wengine wanaweza kuchukua tafsiri tofauti ya maneno kama haya. Yametokea malumbano makali na marefu katika nyanja zote za mawasiliano kuhusu rai, nafasi na maamuzi mbalimbali yaliyochukuliwa na viongozi,” amesema Assad.

“Binafsi na ofisi ya Taifa ya ukaguzi hatuna namna ya kuathiri tafsiri za viongozi, wanasiasa na wachangiaji wa kawaida. Tunachoshauriana ni uungwana utawala katika mawasiliano.”

Na Bakari Kiango, Mwananchi
Share:

WATU 900 WAUAWA DR CONGO

Vita vya kikabila magharibi mwa Jamhuri ya Kidmeokrasi ya Congo vimesababisha vifo vya takriban watu 890 katika muda wa siku tatu mwezi uliopita, Umoja wa mataifa unasema.


Duru za kuaminika zinaeleza mapigano kati ya jamii za Banunu na Batende yalizuka katika vijiji vinne huko Yumbi, ofisi ya Umoja wa mataifa kuhusu haki za binaadamu inasema.

Idadi kubwa ya wakaazi wa eneo hilo inaarifiwa wameachwa bila ya makaazi.

Uchaguzi mkuu wa Desemba 30 uliahirishwa huko Yumbi kutokana na ghasia.

Mashambulio hayo yanaarifiwa kutokea kuanzia Desemba 16 hadi 18.

Raia walioachwa bila ya makaazi ni pamoja na watu 16,000 waliotafuta hifadhi kwa kuvuka mto Congo hadi katika nchi jirani ya Congo-Brazzaville, umeongeza.

Chanzo:Bbc
Share:

MWANAMKE AUAWA KWA KURARULIWA NA MAMBA SHAMBANI

Mnyama huyo aliwekwa pasipo kibali katika shamba kaskazini mwa Sulawesi.

Mwanamke mmoja raia wa Indonesia ameuawa na Mamba huko Sulawesi baada ya kuanguka karibu nae.

Deasy Tuwo, 44, inasemekana alikuwa akimlisha Mamba huyo kwenye shamba huko Sulawesi mahali anapofanyia kazi na sehemu ambayo mamba huyo alihifadhiwa bila kibali.


Mamba huyo mwenye kilo 700 aitwae Merry inasemekana alimng'ata mkono na sehemu kubwa ya tumbo.

Mnyama huyo amehamishiwa katika hifadhi wakati mamlaka ikimtafuta mmiliki, Tuwo alivamiwa na mamba wakati akimpatia chakula

Bi Tuwo alikuwa ni msimamizi wa maabara katika eneo hilo na alikuwa akimpatia chakula Merry tarehe 10 mwezi januari ambapo aliangukia mikononi mwamnyama huyo.

Wafanyakazi wenzie waliuona mwili wake asubuhi ya siku inayo fuata.

Chanzo:Bbc
Share:

SERIKALI YAMJIBU LISSU

Mbunge wa Singida mashariki (Chadema) Tundu Lissu.

 Msemaji wa Serikali, Dk Hassan Abbas amemjibu mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) Tundu Lissu, akidai kuwa mwakilishi huyo wa wananchi anazungumza uongo kuhusu maendeleo ya Tanzania.

Dk Abbas amesema kwamba licha ya kuulizwa mazuri ya Serikali lakini Lissu alishindwa kujibu na badala yake aliishia kubabaika.

Akihojiwa na kituo cha Utangazaji Uingereza (BBC) jana Januari 16, 2019, Lissu amezungumza masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na maoni yake kuhusu maendeleo ya nchi, utawala wa katiba na mpango wake wa kugombea urais.

"Unakwenda Ulaya unaponda nchi yako eti haifuati Katiba wakati wewe mwenyewe kuanzia ubunge wako, sifa za ubunge wako na taratibu za uchaguzi wa ubunge wako vyote vipo kwenye Katiba na ndio maana ukawa mbunge,” alisema Dk Abbas.

Dk Abbas amedai Lissu hata alipoulizwa mazuri aliyoyaona licha ya changamoto zilizopo, alishindwa kujibu vyema.

"Angalia alivyoshindwa si tu kueleza jema moja la nchi yake baada ya kupewa fursa hiyo, bali kashindwa hata kueleza jema moja alilofanya yeye binafsi jimboni kwake, kaishia kubabaika tu," amedai Dk Abbas.

Amesema Serikali ya Awamu ya Tano ina dhamira tofauti na ile waliyonayo watu wa aina ya Lissu, hivyo itaendelea kutekeleza wajibu wake katika kuwaletea Watanzania maendeleo ya kweli.

"Sisi tunapigania maendeleo na Watanzania wanaona kazi kubwa inayofanyika kote nchini iwe reli, maji, viwanda, umeme na mambo mengine. Hakuna wa kutuzuia katika kuiletea Tanzania maendeleo. Hakuna,” amesisitiza.

Chanzo:Mwananchi
Share:

WAJASILIAMALI KATA YA MWANGATA IRINGA WAUNGA MKONO JITIHADA ZA JPM WACHANGIA MILIONI 2.

NA Francis Godwin,Iringa WAJASILIAMALI wa kata ya Mwangata katika manispaa ya Iringa wamechanga jumla ya shilingi milioni 2 kwa ajili ya kumuunga mkono Rais Dkt John Magufuli kwa ajili ya uendelezaji wa sekta ya elimu nchini. Wajasiliamali hao ambao walitumia pesa hizo kununua mifuko ya saruji 130 walikabidhi msaada huo kwa naibu meya wa Manispaa ya Iringa Joseph Lyata kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi Jana. Akizungumza kwa niaba ya wajasiliamali hao Diwani wa kata ya Mwangata Edward Chengula mara baada ya kongamano la wajasiliamali alisema…

Source

Share:

BABA MZAZI WA MSANII ALI KIBA AFARIKI DUNIA.

Na Bakari Chijumba, Mtwara. Baba mzazi wa msanii wa Bongo Fleva, Alikiba Mzee Saleh amefariki dunia alfajiri ya leo Januari 17, 2019 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.. Inaelezwa kuwa, Mzee Kiba ambaye pia ni baba mzazi wa msanii Abdu Kiba na Zabibu Kiba amekua akiugua kwa muda sasa huku akiendelea kutibiwa. Msiba upo nyumbani kwa marehemu Kariakoo mtaa wa Muheza jijini Dar es salaam (unaingilia China Plaza) ambapo mipango ya mazishi inafanywa. Kwa mujibu wa Ndg wa Marehemu, ratiba ya Mazishi ni kwamba, Maiti itaswaliwa katika…

Source

Share:

SPIKA NDUGAI : ZITTO KABWE ANANIPA TABU


 Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema mbunge anayempa shida pale anapotaka kumwadhibu ni Zitto Kabwe.

Ndugai ametoa kauli yake hiyo leo Alhamisi Januari 17, 2019 katika mkutano na waandishi wa habari katika ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam.

Ndugai amesema amekuwa akichelea kumfukuza bungeni mbunge huyo wa Kigoma Mjini kwa kuwa ndiye pekee anayewakilisha Chama cha ACT-Wazalendo.

"Unajua niseme ukweli, huyu mbunge amekuwa akinipa tabu sana, ananipa tabu sababu ndio mbunge mmoja wa chama chake,” amesema Ndugai.

“Hawa wengine huwa nafukuza sababu wenzao wapo, sasa huyu (Zitto) ni mmoja tu wa chama chake (ACT Wazalendo).”

Na Kelvin Matandiko Mwananchi 
Share:

NAIBU WAZIRI WA MADINI STANSLAUS NYONGO AMEAGIZA WAMILIKI WA MGODI KUKAMATWA

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo ameamuru kukamatwa kwa Wamiliki wa mgodi wa Nyakavangala unaomilikiwa na Thomas Masuka and Partners kufuatia wamiliki hao kutofautiana juu ya taarifa waliyoiwasilisha kwa Naibu Waziri kuhusu namna mgodi huo unavyoendeshwa ikiwemo ulipaji wa kodi na mrabaha wa serikali.

Naibu waziri amewataka wamiliki hao kutoa maelezo ya kina kuhusu ni lini watalipa kodi zote wanazodaiwa na serikali baada ya kuonekana kuwa mgodi huo unadaiwa zaidi ya shilingi milioni 128 za mrabaha ambazo imedaiwa kuwa, wapo baadhi ya wamiliki ambao wamekuwa wakikusanya fedha hizo lakini zimekuwa hazilipwi.

Katika ziara yake mkoani humo, Naibu Waziri alisema kuwa pamoja na kujionea shughuli za uchimbaji katika migodi ya dhahabu ya Ulata na Nyakavangala, amebaini ukwepaji mkubwa wa kodi pamoja na mrabaha wa serikali.

Amemtaka Afisa madini kutoa maelekezo ya kina kuhusu suala zima la ulipwaji wa kodi na mrabaha wa serikali, huku akiagiza zoezi hilo pia limuhusishe Afisa Msimamizi wa madini aliyekuwepo katika kipindi ambacho fedha hizo hazikulipwa.

Hatutaki ugomvi hapa kwenye migodi. Tunataka mgodi ufanye kazi. Dhahabu ziuzwe mahali panapoonekana. Hapa naona hesabu za viroba tu. Mnunuzi wa dhahabu hapa ni nani”, alihoji Naibu Waziri Nyongo.

Wakati akizungumza na wachimbaji katika mkutano wa hadhara, amewataka wachimbaji hao kuchimba kwa kuzingatia usalama huku akisisitiza suala la kufuata sheria na taratibu huku akiwataka kutoa taarifa za uhakika kwa wale wote wanaokikuka sheria ikiwemo watoroshaji wa madini huku akisisitiza utoaji taarifa hizo usiwe wa majungu.

 Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela aliwataka wamiliki hao kukaa chini na kukubaliana namna ya kulipa kiasi cha fedha ambacho wanadaiwa na serikali huku akimtaka afisa kutoka halmashauri anayehusika na masuala ya usimamizi wa fedha kuhakikisha kwamba fedha ambazo mgodi huo ulipaswa kuzilipa kama mrabaha zinapatikana.

Mgodi huo wa Nyakavangala unamilikiwa na Thomas Masuka kwa ushirikiano na wawekezaji wengine wazawa wapatao 20. Wakati akiagiza kukamatwa kwao, wamiliki 8 kati ya 20 ndiyo walikuwa wamehudhuria kikao kati yake na wamiliki hao.

Naibu Waziri Nyongo alitoa agizo hilo Januari 15 wakat akihitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani humo.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger