MFANYABIASHARA maarufu nchini, Mohamed Dewji, maarufu kama Mo, ambaye Oktoba mwaka jana alitekwa na watu wasiojulikana na kukaa naye kwa takribani siku tisa, amepata janga lingine, baada ya serikali kuchukua mashamba yake sita.  MFANYABIASHARA maarufu nchini, Mohamed Dewji, maarufu kama Mo picha mtandao Serikali imetangaza imeyafuta mashamba sita yenye ukubwa wa hekari 12,915.126 ya kampuni ya Mohamed Enterprises, ambayo Mo ndiye mtendaji mkuu wake, yaliyopo Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga. Uamuzi wa kufuta mashamba hayo unafuatia mapendekezo yaliyotolewa na Halmashuri ya Wilaya ya Korogwe kutokana na kutoendelezwa kwa muda…
Tuesday, 15 January 2019
TOURE KUREJEA TENA UINGEREZA.
Na Shabani Rapwi, Dar es Salaam. Kiungo wa zamani wa klabu ya Manchester City, Yaya Toure, (35) amesema kuwa bado ana muda wa kuendelea kucheza soka angalau kwa miaka miwili au zaidi ndipo afikilie kustaafu kucheza soka. Toure ambaye kwa sasa hana timu baada ya klabu ya Olympiocos kusitisha mkataba wake kwa kushindwa kufanya vizuri kwenye klabu hiyo aliyodumu kwa muda wa miezi mitatu na alicheza mechi 5 alizopewa nafasi na kocha Pedro Martin. Akiongea kwenye kipindi cha Monday Nighat Football, Toure alisema “Huu sio mwisho wangu nataka kucheza tena,…
WAZIRI AAGIZA KINA MBOWE WAACHIWE
Wito umetolewa kwa Mamlaka zenye dhamana nchini kuwaachia huru Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo nchini pamoja na Mbunge wa Tarime Mjini Mh. Esther Matiko Wito huo umetolewa mapema leo na aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii nchini, Mh. Lazaro Nyalandu. Nyalandu amesema kuwa jambo la kuwaachia huru viongozi hao ambao wapo mahabusu ya Segerea jijini Dar es salaam kwa kufutiwa dhamana na Mahakama ya Kisutu, lina tija sana kwa nchi na Watanzania kwa ujumla. Novemba 23, mwaka 2018, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliwafutia dhamana Mbowe pamoja na…
WANANCHI WANGING’OMBE WAANZA UJENZI KITUO CHA AFYA, WAITAKA SERIKALI KUUNGA MKONO.
Na,Mwandishi Wetu. Wananchi wa kata ya Makoga wilayani Wanging’ombe mkoani Njombe wameanza ujenzi wa baadhi ya majengo ya kituo cha afya cha makoga lengo likiwa ni kutatua baadhi ya changamoto zinazokikumba kituo hicho kilichopo katika kata hiyo ili kunusuru upatikanaji wa huduma za afya kituoni hapo. Hatua hiyo inakuja kufuatia kituo cha afya makoga kukumbwa na changamoto nyingi ikiwemo upungufu wa wahudumu pamoja na ukosefu wa gari ya wagonjwa katika kituo cha afya kilichopo huku jengo lililopo likiwa limechoka. “Yaani huwa tunatafuta tu Magari kwa gharama ambazo sisi niwakulima hatuna…
ZAIDI YA MILLIONI 902 KUNUNUA MAGARI,PIKIPIKI KUONGEZA NGUVU KWA WASIMAMIZI WA AFYA NCHINI.
Serikali imetoa Takribani million 902 na LAKI TISA kwa ajili ya kununua magari 10 na pikipiki 35 ili kuongeza nguvu kwa waratibu na wasimamizi wa huduma ya afya kuweza kuwafikia watoa huduma katika mikoa yao kudhibiti magonjwa ya kifua kikuu na ukoma. Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Ummy Mwalimu alieleza hayo jijini Dar es salaam ambapo alisema serikali imejikita katika kuzuia na kudhibiti ugonjwa wa kifua kikuu na ukoma ili kuweza kuwagundua wagonjwa na kuwapatia huduma ya matibabu. Waziri Ummy alisema lengo la serikali…
BOT YAHAMISHA MADENI NA MALI ZA BANK M KWENDA AZANIA BANK….NI BAADA YA KUSHINDWA KUJIENDESHA.
Na.Mwandishi Wetu Benki kuu ya Tanzania (BOT) imehamisha madeni na mali zote za Bank M kwenda Azania Bank kutokana na Benki hiyo kushindwa kujiendesha. Uamuzi wa kuunganishwa kwa benki hizo ulifikiwa Januari 2, 2019 hii ikiwa ni baada ya kuiweka Benki M chini ya uangalizi tangu Agosti 2,2018. Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Januari 15, 2019 Naibu Gavana wa BOT, Dk Benard Kibese amesema licha ya kufanyika kwa mikutano mingi kati ya wamiliki, bodi na uongozi ndani ya siku 90 zilizotolewa awali lakini hazikuzaa matunda. “Benki inapoonekana kutetereka…
KORTINI KWA KUBAKA NA KUMPA MIMBA MWANAFUNZI MWINGINE ACHOMA MOTO NYUMBA
Na,Naomi Milton Serengeti Thomas Mokiri(25) mkazi wa kijiji cha Issenye wilayani hapa amefikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayomkabili ikiwemo kumpa mimba mwanafunzi wa kidato cha tatu mwenye umri wa miaka(17). Akisoma mashtaka mbele ya Hakimu mkazi mfawidhi wa wilaya Ismael Ngaile mwendesha mashtaka wa Jamhuri Faru Mayengela alisema katika shauri la Jinai namba 6/2019 mshitakiwa anakabiliwa na makosa mawili kosa la kwanza ni Kubaka kinyume na kifungu 130(1)(2)(e)na kifungu 131(1) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002. Kosa la pili ni kumpa mimba mwanafunzi kinyume na…
GCLA KANDA YA KASKAZINI YAJIPANGA KUANZISHA MAABARA YA VINASABA VYA WANYAMA.
NA WAMJW, ARUSHA Mamlaka ya maabara ya mkemia mkuu wa serikali,kanda ya kaskazini – Arusha, ipo mbioni kuanzisha Maabara maalum ya vinasaba vya wanyama ambayo itasaidia kutambua asili ya mnyama ikiwemo wanyama waliopo ama waliokufa. Akizungumza wakati wa ziara maalum ya maafisa uhusiano waliotembelea Kanda hiyo leo, meneja kanda ya kaskazini Christopher Anyango abainisha kuwa kwa sasa wapo katika ukarabati wa jengo ambalo Maabara hiyo itakuwepo. Awali ujenzi wa jengo hilo ulisimama baada ya ufadhili wake kukoma na hivyo kuilazimu mamlaka kufanya ukarabati ili kujipatia sehemu ya kufanyia kazi. “Maabara…
RAIS MAGUFULI ASITISHA MARA MOJA ZOEZI LA KUONDOA VIJIJI NA VITONGOZI MAENEO YA HIFADHI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza kusitishwa mara moja kwa zoezi la kuviondoa vijiji na vitongoji vinavyodaiwa kuwepo katika maeneo ya hifadhi na amewataka viongozi wa wizara zote zinazohusika kukutana ili kubainisha na kuanza mchakato wa kurasimisha maeneo ya vijiji na vitongoji hivyo.
Mhe. Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo tarehe 15 Januari, 2019 Ikulu Jijini Dar es Salaam alipokutana na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamis Kigwangallah, Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi John Kijazi, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhandisi Joseph Nyamhanga na Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Bi. Dorothy Mwanyika.
Pamoja na agizo hilo Mhe. Rais Magufuli ametaka viongozi wa wizara husika kubainisha maeneo ya hifadhi za wanyamapori na misitu ambayo hayana wanyamapori ama misitu ili yagawiwe kwa wafugaji na wakulima ambao kwa sasa wanataabika kupata maeneo ya kufugia wanyama na kuzalisha mazao.
Mhe. Rais Magufuli pia ameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kuangalia upya zoezi la uwekaji wa mipaka ya hifadhi na makazi, na kutumia busara katika uwekaji wa mawe ya mipaka hiyo ili kutowaondoa wananchi katika maeneo ambayo hayana ulazima wa kuwaondoa.
“Mimi sifurahii kuona wafugaji kila mahali wanafukuzwa, kama kuna eneo ambalo tunafikiri lilikuwa hifadhi ya wanyama lakini halitumiki, tutabadilisha sheria, tunalimega na tunaligawa kwa wafugaji, vivyo hivyo hata kwa wakulima kama kuna eneo tunaona ni hifadhi lakini halina msitu wala wanyamapori, na lina rutuba, na wakulima wanataka kulima nalo tunalimega tunawapa wakulima.
Baadaye tutajua kabisa eneo hili ni la hifadhi, hili ni la mifugo, hili ni la wakulima, hili ni la makazi. Kwa hiyo nyinyi Mawaziri na Makatibu Wakuu mkakae mkatangulize maslahi ya hawa tunaowaongoza ambao ni wakulima, wafugaji, wavuvi nakadhalika, lakini pia tunahitaji wanyamapori, sijasema sasa hifadhi zote za wanyama tunazimaliza, hapana, hifadhi za wanyama lazima tuzihifadhi” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.
Mhe. Rais Magufuli ameagiza vijiji vyote 366 vilivyoainishwa kuwepo ndani ya maeneo ya hifadhi hapa nchini visiondolewe katika maeneo hayo na badala yake ametoa mwezi mmoja kwa viongozi wa wizara zote zinazohusika kubainisha maeneo ya vijiji hivyo na kuanzisha mchakato wa mabadiliko ya sheria ili yawasilishwe katika kikao kijacho cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Amefafanua kuwa ni lazima Serikali ifanye maamuzi haya sasa kwa kuwa idadi ya Watanzania imeongezeka hadi kufikia Milioni 55, idadi ya mifugo imeongeza hadi kufikia Milioni 35 na hivyo kuna ongezeko kubwa la mahitaji ya maeneo ya ardhi ikilinganishwa na wakati nchi inapata uhuru ambapo Watanzania walikuwa Milioni 9 na mifugo ilikuwa Milioni 10.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli ameagiza sheria ya vyanzo vya maji pia iangaliwe upya ili kutowazuia Watanzania wanaozalisha mazao kandokando mwa mito na ameelezea kutofurahishwa kwake na vitendo vya kufyeka mazao ya wakulima kwa madai kuwa wamelima ndani ya mita 60.
Halikadhalika Mhe. Rais Magufuli ameipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kuwasilisha kwake mapendekezo ya kufutwa kwa mashamba ambayo hayajaendelezwa na ameagiza wizara hiyo iendelee kumpelekea mapendekezo ya mashamba yote yaliyotelekezwa ili ayafute na wananchi wagawiwe kwa ajili ya kuyatumia kwa uzalishaji wa mazao na mifugo.
Hata hivyo Mhe. Rais Magufuli amesema maagizo hayo hayana maana kuwa sasa wananchi waruhusiwe kuvamia maeneo ya hifadhi, na ametaka zoezi la uwekaji wa mipaka lifanyike haraka na kwa uwazi.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
15 Januari, 2019
MBOWE ANYANG'ANYWA OFISI NA KUPEWA UHAMIAJI
Mwenyekiti wa (CHADEMA) taifa, Freeman Mbowe.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) taifa, Freeman Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai, amenyang'anywa Ofisi yake ya Ubunge na Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na kuagiza itumiwe na Idara ya Uhamiaji.
Ole Sabaya amefikia uamuzi huo kwa kile alichodai kuwa ameelezwa kuwa Mbowe hajaitumia ofisi hiyo tangu mwaka 2010, hivyo haina haja kuendelea kuwepo na kutotumika katika matumizi yaliyo kusudiwa.
"Tangu Mbowe achaguliwe Mwaka 2010 hajawahi kuingia katika Ofisi hiyo kusikiliza kero za wananchi, sijui yupo wapi namsikia huko maeneo mengine akifanya vurugu, sasa ofisi hii itatumika kusaidia wananchi", amesema Ole Sabaya.
Mbowe amenyang'anywa ofisi hiyo akiwa gerezani baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwafutia dhamana Novemba 23, 2018 kwa kukiuka masharti ya dhamana ikiwemo kutoka nje ya nchi bila kibali, yeye pamoja na Mbunge wa Tarime Mjini Ester Matiko.
Mbowe na Matiko wako mahabusu baada ya kufutiwa dhamana kwenye kesi yao ya msingi inayowakabili juu ya kusababisha kifo cha aliyekuwa mwanafunzi wa NIT, Akwilina Akwilini baada ya kufanya maandamano kuelekea katika ofisi za Mkurugenzi wa Kinondoni Februari 2018.
Chanzo:Eatv
MANJI KUSUBIRIWA LEO OFISINI JANGWANI
Makao Makuu ya klabu ya Yanga.
Taarifa hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini la klabu hiyo ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika, Novemba mwaka uliopita kufuatia sintofahamu juu ya uchaguzi mkuu wa klabu hiyo.
Mkuchika alisema kuwa, Manji aliliambia baraza hilo la wadhamini wa Yanga kuwa tarehe ya leo ndipo ataanza kwenda ofisini kwake Yanga, alipokuwa akijibu barua ambayo aliandikiwa na Baraza hilo.
Ikumbukwe kuwa mchakato wa uchaguzi wa klabu hiyo umesimamishwa na Mahakama kufuatia baadhi ya wanachama kushtaki juu ya mwenendo mzima wa uchaguzi huo ambao ulitakiwa kufanyika wikiendi iliyopita.
Mashabiki na wanachama wa Yanga, wanasubiri endapo Mwenyekiti wao wa zamani, Yusuph Manji atarejea katika nafasi yake hii leo ama la!.
Chanzo:Eatv
MAPYA YAIBUKA KISA CHA MTOTO ALIYEFUNGIWA KABATINI
Neema Matimbe (15) akiwa na mwanaye.
Uongozi wa hospitali ya Mkoa wa Dodoma umesema kuwa tayari wamemruhusu, Neema Matimbe (15) ambaye inadaiwa mwanaye wa miezi mitano alifungiwa kabatini na mwajiri wake tangu alipozaliwa, lakini hajapata mtu wa kumchukua hivyo atakaa hospitali wakati uongozi ukiwasiliana na
Idara ya Ustawi wa Jamii ili waishi nae kwa sasa.
Imebainika kuwa mama mzazi wa Neema (15) naye ni mfanyakazi wa ndani kama alivyo mwanaye, hivyo kutokana na sababu hiyo, hospitali hiyo imesema ni vigumu kumruhusu binti huyo kwa sababu ya usalama wake.
Akizungumza na www.eatv.tv leo Januari 15, mganga mfawidhi wa hospitali hiyo, Ernest Ibenzi amesema mama wa binti huyo yupo lakini naye anafanya kazi za ndani jijini Dodoma, jambo ambalo ni ngumu kwa binti huyo kuruhusiwa kuishi naye.
Mwalimu Anitha Kimako anayedaiwa kuwa mwajiri wa binti huyo ambaye anatuhumiwa kumpiga na kumshinikiza kumuweka mwanaye kabatini tangu alipozaliwa, alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Dodoma Januari 7 na kusomewa shtaka la kushambulia mwili ambalo alilikana na kesi hiyo kuahirishwa hadi Februari 7.
Wakati hayo yakiendelea, kijana anayedaiwa kumpa ujauzito binti huyo na kumkataa, Salum Waziri atafikishwa mahakamani muda wowote kujibu mashtaka ya kumpa mimba mtoto aliye chini ya umri wa miaka 18.
Chanzo:Eatv
B.O.T YAIFUNGA BENKI NYINGINE
Naibu Gavana Dk. Bernad Kibese.
Benki Kuu ya Tanzania BOT imehamishia mali na madeni yote ya Bank M kwenda Azania Bank baada ya benki hiyo kushindwa kuwahudumia wateja wake pamoja na kulipa madeni yao.
Akitangaza taarifa hiyo asubuhi ya leo Januri 14, Naibu Gavana Dk. Bernad Kibese amesema kwamba baada ya kutafuta njia mbalimbali za ufumbuzi wa matatizo ya Benk M, muafaka uliopatikana ni kuhamisha mali zote kwenda Benki ya Azania Bank Limited kwa mujibu wa sheria.
Aidha Dk. Kibese ameeleza kwamba wateja wenye mikopo wametakiwa kuendelea kulipa mikopo yao kulingana na mikataba yao huku benki kuu ikiahidi kufuatilia suala hili kwa ukarubu zaidi.
Aidha Dk Kibese amewatoa wasiwasi wateja wanaohamishiwa Azania Bank, kwamba Benki hiyo inatarajia kuwa na mtaji wa shilingi bilioni 164, ambayo ni kiwango cha juu cha mtaji unatakiwa kuendesha shughuli za kibenki ambayo ni zaidi ya shilingi bilioni 15 hivyo itaweza kuhudumia wateja wake wa zamani na wapya.
Benki kuu itaendelea kulinda maslahi ya wateja wa huduma za kibenki na kuimarisha uhimilivu wa sekta ya fedha nchini.
Chanzo:Eatv
NECTA YATOA UFAFANUZI KUHUSU MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2018
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Charles Msonde amesema bado hawajatangaza matokeo ya kidato cha nne na kuwataka Wananchi kuachana na taarifa feki zilizosambazwa katika mitandao.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Charles Msonde amesema bado hawajatangaza matokeo ya kidato cha nne na kuwataka Wananchi kuachana na taarifa feki zilizosambazwa katika mitandao.
Akizungimza na Nipashe Msonde alisema kuna baadhi ya watu ambao sio waaminifu na kazi yao ni kutengeneza taharuki kwa wananchi pasipo na sababu za msingi.
"Bado hatujatangaza matokeo na muda ukifika tutawatangazia kama ilivyo kwa miaka mingine na wananchi mtapata taarifa naomba muachene na taarifa feki katika mitandao," alisema Dk Msonde.
Via Nipashe
MALUNDE1 BLOG ITAKUTUMIA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE MARA TU YATAKAPOTANGAZWA...
Tembelea Mara kwa mara Mtandao huu...Lakini kama wewe ni mjanja pakua App Yetu ...Ingia Play store kisha Andika Malunde 1 blog halafu bonyeza Install
Tembelea Mara kwa mara Mtandao huu...Lakini kama wewe ni mjanja pakua App Yetu ...Ingia Play store kisha Andika Malunde 1 blog halafu bonyeza Install
KINA MAMA NA WATOTO WAJITOLEA KUIMARISHA ULINZI MITAANI
Wanawake wanaoishi maeneo ya mabanda nchini Kenya wamejitolea kukabiliana na ukosefu wa usalama katika maeneo yao, jukumu ambalo kwa muda mrefu liliachiwa wanaume.
Wanawake wanaoishi maeneo ya mabanda nchini Kenya wamejitolea kukabiliana na ukosefu wa usalama katika maeneo yao, jukumu ambalo kwa muda mrefu liliachiwa wanaume.
Kupitia mpango walioupa jina ‘wamama na usalama' wanawake hao wanasema wanatambua jukumu lao kubwa la kuielekeza jamii ndiposa wanataka kuwa mstari wa mbele katika harakati za kukabiliana na ukosefu wa usalama.
Maeneo ya mabanda yanasifika kwa kila aina ya uhalifu hali inayochangiwa na wingi wa watu, umasikini na kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira.
Kina mama na watoto huathirika zaidi kutokana na visa vya uhalifu katika maeneo hayo huku vijana wakilaumiwa zaidi kwa kusababisha uhalifu.
Chanzo:Dw
MAHAKAMA YA KATIBA IMEANZA KUSIKILIZA RUFAA YA KUPINGA MATOKEO NCHINI DRC
Mahakama ya Katiba katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo leo inaanza kusikiliza rufaa ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais wa Desemba 30.
Mahakama ya Katiba katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo leo inaanza kusikiliza ombi la kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais yaliyompa ushindi kiongozi wa upinzani, Felix Tshisekedi.
Ombi hilo limewasilishwa na mgombea mwengine wa upinzani, Martin Fayulu, aliyetangazwa kushika nafasi ya pili kwenye uchaguzi wa Desemba 30 ulioitishwa kumrithi Joseph Kabila.
Fayulu ameyaita matokeo hayo yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi, CENI, kuwa ni mapinduzi ya uchaguzi. Tshisekedi alitangazwa kupata asimilia 38.57 ya kura dhidi ya asilimia 34.8 za Fayulu.
Kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzio, CENI, mgombea aliyekuwa akiungwa mkono na Kabila alishika nafasi ya tatu akiwa na asilimia 23.8.
Hata hivyo, akitegemea matokeo yanayosemekana kukusanywa na mawakala wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki, CENCO, Fayulu anasema ni yeye aliyechaguliwa kwa zaidi ya asilimia 60 ya kura. Mahakama ya Katiba ina wiki moja ya kuamua juu ya madai ya Fayulu.
Chanzo:Dw
MBIVU NA MBICHI KUJULIKANA LEO.. UINGEREZA KUJITOA UMOJA WA ULAYA AMA LA
Wabunge Uingereza wanajitayarisha kupiga kura kwa iwapo kuunga au kutounga mkono mpango wa Theresa May wa kujitoa katika Umoja wa Ulaya.
Kura hiyo inayotajwa kuwa Kura yenye umuhimu itafanyika baadaye leo wakati mjadala wa siku tano kuhusu Brexit ukikamilika.
Bi May amewataka wanasiasa kuunga mkono mpango wake au kuhatarisha kuwavunja moyo raia wa Uingereza.
Lakini huku wabunge wake mwenyewe wakitarajiwa kujiunga na wa vyama vya upinzani kupiga kura dhidi ya mpango huo, inatarajiwa pakubwa kwamba mpango huo hautofaulu.
Wabunge pia watapata fursa ya kutoa mapendekezo ya marekebisho ambayo yanaweza kuunda upya mpango huo kabla ya kura kuanza 19:00 kwa saa ya GMT.
Chanzo:Bbc