Sunday, 13 January 2019
WABUNGE WATANO KUTINGA MAHAKAMANI SAKATA LA CAG
Wabunge watano wanatarajia kufungua kesi ya kikatiba kuiomba Mahakama Kuu ya Tanzania kutoa tafsiri ya kisheria juu ya mipaka ya kinga ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na mamlaka ya Spika wa Bunge.
Wabunge hao ni Zitto Kabwe (Kigoma Mjini), Salome Makamba (Viti Maalumu), Hamidu Bobali (Mchinga), Saed Kubenea (Ubungo) na Anthony Komu (Moshi Vijijini).
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Zitto amesema wamemuagiza Wakili wao Fatma Karume kuisajili kesi hiyo chini ya hati ya dharura.
"Tutaenda Mahakamani ili kupata tafsiri ya kisheria kuhusu ni wakati gani Spika anatakiwa kumuita mwananchi yoyote kwenda kwenye kamati ya Kinga, Maadili na Madaraka ya Bunge, je atahitaji Azimio la Bunge au yeye tu binafsi na tafsiri hiyo irekodiwe.
"Kama Spika anaweza kumuita mtu mwenye kinga ya kikatiba kwa 'style' ile vipi mwananchi wa kawaida? Tumeomba tafsiri hiyo ili kulinda uhuru wa maoni, Mahakama ikisema yuko sawa sisi tutaheshimu maamuzi lakini akisema hayuko sawa nawaomba nao wakubali" Amesema Zitto na kuongeza;
"Katibu Mkuu wa mabunge ya Jumuiya ya Madola (CPA) ameniandikia kuwa tayari ameshasilisha suala langu kwa Mwenyekiti wa CPA pia amewasiliana na Spika wa Bunge la Cameroon ili ashauriane na Spika wetu kushughulikia suala la CAG bila ya kuvunja katiba"
Hivi karibuni, Spika wa Bunge, Job Ndugai, alimuagiza CAG, Profesa Mussa Assad kuripoti kwenye Kamati ya Kinga na Maadili ya Bunge, kuhojiwa kwa madai ya kulidhalilisha Bunge.
RATIBA YA LIGI KUU BARA YAPANGULIWA

Ratiba ya ligi kuu soka Tanzania bara, imepanguliwa kwa mchezo mmoja kusogezwa mbele.
Mchezo huo ni namba 220 ambao ulikuwa unazikutanisha timu za KMC ya Kinondoni dhidi ya Coastal Union ya Tanga.
Awali ulipangwa kuchezwa Jumatano Januari 16, 2019 lakini sasa utapigwa Alhamis Januari 16, 2019 kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
Ligi kuu hiyo ipo kwenye raundi ya pili mechi za 20 kwa baadhi ya timu huku Simba ndio ikiwa timu yenye viporo vingi zaidi ambapo imecheza mechi 14 pekee.
Msimamo unaongozwa na Yanga wenye alama 50 katika mechi 18 huku Tanzania Prison ikiwa na alama 12 katika nafasi ya 20 ikiwa imecheza mechi 19.
AZAM FC MABINGWA KOMBE LA MAPINDUZI...WAMECHINJA MNYAMA SIMBA 2 -1
Azam FC wameichapa Simba SC 2-1 katika mechi kali ya fainali ya kombe la Mapinduzi ndani ya Uwanja wa Gombani uliopo Pemba, Zanzibar jioni hii.
Goli la kutangulia la Azam limefungwa kwa mkwaju mkali wa Mudathir Yahya dakika ya 44.
Simba wamesawazisha kupitia kichwa cha Yusuph Mlipili akimalizia kona ya Shiza Kichuya dakika ya 63.
Obrey Chirwa akaifungia Azam FC bao la pili akimalizia kwa kichwa krosi ya Nickolas Wadada dakika ya 72.
Kwa matokeo haya Azam FC ndiyo bingwa mpya wa kombe la Mapinduzi kwa mwaka 2019.


Kikosi cha Azam Fc kilichoua Simba SC
1-Razak Abalora
2-Nickolas Wadada
3-Bruce Kangwa
4-Agrey Moris
5-Yakubu Mohamed
6-Stephan Kingue Mpondo
7-Salum Abubakar Sure Boy
8-Mudathir Yahya
9-Obrey Chirwa
10-Tafadzwa Kutinyu
11-Enock Agyei Atta
SUBs
-Mwadini Ally
-Hassan Mwasapili
-Lusajo Mwaikenda
-Salimin Hoza
-Ramadhani Singano
-Daniel Lyanga
-Donald Ngoma
SPIKA WA BUNGE KUSHITAKIWA
Zitto Kabwe na wabunge wengine wanne wanatarajia kufungua kesi ya kikatiba Mahakama Kuu ili kupata tafsiri ya kisheria, juu ya mipaka ya kinga ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na mamlaka ya Spika kumshtaki mwananchi bila kuathiri uhuru wa maoni ya kikatiba. Zitto kabwe mbunge wa kigoma mjini act-wazalendo, picha mtandao Zitto Kabwe na wabunge wengine wanne wanatarajia kufungua kesi ya kikatiba Mahakama Kuu ili kupata tafsiri ya kisheria, juu ya mipaka ya kinga ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na mamlaka…
MILIONI 433.46 KULIPA WAKANDARASI WA MIRADI YA MAJI NGARA
Na Mwandishi wetu, Ngara. Naibu waziri wa maji,Juma Aweso ameahidi wizara yake kuwalipa wakandarasi wa miradi ya maji inayofadhiliwa na benki ya dunia katika wilaya ya Ngara mkoani Kagera kiasi cha Sh433.46 milioni baada ya kucheleweshewa fedha hizo kutoka serikalini tangu mwaka 2014. Naibu waziri huyo pia amepongeza uongozi wa wilaya hiyo kwa kusimamia miradi ya maji katika vijiji inayofadhiliwa na benki ya dunia na kwamba halmashauri hiyo imedhibiti matumizi mabaya ya fedha za serikali zinazoelekezwa kwa wananchi kupata maji safi na salama. Aweso ametoa pongezi hizo Januari 13, 2019…
WABUNGE WATANO WATAKAO FUNGUA KESI KUITAKA MAHAKAMA ITAFSIRI MIPAKA YA CAG NA SPIKA WABAINIKA
Wabunge watano wanatarajia kufungua kesi ya kikatiba kuiomba Mahakama Kuu ya Tanzania kutoa tafsiri ya kisheria juu ya mipaka ya kinga ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na mamlaka ya Spika wa Bunge. Wabunge hao ni Zitto Kabwe (Kigoma Mjini), Salome Makamba (Viti Maalumu), Hamidu Bobali (Mchinga), Saed Kubenea (Ubungo) na Anthony Komu (Moshi Vijijini). Akizungumza na waandishi wa habari leo, Zitto amesema wamemuagiza Wakili wao Fatma Karume kuisajili kesi hiyo chini ya hati ya dharura. “Tutaenda Mahakamani ili kupata tafsiri ya kisheria kuhusu ni wakati…
KOCHA JS SOURA AWATUPIA LAWAMA KINA ‘SHAFII DAUDA’ KIPIGO CHA GOLI TATU
Ligi ya mabingwa Afrika (CAFCL) hatua ya makundi (16 bora) imeanza rasmi siku ya Jumamosi tarehe 12-01-2019 ambapo vilabu mbalimbali vilijitupa katika viwanja tofauti kutafuta pointi 3 muhimu.Wawakilishi pekee ukanda wa Afrika Mashariki Simba sports Club (SSC) wao walikuwa na kibarua kigumu katika ardhi ya nyumbani walipowakaribisha waarabu klabu ya JS SOURA anayoitumikia pia mtanzania Thomas Ulimwengu katika uwanja wa Taifa(kwa mchina) Mechi hiyo iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na wapenzi wa soka nchini nan chi jirani ulimalizika kwa matokeo ya kufurahisha na kutia moyo kwa Wekundu wa msimbazi Simba kuibuka…
SHAFII DAUDA,YANGA SC WAUNDA KAMATI NZITO,KUIPA SIMBA UBINGWA WA AFRIKA
Ligi ya mabingwa Afrika rasmi ilianza jana kwa michezo mbalimbali ambpo kundi D linaloundwa na Vilabu vya Al Ahly ya Misri,Simba SC ya Tanzania,AS Victor ya DRC na JS Soura ya Algeria vilitupa karata zao za kwanza na kushuhudiwa wenyeji (Simba sc na Al Ahly) kwa mechi za mzunguko wa kwanza zikishinda michezo yao,Hapa Tanzania mnyama Simba aliibugi JS Soura mabao 3-0 na kule Misri Al Ahly wakiibuka na ushindi wa goli 2-0 hivyo kufanya kundi hilo kuongozwa na Simba mpaka sasa kwa pointi tatu na magoli matatu Kikosi cha…
WAZEE 25499 KUTIBIWA BURE MAGU
Na Shushu Joel Halmashauri ya wilaya ya Magu mkoani Mwanza imefanikiwa kuwakabidhi wazee 25499 vitambulisho kwa ajili ya kupata matibabu bure. Akikabidhi vitambulisho hivyo kwa wazee hao mkuu wa wilaya hiyo Dr Philemon Sengati alisema kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya Raisi Magufuli imejipanga kuhakikisha wazee wote nchini wanapata matibabu bila malipo kama walivyoahidiwa mwaka 2015 wakati wa kampeni. Aidha aliongeza kuwa mbali na kuwakabidhi vitambulisho wazee hao, pia limetengwa dirisha maalum kwa ajili ya utoaji wa huduma kwa wazee ili kurahisisha kufikia huduma bila kupanga foreni kutokana…
CHANGAMOTO YA MIUNDOMBINU YA ELIMU YAPUNGUZWA USHETU
Na Maiko Luoga Ili kupambana na changamoto zinazoikabili sekta ya elimu katika maeneo mbalimbali nchini hatimae Mh Elias Kwandikwa Mbunge wa Ushetu na Naibu waziri wa ujenzi amefanya ziara ya kikazi katika kata ya Igwamanoni Jimboni kwake ili kuona changamoto mbalimbali zinazoikabili secta ya Elimu Sekondari na msingi na kuzitafutia ufumbuzi. Katika ziara hiyo Mh Mbunge alipata fursa ya kukagua shule ya sekondari Igwamanoni, shule ya msingi Luhaga na Shule ya msingi Iramba ambapo alibaini upungufu wa madarasa ya Shule ya sekondari Igwamanoni hali iliyomlazimu Mh Kwandikwa kutoa pesa kiasi…
NAIBU WAZIRI MAJI AWASHUKIA WANANCHI WANAOHUJUMU MIRADI YA MAJI
Na Allawi Kaboyo-Kagera. Naibu waziri wa maji Juma Aweso akiwa mkoani Kagera ametangaza kiama kwa wananchi wanaojihusisha na hujuma za miundombinu ya maji na kupelekea wanachi kukosa huduma ya maji Aweso ametoa tamko hilo alipokuwa akiendelea na ziara yake katika wilaya ya Ngara ambapo imesemekena miradi mingi ya maji inahujumiwa na wananchi wachache wasioitakia mema nchi yao na kuahidi kuwashugulikia bila kujali wala kuangalia nafasi zao. “Haiwezekani serikali tutoe pesa nyingi ili kutekeleza miradi hii alafu watokee majangili wachache waanze kuhujumu jitihada hizi, hatutakubali tutawashugulikia hatakama wanamapembe makubwa kiasi gani…
WACHEZAJI AZAM,SIMBA WAPAA KWA NDEGE MAALUMU KUKIPIGA FAINALI PEMBA

Kamati ya maandalizi ya michuano ya Mapinduzi mwaka 2019, inayofikia tamati leo, imeeleza kuwa timu za Azam FC na Simba zimesafiri leo kwa ndege kutoka Unguja kwenda Pemba tayari kwa mchezo wa fainali.
Kamati hiyo kupitia kwa Mwenyekiti wake imeeleza kuwa timu hizo ambazo zimecheza mechi za makundi na nusu fainali katika visiwa vya Unguja imebidi zisafiri kwa ndege ya kukodi ili kwenda kumaliza fainali leo.
''Maandalizi yote kwaajili ya mchezo wa fainali yamekamilika na timu zimesafiri kwa ndege leo, hivyo mchezo utafanyika muda uliopangwa kwenye uwanja wa Gombani ambao una ubora wa kutosha'', amesema.
Azam FC inacheza fainali yake ya tatu mfululizo huku ikiwa tayari imeshachukua ubingwa huo katika fainali zote mbili zilizopita ikiwemo ile ya mwaka jana (2018) ambayo waliwafunga Simba.
Kwa upande wa Simba wachezaji Haruna Niyonzima, Shiza Kichuya na Rashid Juma tayari wamewasili visiwani Pemba kuongeza nguvu kwenye kikosi cha Simba ambacho kina wachezaji wengi wa kikosi B.
DOGO JANJA AMPIGA CHINI UWOYA...HUYU HAPA MPENZI WAKE MPYA

Dogo Janja akiwa na mwanamke anayedaiwa kuwa mpenzi wake mpya
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Abdulaziz Chende maarufu 'Dogo Janja' ameonekana akiwa kwenye mapozi yenye utata na mwanamke ambaye anadaiwa kuwa ndiye mrithi wa Irene Uwoya.
Picha pamoja na video zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii zikimuonyesha Janjaro akiwa na mwanamke asiyefahamika jina na wengi kudai kuwa Irene Uwoya amepinduliwa kwa Dogo Janja, ikiwa mpaka sasa wawili hao hawajaweka wazi kuachana.
Uwoya na Dogo Janja walianza kurushiana maneno ya mafumbo katika mtandao wa Instagram Januari 07, hali ambayo ilitafsiriwa kuwa ni wazi kuwa ndoa yao itakuwa imevunjika.
Baada ya sakata hilo, baba mlezi wa Dogo Janja, Madee Ali 'Seneda' ameingilia kati suala hilo na kuwaonya kutorushiana maneno mitandaoni.
TFDA YAJIVUNIA KUIPAISHA TANZANIA KWA KUWA NA MIFUMO BORA YA UDHIBITI WA BIDHAA
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imesema katika kipindi Cha Miaka mitatu imeweza kufanya mambo mbalimbali ya udhibiti wa usalama, ubora na usalama wa bidhaa za ndani na nje ya Nchi ikiwemo kutambulika kimataifa kwa kuzingatia viwango vya Kimataifa vya ISO 9001: 2015.
Hii ni kutokana na mafanikio ya miaka mitatu ya utekelezaji wa kazi chini ya Serikali ya Awamu ya Tano, kwa kufikia na kuvuka malengo iliyojiwekea katika udhibiti wa ubora, usalama na ufanisi wa chakula, dawa, vipodozi, vifaa tiba na vitendanishi ili kulinda afya ya jamii nchini.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Bw. Adam Fimbo amebainisha hayo wakati akitoa ripoti ya miaka mitatu ya Mamlaka hiyo wakati wa ziara maalum ya Maafisa Mawasiliano na habari wa Wizara ya Afya na taasisi zake katika kampeni maalum ya ‘Tumeboresha Sekta ya Afya’ inayolenga kueleza mafanikio makubwa yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli.
“Kutokana na kuwa na mifumo thabiti ya udhibiti wa ubora, usalama na ufanisi wa dawa, mnamo Mwezi Desemba 2018, TFDA imetambulika kufikia ngazi ya tatu (Maturity Level 3) ya Shirika la Afya Duniani (WHO) ya ubora wa mfumo wa udhibiti wa dawa, vifaa tiba na vipodozi, ambapo hatua hii imeifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kufikia hatua hii
Fimbo ameeleza kuwa, TFDA katika mikakati yake hiyo imeweka mifumo na taratibu za ndani za utoaji huduma na utendaji bora ili kukidhi mahitaji na matarajio ya wateja kwa kuzingatia viwango vya kimataifa vya ISO 9001:2015 kwa huduma za kawaida na ISO 17025:2005 kwa huduma za maabara.
Aidha, ameongeza kuwa huduma za TFDA hutolewa kwa kuzingatia viwango vya Mkataba wa Huduma Wateja kama ulivyorejewa mwaka 2016.
“Mfumo wa usajili wa bidhaa umeendelea kuimarika mwaka hadi mwaka ambapo idadi ya bidhaa za chakula, dawa, vipodozi, vifaa tiba na vitendanishi vilizosajiliwa imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka, katika kipindi cha 2015/16 hadi 2017/18.
Pia tumesajili jumla ya bidhaa 14,345 kutoka bidhaa 8,866 zilizokuwa zimesajiliwa mwaka 2015/16 ambapo ni sawa na ongezeko la 62%. Hii imetokana na kuongezeka kwa uelewa wa matakwa ya sheria miongoni mwa wafanyabiashara na kukua kwa biashara.” Ameeleza Fimbo.
Aidha, Fimbo ameongeza kuwa TFDA imekuwa ikifanya tathmini na usajili wa bidhaa kwa lengo la kuhakiki endapo bidhaa zinakidhi vigezo vya usalama, ubora na ufanisi kabla ya kuruhusiwa katika soko.
“Kuwepo kwa bidhaa nyingi zilizosajiliwa katika soko ni uthibitisho kuwa walaji wanapata bidhaa zilizo salama, zenye ubora na ufanisi.
Pia tumeweza kusajili maeneo ya biashara za bidhaa za chakula, dawa, vipodozi, vifaa tiba na vitendanishi kwa lengo la kutambua maeneo ambayo bidhaa hizo zinazalishwa, kuhifadhiwa, kusambazwa na kuuzwa. Mfumo huu husaidia kuhakikisha kuwa maeneo husika yanakidhi vigezo ili kutoathiri usalama, ubora na ufanisi wa bidhaa”. Alieleza Fimbo.
Aidha ameongeza kuwa, TFDA katika kipindi cha miaka mitatu (2015/16 – 2017/18), imeweza kusajili jumla ya maeneo 25,630 ya biashara za bidhaa zinazodhibitiwa ikiwa ni pamoja na maeneo 9,000 yaliyosajiliwa mwaka 2016/17 na maeneo 5,606 mwaka 2015/16, hii ikiwa ni sawa na ongezeko la 60.5%.
Aidha, katika kipindi hiki, TFDA imeendelea kushuhudia kufikiwa kwa dira yake ya kuwa taasisi ya mfano barani Afrika katika udhibiti wa bidhaa za chakula, dawa, vipodozi, vifaa tiba na vitendanishi na hivyo kuvutia nchi mbalimbali kuja kujifunza mifumo iliyopo na kwenda kuitekeleza nchini kwao.
(mfano nchi za Zimbabwe, Rwanda, Kenya, Uganda, Ethiopia, Sudan Kusini, Botswana, Mauritius, Lesotho na Bangladesh zinekuja kujifunza TFDA).
“Katika kipindi cha mwaka 2015/16 – 2017/18, Mamlaka imefanikiwa kufikia na kuvuka malengo iliyojiwekea katika utekelezaji wa mipango kazi yake.
Mamlaka katika kipindi cha 2017/18 itaendelea kutoa kipaumbele katika utekelezaji kwa ufanisi wa malengo mahususi nane (8) yaliyomo katika Mpango Mkakati mpya wa miaka mitano (5) yaani 2017/18 – 2021/22, ili kulinda afya ya jamii.” Alieleza Fimbo.
Mafanikio mengine ni pamoja na kukamilika kwa jengo la Maabara na kufungwa kwa vifaa vya kisasa vya uchunguzi jijini Mwanza jambo ambalo limesaidia kusogeza huduma zaidi kwa jamii .

