Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam amewataka wanafunzi wote waliofaulu na kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kuripoti shuleni bila kisingizio chochote. Agizo hilo amelitoa mapema leo ofisini kwake wakati akizungumza na waandishi wa habari na kuwataka wazazi kuwapeleka watoto wao mashuleni kujiandikisha kidato cha kwanza kwa wale waliofaulu na ikibainika mwanafunzi yeyote amefaulu kisha ameacha kwenda shuleni atakamatwa. “Tukibaini wewe ni mwanafunzi umefaulu halafu umeacha kwenda kwa sababu yoyote ile ya kisingizio tutakukamata,tunachotaka tutumie fursa hii watoto wote wa kitanzania na wanyonge ambao Rais Magufuli amekusudia wapate elimu…
Tuesday, 8 January 2019
SPIKA NDUGAI ASUTWA KILA KONA,NI BAADA YA KUMTAKA CAG AJISALIMISHE ,WENGI WATAMANI KUONA CV YAKE
NI siku moja kupita tangu spika wa Bunge Job Ndugai akimtaka Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG)profesa MUSA ASSAD kufika mbele ya kamati ya Haki,Maadili na Madaraka ya Bunge Januari 21 mwaka huu ili akajieleze na kuthibitisha maneno yake aliyoyatoa nchini Marekani wakati akihojiwa na chombo kimojawapo cha habari.Lakini hali na mapokeo kwa baadhi ya wasomi,viongozi na wanasiasa mbali mbali nchini wamekuwa na mapokeo tofauti na kukosoa wazi wazi katika mitandao ya kijamii juu ya agizo hilo kwa mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali.Agizo la Spika NDUGAI linatokana…
MANARA : NITAONGOZA JESHI LA POLISI KUSAKA WANAOUZA JEZI FEKI ZA SIMBA

'Kwenye mambo muhimu yanayohusu klabu yangu nipo tayari nisiangalie mpira 'Yes' nitaongoza jeshi la polisi kusaka wanaouza jezi feki''.
Ni kauli ya msemaji wa Simba Haji Manara leo alipokuwa akiongea na wana habari kuelekea mchezo wa Klabu Bingwa Afrika hatua ya makundi dhidi ya JS Souara Jumamosi ya wiki hii.
Katika mchezo huo, Manara amesema moja ya jambo ambalo watalitilia mkazo siku hiyo ni kuuza jezi halisi za Simba na sio feki.
''Siku ya mchezo wetu dhidi ya JS Souara nitaongoza jopo la wanasimba wenzangu kwa kushirikiana na Polisi kukamata wale wote wanaoihujumu klabu kwa kuuza jezi feki'' ameongeza Manara.
Aidha Manara amebainisha kuwa wapinzani wao klabu ya JS Souara watafika hapa nchini Januari 10, na Ijumaa watafanya mazoezi kwenye uwanja wa Taifa ambao ndio utatumika kwenye mchezo wa Jumamosi.
Kwa upande wa kikosi cha kwanza cha Simba kinatarajiwa kurejea Dar es salaam kutoka Zanzibar kesho asubuhi tayari kwa maandalizi ya mchezo huo.
Chanzo- EATV
MAKONDA AFUNGUKA KUHUSU 'MA HOUSE GIRL DAR'

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema kuwa wanaoishi na wafanyakazi wa ndani, wanatakiwa kuona uchungu kuwatumikisha watoto wadogo wanaotakiwa kuwa shule.
Makonda ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na wanahabari, ambapo amesema kuwa kukaa na mtoto mdogo na kumuagiza kazi za nyumbani ni kuitumia vibaya kodi yao kwani Rais amelipia ada watoto wote.
"Rais Magufuli amelipa ada kwa watoto wote, muwaache wasome kwani kufanya hivyo ni kuharibu kodi zenu wenyewe maana ada iliyolipwa ni kodi zenu", amesema Makonda.
Aidha katika hatua nyingine amewataka wazazi kutowapeleka watoto kujiunga na elimu ya sekondari kwa kigezo cha mahitaji, kwani walitakiwa kujiandaa mapema pindi mtoto amemaliza darasa la saba na watakaofanya hivyo watachukuliwa hatua.
"Ada imelipwa na hakuna michango, lakini utakuta watu wanawaficha watoto kisa hana hela ya sare na madaftari", amesema Makonda.
RAIS WA BENKI YA DUNIA AJIUZULU
Rais wa Benki ya Dunia, Jim Yong Kim ametangaza kujiuzulu Februari Mosi, ikiwa ni miaka mitatu kabla ya muhula wake kumalizika mwaka 2022.
Kim ambaye anajiunga na kampuni binafsi inayoangazia uwekezaji katika mataifa yanayoendelea, amesema imekuwa ni heshima kubwa kwake kuiongoza taasisi hiyo muhimu.
Ofisa Mkuu wa Benki ya Dunia, Kristalina Georgieva, atachukua nafasi ya rais wa mpito baada ya Kim kuondoka.
Kim alianza kipindi chake cha pili kama Rais wa Benki ya Dunia, Julai, 2017.
Alichukua mikoba ya Robert Zoellick mwaka 2012, chini ya rais wa zamani wa Marekani, Barack Obama.
Taasisi hiyo inayohusika na kufadhili miradi katika nchi zinazoendelea, kwa kawaida imekuwa ikiongozwa na raia wa Marekani.
Taasisi hiyo ilianzishwa mwishoni mwa Vita Kuu ya Pili ya Dunia sambamba na Shirika la Fedha Duniani, IMF ambalo huongozwa na raia wa Ulaya.
WENYEVITI WAGOMEA KIKAO KISA DIWANI KUKAIMISHA NAFASI YAKE KIMYA KIMYA
Na.Amiri kilagalila Wenyeviti wa serikali za mitaa kata ya kivavi halmashauri ya mjini makambako wamegoma kushiriki kikao cha kujadili maendeleo ya kata hiyo (KAMAKA) kwa kile kilicho elezwa kuwa ni kutokana na diwani wao kutokuhudhuria vikao. Wakizungumza na mtandao huu wenyeviti hao wamesema kuwa diwani wa kata hiyo BARAKA KIVAMBE ameshindwa kuhudhulia takribani vikao vinne pasipo kuwa na sababu za msingi, hali ambayo imepelekea shughuli za kimaendelo kukwama ndani ya kata hiyo hususani ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari DEO SANGA. “Tumefika hivi leo ni kwasababu ya…
Mbunge Ritta Kabati Mgeni rasmi mchezo kati ya Panama Girls fc na Evergeen kesho uwanja wa Samora
NA mwandishi wetu , IRINGA MBUNGE wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM) kesho jumatano kuwa mgeni rasmi katika mchezo wa ligi kuu ya mpira wa miguu wanawake Tanzania maarufu kwa jina la Serengeti Lite Wome’s Premier League 2018/2018 kati ya wenyeji Panama Girls FC (Iringa ) na Evergreen Queens (Dar Es Salaam) Afisa habari wa Panama Girls Fc, Francis Godwin alisema kuwa mchezo huo ambao ni wa tatu kuchezwa nyumbani utachezwa katika uwanja wa Samora majira ya saa 10 jioni na wamemualika mbunge Kabati pamoja na viongozi…
Breaking : RAIS MAGUFULI AFANYA MABADILIKO KWENYE BARAZA LA MAWAZIRI
Rais Magufuli leo amefanya mabadiliko ya baraza la mawaziri ambapo amemteua Angela Kairuki kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu/Uwekezaji.
Naibu Waziri wa Madini Dotto Biteko amekuwa waziri kamili wa madini, na Stanslaus Nyongo ataendelea kuwa maibu waziri wa wizara hiyo
Rais amemteua Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dr. Mpoki Ulisubisya kuwa balozi, kituo chake cha kazi kitatangazwa baadaye, pia Magufuli ametangaza kufungua ubalozi wa Tanzania nchini Cuba ambapo balozi atatangazwa baadaye.
Pia, Rais Magufuli amemteua Dr. Zainab Chaula kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya kuziba nafasi ya Dr Mpoki .
Kadhalika, Engineer Joseph Nyamuhanga ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu TAMISEMI
JE HUWA UNALALA NA NGUO?? KUANZIA LEO USILALE NA NGUO KUNA FAIDA KIBAO

Binadamu alivyoumbwa na Mungu anapaswa kujisitiri kwa kuvaa mavazi yatakayofunika mwili wake. Lakini mavazi haya hayapaswi kuvaliwa kwa muda wote (masaa 24 kwa siku), kutokana na sababu mbali, za kiafya au za kawaida kama ilivyo asili ya uumbaji.
Nchi zenye ukanda wa hali joto ikiwemo Tanzania, kulala huku ukiwa umevaa nguo ni moja ya vitu hatari kiafya, kwani inaweza kusababisha madhara kiafya.
Hapa nakupa sababu tano muhimu ambazo zitakazokufanya kuanzia leo usilale na nguo yoyote, na hii ni kwa faida yako mwenyewe.
1. Kulala vizuri
Hapa inaeleweka wazi kisayansi kuwa ili ulale vizuri mwili wako unahitaji kutulia, upoe, na ndio maana tunaoga kabla ya kulala, ili kupunguza joto mwilini, ukiwa umevaa nguo mwili wako unabaki kuwa na joto, na kukufanya ukose usingizi na kukosa utulivu, lakini ukilala bila nguo, unaruhusu mwili wako kupata hewa ya kutosha na kusaidia kupoza joto la mwili, na kukupa usingizi mzuri zaidi.
2. Kuacha mwili upumue
Kila sehemu ya mwili wetu umeundwa kwa seli zinazohitaji hewa ili zipumue, ukiwa unalala na nguo zinakuwa hazipati hewa ya kutosha hata kama mwili unakuwa haufanyi kazi yoyote zaidi ya kutulia tu. Hii ni zaidi kwa wanawake ambao wanalala na nguo za ndani , ukilala na nguo za ndani unawapa fursa backeria na aina ya 'yeast' kukua ndani ya mwili. Hivyo kulala bila nguo itakuepusha na magonjwa yatokanayo na bacteria hasa kwa wanawake.
3. Husaidia kuondoa msongo wa mawazo na mwenza wako
(Stress free with parter)
Wote tunajua kukumbatiana wakati umelala na mwenzi wako ni njia bora ya kuondoa msongo wa mawazo, lakini iwapo utafanya hivyo mukiwa hamjavaa nguoo ni bora zaidi. Unajua kwa nini!?. Hii ni kwa sababu mawasiliano ya ngozi kwa ngozi bila kujihusisha na tendo la ndoa ni bora zaidi na kukufanya akili itulie na kukufanya ujihisi vizuri zaidi, na kuondoa mawazo yote. Pia husaidia kupunguza uwezekanao wa kupata maradhi ya moyo na kukufanya uwe mwenye furaha.
4. Kuwa karibu na mwenzi wako
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa kwa zaidi ya wanandoa 1000 wa nchini Uingereza, ulionesha kwamba wanandoa wanaolala bila nguo wana furaha zaidi kuliko wale wanaolala na nguo. Hii ni kutokana na yale yalioyoelezwa kwenye maelezo ya kipengele chana 3, hivyo inasaidia kukuza uhusiano wao na kuburudishana, kutengeneza 'muunganiko' zaidi kutokana na kulala bila kikwazo chochote kati yao.
5. Kupunguza uzito
Utaona kama ni jambo la ajabu kuwa kulala bila nguo kunahusiana vipi na kupunguza uzito!?. Lakini ukweli ni kwamba ukiwa unalala 'uncomfortable', utakuwa na stress zaidi ambazo zitakusababisha kula vyakula ambavyo havifai kwa afya ya mwili, ili tu ujifurahishe. Lakini ukilala ukiwa umetulia hukupunguzia msongo wa mawazo, na kukufanya uwe usiyekuwa na wasiwasi wa jambo lolote.
Hebu fikiria kuanzia sasa kufuata muongozo huu kwa afya yako ya mwili na kiakili pia.
MBUNGE NYAMAGANA ATOA SH. 7,230,000.00 KUBORESHA SEKTA YA ELIMU KATA YA PAMBA NA BUTIMBA
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Stanslaus Mabula ametoa msaada wa shilingi 7,230,000.00 kuboresha sekta ya elimu Katika Kata mbili za halmshauri ya Jiji la Mwanza ikiwemo Kata ya Pamba na Butimba, msaada uliolenga ukarabati wa madarasa mawili shule ya Msingi Butimba B, ukamilishaji wa ujenzi wa darasa moja shule ya Msingi Amani pamoja na ujenzi wa uzio kudhibiti utoro kwa wanafunzi Shule ya Sekondari Mlimani. Mhe. Mabula akikabidhi msaada huo kwa nyakati tofauti amefafanua shilingi 4,000,000.00 fedha taslimu zimetolewa kupitia mfuko wa Jimbo na vifaa vya ujenzi Bati na Saruji…
MFALME WA SOKA AFRIKA KUJULIKANA LEO...NI SALAH,MANE AU AUBAMEYANG

Wanaowania tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika
Tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika inatarajiwa kutolewa leo Jijini Dakar nchini Senegal, ambapo jumla ya mastaa watatu wanaocheza Ligi Kuu ya Uingereza (EPL), Mohamed Salah, Pierre-Merick Aubameyang na Sadio Mane.
Listi hiyo ni marudio ya wachezaji watatu waliotajwa kuwania tuzo ya msimu uliopita, ambapo itatolewa kwa kuzingatia kiwango cha mchezaji husika katika mwaka 2018.
Pierre-Merick Aubameyang ambaye ni raia wa Gabon, amefanikiwa kuwepo katika listi ya mwisho ya wachezaji watatu wa tuzo hizo kwa mara ya tano mfululizo sasa tangu mwaka 2014 na kuifikia rekodi ya mkongwe wa Ivory Coast, Yaya Toure na wa Ghana, Michael Essien.
Mohamed Salah ambaye aliweka historia ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Misri kushinda tuzo hiyo tangu ilipoasisiwa mwaka 1992. Ametajwa katika listi ya wachezaji watatu wa mwisho kwa miaka miwili mfululizo huku akishinda kwa mara ya kwanza msimu uliopita.
Kwa upande wa Sadio Mane, ametajwa katika listi ya wachezaji watatu wa mwisho wa tuzo hiyo kwa mwaka wa tatu mfululizo huku akiwa hajashinda tuzo hiyo mpaka sasa.
Jana, Januari 7, ulifanyika mchezo wa mastaa wa zamani wa soka barani Afrika, mchezo uliohusisha kati ya magwiji wa soka wa Senegal walioshiriki katika fainali za Kombe la Dunia mwaka 2002 na magwiji wa zamani wa soka kutoka sehemu mbalimbali barani Afrika, akiwemo mchezaji bora wa Dunia na Rais wa Liberia, George Weah.
Pia kabla ya kilele cha tuzo hizo, Shirikisho la Soka Barani Afrika CAF itafanya kikaom maalum ambacho kitatangaza nchi itakayoandaa michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka huu, baada ya nchi ya Cameroon kupokonywa uenyeji wa michuano hiyo kwasababu ya kutokidhi vigezo.
KANGI LUGOLA APIGA MARUFUKU KUTAMBUA WAHAMIAJI HARAMU KWA PUA NDEFU

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amepiga marufuku tabia ya Maafisa Uhamiaji kuwatambua wahamiaji haramu kwa kigezo cha Pua ndefu.
Lugola amepiga marufuku hiyo jana alipokuwa akiongea kwenye moja ya mikutano yake mkoani Kagera ambako yupo kwenye ziara ya kikazi aliyoianza Januari 2, mwaka huu.
''Idara ya uhamiaji kutambua wahamiaji haramu kwa kigezo cha pua ndefu, kuimba wimbo wa taifa na urefu wa mwili wake nimepiga marufuku'', amesema.
Aidha Lugola ameongeza kuwa Idara ya Uhamiaji ina taratibu na vigezo vyake vya kiweledi katika kushughulika na suala hilo hivyo amesisitiza viendelee kutumika kubaini nani raia na nani sio raia.
MUWAWATA WATAKA SERIKALI IWATUMIE KUSHAURI MAENDELEO
Na Stephen Noel Mpwapwa -Dodoma Muungano wa wanajeshi wastafu(MUWAWATA) wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma wameomba uongozi wa serikali sehemu walipo kuweza kutumika kuishauri kamati za ulinzi na usalama juu ya masuala ya ulinzi ndani ya wilaya. Kauli Hiyo imetolewa na Leftnant Kanali Mstafu Mathias Ngimba kwenye sherehe za kuukaribisha mwaka mpya 2019 zilizo fanyika Katika Ukumbi wa Padre Pio wa kanisa katoliki mjini hapa. Leftnat Kanal mstaafu Ngimba amesema Kama wanajeshi wastafu wameamua kuunda umoja huo ili kuweza kusaidiana kujikimu katika maisha baada ya kuachana na utumishi wa serikali. Aidha Leftnant…
WANAFUNZI KUTOKA CHUO CHA ULINZI CHA TAIFA WATUA KAGERA KUJIFUNZA
Na: mwandishi wetu Bukoba- Kagera Ujumbe wa Kitaifa wa Maafisa wa Vyombo Mbalimbali vya Ulinzi na Usalama kutoka Chuo cha Ulinzi cha Taifa (National Defence Collage) ukiwakilisha nchi 11 tofauti wautembelea Mkoa wa Kagera Januari 7, 2019 kujifunza na kubadilishana ujuzi na Uongozi wa Mkoa hasa katika masuala ya Ulinzi na Usalama na kutumia fursa hiyo kushauriana namna bora ya kukuza uchumi wa Mkoa wa Kagera. Ujumbe huo wa Maafisa 16 kutoka Chuo cha Ulinzi cha Taifa ukiwa na Maafisa kutoka nchi za Tanzania, Kenya, Nigeria na China mara baada…
VITA YA UBUNGE YAANZA MAPEMA IRINGA, CCM WATAKA,MSIGWA AKOMAA
Vita ya kuwania Jimbo la Iringa Mjini imeanza mapema baada ya mwenyekiti mpya wa CCM mkoani humo, Dk Abel Nyamahanga kuahidi kulirejesha mikononi mwa chama hicho.
Hata hivyo, mbunge wa jimbo hilo, Mchungaji Peter Msigwa, amemjibu akisema hayumbishwi na kauli hiyo na kwamba CCM haiwezi kulichukua kwa kuwa Chadema ina wafuasi wengi.
Akizungumza juzi na wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM baada ya kutangazwa mshindi, Dk Nyamahanga aliahidi kuwa atahakikisha jimbo hilo linarudi mikononi mwa CCM kwa njia yoyote akianza na kutatua changamoto za wananchi.
“Nashukuru kuchaguliwa kuwa mwenyekiti, ndoto yangu ni kuhakikisha navunja makundi ya baadhi ya wanachama na kuhakikisha tunaungana kuchukua jimbo kwa masilahi ya wananchi wanaokiamini chama kilichopo madarakani ambacho ni CCM,” alisema.
Mwenyekiti huyo alikuwa akirejea maagizo ya Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda ambaye ni mlezi wa CCM Mkoa wa Iringa aliyehoji kwa nini jimbo hilo liko chini ya chama cha upinzani na kuagiza katika uchaguzi wa 2020 lirudishwe CCM.
“Tunahitaji kufanya uchunguzi kwa nini jimbo lipo upinzani. 2020 ni muhimu likarudi CCM tu, nataka kujua je, ni wapigakura ndiyo tatizo au wana CCM wenyewe tunashindwa kusimamisha mgombea tunayemtaka?” alihoji Pinda.
Akizungumza na Mwananchi jana, Msigwa ambaye alishinda katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 na 2015, alisema haoni kama CCM ina ubavu wa kulichukua jimbo hilo. Msigwa ambaye pia ni mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Nyasa, alisema katika mkoa huo wafuasi wa Chadema ni wengi zaidi na haoni kama chama chake kitapokwa jimbo katika Uchaguzi Mkuu ujao na kuwataka wanachama wake kuendelea kujenga imani kwa chama na viongozi mkoani humo.
“Tunajipanga vizuri kukabiliana na hali yoyote, hatutaki tupate mgombea mwepesi na tutawashinda kwa nguvu sana,” alisema.
Na Berdina Majinge na Cledo Michael mwananchi
WAZIRI MKUU : KAMPUNI ZOTE ZINAZOSAMBAZA NGUZO ZA UMEME ZILIPE USHURU KWA HALMASHAURI
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kampuni zote zinazosambaza nguzo za umeme zinatakiwa zilipe ushuru wa halmashauri wanakotoa nguzo hizo ambazo ni asilimia tano ya gharama ya kila nguzo kama ilivyoelekezwa na Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa.
Ametoa agizo hilo jana (Jumatatu, Januari 7, 2019) baada ya kupata taarifa kuhusu kampuni ya New Forest ambayo inamkataba na TANESCO wa kusambaza nguzo za umeme, kwa muda mrefu kampuni hiyo imekuwa ikikaidi kulipa ushuru wa asilimia tano ya gharama ya kila nguzo. Ushuru huo umefikia sh. bilioni 2.9 hali iliyopelekea uongozi wa mkoa kuzuia nguzo hizo zisitoke.
Wiki iliyopita akiwa katika ziara ya mkoa Ruvuma, Waziri Mkuu alipokea malalamiko kuhusu mkoa wa Iringa kuzuia kusambazwa kwa nguzo za umeme ndipo alipoamua kuwaita Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happi pamoja na wakuu wa wilaya, wakurugenzi pamoja na wenyeviti wa halmashauri wanaotoka katika wilaya zinazozalisha nguzo.
Viongozi wengine waliohudhuria kikao hicho ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye ulemevu, Jenista Mhagama, Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Josephat Kandege, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, Naibu Waziri Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya pamoja na maafisa wengine wa Serikali.
Amesema lengo la kikao hicho lilikuwa kupata ufafanuzuzi kuhusu malalamiko yaliyotolewa dhidi ya uongozi wa mkoa wa Iringa kuhusu kuzuia usafirishaji wa nguzo za umeme zinazotomika kwenye miradi ya Kusambaza Nishati ya Umeme Vijiji (REA).
Baada ya kupata maelezo hayo, Waziri Mkuu amemuagiza mkuu wa mkoa wa Iringa kuiandikia bili kampuni ya New Forest ili ilipe ushuru huo kuanzia Julai 2018 walipoanza kusambaza nguzo. Asilimia 90 ya nguzo za umeme nchini zinatoka Iringa. Tanzania ina viwanda tisa vya kutengeneza nguzo na kati ya viwanda hivyo vinane vipo Iringa na kimoja kipo Tanga.
Kampuni ilizuiwa kutoa nguzo ndani ya mkoa wa Iringa tangu Novemba 2018 hadi Januari 2019 huku ikitakiwa kulipa ushuru wa asilimia tano ya gharama ya kila nguzo ambapo ilikaa ikitaka iendelee kulipa sh. 5,000 kwa kila nguzo kama walivyokubaliana na TANESCO jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
Hata hivyo, nguzo za umeme ambazo zilikuwa zimezuiwa kwa muda mrefu katika maeneo ya uzalishaji hususani mkoani Iringa na kusababisha kukwama kwa baadhi ya miradi ya usambazaji umeme kwenye baadhi ya mikoa nchini juzi zimeanza kusambazwa huku taratibu nyingine za malipo zikiendelea.
DKT. BASHIRU AWATAKA WATUMISHI WA SERIKALI KUJIFUNZA KUFANYA MAAMUZI KUTOKA KWA RAIS MAGUFULI
Na Stella Kalinga, Simiyu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Dkt. Bashiru Ally amewataka Watumishi wa Serikali kujifunza kufanya maamuzi kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, kwa ajili ya maslahi mapana ya Taifa. Dkt. Bashiru ameyasema hayo mjini Bariadi katika kikao na Wakurugenzi wa Taasisi zitakazoshirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kujenga kiwanda cha (vifaa tiba) bidhaa za afya zitokanazo na pamba wilayani Bariadi, baadhi ya viongozi, watendaji wa Chama…



