Saturday, 25 February 2017
Friday, 24 February 2017
Mahakama Yamzuia RPC Kujibu Swali la Tundu Lissu
Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imemzuia shahidi wa kwanza
katika kesi inayomkabili Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na
wenzake watatu, kujibu swali linalohusu mamlaka ya kikatiba ya
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), kufuta uchaguzi
uliofanyika Oktoba 25,2015. Kwa mujibu wa Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas
Simba , swali hilo la Lissu halina mashiko.
Lissu
alimuuliza shahidi ambaye ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Ilala,
Salum Hamduni kwamba, Jecha Salim Jecha ana mamlaka gani kikatiba kufuta
uchaguzi uliofanyika Oktoba 25, 2015.
Lissu
alimuuliza Kamanda Hamduni kama anafahamu mamlaka yapi ya kikatiba
ambayo Mwenyekiti wa ZEC, Jecha aliyatumia kufuta uchaguzi mkuu wa
madiwani, wabunge na Rais.
Wakili
wa Serikali, Paul Kadushi amedai kuwa shahidi huyo amekwenda mahakamani
kutoa ushahidi kuhusu maelezo na kwamba si kutoa tafsiri ya kisheria
kuhusu Katiba ya Zanzibar.
Kadushi
amedai anapinga shahidi wake kujibu swali hilo kwamba Mwenyekiti wa ZEC
ana mamlaka ya kufuta uchaguzi ama la na kueleza kuwa shahidi huyo hana
ufahamu wa sheria na si mtaalamu wa Katiba na sheria.
''Napinga
shahidi kujibu swali hili ambalo kimsingi linamtaka atafsiri sheria,
jambo ambalo silo lililomleta na wala hana utaalamu wa kisheria. Hata
hivyo, mahakama hii haina mamlaka ya kutafsiri Katiba isipokuwa ni
mahakama ya kikatiba na mahakama kuu ndio yenye uwezo huo,'' alidai Kadushi.
Lissu
alipinga hoja hizo kwa maelezo kwamba, pingamizi la wakili wa serikali
halina maana kwa sababu suala la mamlaka halali au si halali ya Zanzibar
limeletwa na upande wa mashitaka wenyewe, kama ambavyo mashitaka ya
pili katika kesi hiyo wameeleza kuwa habari iliyochapishwa ingeweze
kuleta chuki kwa Wazanzibar kuichukia nchi yao.
Alidai
kuwa, masuala ya mamlaka wameyaleta wenyewe wanapaswa kukabiliana nayo,
kwa kuwa Sheria ya Ushahidi namba 147, kifungu kidogo cha pili na
Sheria namba 157 ya sheria hiyo, vinaweka wazi kwamba shahidi anaweza
kuulizwa swali lolote na kwamba si lazima liwe ndani ya kile
anachokitolea ushahidi.
Hakimu Simba amesema, mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kuzungumzia Katiba ya Zanzibar.
Amesema
mahakama katika kesi hiyo haitazungumzia uhalali au kutokuwa halali kwa
Mwenyekiti wa ZEC, Salim Jecha kufuta au kutofuta uchaguzi mkuu
Zanzibar.
"Pingamizi
la upande wa mashitaka ambao ulipinga masuala ya kikatiba ambayo mbunge
huyo alikuwa akimuuliza shahidi kuhusu Jecha ana mamlaka gani kikatiba
kufuta uchaguzi uliofanyika Oktoba 25, 2015, ni sahihi na shahidi
hatakiwi kujibu swali hilo," amesema Hakimu Simba.
Lissu
amedai uamuzi huo hautamuathiri na kwamba anakubaliana nao kwamba
haruhusiwi kuuliza swali hilo kwa shahidi hivyo waendelee na ushahidi.
Hakimu
Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Machi 8 na 9, mwaka huu na kuutaka
upande wa mashitaka kupeleka mashahidi ili kesi iishe kwa kuwa watu
wengi wanaifuatilia hivyo iishe waendelee na shughuli za maendeleo.
Washitakiwa
wengine katika kesi hiyo ni Mhariri wa gazeti la Mawio, Simon Mkina,
mwandishi wa gazeti hilo, Jabir Idrisa na Mchapishaji wa Kampuni ya
Jamana, Ismail Mehboob.
Wanadaiwa
kati ya Januari 12 na 14, mwaka huu, Dar es Salaam, kwa lengo la kuleta
chuki kwa wananchi wa Zanzibar, Jabir, Mkina na Lissu, kwa pamoja
waliandika na kuchapisha taarifa za uchochezi zenye kichwa cha habari
kisemacho, 'Machafuko yaja Zanzibar'.
Katika
mashitaka yanayomkabili Mehboob, anadaiwa kuwa, Januari 13 katika jengo
la Jamana, Dar es Salaam, alichapisha gazeti la Mawio lililokuwa na
taarifa za uchochezi, pia alichapisha gazeti hilo bila ya kuwasilisha
hati ya kiapo kwa Msajili wa Magazeti.
Wednesday, 22 February 2017
Mahakama Yamkingia Kifua Mbowe,Yaamuru Asikamatwe
Mahakama
Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetoa zuio la muda kuzuia Mwenyekiti wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe asikamatwe na
Polisi hadi maombi yake, aliyoyaomba ya kutaka asikamatwe,
yatakaposikilizwa kesho.
Katika
kesi hiyo ya kikatiba namba 1 ya mwaka 2017, Mbowe anapinga mamlaka ya
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Kamanda wa Polisi Kanda
Maalum, Simon Sirro na Mkuu wa Upelelezi wa kanda hiyo (ZCO), Camilius
Wambura, ya kutaka kumkamata hadi maombi hayo yatakaposikilizwa.
Maombi
ya kesi hiyo yataanza kusikilizwa Februari 23, mwaka huu saa 7:30
mchana katika chumba cha wazi cha mahakama ili kuruhusu watu mbalimbali
kusikiliza kesi hiyo.
Jopo
la majaji watatu likiongozwa na Sekieti Kihiyo akisaidiana na Jaji
Lugano Mwandambo na Jaji Pellagia Kaday lilitoa zuio hilo, hata hivyo
walisema Polisi wanaweza kumuita Mbowe kwa mahojiano pindi
watakapomhitaji.
Kesi
hiyo ambayo ilisikilizwa kwa vipindi vitatu kuanzia saa 4 asubuhi hadi
saa 7 mchana, mahakama iliamuru upande wa wadai ambao uliongozwa na
Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu, kurekebisha maombi yao kwa
kuwa hawakumuingiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) licha ya
kuishitaki serikali.
Hali
hiyo ilitokana na mawakili wa upande wa wadai, Lissu ambaye alipinga
kitendo cha Mwanasheria wa Serikali, Gabriel Malata kuwatetea wadaiwa
hao ambao ni RC, RPC na ZCO katika kesi hiyo kwa kuwa hawajaitaja
serikali.
Akijibu
hoja hiyo, Malata alidai kuwa waliofunguliwa madai hayo sio Makonda,
Sirro wala Wambura, bali ni serikali hivyo ana mamlaka yote ya
kuwawakilisha.
Baada
ya pande zote kuwasilisha hoja zake, mahakama ilimruhusu Malata
kuendelea kusikiliza kesi hiyo ambapo pia iliagiza upande wa wadai
kufanya marekebisho ya maombi hayo na kumuongeza AG kama mdaiwa.
Hata hivyo, Lissu aliomba waruhusiwe kufanya marekebisho hayo kwa kumuongeza AG, ombi ambalo halikuwa na pingamizi.
‘’Tutafanya
marekebisho ya maombi yetu na marekebisho mengine madogo madogo kwa
namna tutakavyoona inafaa siku ya Jumatatu na tutawapa wajibu maombi
Machi 6 mwaka huu na Machi 8 mwaka huu itatajwa kwa ajili ya kusikiliza
maombi hayo,’’ alidai Lissu.
Mbowe
aliwasili mahakamani hapo akiwa na gari lenye usajili namba T 830 aina
ya Land Cruiser, saa chache kabla ya kesi yake kuitwa katika chumba
namba 64 kwa ajili ya kusikilizwa.
Mbowe
ambaye pia ni Mbunge wa Hai mkoani Kilimanjaro, alifika mahakamani hapo
baada ya kutoka Kituo Kikuu cha Polisi saa 7 usiku, alikokuwa anahojiwa
na kupekuliwa kuhusu sakata la dawa za kulevya.
Aidha,
viongozi mbalimbali wa chama hicho wakiwemo Mbunge wa Kibamba, John
Mnyika, Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya, Mbunge wa Iringa Mjini,
Mchungaji Peter Msigwa, madiwani na wafuasi wao walijitokeza kwa wingi,
kusikiliza kesi hiyo huku wakifurahia amri ya mahakama ya kuzuia
kutokamatwa kwa mwenyekiti huyo.
Katika
kesi ya msingi, Mbowe anaomba mahakama iwazuie wadaiwa kutekeleza azma
yake ya kumtia mbaroni, pia itoe amri ya kuwazuia kumkamata hadi hapo
kesi hiyo ya kikatiba, itakapomalizika na kwamba polisi wasiendelee na
mchakato wowote dhidi yake hadi hapo kesi hiyo itakapomalizika.
Anadai
kuwa sheria inayompa Mkuu wa Mkoa mamlaka ya kutoa amri ya kumkamata na
kumweka ndani mtu, iko kinyume cha katiba, kwa madai kuwa ilitungwa
katika mazingira ambayo hapakuwa na vituo vya polisi vya kutosha.
Pia anadai kuwa kwa mazingira ya sasa, sheria hiyo imeshapitwa na wakati na anaiomba mahakama itamke kuwa ni kinyume cha katiba.
Mbowe
pia anadai kuwa hata kama Mkuu wa Mkoa alikuwa anatekeleza mamlaka yake
kwa mujibu wa sheria hiyo, basi hakutimiza matakwa ya kisheria, ambayo
ni pamoja na kutoa taarifa kwa Hakimu wa Mahakama ya Wilaya au ya Hakimu
Mkazi.
Vile
vile, anaiomba mahakama kama itaona kuwa Mkuu wa Mkoa alikuwa sawa
kutoa amri hiyo, basi imwamuru afuate matakwa ya kisheria, ikiwa ni
pamoja na kulinda haki za binadamu katika kutekeleza madaraka yake hayo.
TCU: ORODHA YA WANAFUNZI WASIO NA SIFA KATIKA VYUO VYA ELIMU YA JUU 2016/2017
TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA
TAARIFA KWA UMMA
WANAFUNZI WASIO NA SIFA KATIKA VYUO VYA ELIMU YA JUU
Tume ya Vyuo Vikuu
Tanzania (TCU) inautangazia Umma kuwa zoezi la uhakiki wa sifa za wanafunzi
wanaondelea na masomo kwenye Vyuo vya Elimu ya Juu nchini kwa mwaka 2016/2017
limekamilika katika baadhi ya vyuo. Katika kutekeleza zoezi hilo Tume imebaini
kuwa kuna wanafunzi ambao wamedahiliwa katika programu ambazo hawana sifa.
Orodha ya wanafunzi
wasio na sifa imeshawasilishwa kwenye vyuo husika. Hivyo, wanafunzi wote
wanaondelea na masomo kwenye Vyuo vya Elimu ya Juu nchini wanaweza kutazama
matokeo ya uhakiki wao kupitia kiunganisho (link) (Bonyeza Uhakiki wa Sifa za Udahili).
Tume inawaarifu
wanafunzi wote ambao majina yao yameorodheshwa wawasiliane na vyuo vyao ili
kuthibitisha sifa zao kabla ya tarehe 28 Februari 2017. Wanafunzi ambao
hawatafanya hivyo hawatatambuliwa na Tume na hivyo kukosa sifa za uanafunzi.
TCU inatoa rai kwa
wanafunzi wote kutembelea tovuti ya Tume (www.tcu.go.tz) mara kwa mara ili
kupata taarifa mpya kuhusu uhakiki wa sifa za wanafunzi.
Imetolewa na
Katibu
Mtendaji
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania
20/02/2017
WANAOSOMA CHINA KUISOMA NAMBA,SERIKALI YASISITIZA KUSITISHA FEDHA ZA MIKOPO KWA WANAFUNZI WANAOSOMA NCHINI CHINA
Serikali kupitia wizara ya elimu,sayansi na teknolojia imesisitiza kusitisha pesa za mikopo ya nauli za kwenda masomoni na malipo mengine yote yaliyokuwa yanatolewa kwa wanafunzi wanapata ufadhili wa masomo kutoka kwa nchi rafiki ikiwemo nchi ya China.
Kauli hiyo imetolewa kupitia barua(ya tarehe 7,February,2017) iliyoandikwa na wizara ya elimu ,sayansi na teknolojia kwenda ubalozi wa Tanzania chini
China wakati wakijibu barua iliyoandikwa na wanafunzi wanaosoma nchini
china kuomba serikali kuangalia vizuri maamuzi hayo.
Takribani miezi miwili iliyopita,Bodi
ya mikopo (HESLB) iliauandikia barua ubalozi wa Tanzania nchini china
kuueleza maamuzi ya serikali kusitisha utoaji wa fedha za nauli kwa
wanafunzi hao.Lakini wanafunzi hao hawakuridhika na maamuzi hayo hivo
kuamua kuiandikia barua wizara ya elimu kuangalia vizuri maamuzi hayo.
Kwa mujibu wa barua hii
,wanafunzi watatakiwa kujigharamia wenyewe gharama za kwenda na kurudi
masomoni kitu ambapo awali walikuwa wanapatiwa na serikali ya Tanzania.
Hii hapa barua mpya uliyosisitiza kutotoa pesa hizo na nauli kwa wanafuni hao
Tuesday, 21 February 2017
HIZI HAPA HABARI KALI SIKU YA LEO JUMANNE FEB 21 2017
MBOWE APEKULIWA USIKU ARUDISHWA POLISI,SOMA ZAIDI HAPO>>>>>https://goo.gl/T5jbX8
MAGAZETI YA LEO JUMANNE FEB TAREHE 21.2.2017,SOMA ZAIDI HAPO>>>>>https://goo.gl/PHqMKK
SHAMSA FORD AMLILIA MUMEWE ALIEKAMATWA KWA KESI YA MADAWA YA KULEVYA,SOMA ZAIDI HAPO>>>>>https://goo.gl/6s58nV
NECTA YAWATAKA WANANCHI KUPUUZA TAARIFA ZILIZOTOLEWA KUHUSU MCHUJO KIDATO CHA KWANZA,SOMA ZAIDI HAPO>>>>https://goo.gl/gmq5ds
AUDIO | Shamba Darasa(Mkubwa na Wanawe) - Mwanamke | Download,SOMA ZAIDI HAPO>>>>>https://goo.gl/Ce1kdr
Mahaba Niue!! MZEE WA MIAKA 98 AFUNGA NDOA NA BIBI WA MIAKA 88,SOMA ZAIDI HAPO>>>https://goo.gl/pU13e0
Mahaba Niue!! MZEE WA MIAKA 98 AFUNGA NDOA NA BIBI WA MIAKA 88
Mzee Willy Kinyua (98) amefunga ndoa na Joyce Nyambura (88) baada ya wenza hao kuishi pamoja kwa zaidi ya miaka 60.
SHAMSA FORD AMLILIA MUMEWE ALIEKAMATWA KWA KESI YA MADAWA YA KULEVYA
Mwigizaji
Shamsa Ford ambaye ni mke wa Mfanyabiashara Chidi Mapenzi aliyeitwa
Polisi kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya,
ameandika yafuatayo ikiwa ni mara ya kwanza toka aitwe Polisi kuhojiwa.