Friday, 21 October 2016
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Kufumuliwa.....Waziri Mwijage Asema Litaundwa Upya, Vijana 136 Kuajiriwa
WAZIRI
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amesema atalifumua
na kuliunda upya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na kwamba wameshaanza
kutafuta vijana 136 watakaoajiriwa katika shirika hilo kwa lengo la
kudhibiti bidhaa, zinazoingizwa nchini chini ya viwango.
Serikali Yakubali Kurejesha Posho ya Sh. 8500 kwa Siku kwa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Nchini
Bodi
ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetuliza hasira za
wanafunzi wa vyuo vikuu kwa kurejesha posho ya chakula na malazi ya
Sh8,500 kwa kila mmoja na kwamba tofauti baina yao itakuwa viwango vya
ada.
Ufafanuzi huu uliotolewa jana usiku na Waziri wa Elimu, Sayansi , Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako wakati akizungumza katika mahojiano maalimu na kituo cha runinga cha Taifa -TBC utakuwa faraja kwa wanafunzi ambao chini ya Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Daruso) walipanga kushinikiza walipwe posho ya Sh8,500 kwa siku kama ilivyokuwa awali.
Ufafanuzi huu uliotolewa jana usiku na Waziri wa Elimu, Sayansi , Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako wakati akizungumza katika mahojiano maalimu na kituo cha runinga cha Taifa -TBC utakuwa faraja kwa wanafunzi ambao chini ya Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Daruso) walipanga kushinikiza walipwe posho ya Sh8,500 kwa siku kama ilivyokuwa awali.
Hatua
ya wanafunzi kujenga umoja ili kushinikiza haki katika posho ilitokana
na baadhi yao kuingiziwa kati ya Sh40,000 na 70,000 badala ya Sh
510,000, hali ambayo ilizua sintofahamu.
Ndalichako alisema tofauti ya malipo itakuwa katika ada na siyo posho, “Vigezo
vya mikopo vimebadilika, kila mwanafunzi atapata fedha tofauti lakini
tumefanya marekebisho kwenye posho ya chakula ambayo kila mwanafunzi
atalipwa Sh8,500 kama awali.”
Kwa mujibu wa utaratibu wa Bodi hiyo, malipo hayo ya chakula na malazi hutolewa kila baada ya miezi miwili.
Mapema jana, Daruso iliwataka wanafunzi wa chuo hicho kutotia saini fomu za fedha za mikopo yao mpaka itakapowapa ruhusa ya kufanya hivyo.
Mapema jana, Daruso iliwataka wanafunzi wa chuo hicho kutotia saini fomu za fedha za mikopo yao mpaka itakapowapa ruhusa ya kufanya hivyo.
Rais
wa Daruso, Erasmi Leon alisema hayo jana wakati akizungumza na
wanafunzi wenzake kuhusu kusudio la kwenda HESLB kwa ajili ya kutafuta
haki yao ya msingi.
“Ninachowasihi
tuwe pamoja. Tuwe wamoja na twende pamoja. Tutakwenda wawakilishi
kutafuta nafasi kwa amani waweze kusikia tuna hoja gani lakini
tukinyimwa hii nafasi tutaenda kuitafuta tukiwa wengi,” alisema na kuongeza:
“Tuwe
watulivu kwa sasa tutakapowahitaji muda na wakati wowote kwa lolote
tushirikiane ili twende pamoja tumalize pamoja tuhakikishe tunapata
Sh8,500 kwa kila mwanafunzi kwa chakula na malazi,” alisema.
Kuhusu
suala hilo, uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ulisema
wajibu wake ni kupokea na kusambaza majina na taarifa kutoka Bodi kwa
wanafunzi.
Akitoa
ufafanuzi kwa wanafunzi waliofika ofisini kwake kujua hatima yao na
waliopata mikopo kuchukua fomu za kutia saini, Ofisa Mikopo wa UDSM,
Lugano Mwakyusa alisema wenye jukumu la kujua walio na sifa ya kupata
mikopo ni Bodi ya Mikopo.
“Tunaendelea
kupokea majina kutoka bodi. Tayari hapa kuna majina 949 yameshatoka,
wengine tuzidi kusubiri na wale mwaka wa pili na tatu ambao walikuwa na
mitihani ya marudio taarifa zao zitapelekwa bodi,” Mwakyusa aliwaambia wanafunzi waliokuwa wamejaa ofisini kwake.
Kulikuwa
na hali ya sintofahamu chuoni hapo jana baada ya wanafunzi wengi wa
mwaka wa kwanza kuonekana wakiwa wameshika bahasha za kaki zilizokuwa na
fomu za usajili wanazotakiwa kujaza huku wakihangaika kutokana na
kutojua kiasi cha mkopo.
Juzi, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, AbdulRazaq Badru
alieleza kwamba ingawa wanafunzi 88,000 waliomba mikopo kutoka HESLB,
uwezo wa bodi hiyo ni kutoa kwa wanafunzi 21,500 pekee sawa na asilimia
24 na waliokuwa wameshapatiwa walikuwa 11,000 sawa na asilimia 12.
Takwimu hizi zinaonyesha zaidi ya robo tatu ya wanafunzi wanaohitaji mikopo watakosa kutokana na uwezo mdogo wa kifedha.
Thursday, 20 October 2016
PROF NDALICHAKO:WANAFUNZI WALIOKOSA MIKOPO KUPEWA

waziri wa elimu sayansi na teknolojia prof ndalichako amewatupia lawama
bodi ya mkopo elimu ya juu kuwa wanafanya kazi kwa mazoea amesema pamoja
na kutumia jitiada za kusafisha watumishi bodi hiyo amesema wapo
watumishi bado wanafanya kazi kwa mazoea;
ndalichako amesema ameyasikia
malalamiko kutoka kwa wananchi na anayafanyia kazi na amesema wanafunzi
wapewe mikopo semista hii kwa mwaka wa kwanza na wote bila kufata mean
tested.
amesema lengo la serikali ni kuwapa wote wahitaji amesema na
kuiagiza bodi ya mikopo kuwapa kama mfumo wa zamani Pia bodi ya
mkopo imekosea kuwapa wanafunzi shilingi elfu tano kwa miezi kama pesa
za kujikimu amesema bora kutompa.
source.TBC
source.TBC
TCU yaongeza muda wa udahili vyuo vikuu
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania TCU
imetoa muda wa siku 3 kwaajili ya wanafunzi zaidi ya 4000 ambao wamekosa
fursa ya kudahiliwa katika hawamu tatu za udahili zilizofanywa na tume
hiyo
Kaimu mkurugenzi wa udahili na
nyaraka wa TCU Dkt. Kokuberwa Mollel amesema udahili huo utaanza tarehe
24 hadi tarehe 26 mwezi huu kwaajili ya kozi mbalimbali ambazo bado
hazijajazwa kwani tayari udahili umekamilika kwa wanafunzi wanaosomea
masomo ya udaktari ambapo Jumla ya wanafunzi zaidi ya 2000 wamechaguliwa
kati ya wanafunzi zaidi ya 10,000 waliotuma maombi yao
Dkt. Kokuberwa amesema wanafunzi
wengi walioachwa kwenye usajili wameshindwa kutofautisha viwango vya
ufaulu wao na vigezo vya vyuo husika hivyo wameaswa kuchagua kozi
watakazo zikuta katika tume hiyo na kuacha kung'ang'ania kozi ambazo
hawajakidhi vigezo vyake.
Dk Slaa Aingilia Kati Ugomvi wa Godbless Lema na RC Gambo,Huu Hapa ni Ujumbe Wake
Ugomvi
wa maneno kati ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na Mbunge wa
Arusha Mjini, Godbless Lema limemuibua katibu Mkuu wa zamani wa Chadema,
Dk Wilbroad Slaa aliyeandika ujumbe mrefu akimkingia kifua mbunge huyo.
TAARIFA MUHIMU KWA WANAFUNZI WOTE MLIOCHAGULIWA CHUO KIKUU UDOM 2016/2017

Important information for accessing the University of Dodoma
From the Dodoma bus station, there are two common options of public transport to reach the University of Dodoma.
First, by Taxi
First, by Taxi
- Around the Dodoma regional bus station, there are taxis for transportation services.
Waziri Mkuu Amsimamisha Kazi Mhandisi Wa Maji Lindi
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji
Lindi (LUWASA), Mhandisi Adam Alexander (pichani mwenye mafaili) kwa
kosa la matumizi mabaya ya ofisi pamoja na kushindwa kusimamia ujenzi wa
kituo cha kuzalisha maji katika Manispaa ya Lindi.
Waziri
Mkuu amemkabidhi Mhandisi huyo kwa Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Lindi,
Bw. Stephen Chami na kumuelekeza afanye uchunguzi zaidi juu ya suala
hilo.
Waziri
Mkuu ametoa agizo hilo jana Jumatano, Oktoba 19, 2016 wakati
alipotembelea mradi wa maji wa Ng'apa ambapo aliagiza nafasi hiyo
ikaimiwe na Mkurugenzi Msaidizi wa mamlaka hiyo, Mhandisi Idrisa
Sengulo.
"Kamanda
wa TAKUKURU fanya mapitio ya kina ya mshahara wake. Yeye anasema
analipwa Wizarani, mimi najua analipwa na LUWASA. Angalia kazi
aliyokwenda kuifanya Dar es Salaam kama inalingana na siku alizokaa,” alisisitiza Waziri Mkuu.
Mhandisi
hiyo anakabiliwa na tuhuma mbalimbali ikiwemo matumizi mabaya ya fedha
za ofisi pamoja na kupokea mshahara bila la kulipa kodi ya mapato ya
mshahara (PAYE), kujilipa kiwango kikubwa cha posho pamoja na kusafiri
kwa muda mrefu.
Waziri
Mkuu alisema Serikali haiwezi kuvumilia kuona wananchi wanapata shida
huku watendaji waliopewa dhamana ya kuwatumikia hawaonekani kwenye vituo
vyao vya kazi. "Huyu nimemuita mimi aje huku, hadi jana alikuwa Dar es
Salaam."
Alipoulizwa
sababu za kutokuwepo ofisini kwake kwa muda mrefu, Mkurugenzi huyo
alisema kwamba alikuwa Dar es Salaam akiandika maombi ya fedha kwa ajili
ya kutatulia changamoto mbalimbali zinazoikabili mamlaka hiyo.
"Unatumia
siku ngapi kuandika proposal, msomi unatumia mwezi mzima kuandika
proposal na unakaa Dar es Salaam hata Katibu Mkuu wako hajui na huko
unajilipa posho tu! Tena badala ya kulipwa sh.120,000 kwa siku wewe
unajilipa sh.150,000. Hatuwezi kuvumilia hali hii,” amesema.
Waziri Mkuu amemaliza ziara yake siku tatu mkoani Lindi na amerejea jijini Dar es Salaam.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
Kamati ya Bunge Yakataa faini ya 500,000/- Kwa Kila Kosa Barabarani
Kamati
ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala imekataa mapendekezo ya kufanyia
marekebisho Sheria ya Leseni za Uchukuzi ya mwaka 1973 yenye lengo la
kuongeza kiwango cha adhabu ya faini hadi kufikia asilimia 500 kwa
watakaokiuka masharti ya leseni hizo.
Mapendekezo hayo yaliwasilishwa mbele ya kamati hiyo mjini Dodoma jana na Mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra).
Baada
ya kuyakataa mapendekezo hayo, kamati hiyo imetoa muda wa siku mbili
kwa Sumatra kuhakikisha inawasilisha mbele ya kamati hiyo mapendekezo
yanayokubalika.
Sumatra
inapendekeza kuongeza kiwango cha adhabu ya faini kutoka kati ya Sh
10,000 na Sh 50,000 hadi Sh 200,000 na 500,000 kwa watoa huduma za
uchukuzi, watakaokiuka masharti ya leseni zao.
Mwenyekiti
wa kamati hiyo, Mohammed Mchengerwa alisema mapendekezo hayo, yatazidi
kuwaongezea mzigo Watanzania badala ya kuwasaidia.
Alisema
kiwango hicho cha faini kubwa, kamwe hakitazuia tatizo la ajali za
barabarani, zaidi ya kuongeza ukubwa wa tatizo la rushwa.
“Serikali
ya Awamu ya Tano imejipanga kuwasaidia wananchi, lakini mapendekezo
haya yatazidi kuwaongezea mzigo kwa sababu kiwango cha faini hizi kama
kitapitishwa, watoa huduma za uchukuzi watahamishia hasara yao kwa
wananchi,” alisisitiza.
Aliitaka
mamlaka hiyo, kwenda kuyafanyia kazi tena mapendekezo hayo kwa
kuwasiliana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kuwasilisha viwango vya
faini vinavyokubalika.
Mmoja
wa wajumbe wa kamati hiyo, Joseph Mhagama ambaye pia ni mbunge wa
Madaba, alisema mapendekezo hayo hayana nyongeza yoyote, itakayoisaidia
serikali katika kudhibiti tatizo la ajali barabarani.
“Kwa
sasa serikali imeweka nguvu zake katika kupunguza ajali za barabarani,
lakini kiwango cha faini hizi hakina uhusiano wowote na jitihada hizi
zaidi ya kuiongezea Sumatra mapato na kuwapa mzigo walipa kodi,” alisema.
Akiwasilisha
mapendekezo ya mamlaka hiyo mbele ya Kamati hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa
Sumatra, Gilliard Ngewe alisema mapendekezo ya marekebisho ya sheria
hiyo, yamelenga kuiboresha zaidi sheria hiyo ya leseni za uchukuzi.
Alisema
marekebisho hayo, pia yatasaidia mamlaka hizo kuendana na mahitaji ya
sasa hasa katika eneo la adhabu ya faini, hali itakayopunguza kiwango
kikubwa cha kukiukwa kwa masharti ya leseni hizo za uchukuzi.
Wanavyuo 66,000 wakosa mikopo
Dar es Salaam. Ahadi iliyotolewa na Rais John Magufuli wakati wa kampeni mwaka jana kwamba katika Serikali yake hakuna mwanafunzi atakayekosa mkopo wa masomo ya elimu ya juu imekuwa ngumu kutekelezeka.
Uchunguzi wa Mwananchi umebaini kwamba kati ya wanafunzi 88,000 walioomba mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), wengi hawatapata.
Uwezo wa bodi hiyo ni kutoa mikopo kwa wanafunzi 21,500 pekee sawa na asilimia 24 na waliopatiwa hadi sasa ni wanafunzi 11,000 sawa na asilimia 12.
Takwimu hizi zinaonyesha kwamba zaidi ya robo tatu ya wanafunzi wanaohitaji mikopo watakosa kutokana na uwezo mdogo wa kifedha.
Wednesday, 19 October 2016
HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA CHUO KIKUU SEKOMU 3RD ROUND 2016/2017
KUONA MAJINA TAFADHALI
>>BONYEZA HAPO<<
ADMISSION ISSUES AND DOCUMENTS (2016/2017)
- ADMISSION LETTER - Bachelor of Education Special Needs – [Arts Subjects (BEdSN.ART)/ Science Subjects (BEdSN.Sc)]
- ADMISSION LETTER - Bachelor of Science with Education.
- ADMISSION LETTER - Bachelor of Laws (LL.B)
- ADMISSION LETTER - Bachelor of Science in Mental Health and Rehabilitation (BSc.MHR)
- ADMISSION LETTER - Master of Education in Special Education
- ADMISSION LETTER - Technician Certificate in Primary Teachers Education
- ADMISSION LETTER - Ordinary Diploma in Primary Education
- ADMISSION LETTER - Certificate in Law - TANGA CENTRE
- NAMES OF ADMITTED APPLICANT ROUND ONE
- NAMES OF ADMITTED APPLICANT ROUND TWO
- ATTACHMENT-->| LANDLORDS
- ATTACHMENT-->| MEDICAL FORMS
- ATTACHMENT-->|FEE STRUCTURE
- ATTACHMENT-->| DRESS CODE
- ROUND THREE:ADMITTED APPLICANTS BACHELOR OF SCIENCE WITH EDUCATION
- ROUND THREE: ADMITTED APPLICANTS BACHELOR OF EDUCATION SPECIAL NEEDS SCIENCE
- ROUND THREE: ADMITTED APPLICANTS BACHELOR OF EDUCATION SPECIAL NEEDS ARTS
MPYA:WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA ST.FRANCIS IRAKARA WAANIKA "MADUDU" YA CHUO HICHO HADHARANI,
Habari zenu,leo wanafunzi wa chuo kikuu cha st.francis ifakara wameuandikia uongozi wa maswayetu blog barua,ili tuifikishe mahala husika,naamini kila siku waziri wa elimu lazima usome blog hii,natumaini utaliona hili na kulitolea maamuzi siku si nyingi.











































