Wednesday, 7 September 2016

Magufuli aipa makali NHC




Rais John Magufuli .
Rais John Magufuli . 

Dar es Salaam. Rais John Magufuli ametoa siku saba kwa wizara zote zinazodaiwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ziwe zimelipa madeni yao na zikishindwa ziondolewe kama ilivyokuwa kwa kampuni ya Mbowe Hotels inayomilikiwa na mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.
Rais pia amefanyiwa maombi maalumu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam  Paul Makonda alipotembelea Chuo Kikuu (UDSM), ambako mkuu huyo wa mkoa alisema katika maombi yake kuwa Magufuli ndiye ambaye wananchi walimtaka na kumuomba Mungu azidi kumsaidia katika kutekeleza majukumu yake.
Katika shughuli ya awali, Rais Magufuli alitoa maagizo kwa taasisi hizo alipozungumza na wananchi wa Magomeni wilayani Kinondoni kwenye eneo la Magomeni Quarters ambako Manispaa ya Kinondoni ilibomoa nyumba za wakazi miaka mitano iliyopita kupisha ujenzi wa nyumba za kisasa, ikiahidi kuwalipa wananchi hao kodi ya mwaka mmoja na kuwarejesha baada ya ujenzi kukamilika.
Hata hivyo, manispaa hiyo imeshindwa kujenga nyumba hizo na pia kuwalipa wakazi hao kodi za miaka iliyofuata.
 Rais Magufuli amesema atafurahi kama wizara zinazodaiwa na NHC zitaondolewa kwenye majengo ya NHC kama ilivyofanya kwa mtu ambaye hakumtaja jina na hivyo kulazimika kuhamia Dodoma mapema.
“Nakupongeza sana (mkurugenzi mkuu wa NHC, Nehemiah) Mchechu kwa kazi nzuri unayofanya,” alisema Rais Magufuli.
“Nataka ndani ya siku saba wizara zote zinazodaiwa, ziwe zimelipa madeni yote. Kama hawajalipa watoe nje kama ulivyomtoa yule jamaa.”
Siku chache zilizopita, Mchechu alitangaza majina ya wadaiwa sugu ambao ni pamoja na Mbowe Hotels, taasisi za serikali na watu binafsi na kutoa mwezi mmoja kulipa madeni hayo.
Baadhi ya wadaiwa hao Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sh2 bilioni); Wizara ya Habari (Sh1 bilioni), Wizara ya Afya (Sh1 bilioni); Mambo ya Nje (Sh613 milioni) na Mbowe Hotels iliyopanga kwenye jengo ambalo kulikuwa na ofisi za kampuni zake za Freemedia na klabu ya Bilicanas, ikidaiwa Sh1 bilioni.

Share:

Musoma:Adakwa akiuza wasichana kama njugu



Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Ramadhani Ng’anzi amesema Septemba 3, saa 9.00 alasiri, Lucas alikutwa akiwa na wasichana watano (majina yamehifadhiwa) aliokuwa amewaficha nyumbani kwake kwa lengo la kuwauza na wengine kuwaozesha kwa wanaume wenye kuhitaji.
Amesema baada ya mama huyo kuhojiwa alikiri kufanya biashara ya kuuza wasichana kwa bei ya kati ya Sh 150,000 hadi 300,000, kwa kuangalia ukubwa wa umbo na siyo umri.
“Baada ya kufanya mahojiano na wasichana hao wenye umri kati ya miaka 15 hadi 28, walisema wametokea katika kijiji cha Muhejangila Wilaya ya Karagwe Mkoa wa Kagera,” amesema.
Kamanda Ng’anzi  amesema polisi wanaendelea na uchunguzi dhidi ya mama huyo, ili kubaini mtandao wa biashara hiyo haramu ya binadamu.
 “Tunaendelea kumuhoji, tunataka kujua iwapo kituo cha mwisho cha biashara hiyo ni hapa ndani tu au ni hadi nje ya nchi , biashara hiyo ilianza lini na idadi ya wasichana waliokwisha uzwa na waliuzwa wapi,”
Kamanda Ng’anzi alisema baada ya upelelezi kukamilika, mama huyo atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo.

Share:

Nature amsikitikia KR Muller


 Kiongozi wa kundi la Wanaume Halisi, Juma Nature amehudhunishwa na hali aliyokuwa nayo mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva KR Muller akisema inatokana naa kutokusikiliza ushauri wake.
KR Muller ambaye kwa sasa anajitambulisha kama rais wa Rader Entertaiment iliyo chini ya mwanamuziki TID, alfajiri ya Jumapili alikutwa akiwa hajitambui kwa kuzidiwa na kilevi nje ya baa maarufu maeneo ya Mwembeyanga, Temeke.
 Nature amesema alijitahidi kuizuia hali hiyo, lakini kwa bahati mbaya aliondoka bila kuaga katika kundi na kumtaka amuache kwanza afanye mambo yake kwa sababu ya kumshauri kuepukana na makundi mabaya.
Hapo awali KR Muller alikua kwenye kundi moja na Juma Nature pamoja na Dollo lililoitwa Wachuja Nafaka kabla ya TMK na  baadaye walizalisha kundi la Wanaume Halisi.
“Alfajiri nikiwa nyumbani nilipigiwa simu kwamba ndugu yako tumemkuta huku kalewa, hajitambui kwa kuwa yeye alishaondoka kwenye kundi sisi tulibaki wenyewe kwenye kundi na kina Dolo, tukaona si vibaya tukodi taxi impeleke kwake anakoishi sasa,” alisema Juma Nature.
Nature amesema alipopigiwa simu alfajiri ya Jumapili, ilimrudisha kukumbuka ya nyuma namna alivyomshauri kukaa mbali na matendo yasiyofaa na makundi mabaya.
“Binafsi sijachukulia vizuri yeye ni kioo cha jamii na nilishamshauri huko anakohamia, kwa sababu tangu yupo kwetu alikuwa na matatizo, lakini yamezidi tangu aende huko kwa sababu hivi vitu vinasababishwa na makundi, sasa ukiwa unakaa na makundi ambayo watu wanavyoishi ni tofauti na jamii tayari ni tatizo,” amesema Nature.
Share:

magazeti ya leo jumatano tarehe 7.9.2016


Share:

Tuesday, 6 September 2016

Taarifa ya spika Job Ndugai kuhusu Rais Magufuli kupitisha miswada mitano


Na Eleuteri Mangi-Maelezo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameridhia na kusaini Miswada mitano kutumika kama Sheria kamili za nchi.

Hayo yamesemwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai mara baada ya kufungua Mkutano wa nne wa Bunge la 11 leo mjini Dodoma.

Miswada iliyoidhinishwa na Rais ni pamoja Sheria ya Fedha na Matumizi ya mwaka 2016, Sheria ya Fedha namba 2 ya mwaka 2016, Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali ya mwaka 2016, Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbambali namba 2 na 4 ya mwaka 2016 na Sheria ya Marekebisho ya Ununuzi ya Umma namba 5 ya mwaka 2016.

Aidha, Mhe. Spika amewakumbusha Wabunge kusoma na kuelewa kila kinachokuja Bungeni ili waweze kutekeleza majukumu yao ya kibunge ipasavyo kwa niaba ya wananchi waliowatuma kufanya kazi hiyo ili kuwaletea maendeleo.

Wabunge wametakiwa kutekeleza majukumu hayo ya uwakilishi wa wananchi ili waweze kujadili masuala mbalimbali kwa kuzingatia haki, ustahimilivu, busara, hekima na kutumia lugha ya staha katika mijadala ya Bunge.

Vile vile Mhe. Spika amempongeza Naibu Spika Dkt. Tulia Akson kuongoza vema mkutano wa tatu wa Bunge ulioanza Aprili 19 na kumalizika Juni 30 mwaka huu kwa kushirikiana na wenyeviti wa Bunge Andrew Chenge, Mussa A. Zungu na Najima Giga.

Katika hatua nyingine Mhe. Spika amemshukuru Rais Dkt. Magufuli, Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Watanzania wote walimuombea alipokuwa kwenye matibabu nje ya nchi pamoja na Madaktari waliomhudumia akiwa kwenye matibabu na kumshukuru Mungu kwa kumwonesha upendo alipokuwa kwenye mapito ya kuugua.

Katika mkutano huo wa Bunge yameulizwa maswali 14 ambayo yalielekezwa kwenye Wizara mbalimbali na kujibiwa kwa llengo la kutolea ufafanuzi masuala yanayotekelezwa kwa Serikali.
Share:

Serikali Yakanusha Taarifa Inayosambazwa Katika Mitandao ya Kijamii Kwamba Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan Ameomba Kujiuzulu


Ofisi ya Makamu wa Rais inakanusha taarifa inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan, ameomba kujiuzulu nafasi yake na kwamba taarifa hiyo ni ya uzushi na uongo haina ukweli wowote.

Taarifa hiyo ni ya uchochezi inayolenga kuliweka Taifa kwenye taharuki.  Mhe. Makamu wa Rais yuko bega kwa bega na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kufanya kazi zao kwa mujibu wa Katiba ya nchi ili kuwaletea wananchi maendeleo.

Ofisi ya Makamu wa Rais inawataka wananchi na Watanzania kwa ujumla kupuuza taarifa hiyo ambayo inalenga kupotosha umma kuhusu ushirikiano mzuri uliopo baina ya Viongozi wetu.

Mwisho, Ofisi ya Makamu wa Rais inawasihi Watanzania kufanya kazi kwa bidii na wajiepushe na vitendo vinavyolenga kuvuruga amani na utulivu nchini.

Share:

New AUDIO | Bushoke - Mpita Njia | Download

Share:

Rais Magufuli akagua ujenzi wa mabweni UDSM asubuhi hii

Rais Magufuli leo asubuhi amekagua ujenzi wa majengo ya hostel kwa ajili ya wanafunzi Chuo Kikuu Dar es Salaam.

Rais Magufuli kukabidhiwa rasmi majengo hayo mwezi Desemba mwaka huu.

Hosteli hizo zitakuwa na uwezo wa kuhifadhi jumla ya wanafunzi 3,840.


Share:

Rais Magufuli atoa siku 7 kwa wapangaji wote Serikalini wanaodaiwa na NHC walipe

Rais John Pombe Magufuli ametoa siku saba kwa wapangaji wote serikalini wanaodaiwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kulipa madeni yao, pamoja na kutoa agizo kwa viongozi wa shirika hilo kuwatolea vitu nje watakaoshindwa kulipa madeni yao kwa wakati.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waliokuwa wakazi wa Magomeni Kota.

“Wapangaji wote lazima walipe madeni yao, natoa agizo leo wapangaji wote serikalini wanaodaiwa na NHC ndani ya siku saba wawe wameshalipa madeni yao, ” amesema.

Ameongeza kuwa “Wasipolipa endeleeni kuwatolea vitu vyao nje kama mlivyotoa vya jamaa, awe wa UKAWA toa nje, wa CCM toa. “

Chanzo: Dewji Blog
Share:

MAJIBU YA MASWALI NA HOJA ZA WADAU KWA MWEZI AGOSTI, 2016.

Image result for serikali ya tanzania

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, inapenda kuwashukuru wadau na wananchi wote waliotuandikia maoni pamoja na kuuliza maswali mbalimbali kwa kipindi cha mwezi Agosti, 2016. Tunapenda kuwajulisha wale wote waliotuandikia maoni na maswali na hawajafungua baruapepe zao (Emails) na kurasa zao za Facebook wazifungue kwani tumejibu kila swali na kuwatumia katika anwani husika na baadae kuyaunganisha maswali na maoni yanayofanana na kuyatolea majibu ya jumla kwa faida ya wasomaji wetu wengine ili kuendelea kuelimishana kuhusu masuala yanayohusu Uendeshaji wa Mchakato wa Ajira Serikalini.
1. Swali
Nawapongeza kwa kufanya kazi nzuri ya kuendesha mchakato wa ajira Tanzania, pili napenda kuuliza maswali mawili kama ifuatavyo, A. Napenda kujua ni vigezo vipi na ni kada gani ambayo huajiriwa kuwa Maafisa Mipango?  B. je ni muda gani umebaki ili kuanza kutangaza Ajira?
Jibu
Tumepokea pongezi zako. Tukirudi katika maswali yako, nikianza na swali la kipengele A. ambalo unapenda kufahamu ni vigezo vipi na kada gani huajiriwa kama Maafisa Mipango. Vigezo vya kukuwezesha kuajiriwa kama Afisa Mipango DRJ II kwa mujibu wa Waraka wa Maendeleo ya Utumishi NA. 3 wa Mwaka 2015, Nyongeza VII Muundo wa Utumishi wa Maafisa Mipango sifa za kuingilia moja kwa moja ni, Kuajiriwa wenye shahada /Stashahada ya juu ya Mipango kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali ambao wamejiimarisha katika mojawapo ya fani zifuatazo:
• Mipango ya Maendeleo ya Mikoa,
• Mipango ya Menejimenti ya Mazingira,
• Mipango ya Maendeleo ya Idadi ya Watu,
• Mipango ya Uwekezaji na Maendeleo ya Fedha,
• Mipango ya Menejimenti ya Rasilimaliwatu,
• Menejimenti ya Mazingira na Maendeleo ya Miji, na
• Maendeleo ya Uchumi.
Swali la kipengele B. ambalo umeuliza ni muda gani umebaki ili kuanza kutangaza ajira, Kwa kuwa Serikali bado inaendelea kukamilisha zoezi la uhakiki wa Watumishi hewa ni vyema tukaendelea kuvuta subira hadi pale zoezi hilo litakapokamilika na kama mlivyoarifiwa awali juu ya kusitishwa kwa Ajira,  vivyohivyo mtapewa taarifa rasmi na mamlaka zinazohusika za kuendelea kutoa nafasi za Ajira.
2. Swali
Habari yako kiongozi? natumaini  u mzima wa afya na unaendelea vizuri na majukumu ya kulijenga Taifa. Nina maswali ambayo naamini utanipatia majibu.
Je, endapo kijana amepata kazi serikalini kwa kupitia Sekretarieti ya Ajira baada ya kupita usaili na kuripoti katika kituo chake cha kazi na amefanya kazi kwa muda wa miezi kadhaa ila tatizo limetokea yeye hajapendezwa na mazingira ya kazi kwa namna moja au nyingine, Je!
1. Anaruhusiwa kufanya usaili mwingine pale utakapo tangazwa na Sekretarieti ya Ajira?
2. Kuna utaratibu gani wa mtu kuomba kubadilishiwa taasisi moja kwenda nyingine yoyote na sekretarieti ya Ajira? baada ya yeye kuripoti kituo chake cha kazi.
Jibu
Asante kwa swali lako. Ni kweli inawezekana ukawa umeripoti na hujapendezwa na mazingira ya kazi kwa sababu moja au nyingine japokuwa Serikali imejitahidi sana kuboresha mazingira ya utendaji kazi kwa kiasi kikubwa ikiwemo maeneo ya huduma za jamii, vitendea kazi, miundombinu na hata maslahi kwa watumishi wake yameimarishwa ili kuhakikisha watumishi wake wanaweza kwenda kufanya kazi mahali popote ndani ya nchi na kutoa huduma kwa jamii inayomzunguka kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu, ingekuwa vizuri pia kama ungeleza kwa nini hujapendezwa na mazingira husika ila tunachoweza kukuelimisha ni kwamba unaruhusiwa kuomba kazi Sekretarieti ya Ajira pindi itakapotangaza nafasi ya juu zaidi ya ile uliyonayo. Mfano wewe ni mchumi daraja la II na Serikali imetangaza nafasi ya mchumi daraja la I ambayo itahitaji mtu mwenye uzoefu wa kazi (utendaji mzuri katika fani yake) kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu (3), hivyo endapo utakuwa na sifa/kigezo hicho unaweza kuomba na kushindanishwa na waombaji wengine ila ni lazima pia upitishe barua kwa mwajiri wako ili akuidhinishie kabla ya kuwasilisha maombi yako ya kazi. Aidha, utambue wazi huruhusiwi kuomba nafasi ya kazi inayolingana na nafasi uliyonayo kwa kuwa utakuwa unaziba kwa makusudi mwanya wa wale wanaotafuta kazi kukosa kutokana na wewe uliyonayo kutaka kubadilisha kwa kutaka kuchagua maeneo ya kufanyia kazi, pasipokujua Utumishi wa Umma ni kutumikia watanzania wote mahali popote iwe mjini au kijijini.
Aidha, umeuliza kuhusu utaratibu gani wa mtu anaweza kutumia kuomba kubadilishiwa taasisi moja kwenda nyingine yoyote na Sekretarieti ya Ajira? Tunapenda kukufahamisha kwamba Sekretarieti ya Ajira haina utaratibu wa kumbadilishia mtu kituo cha kazi baada ya kupangiwa na kuripoti kazini, kwakuwa jukumu la Taasisi hii kuendesha mchakato wa Ajira kwa niaba ya waajiri wengine katika Utumishi wa Umma, ikisha kamilisha kazi hiyo na kukupangia kituo cha kazi na wewe kwenda kuripoti na kukamilisha zile taratibu za msingi na kuajiriwa mwenye uwezo wa kukuamisha kituo kimoja kwenda kingine ni Katibu Mkuu, Menejimenti ya Utumishi wa Umma kwa kuwa ndio mwenye dhamana ya kusimamia watumishi wote. Anaweza kukuandikia barua ya uhamisho ukiomba kubadili kituo kutokana na sababu utakazotoa, nae atapima endapo zitakuwa za msingi atakuhamisha kwa mujibu wa Sheria, kanuni na taratibu kulingana na mahitaji na uwepo wa nafasi husika kule unakotaka kuhamia.
3. Swali
Hello, hongera sana kwa kazi nzuri mnayofaya ya kurahisisha mawasiliano kati ya Umma na  Sekretarieti ya Ajira na katika Utumishi wa Umma. Mimi niliwahi kuajiriwa na Serikali  ila Ajira yangu ilisitishwa kwa kuwa nilienda kusoma  bila ya ruhusa ya mwajiri. Hivyo niliamua kuandika barua kwa lengo la kuajiriwa tena baada ya ajira ya awali kusitishwa, ambapo ningependa kujua ombi langu limefikia wapi tangu nilipowatumia  barua mwezi Mei, mwaka 2015 kwakuwa sijapata majibu ya barua yangu hadi sasa, nitafurahi sana endapo ombi langu litapata majibu. nakutakia makujumu mema.
Jibu
Asante kwa swali lako pamoja na pongezi zimepokelewa. kuhusu majibu ya barua yako tumejaribu kufuatilia katika kumbukumbu zetu hatujaweza kuona nakala yoyote kutoka kwako na kwa kuwa hujaeleza ni wapi ulipoituma inakuwa vigumu kwetu kuweza kukupa majibu ya hatua iliyofikiwa, hivyo tunakushauri endapo una nakala au unaweza kuandika barua nyingine ielekeze kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma. Maana ofisi hiyo ndio yenye dhamana ya kushughulikia Watumishi wa Umma ambao ni waajiriwa tayari kutokana na maelezo yako Ajira yako ilisitishwa kutokana na kuonekana mtoro kazini kama ulivyobainisha ulienda kusoma bila ya kupata kibali kutoka kwa mwajiri wako.
4. Swali
Habari Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, poleni na kazi ya kujenga Taifa. Mimi ni kijana wa kiume  na mkazi wa Mwanjelwa Mbeya na pia ni muhitimu Chuo Kikuu cha Jordan.
Kuhusu kusitishwa kwa ajira mpya, kwanza naweza sema Rais wetu alikuwa sahihi kusitisha Ajira kutokana na uwepo wa watumishi hewa, nilikuwa nataka niwambie kuwa muda unazidi kwenda na atujapata taarifa yoyote nini kinaendelea japo mlisema zoezi la kuhakiki watumishi hewa bado linaendelea lakini bado hamjasema mtamaliza lini, nikimaanisha tarehe na siku, ilihali vijana asilimia kubwa waliohitimu wameanza kukata tamaa wakiamni Ajira zaweza zisiwepo sababu hawajui kesho yao na kuna baadhi walishindwa kusaini mikataba kwenye Taasisi binafsi wakiwa na uhakika wa Ajira sasa muda unaenda wengi wao wapo nyumbani na wakiwa njia panda bila kujua pakwenda.
Maoni yangu ningewaomba mjitahidi kabla ya mwezi huu kuisha muwe mmesha toa taarifa kamili kuhusu ajira mpya, na kama zoezi la kuhakiki watumishi hewa limekua bado linahitaji muda mwingi mwambieni Mhe. Rais John Pombe Magufuli aruhusu Ajira hata kama ishu ya watumishi hewa bado, kwa hawa wahitimu mliopanga kuwaajiri waajirini kwa kuwatengea (folder) lao ambalo alita ingiliana na waliopo kazini na Rais alisema hata toa ajira mpya akimaanisha zoezi litakuwa gumu zaidi kwa kuongeza watumishi wapya waunganishwe na wazamani, na sina imani kama nyie wenye dhamana ya kuajiri kwamba hamuwezi teknologia ya kutenganisha waajiri wa zamani na wapya ilihali sasa hivi teknolojia imekua, jamani nchi kama Rwanda watushinde? najua Rais wetu yupo siliazi mpelekeni hata proposal jinsi ya kufanya namna gani mtatenga watumishi waliopo na wa zamani ili operation ya kucheki watumishi hewa iendelee na waajiriwa wapya waanze kazi.
Na  sera ya Rais wetu ni hapa kazi tu na sasa hivi nikiangalia kuna upungufu wa watumishi kama Madaktari, Walimu na sekta nyingine zenye uhaba wa wafanyakazi na muda unazidi kwenda je sera ya hapa kazi tu itaendana wakati mahospitalini hakuna wafanyakazi wa kutosha, vijijini hakuna walimu wa kutosha, tena gepu la watumishi walio hewa bado lipo wazi, jamani jitahidini nimeandika haya kwa maendeleo ya nchi pamoja na kupunguza idadi ya wahitimu waliopo nyumbani kwa mwaka na miezi sasa huku tegemeo na walichosomea kinahuishwa kuajiriwa serikalini na ofisi ya TAMISEMI Naibu Waziri Suleiman Jafo alisema wametenga budget ya kuajiri Watumishi wapya 71,000, kwa niaba ya wahitimu wanaosubiri Ajira nategemea mawazo yangu yatafanyiwa kazi na kupata majibu sahihi kabla ya mwezi huu kuisha. Asanteni sana na kazi njema.
Jibu
Tunashukuru kwa swali lako pamoja na maelezo marefu tumeyaopokea, yataendelea kufanyiwa kazi kadri inavyowezekana. Aidha, Serikali imejitahidi kutoa taarifa ya hatua iliyofikia katika uhakiki wa watumishi hewa mara kwa mara hata wiki iliyopita Waziri mwenye dhamana ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora alizungumza na Waandishi wa habari na kuelezea kuwa zoezi hilo liko katika hatua nzuri na kuzitaka baadhi ya taasisi ambazo bado hazijawasilisha taarifa zao za watumishi hewa ziwasilishe kabla ya  tarehe 26 Agosti, 2016 ili taarifa hiyo iweze kuwasilishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa hatua zaidi.
Hivyo, ni vyema tukaendelea kuvuta subira ili kupisha mamlaka husika kuweza kuratibu zoezi hilo kwa ufanisi kutokana na unyeti wake kwa mustakabali wa Taifa hili. Mwisho, nimalizie kwa kukuelewesha kuwa Sekretarieti ya Ajira ina dhamana ya kuendesha mchakato wa ajira kwa niaba ya waajiri katika Utumishi wa Umma ila siyo inayosimamia zoezi la uhakiki wala haiwezi kuendesha mchakato wa ajira bila ya kupata kibali cha kufanya hivyo kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, kwa kuwa suala la Ajira lina miongozo yake, linahitaji bajeti, kutengwa nafasi kwa mujibu wa ikama. Hivyo tusubiri zoezi hilo likamilike na baada ya hapo taarifa rasmi kuhusu mchakato wa Ajira Serikalini itatolewa na Mamlaka zinazohusika.
5. Swali.
Habari, mimi ni mkazi wa  Arusha na ni Mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dodoma  tangu mwaka 2014 katika fani ya Utalii, Ombi langu kwenu ni kutupunguzia sisi waombaji wa kazi gaharama za kusafisiri hadi Dar- es -salaam kwa gharama kubwa na kulala hotelini unatumia zaidi ya TZS150,000 na mwisho wa siku mtu unaambulia patupu. naomba muwe na zonal offices hata temporary tu mimi nilisha hudhuria interview zenu ambazo kiukweli sikuona sababu ya kuwepo kwa ofisi moja tu.
Kila kanda sasa hivi ina Vyuo Vikuu kwa hiyo kama ni sehemu ya kufanyia interview ipo Arusha tuna vyuo vingi Kilimanjaro na Tanga pia manake ofisi zinaweza kuwa Kilimanjaro ni bora waombaji waliochaguliwa interview wa kanda fulani wakalipa walao 10,000 kwa ajli ya kuhamisha ofisi kwa muda ili waweze kufanyiwa interview kwa mtu ambaye hana kazi afu unataka mtu asafiri kutoka labda muleba hadi dar tu afu pia hana ndugu na aje akose hiyo kazi inauma sana.
Ni matumaini yangu kwamba kwa ajira zinazosubiriwa mapema mwezi ujao Sekretarieti ya Ajira itafikiria hili suala.
Jibu
Tunashukuru kwa hoja yako. Ni kweli gharama ya msailiwa kutoka eneo moja kwenda lingine kwa ajili ya usaili ni kubwa. Hili Sekretarieti ya Ajira imeliona na imeweza kujitahidi mara kadhaa kusogeza huduma zake karibu na wadau pale bajeti iliporuhusu. Kwa kuwa imeshafanya saili kadhaa katika mikoa, nyingine kikanda na pale iliposhindwa kutokana na ufinyu wa bajeti ndio imekuwa ikifanyia Dar es Salaam. Tunakuahidi kuendelea kuhakikisha tunasogeza huduma zetu karibu na wadau kadri bajeti itakavyoruhusu.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma. 06 Septemba, 2016.

Share:

New AUDIO | BARAKA DA PRINCE - INODAE | Download

Share:

New AUDIO[Snippet] Diamond Ft. French Montana - All The Way Up Remix | Download

Share:

BAKWATA yatangaza siku ya Sikukuu ya Eid ya kuchinja.

Share:

Serikali Yakusudia Kuwapeleka Watoto Wa Mitaani Katika Mafunzo Ya JKT Ili Kusaidia Uzalishaji Mali


Na Ismail Ngayonga - Maelezo.
SERIKALI inakusudia kuwapeleka katika kambi za mafunzo  ya Jeshi la Kuujenga Taifa (JKT) watoto wa mitaani wenye umri wa zaidi ya miaka 18 ili wajifunze  stadi za kazi na shughuli  za uzalishaji mali.

Hayo yamesemwa jana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu  wakati wa mahojiano maalum katika kipindi cha Tunatekeleza kinachoandaliwa na Idara ya Habari (MAELEZO) na Televisheni ya Taifa (TBC1).

Waziri Ummy alisema hatua hiyo inalenga kuliwezesha kundi hilo la vijana kujihusisha na shughuli za uzalishaji mali badala ya kuzurura hovyo mitaani sambamba na kujihusisha na tabia na vitendo  vinavyokiuka maadili katika jamii.

Alisema tayari  watendaji wa Wizara yake kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Ofisi ya Waziri Mkuu tayari wamekutana kujadiliana kuhusu suala hilo ili kuangalia namna bora zaidi ya kusadia kundi hilo.

Alifafanua kuwa vituo vingi vya kulelea watoto hao vimekuwa na watoto waliozidi umri wa miaka 18, ambapo kwa mujibu wa sheria hawatakiwi kuwa katika vituo hivyo na kuongeza kuwa  ofisi yake itahakikisha zoezi la kuwapeleka katika mafunzo hayo linatekelezeka.

Katika hatua nyingine Waziri Ummy alipiga marufuku tabia za baadhi ya watu,  asasi na vikundi kuanzisha vituo vya kulea watoto yatima pasipo kuwa na usajili  kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Kwa mujibu wa Waziri Ummy alisema tayari ofisi yake imetoa maelekezo kwa Kamishina wa Ustawi wa jamii kufanya tathimini na utafiti wa kina kuhusu vituo vya kulea watoto yatima, ambapo iwapo kutabainika vituo vitakavyokosa sifa hatua za kisheria zitachuliwa kwa wahusika.

Kuhusu chanjo, Waziri Ummy alisema Serikali itaanza kutoa chanjo ya saratani ya shingo ya kizazi kwa watoto wenye umri wa miaka 9-13 ili kukabiliana na changamoto ya maradhi hayo nchini.

Waziri Ummy aliwataka wazazi kutoa ushirikiano pindi zoezi hilo litakapoanza kwa kuwa halitakuwa na madhara ya kiafya kwa watoto wao.

Aidha, alisema  Serikali imekuwa ikipoteza kiasi kikubwa cha fedha kila mwaka kwa ajili ya matibabu ya magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo saratani ya shingo ya kizazi kwa akina mama ambayo inaambukizwa na virusi vinavyojulikana kwa jina la Human Papiloma Virus (HPV).

“Tumeamua kuteua kundi la watoto wa lika huo kwani wengi wao katika umri huo wanakuwa bado hawajaanza kujihusisha na vitendo vya mapenzi”  alisema Waziri Ummy.

Alisema katika bajeti ya mwaka 2016/17 Serikali imepanga kuipatia taasisi ya saratani ya ocean road  kiasi cha Tsh. Bilioni 3 kwa ajili ya ununuzi wa madawa, ikilinganishwa na kiasi cha Tsh. Milioni 600 zilizokuwa zimetengwa katika bajeti ya mwaka 2015/16.

Akizungumzia changamoto iliyojitokeza hivi karibuni ya ukosefu wa chanjo katika vituo vya huduma ya hivi nchini, Waziri Ummy alisema suala hilo litakuwa historia hivi karibuni kwani tayari Serikali imeagiza kutoka nje ya nchi baadhi ya chanjo hizo.
Share:

Polisi Washuhudia Majambazi Yakitwangana Risasi,Zakamatwa Shehena za Silaha na Vifaa vya Uhalifu

WATU watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wa kutumia silaha, ambao wamehusika kufanya matukio mbalimbali ya kihalifu katika mkoa wa Dar es Salaam, wameuawa na majambazi wenzao katika eneo la Vikindu wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.

Licha ya kuuawa kwa majambazi hao, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limefanikiwa kuwakamatwa watu zaidi ya saba, wanaosadikiwa kuhusika na tukio la majibizano ya risasi na polisi, lililotokeo Vikindu lililosababisha kifo cha askari mmoja.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu, Simon Sirro alisema kabla ya kuuawa watuhumiwa hao walikamatwa katika maeneo tofauti ya Mbagala, Keko na Kawe jijini humo.

Alisema watu hao walikamatwa kufuatia tukio la ujambazi, lililotokea Agosti 29, mwaka huu katika Jengo la Sophia House maeneo ya Veta Changombe, ambapo majambazi hao walidaiwa kupora Sh milioni 35 na kutoweka kwa kutumia gari aina ya Toyota Noah lenye namba bandia T 549 BPK.

Aliongeza kuwa uchunguzi wa tukio hilo, uliendelea kufanyika na Septemba 3, timu ya upelelezi kutoka Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, iliweka mtego na kufanikiwa kuwakamata majambazi hao watatu na walipohojiwa walikiri kufanya matukio mbalimbali ya ujambazi wa kutumia silaha na kuweza kutaja silaha mbalimbali walizonazo.

Kamanda Sirro alisema majambazi hao, waliwapeleka askari eneo la Mbezi Chini katika nyumba waliyokuwa wamekodi na askari walifanya upekuzi na walifanikiwa kupata silaha mbalimbali, zikiwemo bunduki 23 na risasi zaidi ya 800 na vitu vinginevyo.

Alitaja silaha hizo kuwa ni bunduki za kijeshi tatu aina ya SMG zikiwa na magazini nane na risasi 120, bastola 16, magazini tatu za bastola na risasi moja, Shot gun pump action tatu na risasi 130, bastola 16 magazini na risasi 548 na bunduki tatu aina ya Shot gun na risasi zake 130.

Aidha alisema walikuta redio za mawasiliano 12 na chaja zake tatu, darubini za kuonea mbali tatu, pingu za plastiki 45, majaketi ya kuzuia risasi matatu, mkasi mmoja wa kukatia vyuma, mtarimbo mmoja, risasi baridi za kutishia 37, boksi moja la kusafishia silaha, nyundo kubwa moja, pingu za chuma tatu, mashine moja ya kuhifadhia kumbukumbu na magari mawili.

Alisema uchunguzi wao ulibaini kuwa majambazi hao Septemba 6, mwaka huu walipora bunduki aina ya Shot gun yenye namba 006091830, ikiwa na risasi moja katika barabara ya Mbozi Chang’ombe.

Sambamaba na hayo, majambazi hao walikiri kuhusika na wizi wa mamilioni ya fedha katika Benki ya Habib African ya Kariakoo mwaka 2014 na Benki ya Stanbic mwaka 2014, wakitumia gari aina ya Toyota Noah.

Kamanda Sirro alisema baada ya mahojiano zaidi, majambazi hao walisema wanazo silaha nyingine ambazo wamezificha Vikindu wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani. Ndipo askari walifuatana na watuhumiwa hao hadi kwenye msitu wa Vikindu.

Alisema askari walipofika eneo hilo, walilodai ni karibu na zilipo silaha hizo, walishuka kwenye gari na kuingia porini wakiwa wamewatanguliza watuhumiwa mbele majira ya usiku.

Aliongeza kuwa wakiwa msituni humo na askari wakiwa wenye tahadhari kubwa, ghafla walisikia milio ya risasi ikitokea mbele, ambapo askari walilala chini na baadaye zikisikika sauti zikisema ‘mmetuua sisi’.

Alisema baada ya risasi za mfululizo kutulia, askari walishuhudia majambazi hao ambao walichelewa kulala chini wakati risasi zikipigwa wakiwa wamejeruhiwa sehemu za kifuani na tumboni huku wakivuja damu nyingi.

Alisema askari walipiga risasi kuelekeza eneo zilikotokea risasi na walipoendelea kusonga mbele, walikuta silaha aina ya SMG ikiwa imetelekezwa na haikuwa na risasi ndani ya magazine, hivyo kufanya idadi ya silaha za SMG kufikia nne.

Aidha alisema askari waliwabeba majambazi hao na kuwapeleka kwenye gari kuelekea hospitalini, lakini wote walifariki dunia wakiwa njiani kutokana na kutoka damu nyingi. 
Akizungumzia tukio la Vikindu, Sirro alisema wamefanikiwa kuwakamata watu hao wanaosadikiwa kuhusika na tukio ambalo lilisababisha kifo cha askari mmoja.

“Majambazi hao walikuwa ni kundi la kama watu 14 na tayari tumewakamata zaidi ya saba ambao mpaka sasa tunawashikilia kwa mahojiano zaidi ili kufanikisha upelelezi,” alisema Kamanda Sirro.

Pia alisema kumekuwa na taarifa mbalimbali, zikisambazwa katika vyombo vya habari zikidai kuwa katika tukio la Vikindu, kuna askari anahusika na tukio hilo na kudai taarifa hizo si za kweli na hakuna askari aliyehusika katika tukio hilo.

Katika tukio lingine, jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wanne kwa makosa ya wizi wa magari manane, likiwemo gari moja la kibalozi. 
Kamanda Sirro alisema magari hayo yaliibwa jijini Dar es Salaam na kuuzwa kwa watu mbalimbali jijini hapo na mikoani na watuhumiwa wote wanaendelea kuhojiwa na mara upelelezi utakapokamilika watapelekwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

Sirro alisema katika tukio lingine jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa sita wanaodaiwa kuhusika na kuvunja nyumba usiku na kuiba. 
Alisema watuhumiwa wote wanaendelea kuhojiwa na mara upelelezi utakapokamilika watapelekwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger