Tuesday, 19 April 2016

YALIYOJIRI BUNGENI LEO

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
April 19 2016 Mkutano wa tatu wa Bunge la kumi na moja umeanza, na lengo lilikuwa ni  ni kujadili na kupitisha bajeti ya Serikali.
Katika baadhi ya sekta zilizojadiliwa ni pamoja na Wizara ya  Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, na Philipo Gekul ambaye ni Mbunge wa Babati Mjini aliuliza ‘Je, ni lini Serikali itamaliza tatizo la ulipaji ushuru wa huduma ambao ni asilimia 0.3 unaotozwa kutoka mitandao ya simu ambao kwa sasa halmashauri zimeshindwa kukusanya ipasavyo
Naibu Waziri Mhandisi Edwin Ngonyani  akajibu >> ‘Suala la ulipaji ushuru wa huduma za mawasiliano ambao ni asilimia 0.3 limekuwa tatizo kwa pande zote mbili, yaani Halmashauti ambazo ndio zinakusanya na kampuni ambazo zinakabiliwa na ugumu wa kuzilipa.’
Kwahiyo Serikali kupitia Ofisi ya Rais Tawala za mikoa, hivi sasa inafanyia marekebisho sharia ya fedha ya Serikali za mitaa ili kuwezesha kukusanya ushuru wa huduma za mawasiliano mahala pamoja
Baada ya hapo Spika wa Bunge Job Ndugai akaahirisha kikao, na kitaendelea tena April 20 2016 siku ya Jumatano

Share:

mpya:HII HAPA ADA KWA KOZI YA UUGUZI NA AFYA YA JAMII (CHETI).-CHUO CHA KOLANDOTO KWA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA APRIL 18 2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Joomla!

ADA KWA KOZI YA UUGUZI NA AFYA YA JAMII (CHETI). hii ni kwa watakaoripoti tarehe 18 april 2016 tu.

Share:

BREAKING NEWS:MKURUGENZI WA JIJI LA DAR WILSON KABWE ASIMAMISHWA KAZI LEO

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Kwa habari zilizotufikia mda huu Ni kwamba Mh.Wislom kabwe amesimamishwa kazi ,kutokana na kuhusika katika mikataba inayoipelekea serikali hasara kubwa.

 hatua hiyo imefikia wakati MH.MAKONDA aliesema mbele ya MAGUFULI katika uzinduzi wa daraja la kigamboni leo tarehe 19.4.2016 kwamba mikataba iliyofanywa na mkurugenzi huyo wa jiji.ikiwemo ya parking ya magari kuwa haipo kihalali na inaleta hasara kwa serikali.
Tafadhali endelea kutembelea MASWAYETU BLOG Tutawaletea taarifa zaidi mda si mrefu.
Share:

ALLY SALUM HAPI ACHAGULIWA KUWA MKUU WA WILAYA YA KINONDONI

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Share:

Davido–Ft Akon & Runtown–Chillin

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Untitled-1-2
Share:

Jide Ampeleka RAY C kwenye Maombi

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Dar es Salaam: Tenda miujiza Bwana! Lile sakata la mwanadada Rehema Charamila ‘Ray C’ kuandamwa na pepo mbaya wa utumiaji wa dawa za kulevya ‘unga’ hata baada ya Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ‘JK’ kumsaidia, inasemekana Mwanamuziki Judith Wambura ‘Jide’ ameambatana naye kanisani kwa ajili ya maombi.

Kikimwaga ‘ubuyu’ mbele ya Ijumaa Wikienda, chanzo chetu kilitonya kuwa hivi karibuni Ray C alitinga nyumbani kwa Jide, Masaki jijini Dar kwa ajili ya kumsalimia na kumpa hongera kwa wimbo wake mpya wa Ndi Ndi Ndi, lakini wakati huohuo kukawa na dada anayefahamika kwa jina la Anitha ambaye huwa anasali na Ray C.


Ilifahamika kwamba Anitha ni rafiki wa Ray C na pia wa Jide hivyo ulipofika muda wa kwenda kwenye maombi ndipo Jide akaungana na Anitha kumpeleka Ray C kanisani kwa ajili ya maombi.

“Jide na Ray C wana muda mrefu sana hawajaonana kwa zaidi ya miaka mitano au sita ila hivi karibuni Ray C alikuja nyumbani kwa Jide (Masaki) kwa ajili ya kumsalimia na kumpa pongezi kwa wimbo wake mpya ndipo Jide alipojumuika kumpeleka Ray C kanisani kwenye maombi ingawa nasikia kuna watu wengi ambao wanamsaidia Ray C na muda mwingi anaenda kanisani kwa ajili ya maombi,” kilisema chanzo hicho.

Kwa upande wake, meneja wa Jide, Christina Mosha ‘Seven’ alithibitisha Jide kutembelewa na Ray C kisha kwenda kanisani kwa maombi.
SOURCE: GPL
Share:

Aliyemtukana Rais Magufuli Aachiwa kwa Dhamana

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
HAKIMU Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Augustine Rwezile jana amempa dhamana aliyemtukana Rais John Magufuli, Isack Emiliy (40) ambaye ni mkazi wa Olasiti jijini Arusha.

Hakimu Rwezile alitoa uamuzi wa dhamana dhidi ya Emiliy baada ya mahakama hiyo kusema haioni sababu za kisheria inayomzuia mshtakiwa huyo kupata dhamana kwani kosa analoshtakiwa nalo lina dhamana kisheria.

Alisema ili mahakama imnyime Emiliy dhamana ni lazima upande wa mashtaka ulete ushahidi mahakamani hapo unaoonesha kama mshtakiwa akipewa dhamana atadhurika huko uraiani au la. Alisema mahakama haichukulii taarifa za maneno bali ushahidi ndio utakaoonesha kama mshtakiwa huyo akipewa dhamana ataweza kudhurika huko uraiani au la.

Alisema kwa mujibu wa kifungu cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai namba 148 kifungu kidogo cha 5(i -e), mahamaka ndio itakayothibitisha kama mshtakiwa akipewa dhamana kutokana na kosa hilo anaweza kupata madhara uraiani au la, lakini kwa sababu upande wa mashtaka haukutoa uthibitisho huo kwa maandishi bali umetoa kwa maneno basi mahakama hiyo inamwachia kwa dhamana mshtakiwa huyo.

“Mahakama haichukulii maneno maneno ndio yaongoze kumpa dhamana mshtakiwa bali ushahidi wa maelezo ndio unaweza kumsababishia mshtakiwa kupewa dhamana au la hivyo nakupa dhamana uwe na madhamini wawili ambao wataweza kusaini bondi ya Sh milioni tano kila mmoja pamoja na kuonesha mahakamani hapa vitambulisho vinavyokubalika kisheria,” alisema hakimu huyo.

Baada ya uamuzi huo, Wakili wa mshtakiwa Mosses Mahuna alidai mahakamani hapo kuwa wapo tayari kwa uamuzi wa dhamana ya mshtakiwa huyo na baadaye wadhamini wa mshtakiwa huyo walitimiza masharti ya dhamana yake. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 17, mwaka huu.
Share:

Makonda Aibua Madudu Zaidi Jengo la Machinga Comlpex

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameagiza kufanyika kwa uchunguzi jengo la Machinga Complex kubaini uhalali wa mkataba uliowezesha ujenzi wa jengo hilo, ikiwa ni pamoja na gharama halisi za ujenzi.

Alisema hayo kutokana na jengo hilo kuwa na deni la zaidi ya Sh bilioni 36, kiasi ambacho ni mara tatu ya thamani halisi ya jengo hilo na kuleta shaka ya ufisadi ndani yake. Jengo hilo lina thamani ya Sh bilioni 12.

Alisema kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa itaanza kufanya uchambuzi wa mkataba ili kupata uhalali wa gharama na kujua kiwango kinachostahili kulipwa na wafanyabiashara hao.

“Katika miradi mingi duniani huu ni wa aina yake, mradi ambao kabla haujaanza unaweka jiwe la msingi unaanza kudaiwa benki, mpaka unakuja kumaliza deni lako ni kubwa linakaribia robo mbili au tatu ya mkopo wenyewe, kabla hata hujaanza kupangisha hata mtu.
“Kwa takwimu zinaonesha tumekopeshwa na jengo limejengwa Sh bilioni 12.7, lakini mpaka dakika hii mnadaiwa Sh bilioni 36 na nyinyi ndio mnatakiwa kuzilipa, sasa kwa maelezo hayo ndio mnapata picha kwa nini tumeamua kujipa muda,” alisema Makonda.

Alisema katika maelezo ya awali yanaonesha kuwa jengo hilo lina mkanganyiko mkubwa na inawezekana kuwa ni miongoni mwa miradi iliyofanyiwa ufisadi mkubwa.

Hivi karibuni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simbachawene aliifuta bodi inayosimamia jengo hilo na kumsimamisha kazi meneja anayesimamia jengo hilo na kumtaka kwenda katika ofisi za jiji kwa ajili ya kumpangia kazi nyingine.

Katika hatua nyingine, Simbachawene alilikabidhi jengo hilo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili ya kuandaa mpango wa kuwaingiza wafanyabiashara bila masharti huku ukiangaliwa utaratibu mpya kwa wafanyabiashara hao.
Share:

TCU:HAYA HAPA MAJINA YA QUALIFIED AND NON QUALIFIED STUDENTS FROM ST.JOSEPH LEO TAR 19.4.2016

Share:

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) Yamuonya Uhuru Kenyatta

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) imetishia kuichukulia Kenya hatua kali isiposalimisha kwa mahakama hiyo washukiwa watatu wanaokabiliwa na mashtaka ya kutatiza mashahidi.

Msemaji wa ICC Fadi el Abdallah alisema mahakama hiyo itairipoti Kenya kwa Baraza la Mataifa Wanachama wa Mkataba wa Roma (ASP)  kama itaendelea  kushikilia msimamo wa kutowawasilisha Wakenya hao watatu mbele ya mahakama hiyo mjini Hague, Uholanzi.

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC, Bi Fatou Bensouda, amepata kibali cha kuwakamata aliyekuwa mwanahabari Walter Osapiri Barasa, wakili Paul Gicheru na Philip Bett kwa madai ya kutatiza mashahidi katika kesi dhidi ya Naibu Rais William Ruto na mwanahabari Joshua arap Sang.

Agizo la kukamatwa kwa Bw Barasa lilitolewa Oktoba 2013 ilhali lile la kukamatwa kwa Philip Bett na Paul Gicheru lilitolewa Septemba 2015 kwa madai kuwa walihonga mashahidi.

Kesi dhidi ya Bw Ruto na Sang ilitupiliwa mbali mapema mwezi huu kwa misingi kuwa ilikosa ushahidi wa kutosha kutokana na mashahidi kutatizwa.

Akihutubia hafla ya maombi mjini Nakuru mnamo Jumamosi, Rais Kenyatta alitangaza kuwa hakuna Mkenya mwingine atakayefikishwa katika mahakama ya ICC kujibu mashtaka.

Alisema kusitishwa kwa kesi hizo ndio mwisho wa ushirikiano baina ya Kenya na mahakama hiyo ya kimataifa.

“Ukurasa huo tayari tumefunga na hatutakubali Mkenya kurudi katika mahakama ya ICC. Tuna mahakama zetu za kutatua matatizo yetu,” akasema rais katika uwanja wa michezo wa Afraha.

“Kenya ikipuuza agizo la kuwasilisha washukiwa hao, majaji watawasilisha ripoti yao mbele ya Baraza la Mataifa Wanachama wa Mkataba wa Roma ambalo litachukua hatua zinazostahili,” akasema Bw Fadi.

Kifungu cha 87(7) cha Mkataba wa Roma kinasema: “Nchi mwanachama ikikataa kushirikiana na ICC na kutatiza utendakazi wake, mahakama inaweza kuwasilisha malalamishi kwa baraza la ASP.”

Wiki iliyopita, Bi Bensouda alisema kusambaratika kwa kesi dhidi ya Bw Ruto na Bw Sang kulichangiwa kwa kiwango kikubwa na kutatizwa kwa mashahidi na akataka washukiwa hao watatu wapelekwe ICC.

Alisema mashahidi 17 ambao walikuwa wameandaliwa na upande wa mashtaka walijiondoa baada ya kutishwa na kutengwa.

Hapo jana, Fadi alisema ICC inajua kuhusu tangazo la Rais Kenyatta wa Kenya kutosalimisha washukiwa hao na kuwa inafuatilia hatua hiyo kwa karibu.

“ICC haijapokea pingamizi zozote rasmi kutoka Kenya kuhusu mashtaka ya Wakenya watatu wanaoshukiwa kutatiza mashahidi wa kesi za ghasia  baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2007,” alisema Bw Fadi
Share:

Mzee Yusufu: Zipigwe Ngumi kati ya ALIKIBA na DIAMOND ili tujue kama kweli wana bifu.

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY


Mzee Yussuf ni miongoni mwa wasanii ambao hawaamini kama Diamond na Ali Kiba wana beef kutokana na wawili hao kutokutana pamoja na kuonyesha tofauti zao.
Akizungumza Jumamosi hii, Mzee Yussuf amesema beef ya Diamond na Ali Kiba zinakuzwa na mashabiki lakini sio beef kweli.

“Mimi Ali Kiba na Diamond sidhani kama wana beef kweli,” alisema Mzee Yussuf. 
Bado siamini kwa sababu ni watu ambao hawakutani tukaona kama kweli ni beef kweli zikapigwa ngumi watu tukaona,
Aliongeza, “Kwenye taarab kuna beef za kweli, watu wanazipiga kweli. Mimi naamini wanaume hawanuniani,”

Katika hatua nyingine Mzee Yussuf amesema anajipanga na wasanii wenzake kuanzisha umoja wa wasanii wa taarab ili na wao waweze kupeleka kero zao kwa pamoja.
Share:

Prof. Lipumba Aipasua CUF Vibaya

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Prof. Ibrahim Lipumba (kushoto), aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF akiwa na Maalim Seif Sharrif Hamad, Katibu Mkuu wa chama hicho
NDANI ya Chama cha Wananchi (CUF) kuna makundi mawili makuu, moja likimtaka Prof. Ibrahim Lipumba aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho na lingine likitaka atoswe.


Taarifa kutoka ndani ya chama hicho zinaeleza kuwa, kundi linalotaka atoswe limedhamiria kuvunja katiba huku kundi linalotaka arejeshwe kwenye nafasi hiyo limeapa kusimama na katiba ya chama hicho.

Taarifa zaidi zinaeleza kwamba, kundi linalotaka atoswe linafanya mkakati wa kuvunja Katiba ya mwaka 1992 Toleo 2013 Ibara ya 117 inayoeleza kwamba, “… kama hakuainisha tarehe ya kujiuzuli kwake basi mara baada ya katibu wa mamlaka iliyomteua ama kumchagua kupokea barua hiyo na kumjibu.”

Taarifa zinaeleza kuwa, maombi ya Prof. Lipumba kujiuzulu yalimfikia katibu wa mamlaka ambaye ni Maalim Seif Shariff Hamad na kwamba, kwa mujibu wa ibara hiyo, alipaswa kupeleka maombi hao katika Mkutano Mkuu wa chama hicho kuijadili barua hiyo na baadaye kujibu baada ya Mkutano Mkuu kujadili jambo ambalo mpaka sasa halijafanyika.

Prof. Lipumba aliyeteuliwa kutwaa nafasi hiyo na Mkutano Mkuu mwaka 1999 na kuwa, Ibara hiyo inaipa mamlaka mkutano huo kukubali ama kukataa kujiuzulu kwake.

“Kwa mujibu wa Katiba ya CUF Prof. Lipumba bado ni mwenyekiti wa CUF. Uenyekiti wake unakoma pale tu katibu wa mamlaka (baada ya Mkutano Mkuu) kuridhia maombi yake ya kujiuzulu na kumjibu kwa barua, Prof. Lipumba mpaka sasa hajajibiwa,” ameeleza mjumbe mmoja wa Mkutano Mkuu aliyeomba kuhifadhiwa jina lake na kuongeza;

“Watu walidhibitiwa sana kwenye mapato ya chama ndio maana wanataka asirudi, hili ndio linalosababisha hata kutaka kuvunja Katiba. Lakini cha kujiuliza kwanini wanataka kukwepa ibara ya 117? Wanajua kwenye Mkutano Mkuu wajumbe hawawezi kukubali.”

Kwa mujibu wa taratibu za CUF, Baraza Kuu halina mamlaka ya kukubali ama kukataa.

“Mpaka sasa katibu wa mamlaka halijaleta taarifa ama maombi ya kujiuzulu kwa Prof. Lipumba, tunaisuburi ije na hakuna chochote kitakachofanyika mpaka utaratibu huu ufuatwe. Hatopatikana mwenyekiti mwingine mpaka taarifa hiyo itufikie,” amesema.

Mvutano wa CUF umedhihiri juzi kwenye kongamano lililoandaliwa na Kata ya Makurumla Manispaa ya Kinondoni ambapo wajumbe waliibua hoja ya ukimya wa taarifa kuhusu maombi ya kujiuzulu ya Prof. Lipumba.

Katika kongamano hilo, Mohamed Mgomvi, mmoja wa wanachama wa CUF alisema, upande wa bara chama hicho kimebaki kwenye uyatima na kwamba hakuna mtu madhubuti anayeweza kukiendesha kama Prof. Lipumba.

“Nashangaa viongozi wetu mnasema habari zisizoeleweka juu ya kujiuzulu kwa Lipumba badala ya kusema ukweli nini kinaendelea huko ndani, tangu alipoondoka Lipumba hakuna maendeleo alafu mnasema tupo pamoja naye, haiingii akilini hata kidogo,” alisema.

Maganga Dachi, mwanachama wa CUF katika mkutano huo pia alisema, kwa mujibu wa Katiba ya CUF, barua ya kujiuzulu inatakiwa ifike katika Mkutano Mkuu uliomchagua jambo ambalo halijafanyika.

“Kwa hatua hiyo chama kinavunja Katiba maana hadi leo hakuna kinachoendelea kama hivyo suala la Lipumba, linatakiwa kuwasilishwa kwenye Mkutano Mkuu nasi tunamtaka Lipumba arudi katika nafasi yake ili chama kiendelee na shughuli za kimaendeleo,” alisema Dachi.

Ushawishi ndani ya chama hicho unaendelea kufanywa na baadhi ya wanachama pia viongozi wa chama hicho kumrejesha Prof. Lipumba kwenye nafasi hiyo.

Prof. Lipumba alijiuzulu nafasi yake mwaka jana kwa madai ya kutoridhishwa na uamuzi wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kuridhia Edward Lowassa kuepusha bendera ya umoja huo kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015 kupitia Chadema.

Akizungumza na MwanaHALISI Online leo Sheweji Mketo, Naibu Mkurugenzi wa Uchaguzi na Mipango wa CUF amesema, kwa mujibu wa Katiba ya CUF, Prof. Lipumba anayo nafasi ya kurejea kwenye nafasi hiyo.

Mketo amesema, Katiba ya chama inamruhusu mwanachama aliyejiuzulu uongozi kurudi kuwania tena nafasi yoyote kwani kujiuzulu ni haki ya mwanachama.

Akijibu hoja ya Prof. Lipumba kurejea kwenye nafasi hiyo amesema, “anaruhusiwa kurudi kama kawaida, atajaza fomu za kuomba kuwania uongozi na atapigiwa kura na baraza la chama kama wagombea wengine.”

Amesema utaratibu wa chama hicho katika kumpata mwenyekiti ni kuitisha Mkutano Mkuu ndani ya miezi sita ili kumchagua mwenyekiti mpya.

“Tatizo ni kwamba, mpaka hadi sasa bado hatujafanya kikao kutokana na kukosa fedha hivyo chama kimeongeza miezi mingine sita ambapo mkutano mkuu unatarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu,” anasema.

 
chanzo: Mwanahalisionline
Share:

Serikali Yatoa Agizo Kwa Shule Binafsi Kuwa na Mihula Miwili

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
WIZARA ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi imeziagiza shule zote za binafsi kuwa na mihula miwili tu ya masomo kwa mwaka badala ya kuwa na mihula mitatu au minne kama ilivyo kwa sasa katika shule hizo.
Agizo hilo liko kwenye Waraka wa Elimu Namba Moja wa Mwaka 2015, ambao unaeleza kuwa kuanzia sasa mihula ya masomo, itakuwa miwili kwa kila mwaka wa masomo kwa shule zote za serikali na zisizo za Serikali.eustella-Bhalalusesa1
Waraka huo uliosainiwa na Kamishna wa Elimu, Profesa Eustella Bhalalusesa umefafanua kuwa kila muhula, utakuwa na likizo fupi na likizo ya mwisho wa muhula. Siku za masomo kwa mwaka zitakuwa ni 194.
Waraka huo pia umeagiza wanafunzi wote, wapumzike mwezi Juni na Desemba na mashindano ya michezo ya shule za msingi (Umitashumta) na michezo ya sekondari (Umiseta), ifanyike mwezi Juni wakati wa likizo.
Kutokana na agizo hilo, wamiliki wa shule zisizo za serikali wametakiwa kuwasilisha wizara ya elimu kalenda za mihula ya masomo. Nakala ya waraka huo wamesambaziwa wakaguzi wote wa shule, walioko kwenye kanda na wilaya kuhakikisha wanazifuatilia shule zote ili ziweze kutii agizo hilo la Serikali.
Profesa Bhalusesa alifafanua katika waraka huo, umekazia Waraka wa Serikali Namba 5 wa mwaka 2012 ambao ulikuwa unaelekeza mihula ya masomo kwa shule za sekondari na vyuo vya ualimu, ifanane ili kuepusha usumbufu kwa walimu na kwa wanafunzi.
Share:

BUNGE: Maswali 553 Serikali Itajibu, 88 ni ya Waziri Mkuu

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Serikali inatarajiwa kuwasilisha miswada mbalimbali ya sheria katika Mkutano wa Bunge la Bajeti utakaloanza kesho mjini Dodoma ili ijadiliwe na kupitishwa na wabunge.

Miswada mingi ya sheria imekuwa ikilalamikiwa na wadau, hata Rais John Magufuli wakati akizindua Bunge la 11 mwaka jana, alilalamikia Sheria ya Manunuzi ya Umma ya Mwaka 2011.

Alisema kuwa sheria hiyo inatoa mianya kwa watumishi kuiba fedha za umma.

Katika mkutano huo, Bunge linatarajia kujadili na kupitisha miswada miwili ambayo ni wa Sheria ya Matumizi wa mwaka 2016 na Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2016.

Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bunge, Owen Mwandumbya jana alisema Serikali itawasilisha pia bungeni miswada mingine ya sheria ijadiliwe na kupitishwa baada ya kupitisha bajeti kukamilika.

Hata hivyo, alisema Bunge bado halijapokea miswada itakayowasilishwa na Serikali zaidi ya hiyo miwili, lakini kuanzia Juni 24 hadi 30 zimetengwa kwa ajili ya kujadili miswada mingineyo.

Mwandumbya alisema pamoja na shughuli hizo, jumla ya maswali 465 yataulizwa na kujibiwa na Serikali bungeni na kila Alhamisi yataulizwa Maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu na anatarajia kujibu jumla ya maswali 88.

“Baada ya wabunge kujadili miswada itakayowasilishwa na Serikali, hoja ya kuahirisha Bunge itatolewa Julai Mosi. Hapo Bunge litakuwa limemaliza kazi yake ya kujadili bajeti za wizara zote katika mkutano huu,” alisema Mwandumbya.

Share:

TANESCO:HAKUNA MGAO WA UMEME TANZANIA

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeibuka na kukanusha taarifa zinazoenezwa na baadhi ya wananchi juu ya kuwepo kwa mgao wa umeme kutokana na kukatika kwa umeme kunakoendelea hivi sasa.

Katika mahojiano maalum na mtembezi.com Kaimu Afisa Mahusiano wa Tanesco, Leila Muhaji, amesema kukatika kwa umeme kunasababishwa na uboreshaji wa miundombinu chakavu iliyodumu kwa kipindi cha zaidi ya miaka 20 na ujenzi wa vituo vipya vya umeme vitakavyofanyakazi kwa ufanisi zaidi.

Aidha amewataka wananchi kuwa wavumilivu kwa kipindi hiki cha maboresho yanayoendelea kufanyika na kuahidi mara baada ya kukamilika kwa zoezi hilo watapata umeme wa uhakika na usiokatika mara kwa mara.

Ametoa wito kwa wananchi kushirikiana kwa karibu na shirika hilo hasa katika kipindi hiki cha mvua ili kuweza kutatua kwa haraka changamoto zinazojitokeza katika maeneo mbalimbali.

Share:

Mkuu wa Idara ya Utumishi Jijini Mwanza Kikaangoni Kwa Mikopo ya Watumishi Hewa

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amemueleza Mkuu wa Idara ya Utumishi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Sigrifid Kaunala kuwa ni miongoni mwa watumishi watakaochunguzwa kutokana na kugundulika kuwepo kwa baadhi ya watumishi hewa waliopata mamilioni ya fedha kama mikopo kutoka taasisi za fedha.

Mongella alitoa kauli hiyo jana wakati alipokuwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Jiji hilo ambao pamoja na mambo mengine alitumia nafasi hiyo kuzungumzia suala la watumishi hewa.

Alisema baada ya uchunguzi wa uhakiki wa awamu ya pili wa watumishi hewa uliofanywa na Serikali mkoani humo umebaini kuwepo kwa watumishi watano (majina yao yanahifadhiwa) waliojipatia mikopo ya mamilioni ya fedha kutoka taasisi za fedha hali inayoonesha baadhi ya mikopo hiyo isingetolewa bila ya kibali cha waajiri wao.

“Mkuu wa utumishi nasikia hata wewe unahusika kwenye sakata hili la watumishi hewa, haiwezekani mambo haya yatokee na wewe usijue na wewe ni miongoni mwa watu tunaowachunguza,” alisema Mongella.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Mkoa ya kuhakiki watumishi hewa, Waryoba Sanya alisema kazi ya kuhakiki watumishi walioko kazini lilianza jana kwa kuanza na uhakiki wa watumishi wote wa Ofisi Kuu ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza walioko kazini na kuwa lilikuwa linaendelea vizuri.
Share:

UZINDUZI DARAJA LA KIGAMBONI LEO

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Picha 6 za Muonekano wa Daraja la Kisasa la Kigamboni Litakalozinduliwa Leo na Rais Magufuli 

Daraja la kisasa la Kigamboni linalounganisha eneo la Kigambonina upande wa Kurasini likikatisha bahari ya Hindi. Rais Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kulizindua rasmi daraja hilo  leo Jumanne Aprili 19, 2016.
Akina mama na watoto wao wakilishangaa daraja hilo la kisasa
Barabara inayoelekea kwenye daraja hilo

 

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger