Wednesday, 18 November 2015

HAYA HAPA MAGAZETI YOTE YA LEO JUMATANO

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Share:

HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOPATA MKOPO AWAMU YA NNE 2015/2016-BATCH 4

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Tokeo la picha la HESLB

AWAMU YA NNE YA WANAFUNZI WALIOPANGIWA MIKOPO

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kuwafahamisha waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2015/2016 kuwa imetoa orodha ya AWAMU YA NNE yenye jumla ya waombaji wa mwaka wa kwanza 718 waliopangiwa mikopo.
Itakumbukwa kuwa wiki iliyopita, Bodi ilitoa orodha ya Awamu ya Tatu iliyokuwa na waombaji 6,915 waliopangiwa mikopo. Kati ya waombaji hao waliopangiwa mikopo, waombaji 4,642 ni walikua ni wale wanaojiunga na shahada ya kwanza katika vyuo mbalimbali nchini na waombaji 2,273 ni wanafunzi wanaojiunga na Stashahada (Diploma) ya Ualimu wa masomo ya sayansi na hisabati katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
Kwa msingi huo, Bodi inapenda kuufahamisha umma kuwa hadi sasa imekwishawapangia mikopo jumla ya waombaji mikopo wenye sifa 48,469 wa mwaka wa kwanza. Katika awamu ya kwanza, Bodi ilitoa orodha yenye jumla ya waombaji 12,282; Awamu ya Pili wanafunzi 28,554; Awamu ya Tatu wanafunzi 6,915 na Awamu hii ya Nne wanafunzi 718 wamepangiwa mikopo.
Majina yote ya waombaji waliofanikiwa kupangiwa mikopo kutoka katika awamu zote tatu yanapatikana kupitia mtandao wa Bodi wa olas.heslb.go.tz na tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz). Aidha, orodha hizo pia zimetumwa vyuoni kwa ajili ya taratibu za usajili.

Mwisho.
Share:

Tuesday, 17 November 2015

NDUGAI ASHINDA USPIKA KWA KURA 264 SAWA NA 70% YA KURA ZOTE

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Mbunge wa Kongwa (CCM) Job Ndugai ashinda kiti vcha Uspika kwa kura 264 sawa na kura asilimia 70 huku mpinzani wake kupitia Chadema Goodluck Ole Medeye akipata kura 109 huku wagombea wengine wakipata kura 0.
NDUGAI anakuwa Spika wa Bunge la 11 la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 
Share:

MAGAZETI YA LEO JUMANNE NOVEMBER 17 2015

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

I have set here headlines of various Tanzania News paper today, spend your time to read what is written here
Share:

Monday, 16 November 2015

TAARIFA KWA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA STASHAHADA ZA UALIMU ELIMUMSINGI NA ELIMU YA SEKONDARI KUPITIA MFUMO WA UDAHILI WA PAMOJA (CAS) KATIKA CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM)

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
  TAARIFA KWA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA STASHAHADA ZA UALIMU ELIMUMSINGI NA ELIMU YA SEKONDARI KUPITIA MFUMO WA UDAHILI WA PAMOJA (CAS) KATIKA CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM)
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linapenda kuwataarifu wote waliochaguliwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) baada ya Mfumo wa CAS kuonyesha kuwa umechaguliwa kwenda Chuo Kikuu cha Dodoma, utaratibu ni kusubiri UDOM na vyombo vyake vya ndani kuthibitisha majina hayo. Waliodahiliwa wanatakiwa kwenda chuoni baada ya kupata joining instructions na wito kutoka Chuo husika.

Kumekuwapo na wanafunzi waliosafiri kwenda kuripoti chuoni kabla ya taratibu hizi kukamilika na hivyo kusababisha usumbufu kwao wenyewe na kwa taasisi za NACTE na UDOM. Majina ya wanaotakiwa kwenda kuripoti na tarehe za kuripoti mara zote hutolewa na chuo husika. Kwa kuwa majina yamekwenda vyuoni kwa makundi (batches) sio makundi yote yamepitishwa na katika mchakato wa ndani ya vyuo.
Baraza (NACTE) hutoa uchaguzi wake ili kuondoa usumbufu kwa wanafunzi kuangalia tovuti za vyuo mbalimbali kusaka majina yao. Iwapo kwa sababu zozote UDOM itashindwa kuwapokea baadhi ya waliochaguliwa, Baraza litawapa nafasi katika vyuo vingine. Ikumbukwe kuwa kuna vyuo vingi ambavyo havijapata wanafunzi wa kutosha.
Imetolewa na:
Katibu Mtendaji
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE)
15 Novemba 2015
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger