Mh.
Job Ndugai ameteuliwa kuwa mgombea rasmi wa nafasi ya Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM).
Wabunge wateule wa CCM wamempitisha Job Ndugai kuwania uspika wa Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya wenzake wawili kujitoa.
Rais
wa Tanzania Dk. John Magufuli amemteua Dk. Tulia Ackson Mwansasu kuwa
mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kutengeua nafasi yake ya
awali aliyokuwa akishikilia kama Naibu Mwanasheria Mkuu wa serikali.
Mh. Dk Tulia anakuwa Mbunge wa kwanza wa kuteuliwa na Rais, kumbuka pia
Dk. Tulia ni mmoja kati ya watu watatu waliopitishwa na CCM kuwania
nafasi ya Spika wa Bunge
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph
Magufuli amepokea salamu za pongezi kutoka kwa Malkia Elizabeth II wa
Uingereza kufuatia kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Katika salamu hizo Malkia wa Uingereza amemueleza Mhe. Rais Dkt.
Magufuli kuwa “Natumaini kuwa mahusiano baina ya nchi hizi mbili ambazo
ni wanachama wa Jumuiya ya Madola yataendelea wakati wa utawala wako,
nakutakia kheri pamoja na wananchi wa Tanzania” amesema malkia katika
salamu zake.
Salamu pia zimetoka kwa Mfalme Akihito wa Japan ambaye amemueleza Mhe.
Rais Dkt. Magufuli “Nakutumia salamu za dhati, mafanikio na furaha
kwako Mheshimiwa Rais na watu wa nchi yako” Amesema.
Salamu zingine kwa Mhe. Rais Dkt. Magufuli zimetoka kwa Rais wa Jamhuri
ya kidemokrasia ya Kiarabu ya Saharawi, Mhe. Mohamed Abdelaziz ambaye
amemtakia kheri Mhe. Rais Dkt. Magufuli na kumueleza kuwa “Nina imani
kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea vyema chini ya uongozi
wako kuelekea katika kupata maendeleo na mafanikio zaidi”.
Amesema;
na pia amekipongeza Chama Cha Mapinduzi na Watanzania kwa uchaguzi wa
kidemokrasia ulioendeshwa katika mazingira ya kistaarabu chini ya
usimamizi wa waangalizi kutoka kwenye kanda, bara na kimataifa na hivyo
kuliletea sifa bara la Afrika.
Mhe. Rais Dkt. Magufuli pia amepokea salamu kutoka kwa Rais wa Namibia
Mhe. Hage Geingob na kumueleza Mhe. Rais Dkt. Magufuli kuwa salamu zake
na zile za wananchi wa Namibia ni za dhati kwa Serikali na Watanzania
kwa ujumla kwa ushindi wa kiti cha Urais.
“Pia napenda kutoa pongezi kwa Chama Cha Mapinduzi kwa ushindi
uliopatikana katika uchaguzi wa Oktoba 25, 2015”. Amesema na kuongeza
kuwa “Kwa hakika Watanzania wamezungumza na kukipa tena CCM Mamlaka ya
kuipeleka mbele Tanzania kuelekea kwenye mafanikio zaidi”. Ameongeza.
Salamu zingine ni kutoka kwa Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ambaye amesema
Tanzania kwa mara nyingine tena imedhihirisha kuwa ni nguzo ya
demokrasia barani Afrika.
Naye Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Joachim Gauck
amemtakia Mhe. Rais Dkt. Magufuli na Watanzania kwa ujumla mafanikio
katika kuendeleza Taifa kwa ujumla.
TAARIFA KUTOKA WILAYANI KAHAMA MKOANI SHINYANGA ZINASEMA KUWA WATU
WATANO KATI YA SITA WALIOKUWA WAMEFUKIWA NA KIFUSI KATIKA MACHIMBO YA
NYANGARATA KWA SIKU 41 WAMEOKOLEWA USIKU WA KUAMKIA LEO WAKIWA HAI.
KWA MUJIBU WA TAARIFA ZA AWALI INASEMEKANA WATU HAO WALIKUWA WANAISHI
KWA KULA MENDE,MAJI,UDONGO NA MAGOME YA MITI MAARUFU KAMA MATIMBA
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Dkt Tulia Ackson amesema ana mpango wa kuchukua fomu ya kugombea nafasi
ya Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, ameongeza kuwa fomu hiyo anaweza
kuichukua leo au kesho maana siku ya kurudisha fomu ni kesho
"Nashukuru kwa kuaminiwa na kuteuliwa mbunge, sasa mpango wangu ni kugombea kiti cha Naibu Spika wa Bunge la 11"
Chuo kinakaribisha maombi ya kujiunga na masomo katika programu za
Astashahada (Certificate), Stashahada (Diploma) na Shahada za Kwanza
(Bachelor Degrees). Je, wewe ni Mhitimu wa Kidato Cha Nne na umefaulu
masomo kuanzia matatu kwa alama "D" na ungependa kusoma masuala ya
Mipango? Kama ndio; <<<Bofya Hapa>>>
MNCH Research Coordinator Overall Description: This full-time Research Coordinator will
provide technical expertise and oversee the day-to-day activities of the
Canadian government funded research project â€Å“Innovating for Maternal
and Child Health in Africa (2015-2020)†project and support Monitoring
and Evaluation for the PS-MNCH Mama Toto Initiative (2016-2020).
He/she will serve as a liaison between investigators from the Catholic
University of Health Allied Sciences (CUHAS), University of Calgary
(UC), Mbarara University of Science and Technology (MUST) and
collaborators from Agriteam, Save the Mothers, Canadian Paediatric
Society, and Geita and Mwanza Region and District Health Teams.
MNCH Research Administrator Overall Description: This full-time Research Administrator will
oversee the day-to-day activities of the Canadian government funded
research project â€Å“Innovating for Maternal and Child Health in Africa
(2015-2020)†project and support Monitoring and Evaluation for the
PS-MNCH Mama Toto Initiative (2016-2020). He/she will support the
Research Coordinator and Principle Investigator.
Habari yenu, Kama kawaida yetu Maswayetu blog tunaendelea kutoa huduma ya kuangalizia watu majina ya waliopata mkopo awamu ya tatu 2015/2016 Ili kuangaliziwa mkopo fanya yafuatayo; 1.TUMA JINA LAKO NA EXAM NAMBA YA FORM 4 MFANO JOHN JOHN S2000/0018/2012 HESLB 2015/2016 3RD LOT kwenda namba 0768260834 2.HUDUMA HII UTATOZWA TSHS 1000 AMBAYO UTAITUMA KWA MPESA KWENDA NAMBA 0768260834 AU TIGO PESA(0652740927) 3.UTAJIBIWA NDANI YA DK MOJA TU 4.TUMA KWANZA PESA NDIO UJIBIWE